IMEANDIKWA NA : ALEXIS WAMILLAZO
*********************************************************************************
Simulizi : Uko Wapi Mama?
Sehemu Ya Kwanza (1)
"Nyanzala Nyanzala Nyanzala"
"Bee mama" "embu amka unalalaje hadi muda huu,unamaisha gani mwanaidhaya mkubwa wewe" yalikuawa ni maneno ya mama yake wa kambo Nyanzala ambapo asubauhi mapema alisikika akimwita kwa sauti Kali iliyoambatana na matusi ndani yake. Hivyo Nyanzala aliamka kisha akajiaandaa ili aende shuleni,lakini kabla hajaondoka ghafla mama yake wa kambo alimuita na kumwambia "unaweza kwenda shule bila kufanya usafi wa mazingira? Au unataka mama yako afufuke kutoka kaburini ili aje akusaidie kazi zako " Nyanzala hakujibu kitu zaidi alikaa kimya. Na ndipo mama huyo wa kambo alipompiga kofi kisha akarudia kusema "ninapo ongea nahitaji unijibu mbwa wewe,unajifanya msomi kumbe sio lolote sio chochote.. haraka sana Kavue hayo magunia yako na uanze usafi kimburu wewe" Hakika Nyanzala baada kuyasikia maneno yale, aliumia saana moyoni mwake. Punde si punde akatokwa na machozi huku moyoni mwake akijiuliza ukowapi mama?CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nyanzala alibadisha nguo zake za shule akavaa za nyumbani ambazo nazo zilikuwa zimechakazwa na viraka vya kila aina kwani mtoto huyo hakuwa na nguo nyingine zaidi ya sare za shule. Hivyo Nyanzala alifanya usafi wa nyumbani kwa kufagia uwanja na kuosha vyombo,hali ya kuwa upande mwingine nako wale watoto wa yule mama yake wa kambo Nyanzala walikuwa wamependeza wakielekea shuleni kutafuta Elimu itakayo wasaidia hapo baadae. Maskini Nyanzala aliwatazama wale watoto kwa macho ya huzuni hima machozi yake hayakuwa mbali ambapo yaliweza kumtoka ila aliyafuta kwa kutumia nguo yake kukuuu aliyokuwa ameiva. "Unamlilia nani sasa?..acha kuwawekea uchulo wanangu. We wakumlilia kalala palee nyuma ya nyumba sawaeee" Nyanzala alishtuka akiambiwa hivyo na mama yake wa kambo. Maneno ambayo yalizidi kumfedhehesha Nyanzala akajiuliza kwani anafanyiwa vitendo vile na mama yake wa kambo..kosa lake lipi? Lakini wakati akiwaza hayo ghafla alipigwa kofi la mgongoni.. nae aliempiga hakuwa mtu mwingine bali ni mama yake wa kambo mke wa baba Nyanzala ambae alimuoa baada kufiwa na mke wake wa kwanza ambae ndio mama Nyanzala. "We kenge wewe unaosha vyombo mwaka mzima? Fanya haraka uende polini kuchanja kuni pumbafu" "sawa mama nimekuelewa" Nyanzala alijibu kwa sauti ya kinyonge. Kweli baada kumaliza kazi hiyo,alizipiga hatua kuingia ndani kisha akatoka na panga ambalo halikuwa na makali ya aina yoyote. Nyanzala akitokwa na machozi mengi katika mboni zake alichikichia kuingia polini kuchanja kuni kama alivyoamuliwa na mama yake wa kambo. Basi baada Nyanzala kufika polini Alichanja kuni.. hakika haikuwa kazi rahisi kwake kwani panga alilokuwa akitumia halikuwa na makali yoyote. Hali iliyompelekea kuchukuwa muda mrefu kueneza mzigo. Ila baada ya muda wa dakika arobaini,Nyanzala alieneza mzigo ambao kiukweli hata kujitwisha alisumbuka lakini mwishowe alifanikiwa..na hivyo safari ya kurejea nyumbani ikawa imeanza. Njia nzima Nyanzala alikuwa akilia yote ni kutokana na maisha aliyokuwa akiishi tangu aondokewe na mama yake mzazi.
Basi baada ya mwendo mrefu huku akiwa na mzigo mzito kichwani kwake,hatimae Nyanzala alitua mzigo chini ili apumzike. Na baada kupata walau nguvu kidogo..Nyanzala alirudia kujitwishwa mzigo wake moja kwa moja akaanza safari yake hadi nyumbani. Na mala baada kukaribia kufika nyumbani kwao. Mtu wa kwanza kumuona alikuwa ni Kagaruki mtoto wa mama yake wa kambo Nyanzala. Hivyo Kagaruki akasema "Mama unamuona Nyanzala kamzigo alikoleta" kwisha kusema hivyo. .mama yake wa kambo Nyanzala ambae alikuwa amekaa akijipamba aligukia upande ule alikokuwa akitokea Nyanzala kisha akasema "mwache kesho haendi shule lazima arudi tena polini" wakati mama huyo akisema hivyo. Nyanzala alikuwa tayali ameshautua mzigo wake chini ambapo alimsogelea mama yake wa kambo ili amsalimie baada kuachana kwa muda wa masaa kadhaa. "Hivi kwa siku unasalimia mala ngapi mbwa wewe embu toka mbele yangu hapa" Nyanzala alishusha pumzi kwa unyonge akatoka mbele ya mama wake wa kambo..kisha akaingia ndani kunywa maji apoze japo kiu kali aliyokuwa nayo. Lakini baada kunywa maji..ikabadi amuombe chakula mama yake kwani wakati ule tumbo lake nalo lilihisi njaa. "Unataka chakula? Zunguka nyuma ya nyumba hapo utaona kaburi la mama yako hivyo mwombe chakula na sio kuniomba mimi.. wewe hunihusu katika kizazi changu " chozi la mnyonge lilimtoka Nyanzala huku akisema "Mama naomba unionee huruma mamaaa njaa inaniuma mamaaa " alisema Nyanzala kwa sauti iliyoambatana na kilio. Lakini kilio kile cha Nyanzala hakikuweza kumfanya mama yake wa kambo kumuonea huruma zaidi mama huyo alisema" usinililie mimi. Bali mlilie yule mjinga aliekuzaa na kukutelekeza duniani"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Usinililie mimi, Bali mlilie yule mjinga alie kuzaa na kukutelekeza duniani" Nyanzala aliambiwa hivyo na mama yake wa kambo. Kiukweli maneno yaliyozidi kuiumiza nafsi yake akajikuta akilia bila kunyamanza. "Nilisha kuambia masuala ya kuniletea uchulo mimi sitaki mbwa wewe mbona hutaki kunielewa?.. sasa naingia ndani olewako nitoke nikute bado unalia lia " Mama yake wa kambo Nyanzala aliingia ndani. Muda huo huo Nyanzala aliyafuta machozi yake akawa amebaki akililia moyoni. Na baada mama wa kambo kuingia ndani,hatimae alitoka ndani huku akiwa na mzigo wa nguo chafu. Nguo zake na watoto wake,moja kwa moja akazibwaga mbele ya Nyanzala kisha akasema "we mnuka ngozi wewe,unaona nguo hizi.. nataka ukazifue ziwe safiii kama zimetoka dukani leo leo tena ufanye haraka kabla baba yako hajarudi kutoka shamba " alisema hivyo mama yake wa kambo Nyanzala. Nyanzala alizitazama zile nguo kisha akainua paji la uso wake. Ama hakika machozi yalimtoka kila alipokuwa akijaribu kuyazuia alishindwa kwani nguo zile zilikuwa nyingi mno tofauti na umri aliokuwa nao"Sawa mama mimi nipo tayali kuzifua hizi nguo,lakini mama nisaidie japo chakula kidogo nile ili walau nipate nguvu za kufiria hizi nguo..mama naomba mama" alijibu Nyanzala kwa huzuni kubwa iliyoonekana machoni. "Nimesha kuambia chakula kachukuwe kwenye kaburi la mama yako na sio kuniomba mimi.. wapo watu wa kuniomba chakula ambao ni Kagaruki na shani pia baba yako..ila wewe haaah! Hupati kitu" "sawa mama" Alijibu Nyanzala kisha akazikusanya zile nguo alizorundikiwa na mama yake wa kambo. Moja kwa moja akaelekea kisimani kufaua. Wakati huo watoto wa mama yake wa kambo Nyanzala wao walikuwa wakicheza ambapo waliachia kicheko baada kumtazama Nyanzala ambae alikuwa amebaba furushi la nguo mfano wa mtu mkimbizi. Basi hatimae Nyanzala alifika kisimani akatua mzigo wa nguo chini,na kabla hajaanza kazi yake ya kufua. Alikaa kwanza chini kwanza kisha akajiinamia na kuanza kujiuliza "hivi kwanini natesaka kiasi hiki? Kwanini mama umekufa mapema? Embu tazama sasa mwanao ninavyoteseka mama mama mama uko wapi mamaaaaaaa!" Maskini Nyanzala akaanza Kulia kwa uchungu..lakini kilio chake kilikata baada kuinua uso wake na kisha kutazama pembeni yake ambapo aliona mzigo mkubwa wa nguo chafu zikingojea kufuliwa. "Tena ufanye haraka kabla baba yako hajarudi kutoka shamba " Nyanzala aliyakumbuka maneno hayo ya mama yake wa kambo..haraka sana alinyanyuka na kisha kuanza kufua.
Baada kufua kwa muda mrefu..hatimae Nyanzala aliweza kuzimaliza japo kwa mbinde. Hivyo binti huyo aliamua kuoga hapo hapo kisimani kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani kwao ambapo baada kufika alikuta baba ameshafika nyumbani. Wakati aliambiwa na mama yake wa kambo kuwa arudi kabla baba yake hajafika. "Shani fanya haraka kampokee dada yako au humwoni kaelemewa na mzigo? Alisema mama Shani mama yake wa kambo Nyanzala ambae alikuwa akiyaficha makucha yake ili asigundulike na mume wake baba Nyanzala. "Pole mama yangu wee pole saana ndio maana mimi nakupenda " Mama yake wa kambo Nyanzala alizidi kujionyesha kuwa ni mtu mwema mbele ya Nyanzala kwa kumwabia maneno hayo mazuri. Lakini Nyanzala hakusema chochote zaidi baada kumaliza kuanika nguo aliingia ndani bila kusema na mtu yoyote. Hivyo kitendo kile kilimshangaza sana baba Nyanzala ambae alikuwa amekaa pembeni kidogo ya nyumba akisikiliza radio. "Nyanzala Nyanzala Nyanzala " baba Nyanzala alimwita mwanae ili ajue kitu gani kilicho mfanya asimsalimie wakati kutwa nzima hawajaonana. Nyanzala alitii wito ambapo baba Nyanzala kwa sauti ya upole alimuhoji mwanae "mwanangu kwanini hujanisalimia? Wakati kutwa nzima hatujaonana..ama unanini Leo maana sio kawaida yako" Alisema baba Nyanzala huku akimtazama mwanae. Basi Nyanzala baada kuyasikia maneno hayo ya baba yake alilia tu bila kusema chochote..na mwishowe aliamua kurudi chumbani kwake. Wakati huo upande wa pili mama Shani alikuwa akiendelea na kazi yake ya kuandaa chakula. Baada ya muda kadhaa chakula kilikuwa tayali hivyo wakala kisha wakasambaa kwenye vyumba vyao hali ya kuwa baba Nyanzala akiwa na sintofaham kuhusu kilio kile cha mwanae.
Asubuhi ilipo pambazuka baba Nyanzala alimuaga mke wake tu kwamba anakwenda katika kazi yake ya machimbo..ambapo katika kazi hiyo atakaa ndani ya siku tano. Mama Shani mke wa baba Nyanzala ambae ndio mama yake wa kambo Nyanzala,aliamtakia safari njema mume wake. Na mala baada baba Nyanzala kuondoka,mama wa kambo aliingia chumbani kwa Nyanzala na kisha kumkuripusha kutoka usingizi kwa kumginya sehem mbali mbali za mwili wake..bila kusahau kipigo kikali alichokuwa akikitoa kwa Nyanzala akimpiga bila kuangalia sehem ya kupiga "Jana nilikwambia nini? Eeh kwanini ulichelewa kurudi ulipoenda kisimani? Sasa leo utanitambua mimi ni nani mbwa koko mkubwa wewe" mama huyo wa kambo alisema maneno hayo huku akiendelea kumpiga Nyanzala. Maskini Nyanzala alilia saana "Mama nakufaaa mama nakufaaa mamaa njoo uniokoe.. nisameheeee" Hakika Nyanzala alipasa sauti kwa uchungu wa maumivu aliyokuwa akiyapata asubuhi yote ile mapema..lakini baadae sauti ile ilikata ghafla. Nyanzala alizimia baada Kulia kwa muda mrefu.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nyanzala akawa amepoteza fahamu baada kupigwa kikatili na mama yake mzazi. Ambapo mama Shani alishtuka kuona pumzi ya Nyanzala imekata ghafla,hivyo akaanza kuhaha huku na kule kitenge chake kikiwa hakitulii kiunoni kwake. Yote hiyo ni hufu ya kudhania kuwa amemuua mtoto wa watu. Basi haraka sana mama shani alianza kumpepea Nyanzala. Lakini Nyanzala hakuzinduka kitendo ambacho kilimtia woga mama Shani ambae ndio mama yake wa kambo Nyanzala. Na hivyo akaanza kupanga mikakati ya kutoroka kwenda kijiji jirani..ili akwepe kesi ya mauaji. Ila wakati akijiandaa kutoroka,ghafla alisikia sauti ya Nyanzala akiwa amekoho "oooh mungu wangu " alisema mama yake wa kambo Nyanzala asiamini kama kweli Nyanzala kazinduka..hivyo aliamua kuzipiga hatua kurudi chumbani kwa Nyanzala ili ahakikishe kama kweli Nyanzala kazinduka. Kweli mama huyo alipo ingia chumbani alimkuta Nyanzala akiwa amekaa kitandani huku mkononi akiwa ameshika picha ya marehem mama yake. Nyanzala aliitazama ile picha huku machozi yakimtoka ,machozi ambayo yaliangukia kwenye picha ya marehem mama yake. "Nyanzala mwanangu samahani sana,nisamehe mwanangu " Mama yake wa kambo Nyanzala alisema huku akijifanya kuwa na huruma. Lakini Nyanzala aliyafuta machozi yake..akapandisha kamasi jepesi lililokuwa likikalibia kumtoka. Kisha akasema "usijali mama haya yote ya dunia tu" Alisema Nyanzala kwa sauti ya huzuni. Na kwisha kusema hivyo mama shani alimshika mkono Nyanzala na moja kwa moja wakaelekea sebleni lakini kabla hawajafika,Nyanzala alilalama kuhusu maumivu aliyokuwa akiyapata pindi apigapo hatua. Kitendo ambacho kilimfanya ashimdwe kufika sebleni na hivyo akawa amerudi kitandani kulala. Na mama Shani baada kuona hali ile ya Nyanzala...hakika siku hiyo alimfanyia Nyanzala kila kitu alichostahili kufanyiwa mtoto wa kike haswa yatima. Yote hayo aliyafanya ili kumsahaulisha Nyanzala juu ya kile alicho mfanyia.
******************
Naam! Siku zilisonga Nyanzala akiwa mtoto wa kukaa nyumbani..kwani kwa kipigo kile alichokipata. Alishindwa hata kutoka ndani,,hali ya kuwa watoto wa mama yake wa kambo wao walikuwa wakiendelea kuhudhulia masomo kama ada. Hakika jioni hiyo moja baba Nyanzala alirejea kutoka kazini kwake ambapo ikikumbukwe alimuaga mkewe kuwa anakwenda kwenye kazi za machimbo na huko atakaa taklibani siku tano. Na hatimae siku hiyo ya tano akawa amerejea saa za jioni. Hivyo baada baba Nyanzala kutulia ndani ya masaa kadhaa. Alishangaa kuwaona watoto wa mke wake Kagaruki na Shani bila kumwona Nyanzala. Baba Nyanzala akaamua kumuuliza mkewe "Mama Shani mbona hawa watoto nawaona hawajatimia na jioni imeingia.je, mwenzao yuko wapi?" Alihoji baba Nyanzala huku akipunguza sauti ya radio yake ambayo aliipenda kusikiliza radio Tanzania ambayo kwa sasa ni Tbc taifa. "Baba Nyanzala, mwanao kaumia mguu wakati alipo kuwa akitoka kisimani kuchota maji..kwahiyo mguu umevimba kweli! " Mama yake wa kambo Nyanzala alimjibu hivyo mume wake kwa sauti ya kujiamini kabisa. Na mala baada baba Nyanzala kusikia kuwa mwanae kaumia.haraka sana alinyanyuka kutoka kwenye kigoda alichokuwa amekalia. .kisha akazipiga hatua kuelekea ndani ili amjilie hali mwanae. Lakini kabla hajaelekea chumbani kwa Nyanzala, ghafla mama yake wakambo nyanzla akamshika bega na kusema. "Mume wangu kwa umri aliokuwa nao Nyanzala hustahili kuingia chumbani kwake je, ukimkuta uchi? " Alisema mama Shani ambae ndio mama yake wa kambo Nyanzala. Ila licha ya baba Nyanzala kuambiwa hivyo...hakutaka kukubaliana na hilo suala ambapo aliusogelea mlango wa chumba cha Nyanzala kisha akabisha hodi. Na wakati baba Nyanzala akifanya hayo..upande mwingine mama Shani aliipua sufuria lenye maji aliyokuwa ametenga jikoni. Maji ya kusongea ugali. Akayamwaga jikoni ambapo majivu ya uvuguvugu yalimrukia kwenye miguu yake.. mama Shani alipiga mayowe ambayo yalimfanya baba Nyanzala kuachana na Nyanzala, hima akaenda kuangalia mke wake kakutwa na nini. "Hivi mimi na mwanao nani bora? Eeh mimi naunguzwa na moto alafu wewe bado unaongea na huyo mpuuzi wako" Alisema mama Nyanzala kwa sauti Kali ila baba Nyanzala alijishusha kwa kumwomba radhi huku akimpaka asali mahali alipoongua. Lakini licha ya mama huyo kupewa huduma hiyo ya kwanza na mume wake. Hakulizika ambapo alimwambia mume wake kuwa akamletee maziwa, Na katika kijiji hicho maziwa yalipatikana katika Jamii ya kimasai. Hivyo bila kujali giza lililokuwa tayali limetanda. .baba Nyanzala alikwenda kumnunulia mke wake maziwa kwa wafugaji hao wa kimasai. Wakati huo huo mke wake nae aliingia chumbani kwa Nyanzala na kisha kumpa kwa kusema "we mwanaharam wewe,nakuambia hivi endapo kama utamwambia baba yako kama nimekupiga..heeeh nitakufanyia kitu kibaya hadi mama yako atoke kaburini aje akutetee" Alisema mama yake wakambo Nyanzala akimwambia Nyanzala.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Onyo ile aliyopewa Nyanzala na mama yake wa kambo. Ilimuogopesha sana hivyo akawa anajiuliza amwambia baba yake au asimwambie.. Kiukweli hata baba Nyanzala alipo rudi kutoka kununua maziwa kwa wamasai.. Alimkabidhi mkewe. Kisha moja kwa moja akaelekea kwenye malango wa chumba cha mwanae akamwita ili amwangalie ajue kaumiaje...Nyanzala akiwa kitandani alijikongoja polepole hatimae alitelemka kisha akafungua mlango.."shkimo
o baba"Nyanzala alimsalimia baba yake kwa sauti ya onyonge iliyo jaa upole..."malakh
abaa mwanangu,nasikia umeumia wakati unatoka kisimani kuchota maji ?"..Baba Nyanzala alimuuliza mwanae huku akimwangalia usoni,na ndipo Nyanzala alipo shusha pumzi kisha akamjibu"ndio baba lakini..naendelea vizuli"
"Aya mamaa ugua pole sawaee"
"sawa baba"
Baada baba Nyanzala kumjulia hali mwanae,aliondoka huku akimwacha Nyanzala akiwa akitokwa na machozi ya uchungu.. kwani alitamani kumwambia baba yake mateso yote anayo yapata kutoka kwa mama yake wa kambo lakini alishindwa kwa sababu alitishiwa kufanyiwa kitendo kibaya na mama yake wa kambo.
Naam! Hatimae muda wa chakula cha usiku uliwadia lakini Nyanzala hakupewa chakula .. baba yake alipo uliza kama mwanae kapewa chakula, alijibiwa.."tayali kapelekewa chumbani kwake"...Na baba Nyanzala akawa amelidhika na jibu alilopewa na mke wake hivyo akawa amemsifu na kumponda mke wake wa kwanza ambae ameshatangulia mbele ya haki,,mama mzazi wa Nyanzala.
Hakika ilipo fika mnamo saa sita usiku..njaa kali ililindima tumboni mwa Nyanzala ambapo alikosa usingizi na kitanda akakiona kichungu..kiukweli alitamani kumwomba chakula mama yake wa kambo usiku ule lakini aliogopa..na hakua na lakufanya zaidi kuishia kulia tu.
Lakini wakati akilia bila kunyamanza huku akimtaja marehem mama yake,ghafla akasikia sauti ya marehem mama yake ikimwita.."Nyanzala..Nyanzala..Nyanzala"
"..Nyanzala alitulia kwa umakini akisikilizia sauti ile iliko kuwa ikitokea mwishowe alisikia ikitokea nyuma ya nyumba yao ambapo ndipo lilipo kaburi la mama yake..hivyo baada kuisikia sauti ile ikitokea upande lilipo kaburi la mama yake ndipo alipo jisogeza hadi kwenye dirisha la chumba chake kisha akafunua pazia ya dirisha..akawa amechungulia kaburi la mama yake..Kiukweli Nyanzala alishtuka baada kuona mishumaa ikiwa juu ya kaburi la mama yake,na punde si punde ile mishumaa akapotea..muda huo huo akatokea nyoka mkubwa aina ya chatu..Hayo yote yalikua yakifanyika huku Nyanzala akishuhudia kwa macho yake akiwa haamini kama ni kweli anacho kiona kwenye kaburi la mama yake.
Basi yule nyoka alie kua juu ya kaburi la mama yake Nyanzala..alipanua mdomo wake kisha zikatokea sahani mbili za chakula ambapo baada Nyanzala kukiona kile chakula,hakuweza kuogopa hivyo alifungua mlango kisha akazunguka nyuma ya nyumba ilipo kaburi la mama yake..bila kujali alikaa juu ya kaburi na akakila kile chakula haraka haraka maana alikuwa na njaa kali mno. Na wakati huo yule nyoka alikuwa ameshatoweka pale kaburini .
Baada Nyanzala kumaliza kula chakula kilichokua juu ya kaburi la mama yake,aliangalia huku na kule kisha alizipiga hatua kurudi ndani..wakati huo njaa yote ikiwa imepotea tumboni..Sasa wakati Nyanzala anakalibia kuingia ndani,ghafla mama yake wa kambo nae alikua akitoka ndani akielekea chooni hivyo wakawa wamekutana mlangoni..
"Unatoka wapi usiku huu wote"..Nyanzala aliulizwa hivyo na mama yake wa kambo.."nimetoka kujisaidia mama"..Nyanzala alimjibu hivyo huku akiwa na wasiwasi..lakini licha ya yule mama kujibiwa hivyo ila hakulizika na jibu la nyanzala hivyo aliamua kumpiga kofi Nyanzala huku akimwambia"marufuku kutoka nje usiku pumbafu"
Basi Nyanzala aliingia ndani,na moja kwa moja akaelekea mahali palipokua mtungi ili anywe maji kwa sababu alikua ameshiba..Lakini baada mama yake wa kambo kutoka chooni kujisaidia..alimkataza Nyanzala asichote maji huku akimwambia.."maji ya mtungini huja yachota wewe,sawaee sasa ole wako nikuone unachota maji hum mtungini utanijua me nani.."Baada kumwambia hivyo alifyonya.. hakika Nyanzala aliumia saana. Nyanzala kwa unyonge akasema "Mama chakula umeninyima hata maji nayo pia uninyime kwelii?"Nyanzala aliongea hivyo..ila mama yake wa kambo hakujali.."nilisha kwambia ukitaka chakula nenda kwenye kaburi la mama yako hapo nyuma sasa ukiniomba mimi ni sawa na machozi ya samaki baharini..embu kalale mbwa wewe"..Daah inauma kiukweli. Na yote hayo yalikua yakifanyika huku baba Nyanzala akiwa amesinzia usingizi mzito yote ni kwasababu ya uchovu wa kazi alizokua akizifanya.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baaada Nyanzala kunyimwa maji ya kunywa na mama yake wa kambo..Hatimae Nyanzala alikwenda chumbani kwake huku akilia kilio cha chinichini kwani yale maneno yalimuumiza sana nafsi yake kwa sababu hakupenda mama yake atangulie mbele ya haki bali ni mipango ya mwenyezi mungu tu.
"hivi ni lini na mimi nitakua na furaha kama watoto wenzangu??
"je,mungu mpaka anamchukua mama yangu ameona nini hapo mbeleni??
"na kuhusu haya manyanyaso ambayo nayapata,baba anajua chochote??..na kama anajua mbona hanitetei?? Eee mungu wangu nitazame na mimi."..Yalikua ni mawazo ambayo Nyanzala alikua akiyafikilia kichwani mwake huku mkono wake wa kulia ukiwa umeshikila kibatari pia mkono wa kushoto ukiwa umeshikilia picha ambayo alipiga akiwa na marehem mama yake inzi ya uhai wake..Hakika Nyanzala alilia sana huku chozi likidondokea picha aliyokua kaishika.
Lakini baada kunyamanza alipanda kitandani kisha akalala ambapo alishindwa kupata usingizi kwa haraka kwani kila alipomkumbuka mama yake usingizi ulitoweka..yote ilitokana na maisha anayo ishi na mama yake wa kambo.
Lakini baadae usingizi ulimpitia..mpaka asubuhi ambapo aliamshwa na mama yake wa kambo ili afanye usafi wa mazingira ya nyumbani wakati huo watoto wa yule mama wakijiandaa kwenda shule.."mama leo ngoja niende shule siku ya nne sijafika shuleni,hivyo kwa kuwa nimepata ahueni naomba tu na mimi niende kujenga taifa"..Nyanzala alimwambia hivyo mama yake wa kambo kwa upole na wingi we wasiwasi "mama ngoja leo ni ng'ong'ong'o pumbafu nimesha kwambia fanya usafi mjinga wewe wangapi wamesoma wanaishia kua wauza nyanya barabarani" Hakika ilikua ni rugha ya kebehi kwa Nyanzala, na kilicho muumiza zaidi ni pale mama yake wa kambo alipo zarau suala la Elimu haliyakua wanae wanaenda shuleni kutafuta elimu.
Basi yote kwa yote Nyanzala alivaa nguo zake za shule kisha akaenda shuleni huku akimwacha mama yake wa kambo akilalama kwa kumwambia asirudi nyumbani kama kabisha alichokisema yeye. Lakini Nyanzala hakujali hilo japo alikua ni mtoto wa darasa la nne..na yote aliamua kukubali kipigo chochote atakacho kipata kutoka kwa mama yake wa kambo na ndio maana alikataa kubaki nyumbani wakati watoto wa yule mama wameenda shule.
Kiukweli Nyanzala alipofika shuleni alionekana kua tofauti sana na Wanafunzi wenzake..kwa maana alikua kitazama kitu,basi hapepesi macho. Yote ni kwa sababu ya kuwa na nawazo mengi sana kichwani mwake. Na hivyo hata muda wa wanafunzi kurudi nyumbani ulipo wadia..Nyanzala hakuwa na furaha hata kidogo moyoni mwake kwani alijua ni kitu gani kitakacho mkuta endapo kama atafika nyumbani .
Nyanzala alitembea polepole huku akitamani asifike nyumbani haraka vilevile akiomba mungu kwamba endapo kama atafika basi amkute baba yake nyumbani..maana endapo kama atamkuta baba yake nyumbani,basi mama yake wa kambo atakosa njia rahisi ya kumuadhibu.
Kweli hatimae dua ya Nyanzala ilisikika ambapo alipofika nyumbani alimkuta baba yake tayali kafika kutoka kazini..hivyo Nyanzala alitabasam huku akizipiga hatua kuelekea kwa baba yake ambae alikua amekaa chini ya mwembe akisikiliza radio..."baba shkamooo"..Nyanzala alimwamkia baba yake,lakini kilicho mshangaza Nyanzala ni pale baba yake alipoitikia salam kama kalazimishwa..."mmh kuna kitu hapa sio bure"..Nyanzala aliguna kisha akajisemea hivyo kwenye nafsi yake huku akiinuka na kuelekea moja kwa moja chumbani kwake kubadilisha nguo za shule..
Na mala baada kumaliza kubadilisha sare za shule,ndipo alichukua vyombo vilivyotumika kulia chakula kisha akaviosha.Baada kumaliza,baba yake Nyanzala alimwita mwanae kwa sauti iliyokua kali ambayo ilimfanya Nyanzala kuhofia wito..."Abee baba"Nyanzala akaitika haraka sana akamkalibia baba yake "hivi mimi ni nani kwako"..Nyanzala aliulizwa hivyo na baba yake.."we ni baba yangu"..Nae alimjibu baba yake kwa kuogopa.."na huyu mwanamke ninae ishi nae hum ndani unamwitaje..?".. Kiukweli lilikua ni swali ambalo lilimpa hofu Nyanzala hadi kujishtukia na kujiuliza kwa nini baba yake kamuuliza vile..."huyo ni mama"..Nyanzala alijibu.."sasa kama ni mama yako mbona unamzarau au kwa kua hajakuzaa yeye?"...Maswali hayo yote baba Nyanzala alikua akimuuliza mwanae huku akionekana kakasilika..."hapana baba me simdharau kabisa ila..." ghafla Nyanzala alipigwa kofi ambalo lilikatisha sentesi aliyokua akitaka kuongea,na hata huvyo hakulizika ndipo alipo chukua bakora na kisha kumchapa mwanae haraka haraka kama vile anapiga gunia la mpunga..Hakika Nyanzala alilia sana huku akimwomba msamaha baba yake..."baba nisameheee..baba nisamehee sitorudiaaaa..."..Na wakati Nyanzala alipokuwa akila kipigo kutoka kwa baba yake,upande wa pili nako yule mama yake wa kambo na watoto wake walikua wakifrahia kipigo alichokua akikipata Nyanzala. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kiukweli Nyanzala aliangua kilio kwa sauti,ambayo iliweza kukusanya baadhi ya majirani ambao waliingilia kati na komwomba baba mtu amsamehe mwanae...na hiyo ndio ikawa bahati ya Nyanzala ...Lakini licha ya hayo baba Nyanzala alizidi kumtukana mwanae matusi ambayo yaliweza kumjengea fikla Nyanzala na kuhisi kua huwenda mama yake wa kambo kamchongea kwa baba yake kuwa anamdharau..ambapo sivyo ilivyo.. "ukowapi mama? " Nyanzala alihoji huku machozi yakimtoka.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment