Search This Blog

MZIMU ULIOREJEA - 5

 







    Simulizi : Mzimu Uliorejea

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Bado mawazo yalimsonga ni kwa namna gani angeweza kupata nauli ya kwenda kijijini kutafuta hiyo hazina aliyoambiwa na kaka yake...



    Lakini wazo lingine likagonga katika fikra zake!,



    Hata kama angeenda ni vipi angeitambua njia ya kupata hazina ile!...

    Akaamua itakavyokuwa na iwe ila lazima arudi kijijini,alifurahi zaidi baada ya kukumbuka kuwa kaka yake alimuhaidi kuwa naye bega kwa bega!



    Kumbukumbu hizo zikampa nguvu na hari ya kutafuta nauli kwa juhudi!



    Akutaka kupoteza muda siku hiyo hiyo akazunguka mtaani kutafuta kazi!,akapata katika car wash ya kuosha magari...



    Siku moja ilikuja gari la kifahari,Martin akaisogelea tayari kwa kuiosha!,kioo kikafunguliwa na kuruhusu harufu Kali ya manukato kusikika katika pua za Martin,macho yake yakatua Mbele ya mtoto mzuri,



    Akukumbuka kama alishawahi kukutana na binti Mrembo kama yule au kumzidi tangu amezaliwa,macho yake akabaki ameyagandisha kwa binti yule!



    Ghafla nywele zikamsisimka!,mwili ukaanza kumtetemeka,



    "Kwa jina naitwa Zena bin Kureysh!"



    Sauti laini mfano wa kinanda,lafudhi ya kipwani ikatoka kinywani kwa binti yule!



    "Zena Kureysh?!...."



    Martin akauliza kwa mshangao,wasiwasi ukiongezeka katika fikra zake



    Binti yule akaachia tabasamu jembamba,tabasamu ambalo lilimuongezea uzuri Mara dufu...



    "Ndiyo naitwa Zena Kureysh! Kaka vipi kwani au unanifahamu mbona umeshtuka?!"



    "No..ha...pa.na..sikufa..hamu" Martin akaongea kwa kigugumizi



    Dada yule mwenye asili ya kiarabu akaachia tabasamu tena,bila shaka alitambua udhaifu wa Martin kwake



    Ni uzuri wake



    Akaachana na jambo lile,akaeleza kilichompeleka



    "Ok unaoshaga gari kwa shilingi ngapi?!"



    "Elfu tano tu!"



    Akatamka Martin kwa haraka



    "Ok naomba unioshee naja kulichukua baada ya nusu saa"



    Akatamka Dada yule akifungua mlango wa gari lake akashtuka



    Macho ya watu wote yakageuka kumtazama Dada yule,alivaa nguo za thamani,Vito vya thamani vilivyoendana na uzuri wake



    Dada yule akaenda umbali mrefu alipokuwa mbali na macho ya watu ghafla akatoweka...



    Lilikuwa ni jini lililoagizwa....



    Liliagizwa nini duniani?!.....



    Tuendelee kuwa pamoja



    ********



    ARDHI YA KUZIMU



    Ilikuwa ni sherehe kubwa,katika ulimwengu mwingine wa dunia hii

    Chini kabisa ya ardhi waloishi wafu walodhulumiwa roho zao



    Mizimu,walokuwa na utawala kama wa hapa hapa duniani ila wenyewe waliongozwa na mfalme pamoja na malkia....



    Miaka mingi nyuma kipindi cha ukoloni Chrispher akiwa askari wa kikabila aliwahi kuiona hazina ilofichwa na wakoloni wa kiingreza



    Kwa kutumia nguvu alojaliwa akaiba kiasi kikubwa cha hazina ile na kuificha katika pori panda



    Akaweka ulinzi imara wa kiutamaduni...



    Mpaka wakoloni wanaondoka hawakufanikiwa kuiona hazina ile,Chris alifanya siri hata mke wake alijua...



    Baada ya wakoloni kuondoka wakasajiliwa katika jeshi la wananchi kipindi icho Chriss alikuwa na watoto wawili Brayson akiwa na miaka 7 na mdogo wake Martin akiwa na miaka 4



    Bado aliifanya siri akiogopa kutaifishwa pindi akizitoa Mali zile



    Rafiki yake wa pekee John alikuja kufanikiwa kuiona 'diary' iliyoeleza juu ya hazina ile,japo aikueleza mahali ilipo kwa vyovyote alijua mke wake Christopha lazima atajua mahali ilipo



    Akaanza kupanga njama za kumwangamiza rafiki yake yule...



    Na njama hizo alikuja kuzifanikisha baada ya kupangwa pamoja kwenda Uganda kupigana vita baada ya serikali ya huko kumega kipande cha Tanzania kagera wakisema ipo upande wao



    Wakati vita vikiendelea John alimtwanga Chriss bastola ya kichwani

    Na kuondoka na uhai wake,jambo ilo liligunduliwa na jeshi na John akafukuzwa jeshini bila mafao yoyote



    Tukio lile alilofanya likabaki siri ya jeshi,John akarudi kijijini kwa kuwa alikuwa na dhamira ya kuisaka hazina ile baada ya miaka kadhaa akamuoa mke yule wa rafiki yake alijua anajua mahali alipoifadhi hazina ile!



    Miaka ikasonga akiwanyanyasa watoto wale,mpaka Brayson ( jb) akaamua kutoroka baada ya kumpiga mtoto wa Piter mpaka akazimia



    Baadaye Martin naye akaja kutoroka akakimbilia dar

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    NDIVYO ILIVYOKUWA....



    katika sherehe ile katika kiti cha mfalme aliketi jb akiwa mwingi wa tabasamu, pembeni alipepewa na wanamwali warembo walonukia...



    Kulia kwake alikwepo kijana mmoja shupavu mwili ulijengeka kimazoezi mkononi alishika mkuki na upinde na kushoto kwake aliketi kijana wa dizaini ile ile



    Mbele yake aliketi baba yake Mzee Chriss,naye pia alilindwa kama mwanae...



    Walikuwa wakitazama ngoma zilizojipiga huku wadada warembo wakikatika



    Ghafla mshereshaji akanyanyua mkono juu na ngoma zile zikagoma



    Wadada wale wakainama chini kidogo ishara ya kutoa heshima



    Ghafla vilio vya watu wakilia vikasikika!,watu wote wakashtuka kwa jambo lile wakawa tayari kwa kuusubiri ujio huo



    Vilio hivyo vikazidi na kuwaumiza masikio na ghafla....



    Hali ya hewa ikaanza kubadilika,radi likapiga likitoa mpasuko,upepo mkali ukawa ukivuma na kuepua mapaa



    Gharika



    Likatanda katika ulimwengu wa kibinadamu,ndani ya makaburi ya njoro makaburi yalikuwa yakigawanyika na kuacha ufa



    Ndani baadhi ya makaburi Yale,vilio vile vilivyosikika kuzimu katika ulimwengu wa wafu



    Vilisikika ndani ya makaburi Yale kwa baadhi ya viumbe wenye uwezo wa kuskia



    Hata kumomonyoka na kudidimia kwa baadhi ya makaburi Yale laiti kama binadamu na viumbe vyote vingekwepo si wote wangekuwa na uwezo wa kuona matukio Yale



    Mpaka uwe na jicho la zaidi,au uwe na uwezo wa ziada...

    Makaburi Yale yaliendelea kudidimia ARDHI ikiwabana wafu wale walokuwa ndani yake na kuendelea kuwashusha chini...



    Na ghafla wakatokea kule katika ulimwengu wa kuzimu, ulimwengu wa wafu walodhulumiwa roho zao



    Ulimwengu waloishi wafu hao mpaka kipindi ambacho MUNGU muumba angeamua kuchukua roho zao na kuzipeleka mbinguni...



    Kikawaida mtu akifa kwa kuuwawa au kujiua ni wazi aliidhulumu au kudhulumiwa nafsi yake,



    ivyo roho yake uishi kuzimu mpaka pale siku halali alopangiwa na MUNGU ikifika



    ndipo usafirishwa kuelekea katika mbingu ya saba na kuweka sahii kabla aijarudi tena duniani na kuwa karibu na maiti au mwili wa marehemu



    ambapo uifadhiwa katika makaburi na kusubiri parapanda au siku ya mwisho (ya umul kiama) kama matendo yako yalikuwa mabaya mateso utaanza kuyapata huko huko kaburini na kama matendo yako yalikuwa mazuri pepo ( paradiso) utaanza kuipata huko huko



    Hivyo basi wale wanaotegemea kuwa makaburini ni mahali pa kupumzika si kweli ndugu zanguni,



    Makaburi ni nusu ya pepo na pia kaburi ni nusu ya moto....



    Watu wale walopiga mayowe ndani ya makaburi walikuja kutokea katikati ya mkusanyiko wa watu kule kuzimu katika miili yao wakiwa wamefungwa minyororo kama watumwa



    Miili yao ilijaa funza na kumomonyoka kama udongo usingeweza kuamini kama watu wale miaka kadhaa nyuma walokuwa watanashati na warembo katika ulimwengu wa dunia



    Mfalme mteule jb akaachia kicheko kilichotoka kwa mfumo wa radi na kuacha mwangwi nyuma yake



    Ghafla kimya kikatawala,hata MIZIMU I le ilorejea nayo ikanyamaza kulia



    Mshereshaji akampa nafasi Jb aongee mawili matatu



    "Na shkuru kwa nafasi niliopewa kwanza namshukuru baba yangu Mzee Chriss kwa moyo wake na msaada wake kwangu,mpaka kufanikiwa kuwaangamiza wabaya wangu hawa...



    Akawanyooshea kidole viumbe vile vilivyo lala pale chini



    ...Pili nawashkuru wana kuzimu kwa kuwa na Subira wakati wote nlokuwa duniani kwa kazi maalumu na sasa nimeimaliza na nipo tayari kuwa mfalme wenu na kuwa tumikia kwa kila khali...



    Ghafla miguno ikasikika...



    Alijua ni miguno ya nini!,akatabasamu na kuendelea...



    " ndiyo najua mnachoguna ni juu ya sheria ya himaya hii ya KUZIMU kwamba mfalme lazima awe na mtoto au mke yani malkia atakayerithi ufalme huu ikiwa ntakufa mapema...



    "Ndiyoooo"



    Mizimu ile ikaitikia...



    "Niwatoe shaka kwa ilo na napenda kuwajulisha Mimi sasa ni baba kijacho...."



    "Haaaaaaa!"



    Mizimu ile ikaguna,wengi walimtambua jb hakuwai kuwa na mpenzi hata rafiki wa kike kule kuzimu sasa anawaambia yeye ni baba kijacho kivipi?!



    Jb akawajibu fikra zao...



    "Nadhani nyote mnajua Mimi niliuwawa kwa tamaa za Mali na hawa ndiyo chimbuko la yote haya huyu binti ambaye kakondeana...



    Jb aliongea kwa uchungu akimnyooshea kidole binti mmoja



    " huyu alikuwa mpenzi wangu ila tamaa ya gari na nyumba alohaidiwa na mdogo wangu vikamfanya anisaliti,



    Pili huyu Dada mwenzake naye alikuwa mpenzi wa mdogo wangu huyu ndiyo chimbuko la matatizo yote

    Alimshauri mpz wake aniangamize ili Mali zote zibaki chini yao,huyu ndiye aliyetoa wazo la kumtumia mpz wangu kuiba nyaraka na hati zote...



    Hawa vijana wa nne wanajiita eti 4 killers ndio waloniteka na kuniua kwa kunichoma kisu nami niliwaua hivyo

    hivyo



    na huyu babu Jana ndo nimemuua huyu ni rika na rafiki yake baba mchawi mkubwa alomuua baba yangu akatutesa duniani.



    Pia nadhani wengi mnajiuliza mbona kuna watu wengine ambao hawapo hapa akiwemo kamishna,Chaka na hata mratibu wa mauaji yote bwana Martin



    "Ndiyoooooo"



    "Na pia mnataka kujua juu ya mtoto au malkia wangu si ndiyo?..."

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ndiyoooooo"



    "OK ningependa nianze na swala LA Martin kwanza naomba mtambue Martin ni mdogo wangu wa damu"



    Mizimu yote ikaguna,minong'ono ikaanza



    "Amemuacha kisa mdogo wake hafai kutuongoza ana upendeleo atukuitaji...



    Kelele zikatawala....



    Hali ya utulivu ikakosekana ni wazi jb angetakiwa haukumu wote bila upendeleo



    Kuwa mfalme ingemaanisha hata katika kiti chake angeongoza kiupendelea



    Ni lazima Martin afe kwa kuwa naye aliua tena akiwa mshirika mkuu



    Jb akakosa raha....



    khofu ikaanza kumtanda,akujua angewajibu nini wananchi wake!...

    Macho yake akayagandisha kwa baba yake,baba yake alikuwa kimya,akionekana kuwa katika tafakari kuu...

    mshereshaji akaunyanyua mkono wake juu,kelele,minong'ono ile ikakoma,akamwangalia Jb ni wazi alikuwa akitaka atamke neno!,



    atoe majibu ya maswali ya wananchi wake wale!



    Jb akasafisha koo! na kuendelea...



    "ndiyo! najua mwajiuliza kwa nini sikuwa angamiza Chaka,kamishna na mdogo wangu Martin!"



    "ndiyooo!"



    "kwa sheria zetu za uku kuzimu upaswi kuangamiza asimu ya damu yako! nadhani wote amuijui sheria hiyo itokayo katika familia za kifalme..."



    akaweka tuo na kushika kalmati akang'ata na kushika glasi ya sharubati akanywa kidogo na kuendelea...



    "ila nimemfilisi kwa kumwambia atoe sadaka mali zangu zote kanisani ametii na sasa ni muosha magari,hiyo nisa babu ilonifanya nimwache hai pili,ni kuhusu baba..."



    akaweka tuo tena. na watu wote wakageuza vichwa kumwangalia mfalme wao anayemaliza muda wake...



    "nilikuwa na nia thabiti ya kumuua Martin tena kifo kibaya sana,ila baba alizuia hiyo...



    ni baada ya kuona kama ningemuua mdogo wangu hazina yake isingepata mtu wa kuitumia mkumbuke mama kashazeeka na mwangalizi mkuu ni Martin japo bado ajafika kijijini,ivyo nilimuachia kazi arudi kijijini akaisake hazina hiyo na kuitumia na mama..."



    Mizimu yote ikaridhika kwa jambo lile,Martin kweli alikuwa na haki ya kuishi akimwangalia malkia wao kwa ukaribu zaidi...



    Je vipi kuhusu Chaka na kamishna?!



    ndiyo lilibaki swali la utata! naye Jb akalijibu kwa ufasaha akianza na komandoo Chaka!



    "mkumbuke Chaka alikuwa katika wajibu wake wa kazi!,alotumwa na taifa lake! na nilimwacha kwa kuwa nilimpa onyo akalifatilia na kuacha kunifatilia,mkumbuke Chaka akuhusika na mauaji yangu ila alikuwa akinizuia Mimi kuua na nilipojitoa kwake na kumkanya alinitii je ilo ni kosa wana kuzimu wenzangu



    " hapanaaaaaa"



    Mizimu yote ikaitika kwa pamoja



    "Tuna taka kujua kuhusu kamishna kwa nini umuache hai wakati ndiyo aloshirikiana na Martin kwa ukaribu na yeye ndiyo aliye mwonesha martin kwa mganga Nwalau Nwalau"



    Jb akaachia tabasamu pana likifatiliwa na kicheko chembamba sambamba na kuokota kalmati lingine na kumezea na Sharubati akasafisha koo kidogo na kuendelea...



    "Nadhani mnakumbuka kauli yangu ya awali kuhusu sheria za huku kwetu kuzimu katika familia za kifalme uwezi kuua nasaba ya familia yako damu moja!"



    "Ina maana pia Kamishna ni ndugu yako?!"



    "La asha kamishna si ndugu yangu ila nadhani mwakumbuka niliwaambia kuwa kwa sasa Mimi ni baba kijacho,mtoto wake Maimuna ndo kambeba malkia wenu mtarajiwa hivyo kamishna ni baba mkwe wangu sikupaswa pia kumuua"



    Mizimu ile ikapiga vigelegele,kufurahia jambo lile



    Jb aliwatoa kwenye utata ulogubika vichwa vyao,



    Sherehe ya kumsimika ufalme ikaendelea kama kawaida japo kuna kitu kilimuumiza kichwa



    Ni juu ya malkia wake Maimuna!



    Alitamani sana aishi na mwanamke yule,lakini akujua angeishi naye vipi hali ya kuwa Binti yule alikuwa bado yu hai



    Na kuzimu waliitajika wafu tu



    Wazo la kumuua likamjia kichwani,akulipinga akaita vibaraka wake wawili na kuwatuma duniani waakikishe wakirudi kwenye ardhi ya kuzimu warejee na malkia yule



    Viumbe vile vikatoweka,kuelekea duniani...



    ********



    DUNIANI



    KATIKA ULIMWENGU WA BINADAMU



    Pale pale binti Yule wa kijini alipotoweka Mara ya mwisho ndo hapo hapo alipotokea



    Wapita njia awakuweza kumuona



    Alitembea kwa mwendo wa madaa,hakika alikuwa amependeza na uzuri wake uliongezeka Mara dufu ya awali...



    Alipofika katika kona ya kuelekea katika 'car wash' ile akajiruhusu aonekane,...



    Watu walimshangaa kwa uzuri alokuwa nao....



    Kwa upande wa Martin baada ya kumaliza kuosha lile gari akaenda kuketi katika kiti akisubiria gari lingine



    Ghafla mawazo juu ya yule binti Mrembo yakamjia akatamani angekuwa naye kimapenzi,lakini tabasamu lake likafifia baada ya kukumbuka hali ya umaskin alokuwa nayo



    Laiti kama ingekuwa kipindi chake,kipindi kile akimiliki ma kampuni angeweza kutumia nguvu ya hela kumiliki chombo kile



    Kwanza akaguna



    Alijua fika chombo kizuri kama kile lazima kitakuwa kimeolewa wazo kwamba kiumbe kile ni jini alikuwepo kabisa



    Martin alinasa akanasika



    Kwa Mara ya kwanza akauchukia umaskini...



    Hamu ya kuinasa hazina ile ikamjia lakini wiki nzima alofanya kazi pale nauli aikumtosheleza kabisa



    Hali ilikuwa ngumu,mwisho akayatupia mbali mawazo Yale aloyaona ayatotimia zaidi ya kumfukuzia mteja



    Ghafla akamuona binti yule kwa mbali akija



    Mwendo wake wa kimadaa,akanata akiwa anamwangalia mpaka alipomfikia Martin akajikuta karopoka



    "Zena Kureysh?!"



    "Rabeyka"



    Akaitika binti yule akimkabidhi noti ya elfu kumi Martin naye akamkabidhi ufunguo



    "Ngoja nikupe chenchi"



    "Hapana iyo baki nayo"



    Martin akashkuru na kuitumbukiza mfukoni



    Dada yule akaingia ndani ya gari lake na kumpungia Martin mkono wa kumuaga akaondoka zake



    Alipofika kwenye kona AKATOWEKA!!!



    Martin kila Mara aliinusa ile ela alopewa akiyanusa marashi mazuri ya binti Yule



    Ghafla pikipiki ikaja akashika tenda ya kuiosha ikabidi ile 10000 aiweke mfukoni akaiosha fasta ile pikipiki na baada ya hapo ikaondoka



    Bado kumbukumbu juu ya binti yule zilimtesa akatamani kunusa manukato yake



    Akaingiza mkono wake mfukoni



    Akatoka na bahasha



    Mshangao ukamshika



    10000 aikwepo akatafuta mifuko yote akuiona



    Akazidi kuchanganyikiwa



    Na vipi kuhusu ile bahasha akaiangalia vizuri iliandikwa jina lake kwa mwandiko mzuri kupindukia



    Akukumbuka kama alipokea bahasha ile kwa MTU



    'Sasa imefikaje katika mfuko wake?!'



    Akajiuliza swali pasina jibu sahii



    Ikamlazimu aifungue



    Ghafla akatoa macho Pima,mdomo akauachama wazi,butwaa likambumbukia,mikono ikaanza kumtetemeka,nywele kumsisimka....





    Kwak Martin!



    Bila shaka u mzima,nafrah kwa ilo!...

    Najua unashangaa juu ya barua hii ya kimaajabu ajabu usishangae kwa ili!



    Dhumuni la barua hii ni kikueleza juu ya upatikanaji wa hazina ya marehemu baba yako

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara ya mwisho kaka yako alikwambia urudi kijijini ukujua pa kuanzia!



    Nenda katika kijiji chenu mtafute mganga Nwalau Nwalau yule yule unayemjua yupo kijijini kwa dhihara mwambie waitaji utajiri



    Kuna masharti atakupa yatakayokufikisha katika hazina ile ya baba yako



    Kumbuka hazina ile inalindwa na mizimu kuwa makini katika masharti na ukikosea kidogo kifo ni haki yako



    Wengi walioenda hawakurudi



    Ila kwa kuwa ni haki yako naimani utashinda...



    Kila la kheri



    Ni mimi



    Zena Kureysh



    Martin akashusha pumzi ndefu,akairudia kuisoma ile barua Mara mbili iliandikwa vile vile akaiweka mfukoni



    Ni wazi alikuwa amechanganyikiwa



    Akaingiza mkono mfukoni na kuitoa



    Akapigwa na butwaa,barua aikwepo zaidi ya ile 10000



    Macho yakamtoka...



    Akuona haja yq kumsimulia mtu



    Ni yupi angemuelewa achia mbali kumuamini?!



    Akaendelea na kazi raha ikiwa imemtoweka,akipania kesho yake kuelekea kijijini...na ndivyo ilivyokuwa



    ************



    Hali ya kijiji kile ilibadilika,ukame ulitawala,kwa kuwa Martin alikuwa na kiakiba kidogo akachukua chumba katika nyumba vya wageni



    Akutaka kwenda nyumbani kwao mwanzo alipania mpaka amalizane na kazi ya kuikomboa hazina ile ndo angerudi kwao...



    Kwa kuwa alifika kijijini usiku alipumzika na hasubui alianza kuyatafuta makao ya bibi mganga yule



    Kijijini kile kilikuwa ni kidogo akupata tabu kumpata...



    "Hahahahaha waitaji utajiri?! Utaweza?!"



    "Ndio bibi"



    "Hahahaha kuna hazina ipo katika mapango ya maajabu uko milimani ni wajibu wako kuifuata wengi wameenda hawakurudi ni hatari ha ha ha ha "



    "Nipo tayari bibi"



    Mganga yule akamtumbulia macho Martin,macho ya mshangao



    "Ok kama upo tayari ntakuelekeza,hayo mapango ntakupa dawa ukifika hapo utajipaka usoni na mapango Yale yatageuka na kuwa nyumba ya kisasa kuna ulinzi mkali wa mizimu tafuta njia yoyote uingie huko



    Mizimu ile inahisia sana unaweza ukaendaaa...."



    Mganga yule akamalizia na kumruhusu Martin kutoka kwa kinyume nyume



    Martin akawa tayari kwenda katika mapango Yale



    Aliyajua fika kwani anakumbuka wakati wakiwa watoto walikuwa wakikatazwa kwenda katika mapango hayo waloyaita 'mapango ya mizimu'



    Pia ndiyo yalikuwa mapango yalotambikiwa na waganga na wazee kwa mila zao



    Pindi ukienda kwa nia ya kutambika au kuangalia hayakuwa na shida yalikuwa kawaida tu



    Ila ukienda kwa nia ya Hazina mizimu ile ilijua na kukugeuza kitoweo



    Ni vipi Martin angeweza kuikomboa hazina ya baba yake?!



    Akazidi kusonga mpaka katika pori lile,akawa anaelekea maeneo ya mapango Yale.....



    NDANI YA MAPANGO



    Walinzi wa falme hii kuna binadamu anakuja,kwa ajili ya hazina kuweni makinii,ulinzi uimarishwe



    Sauti kubwa ilisikika katika masikio ya walinzi wale wakawa tayari kumkabili kiumbe yoyote ajaye...



    Martin akujua juu ya hilo,yeye alizidi kusonga moyoni akiwa na amani



    Baada ya kufika katika mapango Yale akaitoa dawa ile na kujipaka usoni akinuidhia maneno machache aloambiwa na mganga na ghafla Mbele yake pakatokea jumba La kifahari



    Walinzi wakiwa pembeni yake,walinzi waloshika silaha ambazo akuziona kabla



    Wazo kwamba ataingiaje likamvaa



    Uwezo wa kuingia kule aukwepo kabisa...



    Ghafla akaguswa nyuma alipogeuka tuu



    Akaachia yowe,yowe lililowashtua mpaka walinzi wale wa Mbele



    martin alikuwa hatarini tena katika mikono hatari ya viumbe vyenye uchu....akabaki akitetemeka akisubiria miujiza



    "Wewe ni nani na unataka nini?!"



    Akaulizwa swali ambalo katu akuweza kulijibu akikumbuka sharti alilopewa juu ya kutofunguwa mdomo wake



    "Na kuuliza wewe ni nani?!"



    Akapachikwa swali lingine kabla maumivu makali ayajatambaa katika mwili wake



    Ni mkia wa taa alochapwa nao....



    "Tuna kuuliza tena wewe ni nani na unataka nini?!"



    "Mimi ni Martin na nataka Hazina"



    Akavunja masharti pasina mwenyewe kujielewa akaropoka



    Viumbe vile vilistaajabu vikamnyanyua mzoba mzoba mpaka ndani kabisa ya jengo lile katika jiko palipokuwa na sufuria kubwa ilochemka mafuta wakamtupa



    akaachia mayowe huku akiporomoka kushuka chini ya mafuta Yale Yalochemka



    Akiacha juu viumbe vile vikishangilia kwa kupata nyama ya kukaanga





    CHINI YA ARDHI



    HIMAYA YA WAFU



    Ilikuwa ni katika hekalu la kifalme,hekalu lililotengenezwa kwa almasi na dhahabu tu!



    Hekalu lililolindwa kwa ulinzi mkali



    Ndani ya hekalu lile katika sebule nadhifu aliketi Mzee wa makamo kichwa chake kilijaa mvi...



    Pembeni yake aliketi mwanaye aliyekuwa kava joho la kifalme na kakaa katika kiti cha mfalme pembeni yake walikwepo walinzi shupavu wenye silaha za jadi,silaha ambazo katika macho ya kibinadamu azikuleta maana kabisa



    Walishika magamba ya konokono,na zaidi ya hapo hata viungo vyao vilikuwa ni silaha tosha



    "Baba lazima nirudi duniani nikamchukue mpz wangu baba siwez ishi mwenyewe humu baba"



    Jb alipeleka ombi lake kwa baba yake...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Vizuri sana mwanangu ila mwenzako kwa sasa kaokoka ni vigumu kumsogelea!"



    "Hapana baba Mimi ni shujaa na kama ni shujaa yule ana kiumbe changu ndani ni lazima nimchukue kumleta huku kuzimu"



    "Sijakataa si una kumbuka vijakazi wako tulowatuma duniani wakamuue Maimuna wailete roho yake aje akiwa mfu awe miongoni mwetu unakumbuka kilichowakuta?!.....



    Jb akarudisha kumbukumbu............



    " pepo maiti nawatuma duniani mkaakikishe mnarudi na roho ya mpz wangu Maimuna ilobeba kiumbe changu,nawaamini na najua amshindwi na kitu"



    Baada ya jb kuongea vile roho zile zikatoa heshima sambamba na kutoweka eneo lile...



    Vilikuja kutoka juu ya makaburi yao,ilikuwa ni vigumu kwa binadamu wa kawaida kuviona vikatoweka tena vilikuwa vikimsaka MAIMUNA....



    BARABARA YA KIBOROLONI



    PEMBEZONI YA KANISA ANGlKANA



    Wadada warembo wawili walikuwa wakipita njia huku wakiwa bize kwa stori,mmoja hapo akiwa ni Maimuna mtoto wa kamishna na mpz wa Jb



    Wakiwa maeneo ya uwanja mkubwa wa kanisa wakiendelea na safari yao ghafla kizunguzungu kikali kikamvaa Mai,na kumpeleka chini



    Watu wote waliokuwa katika kongamano lile la dini wakageuza vichwa vyao kumwangalia mtu yule alodondoka na kupiga makelele



    Mchungaji akaagizwa apelekwe Mbele yake,bado Mai alilia moto vijana kadhaa wakambeba na kumpeleka Mbele ya mchungaji



    "Ni nani nyinyi?!" Mchungaji yule akamuuliza Maimuna



    "Sisi ni pepo maiti "



    "Mnataka nini katika mwili huu"



    "Roho yake"



    "Mmetumwa na nani?!"



    Maimuna akabaki kimya



    Mchungaji akauliza tena mmetumwa na nani?!



    Pepo wale bado hawakuwa tayari kuongea...



    "Sasa nawahamuru kwa jina la Yesu christo mwachieni huyu Dada na mrudi mlipotoka toka toka kwa jina la yesu christo toka...."



    Maimuna akazidi kupiga kelele moto,moto ni wazi hakuwa yeye ni pepo wale walotumwa na jb



    Baada ya dakika chache Maimuna akatulia na pepo wale wakatoka



    Alipozinduka alikuwa mzimaaa mzima wa afyaaa



    Waumin wakaanza kuimba



    "Mwambie farao nimeokoka sitorudi nyuma tena naenda kwa bwana...



    Mwambie farao nimeokoka sitirudi nyuma tena naenda kwa bwana"



    Kwa nzia siku hiyo Maimuna akaokoka na kuwa mwinjilisti mzuri katika kanisa lile



    KUZIMU



    HIMAYA YA WAFU



    Ghafla mapepo wale wakiwa wanapiga kelele miili yao ikiwa imeungua kwa kuchomwa moto ikatokea Mbele ya jb na baba yake



    Wakatoa heshima kwa mfalme na kuwaeleza kilichowakuta...



    "Ina maana Maimuna kaokoka?!"



    Jb akauliza kwa mshangao



    "Yah ndo jibu hilo na kiumbe chako kipo hatarini"



    "Hapana baba nitarudi duniani kupambania damu yangu haiwezekani"



    Akazidi kumsisitizia baba yake baada ya kukumbuka akatingisha kichwa kwa masikitiko makubwa sana



    "Mwanangu jb yule sasa ana nguvu kuliko wewe au kuliko sisi kitabu akishikacho akikunyooshea kuna uwezo mkubwa wa kupoteza maisha"



    "Ila kumbuka ananipenda baba"



    "Alikupenda kipindi ulipokuwa ujajifunua kwake kama mfu ila sasa si rafiki yako tena"



    "Hapana ntaenda duniani kuikomboa nafsi yangu ntajivunia na nini kama mfalmeee....



    Kabla ajamaliza kuongea kikasikika king'ora kikipiga kelele



    Ishara ya hatari



    "Kuna nini tena?!"



    Baba jb akiwa anatetemeka akaoji



    "Hata sijui" jb akamjibu



    Walinzi walikuwa tayari kwa lolote na ghafla......





    Na ghafla viumbe vyeusii tii,vyenye pembe katika vichwa vyao vikatokea



    Vilikuwa kama vitatu,kutokea kwao muda huo huo vilishawekwa kati na walinzi shupavu wa Himaya ya KUZIMU



    Ila baba yake Jb alipoviangalia akavitambua na kukumbuka miaka kadhaa nyuma wakati akiweka mazindiko katika hazina yake



    'Si ruksa Mali hii kuchukuliwa na kiumbe chochote isipokuwa watoto wangu wawili Brayson au Jb au mke wangu! Kiumbe chochote kitakachoitaji kiangamizwe katika sufuria la mafuta"



    Baada ya Mzee yule kutoa maelezo yake na kuachia mizimu kulinda wazo Fulani likamjia



    Kwa kuwa kazi aliitoa kwa mzimu mkuu wa pango lile,alijua kwa vyovyote watakao kuwa lindoni ni mizimu tofauti tofauti kutokana na miaka itakavyoenda



    Na si wote watakaowajua wanaye!,wazo flani likapita katika kichwa chake



    Kuweka ulinzi mwingine wa siri ambao mizimu ile isingejua uwepo wao



    Pia hii ingesaidia hazina ile kuwa salama zaidi!



    Na ndio akavipachika viumbe vile vitatu,viumbe ambavyo vilikuwa Mbele yao muda huo vikija kwa king'ora



    "Waacheni nawafahamu"



    Baba jb akatoa amri,walinzi wake wale wakatawanyika na kurudi kila mmoja eneo lake



    "Ehe kipi kikichotokea katika hazina yangu ewe viumbe Wang watiifu"



    "Mtoto wako Bry yupo hatarini"



    "What?!!"



    Jb na baba yake wakashtuka kwa taharifa zile baba Martin akamwangalia jb kwa kumsuta...



    "Nisamehe baba!,nilipitiwa na kichwa changu kilikuwa na mawazo juu ya malkia wangu nikaacha kufatilia maisha ya mdogo wa ngu juu ya kuifata hazina ile



    Mara ya mwisho nilimuachia kazi zena binti Kureysh amwambie mahali ilipo hazina



    Baba Martin akusema kitu akanyoosha mkono wake wa kuume juu katika ukuta na kutoa shoti sambamba na kuachia cheko Kali



    Katika ukuta ule ikaonekana picha ya Martin akiwa kabebwa mzoba mzoba na kupelekwa katika sufuria lichemkalo moto akatupwa mule



    " noooooooo"



    Wote wakapiga kelele,ila baba mtu akaunyooshea mkono sufuria ile na ghafla Jb kule ndani akanata



    Akaunyanyua mkono wake kwanguvu kwenda juu,na ghafla Jb akatupwa juu ya sufuria ile...



    Baada ya tukio lile mzee yule akatoweka na kuacha walinzi na Jb wakibaki na mshangao...



    "Lazima nirudi duniani kumkomboa malkia wangu"



    Jb akala kiapo,mapenzi yana nguvu,akumuwazia kabisa mdogo wake...



    Yeye alikuwa kwa Maimuna muda ule ule baada ya baba yake kutoweka naye akatoweka



    Viumbe vile vilivyobaki vikajua kamfata baba yake kumbe kayafata matatizo....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Matatizo makubwa ambayo ayakuwepo katika uwezo wake....



    ************



    HIMAYA YA MAPANGONI



    PALIPO NA HAZINA



    viumbe vile baada ya kumshusha Jb katika sufuria lile vikaachia cheko



    Mate ya uchu wa kula nyama yakawatoka,ni takribani miaka mitatu awakuonja nyama katika pango lile



    Wakati wakitingisha vichwa vyao ghafla tetemeko Kali la ardhi likawatetemesha na ghafla macho yao yakatua ndani ya sufuria ile...



    Walishughudia kiumbe kile kimenata chenyewe,wakiwa bado wametawaliwa na bumbuwazi wakakishughudia kikirudi juu



    Wakatokwa na mayowe jambo kama ilo alikuwahi kuwatokea kabla

    Wakajua wameshaingiliwa na hadui wakawa tayari kukishambuliwa kabla awajapata amri ya kuachia Mara moja kutoka kwa mfalme wao



    Mfalme wa mapango Yale!



    Ni baada ya baba Martin kupotea akaja kutokea ndani ya mapango Yale Mbele ya mfalme mwenzake alompa dhima ya kuilinda hazina ile



    "Nadhani umesahau juu ya watu wa aina tatu niliokwambia ndio walostahili kuimiliki au kuwa na ruksa ya kuchukua hazina ile"



    "Salam kwanza baba Martin!"



    "Salam gani wakati vijakaz wako wanataka kumtafuna mwanangu ndo maelewano yetu? Kwa nini ukuwapa taharifa ?!"



    Mfalme wa mapango Yale akashtuka...



    Akayatoa macho yake makubwa na kutazama eneo lilipo sufuria lile akashughudia vijana wake wakiwa tayari kumshambulia Martin akapaza sauti kuwaamrusha waache



    Nao wakamtwiii



    "Naomba msamaha Mimi kaka sikuwapa taharifa juu ya kuja kwa kijana wako lakin nawe swaiba ni msiri sana"



    Wote wakaangua kicheko wakielekea maeneo alipo Martin



    **************





    **************



    Jb alikuja kutokea katika nyumba aloishi Maimuna,ghafla akashtuka baada ya kuiona ni bahari na nyumba aikwepo



    Akaachia kicheko hafifu,alijua ni mchezo,akanyoosha mkono wake katika bahari ile tayari kwa kuipiga kombora



    Miale ya radi ikapiga kutoka mbinguni Jb akarushwa usawa wa bahari ile



    Yowe likamtoka



    Maji Yale yalikuwa yakichemka....



    Kwa Mara nyingine tena Jb akawa kaingia SEHEMU ambapo siyo



    Ghafla akaanza kuzama chini ya maji Yale,akazidi kupiga mayowe



    MUNGU tu aliamua kumuonesha nguvu zake azipambanishwi na kitu chochote





    Jb alipiga kelele akinyoosha mikono yake juu,ghafla akatupwa nje ya bahari ile...



    Mwili wote ulilowana kwa jasho,baada ya kutupwa muda ule ule akatoweka kurudi katika ulimwengu wao



    Bado mawazo yalikiumiza kichwa chake!,ni vipi ataweza kimmiliki Maimuna?!



    Na kiapo alishakula,alikosa raha,



    "Ina maana Mimi kwa MUNGU ni hadui?!,iweje asiwe upande Wang!"



    "Yah! Wewe kwake ni hadui,ni lipi jema ulilomfanyia wewe amewafundisha kusamehe wewe umeangamiza viumbe vyake vingapi?!



    Kwa nini ulipize kisasi?!"



    Kuna sauti ikamjibu,sauti takatifu,Jb akazidi kukosa raha



    "Hapana,ndiyo natakiwa nifanye kitu kumrejesha hapa May lazima"



    Akaachia tabasamu dogo lililobadilika na kuwa cheko...



    Alishapata jibu!,kipi cha kufanya...



    Sasa alihisi MAY ni wake ikiwa atafanya vile alivyowaza....



    Ni nini?!....



    *********



    Martin alishangaa viumbe vile vikitawanyika tena vikionekana kuwa na waswas,ghafla wazee wawili wqkatokea...



    Mmoja akiwa na nguo za kifalme, na vile viumbe vyote vikatoa heshima,hakuwa na shaka kuwa yule ndo mfalme wao



    Macho yake yakadondokeq kwa Mzee mwingine,akashtuka...



    Sura yake ilishabiana vikubwa na ya mtu yule,alikuwa ni baba yake...



    "Dah akuna haja hata ya kuntambulisha kwa mlivyofanana,ni mwanao copyright"



    Yule alovaa nguo za kifalme akasema maneno Yale yalomshtua Martin,alihisi yupo ndotoni baba yake?!



    Akabaki kamtumbulia macho Mzee yule kwa mshangao,akubahatika kumuona akiwa na akili kwani yeye akiwa na miaka mitatu kasoro baba yake yule ndo alikufa vitani...



    "Karibu mwanangu na pole kwa matatizo yalokutokea duniani amini sasa yamefika mwisho...



    Aliongea baba Jacob, akimnyanyua na kwenda sehemu nzuri ya kuongelea...



    Martin akakabidhiwa rasmi hazina ile,akionywa kutokumuonesha au kumruhusu mtu mwingine kuja kuichukua labda mwanae au mke wake

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaoneshwa njia rahisi za kupitia,kuipata hazina ile....



    BAADA YA SIKU CHACHE



    Martin alirudi kwenye ile hadhi yake,tena zaidi akimiliki kampuni ya uuzaji na usafirishaji madini



    Akawa mmoja wa matajiri wakubwa nchini Tanzania,japo mpaka muda huo akuwa na mke na akutaka kukurupuka,

    Baada ya kufanikiwa alienda yalipo makazi ya mama yake,japo awali alimuogopa ila kwa kuwa hakukuwa na nguvu za Giza alimwelewa na mama akamuomba mtoto msamaha



    Martin akawajengea nyumba nzuri kijijini,maisha ya mama yake yakabadilika,akawa akienda kijijini anafikia nyumbani kwa mama yake



    Kabla ajaelekea msitu wa panda..



    ambapo alipitia njia alizoelekezwa na kuchukua kiasi cha hazina,...na kurejea nacho mjini



    Akazidi kujipaisha,wanawake mbalimbali wakijigongesha akiwemo mke wake alomsaliti siku kadhaa baada ya kufilisika



    Martin hakuwa tayari kwa ilo,alifunga akimuomba MUNGU ampatie mke mwema....



    Kila umuombapo yeye kwa nia dhahiri ukujibu muda huo huo,siku chache baadaye jibu lake lilapatikana....



    Kivipi?!!!......



    **********



    Mwanamke yule alikuwa mchafu ombaomba,mawazo yalijaa kwenye kichwa chake alitembea pasina kuangalia barabarani



    Gari la kifahari,Martin alikuwa ndani yeke akiwa anasinzia,dereva naye alikuwa mbali kimawazo katu akumuona binti yule alikuja kushtuka akiwa hatua chache kumfikia na alipojaribu kupiga breki alishindwa



    Akamgonga binti yule ombaomba na kumtupa hatua kadhaa,akiachia yowe



    Martin akashtuka na kuyatoa macho kwa mshangao,



    "Godluck my frandy umeua?!"



    Martin akapaza sauti,God akusema kitu mikono aliweka kichwani,



    Martin akafungua mlango na kutoka akipishwa njia na watu waloanza kuzingira eneo lile,akausogelea mwili ule...



    Ghafla Martin akapiga yowe baada ya kuiona mwili ule,aliufahamu fika...



    Martin akatoa macho ya mshangao,mdomo akauachama wazi,ishara ya mshtuko



    Akamuinamia mtu yule na kumuinua kidogo akaweka mkono wake katika shingo yake...



    "Ja..ja...Janeth my d ni w..ew"



    Akapaza sauti,Dada yule akayafungua macho yake kwa shida



    "Ni na..ni we...we" huku akijitahidi kukuumbuka akamuuliza,ni wazi sauti ile aikuwa ngeni maskioni mwake



    Cha ajabu sasa hata raia walio onekana ni wenye hasira Kali walipigwa na butwaa baada ya kuona wawili wale wanajuana



    Alikuwa ni Janeth yule yule ambaye Martin aliichakaza familia yao kwa kutembea na mama mtu hadi watoto miaka kadhaa nyuma,wakiwa matajiri Leo hii mbona Kurwa au Janeth alikuwa katika hali ile?!



    Hakuwa na muda wa kuliuliza lile baada ya kushtushwa na minong'ono ya watu ndo akatambua mgonjwa alistahili kupelekwa hospitalin



    Akisaidiana na God ambaye alikuwa ndo dereva wake,wakampakia katika gari na safari ya kuelekea hospital ikaanza dakika chache walikuwa katika hospital kubwa ya kcmc kwa kuwa Martin alikuwa na hela Janeth akapewa chumba cha 'vip' chenye huduma nzuri



    Hali yake ilikuwa ni mbaya na alikuwa katika nusu kaputi,mwili ukichunguzwa aliitajika kufanyiwa operesheni ya kiuno kwani kilivunjika....



    'Jamani Janeth ni kipi kilimkuta?' Martin alijiuliza pasina majibu,akubanduka hospitalini pale....



    ***********



    Maimuna alimaliza kula baada ya kumaliza akaiendea "biblia" yake na kuichukua akaanza kuisoma taratibu,na kukariri baadhi ya vipengele,masaa mawili yakakatika akiwa pale kwenye kochi



    Ghafla nywele zi kaanza kusisimka ni baada ya Jb kutokea nje ya nyumba yake na kuiona bahari



    Kitendo cha nywele kusisimka na woga kumtawala kikamfanya aanze ibada Mara moja akaanza kukemea,alijua lazima kutakuwa na viumbe vibaya



    Ni wakati akiomba Martin akapiga pigo moja lililomvuta mpaka katika maji Yale na kuanza kuzamishwa,katika maskio yake Jb alimsikia Mai akiomba kwa kukemea...



    Ghafla akaacha,alikuwa kamaliza maombi, ndo pale Jb aliporudishwa nje ya ziwa lile lenye maji ya moto,hamu ikamuisha Jb akatoweka



    Amani ikautawala moyo wa binti yule,furaha ikarejea alitambua wazi m'baya wake kakimbia japo akujua ni kiumbe gani mchawi,shetani,mzimu au pepo wachafu

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaimba wimbo wa mapambio na kukiendea kitanda chake akajilaza...



    "Nahisi kuna msukumo Fulani katika moyo wangu wa kumtumikia MUNGU na kuwa mchungaji lazima kesho nikaongee na mchungaji wangu"



    Akajiwazia,ndio hamu kubwa ya kumtumikia bwana ilimuingia,aliitaji kuachana na kazi ile ya u polisi...kila tarehe yake ya kwenda zahanati ilipofika alienda na mtoto wake aliendelea vizuri alifurahi kwa ilo....



    UPANDE WA PILI KWA MCHUNGAJI TIMOTHEO



    Mchungaji wa kanisa anglikana,bwana Timotheo siku hii alikuwa peke yake katika kanisa lake akiendelea kuomba,alifumba macho yake akaomba na mwisho wakati anamalizia akasikia sauti nyuma yake ikiitikia ameen



    Sauti nyororo,sauti nzuri,akageuza kichwa chake nyuma kumwangalia yule alooitikia akayatoa macho kwa mshangao,alikuwa ni binti Mrembo ambaye akuwa miongoni mwa watumishi wake



    Akumjua kabisa



    Akabaki kaduwaa



    "Asifiwe Christo"



    Dada yule akamsalimia,...akiacha kulitaja jina la yesu



    "Milele amina karibu katika kanisa langu"



    "Asant mchungaji nimekuja naitaji maombi mchungaji sina raha katika ndoa yangu nimeenda hospitalini kupima sina tatizo nahis tatizo lipo kwa mume wangu tupo katika ndoa kwa miaka 3 atujabahatika kupata mtoto kwa waganga nimeenda sijafanikiwa nisaidie mchungaji....."



    Mchungaji yule akamwambie apige magoti naye akaanza kumuombea,wakati akiendelea na maombi mlango wa kanisa lile ulifunguliwa akaingia binti mkononi akiwa na biblia yake



    Alikuwa ni maimuna kila hatua alokuwa akipiga nywele zilimsisimka,mapigo ya moyo yaliongeza kasi ya upigaji



    Ni wazi kuwa kule ndani au nje ya kanisa lile apakuwa salama



    Ni kwanin?!



    Ndani ya kanisa akuamini kwa kuwa alijua kitu kibaya,pepo mchafu aingii katika nyumba takatifu wazo lile likamsukuma kuamini pepo mbaya yupo nje



    Msukumo mkali ukamsukuma kurudi nje,yah ni msukumo wa shetani, ila msukumo mwingine ukamwambia aendelee na safari....



    Ila akaona kutoka ndo vizuri zaidi!,



    Kumbuka ndugu msomaji!



    MUNGU baada ya kumuumba Adamu,na kuwaambia malaika wote wamsujudie adamu wote wakamtwii MUNGU wakamsujudia nabii adamu kasoro ibilisi naye pia kipindi icho alikuwa ni malaika aliemtwii MUNGU



    Akakataa katakata na kusema



    "Mimi umeniumba kwa moto huyu umemuumba kwa udongo,iweje nimsujudie hali ya kuwa utampeleka katika dunia na kuiharibu kwa kumwaga damu?!"



    Baada ya ibilisi sheitwani kwenda kinyume na maamrisho ya ALLAH



    MUNGU akamfukuza na kumuweka mbali na Rehema zake,na kumwambia wazi atakuwa katika moto wa jehannam,hapo ibilisi alicheka akamuomba MUNGU basi ampe nafasi ya kuwahadaa binadamu ili apate wafuasi wa kuingia nao motoni



    MUNGU alimkubalia,hivyo ibilisi alitumia njia hiyo kuhadaa katika nafsi ya MAIMUNA ibilisi alimsihi arudi nje,lakini MUNGU alimsihi aendelee Mbele



    Mai akiamini pepo awezi kuingia kanisani na uishia nje akaona atoke



    Kosa kubwa sana!...



    kitendo cha kutoka tu,binti yule aliyeitaji mtoto padri aliyeendelea kuomba akajifanya amepandisha mapepo akajidondosha



    Na kujifunua akaanza kupiga kelele padri akafungua macho



    Akapatwa na mshtuko,macho ya tamaa yakamvaa,ibilisi akamzidi nguvu



    Akabaki ameganda....



    Wazo Fulani la kumwingilia binti yule ambaye akumuona kabla likamjia naye akafanya ivyo.....



    Ndani ya lile lile kanisa lake



    Ghafla alama ya 666 ikajichora katika paji lake la uso



    Akuiona,wakazidi kufurahia tendo lile mpaka walipotosheka



    "Nenda na utapata mtoto"



    Mchungaji yule akamwambia Dada yule alokuwa muda wote akitabasamu



    "Asante mchungaji"



    "Jina ulisema unaitwa nani vile?!"



    "Zena bint Kureysh"



    "OK"



    Zena akavaa vizuri na kuanza kuondoka,ghafla akaachia cheko,cheko lililomshtua mchungaji timotheo ,na kutoweka



    Mchungaji akashtuka na kutoielewa hali ile...bado alama 666 lilikuwa katika paji lake la uso





    Baada ya mwanamke yule kutoweka ghafla,mchungaji yule akaanza maombi,..ya kukemea

    Nguvu aliyokuwa nayo kabla ajafanya mapenzi na binti yule hakuwa nayo tena...

    Akukawia kugundua hilo

    Tayari ibilisi alishamuorodhesha katika watu wake,ilikuwa ni furaha ya JB,kwani kazi yake iliendelea vizuri...



    Hata jumapili katika ibada alipopanda ilikuwa ni tofauti na siku zote,taratibu waumin wakaanza kupungua na kumkosesha raha mchungaji yule....



    Siku hiyo akiwa katika chumba chake kidogo,ofisi alitembelewa na mgeni



    Alikuwa ni jb,akakaribishwa vizuri na kuketi...



    "Mimi kwa jina naitwa Jacob nimekuja kwako mtumishi nipate kukurudishia nguvu zako ikiwa utakubaliana na matakwa yangu"



    Mchungaji alashtuka,na kumkazia jicho



    Aliitaji sana kurudi pale alipokuwepo,



    "Matakwa gani muheshimiwa?!"



    "Saf sana,kuna mtumishi wako mmoja mgeni mgeni anaitwa MAIMUNA atakuja kwako kukuomba awe mchungaji usimkatalie na badala yake nitakupa fedha utakazomfungulia kanisa,wewe saivi utakuwa unatumia nguvu zetu ningependa naye umshawishi mpaka akubali kuwa pamoja nasi"



    Mchungaji akuwa Mbishi akakubaliana na jambo lile,Jb akageuka upande mmoja na ghafla brufcase likatokea katika mkono wake akaliweka katika meza ya mchungaji yule.



    Akalifungua!



    Timotheo akatoa macho kwa mshangao,hizi ni ela chache sana milioni 150 ni kwa ajili ya matumizi na uanzaji wa kanisa chukua Pete hii pindi ukiniitaji utaipuliza Mara Tatu na usiache kuivaa...



    Wakati wakiendelea na maongezi ghafla hodi ikaskika......



    "Ndo huyo anakuja"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda ule ule JB akatoweka......



    **********



    Bado hali ya Janeth ilikuwa mbaya!,baada ya uchunguzi kukamilika daktari akamuitaji Martin ndani katika ofisi yake...

    "Pole sana bwana Martin kwa tatizo lililokusibu,mkeo amepata athari katika kiuno chake na kwa bahati mbaya amevunjika sehemu mbaya atoweza kutembea"



    Martin akuamini kile akisikiacho,moyo ulimpasuka alishindwa kuyazuia machozi kumtoka



    Alijua dereva wake ndiye aliye mpa ulemavu mpz wake akukubaliana na matokeo Yale akaadhimia kumsafirisha mpaka India



    Kila alipomuona mwanamke yule machozi yalimtoka



    Bado alitamani kujua kilichotokea mpaka akawa akiishi katika maisha Yale ya ufukara na kuomba omba



    "Martin mpz wangu ni story ndefu ila nimeteseka sana Mimi na sijui nitaishi vipi na ulemavu huu....



    Janeth akashindwa kuongea akaangua kilio,Martin akaanza kumbembeleza na kumuaidi kuwa lazima atapona tu,kwa Janeth ilikuwa ni kama ndoto za alibacha....



    " wazazi wangu na pacha wangu Jenipha walikufa katika ajali ya pamoja!"



    "What?!"



    "Ndiyo Martin na ndugu zangu upande wa baba,kina baba mdogo wakanidhulumu Mali na kupelekea Mimi kuwa ombaomba,mwingi wa mawazo"



    "Basi usilie mpz madamu tumeonana kila kitu kitaenda vizuri"



    Martin akaanza kuangaikia usafiri wa kumpeleka mpz wake yule India...



    Baada ya kukamilisha kila kitu safari ya kuelekea India ikafuata,tumaini la Janeth kurudi katika hali yake ya kawaida lilikuwa dogo sana



    ************



    Baada ya hodi kusikika Mara ya kwanza mchungaji hakaruhusu Maimuna aingie



    Binti yule naye pasina wasiwasi akakishika kitasa na kukifungua akaingia....



    Ndani alipokelewa na tabasamu pana la mchungaji Maimuna akatabasamu,na kwenda kuketi



    "Mchungaji kuna msukumo mkali unanisukuma natamani sana kuwa mtumishi, kumtumikia MUNGU katika mataifa mbali mbali"



    Mchungaji akatabasamu...



    "Maimuna unajua wewe ni Mrembo sana natamani ungekuwa mama mchungaji nimeiona kipawa chako.....



    Aliongea mchungaji akisimama na kuuendea mlango....



    Akaufunga



    Maimuna akashtuka kwa kauli ile,akuamini kile akisikiacho



    Alikuwa ni mjamzito na watumishi wote walijua ilo,iweje mchungaji ampende?



    Akabaki kaduwaa



    Ile ilikuwa ni janja ya shetani kumuingiza katika maovu



    Kama jini Zeyna Kureysh alivyomuhadaa mchungaji...



    Ghafla Maimuna akahisi mikono ikitambaa katika matiti yake huku akilambwa katika shingo yake



    Akabaki ameganda



    Mchungaji alikuwa nyuma yake



    Kuna hisia mbili tofauti zilikuwa zikishindana katika moyo wake



    Hisia moja ikim'force' akemee,ila hisia ingine ilimbembeleza amuache mchungaji yule asiye na mke amchezee,bila kujua kuwa kumuacha kufanya vile ni kuvunja amri ya sita



    Kuwa mbali na makatazo ya Allah!



    " wacha bhana kwanza utakuwa mama mchungaji, Pili utakuwa karibu zaidi ya kanisa Mara moja si mbayaaaa....."



    Ibilisi alizidi kumsii



    "Kemea kwa jina la yesu,usikubali uchezewe MAIMUNA kuwa mbali na shetani huyo....



    Kauli ingine ikasikika pia



    Mai akawa katikati,akashindwa kumzuhia mchungaji na kumuachia



    Taratibu miguno ya kimapenzi ikamtoka



    Alizidiwa na hisia....



    Mwili wake ulimtetemeka kwa hasira,machozi yalimtiririka ila ilikuwa ana jinsi zaidi ya kukubali matokeo



    Japo alimpenda sana Maimuna ilibidi akubali mchungaji afanye naye kitendo kile kiovu ili avunje nguvu zake...



    Dakika chache baadaye ndani ya kanisa,ndani ya nyumba takatifu viumbe wale wawili walikuwa wakiivunja amri ya sita



    Kwenda kinyume na maagizo ya MUNGU wetu



    Katu hakujua kuwa katika paji lake la uso tayari salama 666 zilishajichora,alama ambazo zilimdhibitishia kama mfuasi wa shetani



    Na hata baada ya tendo lile,lilimbadilisha kabisa MAI na kuwa mtu mwingine...



    Siku chache baadaye akafunguliwa kanisa kubwa na kuanza kuhubir neno akitumia nguvu zile alizopewa



    Nguvu hasi!,kutoka kuzimu



    Akazidi kupata watumishi,umaharufu ukaongezeka



    Mpaka anajifungua Mai alikuwa mtu mwingine kabisa



    "Hivi karibuni ntamleta Mke wang na mwanangu"



    Jb aliwaza akiwa katika kiti chake cha enzi



    *********



    Moyo wake ulimuuma baada ya daktari kumdhibitishia kuwa hatopona tena



    Japo hali ya kiafya ilikuwa ni nzuri aliamua kumrudisha nyumbani Tanzania



    Hapo ndipo Martin aliposikia juu ya mchungaji mmoja anayeponya,moyo ukamtuma akajaribu kuonana naye...



    Katu akujua kama ni shemeji yake,baada ya MAY na Martin kuonana kwa Mara ya kwanza MAY akamdhihirishia Martin kwamba MUNGU yupo



    Japo ni kwa nje tu,ila uponyaji ulitebdeka katika mwili wa Janeth



    Na kwa Mara ya kwanza Janeth akarudi katika furaha yake



    Siku chache baadaye wakafunga ndoa kati ya Janeth na Martin



    Na miezi kadhaa Mbele tayari Janeth alibeba ujauzito



    Baada ya miezi tisa wakapata mtoto wa kiume Martin akampa jina la kaka yake Brayson la ubatizo na JB la nyumbani kama zawadi kwa kaka yake



    Furaha ikatawala katika mioyo yao na amani pia....



    **************



    TAMATI



    Ni ajali mbaya ilotokea njia panda,ya Moshi,ilikuwa Maimuna katoka rombo kuubiri neno



    Maimuna na mtoto wake walifia pale pale,kwa macho ya kibinadamu...



    Wengi wa waumini wake walilia,wengine walipoteza fahamu...



    Hayo yote yalijiri katika ulimwengu hai wa kibinadamu ila katika HIMAYA ya KUZIMU mambo yalikuwa tofauti



    Sherehe kubwa ilifanyika ya kumpokea malkia wa kuzimu!



    Maimuna akiwa kava shela lililomkaa vyema mkononi akiwa na mwanaye walikuwa wakiwasili rasmi kuzimu!



    Moyo wake ulijaa amani na uwoga ulimtoka...



    Furaha ilimtawala

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku chache baadaye wakafungishwa ndoa na kuyaanza maisha upya kwa furaha na amani tele



    Wakisubiri siku halali ya MOLA wao kuzitwaa roho zao



    Bado zilikuwa ni nafsi zilizoishi...



    Huo ndo ukawa mwisho wa Jb kurudi duniani...



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog