Search This Blog

NZITA - 4

 







    Simulizi : Nzita

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ********BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA******



    shele zilifunguliwa zanida alimfanyia mwanae manunuzi(shopping) ya mahitaji ya shule... kisha nzita akarudi shule kuendelea na masomo..... siku moja wakiwa bwenini mwanafunzi mmoja aliamka ili aende kujisaidia.. aliogopa sana aliona vitu vyote vilivyokuwa ndani ya bweni hilo... vikielea hewani mpaka vitanda. mtoto yule aliogopa akakambia kuelekea upande wa nje alipofika nje. alistahajabu kumkuta nzita kasimama peke yake huku akitazama juu mawinguni... mtoto yule alimuita nzita aje aone vitu vikielea bwenini... nzita aligeuza shingo yake ghafla.. kisha akaanza kuzipiga hatua kuelekea kule alipokuwa amesimama yule mwanafunzi mwenzake..

    nzita alipomkaribia mtoto yule alistahajabu kJona macho ua nzita yamekuwa mekundu huku yakiwaka kama kuna taa ndani ya macho... mtoto yule aliogopa sana... akaanza kupiga hatua kurudi nyuma huku akilia.....wakati huohuo mlinzi wa shule alikuwa akizungukia eneo moja baada ya lingine kuangalia usalama... nzita alipohisi kuna mtu anakuja upande wao..... aliyayuka na kutoweka na mtoto yule wakatokezea ndani ya bweni huku mtoto yule akiwa kitandani kwake kalala.....



    ************



    palipokucha mtoto yule alimfuata nzita na kumwambia jana nimekuota nikaona unamacho mekundu.. nzita hakuonge kitu alibaki kimya...siku hiyo ilikuwa ni umamosi hivyo wanafunzi hawakwenda madarasani... mlezi wa wanafunzi silent hapo aligawa maeneo"" kila mmoja eneo lake la usafi...aliwagawia wanafunzi wote maeneo kisha wakaanza kufanya usafi... nzita alikuwa mtu wa mwisho kabisa kugawiwa eneo afanye usafi""" mlezi huyo alimwambia nzita aokote takataka zote zilizokuwa zikizagaa mbele ya bweni kisha mlezi huyo akaanza kuzipiga hatua na kuondoka zake... ghafla alisikia vishindo vikubwa vya mtu akikimbia... aligeuza shingo yake afizame ni nani!!!!

    alistahajabu sana alimuona nzita kaketi kwenye kibaraza.. huku eneo la mbele ya bweni likiwa safi kabisa.. kama kumefagiliwa kwa ufagio..... mlezi yule alimuangalia nzita kwa macho ya mshangao!!! hakusema kitu aliamua kuondoka zake.... nzita alishika nafasi ya kwanza mpaka darasa la nne(4) mwalimu mkuu aliamua kumvusha darasa kwa sababu alionekana alikuwa na uwelewa wa kimasomo wa hali ya juu..nzita alivushwa mpaka darasa la sita...wakati darasa la saba wanakaribia kufanya mtihani wa taifa nzita aliomba na yeye afanye mtihani huo.. mwalimu mkuu alikubali ombi la nzita.... huwezi amini matokeo yalipotoka nzita aliongoza kitaifa.. alipata alama zote bila kupoteza hata moja...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***BAABA YA MIAKA KUMI NA MOJA KUPITA***



    nzita alihitimu kidato cha sita.... alikuwa katimiza umri wa miaka kumi na nane(18)nzita alikuwa ni mrembo sana.....sikumoja yule mtu wa ajabu ambaye ni baba yake nzita alimtikea nzita na kumwambia.. umekuwa binti yangu... sasa umetimiza umri wa kuianza kazi ya WAKALA WA KUZIMU... na kazi hiyo utaianza rasmi kuanzia leo hii.. kisha mtu yule wa ajabu na kutisha alipandikiza roho ya ukatili katika akili ya nzita... kisha mtu yule wa kutisha alitoweka....



    Nzita alinyanyuka kitandani kwake... na kutoka nje ya chumba alichokuwa analala....nzita alistahajabu sana alihisi kuna kitu kinachomoza kutoka ndani ya mwili wake sehemu ya mgongoni.... punde yalianza kuchomoza mabawa nzita alizidi kistahajabu.. hatimae mabawa yakawa marefu kabisa.... nzita alijaribu kupaa,,, aliona anaweza kupaa angani kama ndege... jambo lile nzita alilifurahia sana.... usiku huo alipaa na kuzunguka zunguka angani...kisha alipo ona roho karidhika aliamua kurudi nyumbani,,, aliingia chumbani kwake bila kupitia mlangoni wala dirishani alipoingia chumbani yale mabawa yalirudi upande wa ndani ya mwili wake. kisha akapanda kitandani na kuutafuta usingizi....



    ************



    Asubuhi palipokucha nzita alidamka mapema kabla ya mama yake...nzita aliingia bafuni kuoga... wakati nzita yumo bafuni,, zanida alikuwa kadamka muda si mrefu alitoka chumbani na kuelekea sebuleni... akiwa koridoni anazipiga hatua alisikia sauti ya watu wakiongea ndani ya bafu...zanida alistuka... mmmh!! nzita anaongea na nani? aliamua kuchungulia kupitia tundu la ufunguo kwenye kitasa.. alistahajabu sana aliogopa baada ya kumuona nzita akiwa amesimama huku yule mtu wa kutisha akimuogesha nzita kwa kum-mwagida damu mwili mzima.... zanida alishindwa kuvumilia aliamua kutimua mbio kuelekea sebuleni ili atoke nje.. alipofika sebuleni aliogopa kukuta watu wawili wamevalia mavazi meusi huku wamefunika nyuso zao... zanida alizidi kuchanganyikiwa... kisha watu wale walianza kuzipiga hatua kumfuata zanida...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    zanida alitimua mbio kurudi chumba ajifungie.. ile anageuka alijigonga kwenye mwili wa yule mtu wa kutisha aliyemuingilia kimwili kule kwaganga sumbi....ghafla alitokea nzita huku akiwa na mabawa na mwili wake umekuwa mweusi kama kapakwa mkaa huku macho yake yakiwa mekundu zaidi... nzita alimshika mama yake na kumng'ata upande wa pembeni ya shingo na kufyonza damu ya mama yake.... ghafla zanida alistuka kutoka usingizini... kumbe zanida alikiwa anaota.... alipotazama kushoto kwake alimuona nzita anaingia chumbani... shikamoo mama nzita alimsalimia mama yake"" zanida hakujibu kitu alikuwa akipumua kwa pumzi za kutweta huku macho yamemtoka.... alimtazama nzita kwa macho ua mshangao... nzita aliuliza mama umepatwa na nini!!! mbona nakusalimia hauitikii salamu yangu???zanida alishindwa aongee nini alikuwa kama kapigwa na shoti ya umeme... nzita alimtizama machoni mama yake... walipokutanisha macho nzita aliona ndoto yote aliyokuwa akiota mama yake... kitendo kile cha mama yake kuota hivyo nzita hakukipenda.... ghafla nzita alianza kubadilika... kisha akasimama alimuangalia mama yake huku uso wake ukionekana kujaa hasira... ghafla macho ya nzita yalianza kubadili na kuwa mekundu kabisa.... zanida aliogopa sana mapigo yake ya moyo yalizidi kwenda mbio... nzita alizipiga hatua mbili na kumkaribia mama yake.... zanida alitamani kukimbia lakini alishindwa kulikuwa hakuna upenyo na chumba kilikuwa kidogo... zanida alianza kulia huku akimsihi mwanae asimdhuru... wakati huo nzita hakuwa na huruma kabisa... alimshika mama yake na kumtoboa tumbo kwa kutumia kucha mdefu za vodole vidole vyake kisha akaingiza mkono na kunyofoa moyo wa mama yake na kuanza kuutafuna mbichi..zanida alidondoka chini na kupoteza maisha.... wakati huo mama zanida ambae ni bibi yake nzita alikuwa amekuja kuwajulia hali... alikuwa anagonga mlango wa sebuleni.... alipo ona hakuna anaekuja kufunfua mlango aliamua kuzungusha kitasa... kumbe mlango ulikuwa haujafungwa na ufunguo... akaingia ndani.... alipitiliza moja kwa moja kuelekea chumbani kwa zanida wakati anatembea koridoni.... alihisi kakanyaga maji alipotazama chini... alistuka kuona nyao za miguu iliyokanyaga damu alipotazama kwa makini aliona nyayo hizo zilitokea chumbani kwa zanida.... alianza kuingiwa na wasiwasi.... ile anageuka mara ghafla...



    ile anageuka mara ghafla alikutana uso kwa uso na nzita... mama zanida aliogopa sana alihisi kuishiwa nguvu... alitetemeka kwa uwoga baada ya kumuona nzita kabadilika na kuwa na mwili mweusi na macho mekundu zaidi... huku mdomo wake umezungukwa na damu.. alafu kashikilia moyo wa mama yake ukiwa kipande.... nzita alimtazama bibi yake.. kisha akaanza kuzipiga hatua kumfuata.. mamazanida alihisi kuchanganyikia alitimua mbio lakini hakuona mahala pa kutokea.....aliegemea ukuta huku akimtazama nzita kwa macho ya uwoga wa hali ya juu.. aliamua kusali... na kwa sababu imani yake ilikuwa kubwa.....kipindi anasali aliona nzita anajipinda pinda mwili wake... mama zanida aliendelea kupiga maombi... mara ghafla nzita alitoweka kimiujiza na kutokomea kusikojulikana.... mama zanida alipofumbua macho hakumuona nzita... aliangaza anangaza pande zote pia hakumuona nzita... mama zanida aliamua kuufungua mlango wa chumbani alipokuwa analala zanida... alipoingia ndani hakumkuta zanida alistahajabu kukuta damu zimetapakaa kwenye marumaru... aliogopa zaidi.. akaamua kutimua mbio na kurudi nyumbani kwake....



    ***********CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    upande mwingine alionekana nzita katokezea kando kando ya bahari huku akiwa katika umbile lake la kawaida.... alizipiga hatua kutoka ufukweni na kuelekea kunako barabara... nzita akiwa anatembea....alisikia honi ya gari ikipigwa alipogeuka aliona dereva aliekuwa akiendesha gari hilo ana mnyooshea mkono ishara ua kumuita...nzita alikwenda mpaka pale lilipokuwepo gari hilo... dereva yule alionesha kumtamani nzita kimapenzi... alianza kumtongoza... nzita aliamua kuondokazake.... wakati nzita anazipiga hatua dereva yule alianza kutoa maneno ya kumkashifu nzita.... nzita alichukia aligeuza shingo yake utadhani haina mfupa. huwezi amini shingo ya nzita iligeuka na kutazama upande wa mgongo huku kisogo kikiwa upande wa mbele.... dereva yule alistahajabu aliogopa akaliwasha gari lake kabla hajaondoka... alihisi kunakitu kinavutwa kwenye maumbile yake...alipofungua mkanda na kushusha suruali alianza kupiga mayowe baada ya kuona nyeti zake hazipo.. alipotazama ule upande aliokuwa kasima nzita hakumuona tena...yule dereva alitoka ndani ya gari na kukimbia huku akisema Jamani eee marighafi yangu uuuwiiii...alikimbia na kutokomea kusikojulikana..



    ***********



    kule nyumbani kwa bibi yake nzita... alionekana akiingia nyumbani kwake... alimkuta mumewe alianza kumsimulia kilichotokea... unaona sasa!!! mimi nilisema sikuile huyu mtoto ni jini mkaniona mimi hayawani""" mimi simo wala msinishirikishe kabisa""" alisema hivyo babu yake nzita.. wakati anaongea hivyo ghafla lilitokea tetemeko nyumba ilitikisika huku vitu vikidondoka kutoka mahalapake.... mama zanida na mumewe waliogopa sana.... macho yaliwatoka..... wakati wanashangaa ilisikika sauti ya ajabu kama mtu anakoroma.... kisha tetemeko lile lilitulia na ukimya ukatawala.... babu yake nzita alitimua mbio kuufuata mlango atoke nje..kabla hajapiga hatua nyingi mara ghafla alihisi miguu yake haikanyagi chini alihisi anaelea... aliingiwa na uwoga wa hali ya juu huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio... mama zanida alipo ona hivyo aliamua kutoka nje kwa kupitia mlango wa nyuma... akamuacha baba zanida ndani.... baba zanida alijaribu kuzipiga hatua akimbie lakini alishindwa kwa sababu alikuwa akielea hewani

    mara ghafla alihisi anakabwa shingoni alijaribu kutetea pumzi yake lakini alishindwa na baada ya dakika moja kupita baba zanida alikata roho.... kisha akadondoka chini sakafuni...mara ghafla nzita alijitokeza na kuoneka katika umbile la ajabu.. kisha akazipiga hatua kuelekea upande wa nje...nzita hakupitia mlangoni wala dirishani.... alipenya katikati ya ukuta na kutokea upande wa nje.. mara ghafla...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mara ghafla... akarudi katika umbo lake la kawaida...... wakati huo mama zanida alikuwa.... akichungulia dirishani alishuhudia mumewe akiuwawa...... mama zanida alistuka kumuona nzita upande wa nje... aliamua kutimua mbio huku kanga zikimdondoka.... alikimbia na kutoka nje ya geti..akatimua mbio bila kugeuka nyuma ...alikwenda moja kwa moja mpaka kwa mchungaji wa kanisa alilokuwa akienda kumuabudu Mungu... alipofika alimuelezea mchungaji yale yote yaliyotokea.... mchungaji na mama zanida walianza kufanya maombi muda huohuo.....



    **********



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog