Search This Blog

CHOZI LA UKOMBOZI - 2

 







    Simulizi : Chozi La Ukombozi

    Sehemu Ya Pili (2)



    alionekana komba akimtaza mkuu wa jeshi la ghemi kwa hasira......huku nguo zake zimetapakaa damu utadhani kamwagiwa damu hiyo.... kisha akaamuru jeshi lake lirudi ghemi.. punde walipanda farasi wao na kondoka zao....



    **********



    ule upande mwingine alionekana Mazy akiongea na mfalme wa Beha """"walikuwa wakipanga mpango wa kuvamia Ghemi kwa kupitia milango ya siri kwa sababu wameshindwa kuvuka mpaka na kuingia ndani ya falme ya ghemi kwa kuzidiwa mbinu za upiganaji....Mazy alikuwa anaijua vyema milango yote ya siri... kwa sababu ni mtoto wa mfalme wa ghemi na ameishi kwenye jengo hilo la kifalme tangu kizaliwa kwake mapaka sikuile anatoroka..



    *********

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kule upande wa falme ya ghemi.... mfalme alimpongeza sana komba kwa kulipanga vyema jeshi lake na kutoa mbinu za upiganaji mpaka wakashinda vita.....wakati huo wote mfalme alimuangalia komba kwa macho ya mshangao...kisha akasema hakika tumepata mkombozi najivunia sana kuwa na jeshi imara...



    **************



    Maisha yaliendelea komba aliishi vyema na alikuwa akipewa heshma kubwa Ghemi... Prince mody alikuwa karibu sana na komba alikuwa akimdadisi kuhusu chimbuko lake......komba hakutaka kuongea chochote alidanganya kuwa yeye ni mzaliwa wa kisiwa cha Dhaho. na wazazi wake waliuwawa na jeshi la Falme ya Beha miaka mingi iliyopita.. .....



    siku moja komba akiwa katika matembezi alikutana na binti mmoja aitwae SIAM....komba alivutiwa sana na binti yule... aliamua kumtongoza hata Siam alivitiwa sana na komba kutokana kuwa na rangi nzuri ya kahawia kwasababu alikuwa ni mchanganyiko wa kiafrika na kiarabu.... siam alikubali ombi la komba.... wakaanzisha mahusiano....kumbe siam alikuwa akitumiwa na mfalme wa Beha kuchunguza mambo yanayoendelea katika falme ya Ghemi...



    Komba alizama kwenye penzi la Siam""" muda wote alikuwa akimfikiria siam...siku moja komba alimwambia siam kuwa anampango wa kumuoa.. siam alifurahi sana kwa sababu alijua hiyo ndio nafasi pekee ya kuingia ndani kabisa kunako Ngome ya falme ya Ghemi...siam alikubali bila kupinga...



    *********



    ule upande mwingine... mfalme wa Beha aliendelea kuandaa mpango wake wa kuivamia Ghemi kwa kupitia milango ya siri...Mazy alionekana kuwa na chuki kubwa juu ya utawala wa baba yake mfalme wa Ghemi.....Mazy alitoka nje na kuelekea upande wa uwanja wa mazoezi""uwanja huo ulitumika kwa jeshi la beha kufanya mazoezi kila siku.... lakini siku ya leo zoezi lilibadilika...... mazy alitoa Amri kuwa itabidi wafanye zoezi la kufa au kupona.....ili Apate jeshi imara... wanajeshi walikaa tayari na zoezi likaanza.... kila mmoja anatakiwa ampige mwenzake mpaka amuuwe.....ili kujitetea inabidi upambane kwa umakini mkubwa... na baada ya masaa matatu zoezi lilikwisha.... kwahiyo wale waliobaki hai... ndio jeshi alilokuwa analitaka Mazy.. wanajeshi walionekana kutapakaaa damu huku wengi wao walionekana kujeruhiwa kwa mapanga.... mazy alitabasamu ishara ya kufurahishwa na mazoezi ya siku hiyo... kisha akaamuru jeshi litawanyike kila mtu aende kwenye shughuli zake..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********



    kule upande wa falme ya Ghemi... komba naye alikuwa akiliandaa jeshi lake kwa kutoa mbinu za upiganaji wa vita......wanajeshi walimpenda sana komba kwa sababu alikuwa mkarimu sana.... aliwafundisha mbinu mbalimbali bila ubaguzi hivyo walimsikiliza na kufanya mazoezi kwa kujituma... ili kupigania nchi yao.



    Siku iliyofuata komba alichukua farasi wake na kutoka nje ya jengo la kifalme... alikwenda nyumbani kwa siam....lakini alipofika hakumkuta siam.... ilibidi komba abaki hapo akimsubiri siam.



    *******



    ule upande mwingine alionekana mwanamke akiingia kwenye lango kuu la falme ya Beha... mwanamke yule alifunguliwa mlango na kwenda moja kwa moja mpaka kwa mfalme wa beha.. kisha akasema mkuu wa jeshi la Ghemi atakuja nyumbani kwetu hivyo....agiza wanajeshi waende kumnasa...kumbe alikuwa ni yule mwanamke aliyependwa na komba... alisema hivyo" kisha siam akatoka na kuondoka zake.....

    komba alionekana kumsubiri siam yapata masaa matatu yamepita... hivyo komba alikata tamaa kisha akapanda farasi na kuondoka zake...... wakati komba anaondoka... ndio muda huo huo siam alikuwa anafika nyumbani kwake.....lakini hakujua kuwa komba alikuwepo hapo dakika chache zilizopita... siam alisubiri bils kuona dalili za komba kuja nyumbani kwake.... baada ya lisaa limoja kupita wanajeshi wa beha waliizunguka nyumba ya siam"" waliamini komba atakuwa ndani... walivamia ghafla lakini hawakumuona komba..... Mkuu wa jeshi la beha ambae ni Mazy alichukia sana alihisi siam kawadanganya""" kwasababu kamdanganya Mtuku mfalme inabidi siam achinjwe..... alisema mazy huku uso wake ukionekana kuwa na jazba... alishuka kutoka kwenye farasi....wakati anashuka alidondosha mkufu...bila yeye kujua....kisha akazipiga hatua kumfuata siam.... siam aliogopa sana kisha mazy alitoa upanga na kuifyekelea mbali shingo ya siam... damu nyingi ziliruka kutoka mishipa ya damu ya shingoni mwa siam alidondoka chini na kuiaga dunia.... kisha mazy na keshi lake wakaondoka.......kumbe wakati huo huo komba alikuwa njiani anarudi nyumbani kwa siam"" alipofika kwa mbali aliona mwanamke kalala chini huku maiti yake ikiwa haina kichwa!!!! komba alipoisogelea maiti ile aligundua kuwa ni siam... komba alisikitika sana"ghafla aliuuona mkufu ukiwa chini aliuokota na kuutazama aligundua ni mkufu wa mazy aliuona shingoni kwa mazy siku ile walipokuwa wakipigana vita.... komba alikasirika sana.... lazima itailipa damu hii" komba alijisemea moyoni kisha akaondoka na mkufu ule.... kabla hajafika mbali mara ghafla.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kabla hajafika mbali alihisi anafuatwa kwa nyuma....alipogeuka aliona wanajeshi wa tano wa jeshi la BEHA..... wakimfuata huku wakiwa juu ya farasi.... komba aliamua kupita njia za mstuni.... akashuka kwenye farasi wake..akavuta kamba na kumfunha farasi kwenye mti... kisha akachukua upinde na mishale akakimbia hatua kama saba hivi"" kisha akapanda juu ya mti... punde wanajeshi wale waliingia kwenye msitu huo koma aliwaona kwa mbali akachukua upinde na mshale akauweka mshale kunako upinde akauvuta baraabara alipoachia mshale ule ulikwenda moja kwa moja

    mpaka kifuani mwa mwanajeshi mmoja... akadondoka.... mwanajeshi wa pili pia alipigwa mshale akadondoka na mwanajeshi wa tatu pia alipigwa mshale akadondoka.... wale wanajeshi wawili waliogopa kuona wenzao watatu wameuwawa na mtu aliyekuwa akirusha mishale hiyo hakuonekana... waliamua kugeuza na kutimua mbio kurudi walipotoka.....komba ilishuka kutoka juu ya mti na kupanda farasi wake akaondoka... alikwenda moja kwa moja mpaka ghemi..



    ***********



    ule upande mwingine wale wanajeshi wawili waliobaki walionekana wakiingia katika lango kuu la falme ya beha... Walipitiliza moja kwa moja mpaka kwa mfalme kisha wakaeleza kilichowatokea huko porini.... mfalme alichukia sana...



    ***********



    ule upande mwingine alionekana komba akiingia ndani kwake katika ngome ya kifalme.......prince mody alimfuata komba.... akawa anampeleleza juu ya maisha yake... prince mody aliamua kumpa upanga wenye thamani kubwa..... upanga huo hutumiwa na watoto wa wafalme pekee....komba aliupokea upanga huo kwa heshma....



    ********BAADA YA MIAKA MITANO KUPITA******

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    maisha yaliendelea.....amani ilitawala katika falme ya Ghemi... sikumoja usiku jeshi la falme ya beha lilivamia Ghemi majira ya usiku wa manane.....kwa kupitia milango ya siri"" komba alistua akahisi wamevamiwa"" akaamua kutoka akapanda upande wa juu.. kwa mbali aliona kundi kubwa la watu wakiwa wameshikilia miale ya moto...komba alijua wazi kuwa muda si mrevfu wanavamiwa... alitimua mbio kurudi upande wa chini akatoa taarifa punde jdshi lake lilijipanga likawa tayari kwa mapambano.... punde ilianza kurushwa mishale kama mvua.... ghafla jeshi la beha likavamia ndani kabisa... vita ikaanza......walipigana mpaka kukakucha.....wanajeshi wa jeshi la falme ya beha waliuwa kwa wingi.... mnamo majira ya saa mbili asubuhi wanajeshi wa beha wachache waliosalia walijisalimisha na kuweka panga zao chini...komba aliamuru....jeshi lake liende kuvamia ngome ya falme ya beha na kumteka mfalme.... baada ya masaa kadhaa mfalme wa beha aliletwa..... kisha mfalme wa ghemi aliamuru auwawe.... mfalme wa beha alichinjwa hadharani na kupoteza maisha...... mfalme alimpa pongezi nyingi komba..



    *************



    baada ya ya miezi mitano kupita maisha yaliendelea Prince mody alikuwa na mchumba aitwae Rubi... baada ya nino kutoswa baharini... prince mody alilazimika kutafuta mchumba kwa kukata tamaa ya kumuona tena Nino kwani aliamini nino alikufa maji alipotoswa baharini huku akiwa na mimba ya miezi tisa.

    rubi alianza kuvutiwa na komba alihisi kumpenda kimapenzi.... akaanza kuwa karibu na komba..... alimfata komba mara kwa mara kila alipokuwa akimuona.

    kitendo kile kilimfanya prince mody awe na wasiwasi kuhusu ukaribu wa rubi na komba..... siku moja rubi alimsihi komba waende kutembea maeneo ya baharini...komba alikubali....wakaenda prince mody alimtafuta rubi bila mafanikio... alipojaribu kuulizia aliambiwa kuwa ametoka na komba na kuelekea maeneo ya baharini kutembea... prince mody alianza kuingiwa wivu... alihisi kuanza kumchukia komba...... bila kujua kuwa komba ni mtoto wake wa damu...



    punde komba na Rubi walirudi....pnce mody hakuonesha wazi kama anahisi wivu juu ya mchumba wake kuwa karibu na komba..... alimfata komba na kumuuliza yaonekana mlikwendambali!!!! vipi matembezi???? komba alijibu bila wasiwasi kwa sababu aliamini hakuna kitu cha siri kinachoendelea kati yake na Rubi.... kisha prince mody alimwambia komba waende kufanya mazoezi kwa kutumia upanga.... komba alifurahi kwa sababu huwa anapenda kufanya mazoezi hayo mara kwa mara.... walizipiga hatua kuelekea uwanja wa mazoezi..... kila mmoja alichomoa upanga na mazoezi yalianza..... wakiwa wanafanya mazoezi komba alistahajabu baada ya kuona prince mody anapambana kiukweli kama anapigana na adui....mara ghafla prnce mody alimkata komba na upanga kwenye bega..... komba alichukia sana kwa sababu alikuwa ni hodari wa kupambana kwa kutumia upanga.... komba alizuia mashambulizi ya prince mody kwa kupangua mashambulizi kwa kutumia upanha wake..... kisha aka inama na kurusha teke aina ya PARANAWEE kisha akaachia mtama aina ya MKUCHU.. mtama huo ulimrusha prince mody kimo cha mbuzi.... akadondoka chini na kuangukia kisogo.... alihisi maumivu makali.. alinyanyuka kwa hasira akakimbia na kuchukua upinde na mshale.... kumbe wakati wanafanya mapambano hayo... mfalme alikuwa akishuhudia yote yanayotendeka... alipo ona prince mody anachukua upinde na mshale mfalme aliamuru prince mody aache..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ***************



    ule upande mwingine alionekana Mazy akiendelea kuimarisha jeshi lake jipya"""""ni baada ya mfalme wa beha kutekwa na kuuwawa...mazy aliamua kuchukua nafasi ya mfalme wa beha...



    kule ghemi price mody alichukia akatupa chini ule upinde na mshale akazipiga hatua za harakahataka kuelekea ndani ya jumba la kifalme....

    Rubi alizipiga hatua kuelekea kule komba alipokuwa amesimama.... alipomkaribia komba....rubi alichukua kitambaa na kuanza kumfuta damu komba... kwenye bega... pale kwenye jeraha alilojeruhiwa na upanga..... kumbe princr mody alikuwa akishuhudia hayo yote... kwa kupitia dirisha la chumba chake.... roho ilimuuma sana alijua wazi kuwa komba na rubi watakuwa ma mahusiano ya kimapenzi.....



    **************



    ilipofika majira ya usiku prince mody aliamka na kumfata komba.... ili amdadisi juu ya ukaribu wake na rubi... komba alicheka kisha akasema rubi amekuwa mtu muhimu sana katika maisha yangu ni rafiki yangu tu... amekuwa akinifariji na kunipa moyo...... prince mody alinyanyuka bila kuongea chochote akaondoka zake... roho ilimuuma sana....yani rubi hajawahi kuonesha ukaribu wa namna hii lakini nastahajabu amekuwa karibu sana na komba kuliko mimi mchumba wake""""alijisemea moyoni prince mody""" alizipiga hatua na kuingia ndani kwake... punde rubi alikuja..... mbona kama hauko sawa kifikra??? rubi aliuliza"""

    prince mody hakujibu kitu.... rubi alipo ona kimya aliamua kutoka nje.... alizipiga hatua za harakaharaka..... baada ya sekunde kadhaa prince mody alitoka nje ili amuite rubi...alistahajabu kumuona rubi akielekea kule alipokuwepo komba... prince mody alichukia sana hasira zilimjaa....akarudi ndani kwake... kisha akachukua upanga wake na kutoka nje....



    Alipokwenda kwa huku akiwa na hasira""alipofika eneo lile alilokuwa amesimama Komba na Rubi hakuwaona......hasira zilizidi kumjaa aliamua kwenda kwenye nyumba ya komba....lakini hakuwaona alipogeuza shingo alimuona rubi akizipiga hatua kuelekea nyumbani kwao....prince mody aliamua kumfuata rubi...alipomkaribia alimuita...rubi alisimama kisha akageuka na kumtazama prince mody....prince mody aliongea kwa hasira"" ulikuwa unaongea nini na komba??? rubi alistahajabu kumuona prince mody akiongea kwa kumfokea kwani hakuwahi kumuona hata sikumoja akimfokea""" rubi aliingiwa na uwoga akamtazama prince mody kwa macho ya wasiwasi""" huku akizipiga hatua kurudi nyuma....ghafla.....prince mody alianza kuongea sauti ya upole...kwa sababu alimpenda sana ruby.....lakini muda wote guo rubi alikuwa kimya hakumjibu kitu....... kisha rubi aliamua kuondoka huku akizipiga hatua za haraka haraka......

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **********



    kumbe komba aliona yale yote yaliyikuwa yakitendeka...alisikitika sana kwanini prince mody anamuhisi vibaya kuwa anamahusiano na kimapenzi na mchumba wake.......komba aliamua kuzipiga hatua na kuelekea ndani kwake...



    *************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog