Search This Blog

TAMBIKO - 5

 







    Simulizi : Tambiko

    Sehemu Ya Tano (5)





    upande mwingine walionekana wachawi wakijitokeza kwenye njia panda,, kando kando palikuwa na mti mkubwa wa mzambarau!  wakamkuta mkuu wao ameshafika sekunde chache zilizopita,,, wakiwa uchi wa mnyama! 

    mkuu wa wachawi akasema,, mwanamke yule tayari yupo kule kuzimu,,, atafungiwa huko maisha yake yote. kisha akaongea maneno ya lugha ya kichawi! 

    akimaanisha kuwa yule aliyekabidhiwa kibuyu akilete kwake! yule mchawi aliyekabidhiwa kibuyu hicho akashtuka! akatazama mikono yake,, ilikuwa tupu.... akakumbuka kuwa kile kibuyu kakisahau kule kwenye ile nyumba!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akaongea kwa lugha ya kichawi,,,akimaanisha,, samahani mkuu nimesahau kibuyu kule kwenye ile nyumba.

    mkuu wa wachawi akakasirika akaamua kumuangamiza mtu huyo!  kiwha akatoa tamko kwa kusema;  huyu ni mjinga kupita kiasi! kazi tuliyoifanya imeshaingia dosari,,, kaharibu kila kitu!  kama kibuyu hicho kitaguswa na mtu ambaye si mshirika,, basi tutqkuwa tumefanya kazi bure



    wakati huo huo kule nyumbani kwao Maliwa,,,alionekana Maliwa akizipiga hatua kukifuata kile kibuyu akakitazama kwa makini huku akistahajabu!  akakichukua na kufungua ufuniko uliofungwa kwa ngozi ya mbwa mwitu(wolf)! punde si punde kibuyu hicho kikapasuka,,,,



    wakati kibuyu hicho kinapasuka!  ilionekana minyororo ikifunguka mikononi mwa Conso,, kisha akatoweka kimiujiza,,akajitokeza chumbqni kwake!

    akaonekana akijishangaa! 



    Wakati huo huo alionekana Maliwa,akiwa bado yupo kule sebuleni.... Conso akafungua ,,mlango wa chumbani akazipiga hatua kukifuata chumba cha Maliwa,,akastaajabu kuona taa ya sebuleni ikiwa inawaka!  akaita kwa sauti ya chini chini,, "Maliwa,,,, Maliwa,,, Maliwa,,

    Conso hakujibiwa!  akazipiga hatua za kunyatia kuelekea sebuleni,, akamuona maliwa akiwa amesimama,,alafu kwenye sakafu palikuwa na vioande vya kibuyu kicho pasuka!

    Conso akauliza kwa mshamgao!  nini hicho kimepasuka?  Maliwa akashtuka kuisikia sauti ya amma yake!  akageuza shingo yake haraka kumtazama mama yake,, akasema,, "ni kibuyu,,nimekikuta hapo juu ya sofa!

    Conso akauliza mbona kimepasuka?

    Maliwa akajibu,, nilipokigusa kilipasuka! Conso akaendelea kumtazama mwanae kwa macho ya mshangao huku uwoga umetanda juu yake! 

    Maliwa akasema!  ,,"mama ulitoweka kimiujiza!  ulipelekwa wapi?

    Conso akakumbuka kuwa dakiak chache zilizopita aliona yupo sehemu ya kutisha!  akaamua kumsimulia maliwa kile alichokiona!

    Maliwa akamtazama mama yake kisha akauliza,, "kwa nini mambo haya yanatokea?

    Conso akainamisha uso wake kwa sekunde kadhaa kisha akasema,, mwanangu,, kama nilivyokwambia siku ile kuwa tangu utoto wako,, ulikuwa ukiandamwa na wachawi,, na sijui chanzo ni nini! lakini kunasauti tuliisikia mimi na baba yako kuwa mizimu ya mila yenu imekuteuwa uwe mganga wa kienyeji,,, lakini sauti hiyonpia ikasemq kuwa inahitajika kafara la damu ya uzawa wako,,, kabla Conso hajamaliza kuongea, ikasikika sauti ikisema!!!  La!  hasha sio kweli!  ni mbinu za wachawi tu hizo... hakuna kafara wala sadaka ya damu ya uzawa wa kijana wako!!!!  hiyonilikuwa janja ya wachawi na mapepo wabaya.  lakini bado Maliwa anayo nafasi...yeye ni mteule wa mizimu ya kimila,, hivyo anazo nguvu za ziada kwa ajili ya kupambana na mapepo wabaya pamoja na wachawi! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Conso na Maliwa wkastaajabu sana kusikia maneno hayo! wakqti wanatafakari maneno hayo,,, ikasikika sauti ya mtu akikohoa mfululizo!

    sauti hiyo ilitokea kwenye chumba cha wageni!! Maliwa akasema,, "wacha nikaangalie ni nani huyo,, kisha akazipiga hatua kukifuata chumba cha wageni!

    wakati huo Conso alikuwa amebaki kule sebuleni akimtazama Maliwa akiifuata korido inayoelekea kwenye vyumba! 

    Maliwa alipoukaribia mlango huo ikasikika sauti ikimwambia hakikisha unaishikilia simbi yako kwanguvu! Maliwa akasita kwa sekunde kadhaa,,akainamisha uso wake kutazama mkono wake aliokuwa ameishikilia ile simbi!  alipofunua vidole vyake kuitazama simbi hiyo iliyokuwa kwenye kiganja chake,,ikasikika sauti kali ya mtu akilia kwa maumivu makali!  sauti hiyo ilitoke kwenye hicho chumba cha wageni.....

    Maliwa aliitambua sauti hiyo akafungua mlqngo haraka,,akaingia ndani ya chumba hicho! alipoangaza macho yake akamuina baba yake(Shinje) akiwa amesimama kwe kona ya chumba hicho huku kazungukwa na wafu wawili walio hai,,

    watu hao wasio kuwa na hata chembe ya nyama/mwili,

    walilionekana ni mifupa tu! wakiwa wanamkaba Shinje kwenye shingo!

    maliwa akapaza sauti; MUACHENI BABA YANGU.:

    wakamuachilia na kuzipiga hatua kumfuata maliwa..







    Maliwa akaingiwa na hofu,, macho yakamtoka akataka kutimua mbio lakini,,akakumbuka ile sauti ilimwambia kuwa simbi aliyoishikilia mkononi ndio kinga yake,, hivyo hakuna kiumbe yeyote ambaye angeweza kumdhuru!

    Maliwa akaingiwa na ujasili,,,,akawafuata hao wafu waliohai.. alipowagusa wakayayuka na kuwa moshi,,,mwingi,ukatanda chumba kizima,kisha moshi huo ukatoweka kimiujiza.! Maliwa akamfuata baab yake akamnyanyua pale chini alipokuwa kadondoka. akamtoa kwenye chumba hicho!! akaongozana nae mpaka sebuleni!  Shinje na Maliwa wakashtuka kuona,,kiumbe wa kutisha akiwa amemkamata Conso,, huku qmeshikilia upanga mrefu kauweka shingoni mwa Conso...

    kiumbe huyo akasema,, mimi natokea kuzimu,, nimeamua kuja mwenyewe,,,nitamuacha mama yako akiwa hai endapo utafuata masharti nitakayokwambia!!!

    kwanza kabisa nakuonya achana na mambo ya uganga,, sharti la pili tupa hiyo simbi nje ya nyumba,,, kisha nitaondoka zangu,,na kumuacha mama yako!

    Maliwa akastaajabu sana! akajisemea moyoni,, "mbona ile sauti iliniambia kuwa simbia moja,,,kati ya zile mbili,,  nimkabidhi mama yangu,, imlinde,, sasa mbona kanaswa na kiumbe wa ajabu, ghafla ile sauti ikasikika ikimwambia,, "simbi hiyo haipo mikononi mwa mama yako!  ilidondoka chini,, hii ni sababu ya yeye kunaswa na kiumbe huyu!

    Maliwa akatazama chini pale alipokuwa amesimama mamaal yake pamoja na yule kiumbe wa kutisha aliyemnasa. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maliwa akaiona Simbi hiyo ipo chini kando ya mguu wa mama yake!

    akamtazama mama yake machoni,, damu nzito kuliko maji,, Maliwa akafanya ishara kwa kutumia macho yake,, akimaanisha kuwa Conso aikanyage simbi hiyo,,,

    Conso akaelewa Maliwa anachomaanisha.. akasogeza mguu wake taratibu akaikanyaga Simbi hiyo,,,

    kitendo cha kuikanyaga simbi Conso akapata ulinzi,, mwili wake ukawa kama shogi ya umeme,,, ye kiumbe wa kutisha akaanza kutetemeka,, akamuachia Conso...

    kiumbe huyo aliendelea kutetemeka mpaka akapasuka vipande vipande,,ukawa ndio mwisho wake..

    Maliwa akamkimbilia maam yake na kumkumbatia,,,

    kikqonekana kiganja cha mkono,, kati ya vipande vya mwili wa kiumbe huyo aliyepasuka,, kiganja hicho kilikuwa chini kwenye sakafu,, karibu na mguu wa Conso,, aliposogeza mguu wake akakikanyaga kiganja hicho,,pasipokukiona,, vidole vilivyokuwa vimetapakaa damu ya kijani,,  vikajikunja,, kucha iliyokuwa imechongoka kwenye kidole hicho... ikamkwaruza Conso,,akapata mchubuko kiasi,,akashtuka ni baada ya kuhisi maumivu,, akainamisha uso wake kutazama chini!  akaona kakanyaga kiganja akaruka kando!!!

    punde si punde vipande hivyo vikatoweka kimiujiza,,

    Shinje akasema,, "nashindwa kuelewa nini kilinitokea nimejikuta nipo sehemu ya kutisha!

    Maliwa akaanza kusimulia alichokiona akasema wewe na mama mlichukuliwa na kupelekwa kuzimu,, alafu kunasauti naisikia mara kwa mara ndanibya masikio yangu!

    ikiniambia kuwa mizimu ya mila zetu imeniteuwa niwe mganga wa kusaidia binadamu wenzangu,,

    wakati Maliwa anaongea,,. Conso akaanza kuhisi mwilinwake kuwa tofauti!!  akahisi kama kunakitu kinatanuka ndani ya mwili wake,,,

    kumbe lile kucha la yule kiumbe lililomkwaruza,, damu ya kiumbe huyo ilichanganyikana na damu ya Conso,, kupitia ule mchubuko!

    Conso akaanza kuhisi maumivu makali kupita kiasi,, punde si punde akaanza upiga kelele,, kadri alivyokuwa akipiga kelele,,sauti yake ilikuwa ikibadilika na hatimae akaanza kunguruma kama mnyama! mngurumo huo uliendelea kubadilika na kuwa wa kutisha zaidi,, Shinje akaogopa akataka kutimua mbio,, Maliwa akasema,, "usikimbie... hapa kunatatizo lakini nitakabiliana nalo,, nitahakikisha mama anakuwa salama.. Shinje akaanza kupata faraja kiasi,, ni baada ya kusikia maneno hayo ya Maliwa.

    Conso akaanza kubadilika na kuanza kufanana na yule kiumbe aliyepasuka vipande vipande!



    Maliwa akaingiwa na wasiwasi,, akajisemea moyoni,, "mama yangu kapatwa na nini?

    sijui nitamsaidije? ikasikika sauti ikimwambia,, usiogope,, weka simbi hiyo kinywani mwako, kisha imeze,, alafu mguse maam yako!

    bila kuchelewa Maliwa akafanya kama alivyoambiwa! na sauti ya mtu asiyeonekana.

    kisha akamgusa mama yaeke..

    Conso akadondoka chini na kuwa katika hali yake ya kawaida...

    ikasikika sauti ikisema,, wewe ni shujaa hongera kwa kuifanya kazi yetu kwa usahihi na kuangamiza mapepo wote wabaya! sauti hiyo haikusikika tena! punde si punde Maliwa akahisi kutapika,, akaitapika ile simbi ikadondoka chini.. ikatoweka kimiujiza.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikuku zilizidi kusonga, mambo hayo ya kutisha hayakujitokeza tena,, Maliwa akapanga safari ya kwenda kumtembelea bibi yake,, Shinje na Conso wakaamua kuongozana na kijana wao. wakaelekea kule kijijini! 

    walipofika wakapokelewa kwa furaha na Mama shinje...

    Mama shinje akafurahi sana kumuona mjukuu wake,,, akaamua kummilikisha mashamba pamoja na mifugo,, ng'ombe na mbuzi.. Maliwa akafurahi sana..

    Baada ya wiki moja kupita,, wakarudi Dar es salaam,, tangu siku hiyo wakaishi maisha ya amani na furaha mpaka leo,



            *************************MWISHO****************************





0 comments:

Post a Comment

Blog