Search This Blog

BINTI WA PILI WA MFALME - 2

 







    Simulizi : Binti Wa Pili Wa Mfalme

    Sehemu Ya Pili (2)



    Harusi ilishaweza kuanza na ulikuwa ni wakati wa Mozah kuweza kuweka kauli yake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mtabiri Tambitambi: binti wa pili wa mfalme Nuhu wa kijiji hiki cha Isambala Mozah Nuhu, je upo tayari kuolewa na Hancy kijakazi kutoka katika kijiji cha Isadora....kumfanya mume wako katika shida na raha, tabu na furaha, huzuni na majonzi, njaa na shibe na ukienda tofauti na hivyo basi uadhibiwe na miungu wa Isambala? Kama ndiyo sema ndiyo kama hauko tayri sema hapana"





    Mozah alimtizama Hancy aliyekuwa akiisuburia kauli yake kwa hamu, akamtizama baba yake, akamtizama mama yake stelah akamtizama bibi Yake Lunde na kurudisha tena macho kwa Hancy.



    "Ndiyo" alijibu Mozah na hapo hapo ikisikika sauti ya kike ikisema hapana.



    "Mama" aliita Hancy kwa mshangao.



    "Hapana haiwezekani inawezekanaje ukamuoza binti yako kwa mtoto wa mfalme pasina taarifa zozote zile katika mji wao?? Aliuliza mama yake Hancy na Hancy akijaribu kumpotezea mama yake kile alichokuwa akizungumza.



    " Mfanyakazi mjinga sana wewe Tomimo " alizungumza mama yake Hancy na kwenda kumpiga kibao Tomimo ambaye alipiga magoti chini na kuomba msamaha.



    "Samahani malikia wangu ila nimefanya vile alivyoweza kupendekeza mtoto wa mfalme" alizungumza Tomimo.



    'M...m.....mtoto wa mfalme aliuliza malikia Samela na kuwa kama ambaye hajaelewa.



    "Nani mtoto wa mfalme wa Isadora kati ya wewe na wewe?? Aliuliza Samela.



    " Naitwa Malikia Maua kutoka katika kijiji cha Isadora, labda nimeingia kwa njia ambayo siyo nzuri lakini hata nyie mlichokifanya siyo vyema, kwani mmewezaje kumuozesha mwanangu binti yenu pasina kutoa taarifa yoyote katika mji wetu wa Isadora wala kumjulisha mmoja kati ya wazazi wake. Alizungumza Malikia Maua.



    "Ngoja.... Ngoja......ngoja.....alizungumza mfalme na kumsogelea Karibu Hancy ambaye alianza kutazama chini kwa aibu.



    "Wewe ninani??? Aliuliza mfalme Nuhu.



    " Hancy mtoto wa pekee na wa kwanza wa kiume katka familia ya Mzee Jongo, mmiliki wa mji wa Isadora " alizungumza Hancy.



    Mfalme Nuhu alimgeukia mtabiri tambitambi.



    "Kwani umeshamaliza shughuli zote za ndoa?? Aliuliza mfalme



    Kama bado naomba tuachie hapa hapa. Alizungumza Mfalme Nuhu.



    Kwa mila na desturi zetu ndoa hii tayari imeshaweza kutumia kwahiyo hatuna chaguo lingine. Alizungumza Mganga Kipande.



    "Eti wewe ni nani?? Aliuliza Mozah na kumsogelea karibu Hancy aliyekuwa akishindwa kumtazama na kuzungumza.



    Aliyeeonekana kuchoshwa kati ya wote Malikia Samela na mwanaye kwani wao Ndiyo waliyoweza kufanya mipango yote hiyo.



    ***** ****** *****



    " Mozah sikuwa nahitaji kukudanganya hapana, lakini nilihofia kukupoteza kama nitakwambia ukweli; najua hapo nitaonekana kuwa Mimi nimeijali sna nafsi yangu na kuizulumu nafsi yako, kwani nimetizama kile nafsi yangu inachokitaka na siyo kile nafsi yako ilichokuwa ikikitaka.



    "Hancy; kwanini ukaamua kuja kwa njia hii. Kwanini ukaamua kuja kama kijakazi?? Aliuliza Mozah.



    " Mozah,wasichana wengi hawanipendi Mimi kwa jinsi nilivyo bali wananipenda kulingana na cheo nilichoweza kuwa nacho, ona nilipofika katika kijiji hichi wote, waliweza kumkimbilia Tom, kwaajili ya nini kwa baba nilimpa cheo changu Mimi, lakini wewe........."



    "Hata kama lakini alitaka kuzungumza Mozah na Hancy alimuwahi.



    " Mozah me naamini umenipenda kwa jinsi nilivyo cyo kwa wadhifa nilionao, kwahiyo Tafadhali tayri sasa hivi tumeshakuwa mke na mume, nsamehe Mimi mume wako kwa kuweza kukudanganya wewe " alizungumza Hancy.



    "Nsamehe basi Mozah, alizungumza na kumshika Mkono Mozah.



    " mama yako siyo mkali?? Aliuliza Mozah na kumfanya Hancy atabasamu na kucheka.



    "Me nakuuliza wewe unacheka. Alizungumza Mozah na kutoa mikono yake mikononi mwa Hancy.



    " hapana sijakucheka wewe, alizungumza na kuchukua mikono tena ya Mozah, vipi unamuogopa?? Mama yangu hana shida japo mwanzo najua atakuletea shida ila kwa siku zinavyozidi kwenda atakuzoea na wewe, utaamini haya niyasemayo alizungumza Hancy na kusogea Karibu alipo Mozah kisha kumlaza kifuani mwake Mozah.



    "Alafu nilisahau kukwambia"



    "Nini aliuliza Mozah na kukitoa kichwa chake katika bega la Hancy.



    Hancy alirudisha kichwa kile kisha akamwambia.



    "Nina mdogo wangu wa kike jina lake Fancy, anamawenge kama wewe hivyo nahisi mtaendana.



    " Me sina mawenge alizungumza na kuinua kichwa chake tena.



    "Mozah, nimechoka nahitaji tulale" alizungumza Hancy na Mozah alijitoa kwenye bega la Hancy na kushika nguo zake za juu.



    "Saaa hizi,mbona mapema sana hata giza halijaingia vizuri tusubiri usiku usiku watu wakiwa wamelala" alizungumza Mozah na kuendelea kutengenezea gauni lake vizuri.



    "Hivi unafikiria hichi ninachoweza kufikiria Mimi; au unafikiri zaidi ya kile ninachoweza kukifikiria mimi?? Aliuliza Hancy na kumtazama Mozah kwa makini aliyekuwa akijichekesha chekesha.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Embu njoo tulale alizungumza na kumvutia Mozah upande wa ukutani kisha yeye akalala upande wa mwisho na kuweka mkono yake kiunoni mwa Mozah



    "Kama haujisikia vizuri basi natoa Mkono wangu alizungumza Hancy na kuanza kutoa Mkono wake.



    " hpana siyo hivyo, alizungumza Mozah na kuurudisha mkono wa Hancy kiunoni mwake.



    Hancy alipitisha Mkono wa pili katika kichwa cha Mozah na kutokea mbele ya uso wa Mozah huku Mozah akiushika Mkono ule kwa mikono yake miwili ; kisha kuyafunga macho yake na kuachia Tabasamu mwanana kabisa.



    Asubuhi kulipambazuka na alionekana Sikitu akinyatia maeneo ya karibu na pale waliloweza kulala Mozah na Hancy.



    Alitizama kulia na kushoto na baada ya kuona Hamna watu basi aliweza kuchungulia ndani kupitia vitundu vidogo vilivyoweza kuachia upenyo wa kuweza kuangalia ndani.



    Alipitisha macho yake na hatimaye aliweza kuwaona wakiwa wamelala kwa staili ya kukumbatiana.



    Ghafla alishikwa nyuma na mtu na kumfanya Ashtuke.



    "Hivi unafikiri ungekutwa pale na mama yake na Hancy, angekukubali sasa wewe kam mkwe kwake?? Aliweza kuuliza Malikia Samela na kumtazama mwanaye kwa hasira.



    " Lakini mama Mimi siwezi eti, na nilikwambia kabisa Mimi nampenda Hancy, wewe ukawa unang.ang.ania ya kuwa niwe na yule kijakzi, alafu na huu mpango wa kumuozesha Mozah kwa Hancy, ulikuwa mpango wako wewe , umeona sasa ilivyokuwa. alizungumza Sikitu kwa kumlalamikia mama yake.



    "Usijali kuhusu hilo, kwani nitafanya aonekane mtu asiyekuwa na bahati na Hancy, atakuowa wewe, ila utanipa ushirikiano kwa hilo" alizungumza Malikia Samela na kutazama chumba walichoweza Kulala Hancy na Mozah.



    ***** ***** *****



    Nahitaji kuelekea huko alikoweza kuelekea hyo mwanamke na Hancy " alizungumza mfalme wa kijiji cha Isadora na maandalizi yalianza kufanyika kwaajili ya safari.



    ****** ****** *****

    Hancy akiwa na Mozah katika mto mdogo huku wakiwa wamekaa chini na kuzungumza mambo yao. Aliweza kuja Samela na mwanaye Sikitu kwa nyuma kisha wakatoa kiboksi chenye nyoka na kumuachia nyoka aelekee uelekeo huo waliokuwapo huku wakicheka na kusubiri matokeo. Nyoka yule aliweza kwenda uelekeo waliokuwapo na kuanza kusogelea mguu wa Hancy aliyekuwa hana habari yeye pamoja na mkewe Mozah.



    "Mozah.... Aliita Hancy na ghafla alitulia.



    " Nini?? Aliuliza Mozah na kupandisha macho yake juu.



    "Hamna" alizungumza Hancy na kumtazama nyoka yule aliyekuwa akiishilia kwenye majani baada tu ya kumng.ata mguu wake.



    Waliendelea kukaa pale na ghafla alioweza kuonekena Malikia Samela akimleta Malikia Maua katika maeneo Yale yale aliyoweza kuwemo Hancy na Mozah.



    "Una shida gani mbona mwili wako unatoa jasho ghafla!! Aliuliza Mozah na kusimama pale alipoweza kukaa kwenye jabali mbele ya Hancy.



    " Hamna " alijitahidi kujibu Hancy ila sumu iliendelea kutembea katika mwili wake kidgo kidogo.



    "Unaumwa wapi?! Aliuliza na kuanza kumpapasa Hancy mwilini, mwili ambao tayari ulishalowa jasho.



    " Unaumwa wapi alizungumza na kutazama katika mguu ambao aliweza kuuwona unaalama ya kuumwa na nyoka.



    "Hancy" aliita kwa sauti ya juu iliyoweza kumfikia mama yake Hancy na kuanza mbio za kuelekea mahali alipoweza kuisikia kelele hiyo



    Aliweza kuchana gauni lake na kumfunga katika upande wa paja, na kukaza kwa kiasi kikubwa.



    Aliinama na kutaka kunyonya sumu kupitia mdomo wake, ila Hancy alimkataza kwa kusogeza mguu wake.



    Na hapo hapo aliweza kuingia Malikia Maua akiwa na Malikia Samela huku akihitaji msaada.



    "Hancy, Hancy, mwanangu..... Hancy.....jamani naomba msaada kwa mwanangu.



    Malikia Samela alitizama katika kichaka alichoweza kumuweka mwanaye Sikitu na hatimaye alimpa ishara ya aje pale alipo.



    Sikitu alitoka katika kichaka akiwa na Dawa tayari na alipofika alisema.



    " Niamini Malikia Mimi naweza kumtibu Hancy, alizungumza na kukitizama kidonda kile alichoweza kugongwa na nyoka.



    "Bila shaka huyu atakuwa ni nyoka wa kijani, nani hatari sana alizungumza na kutoa unga unga alioweza kuubeba katika kipoko chake na kumuwekea Hancy, huku akikamua majani aliyoweza kuwa nayo na kumiminia kwenye kidonda cha Hancy,



    Wakati huo nao alionekana Mozah aliyekuwa akija na majani aina ile ile aliyoweza kuwekewa Hancy akiwa nayo mdomoni huku akibeba magome ya mti ambao ndani ulikuwa na unga unga.



    " ahsante, ahsante sana kw kumsaidia mwenangu, alizungumza Malikia Maua na kumtaka Tom, amuinue Hancy, kisha Kuondoka naye eneo lile.



    Tom aliweza kumuona Mozah akiwa katika hali ya kuchuruzikwa na damu katika mwili wake kwni; aliweza kukimbilia kwa haraka sana na kwenda kuchukua dawa kwaajili ya Hancy aliweza kuitema na kumwaga magome Yale ya miti kisha akakaa chini huku kila mtu akiondoka eneo lile.



    Baada ya masaa kadhaa kupita.



    "Yani kama siyo mwanao huyu mkubwa sijui mwanangu angekuwa katika hali gni sasa hivi?? Alizungumza mama yake Hancy akimwambia Mfalme Nuhu ambaye alimtizama tu Sikitu na mama yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    " unaendelea je Aliuliza Malikia Maua



    "Mama Mimi niko vizuri bhana alizungumza Hancy kwa kumtoa mashaka mama yake na kuingia katika chumba alichokuwa akikitumia yey na Mozah kwa siku ya Jana usiku.



    " Mozah ameenda wapi??? Aliweza kujiuliza pasina kupata majibu yoyote Yale.



    Alitoka njee na hapo aliweza kukutana uso kwa uso na Tom.



    "Mozah yuko wapi???



    " hata Mimi nashindwa kujua yuko wapi, ndani hayupo, au Kuna chochote kibaya kimeweza kumkuta Mozah? Aliuliza Hancy na kumtazama Tom.



    Wakati nakuleta nyumbani niliweza kumuona Mozah akitafuna Yale majani ya nyoka kwaajili ya kukuwekea katika kidonda chako, sasa kama hatapata dawa,majani Yale yanaweza kuwa sumu kwke, kwani aliyaweka kwenye kinywa chake.



    "Eeeeeehhhhhh alizungumza Hancy na kuanza kumtafuta Mozah huku akiita kwa sauti.



    " Kuna nini tena?? Aliuliza malikia Maua huku Samela na bintiye wakiwa wametoka njee katika kasiri ya kikao cha kifalme.



    "Aliweza kutafuna majani ya nyoka na likipita lisaa limoja hajapata dawa yoyote basi atapoteza maisha alizungumza Hancy na mama yake alishtuka sana.



    " Mbona Mimi sikutambua hilo" alizungumza na kuwapa kazi wafanyakazi wachache alioweza kuja nao wamtafute Mozah haraka sana .



    "Hancy.......ilisikika sauti ndogo na ya kuchoka ikitokea nyuma ya Hancy, Hancy aliweza kugeuka na hapo alikutana na sura ya Mozah iliyokuwa imelowa kwa jasho huku mdomo wake ukiwa umekauka sana na kuanza kupasuka hatua nazo hakuweza kuzisogeza mbele kwani mwili wake wote uliisha nguvu.



    " Mozah " aliita Hancy na kutaka kumfuata ila kabla hajafika eneo lile.



    Tayari Mozah alishaweza kudondoka chini na damu zilianza mtoka puani.



    'Mozah " aliita Hancy na kuweza kufika pale.



    Tayari damu zilishaanza kumtoka mdomoni.



    Tom alikuja na kumpatia dawa Hancy.



    Hancy aliweza kumsimamisha kichwa na kukiweka ktika mapaja yake huku akijitahidi kumnywesha mdomoni.



    Baadaye kidogo alionekana Hancy akiwa njee ya chumba kimoja huku akiwa anahangaika huku na huko, mama yake na yeye akiwa anaichezesha mikono yake...Tom akiwa amesimama sehemu moja na kukitizama chumba hicho, Mfalme Nuhu akiwa amekaa katika kiti chake cha kifalme huku akionekana kuwa na wasiwasi kwa kutingisha mguu wake huku Sikitu na mama yake wakitizamana tu kwa macho walioweza kuyafahamu wao.



    "Yuko wpi mjukuu wangu?? Aliuliza Bi Lunde aliyeonekana kuja na Stela katika eneo lile.



    " yupo ndani na Tabibu Mchome" alizungumza kijakazi Kibonge.



    "Anaendeleaje lakini?? Aliuliza Stela.



    " Anatoa damu nyingi sana hata baada ya kumpa dawa'



    "Hayo yote ni makosa yangu, kama ningeliweza kumtafuta kwa muda ule basi asingeweza kufikia hali hii" alizungumza mama yake Hancy akijilaumu.



    Tabibu Mchome aliweza kutoka njee.



    "Anaendeleaje aliuliza Mfalme Nuhu na kusimama alipokuwa amekaa.



    " Sumu haijaweza kufika katika moyo wake hivyo, dawa aliyoweza kupatiwa itamuondolea sumu yote katika mwili wake, ila atahitaji apate maziwa mengi kwaajili ya kuweza kusafisha kabisa sumu yote mwilini mwake pamoja na supu kila siku asubuhi ili mwili wake uweze kutengamaa" alizungumza Tabibu.



    "Kwahiyo tofauti na hilo, hmna tatizo lingine aliuliza Malikia Maua.



    " hpana Hamna"



    "Damu nyingi zimeweza kumtoka lakini kwnini sasa?? Aliuliza Maua.



    " Ni kwasababu sumu iliweza kujaa katika mwili wake" alijibu Tabibu Mchome.



    "Kama ndo hivyo mbona umesema haijafika katika moyo wake?? Inamaana gani tena unaposema Sumu imeshatembea katika mwili wake wote?? Aliuliza Malikia Maua.



    " Mama Tabibu amesema hayuko katika shida cha kufanya ni kutafuta hayo maziwa pamoja na supu aliyoweza kushauri" alizungumza Hancy akimshika mama yake.



    "Sawa" alijibu Malikia Maua.



    "Kisude na Pweza, mtaenda kutafuta mnyama yoyote yule mumlete hapa kwaajili ya supu ya binti yangu; alafu Tom tutaenda wote kutafuta maziwa lakini kabla ya hapo naenda ndani kumtazama anaendeleaje Alizungumza Malikia Maua na kuelekea katika chumba alichokuwa amelazwa Mozah aliingia na mwanaye Hancy.



    'Nzanza na Nzenze mtaongozana nao. Alafu Furaha na Zawadi harakisheni mkapate maziwa kutoka kwa ng.ombe sasa hivi, ...... Kishoka utaenda kupiga mbiu na kuwataarifu wanakijiji wote wenye maziwa kwmba mfalme anayahitaji kwa bei yoyote ile ili tukikosa katika kasiri yetu basi tukapate kutoka kwao. Alizungumza Mfalme Nuhu na kuingia ndani ya chumba kile.



    Akifuatwa na Tom, Stela pmoja na Bi Lunde.



    " Hivi mama naona au naota? Aliuliza Sikitu.



    "Sidhani kama hii ni ndoto, ila kupitia hapa bado tunanafasi kubwa San ya kumfanya Malikia Maua apendezwe nawe.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Kivipi tena; wakati tayari umeona kabisa hilo limama linajali kuhusu Mozah wala hajui kuwa bila mimi mwanaye angeweza kufariki. Alizungumza Sikitu.



    "We fanya vile, ninavyoweza kukuagiza" alizungumza Malikia Samela.



    "Sawa" alijibu na kuondoka zake.



    "We njoo hapa" alizungumza Malikia Samela.



    "Nini tena??



    "Tunatakiw tupate maziwa wa kwnza kabla ya mtu yoyote yule"



    "Nini?? Aliuliza Sikitu kwa kumshangaa mama yake.



    ***** ****** ****



    " Bi Lunde kama nilivyoweza kukwambia ya kuwa ukoo wenu una damu ya kifalme, kwhiyo hata tufanyaje hatuwezi kubadilisha utabiri huo. Alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    "Na kweli kwa maana tayri utabiri umeshatimia mjukuu wangu ameolewa na mtoto wa mfalme wa mji wa Isadora.



    " Vipi umeleta ile damu ya Mozah??



    "Ndiyo alizungumza Bi Lunde na kutoa kifuko cheusi kilichokuwa na damu iliyoweza kuchanganykana na udongo; bila Shaka ni damu iliyoweza kumtoka Mozah.



    Mtabiri Tambitambi aliipokea kifuko kile lakini ghafla aliweza kukidosha chini na kuweza kukitizama kwa makini sana.



    "Kuna nini tena?? Aliuliza Bi Lunde akijaribu kukitizama kile kifuko kama ataweza kuona kitu.



    " Kuna nini eti?? Aliuliza tena baada ya kutofanikiwa kuona chochote kile.



    "Damu, damu......damu itamwagika nyingi sana....siyo katika kijiji hichi tu hapana hata katika kijiji cha Isadora na vingine vingine" alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    "Miungu wa Isambala itusaidie tuepukane na hili. Alizungumza Bi Lunde huku akionekana amejawa wasiwasi.



    ***** **** ****



    Alionekena Hancy akitizama sehemu moja.



    " Hancy unashida gani mbona unamtizama Shemeji yako hivyo?? Aliuliza Malikia Maua.



    Hancy aliguna tu na kurudisha Mkono wke katika uso wa Mozah aliyeonekana na yeye kumtazama Sikitu.



    "Mama...nafikiri Hancy pamoja na Mozah wamenielewa vibaya tu lakini Mimi siko hivyo wanavyofikiria wao, mimi ni mtu mzuri sana" Alizungumza Sikitu.



    "Kwanza nashangaa sana ulitokea wapi na Dawa ya sumu wa nyoka wa kijani, kama vile ulikuwa unatambua nitagongwana nyoka" alizungumza Hancy na kauli hiyo aliweza kuisikia Mfalme Nuhu alipotaka kuingia katika chumba kile na kumfanya asimame njee.



    "Ammmhh hamna lakini maeneo yale nilienda kuchuma dawa na kuitengeneza kwa kuwa kijakazi wangu pia aliweza kushambuliwa na sumu ya nyoka wa aina hiyo hiyo" alizungumza Sikitu kwa kujing.ata ng.ata



    Alionekana Mfalme Nuhu baadye akiwa na kijakzi wake Kibonge.



    "Mfalme Nuhu, kati ya Zawadi na Furaha hakuna hata mmoja aliyeweza kugongwana nyoka wa kijani, na kwa kipindi hiki nyoka wa kijani hawawezi kupatikana maeneo ya vyanzo vya maji, bali katikati ya misitu hivyo.......

    Na pia niliweza kuwahoji baadhi ya vijakazi wengine na Nzanza alisema aliweza kumuona Mganga Kipande akiingia na kimfuko cha kijani katika chumba cha Malikia Samela.



    " Kibonge....nataka uwende uka chunguze maeneo yote ambayo ni karibu na pale alipoweza kugongwa na nyoka Hancy na taarifa zote nilitee Mimi pia mwambie Nzanza aje hapa pamoja na zawadi na Furaha.



    "Ndiyo mfalme Nuhu" alijibu na kuondoka zake.



    Baadaye alirudi na majibu.



    "Mfalme nafikiri nyoka aliyeweza kumgonga Hancy ni nyoka aliyeweza kutumwa; kama Nzanza alivyoweza kusema yakuwa alimuona Mganga Kipande akija na kifuko cha kijani ni kweli kwani tumekuta kifuko hicho katika maeneo yale. Alizungumza Kibonge.



    " Nzanza aliita Mfalme.



    "Ndiyo mfalme"



    "Kifuko ulichoweza kukiona ndo hichi alichoweza kukileta Kibonge?? Aliuliza Mfalme.



    " Ndiyo Mfalme Nuhu na kama utakuwa unakumbukumbu vizuri, katika siku ya harusi yako na Malikia Samela aliweza kuja nacho na alitoa zawadi kupitia kifuko hichi" alizungumza Nzanza na kumfanya Mfalme akumbuke tukio hilo.



    "Inamaana Sikitu Ndiyo aliyeweza kupanga mipango yote hii, mpaka kuumia kwa Hancy, basi ntaka kujua lengo lake ni lipi; lakini kabla hajafanya kitu cha ujinga kama mama yake nataka akamatwe na apewe adhabu. Alizungumza MFALME Nuhu na ghafla alihisi Kuna mtu nyuma yake kisha akazungumza kwa sauti kubwa



    " Ni nani wewe unayedhubutu kukaa nyuma ya mfalme!?



    Ilisikika sauti ya juu ya kiume ikisema.



    "Utambulisho.



    " Mfalme wa Mji wa Isadora ameweza kufika katika ardhi ya Isambala "



    Mfalme Nuhu alisimama na kutoka katika kasiri yake na hapo aliweza kukutana macho kwa macho na Mfalme wa Isadora.



    "Baba aliita Hancy baada ya kutoka katika chumba alichokuwepo.



    " Mfalme " aliita Malikia Maua na kutazama chini.



    "Huyu ndo Mfalme wa Isador?? Alijikuta akiuliza na Malikia Samela.



    " Kumbe Hancy ni mzuri kama baba yake" alijikuta akizungumza Sikitu na kuachia Tabasamu.



    "Umefuata nini huku?? Aliuliza Hancy.



    "Nimekuj kukifuata kile ulichoweza kukifuata ww na mama yako huku" Alizungumza Mfalme na akimtizama mwanaye ghafla macho yake yaliweza kudondokea Mkononi mwa mwanaye.



    Alitembea hatua chache zilizoweza kubaki na kumshika Mkono ambao ulikuwa na kingozi.



    "Umeowa?? Aliuliza mfalme wa Isadora.



    "Baba... Ammmhhhh ......



    " Kwa ruhusa ya nani?? Aliuliza Mfalme.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kama hakuna ruhusa ya mtu yoyote yule kutoka katika ukoo wetu Mimi siitambui ndoa hii" alizungumza Mfalme



    Na alionekana Sikitu na mama yake wakishangilia kauli ile.



    Ni baada ya Mfalme wa Isadora kuonekana kuipinga ndoa aliyofunga Hancy na Mozah.



    "Baba, utanisamehe kwa hili lakini Mozah ni mke wangu, Mimi hivyo Haina haja ya ruhusa kutka kwa mtu yoyote yule wa ukoo wenu, kwani huyu ni mke wangu na siyo wa ukoo.

    Alizungumza Hancy.



    Mfalme wa Isadora alimtizama Hancy ambaye na yeye alimtizama baba yake.



    "Kwanzia leo nakunyang.anya cheo cha kuwa mfalme mtaraji wa mji wa Isadora na utabaki tu kuwa kama mtoto wa Mfalme kwni hilo ndo ambalo haliwezi kubadilika. Alizungumza Mfalme wa Isadora.



    "Sijali kuhusu kuwa Mfalme mtaraji wa mji wako,najali sana kuhusu mke wangu kwasasa kwani yeye ndiye furaha yangu" alizungumza Hancy na kucheka huku akimfuata baba yake na kumkumbatia.



    Hahahaha baba yake Alicheka na kumkumbatia mwanaye Hancy.



    "Ndo maana huwaga siupendi utani wao, mpaka nahisi miguu kuisha nguvu eti, alizungumza Malikia Maua.



    Na waliobaki wote walibaki wakishangaa kwani walishindwa kuelewa kipi kinaendelea.



    "Kwanini umeowa baba yngu bila kunipa taarifa ni kamsichana gani hako kamekufanya ukaowe upesi aliuliza Mfalme wa Isadora akiwa bado amekumbatiana na mwanaye.



    Hancy Alicheka tu na kumfanya Mfalme Nuhu apumue pamoja na watu wengine walioweza kubakia.



    " hivi hii ni sinema gani hii?? Aliuliza Malikia Samela na kumtazama mwanaye Sikitu aliyekuwa amebaki kinywa wazi.



    Usiku uliweza kuingia; wakiwa wamekaa wote kwa pamoja.



    Mfalme Isadora, Mfalme Nuhu, Malikia Samela, Malikia Maua, Tomimo, Mozah pamoja na Sikitu.



    "Utanisamehe Mfalme mwenzangu maana inaonekana nina kiherehere sana katika ngome za watu ila utanizoea tu, ammmhhhh kama nilivyoweza kukuta ndoa tayari imeshapita na siwezi kuipinga kutokana na kwamba anachoamua kijana wangu juu ya maisha yake basi Mimi huwa naweka Mkono wangu juu kukibariki kutokana na kwamba, ni maamuzi yake nani furaha yake; hivyo basi siwezi kulipinga hili kwani kwa mila na desturi zetu, mwanamke aliyeweza kuolewa katika koo za kifalme kisha akaachika basi mwanamke huyo hafai tena kuolewa na mtu yoyote yule hivyo siwezi kufanya hivyo kwa binti yako......... Na kingine, eti binti Mozah.



    " abeeee Mfalme wa Isadora.



    "Vipi mmeshalala??? Aliuliza Mfalme wa Isadora.



    "Sijakuelewa, Mfalme Tafadhali unaweza rudia"



    "Hancy; mmeshalala?? Aliuliza Mfalme Nuhu.



    " Mimi na...... Yani unamaanisha Mimi na Mozah?? Aliuliza Hancy.



    "Yani Mfalme kakuuliza hivi, umeshalala na mke wako??? Alizungumza Tom.



    " Eeeee tulilala jana; inamaana hamkutuona tukiingia ndani" alijibu Hancy.



    "Hakuna hata mmoja aliyeweza kuelewa hapo, ila bado hawajalala alizungumza Malikia Maua na Hancy pamoja na Mozah walitizama kisha wakajua maana ya swali waliloweza ulizwa.



    " Hapana " walijibu wote kw pamoja tena kwa sauti ya juu.



    "Sawa; ila hata mngenijibu kwa taratibu mbona ningesikia tu haikuwa na haja ya kuongea kwa nguvu hivyo" alizungumza mfalme wa Isadora jina lake Kantala.



    "Samahani Mfalme alizungumza Mozah kwa sauti ya chini.



    Huku Hancy akimtizama baba yake na kumwambia kama ulikuwa unatka kuniuliza basi ungeniuliza mwenyewe, c mpaka mbele yake" alizungumza Hancy akimtizama Mozah aliyekuwa aking.ata lipsi zake.



    Baadaye kidogo alionekana Tom akiwa nyuma ya Hancy huku akicheka



    Hancy aligeuka na kumtizama Tomimo ambaye aliacha kucheka.



    Hancy aligeuka tena mbele na Tomimo aliweza kucheka tena Hancy aligeuka kwa haraka na Tom aliweza kufunga mdomo wake.



    "Wewe.. Unanicheka Mimi eeee?? Aliuliza Hancy.



    Hapana alijibu Tom kwa kutikisa kichwa chake.



    Pouwa alijibu Hancy kwa ishara ya kidole na kugeuka mbele lakini aligeuka nyuma kwa speed na alikuta Tom akicheka.



    " Nilijua tu unanicheka alizungumza na kuanza kumkimbiza Tom huku akimpiga na vimawe vidongo alivyoweza kuviokota.



    Huku nako alionekana Mozah akiwa na Malikia Maua aliyekuwa akimcheka.



    Aligeuka na kumtizama malikia lakini alinyamaza alitabasamu tu na kugeuka mbele ila alihisi kama Malikia anamcheka Alitembea hatua tatu na kusimama alipogeuka nyuma Malikia Maua alikuwa akimtizama tu. Alitabasamu kisha akamuuliza



    "Malikia Maua eti unanicheka?? Aliuliza na kumfanya Maua acheke



    " hpn " alijibu na kumtangulia



    Hapana na anacheka alizungumza Mozah na kumtizama mama aliyeweza kumlea hata yeye alikuwa anacheka.



    Katika ufalme wa Isadora alionekana baba mmoja ambaye aliweza kuwa Mjomba wa Hancy aliyeweza kuridhishwa ufalme wa muda baada ya familia nzima ya Kifalme kuwa safarini.



    Alikitizama kiti cha Kifalme na kukisogelea kwa karibu huku akikishika na kukitizama kwa uchu wa madaraka.



    "Naamini ipo siku ipo siku tu lazima kasiri hii nitaimiliki mimi, itakuwa mikononi mwngu na nitampta tena Maua. Huyo walimuita Kisoda



    "Mjomba Kisoda unafanya nn hapo kwenye kiti cha kifalme?? Aliuliza Fancy baada ya kufika eneo lile.



    " Hamna nimemkumbuka tu baba yako ndo maana nakitizama kiti hichi" alipotezea kwa kuzungumza namna hiyo.



    "Hata na hivyo baba anakuja kesho, nasikia pia Hancy ameshaowa hivyo atakuja na wifi yangu" alizungumza Fancy na kuacha kutabasamu ghafla tu.



    Kisoda Alicheka na kushuka ngazi kadhaa zilizokuwa katika kufikia kiti cha kifalme.



    "Ahaaaa yani umesema Hancy kaowa?? Aliirudia kauli ile kwa kuwa kama anamuuliza lakini anatabasamu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    " ndiyo kaka yangu kaowa" alizungumza Fancy na kuibuka na kicheko kikubwa sana huku akiwaita wafanyakazi waandae nyumba vizuri kwaajili ya siku ya kesho kumkaribia mfalme Kantala pamoja na familia yake.



    Mjomba Kisoda alimtizama Fancy aliyekuwa akisherehekea sherehe ile ambayo alipanga kwnda kuiandaa yeye kwaajili ya kumkaribisha Mkwe katika familia hiyo ya kifalme.



    Kama Hancy ameshaowa inamaana siku yoyote ile atapewa ufalme,na siwezi kupambana naye akiwa tayari anacheo cha kifalme hivyo nahitajika kummalza akiwa na cheo hichi hichi cha mfalme mtaraji; na kama sitaweza kufanya hivyo basi siwezi mruhusu amuowe mwanamke mwingine tofauti na binti yangu " alizungumza Kisoda na kugeuza macho yake ambako mbele aliweza kumuona Fancy akifanya maandalizi Yale kwa furaha huku akimtizama na kumcheka.



    Usiku uliweza kuingia na Hancy alikuwa wa mwisho kuingia ndani na kumkuta mkewe Mozah akiwa ameka katika kitanda na kumsubiri yeye.



    Mozah aliweza kuinuka baada ya kumuona Hancy ameingia ndani.



    "Ww kaa tu alizungumza na kumfanya Mozah akae.



    "Umeshaandaa vitu vyote kwaajili ya safari?? Aliuliza Hancy.



    " Ndiyo tayari.



    "Sawa" alijibu Hancy na kukaa katika ncha ya pili ya kitanda kile alibaki tu akipiga piga miguu yake chini huku Mozah akipishanisha Mikono yake.



    "Hancy" aliita Mozah na kumfanya Hancy ashtuke hadi aainuke katika kitanda kile cha kamba.



    "Mimi nalala" alizungumza na Hancy alijibu Sawa lala.



    Mozah alipanda kitandani na kulala huku akiacha nafasi yamtu mmoja.



    "Mozah nahsi hutaweza kulala kwa Amani hivyo Mimi nitaenda kulala kwa Tomimo.



    Sawa alijibu Mozah na kujifunika vizuri.



    " Sawa lala salama" alizungumza Hancy na kutoka njee lakini baada ya sekunde kadhaa alirudi tena ndani na kumshtua Mozah aliyekuwa akivua nguo yake ya juu kwaajili ya Kulala.



    "Hancy" aliita kwa sauti ya uwoga na Hancy alimsogelea kwa ukaribu kabisa kisha akamshika mikono iliyokuwa imeshika nguo kifuani isidondoke na kuipandisha juu kidogo pamoja na nguo yake kwani kwa upande wa juu aliweza kupaacha wazi.



    Aliusogeza uso wa Mozah na kumpiga busu katika paji la uso huku akimfanya Mozah aishikilie kwa nguvu nguo aliyokuwa akijizuia isidondoke.



    "Mozah nakupenda mke wangu,na sitakufanya chochote kile bila ridhaa yako pia naomba uufikirie upendo wangu juu yako, Tafadhali na Mimi naomba unipende" alizungumza Hancy na kuteremsha lipsi zake mpaka puani mwa Mozah kisha akambusu na kutoka njee Mozah aliweza kuinua Mkono wake juu taratibu na kugusa paji la uso kisha akateremka mpka palipo na pua yake kisha kuigusa.



    "Hancy" aliita jina hilo kwa msisimko mkubwa huku akilisikilizia katika mwili wake.



    Hancy aliweza kusimama baada ya kufika mbali kidogo na chumba alichoweza kumuacha Mozah



    Mungu wangu kwanini moyo wangu unaenda mbio hivi?? Alijiuliza na kuugusa moyo wake.



    ****** ****** *****



    Ilionekana miguu ya kike ikielekea katika simu za Mkononi na kushika simu moja kisha akapiga na kuanza kuzungumza lugha ya kingereza



    "Hello; Sarah..... Hancy want to see u can't u come Tanzania??" ( habari Sarah Hancy anataka kukuona; vipi huwezi kuja Tanzania)



    Baada ya mazungumzo hayo alikata simu na Kuondoka eneo lile.



    Baada ya simu kukatwa aliweza kuondoka eneo lile.



    Huku nako kuliweza kukucha na alisikika jogoo akilia ishara ya kwamba tayari kumeshaweza kuwa alfajiri.



    Ndani ya chumba alichokuwa amelala Mozah alionekana akiwa bado yuko macho huku akiwa anafikiria busu aliloweza kupigwa na Hancy.



    "Mungu wangu, tayari jogoo ameshawika na kunaelekea kukucha sasa bado tu sijalala nawaza busu la Hancy inabidi nilale sasa alizungumza na kulala wakati akifanya hivyo alionekana Sikitu akiwa amesimama njee ya chumba chake na kukitizama huku akizungumza



    " hivi unafikiri nitakuachia Hancy kwa urahisi namna hii, hapana siwezi kukubali kuzidiwa na wewe hata Mara moja.....hivyo tutaongozana wote mpaka pale nitakapo hakikisha ya kuwa Hancy yuko mikononi mwangu na wewe utabaki kuitwa binti wa pili wa mfalme huku Mimi nikiitwa Malikia wa Isadora.



    Maandalizi ya kuweza kumkaribisha familia ya kifalme yaliweza kuandaliwa huku Mjomba Kisude akionyeshwa kutokupendezwa na maandalizi hayo na kubaki akimtizama Fancy ambaye alionekana akiyaendeleza maandalizi Yale.



    ****** ***** *****



    Sikitu unaelekea wapi?? Lilikuwa swali la Mfalme Nuhu.



    "Baba nataka kumsindikiza mdogo wangu nikapaone kwa wakwe zake kisha nitarejea baada ya mda kidogo alizungumza Sikitu.



    " Hapana hutaruhusiwa kwenda mahali popote pale" alizungumza Mfalme.



    "Na Kuna shida gani Sikitu akimsindikiza mdogo wake?? Aliuliza Malikia Samela.



    " Nimesema hata enda mahali popote pale.....namjua na kumtambua vizuri sana huyu hivy siwezi mruhusu akaenda mahali aendako Mozah. Alizungumza Mfalme Sikitu.



    Bi Lunde aliwatizama tu pamoja na Mtabiri Tambitambi.



    "Lakini Mfalme mwenzangu kama ameamua kumsindikiza ndugu yake ni vizuri, usimzuie mtoto kwahilo kama alivyoweza kusema ya kuwa atakaa kwa muda kisha atarudi" aliomba ruhusa Mfalme Kantala.



    "Lakini.......



    " Sijui kwanini unapendaga kumpinga mwanao Sikitu kwa kila kitu asemacho utafikiri si mtoto wako?? Alizungumza Malikia Samela.



    "Sawa me nitafanya vile baba apendavyo sitaki kwenda kinyume na baba " alizungumza Sikitu na kuanza kurudi ndani.



    "Baba mi nafikiri ni vizuri kama nitaweza kwenda na dada Sikitu huko kisha atarudi baada ya muda kama alivyoweza kusema Alizungumza Mozah akimuombea Dada yake.



    "Lakini Mozah.......



    " Mfalme Nuhu Tafadhali mruhusu" aliongezea Hancy na Mfalme Nuhu hakuwa na kipingamizi tena juu yake.



    Alirudisha macho yake kwa Mtabiri Tambitambi ambaye aliweza kuyasikitikia maamuzi hayo lakini hakuwa na lakufanya.



    "Mfalme naomba nipewe ruksa ya kuongozana naye" aliomba ruhusu hiyo Stela mwanamke ambaye aliweza kumlelea Mozah



    Baada ya muda wote waliweza kupanda farasi na safari ilianza huku wakisindikizwa kwa makofi na vigelegele na wanakijiji wa Isambala huku wengine wakimwaga machozi ya furaha na mengine ya kuweza kuwakosa mabinti wote wa kifalme



    Waliweza kuondoka kwa mwendo wa haraka na baada ya muda kwenda sasa waliamua kuanza kutembea mwendo wa kawaida kabisa na farasi.



    Mozah alionekana kusinzia juu ya farasi wake na kuchoka.



    "Mozah tupumzike kwanza ndo tuendelee na safari, Unaonekana kuchoka na kusinzia juu ya farasi hiyo inaweza hatarisha maisha yako. Alizungumza Hancy.



    " hapana nimechoka kidogo tu lakini tunaweza tukaendelea na safari"



    "Lakini Mozah Hancy kasema kweli lolote laweza kutokea kama utasinzia juu ya farasi alizungumza Sikitu kwa kumuaffiki Hancy.



    " hpn Dada Sikitu wewe usijali Mimi bado ninauwezo wa kuvumilia kwa nusu saa nyingine alizungumza Mozah

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa kuwa makini basi wakati wa kuendesha farasi alizungumza Hancy na kutangulia mbele alipokuwapo Mama yake pamoja na watu wengine hivyo nyuma alibaki Mozah pamoja na Sikitu.



    Sikitu aliweza kutabasamu na kuweza kutazama kamba alizoweza kufungwa farasi aliyekuwa amepandwa na Mozah, alimtizama na Mozah kisha akacheka kidogo na kuweza kuacha kucheka alimvuta kamba farasi wake na kumfanya atembee kidogo sana zaidi ya farasi wa Mozah hivyo kumfanya Mozah awe mbele yake.



    Alitizama mbele na kuona maporomoko alimliga farasi yule teke na kumfanya aanze kasi huku akikumbuka ya kuwa kabla ya kupanda farasi huyo aliweza kwenda na kumkata kamba yake kidogo tu hivyo kila Mozah avutapo alama ile inazidi kuachia.



    Mozah alianza kupiga kelele na kuvuta kamba kwaajili ya kuweza kumsimamisha farasi lakini kamba ile iliweza kukatika na kujikuta hana cha kufanya kwaajili ya kumsaidia alibaki akipiga tu kelele huku akimshika yule farasi kwa kumkumbatia.



    Hancy aliweza muongeza farasi wake mbio kwaajili ya kwenda kumsaidia Mozah; huku Tomimo na yeye akifanya hivyo hivyo.



    Huku nyuma Mfalme Nuhu; Bi Lunde pamoja na Mtabiri Tambitambi walikuwa sehemu moja huku mtabiri akitizama vyombo vyake vya utabiri.



    "Tutafanyaje kubadilisha utabiri?? Aliuliza Mfalme Nuhu.



    "Laiti kungelikuwa na lakufanya kwaajili ya kuyazuia haya yote basi ningeyatekelezaga kabla hata hujaniuliza lakini kwasasa hakuna la kufanya kwasababu ufalme ulikuwa wa koo ya kina Bi Lunde ambaye aliweza kuingiliwa na mama yake Samela na kumfanya Mfalme wa mwanzo amuowe yeye, bado ufalme ukaendelea kuwa wa binti yake Bi Lunde lakini na yeye hakuweza kufanikiwa kwaajili ya Samela lakini kwasasa lazima Mozah afanikiwe kwaajili ya kuupata ufalme huu, na kama haitatokea hivyo basi kizazi cha Mozah lazima kiwe cha kifalme hivyo hatuwezi kubadilisha hili" alizungumza Mtabiri Tambitambi.



    "Na njia anayoweza kuitumia Sikitu ni njia mbaya sana, kwani anajifanya mwema mbele ya watu wote lakini ni nyoka mkubwa sana nyuma ya Mozah" alizungumza Bi Lunde huku akionyesha kuwa na mashaka Makubwa juu ya mjukuu wake Mozah.



    Baada ya muda alionekana Mozah akiwa amekaa chini huku Hancy akiwa amemfunika na nguo yake.



    "Unajisikiaje sasa?? Aliuliza Hancy.



    " vizuri "



    "Lakini kwanini unakuwa mbishi sana ww nilikwambia tupumzike lakini ukang.ang.ania safari, unaona sasa mpaka hata hujui saa ngapi ulimfanya Farasi aendee mbio hivi ungeenda kudondokea kule kwenye Yale maporomoko me ningenwambia nini baba yako! Alikuwa akigomba Hancy



    Hancy aliita Sikitu na kwenda kumshika mkono.



    " Inawezekana alipitiwa na usingizi lakini tayari ameshakutaka radhi si vizuri kumkaripia mbele ya watu wote hawa" alizungumza Sikitu.



    Stela alimtizama sana Sikitu na alikumbuka kabla ya safari aliweza kumuona Sikitu akiwa anamshika farasi aliyeweza kupandwa na Mozah lakini hakuweza kuwaza kitu chochote kile kibaya.



    "Ni sawa lakini Mimi pia sidhani kama hizi kamba za farasi zinaweza zikakatika zenyewe bila mtu kuzigusa alizungumza Stela na kumtizama Sikitu aliyeanza kuweweseka.



    Wtu wote walibaki wakimtizama Stela.



    " mama unaongea nini, samahani kwahichi kilichoweza kutokea ni kutokana na kutokuwa na umakini wakati naendesha ila sasa tumeshapumzika tunaweza tukaenda alizungumza na kusimama.



    "Wewe tutapanda farasi mmoja" alizungumza na kumvutia Mozah kwenye Farasi wake kisha kumpandisha na kukaa nyuma yake.



    "Safari inaweza ikaendelea" alizungumza Mfalme Kantala na wote waliweza kupanda farasi zao kisha safari ikaendelea huku nako.



    Tom alibaki akimtizama Sikitu ambaye alionyesha kumtazama kwa macho makali sana Hancy pamoja na Mozah.



    ***** ****** *****



    Jamani yamebaki masaa machache kabla ya Mfalme kuwasili ni vizuri kila mtu akaingia bafuni akaoge kisha mjipambe kwaajili ya kumpokea Mfalme mtaraji na mkewe



    Huyu alikuwa Fancy aliyeweeza kupendwa na vijakazi wote wa tawala ile kwa alikuwa mcheshi sana na mtu anayewapenda wote kwa pamoja bila kujali wadhifa wake.



    Pembeni alionekana Mjomba Kisude aliyekuwa akiwatizama wafanyakazi wakiondoka eneo lile pamoja na Fancy alielekea moja kwa moja hadi kwenye chakula ambacho kiliweza kuandaliwa kwaajili ya mke wa Hancy.



    "Cha kwanza ni kumuondoa huyu mwanamke kisha mambo mengine yatafuata" alizungumza na kutoa unga unga mweusi aliweza kuja nao katika kikaratasi kidogo alichoweza kuja nacho kisha akamiminia kwenye chakula kile na kuondoka.



    Hakufika mbali sana viliweza kuja viatu na kuweza kuonekana mikono ikikifunua kile chakula kilichoweza kutiliwa sumu.



    "Umekosea sana hii sumu yako haikupaswa kuwa hapa kwa siku ya Leo, hapana Huyo Mwanamke atakufa tena katika mikono yangu na siyo mikononi mwa watu wengine alizungumza na kutoa chakula kile kisha kukiweka kingine sampuli ile ile kisha akaita paka na kuwekea chakula kile chenye sumu na kuondoka.





    Hatimaye waliweza kufika katika kasiri ya kifalme japo ilikuwa usiku sana lakini waliweza kupokelewa kwa shangwe na vigelegele kutoka kwa wananchi wa mji huo wa Isadora.



    Mwanga hafifu ulioweza kutawala chumba cha kulia chakula uliweza kuwafanya baadhi ya watumishi katika nyumba ile wakiri kuwa Mozah ni binti mrembo sana.



    "Wifi yangu ni mrembo sana; sidhani kama Kuna mwanamke yoyote yule anayeweza kufikia uzuri wake" alizungumza Fancy na kutabasamu.



    Wakati huo wote alionekana Sikitu akimtizama Fancy ambaye naye alijikuta akimchukia kutokana na kwamba alikuwa akimsifia sana Mozah jambo amblo halikuweza kumpendeza.



    "Nafikiri ni muda mzuri wa kila mtu kuelekea ndani kwake na kulala na maswala mengine tutaweza kuzungumza kesho asubuhi tutakapokutana....Hivyo mkwe wangu naomba ukapumzike....... Ammmhhhh Zawadi!! Aliita Mfalme Kantala na Mozah alishngaa.



    " Ulivyotaja Zawadi nikajua ni yule wa kule katika kijiji chetu , kumbe ni majina tu yanafanana" alizungumza Mozah na kufanya watu wacheke.



    "Tayari umeshaweza kuandaa chumba atakacholala Hancy na mkewe?? Aliuliza Mfalme.



    "Ndiyo Mfalme Kantala" alijibu na fancy aliweza kusimama



    "Baba kwanini usiniulize .......Mimi Ndiyo nimefanya maandalizi yote juu ya kaka pamoja na wifi yangu natumaini watayapenda maandalizi yangu, twendeni nikawaonyeshe chumba chenu" alizungumza Fancy na kumshika mkono Mozah huku akimvuta kuelekea katika chumba alichoweza kukiandaa.



    Wafanyakazi wengine waliweza kuwa kuchukua Stela na Sikitu kisha kuwa peleka katika vyumba ambavyo walistahili kupumzikia huko kwa siku hiyo.



    ****** ****** ****

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kulikucha asubuhi na Mjomba Kisude ambaye aliweza kufahamika kwa wadhifa wa Shemeji wa Mfalme katika falme ya Isadora.



    Aliweza kuamka akiwa mwingi wa furaha na aliweza kumuita kijakazi mmoja aliyekuwa akimfanyia usafi katika chumba chake



    "Wewe, mke wa Hancy Jana alikuja??



    " Ndiyo aliweza kuwasili"



    "Vipi kuhusu chakula alikula??



    " Ndiyo"



    "Chakula gani???



    " Kile kilichoweza kuandaliwa kwaajili yake"



    "Sawa unaweza ukaenda na sitohitaji mtu katika chumba changu kwa siku ya Leo" alizungumza Kisude na aliweza kuondoka kijakazi yule.



    Huku nyuma alitabasamu na kudai ila ikitokea ni habari za msiba juu ya mkwe wa familia hii basi asumbuliwe alitabasamu na kurudi katika kioo chake na kujitizama.



    Huku nako Hancy aliweza kuamka kutoka pale alipoweza kulala na kuelekea kitandani alipolala Mozah alimtizama kwa makini na kuanza kumpapasa nywele zake huku akitabasamu tu.



    Mozah aliweza kujigeuza na kumsogelea kwa karibu zaidi Hancy ambaye alivuta pumzi ndefu na kuanza kumsogeza Mozah taratibu kabisa akitaka kuondoka pale alipoweza kukaa ila Mozah alimsogelea karibu na kuweza kuweka Mkono wake katika kiuno cha Hancy hivyo kufanya uso wa Hancy ukutane na uso wake wakati huo bado akiwa usingizini.



    Hancy aliushika Mkono wa Mozah uliokuwa katika kiuno chake na kutaka kuutoa lakini ghafla aliweza kuingia Fancy na kumkuta katika hali ile.



    "Ooohhhh samahani nilisahau kugonga kabla sijaingia alizungumza Fancy na kumfanya Mozah ashtuke kutoka usingizini hapo ndipo macho yake yalipoweza kugongana na macho ya Hancy na wakati anaamka haraka haraka alijikuta amekutanisha lipsi zake naza Hancy pasina kutegemea, wote walijikuta wameshtuka na kushindwa kufanya kitu zaidi ya kubaki wakiwa wanatizamana.



    Fancy Alicheka na kutoka njee ya chumba kile



    Hancy alijitoa mdomoni mwa Mozah na wakati anasimama kwa haraka alijikuta anapamiana na uwa lililokuwa katika chumba hicho na kufanya tena adondoke kitandani na kuelekea moja kwa moj katika lipsi za Mozah aliyekuwa ameinuka kwaajili ya kutoka kitandani hapo na kujikuta wakiwa wamelaliana na lipsi zao zikiendana kwa Mara nyingine tena.



    *****Katika kijiji cha Isambala*****



    Alionekena Bi Lunde akiwa katika kaburi la binti yake Sarafinah na huku akiwa katika hali ya masikitiko.



    " Sarafinah uliweza kupoteza maisha na kumwacha mwanao katika dunia hii basi naomba ukapate kumlinda huko alikoweza kwenda, Tafadhali usimuache akapata matatizo uliyoweza kuyapata wewe, Mozah bado mdogo sana na hawafahamu binadamu wa njee kutokana na miaka yake mingi kuweza kuishi na mtu mmoja tu ambaye kwasasa anamfikiria kama mama, usimuache maadui zake wakautumia udhaifu wke katika kumteketeza na kumuharibia ndoa yake kwani baada ya miaka Mingi kupita Hatimaye nimeweza kuliona Tabasamu la ukweli katika uso wake; basi naomba umlinde na umtunzie mume wake.



    ****** katika kijiji cha Isadora*****



    Aliweza kutoka Kisoda na kukuta vijakazi wakiwa wamekaa sehemu moja huku wakionekana kuteta jambo fulani.... Aliweza kufika pale na waliweza kumpisha



    Alishtuka baada ya kuona paka watatu wakiwa wamekufa.



    "Ni nini kimetokea??



    " nini kimetokea hapa?? Aliuliza Mfalme Kantala na kuweza kupewa heshima na vijakazi wake.



    "Hii imekuwaje?? Aliuliza Mfalme Kantala.



    " Mfalme, Jana usiku niliweza kuona paka wakila chakula ambacho waliweza kuwekewa nahisi kilikuwa na sumu ndani yake" alizungumza Zawadi.



    "Na hicho chakula kilikuwa cha aina gani??



    "Ni chakula ambacho Fancy aliweza kuandaa kwaajili ya mke wa Hancy"



    "Na kwanini unazungumza sasa hivi?? Aliuliza Mfalme na kutaka vijakazi wake baadhi waweze kumfuata na wengine waweze kwenda kumleta Tabibu wa mji huo.



    " Ni nini hpa?? Aliweza kuuliza Maua na alipewa taarifa zile.



    "Mungu wangu binti wa watu" wote waliweza kumkimbilia katika chumba alichoweza kulala Hancy na Mozah.



    Sikitu aliweza kuyafikiria maneno Yake na kutabasamu.



    "Hivyo inamaanisha siyo Mimi mwenyewe, ninayehitaji kumuuwa Mozah bali Kuna mtu mwingine ambaye na yeye anahitaji kumuuwa, ila kwanini anahitaji kumuuwa Mozah?? Alijiuliza na kubaki akitabasamu tu.



    "Ila kabla ya kuyafahamu yote haya nahitajika kumjua ni nani ili niipate na sababu" Alicheka na kuelekea katika chumba alichoweza kufikia Mozah.



    Waliweza kuingia kwa mkupuo pasina kupiga hodi na waliweza kumkuta Hancy akizikausha nywele za Mozah kwa kuzifuta na taulo dogo.



    Aliweza kuacha na kumtizama mama yake ambaye aliweza kufika eneo lile.



    "Kuna shida gani?? Aliuliza Hancy na kumfanya Mozah afungue macho yake kisha kutizama sehemu aliyoweza kutazama Hancy.



    "Yuko wapi?? Aliuliza Mfalme Kantala na kuingia ndani akiwa na Tabibu.



    "Uko salama?? Aliuliza Mfalme na kuweza kumsukuma Hancy ambaye aliweza kudondoka chini.



    " Ndiyo Mfalme Kantala "



    "Tabibu ni huyu hapa" alizungumza na Tabibu aliweza kusogea mbele na kutoa baadhi ya vitu ambavyo aliweza kuja navyo.



    Mozah alikalishwa kitanda na Tabibu alimshika Mkono wake huku akiyafungua macho yake na kumtazama mdomoni



    "Kuna nini?? aliuliza Hancy aliyekuwa anashangaa watu walioweza kujaa katika chumba chake.



    Kuna nini?? Alimuuliza Mfanyakazi mmoja.



    " Amekula chakula chenye sumu" alizungumza na kumfanya Hancy aongee kwa sauti



    "Chakula chenye sumu?? Aliuliza kwa sauti na kumfuata Mozah ambaye alikuwa bado akipimwa na Tabibu.



    "Embu sogea" alimsogeza Tabibu na kuushika Mkono wa Mozah kisha kuyafumba macho yake.....akamfumbua mdomo na kumtazama kisha akayafumbua macho ya Mozah na kumtizama.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mbona hana dalili zozote za sumu mwilini" alizungumza Hancy na baba yake alimwambia.



    "We unajua nini embu toka hapo Tabibu Zaramo ampime. Alizungumza Mfalme na Malikia Maua aliweza kumwambia mumewe.



    "Hata Hancy ni Tabibu pia; umesahau??



    " Imebaki njia moja tu ya kumtazama kama anasumu katika mwili wake au hana hivyo wote geukieni mlangoni" alizungumza Hancy na baba yake aliuliza.



    "Kwanini tutizame huko??



    "Kwasabab napomshika kwa sasa huna ruhusa ya kupaona" alizungumza Hancy.



    "Kwanini sina ruhusa ya kupaona na Mimi ni Mfalme??



    " Kwasababu wewe ni Mfalme na huyu ni mke wangu Mimi " alizungumza Hancy na Tabibu Zaramo alimtaka Mfalme ageuke.



    "Haya wote geukieni mlangoni" alitoa amri hiyo Mfalme na wote walifanya hivyo.



    Hancy alimtizama Mozah na kuanza kupeleka Mkono wake katika kifua cha Mozah huku akihema kwa nguvu sana na Mkono wake ukitetemeka Mozah alikohoa kidogo baada ya kuona Hancy anaelekezea wapi Mkono wake.



    Aliyafumba macho yake na Hancy aliweza kuusogeza Mkono wake hadi katika kifua cha Mozah kisha akafunga macho ya kuyasikilizia mapigo ya moyo.



    "Kwanini yanaenda kasi hivi?? Alijiuliza na kufumbua macho yake wakati huo nao Mozah alikuwa amelikamata shuka kwa nguvu zote huku akihema kwa kasi ya ajabu.



    Alianza kusogeza kichwa chake katika upande wa kifua cha Mozah kwa kuyasikilizia mapigo ya moyo wake na ghafla waliweza kusikia sauti ya Fancy.



    "Kuna nini mbona watu wote wapo katika chumba cha Hancy??



    Hancy aliweza kuacha kile alichokuwa akikifanya na kusema



    " Hana sumu "



    "Una uhakika?? Aliuliza Mfalme Kantala.



    " Ndiyo "



    "Sumu ya nini alizidi kuuliza Fancy ambaye alionekana kutokuelewa chochote kile.



    "Naenda kumuandalia Supu pamoja na maziwa Zawadi, Fancy na Sikitu ongozaneni nami" alitoa amri hiyo Malikia Maua na kutoka njee.



    "Wengine wote twendeni njee" alitoa kauli hiyo Mfalme Kantala na walianza kutoka njee



    "Hancy kama Kuna sehemu nyingine ambazo unapaswa kumtizama kama anasumu unaweza ukaendelea sisi tunatoka njee.



    Wote walitoka njee na alibaki Hancy pamoja na Mozah.



    Hancy alikaa chini na kuanza kumtizama sehemu za unyayo Mozah.



    " Hancy Kuna nini mbona Mimi sielew, wanasema sumu gani?? Aliuliza Mozah



    Hancy aliweza kuchukua panga lake na kutoka njee akiwa mwingi wa hasira huku Mozah akimfuata nyuma.



    Kisude aliita Hancy na kumfuata akiwa mwingi wa jazba alipomkaribia alichomoa upanga wake katika chombo alichoweza kuhifadhi.



    Ilipoishia ni baada ya Hancy kumfuata Kisude kwa Jazba akiwa amechomoa jambia lake.



    "Tunaweza tukaenda kuwinda wawili?? Aliuliza Hancy na kuachia Tabasamu ambalo hata Mozah alishindwa kuelewa kama ndicho kilichoweza kumtoa ndani kwa kasi hivyo.



    Alianza kuongoza safari na Kisude aliweza kuvuta pumzi ndefu kabla ya kumfuata tendo lile Tom aliweza kuliona na kugeuza macho yake kwa Mozah aliyeonekana kushikwa na butwaa.



    ***** katika kijiji cha Isambala ****



    " Mfalme Unaonekana kuwa mwingi wa mawazo alizungumza Malikia Samela na Mfalme Kantala alibaki akimtizama tu.



    "Endapo binti yako atamuumiza binti yangu kwa njia yoyote ile Mimi siwezi kumsamehe kwahilo" alizungumza na kumtazama.



    "Unachokiongea mimi sikuelewi" alizungumza Malikia Samela.



    "Sawa, ila nahisi ujumbe utamfikishia alizungumza na kusimama ila kabla hajaondoka eneo lile alisimama na kuzungumza maneno kadhaa



    " Mkumbushe Mganga Kipande aje achukue hicho kikapu chake alichoweza kuletea nyoka "



    "Ki....Ki...kikapu gani?? Aliuliza kwa mgugumizo na Mfalme Nuhu aliondoka zake.



    *** Katika kijiji cha Isadora *****



    Wakiwa mezani wakipata chakula wote kwa pamoja huku meza ikionekana kuwa kimya.



    " Mimi nitaenda kula ndani alizungumza Mozah na kuinuka mezani.



    "Wewe Ndiye malikia mtaraji wa mji huu hupaswi kula sehemu tofauti na hapa tunapokula sisi" alizungumza Hancy akiwa ameushika Mkono wa Mozah na kumfanya akae tena.



    "Wifi usijali kuhusu kile kilichoweza kutokea siku ya Leo, nakuahidi ya kuwa haitajirudia tena kwani sitaweza kumruhusu mtu yoyote yule aweze kukuumiza tena" alizungumza Fancy akionekana mwingi wa furaha.



    "Ammmhh Mozah; kuhusu kile kilichoweza kutokea asubuhi embu tufanye kama hakijatokea kabisa na tuishi kwa Amani kwanza" alizungumza Mfalme Kantala.



    "Ndiyo tufanye kama hakijatokea kabisa na tusiwaze kuhusu hilo" alizungumza Malikia Maua na kuweza kumuongezea chakula Mozah.



    "Nashindwa kuelewa nimtu gani huyo ambaye alihitaji kumuuwa mdogo wangu katika siku ya kwanza kabisa ya ujio wake; hat Mimi naogopa sana na ninawaza kwanini alitaka kufanya hivyo?? Alizungumza Sikitu na kufanya Mozah asite kupeleka chakula chake mdomoni.



    "Sitaruhusu mtu yoyote yule amuumize tena Wifi yangu, na kile kilichoweza kutokea tumshukuru tu aliyeweza kuliona hilo na kuweza kuwapa paka chakula kile" alizungumza Fancy na Kisude alibaki tu akiwatizama huku akipeleka chakula chake mdomoni.



    Kisude alimtizama Fancy na kurudisha macho yake katika chakula chake.



    "Nimeshiba alizungumza Hancy na kutoka mezani.



    " Hancy aliita Mozah, Sikitu na Fancy.



    "Samahani alizungumza Fancy na kumfuata Hancy nyuma.



    " Hancy !! Aliita Fancy na ulisikika mlango ukifungwa Mozah aliinuka na kubeba chakula alichoweza kukiacha Hancy kisha akaondoka eneo lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alifika mpaka Katika chumba alichoweza kujifungia Hancy alisukuma na mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani.



    "Hancy..... Hancy.......fungua basi mlango..... Hancy aliendelea kuita Mozah



    " kama amekataa kunifungulia mlango Mimi hawezi kukufungulia wewe, rudi tu mezani kula" alizungumza Fancy na kuanza safari ya kurudi mezani.



    "Aaaaahhhh nimeungua" alizungumza Mozah na kutoa sauti kwa nguvu iliyoweza kupenya hadi masikioni mwa Hancy na kumfanya aufungue mlango.



    "Umeungua wapi?? Aliuliza Hancy akitoa chakula Mkononi mwa Mozah.



    " Mkononi alisema Mozah na Hancy aliweza kuushika Mkono ule wa Mozah kisha kuanza kuupuliza taratibu kabisa.



    "Wapi umeungua?? Aliuliza Hancy akiutuzama Mkono wa Mozah.



    " nimeshikilia sahani muda mrefu ndo ikaanza kuniunguza.



    "Sasa kwnini ukiishikilia na unajua ya kuwa inaunguza?? Aliuliza Hancy kwa hasira.



    " Sasa si wewe haujala na nimekugongea mlango hujafungua alizungumza Mozah huku akionekana kutaka kulia.



    "Sasa mbona untaka kulia?? Aliuliza Hancy.



    "Wewe si umenigombeza" alizungumza Mozah machozi yakiwa yameshamdondoka.



    "Samahani sasa" alizungumza Hancy na kumfuta machozi Mozah kisha kubeba chakula na kuingia ndani ya chumba chake na Mozah.



    Wakiwa wameingia ndani huku Mozah akiwa anapooza chakula cha Hancy kabla ya Hancy hajakiweka mdomoni ulionekana Mkono wa kike ukiufungua mlango ule taratibu na kuushika mlango ule kwa hasira sana baada ya kuona kitendo kile.



    Huku nako alionekana Kisude akiwa nyuma ya Fancy na kurudia maneno Yake.



    "Kama Hancy amenifungia mlango Mimi hawezi kumfungulia mlango yoyote.......Eti Fancy umeona dunia inavyobadilika sasa....mwanzo wewe ndo ulikuwa mtu muhimu kwa Hancy lakini siyo kwasasa tena Kisude alimpita Fancy ambaye alimtizama kisha akamjibu.



    "Si shangi San kwasababu hata mwanzo ulikuwa mtu wa muhimu kwa Malikia Maua lakini siyo tena kwasasa, ila Mimi sina roho kama yako kama Hancy yuko na furaha na Mimi pia ninafuraha nisichokipenda ni kumuona kaka yangu akiwa na huzuni" alizungumza Fancy na kumpita Kisude



    Mfalme Kantala akiwa na mkewe Maua huku wakionekana kujadili jambo.



    "Unafikiri ni nani atakayekuwa amehusika na hili tena?? Alizungumza Mfalme Kantala



    "Hata Mimi nashindwa kuelewa ni mtu gani huyo ambaye ameweza kufanya hivyo, na Mozah ni binti wa kifalme endapo kitamkuta chochote juu yake basi ufalme wake hautaweza kutuelewa" alizungumza Maua.



    "Na cha muhimu kabisa ni kipenzi cha Mfalme Nuhu hivyo chochote kitakachotokea juu yake hata adhirika Nuhu tu hata Hancy na yeye kitamuadhiri" alizungumza Mfalme Kantala.



    "Na............... Kabla hajamalizia kauli yake alisita na kuita



    " Sarah........



    Malikia Maua aligeuka na kumuona Sarah.



    "Sarah!!! Na yeye pia aliita kwa mshangao.



    "Imekuwaje ukarudi hapa?? Aliuliza Maua.



    "Nilipigiwa simu na .......... Kabla hajamtaja aliyeweza kumpigia simu ilisikika sauti ya Fancy akija kwa makeleke ya furaha.



    " Sarah..........



    "Fancy" aliita Sarah na kwenda kukumbatiana kwa furaha.



    "Haaaaaaaaaa what a surprise" alizungumza Fancy na kumpokea Sarah.



    "Hancy..........Hancy.......... Toka njee uone nani kaja alizungumza Fancy na Hancy aliweza kutoka huku Mozah akimfuata kwa nyuma.



    " Sarah!! Aliita Hancy kwa mshangao na kwenda kumkumbatia.



    "Imekuwaje ukaja hapa?? Aliuliza Hancy



    " Nilipigiwa simu na ......... kabla hajamjibu aliweza kunyamaza baada ya kumuona Mozah.



    "Nani Huyo?? Aliuliza Sarah na kumtizama Mozah ambaye na yeye alibaki akimtizama.



    " ahaaaaa huyu ni.........."



    Kabla hajamtambulisha Mozah kwa Sarah Fancy alikatisha mazungumzo yale.



    "Sarah.......njoo huku nikuonyeshe kitu" alimtoa Sarah na kumtizama Hancy ambaye alionekana kupata shida kumjibu swali lile aliloweza kuulizwa.



    "Ni nani huyo?? Aliuliza Mozah na Hancy alimtizama Mozah tu bila kumjibu.



    " Tunafanyaje??? Alikuwa Fancy akiulizana na Hancy.



    "Kwanza nashindwa kuelewa imekuwaje akawa hapa" Alizungumza Hancy.



    "Mozah akigundua hili sijui itakuwaje?? Alizungumza Fancy.



    " Lakini me nafikiri zilikuwa ahadi za kitoto tu kama yeye alizichukua serious sina cha kumsaidia Mimi sasa hivi, nina mwanamke ninayeweza kumpenda.



    "Tatizo la watu weupe wakiweka ahadi hawawezi kuzivunja mpaka waweze kutimiza alizungumza Fancy.



    " Mimi nitaongea naye" alizungumza Hancy na ulioneka mdomo wa kike ukitabsamu baada tu ya kusikika maneno yale.



    Mozah akiwa ndani ya chumba chake aliweza kukumbuka Hancy alivyokuwa mzito kumjibu swali aliloweza kumuuliza juu ya Sarah.



    "Yule msichana ni nani kwnini Hancy, alishindwa kunijibu alijiuliza Mozah na kukumbuka jinsi alivyoweza kumuuliza Hancy na Hancy alivyokuwa akiweweseka.



    Ghafla alisikia vyombo vikiwa vimedondoka njee tu ya chumba alichokuwa akiishi yeye.



    " Ni nani huyo?? Alijiuliza na kutoka njee ambako alikuta bakuli likiwa limedndoka lakini hakukuwa na mtu.



    "Nani huyu kamwaga hapa chakula alafu kaondoka alijiuliza na kuokota bakuli ambalo tayari lilishaweza kupasuka.



    "Jikoni ni wapi tena? Alijiuliza na kuanza kutembea kuelekea katika njia ambayo alihisi ni jikoni nyuma yake ulioneka Mkono wa kike ukishika shika kuta za nyumba ile huku akimfuata kwa nyuma Mozah na kuachia Tabasamu katika mdomo wake.



    Aliweza kufika jikoni na hakuweza kupiga hatua kuelekea mbele zaidi baada ya kuweza kuona kitu ambacho kilimfanya ashindwe kufanya hivyo.



    Mbele ya macho yake aliweza kumuona Hancy akiwa amekumbatiana na Sarah.



    Alipomaliza kutazama alitoka jikoni pale akiwa amenywea kabisa hata hatua zake nazo ziliweza kupungua na alirudi akiwa na chombo kile kilichoweza kupasuka alirudi na kuingia mpaka chumbani huku nako alionekana Sarah akiwa ameachan na Hancy.



    " Sarah.....natumaini umenielewa na samahani kwa kuweza kuweka ahadi ambyo nimeshindwa kuitimiza natumaini hili kumbatio uliloweza kuliomba Leo ndo ombi la mwisho na utambue ya kuwa yule ni mke wangu na ninampenda sana"



    "Sawa kama hujaweza kunipenda siwezi kukulazimisha unipende ila kuna jambo moja la mwisho nahitaji kukuomba"



    "Jambo gani hilo??



    " Naomba tuendelee kuwa na uhusiano kama tulioweza kuwa nao mwanzo, ctopenda kuona ukikaa mbali na Mimi kwasababu tu tayari una mke wako" alizungumza Sarah na Hancy alitikisa kichwa ishara ya sawa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tuendelee kuwa marafiki" alizungumza Hancy na kutabasamu.



    Wakti huo nao ulionekana mdomo ukisikitikia maneno Yale.



    "Bahati mbay huyo mwanamke wako hajayasikia maneno haya" Alicheka baada tu ya kuzungumza maneno Yale.



    Wakati huo ndani alionekana Mozah akiwa amekaa kitandani na machozi yakiwa yanamtoka aliposikia mlango unafunguliwa aliyafuta machozi yake na kutizama mlangoni aliingia Zawadi akiwa na kibakuli ambacho aliweza kuleta chakula kile kile kilichoweza kudondoka njee ya chumba chake.



    "Ahsanteh alizungumza Mozah na kupokea chakula kile. Hapo hapo aliingia Hancy akiwa na Tabasamu huku akiamini ya kuwa amemaliza kila kitu juu yake na Sarah.



    " Zawadi unaweza ukaenda njee"



    Ndiyo Mfalme mtaraji. Zawadi alijibu na kutoka njee.



    Mozah alimtizama Hancy aliyeonekana kuwa mwingi wa furaha na kukumbuka kumbatio aliloweza kuliona.



    Alijikuta akila chakula kile kilichoweza kuletwa na kukiweka mdomoni pasina kutambua ya kuwa ni chamoto aliweza kuungua na kujikuta akisimama kwa kutafuta mahali ambako ataweza kutemea chakula kile.



    Mozah aliita Hancy na kumfuata Mozah aliyekuwa ameenda kutemea dirishani chakula kile.



    "Unashida gani wewe, kwanini unatema chakula ambacho mama yangu ameweza kutumia muda mwingi kukipika?? Aliuliza Hancy akionekana kutopendezwa na tabia aliyoweza kuifanya Mozah.



    " Samahni, nilikula pasina kutambua ni cha moto" alizungumza Mozah.



    "Ona sasa umemwaga chakula chote" alizungumza Hancy na kumuonyesha ya kuwa chakula kile chote kiliweza kumwagika.



    "Tafadhali usimwambie mama juu ya hili nitafanya usafi hapa" alizungumza Mozah na kutaka kuelekea kwaajili ya kusafish.



    "Wacha nitasafisha Mimi" alizungumza Hancy na kutaka kwenda kusafisha lakini ghafla aliitwa na Sarah.



    "Hancy, bado tu hujajiandaaa?? Aliuliza Sarah.



    " ahaaaa nilisahau kidogo Mozah nakuja" alizungumza na kutoka njee na Sarah ambaye aliweza kumfuata.



    Mozah alipiga hatua kwaajili ya kwenda kusafisha lakini alihisi maumivu katika mguu wake alipotizama aligundua ya kuwa chakula kile kiliweza kudondokea katika mguu wake.



    "Ahhhhhh alizungumza na kujitizama mguuni mwake ghafla aliingia Hancy na alijifunika.



    " twende mahali " alizungumza na kumuinua Mozah.



    "Hancy........aliita Mozah.



    " shshshshsh.......... Hupaswi kunikatalia twende pamoja' alizungumza na kuanza kumvuta Mozah ambaye alibaki akiguguma kimoyomoyo.



    "Mozah unashida gani mbona.......kama jasho linakutoka aliuliza Fancy na Sikitu pamoja na Sarah walimtizam huku Tom na yeye akionekana kuja eneo lile akiwa amebeba baadhi ya nguo.



    " Unaumwa?? Aliuliza Hancy na kumshika Mozah kichwani.



    "Hapana" alijibu Mozah na kuutoa Mkono wa Hancy



    Mozah aliweza kumpanda farasi na hatimaye walianza safari.



    Hancy alimpanda farasi mwingine kisha kumtazama Mozah.



    "Kuwa makini usimuendeshe kwa kasi"



    "Sawa" alijibu Mozah na safari iliweza kuanza.



    Waliweza kutembea kwa umbali mrefu kidogo huku Hancy akionekana kumtazama Mozah Mara kwa Mara.



    "Hancy njoo Mara moja" aliita Sarah na Hancy alimtizama Mozah kisha akaongeza mwendo wa farasi.



    "Wifi unajisikiaje?? Aliuliza tena Fancy aliyeweza kuonekana kuwa na mashaka juu ya Mozah.



    " Nipo salama" alijibu Mozah lakini hali yake haikuwa nzuri hata kidgo mdomo wake uliweza kumkauka na uso wake uliweza kuonekana kupauka huku jasho jingi likiwa linamtoka hii ni kutokana na kuungua na chakula katika sehemu ya mguu wake na kuutembeza mguu ule juani pasina kuupaka dawa yoyote.



    Fancy alipita na nyuma alibaki Tomimo.



    "Mozah......kama mguu wako unakuuma sana usijilazimishe naweza kukurudisha nyumbn na Hancy hataweza kukereka kwa kutoweza kuuona uwepo wako tayri Dada yake Fancy yuko hapa kwahiyo acha kuutesa mwili wako.



    "Hapana bado naweza nikamudi na sitaki kuwa chanzo cha huzuni katika safari ya watu wengi wenye furaha.



    " Lakini hali yako inazidi kuw mbaya alizungumza Tom na wakat huo nao Hancy aliweza kugeuka nyuma kwaajili ya kumtizama Mozah.



    "Bado niko......... Kabla hajamalizia sentensi yake nguvu zilimuishia na kujikuta anaiachia kamba ya faras na kuanza kuona giza huku akikosa muelekeo na kwa mbali akiisikia sauti ya Tom ikimuuliza kama yuko salama.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog