Search This Blog

UKO WAPI MAMA? - 4

 





    Simulizi : Uko Wapi Mama?

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Hakika alifurahi saana mama Shani baada baba Nyanzala  kumwambia kuwa mala Nyanzala  atakapo hitimu  Elimu ya darasa la Saba atamfukuza nyumbani kwake. Hali  iliyompelekea mama Kagaruki kujinasibu kwa kujisemea kuwa dawa inafanya kazi.

    Basi baada hapo Nyamzala aliamka kisha akajikongoja pole pole kuelekea chooni kujisaidia..hakika alionekana uso wake ukiwa umevimba kwa sababu ya kufinywa finywa na mama yake wa kambo usiku uliopita...

    "Shkamoo baba shkamoo mama"...Nyanzala alimsalimia baba yake na mama yake wa kambo ambapo walikua wamekaa chini ya mwembe uliokua kando ya nyumba yao,lakini cha ajabu ile salamu aliitikia baba yeke tu huku mama yake wa kambo akiendelea tu kusuka kilago kama vile hakuisikia salamu.

    Nyamzala akaenda chooni..Ila  alipotoka chooni kujisaidia mala ghafla aliitwa na baba yake..."Nyanzala embu njo hapa"...Nyanzala alitii wito.."ivi unalala hadi saa sita kasoro unamaisha gani wewe"..Baba Nyanzala alimuuliza mwanae kwa sauti ya ukali..lakini Nyanzala hakujibu chochote..."yani unalala mpaka uso unavimba kweli we mtoto hasara ona wenzako waliamka kitambo sana ila wewe tu ndio ulikua umebaki kitandani mpumbafu embu toka mbele yangu"...Aliongea kwa kufoka baba Nyansala huku akimfukuza Nyanzala atoke kando yake....Lakini Nyanzala alipotaka kutoka ndipo mama yake wa kambo alipo mwambia.."haya kuni zinakalibia kuisha pia ndani hakuna maji sasa kazi kwako..ila kabla hujafanya chochote,koka moto kwanza kisha tenga jikoni jungu la maharage haraka sana" Aliabiwa hivyo Nyanzala. Na wakati Nyanzala alipo kua akipewa hayo majukum,cha ajabu watoto wa mama yake wa kambo walikua wakicheza na watoto wengine wa majirani.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nynzala alifanya haraka sana kakoka moto kisha akaweka jungu la maharage jikoni....na hatimae akaanza kazi ya kufuata maji kisimani hivyo alipo rudi ndipo alipo chukuwa panga ambalo halikua na makali siku zote kisha akaingia polini kuchanja kuni.

    Hivyo wakati Nyanzala akichikichia polini kuchanja kuni..huku nyumbani nako sasa.. watoto wa mama yake wa kambo Kagaruki na Shani pia watoto wengine baadhi walipokua wakicheza michezo yao ya kutafutana mahali alipo jificha mwenzake..Hatimae mmoja alizunguka nyuma ya nyumba kujificha lakini punde si punde alipiga kelele baada kumwona nyoka mkubwa aina ya chatu akiwa juu ya kaburi la mama Nyanzala huku akiota jua..Hakika zile kelele ziliweza kuwashtua baba Nyanzala na mke wake,hivyo haraka sana walizunguka nyuma ya nyumba ambapo zilipo tokea kelele za mtoto wao lengo ni kujua kakutwa na nini..."mungu wangu nyoka  gani huyu??  Kiukweli Baba Nyanzala na mke wake hawakuweza kuamini machoni mwao baada kumwona nyoka mkubwa akiwa kajizungusha juu ya kaburi huku akiwa ametulia bila wasiwasi..Kwa woga aliokuwa nao mama yake wa kambo Nyanzala,hatimae  alipiga mayowe yaliyo weza kukusanya wana kijiji na baadhi yao walikuja na mapanga na mikuki baada kusikia kuna nyoka mkubwa nyumbani kwa kina Nyanzala .na wakati hayo yakiendelea,yeye Nyanzala alikua bado yupo polini kutafuta kuni.

    Wanakijiji walikusanyika kwa wingi nyumbani kwa akina Nyanzala kumshangaa nyoka mkubwa akiwa juu ya kaburi...na ndipo mmoja kati ya wanakijij waliokuwepo pale eneo la tukio aliamuru wampige yule nyoka,lakini kila mmoja akawa anaogopa kuanza hivyo ukuwa mwendo wa kutegeana..."amini atakae thubutu kunirushia siraha yake basi ahakikishe awe na mbio la sivyo atakiona cha mtema kuni"...Ilikua ni sauti iliyotoka mdomoni mwa yule nyoka..na ndipo wale wanakijiji walikua wamepania kumuua yule nyoka walishusha siraha zao chini huku wakistaajabu nyoka kuongea kama binadam..

    "namtaka mwanangu Nyanzala "Aliongeza kuongea hivyo yule nyoka,kitendo ambacho kilizidi kuwashangaza wanakijiji na hivyo walizidi kuongezeka kwa wingi hadi wengine walikua wakitoka vijiji jirani lengo kushangaa lile tukio la nyoka kuongea kama binadam.



    Na wakati hayo jakijili,punde si punde Nyanzala nae alilejea nyumbani kutoka polini huku akiwa na mzigo wa kuni kichwani...hivyo alishangaa baada kukuta umati mkubwa wa watu ukiwa umefulika nyumbani kwao..Alijiuliza "kuna nini kimetokea nyumbani??..Alijiuliza hivyo,huku akitua mzigo wa kuni chini.

    Na mala baada kuutua tu watu wote waliokuwepo pale walimtazama Nyanzala kwa mashasha zaidi..na baadhi yao walimuita asogee kwenye kaburi la mama yake..Kweli Nyanzala hakufanya kosa alijongea hadi mahali lilipo kaburi la mama yake ndipo Alito  mkuta nyoka mkubwa akiwa juu ya kaburi...Yule nyoka nae alipo muona Nyanzala alimuita..."mwanangu Nyanzala ,nakuomba uje hapa nilipo mama yako"..Masikini Nyanzala nae hakuogopa alimsogelea yule nyoka..Na baada kumsogelea Nyanzala aliulizwa na yule nyoka mahali alipo kua,hivyo Nyanzala aliogea ukweli bila kuongopa.."nilikua polin kuchanja kuni.."Alijibu Nyanzala .."na chakula umeshakula?..."hapana bado sijala.."  Kwa hakika Nyanzala alikua akiulizwa maswali hayo  na nyoka.Nae akijibu machozi yakimtoka kunako mboni zake yote ni kwa sababu ya kukumbuka manyanyaso ambayo anapewa na mama wa kambo ambae ni mama Kagaruki .



    Hivyo baada Nyanzala kujibu kuwa bado hajala chakula,hatimae yule nyoka alikakamaa mashavu yake..kitendo ambacho kilisababisha watu wote kusambalatika kwa woga wakidhania kua yule nyoka anataka kuwatemea mate..lakini kumbe yule nyoka alikakamaa huku akijiandaa kutema chakula ili Nyanzala apate kupoza chango la njaa...Kweli punde si punde mdomoni mwa yule nyoka zilitoka sahani mbili za wali kama ilivyo ada huku pembeni kukiwa na ndizi mbivu pamoja na Nyama..Hakika watu wote walibaki midomo wazi haswa mama Kagaruki ambae ndio mama yake wa kambo Nyanzala ,hakuweza kuamini kama ni kweli kilichokua kikiendelea pale kwenye kaburi la  mke mwenza...."kula kwanza chakula mwanangu harafu ndio nianze kumwadabisha huyu mtu anaekufanya ulimwengu kuuona mchungu"...Aliongea hivyo yule nyoka mbele ya umati ulikuwepo pale.Na miongoni mwa watu hao alikuwemo baba Maria..."naam hapo sasa huyu mama Kagaruki ndio atajua dunia iko vipi"..Alijisemea hivyo baba Maria huku akimwangalia mama Kagaruki ambae nae alikua kasimama pembeni yake.





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bada Nyanzala kumaliza kula chakula,sahani zilipotea kimaajabu na hakuna mtu hata mmoja aliejua jinsi sahani zilivyo potea....Wakati huo punde si punde wanakijiji waliokuwepo pale walitawanyika baada kusikia yule nyoka akifoka kama upepo wa kimbunga huku ardhi ikitetemeka kama tetemeko linapita..."Kila mtu aliekuwepo hapa nataka asikimbie na kama utakimbia basi ujue tutaungana safari ya kwenda akhela"...Ni amri iliyotoka kinywani mwa yule nyoka huku sauti yake ikijurudia mfano wa mwangwi..Basi wanakiji wale walitulia huku kwa mbaali yakimiminika magari ya watu watokao mjini lengo kuja kumshuhudia nyoka anae zungumza kama binadam...kumbe habali ziliweza kusambaa maeneo tafauti kuhusiana na yule nyoka..

    "Haya namtaka mama Kagaruki na baba Nyanzala wote waje mbele yangu"

    Aliongea hivyo yule nyoka,wakati huo akiwa yupo pembezoni mwa kaburi kajivilingisha huku kichwa kikiwa juu..Wakati huo Nyanzala nae akiwa amemkalia juu. .jambo ambalo liliwashangaza watu wengi waliokuwepo pale kwenye tukio...nadhani labda ingekua zama hizi za smartphone basi watu wangepiga picha nyingi lakini bahati mbaya ilikua enzi za barua.

    Hakika mama Kagaruki na mume wake baba Nyanzala waliogopa kwenda baada kuitwa na yule nyoka...na hivyo yule nyoka baada kuona hawatokei alijikunjua kisha akajivuta mpaka mahali alipokua amesimama mama Kagaruki ambae ndio mama yake wa kambo Nyanzala ..."baba Nyanzala yuko wapi"..Aliuliza hivyo yule nyoka huku akijikunja kwenye mwili wa mama Kagaruki kwa lengo la kumvunja mbavu zake....Maskini ya mungu mama Kagaruki alipiga mayowe huku akimwita baba Nyanzala lakini nae baba Nyanzala aligoma kumsogelea yule nyoka ambae kimwonekano alionekana kua na hasira kali.

    Na baadhi ya watu waliokuwepo pale eneo la tukio waliweza kumwambia baba Nyanzala akamwokoe mke wake ambae alikua katika imaya ya yule nyoka...lakini bado vilevile baba Nyanzala alikataa katukatu kumwokoa mke wake....Na hivyo baadhi ya wazee wa kijiji walikaa faragha kwa dakika chache tu wakaona ili yule nyoka amwachie mama Kagaruki ,wamchukue Nyanzala kisha apelekwe mbali ili yule nyoka amwache mama Kagaruki amfuate Nyanzala ...kweli plan yao hao wazee ilienda sawa kwani waliwateua   vijana watatu ambapo walimvuta Nynazala kisha wakaondoka nae huku Nyanzala akilia kwa sauti..."mamaaa mamaaa mamaa"...Yule nyoka baada kusikia sauti ya Nyanzala alimwachia mama Kagaruki na kisha kumfuata Nyanzala ....Wakati huo mama Kagaruki ameshapoteza faham kwa mshtuko.

    Hakika yule nyoka aliteleza kama mlenda huku akimfuata Nyanzala ambae alichukuliwa na baadhi ya wanakijiji lengo kumsaidia mama Kagaruki ambae alikua tayali kashaingia kunako imaya ya nyoka....Hivyo dakika tatu nyingi yule nyoka aliwafikia wale watu walimteka Nyanzala,na bila kuchelewa aliwagonga mmoja baada ya mwingine hiyo yote ni kutokana na hasira alizo kua nazo yule nyoka....Na chaajabu zaidi kila aliegongwa na yule nyoka,alibadilika rangi kua wa blue na kisha kuaga duniani...Baada ya yule nyoka kuwateketeza wale wanakijiji,ndipo alipo alipo mwambia Nynzaalw..."usijali mwanangu Nyanzala mama yako nipo nyuma yako na hao wanaokufanya dunia uione chungu hakika dawa yao ipo jikoni maana hiyo ni trela tu..kwaheli"

    Ilikua ni sauti iliyokua ikitoka kinywani mwa yule nyoka huku sauti ikijirudia mala mbili mbili kama mwangwi,Kwisha kusema hayo yule Nyoka alimuaga Nyanzala kisha akatokomea polini.

    * ******************

    Naam.Basi baada hayo kupita ndipo wanakijij waliokua wakishudia yale matukio hatimae walifuatilia mburuzo mahali alipopita yule nyoka baada kuwafata wale watu waliokua wamemchukua Nyanzala ...na wengi wao walisikika wakiwasifu wale vijana kwa plan waliyoifanya kwani laiti kama wasingefanya hivyo basi mama Kugaruki angefariki....Lakini sasa baada kusonga mbele zaidi..hakika wanakijiji wale waliofuatilia mbuluzo wa Nyoka hawakuamini kile walichokutana nacho mbele yao kiukweli walijiuliza ni sumu gani aliyokua nayo yule nyoka kwa sababu miili ya wale watu waliogongwa na yule nyoka ilikua imevimba huku paji za nyuso zao zikiwa nyeusi..Na wakati huo wakishanga shangaa,Nyanzala nae alikua pembeni akiwatazama..kiukweli kila mmoja alimtazama Nynzala huku wengine wakimwogopa kabisa. Na jioni ilipoingia hatimae mama Kagaruki alizinduka huku akipiga kelele ..."nisamehee"..Lakini baadhi ya majirani zake waliokua wakimpepea muda wate walimtuliza na ndipo mama Kagaruki alipotulia..Hivyovkadli muda ulivyozidi kwenda ndipo nae mama Kagaruki alizidi kupata nguvu mwishowe alijiweza kabisa...

    "jamani ahsanteni sana tena saana maana daa kweli ilikua balaa" Alisema Baba Nyanzala akiwashukuru watu waliompepea mke wake hadi kuzinduka.







    Naam kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo mama Kagaruki alizidi kupata nguvu na mwishowe alijiweza kabisa...

    "jamani ahsanteni sana tena saana maana daa kweli ilikuwa balaa"

    Aliongea  baba Nyanzala akiwashukuru watu waliohusika kumpepea mke wake mama Kagaruki.Na mara baada watu hao kuondoka  mama Kagaruki alimuita Nyanzala .."we Nyanzala"..."abee mama"...Nynazala alimuitikia mama yake wa kambo kwa nidham..."embu njoo haraka sana kabla sijaja kukubomoa"...Kweli wahenga walisha sema sikio la kufa siku zote huwa halisikii dawa..Kwani licha ya mama Kagaruki kunusulika kifo ila bado alionyesha kiburi na jeuri kwa yatima Nyanzala. Nyanzala alitii wito haraka sana..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mama Kagaruki akamwambia "hivi hii jeuri we mtoto unaitoa wapi?."Aliuliza  mama Kagaruki huku akimwoshe Nyanzala jungu la maharage yaliyoungulia...Maana mkumbuke kabla ya hayo matukio kutokea. Tukio la Nyoka kutaka kumuua mama Kagaruki .Nynazala aliambiwa atenge jungu la maharage jikoni kisha afate maji mtoni na ndipo aende polini kutafuta kuni.lakini baada ya kutokea yule nyoka pale kwenye kaburi la mama Nynzala.Hakuna aliyedili na chungu cha maharage yaliyokuwa jikoni maana kila mmoja alikuwa na hekaheka na hata Nyanzala nae alipotoka polini kutafuta kuni hakuweza kuongeza maji kwenye chungu bali moja kwa moja alielekea kunako kaburi la mama yake ili ashuhudie kilichokua kikiendela...Na mwishowe sasa zigo likasukumwa kwa Nyanzala kuwa kaunguza mboga.

    "enhee embu niambie sasa

    takula nini usiku huu??..au tutamla yule nyoka wako? alisema mama Kagaruki,Lakini licha ya Nyanzala kuambiwa maneno hayo hakuweza kujibu chochote,hapo mama Kagaruki akaongeza kwa kusema "sasa nakwambia hivi we si jeuri?.hivyo

    utakula jeuri yako mjinga wewe toka mbele yangu "

    Nyanzala aliambiwa hivyo...Lakini yote kwa yote aliishia kulia huku akielekea chumbani kwake kulala...Wakati huo baba yake akiwa pembeni tu akisikiliza taarifa ya habari kwenye redio mbao yake  akijifanya kama hamsikii jinsi mama Kagaruki  anavyo mnyanyasa Nyanzala.

     Nyanzala aliingia chumbani kwake kisha akapanda kitandani  akawa amelala bila kula siku hiyo...kwani hata yule nyoka aliyekuwa akimpatia chakula saa za usiku kiukweli siku hiyo hakutokea na hivyo Nyanzala akawa amelala njaa.

    Asubuhi ilipo pambazuka,pia ilikuwa siku ya wanafunzi kupumzika maana ilikuwa siku ya juma pili hivyo Nyanzala na watoto wa mama yake wa kambo hakwenda shule,Nyanzala alijiandaa kwa niaba ya kwenda kanisani kwenye ibada ya watoto(Sunday school)lakini mama yake wa kambo alimkataza huku akimwambia kwa sauti ya ukali.."unakwenda kanisani utakula kanisaaa...eeh je hivi vyombo unategemea nani avioshe pumbafu..sasa olewako unyanyue mguu wako eti unaenda kanisani ntakupiga mpaka ukome mjinga wewe" Alisema Mama Kagaruki akimwambia Nyanazala huku akimsumbua kwa kumsukuma sukuma kwa kidole chake kwenye uso wa Nyanzala ...Basi nae Nyanzala baada kuambiwa hivyo ilibidi abadilishe nguo zake ambazo alikuwa tayali kazivaa kwa niaba ya kwenda kanisani kisha akavaa nguo za kushindia,mara baada ya hapo alikusanya kila chombo kichafu kilichokuwemo ndani kisha akaviosha vyote hali ya kuwa watoto wa mama yake wa kambo wao wakiendelea na michezo ya hapa na pale huku mwenyewe mama Kagaruki nae akiwa pembeni akijipodoa.

    Hatimae Nyanzala alimaliza kazi ya kuosha vyombo na kabla hata hajapumzika aliambiwa akachote maji mtoni istoshe aliwekewa pipa siku hiyo,na kwa kuwa Nyanzala usiku uliopita alilala bila kula hakika nguvu zilimuishia kabla hata hajajaza lile pipa alilo wekewa na mama yake wa kambo lengo ikiwa kumkomoa  huyo yatima .

    "nakwambia hivi usipo lijaza hilo pipa basi hutokula kamwe chakula nilicho pika mimi labda uende kwenye ya kaburi la mama yako ukaombe

    chakula"..Alisema mama Kagaruki,wakati huo Nyanzala akiwa kakaa chini akilia ili apewe chakula na ndipo aendelee na kazi aliyopewa, kilio hicho cha Nynazala kilimfikia baba Maria ambae nyumba yake na yakina Nyanzala hazikuwa mbalimbali hivyo nae aliamuea kwenda kushuhudia kitu kilichokuwa kikimliza Nyanzala..."habali za saa hizi mama Kagaruki "...Baba Maria alimsalimia mama Kagaruki lakini nae aliitikia hiyo salam kama hataki..ila potelea mbali baba Maria hakujali maana alikuwa anajua tabia aliyonayo mama kagaruki. Hivyo moja kwa moja baba Maria alimsogelea Nyanzala ili ajue nini haswa kinacho mliza..."Nyanzala mama"... Baba Maria alimuita Nyanzala. Nyanzala akaitika huku akipandisha kwikwi..."mbona unalia kuna nini"..Aliuliza  baba Maria,lakini Nyanzala aliogopa kusema akihofia kupigwa na mama yake wa kambo...na hapo ndipo baba Maria alipo utumia utu uzima wake kwani aliweza kumshawishi Nyanzala aseme ukweli. Hatimae Nyanzala alisema ukweli wote,kitendo ambacho kiliweza kumkera baba Maria mpaka akanza kumtukana mama Kagaruki ..basi nae mama Kagaruki alishindwa kuvumilia maneno ya baba Maria na ndipo alipo jibu mashambulizi hivyo ikawa vita ya maneno ambayo iliweza kuvuta baadhi ya majirani kuja kushuhudia ugomvi...Wakati ugomvi huo unaendelea,baba Nyanzala yeye alikuwa  kaelekea kijiji jirani kwa shughuli mbali mbali. Basi ugomvi uliendelea kati ya baba Maria na mama Kagaruki lakini mwishowe baba Maria aliamuwa kuondoka,kwani aliona kubishana na mwanamke ni upuuzi,ila sasa wakati anatoka tu pale nyumbami kwa mama Kagaruki ,mara ghafla baba Nyanzala nae akarejea huku akionekana kashika kitu mkononi ambacho kilikuwa kimefunikwa na kitambaa chekundu..Baba Nyanzala alipitiliza kwanza moja kwa moja mpaka ndani kisha akatoka nje mikono mitupu huku kile kitu alichokuwa nacho akikiacha ndani.

    "mmh habali yako mke wangu"...Baba Nyanzala alimsalimia mke wake lakini mama Kagaruki hakuitikia salam ile ya mumewe huku akionekana kanuna.."hivi baba Nyanzala kati ya baba Maria na mimi ni nani mwenye mamlka juu ya ya Nyanzala ??..Alihoji  kwa hasira mama Kagaruki ..nae baba Nyanzala bila kuchelewa alimjibu"wewe ndio mwenye mamlka na sio huyo mzee baba Maria"...

    "sawa vizuri sana,sasa iweje atoke nyumbani kwake moja kwa moja aje nyumbani kwangu kunipiga eti namtuma sana Nyanzala kwanini lakini"...Mama Kagaruki aliongeza tena kwa kusema hivyo huku akilia kitendo ambacho kilimuudhi baba Nyanzala na bila kumfkilia alichukuwa uamuzi wa kwenda nyumbani kwa baba Maria kugombana nae na kwa bahati mbaya baba Maria miaka mingi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa kifua kikuu hivyo kile kitendo cha kujihami na kipigo kutoka kwa baba Nyanzala ,hatimae alianguka chini kisha mapovu yakamtoka mdomoni na mwishowe akawa amefariki.





    Bada baba Nyanzala kuona hali ile hakuweza kurudi nyumbani kwake kwani alijua tayali ni msala hivyo moja kwa moja ilikimbilia polini kujificha...Kumbe wakati alipo kua akigombana na baba Maria,alionwa na moja kati ya wanakijiji hivyo yule alie shuhudia tukio aliamua kwenda kwa mwenyekiti wa kijiji kureporti baada kushuhudia mwanzo mpaka mwisho hadi baba Maria alipo poteza maisha.

    Na wakati hayo majanga yakiendelea,huku nyumbani nako Nyanzala alikua akila kipigo kutoka kwa mama wa kambo huku akimwambia"kwani unidhalilishe hadharani eeh sasa leo ndio utanijua vizuli kenge wewe na hata huo nyoka wako akitaka aje tu pumbavu,je  Baba  Maria  anakulisha"...Kiukweli mama Kagaruki aliongea hivyo kwa kujinasibu akisahau jinsi gani alivyo kabwa na yule nyoka mpaka akazimia...Ama kweli sikio la kifa halisiki dawa.

    Mama Kagaruki alimpiga sana Nyanzala na akaona hautoshi ndipo alipo chuku kuni yenye moto kisha akumuunguza Nyanzala pembeni kidogo na sehem za siri..Hakika ilikua ni adhabu kumbwa iliyomfanya Nyanzala kulia saana mpaka sauti ikakata huku sehem yake ya siri ikivuja dam kwa wingi..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hivyo baada mama Kagaruki kuona vile jinsi Nyanzala anavyovuja dam nyingi sehem yake ya siri,hatimae alimnyanyua kisha akamwingiza ndani akiogopa mtu mwingjne yoyote asishuhudie unyama ule...Kweli baada kumungiza ndani Nyanzala hatimae mama Kagaruki alitoka nje kwenda kuzifukia zile damu zilizokua zimesambaa lakini kabla hajamaliza tu mala ghafla walikuja wanakijiji huku wakiwa na siraha tofauti tofauti wakimtaka baba Nyanzala ili na yeye wamuue kama alivyo muua baba Maria...Ila sasa kabla wale wanakijijji hawajafanya tukio lolote mala ghafla kaburi la mama Nyanzala lilianza kutikisika huku kwa mbali kikitokeza kichwa cha nyoka mkubwa kuliko wa siku zote.

    Hakika kaburi la mama Nyanzala hatimae lilijipasua mala mbili kisha likatoka joka kubwa naweza sema zaidi ya anaconda...Hivyo wale wanakijiji waliokuwa wamekuja na siraha ili kuumua baba Nyanzala ambae nae alikua kamuua baba Maria,waliweza kukimbia licha ya kua na siraha asilia mikononi mwao maana kwa jinsi yule nyoka alivyokua mkubwa kamwe vishoka na mapanga yao yasingeweza kufanya chochote kwa yule nyoka.

    Nyanzala akiwa ndani alisikia sauti zikisema "Nyoka nyoka jamani Nyoka .." Hakika Nyanzala aliposikia hizo sauti,alijuwa kuwa mama yake karudi. Ghafla akatabasamu akajivuta polepole kutoka nje. Punde si punde  aliyafuta machozi baada kumwona yule nyoka haraka sana bila kuogopa alimkimbilia...."mama nateseka mwanao hakika safari huwezi kuniacha me nihangaike peke yangu lazima twende wote huko uliko mama"...Nyanzala alimwambia hivyo yule nyoka huku kwa mbaaali milimani wakionekana watu wakija nyumbani kwa kina  Nyanzala kuja kushudia maajabu mengine maana wale wanakijiji waliokua wamevamia nyumbani kwa baba Nyanzala  walipoondoka walisambaza habali kwamba yule nyoka anae onge kama binadam karudi tena na hivyo wakawa wanitana ili waje waone balaa lingine...."Nyanzala mwanangu nadhani nilisha kwambia kua dawa ya hawa watu wanaokufanya dunia uichukie ipo jikoni ila sasa nina habali njema kwako mwanangu hatimae dawa imechemka na tayali imeiva bado kuwapa dozi"....Hahahahaaaaaaa japo me ndio mtunzi wa hii riwaya Alexis  wamillazo KING niacheni nicheke kidogo....Basi yule nyoka baada kusema maneno hayo aliamuru watu waliokuwepo pale wamlete mama Kagaruki mbele yake,kweli nao hawakugoma walijitolea vijana wanne wenye nguvu zao walimfunga miguu mama Kagaruki kisha wakampeleka mbele ya yule nyoka......"Ni miaka mingi sana huyu mama akimnyanyasa mwanangu hakika namimi kama mzazi wa mwanangu Nyanzala nilikua naumia sana kule niliko ekhela,lakini ninacho taka kuwambia uma wa watu mliopo hapa ni kwamba mwisho wa manyanyaso kwa Nyanzala imefikia kikomo..sasa basi yoyote atakae jaribu kufanya figisu za kumwokoa mama huyu mwenye roho ya kinyama basi nitakula nae sahani moja"...Maneno yote hayo yalikua yakitoka mdomoni mwa yule nyoka alietoka kwenye kaburi la marehem mama Nyanzala...wakati huo wanakijiji waliokuwepo pale wote walikua kimya ila tu mama Kagaruki ndio alikua akihaha jinsi ya kujikomboa..huku Nyanzala akiwa pembeni yake akiendelea kuvuja dam sehem ya siri,kitendo ambacho kiliwaumiza watu wote walioshuhudia jinsi Nyanzala alivyokua akivuja dam....mpaka baadhi yao waliona kama yule nyoka anachelewa kumwadhibu mama Kagaruki

    Na mala baada Mama kagaruki kupelekwa mbele ya yule Nyoka..ndipo yule nyoka alipo jikunja kunako mwili wa mama Kagaruki kisha akamsimamisha na mwishowe akamvunja uti wa ugongo alafu kiaina yule nyoka akang'atuka akimwacha mama noeli akigagaa chini akiomba msaada akiwa hawazi hata kukaa...."mamaaaa mgongo wangu mimiiii mgongo wanguuuu"Kiukweli alilia sana mama Kagaruki huku akifikilia zaidi maisha yake yatakuaje hapo mbeleni haliyakua akiwa hana tena uwezo wa kukaa wala kusimana...lakini yote kwa yote kilio chake hakikuweza kumshawishi yule nyoka asifanye mambo yake kwani baada kumaliza shughuli ya kumvunja mgongo mana,pia alimtemea mate usoni..mate ambayo yaliweza kuharibu mishipa ya macho mwishowe mama Kagaruki akawa haoni yaani kipofu......Lakini wakati hayo yakijili Nyanzala alikua tayali kapoteza faham baada kutokwa na dam nyingi sehem ya siri ila wanakijiji hawakuweza kumsaidia walimwogopa sana yule nyoka asije akawajeruhi kama ilivyokua kwa mana Kagaruki.....Na baada yule nyoka kumaliza kazi yake alimwita Nyanzala lakini Nyanzala hakuitika kwa sababu alikua kapoteza faham ila yule nyoka alijua dhahili Nyanzala tayali kaaga dunia kwa sababu ya kutoka na dam nyingi ."Naam..kazi yangu sasa nimeimaliza hakika sijataka kummaliza kabisa huyu mama ila kwa hili jambo nililomfanyia basi natumai hii dunia ataiona chungu..Ahsanteni mhifadhini mwangu me naondoka"...Kweli yule nyoka baada kiongea maneno hayo alirudi pale kaburini ambapo kulikua na mipasuko kisha akatokomea ndani ya kaburi..Na baada yule nyoka kuondoka hatimae baba Nyanzala alijitokeza huku akionekana mtu mwenye wasiwasi kibao...hakaki hakuamini machoni mwake baada  kumwona mke wake mama Kagaruki akiwa chini akilia bila kukoma,huku macho yake yakiwa yamevimba...

    "mama Kagaruki ...mama Kagaruki embu fumbua macho nitazame mimi mme wako" ....Aliongea hivyo baba Nyanzala huku akionekana akilia kwa uchungu...."mume wangu Nyanzala yuko wapi nataka nimuombe msamaha kwa yote niliyomfanyia hakika me si mtu mwema kwake naumia  najutia  mimiii"...Mama Kagaruki alimwambia hivyo baba Nyanzala kwa sauti ya unyonge lakini kumbe Nyanzala nae alipo pelekwa hospital baada kupoteza faham,alifumbua macho mala moja tu kisha akaaga dunia...."mke wangu Nyanzala nasikia kapelekwa hospital akiwa kapoteza faham ila pindi atakapo pata nafuu utaenda hospital kumwomba msamaha"...Baba Nyanzala alimwambia hivyo mkewe mama noeli wakati huo akiwa bado hajapata taharifa kuhusu kifo cha mwanae Nyanzala.



    Baada mama Kagaruki kuzungumza mambo hayo mawili matatu na mumewe,mala ghafla baba Nynzala akashtukia akiwekwa chini ya ulinzi na mgambo wa kijiji....."kuanzia sasa upo chini ya ulinzi unatuhumiwa kwa kesi ya kuua hivyo hatuhitaji maelezo hapa twende utajieleza mbele ya safari"..Alisema mmoja wa wagambo waliotumwa kumkamata baba Nyanzala nae hakua mbishi kwani laiti kama angekua mbishi basi angepigwa vibaya na wale mgambo...Hakika neno moja tu baba Nyanzala alilomwambia mke wake mama Kagaruki ."Mke wangu buriani"..Nae mama Kagaruki baada kusikia neno hilo aliuliza unamaana gani mumewangu??..Ila jibu hakuweza kupata kwani aliuliza wakati huo baba Nyanzala ameshabebwa na mgambo.

    Na wakati baba Nyanzala alipokua njiani na wale mgambo,hatimae alipewa habali kuhusu kifo cha mwanae Nyanzala...kiukweli alilia sana maana mke wake ambae ndio mama Kagaruki alikua amepanga kumwomba radhi kigoli Nyanzala kwa mabaya aliyomfanyia lakini mwishowe mipango ikawa si matumizi....hakika baba Nyanzala alilia sana huku akipanda gari ya police na kisha kupelekwa mahakamani.

    Hivyo basi upelelezi ulifanyika kuhusu kifo cha baba Maria..na ukweli ukabainika kua licha ya baba Maria kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu ila chanzo cha umauti wake ni Baba Nyanzala ....Na hatimae baba Nyanzala alihukumiwa jela miaka 80 na kila asubuhi kupigwa viboko miamoja.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada Baba Nyanzala kufungwa jela,hatimae maisha yakabaki ya mama Kagaruki ambae nae ameshatiwa ulemavu wa mgongo na macho pia,bila kuwasahau wanae wawili na Hamala.Kiukweli shida juu ya shida kwa mwanamke huyo aliyekuwa kiburi na dharau mama Kagaruki maana hata kusimama kwenda kujisaidia akawa hawezi  kila siku yeye alikuwa mtu wa kulialia tu huku akimtaja Nyanzala binti ambae alimsababishia umauti kingali mdogo kabisa.

         Ulikuwa usiku wa saa nane ambapo mama Kagaruki alisikia sauti ya Nyanzala ikimwita Kagaruki ..."kaka Kagaruki kaka kaka Kagaruki ..njoo unifungulie mlango"

     Mama Kagaruki  alipoisikia sauti ya Nyanzala alifurahi sana kwani alijuwa ndio nafasi ya kuweza kumwomba msamaha kwa mambo mabaya ambayo alimfanyia kabla hajatiwa ulemavu wa mgongo na macho...Hivyo mama Kagaruki alimwita Kagaruki kwa sauti kubwa ili akamfungulie mlango Nyanzala ambaye alikua akiita kwa muda mrefu,Kagaruki aliinuka kutoka kitanda kisha akaenda sebuleni kufungua mlango...lakini alipo fungua mlango mara ghafla alipasa sauti..."mamaaaaaaa nyokaaaa" Ilikuwa ni sauti kubwa aliyoipasa Kagaruki akidai kuwa kaona nyoka baada kumfungua mlango,hapo  mama Kagaruki alizinduka kutoka usingizi na kujikuta kwamba ile ilikuwa ni ndoto na sio kweli kuwa Nyanzala alikuja kumwita Kagaruki ili amfungulie mlango.

    Hakika mama Kagaruki palepale kitandani alipokuwa amelala aliweza kuitafakali mara mbilimbili ile ndoto akijiuliza inamanisha nini lakini hakuweza kupata jawabu sahihi,aliumia sana moyoni alitamani hata ndani ya dakika mbili aisikie sauti ya Nyanzala,lakini haikuwa hivyo alivyotaka maana taharifa aliyokuwa nayo  ni kwamba Nyanzala alipoteza maisha baada kutokwa na damu nyingi sehem ya siri aliyomuunguza moto.

    Mama Kagaruki akalia na moyo wake.

    ********



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog