Simulizi : Uko Wapi Mama?
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi majirani waliokuwa wamekusanyika kumtetea Nyanzala aliekuwa akipigwa na baba yake,hatimae walisambalatika majumbani mwao..Ambapo Nyanzala aliogopa kusogea eneo la nyumbani.Kwani alihofia kua huwenda baba yake akarudia tena kumpiga kipigo cha mbwa mwizi...hivyo Nyanzala akaamua kojisogeza hadi mahali lilipo kaburi la marehem mama yake..
"mama kwa nini umeniacha peke yangu?..au ulitaka mwenyewe niteseke peke yang?? mama mama amka njoo unikomboe mwanao nanyanyasika mimi"..Maskini ya mungu machozi yalimtoka Nyanzala kwenye macho yake huku akionge hivyo na mkono wake wa kulia ukichezea udongo ulioko kwenye kaburi la mama yake..Na pia akaona haitoshi alijilza palepale juu ya kaburi hadi usingizi ukampitia.
Nyanzala alilala pale kwenye kaburi la mama yake mpaka saa moja jioni na hata hivyo aliamshwa na jirani yao ambae alikuwa akitokea shamba saa za jioni.."Nyanzala ..wewe Nyanzala "Yule jirani yao ambae alifahamika kwa jina Baba maria. Alimwamsha Nyanzala ..Nyanzala alishtuka kutoka usingizini"Samahi babaaa"..Aliongea kwa kuogopa akidhania kua baba yake amemfuata ili ampige tena..."nini tena mtoto mzuri Nyanzala usiogope ni mimi Baba Maria"..Yule jirani yao Nyanzala ,alijitambulisha hivyo ili kumwondoa hofu Nyanzala.
"vp mbona umelala hapa??eeh sio vizuri bwanaa embu twende ukalale ndani utalalaje kwenye kaburi??"..Baba Maria ambae ndio jirani yao Nyanzala alimbembeleza namna hiyo Nyanzala .Lakini Nyanzala alikataa na kudai kwamba analala na mama yake palepale kaburini.Hivyo Baba Maria akawa ameachana nae ila akaenda kumueleza Baba Nyanzala hali harisi.
Nyanzala alizidi kulalala pale kaburini,lakini ilipofika saa nne usiku baba yake alienda kumwamsha baada jirani yake baba Maria kumwambia kwamba mwanae kalala kwenye kaburi la mama yake...Hivyo baba Nyanzala alizunguka nyuma ya nyumba lilipokua kaburi,kisha akamwamsha..."Nyanzala nyanzala amka ukulale ndani ....amka basi"..Ilikua sauti ya upole ambayo baba Nyanzala aliongea bila. . shaka alijutia kile kitendo cha kumwadhibu mwanae pasipo kuchunguza kosa.."baba me sina thamani tena kwako hivyo niache nilale hapa hapa kwenye nyumba ya mama yangu." Nyanzala alimjibu hivyo baba yake,huku akipandisha kwikwi baaada kulia kwa mda mrefu.
Licha ya Nyanzala kukataa kwenda kulala ndani,ila baba yake hakulizika na lile suala la Nyanzaa kulala kwenye kaburi la marehem mke wake ambae ndio mama Nyanzala.. ndipo alipo zidi kumbembeleza mwishowe Nyanzala alikubali akawa ameingia ndani.."vipi mama Shani kuna chakula kilichobaki?...Baba Nyanzala alimuuliza hivyo mke wake ...." chakula gani??..Embu akalale atakula kesho" Alijibu hivyo mama yake wa kambo Nyanzala. .akimjibu mume wake ambae nae hakuweza kurudisha neno lolote baada kuambiwa hivyo.
"Nyanzala lala mwanangu chakula kimeisha ila kesho mapema kabla hujaenda shule nitakupa hela ya kutumia shuleni sawaee" Nyanaa aliitikia sawa baba..Ingawa alikua na njaa kali lakini ilibidi akubali tu.
Baada kuonekana kuwa chakula hakuna..Nyanza aliingia chumbani kwake kisha akapanda kwenye kitanda chake, akaanza upya kuutafuta usingizi maana mwanzo alikua amesha sinzia kunako kaburi la mama yake ...lakini Nyanzala aliukosa usingizi kwa sababu ya njaa aliyokua nayo tumboni mwake na pia mawazo juu ya maisha yake kuwa ya mateso kila kukicha..na hivyo ndivyo vilivyo mfanya Nyanzala akose usingizi usiku huo..wakati upande wa pili watoto wa yule mama walikua wakikoroma kwa kunogewa na usingizi mzuli.
Basi wakati Nyanzala akiwaza na kuwazua,ghafra alisikia sauti ikitokea nyuma ya nyumba yao ambapo ndipo lilipokua kaburi la mama yake.."Nyanzala...Nyanzala "..Nyanzala aliisikiliza ile sauti kwa umakini na akajua ile ile sauti ya marehem mama yake,lakini licha ya kufaham hivyo,Nyanzala aliogopa kuitika ila alisogea kwenye dirisha ya chumba chake kisha akafunua panzia iliyokua kwenye dirisha.. akaangalia mahali lilipo kaburi la mama yake..."jamani mamaaaa"Nyanzala aliongea hivyo baada kumwona marehem mama yake akiwa kasimama kwenye kona ya kaburi huku akiwa ameachia tabasam..Hakika Nyanzala alitoka pale dirishani,haraka sana akafungua mlango wa kutokea ndani na akawa amezunguka nyuma ya nyumba ambapo ndiko alipo mwona mama yake juu ya kaburi lake.."mamaaaaa"Nyanzala alirudia kuongea hivyo huku akienda kumkumbatia mama yake,lakini ghafra mama yake akawa amepotea pale juu ya kaburi.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nyanzala alishtuka akataka kurudi ndani,lakini kabla hajachukua uamuzi huo ndipo pembezoni mwa kaburi lilitokea joka kubwa ambalo lilimzunguka Nyanzala akashindwa kukimbia..Mapigo ya moyo kwa Nyanzala yalienda mbio huku jasho jembamba likimtililika mwili mzima..Lakini hatimae punde si punde baada yule nyoka kumzunguka Nyanzala,liliasama mdomo wake kisha ikatokea sahani moja ya chakula ambacho kilikua kizuli kuliko kile alichokua akikipika mama yake wa kambo..."najua ni jinsi gani mwanangu unavyoteseka,ila ipo siku yule anae kunyanyasa atanitambua me ni nani..kula hiki chakula"..Ilikua ni sauti iliyosikika kwa kila neno likijirudia mala mbilimbili..nayo haikutoka kwa mtu mwingine bali ilitoka ndani ya kinywa cha yule nyoka huku likijikunjua ili kumpa nafasi Nyanzala ale kile chakula..
Na baada kumaliza kujikunjua,lile joka lilirudi ndani ya lile shimo ambalo lilikua pembezoni mwa kaburi.
Hakika Nyanzala alishusha pumzi baada lile joka kuondoka..na ndipo alipo ichukua ile sahani iliyojaa chakula kisha akanza kula..Alikula haraka haraka kama mtu aliekua na njaa ya week nzima ila yote ilitokana njaa kali aliyokua nayo ya kutwa nzima bila kula...Na mala bada kumaliza kula,alirudi ndani n haraka.Lakini alipotaka kubana komeo ya mlango kwa ndani.. ghafra mama yake wa kambo akawa amemtokea ila yeye alikua akienda nje kujisaidia kwani ndio yalikuwa mazoea aliyojiwekea."We mtoto wewe nilikwambia nini kuhusu kutoka usiku??."Nyanzala aliulizwa hivyo na mama yake wa kambo,,ambapo nae Nyanzala alikosa jibu la kumpa..."Nadhani unakiburi sasa hii mala ya mwisho,siku nikikufama tena umetoka nje usikuuu...kiukweli utanitambua vizuli mjinga wewe..haya kalale mbwa koko wewe"..Aliambiwa hivyo Nyanzala huku akisindikizwa na kofi la mgongoni...
Kiukweli lilikua kofi ambalo ni kali sana kwenye mwili wa Nyanzala ,lakini alijikaza kisabuni kisha akaingia chumbani kwake na akawa amelala...Pia usingizi haukuchelewa kumjia maana alikua tayali kashiba chakula alichokula kwenye kaburi la mama yake..
Hivyo alilala fofofo mpaka asubuhi ambapo aliamka kwa niaba ya kwenda shule,lakini mama yake wa kambo alimzuia asiende shule ili afanye usafi wa mazingira nyumbani wakati huo watoto wa yule mama wakielekea shule kutafuta maisha ya baadae..Basi Nyanzala alilia sana kwa kukatazwa kwenda shuleni,lakini kilio chake hakikusaidia kwani ndio kwanza mama yake wa kambo alipo mwongezea kipigo huku akimuuliza nani anae mlilia? Na wakati akimuuliza hivyo,huku mkononi akiwa ameshikilia ndoo..."haya kalete maji kwanza sio kulia lia tu,nani unae mlilia hapa??...Wa kumlilia wewe yupo pale kaburini na sio mimi ila wapo wanaoweza kunililia ila sio wewe..nadhani umenielewa nyoooo"..Ni maneno mabaya aliyopewa Nyanzala.Ama hakika yalizidi kumuuza moyo wake na hivyo akawa analia kwa sauti huku akimtaja marehem mama yake..Lakini mama yake wa kambo hakujali kile kilio cha Nyanzala maana ndio kwanza alipo mlazimisha kwenda kuchota maji...Nyanzala nae hakua na budi ya kukataa,aliipokea ndoo, akajifuta machozi kisha akaelekea kisimani kuchota maji.
Ila wakati akiwa njiani akielekea kisimani,alikutana njiani na baba Maria ambae ni jirani yao..."Nyanzala hujambo??..Baba Maria alimsalimia Nyanzala ..."si jambo shkamoo baba Maria"..Alimjibu hivyo Nyanzala huku akipandisha kwikwi kwa sababu ya kulia sana.."malakhabaaa,mbona leo hujaenda shule mtoto kulikoni"...Baba Maria alimuuliza hivyo Nyanzala,ambapo nae alikaa kimya kidogo akifikilia amjibu nini,kwani aliwaza kwamba endapo kama atamwambia kuwa mama yake wa kambo kamkataza,basi mama yule akizipata hizo taarifa kiukweli patakua hapatoshi..."leo najisikia vibaya ila kesho naweza kwenda..vipi Maria kaenda??..
"Ndio kaenda...ila usiwe mzembe mitihani inakalibia sawa mamaaa"
"sawa baba Maria nitajitahidi"..Basi baba Maria alimuaga Nyanzala ambae alikua akielekea kisimani kuchota maji kisha akaondoka zake.
Naaam! Hatimae Nyanzala alifika kisimani,akachota maji kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani...Na hiyo ilikua imeshafika saa tano asubuhi,hali ya kua nyumbani alitoka saa mbili asibuhi vilevile mama yake wa kambo alimwambia kwamba anatakiwa ndani ya lisali moja awe amesharudi nyumbani...
Nyanzala alijitahidi kukazana maaana alijua kama kachelewa...lakini alipo fika nyumbani hata kabla hajatua beseni ndoo chini iliyojaa maji.ghafra mama yake wa kambo akamjia juu kwa kumtukana matusi mabaya kisa kachelewa kurudi nyumbani.
Lakini wakati yule mama wa kambo alipokua akimshambulia kwa matusi Nyanzala,kumbe baba baba Maria alikua akiyasikia matusi yote aliyokua akitukanwa Nyanzala..Hakika Baba Maria alihuzunika saana.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ila yote kwa yote Nyanzala aliomba msamaha..lakini yule mama wa kambo hakuweza kujali kwani alimwambia kwamba adhabu yake ya kuchelewa kutoka kisimani ni kwenda polini kuchanja kuni..Daah maskini Nyanzala aliitikia "sawa mama me nipo tayali,ila naomba chakula kwanza kisha niende polini kuchanja kuni"Nyanzala alionge hivyo kwa sauti ya upole huku chozi likimtlilika shavuni...kwani alikua amechoka baada kumaliza kutoka kisimani kuchota maji na hivyo kabla hajapumzika akawa amepewa kazi nyingime ngumu..hivyo hilo suala ndilo lililo muumiza mpaka akajikuta akidondosha chozi.."anhaa unataka chakula??..yani mwanangu nile mzaa mimi hajala ila wewe ndio ule?? we mpumbavu nini...embu nenda kalete kuni haraka"..Nyanzala alijibiwa hivyo baada kuomba chakula..Ndipo alipo ingia ndani kisha akachukua panga ambalo lilikua butu hima akaanza safari ya kuelekea polini kutafuta kuni huku akiwa na njaa kali tumboni..Lakini kabla hajaondoka eneo lile la nyumbani kwao..ghafra alikuja mgeni nyumbani kwao kwa baiskeli,mgeni ambae hata Nyanzala hakumjua.."habali za saa hizi mama"...Yule mgeni alimsalimia mama yake wa kambo Nyanzala ambae nae alikua ametulia kwenye mkeka huku akijipodoa uso wake..."salama tu karibu"..Mama yake wa kambo Nyanzala alimjibu hivyo yule mgeni.."sina muda wa kukaa ila chukua hii barua kesho unahitajika kwa mwenyekiti wa kijiji"..Yule mgeni alimkabidhi barua mama yake wa Mama Shani kisha akaondoka zake wakati huo achiwalila nae ameshaondoka polini kutafuta kuni. Hakika mama yake wa kambo Nyanzala alishaangaa kuletewa barua ya mwenyekiti wa kijiji. .na kilicho mpa hofu zaidi ni wito kwa mwenyekiti wa kijiji.
"Mmh kwani kunanini mpaka niletewe barua???...eeh mbona sielewi jamani"...Aliji
uliza hivyo mama yake wa kambo Nyanzala ,huku akiwa bado hajaifungua barua aliyopewa na mjumbe
ili ajue ndani ilikua imeandikwa nini zaidi..Lakini yule mama kwa kua shule ilimpiga chenga(HAJUI KUSOMA)..Ilimlazim kuwasabili watoto wake mpaka watakapo toka shuleni na ndio awape ile barua wamsomee..na wakati akiwaza hivyo kwa kuwangoja wanae,punde si punde wakawa wamefika nyumbani...hivyo kabla hata hawajabadilisha sare zao za shule yule mama wa kambo alimwita mwanae mmoja ambae alikua anamkubali kwa kuwa na akili shuleni nae hakua mwingine alikua ni Kagaruki ."we Kagaruki ..Kagaruki "..Yule mama yake wa kambo Nyanzala alimwita mwanae Kagaruki..nae alipo sikia mama yake akimwita aliitika na haraka sana akatii wito..
"Habali za masomo mwanangu"..Mama Kagaruki alimsalimia mwanae Kagaruki baada kumkalibia.
"nzuli tu mama"..Kagaruki alijibu.
"Anhaaa,sasa noeli leo bwana nimeletewa barua na mtu ambae simjui wala sijawahi kumwona hata siku moja hapa kijijini kwetu,na baada yule mtu kunipa barua akawa ameniambia kwamba kesho nahitajika kwa mwenyekiti..embu shika barua hii hapa uisome maana me naogopa hata kuisoma"..Alisema hivyo yule mama wakambo huku akimkabidhi Kagaruki barua..Na baada Kagaruki kupewa barua ili asome,kweli aliisoma na akawa amekuta barua ikimsisitiza mama yake kutii wito alio itwa na mwenyekiti..."kwani umefanya nini mama"..Nyanzala alimuuliza mama yake baada kukuta ile barua ikimsisitiza mama yake kwenda kwa serikali ya mtaa.
"akha hata mimi sielewi mwanangu,me nilikua nimekaa zangu hapa mala nikaona mtu huyoo anakuja na baiskeli yake..akaanza mala ooooh shika barua na kesho unatakiwa kufika kwa mwenyekiti"..Mama yake wa kambo Nyanzala alimjibu hivyo mwanae Kagaruki huku akiongea kwa mshangao.
Lakini yote kwa yote aliamua kuvuta subira akasubiri kesho yake kipi kitaendelea,na ndipo alipo wambia watoto wake wapakue chakula wale chote bila hata kumwachia Nyanzala ambae alikua ameenda polini kutafuta kuni kwa niaba ya kupikia chakula.
Na kweli wale watoto hawakufanya kosa,maana waliweza kumaliza chakula chote kama mama yao alivyo waambia istoshe baada kumaliza kula walitia maji kwenye masufuria na vyombo walivyo vitumia kula..Na baada kumaliza chakula punde si punde Nyanzala nae akawa amefika nyumbani na mzigo mkubwa wa kuni kichwani,na kwa kua alikua amechoka sana pia njaa kali aliyokua nayo..ilibidi atupe chini mzigo wa kuni kisha akajinyoosha shingo yake.Na kabla hata hajaingia ndani,yule mama yake wa kambo alimwambia"embu tazama pale chini ya kichanja"..Aliambiwa hivyo Nyanzala na mama yake wa kambo,hivyo Nyanzala ikabidi atazame kitu alicho onyeshwa.."umeona nini"Aliulizwa tena Nyanzala baada kutazama kule aliko onyeshwa..."kuna vyombo mama"Alijibu Nyanzala .."anhaa sasa nataka kabla hujaingia ndani hakikisha vyombo vile vyote viwe safi"...Daah Nyanzala alikasilika baada kuambiwa vile wakati alikua kachoka baada kutoka polini kuchanja kuni,,na kilicho muuma zaidi ni pale alipo ambiwa aoshe vyombo wakati watoto wake wakiwa wanacheza na watoto wenzie,hakika chozi lilimtoka Nynzala lakini hakua na lakufanya ilibidi aoshe vile vyombo.
************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada Nyanzala kumaliza kuosha vyombo,alimwomba mama yake wa kambo chakula maana kutwa nzima alikua hajatia chakula chochote kwenye kinywa chake.Lakini yule mama akamwambia.."ch
akula hakuna subili chakula cha usiku"Nyanzala aliambiwa hivyo kwa sauti ya ukali na ndipo nae ikabidi awe mpole japo alikua na njaa kali ila alivumilia.
Kweli na hatimae usiku uliweza kuingia, hapo wakati huo Nyanzala akiwa amelala nje ya nyumba maana kulikua na mbala mwezi hivyo akawa amejilaza nje ya nyumba huku akisubilia chakula cha usiku kwa ham kubwa huku mawzo yote yakiwa kwa marehem mama yake...kwani alitamani kudeka kwa mama yake ila iyo bahati hakua nayo.Lakini wakati yeye Nyanzala akiwa kajilaza nje akingojea chakula kiive hatimae alisikia sauti ya mama yake wa kambo ikiwakanya watoto wake kwamba wasikombe mboga,hivyo Nyanzala akajua dhahili chakula kimeshaiva ila wameamua kuto muita..nae Nyanzala licha ya kujua hilo hakwenda kuwaingilia balia aliwaacha wale tu.
Sasa basi walipo maliza kula nae aliinuka kisha akaingia ndani moja kwa moja alipitiliza chumbani kwake kulala na njaa yake..."haaaa we Nyanzala wakati tunakula ulikua wapi??..Mama yake wa kambo alimuuliza hivyo Nyanzala.lakini nae hakujibu chochote bali alishia kulia huku akijuliza..."hivi kwa nini kila siku mimiiiii na sio wengineee...mama mamaaa njoo uniokoe mwanao nateseka mama daah ukowapi mama"
Nyanzala aliongea hivyo,na ndipo uvumilivu ulipo mshinda na akawa ameangua kilio...Na hata hivyo kilio chake kilizimwa baada mama yake wa kambo kumjia juu akitaka akae kimya kwamba anawapigia kelele...Na hivyo Nyanzala akawa anapandisha kwikwi huku machozi yakimtililika kama maji.
Kiukweli alilia sana Nyanzala kimya kimya,na kwa bahati mbaya siku hiyo baba yake ailipata zarula kazini kwahiyo akawa hajarudi nyumbani siku hiyo...na ndio maana yule mama wa kambo akawa anamfanyia vitimbwi Nyanzala kadri awezavyo.
Basi Nyanzala alilia sana usiku huo,ila mwisho akanyamanza na akaanza kazi ya kutafuta usingizi.
Alijitahidi kutuliza akili ili walau apate hata lepe la usingizi,lakini ilishindikana kwa sababu alikua na njaa kali tumboni.
Hivyo mpaka saa sita inafika,Nyanzala macho bado hayana hata dalili ya kusinzia hivyo alichoka mbavu kwa kulala ikabidi ainuke kisha akawasha kibatali chake na hata hivyo nacho hakikuwaka maana hakikua na mafuta ya taa..Hivyo baada kukuta hali ile aliamua kuacha kuwasha kibatali akawa ameegamia ukuta pale pale kitandani huku akifkilia mambo mbalimbali ambayo yalikua yakimkuta juu yake tangu alipo anza kuishi na mama wa kambo.
Lakini wakati akiwaza na kuwazua,ghafla ulivuma upepo mkali upepo ambao ulikua ukipuliza kuelekea kwenye chumba alichokua amelala Nyanzala, punde si punde baada kuvuma ule upepo ilisikika sauti ya marehem mama yake Nyanzala ikimuita mwanae...."Mwanangu Nyanzala ..Nyanza...we .Nyanzalaaaaa"...Nyanzala aliisikia ile sauti ila akawa amenyamanza kwa kuiskilizia zaidi,na baada kugundua ile ni sauti ya marehem mama yake,aliishuka kitandani kisha akaelekea kwenye dirisha la chumba chake alafu akafunua panzia ya dirisha na akawa ametupa macho mahali lilipokua kaburi la mama yake...hatimae akamwona mama yake juu ya kaburi akiwa amevaa mavazi meupe kuanzia chini mpaka juu..Kiukweli Nyanzala alitamani kwenda pale kaburini maana alijua kwamba endapo kama ataenda pale kaburini,atapata chakula...ila akakumbuka kuwa mama yake wa kambo alishamkanya asitoke nje usiku kwani endapo akimfuma akiwa ametoka nje usiku..basi atamfanyia kitu kibaya ..Na wakati akikumbuka hayo,ile sauti ya marehem mama yake ilizidi kumwita mwanae..huku Nyanzala nae akiwa bado haelewi aende au aache.
Kama njaa alikua nayo tumboni,tena njaa kali.Ila ugumu ukaja kwamba endapo kama atatoka ndani kuelekea kwenye kaburi la mama yake..je,akirudi ndani na akikutana na mama yake wa kambo itakuaje??..Kiu
kweli Nyanzala alikua kati kwa kati hajui achague nini...Lakini baadae kidogo uvumilivu ulimshinda na ndipo alipo fungua mlango akaelekea nyuma ya nyumba ambako ndiko kulikua na kaburi la mama yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Basi Nyanzala baada kufika kwenye kaburi la mama yake,aliweza kumwona marehem mama yake akiwa katika mavazi yake meupe huku akiwa kasimama kando kidogo ya kaburi.
"Nyanzala mwanangu"..Ilikua sauti ya marehem mama Nyanzala iliyosikika kwa mwangwi yaani ikijirudia mala mbili mbili...."Abee mama"..Nyanzala alimwitikia mama yake huku akionekana kuogopa kutokana na sauti ya mama yake ilivyokua ikisikika.
"najua ni tabu gani unazo zipata mwanangu ila ipo siku mateso hayo yataisha mwanangu..sawaaa nipo pamoja na wew na pia napenda kila siku usiku uwe unakuja hapa kwenye nyumba yangu nikupe chakula lakini mchana sitoweza..vilevile nakuomba iwe siri kati yangu mimi na wewe.nakupenda sana mwanangu"...Yalikua ni maneno ya marehem mama Nyanzala aliyokua akimwambia mwanae..Na baada kumaliza kumwambia hivyo ndipo mama Nyanzala alipo chuchumaa nghafla akageuka nyoka mkubwa mfano wa chatu...na baada kugeuka hali ile,yule nyoka aliachasama mdomo wake kama ilivyo ada na punde si punde kunako kinywa cha yule nyoka kilitokea chakula..Wakati huo Nyanzala akiwa tayali kajiweka mkao wa kula..."kula mwanangu"..Sauti ilitoka mdomoni mwa yule nyoka wakati sahani tayali ikiwa mbele ya Nyanzala .
Nyanzala alikula chakula kile bila kupumzika maana kutwa nzima alikua hajatia kitu chochote mdomoni mwake,hivyo ndani ya dakika tano alikua tayali kamaliza chakula na wakati huo yule nyoka kashatokomea ndani ya kaburi...Na baada Nyanzala kumaliza kula chakula,hatimae aliinuka kutoka pale kwenye kaburi la mama yake,kisha akajikun'guta vumbi la kaburi alafua akaanza safari ya kurudi ndani.
Kiukweli Nyanzala alimwomba mungu asimkutanishe na mama yake wa kambo kwa mida ule,kwani alishamkanya asiwe anatoka nje usiku....Na kweli dua zake zilifika maana alifungua mlango kisha akaingia ndani alafu akabana komeo za ndani kama kawaida...Na baada kuingia chumbani kwake tu mala ghafla akamsikia mama yake wa kambo nae akienda nje,,,kwahiyo endapo kama engechelewa dakika kadhaa basi angefumwa na mama yake wa kambo.
Hakika usingizi ukawa mororo kwa binti Nyanzala..sababu alikua kashiba hivyo aliweza kusinzia hadi asubuhi..
Na baada kupambazuka aliweza kuvaa nguo zake za shule harakaharaka kabla mama yake wa kambo hajaamka,kisha akatimka shuleni..Na mala baada Nyanzala kwenda shule,kama kawaida yake mama wakambo aliiamka na akaelekea kwenye chumba cha Nyanzala ili ampe majukumu mbalimbali ya nyumbani..."haaaa hili litoto limeenda wapi"..Alishtuka mama yake wa kambo Nyanzala na ndipo alipo tazama mahali ambapo Nyanzala alikua akiweka sare za shule..hivyo akawa hajaziona akajua kua Nyanzala kashaondoka shuleni..."aaan
haaa asinifanye mimi punguwani ngoja akirudi ndio atanijua mimi ni nani...haya na nyie amkeni haraka muwahi namba shuleni sio mnalala hadi muda huu amakeniii"..Kiukweli alikasirika sana mama yake wa kambo Nyanzala baada kukuta Nyanzala kaenda shule bila hidhini yake,na hasira hizo zilimpelekea hadi kuwakurupusha watoto wake ambao walikua bado wamelala muda wa kwenda shuleni.
Basi baada mama yake wa kambo Nyanzala kuonekana kukelwa na kile kitendo cha Nyanzala ...Mala punde si punde akaletewa taarifa na mmoja kati ya wanakijiji kwamba anahitajika haraka sana kwa mwenyekiti...na endapo akichelewa basi atatumiwa mgambo.
Daah mama yule wakambo alishtuka huku akijiuliza kunani kwa mwenyekiti,kosa gani nililolifanya hapa kijijini..???..
Lakini yote kwa yote yule mama yake wakambo Nyanzala alijianda kisha akaelekea kwa mwenyekiti kumsikiliza ana nini juu yake...Lakini wakati akikalibia kwa mwenyekiti wa kijiji alishtuka baada kukuta baadhi ya wazee wa kijiji wakiwemo na wakina mama wote wakiwa nyumbani kwa mwenyekiti na mmoja kati ya watu waliokuwepo pale ni baba Maria ambae ni jirani yake.
Hivyo ndipo mama yake wa kambo Nyanzala alipojisogeza mahali walipo kuwepo wanawake wenzake..."habali za saa hizi jamani"..Mama yake wakambo Nyanzala aliwasalimia wanawake wenzake aliowakuta pale nao waliishia kumwangalia tu pasipo kuitikia salam yake...Lakini hakuchoka alirudia tena kusalimia wakati huo akiwa tayali kakaa kwenye kigoda.."ebwanaee kama unaona salam ni chakula basi mpelekee yatima yule unae mnyanyasa"...Al
ijibu hivyo mmoja kati ya wanawake waliokuwepo pale kwa mwenyekiti.. na hapo ndipo mama yake wa kambo Nyanzala alijua kua dhahili huwenda Nyanzala katangaza kua anamnyanyasa.
Basi baada mama Shani kujibiwa hivyo ilibidi akae kimya maana watu wote waliokuwepo pale kwa mwenyekiti walionekana kumkunjia uso...Naam hatimae punde si punde mwenyekiti alirudi nyumbani kwake maana alikua ametoka kidogo kwenda kijiji jirani kununua dawa za mwanae aliekua akisumbuliwa na malaria...Kiukweli mama yake wakambo Nyanzala alishtuka baada kumwona mwenyekiti kwani alijua hukum inamuhusu kwa kitendo kile cha kumnyanyasa mtoto alie fiwa na mama yake.
"Naam habali zenu ndugu zanguni"..Mweny
ekiti alianza kwa salam wakati huo ameshaipaki chini ya mwembe baiskeli yake aliyotumia kama usafiri wa kwenda kununua dawa za mtoto wake.
"salama tu mwenyekiti sijui kwako"...WaliitiCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kia salam wanakijiji waliokuwepo pale na mmoja akawa ameuliza hali ya familia ya mwenyekiti.."mmmh sisi hatujambo kidogo ndio maana mnaona nimechelewa kwa sababu nilienda kununua dawa za mwanangu anae sumbuliwa na malaria tangu juzi..ila hali yake sio mbaya anaendelea vizuli tu"...Aliongea hivyo mwenyekiti,na ghafla zikasikika sauti za baadhi ya watu waliokuwepo pale wakimpa pole mwenyekiti kwa kuuguliwa na mwanae.
Na mala baada kuongea maneno hayo mawili matatu,hatimae mwenyekiti aliiingia kwenye mjadala ulio wafanya wakusanyike pale..."mama Kagaruki yupo?"..Mwenyekiti aliuliza hivyo.."ndio nipo"..Nae mama Kagaruki ambae ndio mama Shani pia mama yake wa kambo Nyanzala aliitika hivyo baada kusikia mwenyekiti akimuulizia.."anhaa embu sogea hapa mbele ili wazee wa kijiji nao waweze kukuona"..Kweli mama Kagaruki aliweza kujisogeza mbele huku usoni akionekana kua na haibu baada kutazamwa na wazee wa kijiji waliokuwepo pale kwa mwenyekiti.
"mume wako yuko wapi??..Mwenyekiti alimuuliza mama Mama kagaruki.."yuko kazini "...Mama yake wa kambo Nyanzala nae alimjibu hivyo.."ila nadhani barua uliyoletewa jana imekufikia"...Mwenyekiti aliuliza tena hivyo huku akionekana kua na jazba..Lakini licha mama yule kuulizwa hivyo ila alijibu kwa ishara ya kukubali kwa kutumia kichwa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment