Search This Blog

JINA LA URITHI - 3

 







    Simulizi : Jina La Urithi

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Laula akashtuka usingizini ,,,akaangaza angaza macho yake huku na kule,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi ya ajabu! akatimua mbio kutoka eneo hilo,,baada ya dakika kadhaa kupita akajikuta katooezea mtaa wa pili,,kulikuwa na maduka mengi yamefungwa.....akalifuata duka moja na kuketi kwenye kibaraza,,,baridi lilikuwa kali,,kutokana na upepo uliovuma mfululizo.. akajikunyata na uanza kuutafuta usingizi,,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi palipokucha,,akadamka mapema kabla maduka hayajafunguliwa,,akazipiga hatua pasipokujua ni wapi anakwenda!

    baada ya masaa kadhaa kupita,,akahisi njaa kali! akaamua kulifuata soko lililokuwa kando ya barabara...akaona ndizi mbivu.akazitamani ndizi hizo,,,akazipiga hatua mpaka katika meza hiyo...akachukua ndizi na kuanza kula.

    alifanya vivyo hivyo kwa mara kadhaa hatimae akala ndizi tano! alipohisi kashiba akazipiga hatua kuondoka zake! punde si punde ikasikika sauti ya mama muuza ndizi,,akisema,,"wewe mtoto mbona unaondoka pasipo kulipa pesa ya ndizi ulizokula.

    aliongea  maneno hayo huku akizipiga hatua kumfuata Laula akamkamata mkono!

    Laula akamtazama mama huyo kwa sura ya huruma! kisha akasema,,"naomba unisamehe sina hata shilingi....nilikuwa na njaa kali...nihurumie tafadhali.

    mwanamke huyo akaingiwa na roho ya huruma akaamua kumuacha Laula aondoke zake.



    upande mwingine kule kijijini,,hofu ilizidi kutanda ndani ya kijiji hicho! Nyumba ziliungua moto pasipokujulikana chanzo cha moto huo,,,ni zile Nyumba za watu walioshiriki kuichoma Nyumba ya Njile!

    mkuu wa kijiji akaitisha mkutano,,,wanakijiji wote wakakusanyika kujadili nini suluhisho la mambo hayo yanayotokea.......wakakubaliana aletwe mganga mchawi kutazama ni kitu gani kinachoendelea ndani ya kijiji hicho,,



    upande mwingine alionekana Laula akiendelea kurandaranda mitaani,,,alitembea umbali mrefu pasipokujua ni wapi anakoelekea! akajikuta anatoka katikati ya mji...baada ya kutembea masaa kadhaa mfululizo,akahisi uchovu,,akaangaza macho yake huku na kule kutafuta mti wenye kivuli,angalau ajipumzishe,,,

    akafanikiwa kuona mti mkubwa akaamua kuufuata mti huo,,akajipumzisha....Laula akajikuta anazama kwenye dimbwi la mawazo mazito akanyanyua uso wake kutazama kando,,,akashtuka kuona eneo hilo kama alishawahi kuliona,,na sio mara ya kwanza,,alipojaribu kuvuta kumbukumbu,,,akastaajabu sehemu hiyo ni eneo la makaburi aliyoyaona ndotoni usiku wa jana! akanyanyuka harakaharaka....akazipiga hatua kuelekea katikati ya makaburi...huenda akaliona lile kaburi laliloliona kwenye ndoto...punde si punde akasikia sauti ya vishindo vya mtu akitembea nyuma yake!!!!

    TAHARUKI!!!!!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    hofu ikazidi kuongezeka,,akaogopa kugeuza shingo yake,,hakutamani hata kushuhudia, mtu aliyekuwa nyuma yake,,mapigo ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi ya ajabu,,jasho likaanza kumtoka! mwili wa Laula ukaonyesha kutetemeka....punde si punde vile vishindo hakuvisikia tena..akaamua kugeuza shingo yake,lakini hakuona mtu yeyote! akaangaza angaza macho yake huku na kule,kwa mbali akahisi kama kamuona mtu anaishilizia mtu huyo alionekana ni mzee kikongwe! akamtambua mtu huyo kutokana na mavazi aliyoyavaa kikongwe huyo,,si mwingine ni yule babu yake!



    Upande mwingine kule kijijini,,alionekana mkuu wa kijiji ,akiwa tayari kamuita mganga mchawi apige tunguri,,kujua chanzo cha miujiza iliyoonekana kijijini hapo!

    mganga huyo ni moto wa kuotea mbali,,,aliaminika kuwa hakuna jambo aliloshindwa kulifanya! mganga akasema,,"nahitaji muda niachwe peke yangu, naweza kupata chumba?

    mkuu wa kijiji akasema,," chumba kipo...aliongea maneno hayo huku akiongozana na mganga,kuifuata nyumba iliyokuwa jirani na shamba,,,akafungua mlango kisha akauliza,,"nadhani chumba hiki kitakufaa.

    mganga akajibu,,"bila shaka.

    mkuu wa kijiji akazipiga hatua akaondoka na kumuacha mganga akiwa peke yake! mganga huyo akavua nguo zake zote akabaki mtupu kama alivyozaliwa! kisha akatoa zana zake za kichawi tayari kuianza kazi yake ya uganga! akachukua pembe la ng'ombe,,,akanyunyizia dawa ya kichawi ndani ya pembe hilo....kisha akaanza kuongea lugha ya kichawi huku akazunguka ndani ya chumba hicho...alifanya hivyo kwa mara kadhaa....kisha akatabasamu,,akavaa nguo zake,,na kutoka nje ya chumba hicho.

    wakati huo wazee wa kijiji pamoja na baadhi ya wanakijiji,,wakiambatana na mkuu wa kijiji,,walikuwa wamesimama nje wakisubiri majibu ya mganga huyo....wakamuona anatoka ndani ya chumba hicho...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mganga akazipiga hatua kuwafuata kisha akasema,,"msiwe na wasiwasi mimi ndiye SAGALI wa SAGALI...nimeshaweka mtego wa hatua ya kwanza,,mtego huo ni maalumu....kwa yeyote aliyehusika na mambo hayo lazima apatwe na maumivu makali kwenye mwili wake, pia atakuja mpaka hapa yeye mwenyewe na kuongea kila kitu alichowahi kukifanya ndani ya kijiji hiki.



    wakati huo huo,,kule makaburini alionekana Laula akiwa bado kwenye taharuki, akatafakari nini cha kufanya,,ghafla wazo likamjia,akageuza shingo yake kutazama tena,ule upande aliomuna babu yake, Laula aliendelea kukodoa macho yake huenda akamuona babu yake,,lakini hakufanikiwa kumuona..akajisemea moyo,,"lakini hili kaburi lililopo mbele yangu ndio lile ninililoliona jana kwenye ndoto..alijisemea maneno hayo huku akilisogelea kaburi hilo,,akajiuli,,"hili kaburi ni la nani?

    punde si punde akaanza kuhisi maumivu makali tumboni! Laula akashindwa kuvumilia,,akaamua kuketi juu ya kaburi hilo,,huku akiwa ameweka mikono yake tumboni!

    kadri dakika zilivyozidi kusongo ndivyo maumivu yalizidi kumuandama....akanyanyuka na kuvua suruali,,ni ile suruali aliyoitoa kwenye sanduku la nguo za baba yake...

    wakati Laula anachuchumaa  lile jino likadondoka pale juu ya kaburi! lakini Laula hakuona kitendo hicho,kutokana na maumivu makali aliyokuwanayo!

    punde si punde,,maumivu yakatoweka,,na tumbo lake likarudi katika hali yake ya kawaida! akanyanyuka na kuvaa suruali..akaifunga vyema kwa kamba kiunoni.....ghafla ikasikika sauti ya mingurumo ya ajabu,,,matawi ya miti iliyokuwa imeota kulizunguka eneno la makaburi,,yakaanza kutikisikika,,ukavuma upepo mkali,,,nuru ikaanza kutoweka taratibu na giza likatanda..

    punde si punde lile kaburi lililokuwa mbele ya Laula likaanza kutikisika,Laula akalitazama kaburi hilo,,akashtuka kuona jino juu ya kaburi hilo! akaingiza haraka mkono wake ndani ya mfuko wa suruali aliyokuwa ameivaa, akajisemea moyoni,,"hilo jino limetokaje humu kwenye mfuko?

    wakati anajiuliza maswali hayo,,ghafla ardhi ikaanza kutikisika na lile jino likatoweka kimiujiza Laula akaingiwa na hofu akaamua kutimua mbio,,kutoka eneo hilo la makaburi.



    wakati huo huo,,kule kijijini,,waliendelea kusubiri,,punde si punde mganga akashtuka!akahisi harufu isiyoyakawaida akaingiwa na wasiwasi!!! akatimua mbio kukifuata kile chumba akachukua zana zake za kichawi,,akaziweka kando yake kisha akachukua kioo maalumu cha kichawi...akakipaka dawa ili aweze kuona nini kinachoendelea..

    wakati huohuo kule upande wa nje,,wanakijiji hawakuwa na mashaka,,,ghafla ikasikika sauti ya mganga akipiga kelele.kule chumbani,,punde si punde mganga akaonekana akitokea ndani ya chumba hicho huku akitimua mbio....wanakijiji wakaingiwa na hofu...mara ghafla giza likatanda!!

    PATASHIKA!!!!







    Wanakijiji wakaingiwa na hofu kupita kiasi,,hawakuwahi kuona mcha umebadilika kuwa usiku wenye giza totoro! kila mtu akatimua mbio,,pasipo kujua ni wapi wanaelekea!

    ghafla kikasikika kilio cha mtu akilia kwa sauti ya maumivu makali,,punde si punde giza likatoweka na nuru ikarudi,,

    huwezi kuamini kilichompata mganga,SAGALI WA SAGALI..alionekana kutokwa na damu mwilini mwake!!



    upande mwingine,,alionekana Laula akiendelea kutimua mbio,,sasahivi alikuwa tayari katoka eneo la makaburi..

    aliendelea kutimua mbio pasipo kusimama....alipohakikisha yupo mbali na eneo la makaburi,,akageuza shingo yake kutaza ule upande wa makaburi...akaona moshi mkubwa,macho yakamtoka!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alipotazama kwa makini,,akaona miti inatikisika na kudondoka chini...akaamua kutimua mbio..

    alikimbia umbali mrefu mpaka katikati ya mji! akasita kukimbia akaamua kuzipiga hatua za haraka haraka ,,macho yake yakitazama huku na kule,,,uso wake ulionekana kuwa na wasiwasi kupita kiasi,,jambo ambalo liliwafanya watu wamshangae barabarani..Laula hakujali yeye aliendelea kuzipiga hatua pasipokujua ni wapi anakoelekea!



    upande mwingine,,kule kijijini,alionekana mganga Sagali wa sagali akiwa bado yupo pale chini huku akitokwa na damu nyingi kupita kiasi! hali yake ilikuwa tahabani,

    fahamu zikarejea,akafumbua macho yake,,akahisi maumivu makali mwili wote! akaangaza macho yake huku na kule,,hakuona mtu yeyote! hakuwepo hata mwanakijiji moja katika eneo hilo!

    akanyanyuka kwa kujikongoja na kuchukua tunguri zake..akasimama wima akaitazama ile nyumba,,aliyoweka mtego wake wa kichawi,,lakini mambo yakawa ndivyosivyo!

    Sagali wa Sagali akaingiwa na hasira kupita kiasi...ghafla akaona kitu cha ajabu  macho yakamtoka akapiga tunguri zake atoweke kimiujiza katika eneo hilo lakini akawa ameshachelewa,,alipotahamaki mara ghafla!!! Ukaonekana mzimu wa muanzilishi wa ukoo wa Laula....mzimu huo uliamka kutoka makaburini ni baada ya Laula kudondosha lile jino juu ya kaburi hilo!

    Mzimu huo ukamkamata mganga Sagali wa Sagali na kuondoa uhai wake papohapo....kisha mzimu huo ukatoweka kimiujiza kwenda kumtafuta mrithi wa jina lake!..



    wakati huohuo upande mwingine,,alionekana Laula akiwa bado yupo katikati ya mji akirandaranda....akahisi njaa kali lakini akajikaza kutokana hakuwa na pesa ya kununua chakula....

    siku ya leo akaamua kuifuata nyumba moja aliyoiona kando ya barabara akiamini huenda akapata msaada wa chakula!

    alipoikaribia nyumba hiyo akagonga hodi,,,na baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa..Laula akatoa salamu kisha akaeleza shida yake....mtu aliyefungua mlango akamuhurumia Laula akaamua kumkaribisha ndani ya nyumba kwa lengo la kumpa chakula..Laula akazipiga hatua akaingia ndani ya nyumba hiyo!

    akaketi kwenye sofa,,akisubiri aletewe chakula...yule mtu aliyemkaribisha ndani ya nyumba hiyo akazipiga hatua kuelekea jikoni...akafungua jokofu akatoa chakula na kukiweka jikoni ampikie mtoto Laula.

    baada ya dakika kadhaa chakula kikawa tayari,,akakiweka kwenye sahani  kumpelekea Laula kule sebuleni......kabla ya kupeleka chakula akahisi vitu vinadondoka upande wa chumbani!!

    akashtuka! akaingiwa na wasiwasi labda mtoto aliyemkaribisha ndani ni mwizi, huenda ndiye ameingia chumbani!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akaamua kutoka haraka jikoni na kuelekea upande wa sebuleni...

    akastaajabu kumkuta Laula akiwa kaketi vilevile kama alivyomuacha mwanzo!!! macho yakamtoka!!

    Laula akashtuka kumuona mtu huyo akimtazama kwa macho ya msisitizo! akaamua kumuuliza,,"mbona wanitazama? kuna jambo ambalo haliko sawa?

    yele mtu akaamua kudanganya akasema,,"nilikuwa najaribu kukumbuka jambo fulani,,

    aliongea hivyo huku akizioiga hatua kurudi upande wa jikoni....alipofika katika korido,,ghafla akasikia tena vitu vikidondoka kule chumbani...sasahivi hata vyombo vilivyokuwa katika kabati la vyombo jikoni,, viligongana na vingine kupasuka...jambo hilo lilimfanya mtu huyo aingiwe na hofu...punde si punde likatokea tetemeko la ardhi na nyumba ikaanza kutikisika....mara ghafla!!!!!!!!!



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog