Search This Blog

SHUHUDA - 2







    Simulizi : Shuhuda

    Sehemu Ya Pili (2)



    yule muosha magari alipofika katika sehemu yake ya kazi alimkuta kamishna... kumbe kamishna alikuja hapo dakika mbili zilizopita.... habari yako muheshimiwa..nilitoka kidogo nilikwenda kupata chakula cha mchana.....alisema muosha magari""""

    ok"" sipo mbali we endelea na kazi nitarejea baada ya nusu saa... alisema kamishna.. kisha akaondoka zake na kuliacha gari lioshwe....

    bila kuchelewa mtu yule aliiweka bahasha ndani ya droo ya gari kisha akaanza kuliosha gari hilo...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya nusu saa kamishna alirudi alikita tayari gari lake limeoshwa na kuwa safi.... alitoa shilingi efu tatu na kumpa yule muosha magari... kisha akaingia ndani ya gari akaliwasha na kuondoka zake. ......akiwa njiani alifungua droo ili atoe simu yake alistahajabu kukuta bahasha.... alipunguza mwendo akalipaki gari lake kando ya barabara. aliifungua bahasha na kukagua nini kilichomo ndani yake..... alistahajabu kukuta picha alipozitazama zilikuwa ni picha za mke wake akimpapasa karimu..... kamishna alichanganyikiwa uso wake ulionesha kujaa chuki ya hali ua juu... yani karimu huyuhuyu ndio amenisaliti kwa mke wangu??? haiwezekani....alijisemea moyoni kamishna"" kisha akachukua simu na kumpigia mke wake.... mkewe alistahajabu sana jamani mume wangu mimi sijatoka nipo nyumbani tu... alisema mke wa kamishna""...

    kamishna alikata simu na kumpigia karimu.. simu ya karimu iliita bila kupokelewa... kamishna alizidi kichanganyikiwa.....alijiiliza maswali yasiyokuwa na majibu.... mara ghafla simu yake iliita...



    mara ghala simu yake iliita alipoiangalia aliona peter akimpigia... kisha akaipokea simu ile""peter alikuwa akiulizia kuhusu upelelezi wa karimu umefikia wapi..."" kamishna alijibu kuwa atamjulisha kwa sasa yupo na shughuli nyingine hivyo atampigia simu badae......



    ***************



    kule nyumbani kwa peter peter alikata simu ile na kutabasamu.... alipiga simu hiyo kumsanifu kamishna kwani alijuwa wazi kuwa picha zile kaishazipata....... peter alimuita mmoja kati ya watu wake wa kazi....vipi ule mzigo umeshafika?? peter aliuliza" yule mtu alijibu hapana bosi nahisi utaingia saa mbili leo usiku"" ok sawa" peter alijibu.



    usiku ulipoingia peter na vijana wake wa kazi walikwenda Airport.. walipofika peter alionesha nyaraka za migizo ile akaruhusiwa kuchukua mizigo yake..... yalikuwa mabox matatu yaliyo jaa vitabu vya Dini..... kisha vijana wake wa kazi waliyabeba mabox yale na kuyaingiza ndani ya gari.... kisha wakaondoka.....walikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa peter...

    peter alishuka kutoka ndani ya gari"" akaanza kuzipiga hatua na kuelekea upande wa ndani.... wale vijana wake wa kazi waliyabeba mabox yale

    na kuyapeleka upande wa ndani.. kisha wakayafungua na kuvitoa vitabu vile vya dini.... peteralichukua kitabu kimoja na kukifungu kilikuwa kimetobolewa karatasi za ndani katikati"""akutoa pakti iliyokuwa na unga mweupe ndani yake... nakumbe peter mbali na ugaidi pia alikuwa akijihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya



    *************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ule upande mwingine karimu alionekana anaingia nyumbani kwake... karimu alikuwa na mke na mtoto mmoja....alipokelewa na mkewe... kisha akajiandaa kuoga...



    ***************



    palipokucha karimu alidamka na baada ya kumaliza kujiandaa alielekea kazini....alipofika alikuta ujumbe kuwa atakapofika aende kwenye ofisi ya kamishna..... karimu akazipiga hatua kuelekea ofisini kwa kamishna....alipoingia alipiga saluti kisha akaketi... kamishna alitoa ile bahasha na kumpa karimu kisha akamwambia fungua... karimu alipofungua alistahajabu kuona picha zilizomuonesha yeye akiwa chumbani na mwanamke yule""ni nani aliyekuwa akipiga picha hizi!!!!! karimu alijiuliza moyoni.... kisha kamishna akauliza unamfahamu mwanamke huyo???

    karimu alijibu hapana mkuu.. mwanamke huyu aliniita jana MOBI HOTEL....kabla hajamaliza kuongea"""kamishna alidakia na kusema kwa nini umenizunguka na kutembea na mke wangu???

    karimu alistuka... haiwezekani kutakuwa na mchezo mchezo nachezewa!!!! karimu alijisemea moyoni.....karimu alibaki kimya bila kuongea chochote... kutokana na nidhamu mbaya kuanzia leo makusimamisha kazi ya upelelezi hivyo basi utakuwa trafki wa barabarani... toka""" alisema kamishna... karimu alinyanyuka na kutoka ndani ya ofisi ya kamishna.....



    karimu alijiuliza maswali yasiyokuwa na majibu.... lazima kutakuwa na mtu anafanya matukio haya""

    itabidi niwe makini sana na sitoacha kufatilia nilazima nitabaini chanzo ni nini...karimu alikasirika sana aliamua kuondoka na kuelekea nyumbani kwake.



    baada ya karimu kufika nyumbani kwake alikuwa mnyonge sana...kitendo hicho kilimfanya mke wake aingiwe na wasiwasi kwa sababu ajawahi kumuona mumewe akiwa katika hali hiyo... ilibidi amuulize... karimu hakudanganya hata chembe ya uwongo alimueleza kila kitu mkewe.... mkewe alisikitika sana akamfariji kwa kumwambia maneno mazuri...lakini karimu hakuwa anasikiliza maneno ya mke wake..... akili ya karimu iliwaza juu ya kumtafuta mtu aliyesababisha matukio yote yale.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *************



    ule upande mwingine peter alifurahi sana baada ya kupata taarifa kuwa karimu katolewa kwenye nafasi ya upelelezi na kuwa trafki wa barabarani... " yes mambo si ndio hayo sasa nitaweza kufanya bihashara zangu bila bugza yoyote... huyu mtu alikuwa hatari sana amekuwa akifuatilia mambo yasiyomuhusu.... peter alijisemea moyoni"""



    ******BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA*****



    matukio ya kijambazi yalizidi kuendelea.... watu walivamiwa na kuporwa pesa na mali zao.... matukio hayo yalifanyika mfululizo.....na waharifu hawakamatwi wakati sheria na vyombo vya dola vipo.....matukio hayo yalimfanya karimu awe na wasiwasi huenda kunaviongozi wa ngazi za juu wanashirikiana na majambazi.... karimu aliamua kufanya upelelezi bila kushirikisha mtu....siku hiyo majira ya usiku alikwenda bandarini...... alionesha kitambulisho chake getini akaruhusiwa kuingia ndani.....alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye boti mbovu iliyokuwa nje ya bahari... alipanda na kuingia upande wa ndani..... karimu alifanya hivyo ili kujificha asionekane na mtu yeyote aliekuwepo humo ndani ya bandari..... ilipofika majira ya saa saba za usiku kwa mbali aliona meli ndogo ya kubeba mizigo......karimu akawa makini kuangalia kinachoendelea kutokana na giza hakuweza kuona viziri... karimu alitoa kitu ndani ya koti lake na kukivaa usoni kufunika macho yake.... ilikuwa ni

    NIGHT VISIONS "" hiki ni kifaa maalumu kinachovaliwa juu ya macho ili kuona kitu chochote kwenye giza hata kama ni giza totoro... aliona watu wakishusha magodoro kutoka ndani ya meli ile......magodoro yalikuwa mengi kiasi... kisha akaona gari likiingia ndani ya bandari kutokea upande wa nje..... walishuka watu watu watatu... kisha wakayakagua magodoro yale kisha wakayafunga kwa kuyabibanisha matano matano... kisha akashuka mtu mmoja kutoka ndani ya gari... mtu yule alionekana mnene slikuwa amevalia suti ya gharama sana.... alionekana nadhifu..... karimu alimtazama mtu yule kwa umakini wa hali ya juu kisha mtu yule akatoa vibunda viwili vya pesa na kuwapa wale watu walioleta magodoro yale kwa meli.... kisha akaingia ndani ya gari yeye pamoja na wale watu watatu....wakati wanaingia ndani ya gari karimu aliona bastola kwenye kiuno cha mtu mmoja amae alipanda upande wa mbele......karimu alistuka.... akawa na wasiwasi na watu hao..... aliamua kunakili namba za gari hiyo na kuiandika kwenye simu yake.....



    *******CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    palipokucha alidamka na kwenda kazini.... siku hiyo alikuwa zamu kusimamia usalama barabarani kwenye barabara ya kilwa road.......mara ghafla aliiona ile gari aliyoiona usiku wa jana... alipojaribu kufananisha na zile namba alizozinakili kenye simu yake zilikuwa zinafanana....aliisimamisha gari lile akamwambia dereva aoneshe leseni..... dereva akaonesha..... kisha akamwambia aoneshe kadi ya gari...alipoonesha jina la kadi ya gari lilikuwa tofauti na jina la leseni.... karimu akaliandika pembeni jina lililokuwa kwenye kadi ya gari hilo... kisha akaruhusu gari hilo liondoke..... karimu alikwenda mpaka kwenye gari lake akaiwasha laptop yake akalitafuta jina lililokuwa limeandikwa kwenye kadi... ilitokea picha ya peter..... alipojaribu kupekua pekua aliona peter anajihusisha na mtandao wa kigaidi kwa sababu picha ya sura yake ilionekana kwenye matukio tofautitofauti.... aliamua kumfatilia kiundani zaidi........



    **************



    siku moja karimu akiwa barabarani huku amevaa nguo zake za trafki... kunagari lilikuwa likipita barabara hiyo... karimu alilitilia mashaka gari hilo akalisimamisha.... kulikuwa na watu watatu.... akaamuru dereva afungue buti ya gari... mara ghafla..



    Mara ghafla alimuona peter.....karimu akaamuru watu wote waliokuwa ndani ya gari waonyeshe vitambulisho vyao vya kazi...wote wakatoa na kuonesha....vilikuwa vitambulisho halali.....kisha karimu akazipiga hatuana kuangalia ndani ya buti......hapakuwa na kitu zaidi ya tairi moja la gari lililowekwa humo kwa ziada.....alimwambia dereva aondoe gari....wakati gari linaondoka aliona peter anarudisha bastola ndani ya mfuko wa koti la suti..mmmh!! bila shaka hawa si watu wazuri......alijisemea moyoni....kisha akalitazama gari lile kwa macho ya mkazo....mpaka likatokomea.......



    ***************



    ule upande mwingine kamishna alionekana akipokea simu.....alikuwa akiongea na peter...

    peter alimwambia kamishna kuwa karimu kamshtukia kuwa huenda anajihusisha na vitendo vya kigaidi.....kamishna alizidi kuchanganyikiwa"""

    kisha akasema itabidi karimu auwawe bila kufanya hivyo tutastukiwa na tutakuwa matatani pia bihashara zetu zitakwama....peter alimuunga mkono kamisna kisha akakata simu.....peter aliamuru dereva ageuze gari na arudi nyumbani...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***********



    baada ya lisaa limoja peter na vijana wake wa kazi walifika nyumbani. alianza kuandaa mpango wa kumuangamiza karimu....alituma vijana wake wakachunguze karimu anaishi wapi...

    ilipofika majira ya usiku vijana wale walikwenda kuchunguza ni wapi karimu anapoishi....walifanikiwa kuona nyumba ya karimu kutoka kwa kuelekezwa na kamishna...kisha peter akajulishwa kwa simu....



    ************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog