Search This Blog

DAMU YA MWANANGU - 2

 







    Simulizi : Damu Ya Mwanangu

    Sehemu Ya Pili (2)





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Rube akamwambia mganga kuwa ampe muda akajifikirie kisha atarudi tena,,baada ya kutafakari na kupata maamuzi sahihi.

    mganga hakuwa na kipingamizi kwa sababu sio lazima ni hiyari.

    baada ya kumalizana na Rube,,akaendelea na Nyamwela,,,,

    mganga akasema,,wewe ukitaka kuupata utajiri ni lazima utoe kafara la damu ya mwanao kwa kukata shingo yake pamoja na mikono na miguu yote kisha vilete hapa usiku wa manane ,,hakikisha siku hiyo ni usiku wa kuamkia siku ya jumatano,,,,

    Nyamwela hakusita akakubali haraka!

    kitendo hicho kilimshangaza sana Rube,,kwa nini Nyamwela yupo tayari kumtoa kafara mwanae,,hata bila kipingamizi!

    akamtazama Nyamwela kwa macho ya mshangao,,kisha akajisemea moyoni,,"mganga kasema ikishindikana kutoa kafara wazazi wangu wote wawili,,,basi nilete mchanga wa unyayo

    wa mtu yeyote nimpendae....wacha nifanye jambo,,ni bora nimtoe mtu asiyekuwa na faida yoyote hapa duniani,,,tena huyuhuyu Nyamwela.

    mganga akawaruhusu waende,,

    safari ya kurudi nyumbani ikaanza.



                 ******************************



    asubuhi palipokucha Rube akadamka mapema akaelekea kule kijiji cha tatu,,,ni kile kijiji alichokuwa anaishi mwanzo Nyamwela na familia yake,,

    Rube alnakwenda huko,,kutazama maendeleo ya shamba lake,,,ikamlazimu kuba huko kwa masaa mengi kiasi,,,aking'oa majani yaliyokuwa yamezunguka mazao yake.



    baada ya masaa matatu kupita akaonekana Nyamwela akiwa,,nyumbani kwake akijiandaa kuelekea kijiji cha tatu ,,kukamilisha masharti ya mganga,,,akachukua upanga na kuuweka vyema ndani ya suruali aliyokuwa kaivaa!

    ilipofika nyakati saa  kumi za jioni,,Nyamwela akawa amefika kijijini hapo,,



    wakati huo,Muna alikuwa shambani akitafuta mlo wa usiku,mtoto wa Muna alikuwa chumbani kalala usingizi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyamwela akazipiga hatua kuifuata nyumba..

    kwa mbali akaonekana Rube naye akizipiga hatua kuja nyumbani kwa Muna,,aliona si vyema kuondoka pasipo kumjulia hali mke wa rafiki yake,

    ghafla akashtuka kumuona Nyamwela anazipiga hatua za kunyemelea kuifuata nyumba ya Muna....akajisemea moyoni,,"huu ndio wakati muafaka wa kuchukua mchanga wa unyayo wa Nyamwela....

    Rube akazipiga hatua akaanza kuchota mchanga wa unyayo wa Nyamwela,,

    wakati huo Nyamwela alikuwa ameukaribia mlango wa kuingia ndani ya nyumba ya Muna,akaangaza angaza macho yake huku na kule,,ili ahaqkikishe hakuna mtu anayeshuhudia au kumuona anaingia ndani ya nyumba hiyo,,,

    wakati anaangaza angaza macho yake,,akashtuka kumuona Rube akiwa anachota mchanga na kuuweka katika mfuko wa plastiki!

    Nyamwela akakumbuka kuwa mganga alimwambia Rube kuwa akishindwa kuwatoa wazazi wake kafara basi alete mchanga wa mtu yeypte ampendaye,,kwa upendo ulioshibana!

    Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa akapaza sauti,,"Rube unafanya nini hapo?

    Rube akaufunga vyema mfuko uliokuwa na mchanga wa unyayo wa Nyamwela,,akaanza kutimua mbio,,,

    Nyamwela akaacha kuingia ndani ya nyumba ya Muna akaanza kumkimbiza Rube!







    Rube alitimua mbio kama kafungwa mota miguuni,,,

    alikimbia mfululizo hatimae akatokomea kabisa.

    Nyamwela,,,akahisi kuchoka,,ni baada ya kukimbia umbali mrefu pasipo mafanikio ya kumpa Rube! akaamua kusimama akageuza shingo yake,,akatazama ule upande aliotoka,,, wazo likamjia kuwa awahi kule kwenye kijiji anachoishi kwa sasa.....

    baada ya masaa kadhaa kupita akawa amefika katika kijiji hicho,,,akaamua kupitiliza mpaka nyumbani kwa Rube...lakini akakuta mlango wa nyumba ya Rube umefungwa kwa nje!

    akaamua kumsubiri huenda akarudi...

    alibaki hapo kwa masaa kadhaa,,,lakini hakuona dalili zozote za Rude kurudi kwake...

    Nyamwela akaamua kurudi nyumbani kwake,,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    asubuhi palipokucha Nyamwela akadamka mapema,, ili awahi nyumbani kwa Rube,,,lakini alipofika akaona bado mlango umefungwa  kwa nje,,hata apaonyeshi dalili yoyote ya mtu kuwemo ndani ya nyumba!

    Nyamwela akazidi kuchanganyikiwa ,,,wazo likamjia aende nyumbani kwake,,akachukue baiskeli akamtafute Rube kona zote za kijiji hicho...



    Upande mwingine alionekana Rube akiwa,,, njiani kuelekea kwenye milima ya NZOKA kwa mganga kuupeleka mchanga wa unyayo wa nyamwela,, ghafla akasita,, akajisemea moyoni,,"hapa nilipo sina pesa ya kulipia kwa mganga,,,mbaya zaidi pesa zipo kule nyumbani kwangu,,,akaamua kurudi kule kijijini kwao.



    wakati huo huo alionekana Nyamwela akiendelea kumtafuta Rube kwa udi na uvumba,,lakini hakufanikiwa kumpata akaamua kurudi nyumbani kwake...akiwa njiani wazo likamjia,,akajisemea moyoni,,"bila shaka Rube atakuwa kwa mganga wacha niwahi kabla mganga hajaanza kufanya kafala....

    bila kuchelewa akapanda kwende baiskeli yake na safari ya kueleke milima ya Nzoka ikaanza.

    alipofika kwa mganga,,akastaajabu kutokumkuta Rube,,,,akabaki mdomo wazi! akamuuliza mganga,,"yule rariki yangu ameshafika hapa?

    mganga akajibu ,,"bado, pia mbona niliwapa masharti kuwa makafara hayo yatafanyika usiku wa manane,,,mnatakiwa mlete vitu hivyo ussiku huu wa leo,,kwa sababu leo ni jumatano,,au umesahau?

    macho yakamtoka Nyamwela,,,akajisemea moyoni,,"nikifanya masihala nitatoleww mimi kafala,,,mbona huyu Rube ni mjinga kiasi hiki!

    Nyamwela akaondoka bila kuaga,,,akapanda baiskeli yake akaondoka harakaharaka.



    Upande mwingine alionekana Muma akiwa kambeba mwanae,,huku anapika kwenye jiko la kuni..wakati wote Muma alikuwa anaongea peke yake huku akicheka,,,utadhani kunamtu anaongea nae,,,Kumbe Muma huwa kunajambo la kimiujiza analiona mara kwa mara,,hata akiwa anaonge na kucheka peke yake,,wakati mwingine huongea maneno yasiyoeleweka ni kama lugha fulani,,,huwa anatokewa na mzimu wa Mama yake na mzimu huo huwa unaongea na Muna,,lakini jambo hilo hakuna mtu yeyote anayelijua....

    baada ya kumaliza kupika akaingia ndani ya nyumba kumlaza mwanae.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana Nyamwela akiwa anaendesha baiskeli yake kwa mwendo wa kasi mpaka watu wakawa wanamshangaa!

    akiwa njiani akakutana uso kwa uso na Rube,,akiwa anaelekea kwa mganga! Rube akaanza kutimua mbio,,lakini kabla hajafika mbali,,, akakamatwa na Nyamwela....

    Nyamwela akaaanza kurusha ngumi nyingi uwoni mwa Rube...kisha akamfunga kamba,,,huku akisisitiza Rube ampe ule mchanga wa unyayo wake!

    Rube akakataa katakata akidai kuwa ule mchanga si wa unyayo wa mguu wa Nyamwela....

    Nyamwela akaakasirika sana,,,akaamua kumfunga na kamba katika mti mmoja uliokuwa umezungukwa na kichaka kikubwa katika pori dogo akamchinja shingo! kisha akaondoka zake kuelekea nyumbani kwake,,alipofika nyumbani kwake,,akachimba kaburi,,kisha akaingia ndani ya nyumba yake kupumzika.



    ilipofika usiku wa saa nne,,Namela akaandaa upanga wake...kisha akaelekea katika kijiji cha tatu,,kule nyumbani kwa Muna.

    wakati huo Muna alikuwa kalala usingizi kando ya mtoto wake mchanga.

    baada ya lisaa limoja kuoita nyamwela akawa kafika nje ya nyumba ya Muna,,,akavunja mlango na kuingia ndani ya nyumba ya Muna,,

    Muna akashtuka kutoka usingizini! alipofumbua macho,,akastaajabu kumuona Nyamwela,,,

    bila kuchelewa,Nyamwela akaanza kumshambulia Muna kwa kumkata na upanga aliokuwa kaushikilia mkononi!

    alimkata mara nyingi sehemu ya kichwani mpaka Muna akafa papo hapo!

    akachukua guni,,na kuweka maiti ya  Muna ndani ya gunia hilo akalifunga vyema... akalivuruta na kulipeleka kwenye baiskeli yake,,,,ukiangalia kwa haraka haraka huwezi kugundua kuwa ni maiti,,unaweza kusema ni mzigo wa kawaida!

    alipohakikisha kaiweka vyema maiti hiyo,,,akazipiga hatua kurudi ndani ya nyumba ya muna.

    akamfuata mtoto wake mchanga aliyekuwa kalala usingizi juu ya kitanda akamchukua mtoto wake,,,akaangaza angaza macho yake akaona khanga..akaamua kuchukua khanga hiyo  akamfunga mgongoni! akazipiga hatua kutoka nje ya chumba hicho,,ghafla akasikia hodi,,mtu anagonga mlango!

    TAHARUKI!!!!!!!!!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nyamwela akashtuka akaingiwa na wasiwasi,,,akasita kufungua mlango! akabaki kimya! mlango ukaendelea kugongwa mfululizo,,Nyamwela akaamua kufungua khanga aliyokuwa kaifunga mbeleko,,mgongoni,,,akamlaza mtoto kitandani,,kisha akaandaa upanga wake akazipiga hatua kuufuata mlango,akaufungua kisha akauliza kwa sauti ya upole,,"wewe ni nani?

    ikasikika sauti ikisema,," mimi ni daktari wa kitengo cha wagonjwa wa akili....nimekuja kutazama maendeleo ya mwanamke anayeitwa Muna,,,katika kumbukumbu zangu alikuwa anaishi katika nyumba hii...

    Nyamwela akajibu kwa sauti ya ukali,,"hapa hakuna kichaa wala chizi,,wote tunaoishi humu ndani tunaakili zetu timamu,,,huenda mtu huyo alihama hapa.

    baada ya Nyamwela kusema maneno hayo,,yule daktari akaondoka zake...

    Nyamwela akaendelea kumtazama daktari huyo mpaka akaishilizia..

    akaamua kurudi ndani ya nyumba akamchukua mtoto akamfunga mgongoni,,akatoka nje ya nyumba akafunga mlango huo,,akapanda kwenye baiskeli yake akaelekea kijiji cha tatu kule napoishi...



    baada ya lisaa limoja akawa amefika,,,akashushu gunia lililokuwa na maiti ya muna,,akalivuruta gunia hilo na kuliingiza ndani ya nyumba yake,,akachukua jembe akatokanalo nje ya nyumba,,,kisha akarudi ndani ya nyumba,,,,akamlaza mwanae juu yameza ya mbao,,,akachukua upanga wake akamchinja bila huruma,,kisha akanza kukata viungo vya mwili wa mtoto wake,,ikiwemo mikono na miguu,,kisha akavikusanya na kuviweka kwenye mfuko wa plastiki, akabeba maiti ya mwanae kisha akatoka nje ya nyumba...akarusha maiti hiyo ndani ya lile kaburi alilolichimba nyuma ya nyumba yake,,,,akavuruta maiti ya Muna akaitumbukiza ndani ya shimo,,,kisha akachukua jembe na kuanza kufukia shimo hilo.

    alipomaliza akarudi ndani kwake asubirie muda ufike aianze safari ya kuelekea kwa mganga,,kupeleka viungo vya mwili wa mwanae.,,,,

    akaamua kujilaza kitandani,,,,kutokana na uchovu aliokuwanao akajikuta analala masaa mengi,,, aliposhtuka kutoka usingizini,,akatazama saa yake ya mkononi,,akastaajabu kuona ni saa nane kasoro za usiku!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akachukua ule mfuko wa plastiki uliokuwa na viungo vya mwili wa mtoto wake,,akazipiga hatua za harakaharaka akatoka nje ya nyumba,, akapanda juu ya baiskeli yake na safari ya kuelekea kwa mganga ikaanza...

    Nyamwela aliendesha baiskeli yake kwa kasi ya ajabu....hatimae akafika kwenye milima ya Nzoka,,ambapo anapatikana mganga matata.. akatazama saa yake ya mkononi,,ilikuwa ni saa kumi na moja kasoro,,macho yakamtoka,,,akaiacha baiskeli na kuanza kutimua mbio,,huku kashikilia ule mfuko wa plastiki.

    Alipokaribia eneo la ngome ya mganga huyo,,ghafla ikasikika sauti ikimwambia,,"umechelewa,,huu sio muda wa kufanya kafara,,,rudi ulipotoka!

    Sauti hiyo ilimshtua Nyamwela,,kwa sababu ilikuwa inatisha kwa mngurumo kama radi,,pasipo kuonekana anayeongea maneno hayo!

    Nyamwela akautupa ule mfuko akaanza kutimua mbio mpaka kule alipokuwa kaiacha baiskeli yake,,, akaichukua na kuiendesha kwa kasi ya ajabu!!! hatimae akafika nyumbani kwake!

    akafungua mlango na kuingia ndani,,,,akaiegesha baiskeli yake akazipiga hatua kukifuata kitanda akajilaza,,,

    baada ya sekunde kadhaa kupita akahisi harufu ya damu ikinuka ndani ya nyumba yake,,,akasema,,"mi ni mjinga kiasi gani? yani nimesahau kufuta zile damu juu ya meza,,pale nilipomchinjia mwanangu! wacha niifanye kazi hiyo sasahivi.

    Nyamwela akanyanyuka kitandani akawasha koroboi,,akaanza kufuta damu hiyo!! hatimae meza ikawa safi!!

    akazima koroboi akajilaza kitandani,,

    baada ya dakika kadhaa kupita,,akahisi tena harufu ya damu ikinuka zaidi ya mwanzo!! akanyanyuka kitandani na kuwasha korobi,,akaangaza angaza macho yake hakuona kitu chochote....akazima koroboi hiyo,,kisha akarudi kitandani,,,

    harufu ya damu ilizidi kuongezeka kila baada ya dakika kadhaa!!

    Nyamwela akaanza kuingiwa na wasiwasi!!! hofu ikatawala juu yake,,akaanza kuogopa!

    wakati anatafakari nini cha kufanya,,gafla kikasikika kishindo cha kitu kizito kudondoka kule nyuma ya nyumba yake!! ni ile sehemu ya kabuli alilomzika Muna pamoja na mwanae..

    akachukua koroboi akaiwasha kisha akatoka nje kuelekea kule nyuma ya nyumba,, aone je? ni kitu gani kimedondoka!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alipofika akamulika kwenye lile kaburi,,,akashtuka! macho yakamtoka ,,alipotazama juu ya kaburi hilo,,akaona ule mfuko alioutupa kule kwenye milima ya Nzoka,,uliokuwa na viungo vya mwili wa mwanae,,,ukiwa juu ya kaburi hilo!!

    akatupa koroboi na kutimua mbio akarudi ndani ya nyumba yake,,,akafunga mlango! punde si punde akasikia kishindo cha kitu kikitua juu ya meza!!!!

    alipotazama kwa makini akaona ni uleule mfuko!!! akafungua mlango haraka akatimua mbio,,,,kabla hajafika mbali,,mara ghafla!!

    KIZAAZAA!!!!!!



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog