Search This Blog

TOZANI ( PETE YA AJABU) - 1

 







    IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Tozani (Pete Ya Ajabu)

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    UTANGULIZI



    Kwanza nimshukuru MWENYEZI MUNGU muumba ardhi na mbingu,na vitu vyote vilivyomo kwa kuniwezesha afya njema mpaka muda huu ninayo andaa riwaya hii.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pili wazazi ndugu na marafiki zangu kwa kuwa nami kunishauri ninapokosea kununua kazi zangu na hata kulike,share kwa wingi sina cha kuwapa zaidi ya kuwashkuru sana



    Na Leo ndo tunaianza rasmi riwaya hii ambayo hata ivyo vipande kumi vya MWISHO atutavitoa vitapatikana kwa 2000 tu hivyo kwanzia sasa anza kujipanga,Riwaya hi itakuwa inarushwa kila baada ya siku moja ila grp whatsupp ni kila siku



    TUANZE SASA....



    SEHEMU YA KWANZA



    SURA YA KWANZA



    (1)



    Hali ya hewa ilikuwa ni ya kimanyunyu manyunyu na kaubaridi ka mbali Kali chosababisha kuleta uvivu watu kuamka na kuzidi kuvuta mashuka na mablangeti



    Tayari kulikuwa kumekucha lakini kutokana na hali ile ya hali ya hewa bado palionekana ni alfajiri kumbe tayari ilikuwa ni saa mbili ila ilionekana kama bado ni saa kumi na moja!



    Watoto wengi sana walifurahia hali ile kutokana na kujua kuwa hawatoenda shule,na walizidi kufurahi pale radi lilipoanza kupiga na kushusha mvua Kali,mvua iliyoambatana na upepo



    KATIKATI YA PORI PANDE



    Usiku ule ule



    Pori pande lilikuwa ni pori lenye kutisha,tena lenye viumbe wa Kali wenye sauti tofauti tofauti zenye kutisha



    Viumbe jamii ya majini,lilikuwa ni pori lililoogopwa mtu alishindwa kuvuka mwenyewe lazima muwe wawili au zaidi tofauti na ivyo basi ni lazima ungekutana na mambo ya ajabu



    Mbali na mambo hayo pia kulikuwa na wanyama wakali kama nyoka wengi wa wapita njia walipita kwa uangalifu sheria ilokuwepo enzi na enzi za mababu ni kutoua kiumbe chochote katika pori lile



    Ikiwa utaua nawe utomaliza siku tatu nawe utakufa....



    Pembezoni mwa msitu ule alionekana mtoto mdogo kiumri si chini ya miaka kumi na Tatu alikuwa akikimbia,alikimbizwa na viumbe visivyoeleweka,viumbe vile vilikuwa na pembe kichwani,midomoni vikitoa damu,meno mawili yalichongoka katika kila pembe ya mdomo wao viliwaongezea ubaya na mtisho kwa binadamu awaonaye

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndiyo!



    Kijana yule alizidi kukimbia pasina kujali vitisho vya sauti zao,akujali kule akimbiapo wala hakuona kwamba ndo kuna hatari



    Akazama ndani ya msitu ule viumbe vile vilizidi kumkimbiza safari hii spidi zao ziliongezeka kwa kila hatua walopiga



    Na sasa walibakisha hatua chache kumfikia mtoto yule na ghafla akawageukia,naye sura ilibadilika na kuwa ya kutisha



    Viumbe wale wakarudi nyuma kidogo



    Mmoja akanyoosha mkono wake na kuachia kombora,mtoto yule kwa ustadi akaufunua mdomo wake na kombora lile akalimeza



    Viumbe vile vikapigwa na butwaa!



    Vikabaki vinashangaa pasina kuamini jambo lile!...



    Kiumbe kile kikageuka ghafla na kuanza kukimbia tena...akipiga hatua kubwa kubwa,alikuwa ni mwepesi balaa,viumbe vile vikazinduka toka katika mshangao na kuanza tena mbio kumkimbiza mtoto yule



    Safari hii mtoto yule alijishangaa!,kwanza uwoga na Pili ile hali ya kujiamini hakuwa nayo tena ni ghafla tu!



    Ni nini kilichomtokea?!



    Akujua



    Akazidi kukimbia alipoakikisha amewaaacha mbali maadui zake akauparamia mti na kupanda juu yake



    Muda huo aliyekuwa juu ya mti,akitetemeka chini ya mti ule viumbe wale wasioeleweka kwa sura zao waliwasili na kusimama eneo lile



    Wakawa wakinusa nusa na Mara mmoja akamuona mtoto yule juu ya ule mti....



    Akaachia mlio wake wakutisha,ni kama alikuwa akishangilia kupatikana kwa mtoto yule



    Kiumbe yule akaunyoosha mkono wake juu,mkono ukawa ukiongezeka urefu mtoto yule akawa akilia....



    Viumbe vile vingine vikawa vikiruka ruka kushangilia



    Mkono ule ukamfikia mtoto yule na kumkamata kwa nguvu akawa anaurudisha mkono chini na kadri anavyourudisha mkono ulipungua kimo mpaka ukawa kawaida...



    "Twaitaji tozani yetu!"



    "Tozani?!"



    Kabla ajajibiwa kibao kikalia katika paji lake la uso



    "Usijifanye kutuuliza wewe ni kiumbe mdogo sana mwenye nguvu ndogo sana uwezi shindana na majini ya himaya hii kuokoa maisha yako tupatie tozani!"



    "Sina tozani! Jamani tozani ni nini?!"



    " ujui siyo utatupatia tu twende utatueleza"



    Wakawa wanamkokota mtoto yule kwa nguvu,bila kujali kelele alizokuwa akipiga



    Ajabu moja sasa



    Ni katika ulimwengu waliokuwepo,baada ya yule mtoto kuingia katika pori pande lile



    Palibadilika!,nje ya pori palikuwa na mvua ya manyunyu manyunyu ila ndani ya msitu hali ile aikwepo na sasa akiwa mikononi mwa viumbe wale mkono ulojaa miba na kumchoma choma pia mazingira Yale yalibadilika



    Akuelewa!



    Nyumba zilitawala kule alipokuwepo,anga lilikuwa jekundu na alipishana na viumbe pia visivyoeleweka



    Alizidi kuachia yowe labda pengine alijua kulia kwake vile kungemsaidia



    Alijidanganya



    "ABRAHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA...."



    akashtuka anaitwa ghafla akaacha kulia,wale walomteka ni wazi awakuisikia sauti ile...wao walistaajabu kumuona kaacha kulia ghafla



    Nguvu zake za kimaajabu zikawa zinamjia



    Ndani ya mdomo wake meno yakaanza kubadilika,hasira kumtawala



    "ABRAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA"



    Akazidi kuitwa safari hii hata wale viumbe pia waliisikia sauti ile wote wakapiga magoti ishara ya heshima



    Juu kidogo ya mawingu alionekana kijana mzuri akiwa kavaa nguo nyeupe na kofia ya kifalme alikuwa mweupe ni mzuri haswaa mwarabu si mwarabu muhindi si muhindi , msomali si msomali



    Mtoto yule Abrah akabaki kamkodolea macho akiusanifu uzuri wa kiumbe kile



    "Abraaaaaaaa naitaji tozani abraaaaa"



    Akatamka akimwelekezea upanga wake ulowaka waka!



    "Tozani?!"



    Akajiuliza tena ni wazi akuijua tozani hiyo ilosemwa na viumbe vile waloihtaji



    Baada ya kiumbe kile kumuona Abrah ana dalili ya kumuonesha akapiga kibao hewani



    Kibao kile kikamfikia mtoto yule,akaangua kilio



    Mtu yule alokuja akaonesha ishara ya kunyonga



    Maumivu makali ya kunyongwa yakamfikia kijana yule akaweka mikono shingoni akikohoa,nyota nyota zilipita katika macho yake



    Mtu yule ni wazi alikuwa na hasira na alipania kumuua mtoto yule



    Abrah akadondoka chini na kuanza kutapatapa,kiumbe kile kiliamua kuua lengo wakose wote



    Ni wakati huo kiumbe yule akiendelea kutetemeka kwa hasira na kuzidi kuikunja mikono yake ishara ya kunyonga ngafla mtoto yule akajitutumua na kuachia kombora moja,kiumbe kile kilichokuwa juu kikatua chini



    Ilikuwa ni kama Abrah kakitungua,nacho kikaamka kwa ghadhabu, sasa kijana yule mzuri aliongozwa na hasira



    Ghafla pale aliponyanyua kichwa chake kumtazama mtoto yule, akuiona kabisa sura ya mtoto yule zaidi ya kuiona sura ya binti Mrembo,binti alotokea kumpenda akimwangalia kwa tabasamu baya!



    "ZENA KUREYSH?!" Mtu yule akaita kwa hamaki!



    "Mfalme Zuberi,icho utakacho kufanya siyo kwa nini uue kiumbe kisicho na hatia kisichojua nini maana ya TOZANI,ntamlinda mpaka tone la mwisho la uhai wangu hakuna atakaye mgusa yeye ndiyo anayeimiliki TOZANI,yeye ndiyo moyo wangu....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yalikuwa ni maneno makali yalotoka katika mdomo wa Dada yule maneno yalomchoma mfalme yule,maneno ya ukweli



    baada ya Dada yule Mrembo kumaliza maneno Yale akageuka na kuondoka



    Viumbe vyote vilibaki vikimtazama mfalme wao kwa kukaachia katoto kale kaondoke,wao hawakujua kilichomtokea mfalme wao kwani wao waliiona sura ya mtoto ilipobadilika awakuiona



    Kijana yule mzuri kisura mfalme wa majini wa pori lile alilia



    Alilia kuikosa tozani



    Alilia kumkosa Zena!



    Ghafla yeye na wenzake wakatoweka walipanga kwenda kujipanga upya



    **************



    Abrah baada ya kufanikiwa kuwatoroka viumbe vile alizidi kukimbia,akujua anakimbilia wapi



    Alikuwa bado yupo katikati ya pori njia ya kutokea akuiona wakati akiendelea kukimbia ghafla akakanyaga mtego



    Mtego ule ukamfunga mguu mmoja juu ya mti akabaki akining'inia ghafla akashtuliwa na sauti ya vicheko vya watu



    No,hapana si watu wale ni vile viumbe vya kutisha vyeusi tiiii!,macho yao mekundu ya duara yaliwaka waka,meno yao yalitawaliwa na njano mdomoni walifoka moshi,katika vichwa vyao walikuwa na pembe walivaa nguo nyeusi



    Hawa walikuwa ni tofauti na wale wa kwanza!



    Abrah mwili ulimsisimuka, ulimwisha nguvu,akujua ataokokaje katika mtego ule



    Katu akujua kuwa kuna kiumbe kinachomlinda wakati analia ghafla akasikia kibao



    Alipigwa na mmoja wa viumbe wale



    Ghafla Abrah akashtuka!.....



    Kumbe ilikuwa ni ndoto,pembeni yake alisimama mama yake wa kambo akimtazama kwa chuki sana



    Na pale alipohisi kapigwa na kiumbe yule wa ajabu kibao ni pale mama yule alipomnasa kibao



    "Haya amka uende shule"



    Ilikuwa ni sauti ya amri, mvua kubwa nje ilinyesha,na ni mvua haswa



    "Lakini mama mbona mvua inanyesha ntaendaje mama?!"



    "Ilo sijui ila nenda kajiandae uondoke hapa"



    "Peter na Samwel je"



    "Staki kuulizwa maswali amka uende!"



    Yule mama hakuwa na u binadamu kabisa,akumpenda mtoto yule wa mume wake, alimnyanyasa,sa hiyo wanawe walikuwa wamelala bila kujali mvua inyeshayo akataka kumtoa mtoto yule raha yake anyeshewe



    "Haya amkaa,amka saa mbili sasa"



    Abrah kwa unyonge akajiamsha na kuchungulia nje,alikutana na mvua kubwa,akageuza macho kumwangalia mama yake yule akakutana na macho makali



    Mama yule akazivuta nguo za Abrah za shule na kumtupia



    "Haya vaa,vaaa uende"



    "Pori pande ntapitaje mama!"



    "Kwani siku nyingine huwa unapitaje na ona unijui Mimi ngoja nkakuletee fimbo ndo itakufanya ufanye haraka"



    Baada ya mama yule kuongea vile akatoka,kwa uoga Abrah akaanza kuvaa nguo haraka haraka mpaka akamaliza



    Mama yule aliporejea na fimbo alimkuta tayari kashamaliza kuvaa



    "Haya sasa toka toka nje uende elimu ni ufunguo wa maisha yako ila naona wewe unazembea zembea"



    Akaongea mama yule kwa ukali!



    "Mama sijanywa chai!"



    "Chai uliamka hasubui ukapika embu ntokee hapa"



    Akaitimisha mama yule huku akimshika mkono mtoto yule na kumvuta!



    Akamsukumia nje!....



    Abrah akaanza kukimbia,mvua ilizidi kunyesha na kumlowanisha akujali hilo



    Alichowaza ni msitu pande je angevukaje?!



    Alijua asingekuta mtu pale langoni wa kuvuka naye ni vipi angevuka



    Ghafla akakumbuka ndoto



    Akaikumbuka tozani alodaiwa na viumbe vile vya ajabu,ajabu



    TOZANI ni nini?!



    Akawaza ila akupata jibu,mwisho mshawasha wa kutaka kufika shule haraka ukamwingia



    Nia ni kumuuliza mwalimu wake wa kiswahili maana ya neno hilo



    Akazidi kukimbia tena kwa moyo mmoja



    Alikuwa kalowana chapachapa



    Ila sasa moyo wa kijasiri ulimvaa,mpaka hapo alipofikia hakukutana na mtu hata mmoja sasa alilikaribia pori lile



    Pori ambalo usiku aliliota



    Pori ambalo alilijua habari yake



    Moyo ukaanza kumwenda mbio,nywele kumsisimuka



    Ghafla tabasamu likamvaa,baada ya langoni pale kumkuta mwanafunzi mwenzake



    Tena wa kike, lakini yule akulowana hata chembe,alikuwa akimwangalia Abrah kwa tabasamu mwanana



    Mwanafunzi yule alikuwa ni msafi tofauti na wanafunzi wa shule yao



    Shati lake jeupe lilinyooka na kumwongezea umaridadi,sketi yake nayo ilipigwa pasi,hakika alikuwa kivutio machoni mwa Abrah



    Wakabaki wanatazamana



    "Mambo"



    Mtoto yule akatoa salamu kwa sauti tamu huku akimpa mkono abrah , Abrah akaupokea na kukutana na joto lililomfanya asitamani kuachanisha mkono wake na wa mtoto yule.



    "Poa mbona wewe ujaloana?!"



    Kijana yule akaitika na kuuliza swali



    "Mimi Nina mwamvuli huu hapa"



    Macho ya Abrah yakauangalia ule mwa mvuli aloushika yule binti ambaye akuuona kabla na taratibu akayashusha macho yake chini katika miguu ya binti yule viatu hata havikuwa na tone la tope



    Abrah akastaajabu!!!



    "Mbona ujachafuka mguuni?!"



    Akamuuliza safari hii akimwangalia kwa wasiwasi



    "Nimeshushwa katika gari na baba yangu hapa"



    Lile jibu alikumridhisha mtoto yule,akaangalia barabara akitegemea kuona alama za matairi ya gari



    Ayakuonekana!!!....



    Akaamua kupotezea



    "Unaitwa Nani?!"



    Kwa sauti tamu mtoto yule akauliza huku akilitoa begi lake mgongoni



    "Abrah Tuesday"



    "Unajina zuri sana" aka jibu huku akifungua begi lake na kutoa vikopo viwili vya chai na kamfuko ka mandazi,tena yale mandazi ayapendayo Abrah



    Mate ya tamaa yakaanza kumtoka kijana yule binti yule akamtupia kikopo kimoja abrah akakidaka na kukifungua na kuanza kunywa



    "Wewe unaitwa nani?!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Zena bint Kureysh"



    Ghafla Abrah akashtuka baada ya kuskia jina lile....



    Kikopo kile kikamdondoka

    Ni kama jina lile alilisikia mahali!,ila ni sehemu gani kumbukumbu zake zilikataa kabisa kumkumbusha



    Wakabaki wanatazamana



    "Mbona umeshtuka sana Abrah"



    Zena akamuoji kwa sauti ya upole



    Abrah akaona aibu na kutazama pembeni



    Mvua sasa ilikuwa imekatika na kuwapa wasaa watoto wale kuendelea na safari



    Njia nzima Abrah alijihisi mwingi wa amani alipokuwa akimtazama binti yule



    Moyoni mwake alikiri ni binti mrembo,na hakupata kumuona mwanamke Mzuri kama yule katika maisha yake.



    Japo Abrah kiumri alikuwa ni mdogo lakini hilo alikuzuhia hisia Kali za mapenz kujenga kiota ndani ya moyo wake.



    alijikuta akimpenda Zena na kumuitaji kimapenzi



    "Lakini sisi ni bado wadogo Abrah wazazi wakijua?!"



    Zena alijitahidi kupinga



    ",hawawezi kujua na tulivyo wadogo ni vizuri hatuwezi kupata mimba"



    Abrah akazidi kusihi



    "Ok nimekubali"



    Na hatimaye binti yule akakubali hakika abrah akuamini akamkumbatia Zena kwa nguvu na kuanza kummiminia mvua ya mabusu



    Baridi ile ilowatawala ikaondoshwa na joto Kali la miili yao



    Walitembea wakiwa wameshikana mkono mpaka katika shule yao ambapo Zena alimuonesha darasa alilokuwa akisoma



    Kwa kuwa bado hapakuwa na mwanafunzi hata mmoja alowasili waliendelea kukaa pamoja wakipiga stori na hisia zilipowazidi walizipunguza



    Ni wazi penzi la binti yule lilimlevya,dakika chache baadaye wanafunzi walianza kuwa sili na kulazimika Abrah kuelekea darasani kwake wakiahidiana kuonana tena baadaye



    Lakini haikuwa ivyo....



    Baadaye muda wa mapumziko Abrah alijitahidi kumtafuta mwenzake bila mafanikio na hata mchana hali ilikuwa ile ile ikamlazimu kwenda kumuulizia darasani kwao



    Jibu alilopewa hakukuwa na mwanafunzi kama huyo



    Zena Kureysh?!



    Akalikumbuka jina lile ni wapi alipolisikia,ni katika mdomo wa mfalme Zuberi aliyekuwa akihiitaji TOZANI



    Ni katika ile ndoto aliyo ota



    Ni Mara kadhaa kijana yule alilitaja kabla ajamponyoka na kukimbia



    Wasiwasi ukaanza kumvaa



    Mawazo juu ya TOZANI yakamrejea



    Akatabasamu baada ya kugundua kipindi kinachofatia ni kiswahili....



    Ni wazi ange uwasilisha msamiati wa neno lile apate kutambua viumbe vile viliitaji nini!



    'Lazima kuna kitu nyuma ya pazia'



    Akajiwazia akielekea darasani



    Dakika chache mwalimu aliingia,alikuwa ni mwalimu mpole, kwa jina alitambulika kama mwalimu SILVANUS wengi walipenda kumuita mwalimu Silvar mwenyeji wa Moshi mjini



    Baada ya kuweka vitabu vyake katika meza na kuchukua kipande cha chaki na kuanza kuandika ubaoni



    Alifundisha na baadaye aliruhusu maswali,Abrah akanyoosha mkono...



    Mwalimu akamruhusu....



    "Mwalimu ni nini maana ya neno TOZANI?!"



    "TOZANI,?!"



    Mwalimu yule alishtuka macho a kayatoa pima ni wazi akutegemea swali kama lile



    Si mwalimu pekee aloshtuka,



    Hata na baadhi ya wanafunzi pia,wengi wao wakistaajabu jinsi mwalimu yule alivyoshtuka!....



    Na si katika darasa lile viumbe wale walishtuka hata baadhi ya viumbe visivyo onekana vingi vilishtuka na kusimama kusikiliza mwalimu angejibu nini



    KATIKA FALME YA KUZIMU



    Na si duniani tu baada ya Abrah kutaja jina lile viumbe vingi vilitega maskio kusikia mwalimu angejibu nini



    Katika kitanda kilichozungukwa na dhahabu alilalia binti Mrembo



    Zena Kureysh alozungukwa na wasichana wazuri kama yeye wakimpepea



    Wote walikuwa na mabawa



    Hata binti yule pia alishtuka baada ya mtoto yule kutaja jina lile



    "Ooh shit Abrah unafanya nini?!"



    Akapiga kelele,ni wazi maisha ya kijana yule yalikuwa hatarini



    "Jaduuuuuuu"



    Akaita kwa nguvu



    Ghafla kijana mmoja akajitokeza



    "Naitaji ukamuwekee ulinzi mfalme wa badae wa himaya hii"



    Kijana yule akainamisha kichwa ishara ya kukubali....



    Akatoweka.



    Mwalimu akazidi kumkazia macho abrah



    "Ni..nan... Ka..kwa....mbili.a?!"



    Akauliza kwa kigugumizi



    Abrah akaachia tabasamu pana kumuondosha woga mwalimu yuke



    "Hapana ni Mimi mwenyewe nataka kujua"



    "OK nifate ofisini"



    Mwalimu akasema kwa mkato na kuachia miguno kwa wanafunzi



    Akuangaika nao akabeba vitabu vyake na kutoka abrah akimfata nyuma



    Kelele zikazuka darasani





    Abrah alifika katika ofisi ya mwalimu wake yule mwalimu akampa ishara akae,mtoto yule akatii!.



    Kimya cha dakika kadhaa kikachukua hatamu maeneo yale ilhali kila mtu akiwaza lake kichwani!,



    mwalimu kwa dakika zile kadhaa macho yake aliyatambaza katika kitabu chake cha sarufi,lakini ukweli uliodhahiri mawazo hayakuwa katika kitabu kile.



    Mawazo yake yalikuwa mbali,swali aliloulizwa na mwanafunzi wake yule lilimtatiza!



    "kwa nini niumize kichwa hali ya kuwa mwenye majibu yupo mbele yangu?!'



    akawaza



    taratibu akakinyanyua kichwa chake,na kumtazama mtoto yule mdogo!



    "ok! nambie sasa Abrah swali lako!" akauliza kwa Sauti ya utulivu,sauti ya utaratibu



    "ndiyo mwalimu!,nlikuwa nataka kujua maana ya neno tozani." Abrah akaweka tuo,mwalimu yule akaachia tabasamu,kusudi lake amwondoe na kujiondosha hofu ilokuja kwa kasi katika moyo wake



    alifanikiwa



    "hilo neno umelisoma wapi! au umelitoa wapi?"



    Akampachika swali mtoto yule kusudi ajue pa kuanzia!,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "amna mwalimu sijalisoma mahala popote wala sijalitoa mahali!"



    "ok umelijuaje hilo neno?!"



    mwalimu akazidi kumbana,kutokana na akili ya kitoto alokuwa nayo Abrah akaona ili apate jibu ni bora amsimulie mwalimu wake juu ya ile ndoto ya kimaajabu aloiota



    katu akuiona hatari ilokuwa mbele yake!,kwa nje mwalimu Silvar alionekana mwema,ila hakuwa mwema kabisa! ni mmoja wapo wa waanga wa viumbe waloisaka TOZANI ile!



    "usiku nikiwa nimelala,niliota ndoto mbaya sana mwalimu,kuna viumbe sijui madubwasha gani yalikuwa yakinikimbiza na kunlazimisha niwape hiyo tozani"



    "what? uliwapa?!" akauliza yule mwalimu kwa mshangao ilhali alisahau kuwa yule mtoto yule alikuwa hata ajui maana ya neno ilo



    Abrah akapatwa na mshangao!,ndio alishangaa kushtuka kwa mwalimu wake yule kwa vitu vya kufikirika!



    "Sikuwa nayo mwalimu!,na hata siifahamu hiyo tozani yenyewe walokuwa wakiitaka,"



    "kweli uifahamu tozani?!"



    Mwalimu akamuuliza akiwa kamtolea macho makali,...



    Abrah akashangaa tena!



    'huyu mwalimu vipi!,lau kama ningeifahamu au ningekuwa nayo je ningemuuliza?!'



    Abrah akawaza,ni wazi alishaanza kumchukia mwalimu yule



    "kama unayo Abrah tafadhali nipatie nitakupa ela yoyote utakayotaka plz mtoto mzuri!"



    mwalimu akajitahidi kubembeleza



    "kha!!!" Abrah akapatwa ma mfadhaiko,alihisi mwalimu lazima atakuwa anachanganyikiwa kwa namna yoyote ile!



    mwalimu alianz kubadilika! woga,khofu ukamvaa,alitia huruma pindi akimwangalia usoni alionesha kuihitaji zaidi ya kitu chochote tozani ile...



    "mwalimu!" Abrah akaita kwa sauti ya upole



    "Naiomba kama unayo abrah plzzz"



    naona unanchanganya mwalimu lengo langu ni kukifahamu hicho kitu



    "ok pete! tozani ni Pete kama unayo naiomb ntakupa utakacho?"



    "pete?!" abrah akauliza kwa wasiwasi,kwake lilikuwa ni jambo jipya,akuijua wala kuikumbuka pete hiyo ila mwalimu Silvar alikuwa na uhakika abrah anaimiliki pete ile!



    Kwa kigezo cha kwa nini viumbe vile waitake?!



    "ina maana huna pete yoyote nyumbani?" abrah akatingisha kichwa ishara ya kukataa,mwalimu akamruhusu arudi darasani akawaze kwa makini niwapi alipoihifadhi tozani hiyo...



    abrah akuna alichojua.....



    Alijiinamia darasani akiwaza lakini akukumbuka kitu!....



    ****



    5



    Huku nyuma mwalimu alishusha pumzi ndefu!...akaachia tabasamu la kifedhuli!



    "nahisi sasa utajiri upo mbioni!,lazima niimilike tozani,lazima nimmiliki malkia ZENA" kumbukumbu zake akazirudisha nyuma miaka mitano nyuma....



    ILIVYOKUWA



    "Wazazi wangu! siwezi kukubali kirahisi kukaa nyumbani,nilazima mfanye jinsi mnipatie ada niende nikamalizie masomo yangu miaka miwil mmeweza iweje mshindwe huu mwaka mmoja? hapana mama na baba siwey kukubali"



    "mwanangu Silvar!"



    nakuskiliza baba



    "nadhani unajua jinsi gani tumepambana wazazi wako usome! na nadhani unajua wewe ndo tegemeo la kijiji,tumeuza mashamba yetu mawili hili la hapa nyumbani na lile la kule korongoni,kusudi usome!, tumefanya vibarua kufa na kupona katik miaka yako miwil ya awali!, sasa u mwaka ulobakia tumeshindwa kabisa,nguvu zimetuisha hatuna cha kuuza sijui! tutafanyeje?!"



    Aliongea Mzee Servas baba yake Silvar huku akikuna kichwa chake kilichojaa mvi nyeupeee.....



    "itabidi muuze hii nyumba mi nkamalizie masomo yangu!" Silvar akajibu akiwa kakunja sura



    "una wazimu nini?!"



    mama akafoka kwa jazba,mshangao ukigubika uso wake



    "tuuze nyumba nasi tuishi wapi?,mi nilijua mwanetu umesoma utakuwa na akili kumbe afadhal na wenzako walofeli ambao saiv wamejenga na wanamaisha yao kuliko wewe mfyuu"



    akamaliza kwa kusunya mzee yule akanyanyuka na kuondoka!,mama baada ya kuona mume wake kuondoka akamwangalia Silvar kwa dharau! Juu mpaka chini



    "yatakushinda" akatamka maneno hayo naye akaondoka na kumuacha mtoto yule peke yake.....



    Silvar akabaki katika mawazo mazito akaama katika sayari ile!,taratibu machozi yakaanza kumdondoka.....



    Alikuwa ni kijana aliyejitahidi sana katika masomo yake,ndani ya kijiji kile mtoto pekee alofaulu kwenda form one alikuwa ni yeye,tatizo familia yake aikuwa na uwezo ila wakauza shamba moja kwa ajili ya kumsomesha akaenda shule!,baada ya kumaliza form four wazazi wake walikuwa tayari washauza mashamba yao mawili na matokeo yalipotoka silvar alikuwa kafaulu vizuri sana kwenda ' o leval '



    Ila je wazazi wake wangeuza nini wamlipie ada?!



    Taratibu aliisi ndoto zake zikififia,naye akuwa tayari kwa ilo!....



    Alijitahidi kufanya kazi ngumu ila mpaka mwisho wa siku hata robo ya mahitaji akuifikisha



    Taratibu ndoto zake zikaanza kufifia kama kuungua kwa mshumaa,

    Ila moyoni aliuchukia umasikini,na akukubali kuendelea kufanya kazi ngumu akilipwa kidogo



    Wazo Fulani likamjia!



    Aliloliona kuwa ni wazo sahihi kwa wakati huo,

    Kwenda kwa mganga kutafuta utajiri



    Alijiona mjinga wazo hilo kutomjia mapema,hata ada asingeikosa



    Bila kushurutishwa na mtu, bila kushauriwa na mtu akafungua safari kwenda kijiji cha mbali,kwa mganga mashuhuri



    BI Nwalau Nwalau nadhani wengi mnamfahamu bibi huyu



    Na kwa bahati nzuri alipofika jioni jioni ile hakukuta watu wengi akapata wasaa wa kuonana na mganga yule mashughuri....



    "Ha ha ha ha ha Nwalau Nwalau Mzee wa kazi aaaah na jua unataka nini utajiri siyo?!"



    Silva akatingisha kichwa ishara ya kukubali



    "Sema tawileee...."



    "Tawile bibi"



    "Ha!,haaa haaaa usijali hapa umefika mahali pake!"



    Bibi akachukua manyanga na kuanza kupiga akaongea lugha zisizoeleweka,akavunja mayai viza tofauti na matarajio ya Silvar kuwa ingetoka harufu mbaya ndo kwanza ikatokea harufu nzuri....



    Harufu ya marashi ambayo akuisikia kabla ghafla moshi ule ulotoka kwenye chezo ukaanza kuwa mzito ulomfanya silvah aanze kukohoa

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mganga yule akazidi kuongea maneno yasoeleweka na ghafla ubani ukatokea katika kanailoni kidogo mganga yule akauchukua ule ubani na kuufungua katika nailoni lile akaumwagia kidogo katika kichezo kile harufu ile ya marashi akazidi kuzagaaa



    Ghafla akakakamaa,kama kapandwa na degedege mwili ukaanza kumtetemeka,akaanza kucheka.....



    "Zena Kureysh,zena Kureysh,zena Kureysh!"



    akataja jina ilo Mara tatu akinyunyuzia ubani ule katika kichezo kile ambapo moshi wake ulikuwa mzito na harufu Kali ya manukato ikizidi....



    Ghafla taratibu harufu ile ukaanza kupungua na moshi ule kutawanyika na mwisho kabisa ukakata!



    Bibi yule akarudi katika Hall yake ya kawaida



    "Majini yangu yamekubali kukusaidia kukupa utajiri"



    "Asante sana bibi"



    "Na habari nzuri zaidi Zena mtoto wa mfalme wa msitu wa pande mfalme Kureysh ndo atabeba jukumu lako"



    "Tawile bibi"



    "Shika huu ubani usiku kabla ujalala uchomee katika chezo kama hiki unuie unavyotaka Zena Kureysh atakusaidia kukupatia"



    "Na ukiisha huu ubani bibi"



    "Nahisi tayari utakuwa tajiri"



    "Asnte bibi sijui ntakupa Zawadi gani?!"



    "Usijali mjukuu wangu nipo kwa ajili ya msaada kwenu binadamu hivyo ni juu yangu kuwasaidia"



    Silva akampa mkono bibi ishara ya kushukuru na kutaka kunyanyuka kuondoka kabla ajashtushwa na kichwa kikali cha bibi yule ikambidi akae



    "Unataka kwenda wapi na bado atuja maliza tambua ya kwamba majini wana wivu sana utakiwi kuwa na mwanamke mpaka wakuruhusu wenyewe ikiwa awajakupenda ilo ndo sharti kubwa masharti mengine watakupa wao"



    "Ikiwa awajanipenda kivipi bibi?!"



    "Swali zuri sana! Inaeza kutokea zena akakupenda kimapenzi atokuruhusu uwe na mwanamke yoyote ila kama ana mpenzi wake au pengine ajakupenda basi akutokuwa na neno"



    "Kunipenda kimapenzi?!,ina maana niwe mpz wake! Hapana sitokuwa tayari,niwe na jini?!"



    Bibi akacheka....



    "usitake kuaribu dawa Hall ya kuwa bado kabisa,nimekwambia ikitokea akakupenda kwa sababu sijui kama atakupenda au lah ilo mtajuana wenyewe nimekupa tu kama angalizo usije kuwa na mwanamke mpaka akuruhusu yeye"



    "Tawile bibi"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "OK unaweza ukaenda sasa,usiongee na mtu yeyote njiani utakaye kutana naye,.unaweza ukawenda,usiitikie salamu yoyote utakayopewa njiani, unaeza ukaendaaaa,usipeane mkono na MTU yeyote utakayekutana naye,unaweza ukaendaaa nendaaaaaaa na usigewuke nyumaaa nendaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa"



    Silva akatoka,bila kugeuka nyuma



    'Ntamweleza nini Mery wangu anielewe ya kwamba si Mtaki!,mh mpaka jini aniruhusu na je ina maana akinipenda mi na Mery ndo basi tena?!,hapana siwezi nampenda sana Mery"



    Silva alitembea huku mawazo yakikisonga kichwa chake....



    "Silvaaaaaaaaaaaaaaaaa"



    Ghafla sauti nyembamba ya binti Mrembo ikamwita nyuma yake!,sauti TAMU yenye kilafudhi ya mwambao



    Silva akageuka!



    Akuiona kitu,akuiona mtu alomwita



    "Unaweza ukawenda,nenda na usigeuke nyuma pindi ukiitwa"



    Sauti ile ya mganga bi Nwalau Nwalau ikamning'oneza



    Akakumbuka, ni wazi alishavunja sharti akasimama wima pale pale



    Ghafla mkojo ukambana,mkojo ulosababishwa na woga.....



    Akasogea katika shamba na kukojoa alipomaliza akatokezea katika kale ka njia tayari kwa kuendelea na safari



    "Mambo Silva"



    Ghafla akashtuliwa na sauti tamu , sauti ilochujwa ikachujika



    "Mmmh!"



    Silva akaguna baada ya kumuona binti Yule, moyo wake ukaanza kimbelembele kwa kupiga kasia mapigo ya so ya kawaida



    Ulishapenda



    Macho yake yakakiri tangu yapewe Nuru ya kuona hayakuwai kuona kiumbe kizuri kama kile ni wazi macho Yale



    Yalishapenda



    Ubongo wake ulikiri katika kumbukumbu zake ukuwahi kuifadhi au hata kufikiri kummiliki mtoto Mzuri kama yule. ....



    Maskio yake yalikiri tangu yaanze kuskia ayakuwai kusikia sauti TAMU kama ile....



    Silva akabaki amenata



    Akabaki ameganda kama kagandishwa na shoti ya umeme



    Ghafla akagutuka



    "Poa ni nani wewe"



    "Ha ha haaaaa haaaaaaa haaaaa Zena Kureysh haaaaaaaaaaaa uliambiwaje lakini wewe?!"



    Ghafla Dada yule akatoweka.....



    'Mama yangu ni mevunja masharti tena?!'



    Akawaza na kuamua kuutupa ule ubani na kukimbia akuwa na haja tena ya kumuita jini yule aliya kuwa kakosea masharti



    Akajua kwa kufanya vile amepona kumbe alikosea sana!



    Ndo alikuwa kajiingiza kwenye tanuri la mateso!





    Moyo wake tayari ulishagubikwa na woga!,wasiwasi na simanzi tele



    Wakati alipokuwa akikimbia ghafla,akaanza kuskia vicheko tofauti vikipokezana katika ngoma ya maskio yake.



    haaa,haaaaa,haaaaaaaa,haaaaaaaaaaaaa,haaaa

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Silvar akazidi kuchanganyikiwa,tamaa sasa alihisi imemponza!,je angefanyaje kuepukana na vitisho vile?!



    arudi kwa mganga bi Nwalau Nwalau?!,mawazo yake yakapingana akuwa tayari kurudi!.



    Akazidi kusonga kuelekea nyumbani



    Alifanikiwa kufika salama kwao,akaingia chumbani kwake!,alihema kama mtu alokimbia km kadhaa za mraba!,akajitupa kitandani,kutokana na uchovu usingizi ukamchukua muda huo na kumuamisha katika sayari ile...



    *************



    SURA YA PILI



    Mery ni mara ya pili sasa alienda kwa mpz wake Silvar,pasina kumuona akilakiwa na kufuli katika mlango wake



    kwa kuwa waliishi mtaa mmoja!,nyumba zao zilipakana ilo alikumuwia ugumu binti yule kwenda kila dakika chumbani kwa mpz wake yule!,



    'ameenda wapi mpaka sasa ajarudi?!,mbona ajaniaga na si kawaida yake?!,'



    mawazo yakakisakama kichwa chake!, toka asubuhi mida ya saa 5 {tano} mpaka mida ile ya saa 3 (tatu usiku) Silvar wake alikuwa ajaja!



    mbaya zaidi akumuaga!,je alienda wapi? akiipiga simu yake aipatikani?!,mara kadhaa kashampigia mdogo wake Silvar aitwaye Nickson kumuuliza kama amefika nyumbani jibu alilolipata ni hapana kaka ajafika huku!



    ,kila alipojaribu kulala avikulalika!,ghafla usingizi ukamchukua aliposhtuka kitu cha kwanza kukumbuka ni juu ya Silvar,moyo wake ukamsaliti! akatamani kujua kama kasharudi au lah!!!...



    Akajiamsha katika chumba chake na kunyata hadi nje!...



    Moyo wake ukampasuka kwa shangwe!,furaha ikamtawala! usiku ule ule wa manane akatamani kujua mpenz wake yule alikuwa wapi?



    kiherehere kikamponza,akausogelea mlango na kuugonga mara moja "kimya" wazo ajaribu kuusukuma likamjia,naye akalitwii....



    akausukuma mlango ule nao ukamtwiii,akaingia ghafla akayatoa macho pima,pasina kuamini kile akionacho!,



    kwanza akapokelewa na harufu kali ya marashi,harufu tamu!,ndani ya chumba kile kulizungukwa na mishumaa ya rangi tofauti,tofauti!



    akuielewa kabisa hali ile!,macho yake akayaelekeza kitandani kwa mpenz wake! alikuwa amelala tena katika kitanda tofauti na kile alichozoea kukiona chumbani mule,kile kilikuwa cha chuma,tena chuma yenyewe ni ya madini ya silvar kiling'aaa,Mery akabaki ameachama mdomo wazi kwa mshangao!,



    akapiga hatua kadhaa kumsogelea kijana yule,akaupeleka mkono wake katika mwili wake na kuanza kumuamsha Silvar! silvar! silvar



    kimya!



    kijana yule alilala fo! fo! fo!

    taratibu akamuondosha shuka na kukutana na kifua kipana cha mwanaume rijali!



    kifua kilichozungukwa na garden love! pindi alipoipapasa ikampa hamu!,hamu maridhawa,akasahau madhila yote alokumbana nayo,maajabu ambayo si ya kawaida ya chumba kile...



    taratibu akaupeleka mkono wake katika bukta ya kijana yule! msoloboko ulisimama dede tayari kumkabili hadui...



    Silvar akafumbua macho yake,haikuwa mara ya kwanza binti yule kumwingilia chumbani muda wowote hamu ilipomshika!,hisia zilikuwa juu...



    akasahau masharti alopewa akazidi kuyavunja! midomo yao iliungana kama ya njiwa wakibadilishana mate na kuleta Ladha tamu katika midomo yao hiyo!



    wakabiringita Mery akawa juu,silvar chini!,Silvar akiwa chini Mery juu



    Mery macho yalimkwiva!,alilegea aswa aswa!,wakati akiwa anaunyonya mtarimbo ghafla miguno ile ikabadilika!,sauti nzito ilomshtua binti yule,akaacha kwa ghafla na kumtazama mtoaji usoni!



    asalale! sura alokumbana nayo ikamtia wazimu,sura ya kiumbe wa ajabu! akajitoa katika mwili ule tayari kwa kukimbia



    jitu lile likamdaka mkono,mkono wake ulikuwa na miba

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "unaenda wapi mpz wangu?! kwani nini kimetokea" jitu lile likatamka



    Mery akujibu kitu akaukunja mkono wake kidogo na kufanikiwa kutoka katika mikono ya miba



    akawa tayari kuki

    Kukimbia!,ghafla mlango ukajifunga na kupelekea apige breki!



    "haaaaa haaaaaa,haaaaaa"



    ghafla kicheko cha binti kikasikika! alipogeuka nyuma kicheko kilipotokea jitu lile likawa linateremka kwenye kitanda huku likitoa kicheko kile kitamu!



    mkojo bila kutarajia ukamtoka Mery,akuwa na njia yoyote ya kujiokoa!....





    Akabaki hakiwa anatetemeka,mikono kaielekeza mbele kusudi kuzuia jitu lile la kutisha lenye sauti tamu kumfikia!,sauti ilochujwa ikachujika!,



    jitu lile lililokuwa na jicho moja jekundu katikati ya paji lake la uso,manyoya yalokuwa mengi katika mwili

    wake mfano wa nyani,



    katika kichwa chake alikuwa na pembe mbili zilizochongoka kama za mbuzi,kila alipotoa sauti yake ile tamu na kuuacha mdomo wake wazi moto ulionekana ndani ya mdomo ule,na kuzidi kumuogopesha binti yule



    "tokaaa,tokaaaaa,tokaaaaaaaaaaaaaa"



    akapaza sauti na kupelekea sauti yake ile kali iumize maskio yake,ghafla mlango ukafunguka,Mery akatoka spidi mpaka chumbani mwake!



    Akazama!



    ghafla macho yake yakadondokea kitandani,akapokelewa na sura ya binti mrembo aliyekaa katika kitanda chake,



    kilekile kama cha kule kwa mpz wake,kitanda cha chuma madini ya silva,akukumbuka kama alishawah kumuona achilia mbali kuishi na binti mrembo kama yule!



    binti alimwangalia kwa tabasamu zuri lililomzidishia urembo! mara dufu ya ule alokuwa nao! tabasamu la kumtoa khofu



    hapana! pamoja na tabasamu hilo khofu aikumwondoka ndo kwanza akageuka akiwa na dhumuni la kukimbia kutoka nje



    kicheko kikali,kikafatia,kicheko cha kumdhihaki,kabla ajaufikia mlango akaushughudia ukijifunga

    kama ulivyojifunga wakati akiwa chumbani kwa Silvar,alitetemeka,taratibu kwa uwoga akawa akiikunja shingo yake kugeuka nyuma,kuangalia pale kicheko kile kilipotokea



    ahmad! ana kwa ana na jitu,jitu lile la kutisha pembeni ya mdomo akiwa anachurizika damu

    sasa sauti yake ilibadilika na kuwa nene



    "unataka kunikimbia sio?" kwa sauti kali tena nzito jitu likauliza huku likishuka kitandan na kuanza kumfata Mery pale alipo!,



    kama kawaida yake Mery akanyoosha mkono kusudi amzuie!,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alijidanganya,



    ghafla akaanza kuhisi kitu kikimkaba kooni,pumzi ikawa ikimtoka kwa shida,jitu lile likawa linacheka,



    sauti tofauti tofauti zikakisumbua kichwa chake,kukabwa kwake kule kukazidi,pumzi ikawa ya shida,nguvu zikaanza kumuisha!



    ghafla akaporomoka chini na kuanza kutapatapa



    akatulia!



    tayari alishakata roho!,jitu lile likaachia kicheko na kutoweka!,baada ya kutoweka chumba kile kitanda kile kikarudi katika hali yake ya kawaida!



    mwili ule wa mery akiwa kayatoa macho kwa mshangao,ulimi kaung'atia kwa uchungu wa mauti,ulilala pembeni bila uhai!



    ILIVYOKUWA MASAA KADHAA NYUMA:



    Silvar akiwa kalala fo! fo! fo! pasina ufahamu wa aina yeyote ghafla hali ya chumbani mule ikabadilika!



    alikuwa ndani ya chumba kizuri chenye manukato yalizozipendezesha pua zake!,alilalia kitanda ambacho kwa uzuri wake akuwah kukiona kabla,



    alivaa nguo nzuri ambazo hakuwa na kumbukumbu nzuri kama alishavaaga nguo kama zile achia mbali kuzimiliki,



    pembeni ya alipolala,alikwepo binti mzuri,ambaye akukumbuka kama alishawah kumuona hapo awali!



    binti yule alimlalia kifua chake,



    "silvar!..."



    kijana yule akuitika zaidi ya kumwangalia binti yule mwenye urembo wa pekee katika macho yake!



    "wewe ni kijana mzuri!,nimetokea kukupenda ndo maana mpaka sasa upo hai na baada ya kuvunja masharti adhabu yako ilikuwa nikuuwe skuweza kufanya hvyo kwa kuwa nakupenda,nipo tayari kukupa utajiri ikiwa utakubali kuwa na mimi!...



    "lakini mimi na mpz!."



    ssssh! binti yule akamzuhia na kupeleka mkono wake katika kifua na kuanza kukipapasa! hisia zikaanza kumpanda silvar



    Ghafla kabla ajafanya kitu,akashtuka,...



    Baada ya kushtuka,akashtuka kumkuta mtu yupo pembeni yake akikipapasa taratibu kifua chake!



    Alikuwa ni Mery!



    Kwa kuwa tayari hisia zake zilisha panda,akaendelea akisahau kuwa kwa kufanya vile anaendelea kuvunja masharti!



    Ghafla Mery akagutuka!



    Ni baada ya sura ya Silvar kubadilika,silvar akashangaa kumuona mpz wake akimwangalia kwa macho ya woga yalochanganyikana na mshangao!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla akamshughudia akikimbia...



    Ghafla akapiga breki!,ni baada ya kushughudia kujifunga kwa mlango....



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog