Simulizi : Uko Wapi Mama?
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"unaona sasa hili jimama lilivyokua na roho mbaya??..yani anaulizwa swali anajibu kwa kichwa kama vile mdomo umejaa kinyesi"...Ilikua ni sauti mama mmoja ambae nae alikua amehudhulia pale kwa mwenyekiti..hivyo akawa ameongea kauli hiyo iliyo mfanya mama yake wa kambo Nyanzala kushindwa kujuzuia hivyo nae akajibu shambulizi lillilopelekea wawili hao kutukanana....Lakini wote walionywa na wazee waliokuwepo pale na ndipo walipo kaa kimya huku mama yake wa kambo Nyanzala akidondosha machozi kwa hasira..
"jamani hatujaja kutukana mahali hapa ila tumekuja kujadili maisha juu ya yule mtoto yatima Nyanzala ,kiukweli anateseka sana zaidi ya sana tangu baba yake alipo muoa huyu mwanamke.Yalikua ni maneno ya baba Maria aliyokua akiyaongea kwa sauti ya upole huku machozi ya huruma yakielea elea kwenye mboni ya macho yake...
Na hapo ndipo mwenyekiti alipo amua kumuuliza swali mama Kagaruki..."kwanini unamnyanyasa mtoto wa mwanamke mwenzio?"..Mama Kagaruki kimya....Akaulizwa tena "kwanini unamnyanyasa mtoto wa mwanamke mwenzio??..."sawa kama mnaona namyanyasa basi kuanzia leo akakae kwa baba Maria" ...Alijibu hivyo kwa hasira mama yake wa kambo Nyanzala ,kisha akainuka na akawa ameondoka zake akiwaacha watu walio hudhulia pale kwa mwenyekiti wakibaki na mishangao...
"kha kweli bora ukosee kunyoa na sio ukosee kuoa,,hakika baba Nyanzala kapata hasara kwa huyu mwanamke"...Aliongea hivyo mwenyekiti wakati huo mama yake wa kambo Nyanzala ameshaondoka pale kwenye kikao...
Basi baada ya mama yake wakambo Nyanzala kuondoka,ilibidi kikao kivunjwe huku mwenyekiti akidai kwamba atamwandikia barua baba Nyanzala ili aje aambiwe ukweli kuhusu maisha anayo ishi mwanae na Mama yake wa kambo..Hivyo wanakijiji walio kuwepo pale walisambaa kwenda majumbani mwao huku wengine wakaelekea mashambani.
Wakati huo mama yake wa kambo Nyanzala alikuwa ameshafika nyumbani kwake...huku akionekana kumsubili Nyanzala kwa ham ili amuadhibu akidhania yeye ndio alie peleka mashtaka kwa mwenyekiti kwamba mama yake wa kambo anamnyanyasa...Kumbe wakati huo yule mama akionekana kumsubiliia Nyanzala atoke shuleni ili amuadhibu...na muda huo huo Nyanzala akawa amerudi nyumbani kwa sababu ya kutoenda na hela ya mlimzi wa shule hivyo ndio ilipelekea kurudishwa nyumbani..
"shkamoo mama" ..Nyanzala alimsalimia mama yake wa kambo huku akionekana kumwogopa...Lakini yule mama hakuweza kuitikia salam Nyanzala bali alimjibu.."mimi sio mama yako ila mama yako yupo hapo nyuma ya nyumba kaburini..sawaee na leo ndio utanijua vizuli mpumbafuuu mkubwa wewe"...Kiukweli Nyanzala alishtuka sana baada kusikia maneno hayo..alijiuliza kosa lipi alilolifanya mpaka mama yake wakambo ampanie namna hiyo.
Na mala bada Nyanzala kujiuliza kosa gani alilomfanyia mama yake wa kambo...hatimae aliamua kuingia ndani kisha akabadilisha nguo za shule kwani aliogopa hata kumuomba mama yake hela ya mlinzi iliyomfanya arudishwe nyumbani...Alipo maliza kubadilisha sare za shule,alichukua ndoo ndogo kisha akaelekea kisimani kuchota maji ya kufulia nguo zake ambazo zilionekana kuwa chafu mno.
Hakika yule mama yake wa kambo Nyanzala alimwangalia sana Nyanzala kwa jicho la hasira..wakati huo Nyanzala akiwa hajui chochote...."huyu hanijui me ni nikoje sasa leo namkomesha"..Alijisemea hivyo mama yake wa kambo Nyanzala wakati huo Nyanzala ameshapotea maeneo yale ya nyumbani.
****
Hatimae Nyanzala alirudi kutoka kisimani na kabla hajatua ndoo ya maji chini aliambiwa na mama yake wa kambo.."tua hiyo ndoo yako ya maji harafu chuku panga nenda polini ukalete kuni"..."mama mbona kuni bado zipo za juzi za jana eeh"..Nyanzala alimjibu hivyo mama yake wa kambo pasipo kujua kuwa anatafutiwa sababu,na kweli punde si punde baada Nyanzala kumjibu hivyo mama yake wa kambo,ghafla alipigwa kofi la mgongoni..alipigwa kwa nguvu kulinganisha na umri aliokua nao.
Na hata hivyo yule mama hakulidhika,hatCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
imae alinyanyua ile ndoo ya maji aliyokua ametoka kuchota Nyanzala kwa niaba ya kufulia nguo zake,akawa amemwagia...Kiukweli Nyanzala alipiga kelele.Akata kukimbia ila hatua moja tu akawa amenaswa na mwanzo mwisho kipigo..."mamaaaa nakufaaa mama nisamehee mama nisamehee naenda kuchanja kuni mama naendaaa niachilieee"..Nyanzala alilia kwa style hiyo wakati huo tayali kaburuziwa ndani ili majirani wasijue kama anapigwa na mama yake wa kambo.
Na baada ya kipigo alikabidhiwa panga kama ilivyo ada. .akiwa na njaa yake tumboni akaelekea polini kutafuta kuni wakati nyumbani kuna mizigo kibao ya kuni...Hakika majonzi kila kukicha kwa Nyanzala yaani kili siku heli ya jana.
"Nimekosa nini mimi...???
"eeh furaha yangu iko waaaapi mimi.. yani bila kujua kosa langu naadhibiwa??
"jamani mamaa mamaaa..bora ungelinitoa kingali mimba kama ungejua utaniacha peke yangu..UKOWAPI MAMA?
Ni maneno aliyokua akiongea Nyanzala ndani ya nafsi yake huku mboni za macho yake zikitoka machozi...wakati huo akiwa njiani anaelekea msituni kutafuta kuni.
****
Naam.baada kufika msituni alikata baadhi ya kuni na nyingine akawa anaokota tu mahala wakataa mkaa walipo katiakatia magogo na kuacha kuni ndogo ndogo hivyo muda mchache tu Nyanzala akawa ameeneza mzigo ambao anaweza kujitwisha.
Na hivyo akaanza safari ya kurudi nyumbani wakati huo jua nalo likelekea kuzama kigiza nacho kikija kwa mbali...na hapo ndipo Nyanzala alipo kazana ili giza limkute nyumbani ila alipunguza mwendo baada kukumbuka kipigo alichokipata hivyo akahisi kwamba endapo kama atafika nyumbani basi kipigo kitaendelea tena.
Lakini mwishowe akaona liwalo na liwe..akakazana tena mpaka akafika nyumbani na giza tayali lilikua limeshaingia...kiukweli kidogo Nyanzala alitabasam baada kumkuta baba yake nyumbani hivyo alipotua chini mzigo wa kuni,hima alienda kumlaki huku machozi yakimtoka..."shkamoo baba"..Nyanzala alimwamkia baba yake..."malakhabaa mwanangu mzima lakini"...Mzee nae akamjibu mwanae kwa tabasam pana..lakini baada yule mama yake wa kambo Nyanzala kuona hali ile ya baba na mwana wakifurahi,hatimae aliweza kuitowesha furaha baada kusema.."baba Nyanzala ,mwanao kaenda kunishtaki kwa mwenyekiti kwamba me namyanyasa...ivi kweli me ningekua namtesa huyo mwanao angekaa na mimi miaka yote hii??".... Alisema mama Kagaruki akijifanya kuumizwa na kitendo kile.Hakika Nyanzala alishtuka baada kusikia maneno yale aliyokua akiongea mama yake wa kambo..."eti kwanini umeenda kumshtaki mama yako hivi una akili kweli wew"...Baba Nyanzala alimgeukiwa mwanae na akawa amemuuliza hivyo...lakini Nyanzala alikataaa katu katu.."hapana baba me siwezi kufanya hivyo siwezi kweli babaa"...Nyanzala alimjibu hivyo hivyo baba yake huku akitetemeka mwili mzima...Ila licha ya Nyanzala kukataa ajabu mama yake wa kambo alizidi kukazia maneno ambayo yalimfanya baba Nyanzala kuchukuwa jukum la kumpiga Nyanzala ilimladi alimdhishe mke wake ambae ni mama yake wa kambo Nyanza.
Nyanzala alilia sana kwani alitegemea mkombozi pekee ambae angemtetea dunuani ni baba yake...lakini nae ndio kama hivyo hakujali wala kumthamini kama mwanae kwani hata muda wa chakula cha usiku ulipo wadia,baba Nyanzala alimuamuru mkewe ambae ni mama yake wa kambo Nyanzala kuwa ampe chakula kidogo Nyanzala ale peke yake huku akisema"ndio akome na ajue kua mimi sipendi watoto jeuri"...Basi kupitia ile nafasi ya Nyanzala kupewa chakula cha kwake peke yake,ndio hapo hapo mama yule wa kambo alipo tia sumu kwenye chakula cha Nyanzala nia yake ni kumuondoa kabisa duniani....
"Nyanzala mwanangu me nishakusamehe ila baba yako ndio bado anachuki na wewe ila usijali tutayamaliza pindi tutakapo kua wawili mimi na yeye sawaeee...haya chukula hiki hapa naomba ule sitaki kuona sahani ikirudi na chakula sawa mwanangu.."...Yalikua ni maneno ya mama yake wa kambo Nyanzala akimbembeleza Nyanzala ale chakula wakati katia sumu...Basi Nyanzala alikaa akafikilia"iweje anichonganishe kwa baba harafu malahi anibembeleze..??..pia haijawi kutokea hata mala moja huyu mama kunibembeleza kiasi hiki sasa leo hii kipi kimetokea??..
Ni maswali ambayo alikua ajiuliza Nyanzala huku mkono wake ukipeleka tonge mdomo na nafsi nayo ikimsuta kwamba asile kile chakula.
Na mala baada nafsi kumsuta Nyanzala kuhusu kile chakula chenye sumu aliyo wekewa na mama yake wa kambo..Kweli hatimae alikiacha kile chakula..."mama sijiskii kula kwa leo labda nihifadhie nitakula kesho"...Nyanzala alimwambia hivyo mama yake wa kambo huku akiitoa sahani mbele yake sahani ya chakula chenye sumu ambayo aliwekewa na mama yake..."baba Nyanzala unamwona mwanao lakini,anapewa chakula hataki kula ila akitoka hapa utakuta anatangaza mitaani kwamba simpi chakula"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
.."achana nae kama hataki ila ngoja nimalize kula nimnyooshe kwanza na atakula tu kwa lazima tu"..Yalikua ni maneno ya baba Nyanzala ambayo aliongea hivyo baada mke wake kunwambia kwamba Nyanzala anamtangaza mtaani kua mama yake wa kambo huwa anamnyima chakula.
Kweli baada baba Nyanzala kumaliza kula,aliinuka kutoka kwenye kigoda alichokua amekalia wakati wa kula,kisha akausogelea mti ambao ulikua jirani na nyumba yake ndipo akakata fimbo ndefu ambayo ilikua ikinesanesa..."Nyanzala.." Baba Nyanzala alimuita Nyanzala nae akaitika wito wa baba yake huku akilia kabla hajapigwa.."kwanini utaki kula"..Aliulizwa hivyo Nyanzala lakini nae hakujibu chochote zaidi ya kuangua kilio....lakini wakati huo huo Nyanzala akilia ndipo baba yake alipo mchapa huku akimuuliza...utakula au huli??..utakula au huli??...Ila Nyanzala hakuweza kukubali hivyo ndivyo kasi ya kuchapwa nayo ilizidi kuongezeka ilimladi tu Nyanzala akubali kula chakula alichowekewa na mama yake wa kambo..
Hakika kipigo kilizidi sana kwa binti Nyanzala ...hatimae yale mayowe aliyokua akitoa kwa maumivu ya fimbo yakawa yamemwamsha baba Maria ambae ni jirani baba yake baba Nyanzala hivyo yeye ndio aliweza kuingilia kati na kumuombea msamaha Nyanzala kwa baba yake haliyakua mamayake wa kambo yeye alikua akifrahia kipigo ambacho alikua akikipata Nyanzala kutoka kwa baba yake.
Baada Nyanzala kuombewa msamaha na baba Maria hatimae aliingia chumbani kwake moja kwa moja alijifunika shuka lake kisha akaanza kuutafuta usingizi,lakini usingizi ulikataa kwa sababu mwili wake wote ulikua unauma kwa sababu ya kipigo alichokipata kutoka kwa baba yake mzazi...Hivyo basi masaa yalizidi kwenda huku Nyanzala akiwa tongo macho bila kupata hata lepe la usingizi.. Lakini huku upande wa pili baba Nyanzala aliamka na kisha akaelekea chooni kujisaidia lakini wakati anarudi ndani ili akaumalizie usingizi,hatimae alishtuka baada kusikia sauti ya marehem mke wake ikimuita..."bab
a Nyanzala ..baba Nyanzala "..Ile sauti ilisikika mala tatu ikimuita baba Nyanzala hivyo nae kwa kua alikua na roho ya kijasiri hatimae alisimama kwanza huku akiisikilizia ile sauti mahali inapo tokea..na baada kama dakika mbili alishikwa na butwaa baada kugundua kua ile sauti inayo muita ni ya marehem mke wake na ikitokea nyuma ya nyumba ambapo lilipo kaburi la mke wake.
Na wakati baba Nyanzala akishangaa shangaa akiwa haamini anachokisikia masikioni mwake,mala ghafla juu ya lile kaburi la marehem mke wake alitokea nyoka mkubwa kisha yule yoka akatambaa kuelekea mahali alipokua amesimama baba Nyanzala ...
"mungu wangu"...Alijisemea hivyo baba Nyanzala huku akikimbilia ndani na haraka sana akafunga mlango kwa nguvu ambapo mke aliekua amelala ndani aliweza kushtuka kutoka usingizini na alipo papasa mbele ya kitanda ambapo anapo lala baba Nyanzala siku zote...akawa hajamgusa hivyo dhali alijua mtu aliefunga mlango kwa nguvu ni baba Nyanzala kwaiyo akawa ametelemka kitandani kisha akaenda kuangalia mumewake kakutwa na nini...Na kweli mama Kagaruki baada kufika sebleni alimkuta mume wake akiwa ndani ya taulo huku ameegemea mlango na akihema kwa nguvu..."vipi baba Nyanzala mbona sikuelewi hapo mlangoni"..Aliuliza hivyo mama Kagaruki ,lakini baba Nyanzala hakujibu chochote zaidi ya kung'ang'ana na mlango huku jasho tele likimtoka mwili mzima...na wakati hayo yote yakiendelea Nyanzala nae alikua macho kwani usingizi uligoma kuja kwa aababu ya njaa aliyokua nayo pia na maumivu mwilini baada ya kipigo.
"baba Nyanzala unajua sikuelewi"...Mama Kagaruki ambae ndio mama yake wa kambo Nyanzala alirudia kumuuliza hivyo mumewe lakini hakujibiwa...ila baada kama dakika kadhaa baba Nyanzala aliachia mlango kisha akaelekea chumbani kwake bila kuongea chochote na mke wake...
Hivyo hivyo baada baba Nyanzala kuingia chumbani huku akiwa amemuacha mama Kagaruki sebleni..Ghafla alishtuka baada kumwona marehem mke wake akiwa amekaa kitandani huku akiwa amevalia mavazi meupe..."habali yako baba Nyanzala " ...Marehem mama Nyanzala "alimsalim baba Nyanzala huku sauti yake ikijurudia mala mbili mbili mithili ya mwangwi..Lakini baba Nyanzala hakujibu salam aliyopewa na marehem mke wake bali aliogopa sana na akawa anatetemeka mwili mzima huku jasho la kutosha likimtoka na taulo nalo limeshamdondoka kwa woga.
Hakika taulo lilimdondoka Baba Nyanzala kwa woga baada kumkuta marehe mke wake kitandani huku akiwa kavaa sanda.
"Baba Nyanzala yote mnayo mfanyia mwanangu nayaona. .nikiwa hukooo Akhera. Hivyo nimekuja kukupa taarifa kuwa siku zinahesabika" kwisha kusema hivyo. Marehem mama Nyanzala alitoweka. Wakati huo huo mama Shani nae aliingia chumbani akastaajabu kumkuta mume wake akiwa amelowa jasho ndembendembe. Alipotaka kuhoji akaona sio vema hivyo alimwacha alale akiamini kesho ipo.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na muda ule wa Nyanzala kwenda kula chakula kwenye kaburi la mama yake uliwadia. Hivyo alitoka ndani haraka sana akaelekea kwenye kaburi la mama yake. Wakati huo huo mama Shani nae alizama uvunguni akachukuwa mayai na Nazi ikitaka akapausulie kwenye kaburi la mama Nyanzala. Ili aweze kumfunga mume wake kisawasawa ..pindi atakapo amua kitu nae asipinge.
Kweli baada Nyanzala kufika kwenye kaburi la mama yake,lile joka lilitokea kama kawaida likaasama mdomo wake ambapo zilitokea sahani mbili za wali na nyama. Nyanzala alifurahi moyoni mwake hima akala harakaharaka. Baada kumaliza kula alirudi ndani ambapo alikutana mlangoni na mama yake wa kambo. Nyanzala alishtuka kumuona mama yake wa kambo akakumbuka kuwa alikatazwa kutoka nje usiku.
Basi mama Shani alimkabidhi Nyanzala mayai na Nazi.. kisha akarudi chumbani kumwamsha mume wake..ilichukuwa muda kidogo ila mwishowe Baba Nyanzala aliamka na moja kwa moja wakaelekea sebleni ambapo walimkuta Nyanzala akiwa ameshika mayai matatu na nazi moja.
"Baba Nyanzala unaona mwanao kashika nini na anania gani"
Yalikua ni maneno aliyokua akizungumza mama yake wa kambo Nyanzala huku akimwonyesha baba Nyanzala nazi na mayai aliyokua ameshika Nyanzala.."mmh mwanangu Nyanzala nini sasa unafanya eeh mwanangu"...Aliongea hivyo baba Nyanzala kwa sauti ya upole...lakini Nyanzala hakuweza kujibu chochote maana kila alipotaka kuongea ukweli nafsi ilimsuta asijibu chochote.
"baba Nyanzala ,mwanao bado mdogo sana ila anataka kuiga uchawi kweli jamani eeeh hakyamungu huyu mtoto atakuua mtu hum ndani kha"...Mama yake wa kambo Nyanzala aliongea hivyo ilimladi baba yake Nyanzala amuadhibu mwanae. . ila kwa kua baba Nyanza nae alikua ameshaambiwa jambo na marehem mke wake hivyo aliishia kunyamanza tu hakuweza kuchukua hatua yoyote..."mama Kagaruki yawekeni sawa mambo kwani huyo ni kama mwanao istoshe huyo ni mtoto wa kike,kwaiyo kaa nae naumwambie kua ushirikina sio mzuli sawa mke wangu"...Baba Nyanzala alimwambia hivyo mkewe mama Kagaruki kisha akarudi chumbani kulala ili kutuliza akili.
"anhaaa sawa we nenda mme wangu kalale ila me ngoja nikae na mwanao nimwelekeze"...Hivyo nae mama Kagaruki alimjibu mme wake huku akimng'ong'a kwa kutumia mdomo wake.
Basi baada baba Nyanzala kuingia chumbani,hatimae sebleni alibaki mama Kagaruki na mtoto Nyanzala .."embu kwanza leta vitu vyangu mpumbafu wewe"..Mama Kagaruki alimpokonya Nyanzala nazi na mayai mala tu baba mume wake alipoenda kulala...Na baada mama Kagaruki kumpokonya Nyanzala mayai na nazi,ndipo alipo anza kimfinya mtoto wa watu kila kona ya mwili wake huku akimwambia.."we mtoto wewe nilikwambia nini kutoka toka nje usiku eeeh unakiburi eti eee..sasa leo ndio utanikoma mjinga wewe"...Hakika mama Shani alimfinya Nyanzala kwa kutumia vidole vyake viwili..dole gumba na shahada..Nyanzala alijikaza sana lakini mwishowe alitoa sauti ya chini chini huku akiomba msamaha..."nisamehe mamaa naomba nisamehe mama sitoki tena nje usiku mamaaaa"...Nyanzala aliomba msamaha huku akilia kilio cha chini chini lakini mwishowe alipasa sauti na hata hivyo mama Shani ambae ndio mama yake wa kambo Nyanzala ,alimkanya akae kimya .."kimya mbwa wewe"...Maskini ya mungu Nyanzala nae baada kusikia hivyo alinyamanza na akawa analilia rohoni...
**********************
Na mala baada mama Shani kumuuadhibu Nyanzala ,hatimae alilidhika hivyo akamruhusu akalale huku akimuonya asimwambie baba yake ukweli kama alimpiga..."sasa olewako umwambie baba yako kwamba nimekupiga heheee nitakacho kutendea hutokuja sahau maishani mwako"....Aliongea hivyo lakini Nyanzala hakujibu chochote zaidi ya kupandisha kamasi jepesi lililokua likimtililika kwenye pua yake baada kulia kwa muda mrefu.....Hivyo mama Shani alivichukua vitu vyake yani nazi na mayai kisha akaelekea nyuma ya nyumba ambapo ndipo lilipokua kaburi la mama Nyanzala ...na baada kufika pale kaburini alichukua mayai na nazi kisha akanuia maneno ambayo yalikua ni yakumuweka sawa baba Nyanzala ili kila mama Shani atakalo sema basi baba Nyanzala asilipinge(Limbwata)...Basi mama Shani kila alipo nuia ndivyo alivyo pasua kimoja baada yangine pale juu ya kaburi la marehem mama Nyanzala ...."ndio lazima nianze na baba yake kisha ndio nifatie mwanae teh teh teh "...Aliongea hivyo mama Shani mala tu alipo maliza kupasua mayai na nazi juu ya kaburi la mama Nyanzala.
Baada kumaliza mambo yake,ndipo alipo tazama huku na kule na hakuweza kuona kitu chochote hivyo alirudi ndani ili akalale...lakini kabla hajaingia ndani mama Shani ambae ndio mama yake wa kambo Nyanzala ,mala ngafla.....
Alishtuka baada kuhisi mtu akitembea nyuma yake,na bila kucheelewa aligeuka ili amtazame mtu ni nani..Lakini hakuwza hukuona kitu...Hivyo alipuuzia kisha akaingia ndani na moja kwa moja alipitiliza mpaka chumbani kwake kisha akalala.
Kiukweli amani ilitawala ndani ya moyo wa mama Shani kwani zoezi la kumfunga kifra baba Nyanzala alikua tayali kashalikamilisha na hayo yote aliyafanya ili atakapo amua kitu basi baba Nyanzala asikatae..Ivo basi furaha ilizidi kwa mama Shani na mwishowe usingizi ukawa umempitia wakati huo baba Nyanzala nae alikua tayali kasinzia hivyo hata yale mambo aliyoya yafanya mke wake juu ya kaburi la mama Nyanzala hakujua.
***********
Naam.Hatimae asubuhi ilipambazuka...
asubuhi ambayo ilikua siku ya juma mosi hivyo Nyanzala na watoto wa yule mama yake wakambo hakwenda shule....pia hata baba Nyanzala nae siku hiyo hakwenda kazini kwake maana alikua akijisikia vibaya mwili mzima.
Basi watoto wote waliamka na kunawa uso lakini siku hiyo ilikua tofauti kwa binti Nyanzala kwani mpaka inatimia saa tano asubuhi alikua bado yumo ndani kalala...Na hivyo baba Nyanzala ikabidi amuuulize mke wake mama Shani.."vipi kuna mahala umemwagiza Nyanzala??..Baba Nyanzala alimuuliza mke wamke wake kwa sauti ya upole..."me sijui bhana labda huwenda kaenda kuwanga"...Hilo ndio jibu alilo litoa mama Shani..ambapo baba Nyanzala aliishia kutabasam tu huku akimwambia"aamna mke wangu hatuwezi juwa labda yale mayai na nazi alikua...."..kabla baba Nyanzala hajamalizia sentence yake mala ghafla mama Shani alidakia kwa kusema...."acha upuuzi we mbaba haya embu zunguka nyuma ya nyumba kwenye kaburi la mama yake harafu ukirudi unipe jibu na sio kuongea ongea tu"...Aliongea hivyo mama Shani kwa sauti kali...."kaburini?..kwani kuna nini??..Nae baba Nyanzala alihoji kwa mashasha zaidi..lakini mama Shani hakuongea tena jambo lolote.
Hapo ndipo baba Nyanzala alipo nzunguka nyuma ya nyumba yake ambapo lilipo kaburi la marehem mke wake..kiukweli hakuamini machoni mwake baada kukuta vigae vya mayai na nazi iliyopasuliwa juu ya kaburi..."jamani huyu Nyanzala anania gani mbona sielewi eeh"..Alijisemea mwenyewe baba Nyanzala huku akiviondoa vigae vya mayai na vipande vya nazi juu ya kaburi la marehem mke wake...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na baada kumaliza alirudi kichwa chini mpaka mahali alipokua kakaa mama mke wake huku akisuka ukili..."enhee sema sasa umeona nini"..Aliulizwa baba Nyanzala ambae nae alikua kajiinamia muda wote baada kukaa kwenye kigoda..."baba Nyanzala kiukweli me nakwambia huyu mtoto ataua mtu hum ndani shauli yako"..Mama Shani alimwambia hivyo baba Nyanzala huku akiwa ikilikazia hilo suala..."sasa suruhisho nini mke wangu"...Baba Nyanzala aliinua uso wake kisha akamuuliza hivyo mama mke wake ...Lakini mama Shani nae alicheka kwanza kisha akamwambia.."laiti kama ningekua mimi ndio wewe basi ningemtimua nyumbani kwangu"..."nini aah jamani mama Shani sasa kigoli kama Nyanzala ataishi wapi eeh basi vuta subila akihitim darasa la saba tu namtimua sawaee mke wangu.."Hakika yalikua ni maneno mazuli sana kwa mama Kagaruki ambae ndio mama Shani,kwani aliachia tabasam pana huku akimwambia baba Nyanzala..."ndio maana nakupenda sana mme wangu"..Ila rohoni akijinasibu kwa kusem..."naam hapa sasa dawa inafanya kazi"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment