Search This Blog

TOZANI ( PETE YA AJABU) - 2

 







    Simulizi : Tozani (Pete Ya Ajabu)

    Sehemu Ya Pili (2)





    Lakini silvar akuona lile,alishughudia mpz wake akiishika shingo yake kwa maumivu makali....



    Ghafla akatulia ishara kuwa amekata roho



    Ni kweli alikuwa amekata roho!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Silvar alichanganyikiwa akabaki ameutumbulia ule mwili macho katika hali ya sintofahamu



    Kwa wasiwasi alokuwa nao hata kicheko kile kitamu akukisikia...



    Mabadiliko juu ya chumba chake pia akuyaona



    Ni vipi atawaeleza wazazi wa Mery wamuelewe?!



    Lazima angefungwa....



    Akausogelea ule mwili na kuanza kuutingisha machozi yakimtoka akiita kwa hisia



    "Mery!....Mery....amka mpz wangu Mery...Mery.....meeeeeeerryyyyyyyyyyy"



    Akapaza sauti yake kwa nguvu pasina kujali majirani hususani wazazi wa binti watasikia



    Ghafla akapigwa kibao kikali!,kilicho mfanya apepesuke na aufunge mdomo wake muda ule ule....

    ....



    Kicheko kikali kikafatia!,....



    " huyo ni memwangamiza kwa sababu kuu mbili"



    Akasikia sauti laini ya binti yule,ambaye kwa sasa alimchukulia kama aduhi yake,akageuza shingo kila upande kumwangalia mmiliki halali wa sauti ile bila mafanikio....



    "Sababu ya kwanza ni kwa ajili yako ni Mara ngapi nimekwambia juu ya uvunjaji wa masharti uwe makini?! Sasa kitendo chako cha kutaka kufanya mapenzi na huyu ni kinyume na masharti ulopewa adhabu yake ndo umepoteza maisha ya mwenzako..."



    "Lakini Mimi sitaki tena utajiri nirudishieni mpz wangu"



    "Haaaaaa haaaaaaa haaaaaaa haaaaaaa,haaaaaaa



    Kamwe aitotokea na utoruhusiwa kuwa na mwanamke yoyote mpaka pale tutakapo kuruhusu na tofauti na hapo kila utakaye kuwa naye kabla amjanisaliti kitamkuta kama kilichomkuta huyu haaaaaaaa"



    Ghafla jini yule akajitokeza katika pembe ya chumba kile



    Uzuri wake ulikuwa maradufu,alikuwa kavaa nguo kama wavaazo jamii ya wahindi,akawa akitembea kwa madoido,akitoa sauti ndogo ya kubembeleza tofauti na ile ya awali kabla ya kuonekana ya kukemea na kulazimisha...



    " u mwanaume Mzuri sana,kwa nini unsaliti hali ya kuwa nshakwambia wazi ya kuwa na kupenda?! Nifanyeje uamini hili"



    "Mi sikupendi tena na ushindwe katika jina la yesu pepo mchafu......



    Ghafla akaskia yowe,hakika binti yule alikuwa katika maumivu makali

    Kwa nguvu chache alizobaki nazo akajitahidi kutoweka



    Akafanikiwa



    " umenifukuza kwa kuwa nimekueleza hisia zangu!,umenifukuza kwa kuwa umeugundua udhaifu wangu kwako!,umenifukuza kwa kuwa sina thamani ndani ya moyo wako!.....



    Kumbe nilikosea pindi nilipotakiwa nikuuwe ulipovunja masharti?!



    Ni kawasaliti na wazazi wangu juu ya mtoto wa mfalme wa majini alonipenda kwa ajili ulisha uiba moyo wangu?!



    Binadamu?! Binadamu wa kuniliza mim!



    Ghafla kilio kidogo kikafatia,kilio cha uchungu



    Hakika binti yule wa kijini alikuwa katika mateso makali,ghafla akashindwa kuzizuhia hisia zake sauti yake taratibu ikaanza kubadilika na kuwa Nene....



    "Sasa kwa kuwa umeamua kuniweka kwenye mateso utaubeba huo msalaba wa huo mwili hapo wew ndo utaonekana muuaji na utanyongwa kama si kufungwa kifungo cha maisha kwa heri"



    Baada ya maneno Yale kimya kikafuata,harufu ile Kali ya marashi ikatoweka na kumuacha Silvar katika Uhuru alouhitaji



    Akasonya! Kwa dharau,akawaza kwa dakika kadhaa na kupata wazo aubebe ule mwili na kuupeleka chumbani kwake kusudi aukwepe msala ule



    Ndio akuwaza Mara mbili,katikati ya usiku ule akaunyanyua mwili ule na kutoka nao nje katu akujua kama ile ni kiini macho na mwili asili upo huko anapoelekea alitembea kwa uangalifu mpaka chumba cha Mery akausukuma mlango ukamtwii na kufunguka akaingia



    Ahmadi mshtuko aloupata ilibakia kidogo roho ichomoke,ila bahati nzuri siku yake ilikuwa bado



    Ni pale alipouona mwili mwingine ukiwa chini,kwa wahka akauachia mwili ule ukaporomoka...



    Ghafla akalakiwa na kicheko cha dhihaka,akabaki ameganda kama sanamu la Michelin



    Macho yake yakawa yakiitazama miili ile kwa wasiwasi na woga tele,nguo walizovaa zilifanana,kifo walichokufa kilifanana kwani wote walitoa ndimi zao nje



    Akili ilipomkaa fresh akakumbuka kukimbia



    Kurudi ndani ya chumba chake,akanyanyuka na kuufata mlango akaufungua na kutoka mbio mpaka katika chumba chake akafungua mlango



    Heeee mwili ule aloubeba dakika kadhaa na kuupeleka katika chumba chake,ulikuwa pale pale!



    Nani kaurudisha?!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakukuwa na jibu la moja kwa moja



    Silva alichoka,akajitupa chini kama furushi au gunia



    Uchungu ukamshika na kuachia kilio!



    Ni wazi sasa alielekea kuumbuka



    Macho yake yakadondokea katika saa ilokwepo ukutani



    Mishale ya saa ile ilihesabu kwa makini kutopoteza majira yake



    Mshale mdogo ulikuwa kwenye mbili na mkubwa ulikuwa Mbele ya kumi na mbili katika vimistari viwili ikiwa na maana saa nane na dakika mbili



    Hakuwa na shaka kuwa siku hiyo lazima akeshe,wazo Fulani likamjia harudi ndani akacheki ile miili



    Je ataukuta mmoja! au itakuwaje?!



    Akatoka na kuelekea chumbani kwa Mery akaufata mlango ajabu aliukuta umefungwa kwa ndani,Silvar akazidi kuchanganyikiwa....



    Akajaribu kuusukuma bila mafanikio



    'Ni nani kaufunga?!'



    Swali hilo likakitekenyua kichwa chake,lakini hakuwa na jibu sahihi



    Muda ulizidi kwenda,na ilikuwa lazima afanye maamuzi yaliyo sahii



    'Nenda kaufukie huo mwili'



    Wazo hilo likapita katika kichwa chake naye hakuwa mtu wa kudharau akifikiriacho



    Akajigeuza na kurejea chumbani mwake,



    Ule mwili ulikuwa pale pale,akaubeba na kuuweka begani akaushikilia kwa mkono mmoja na mkono mwingine akashika jembe na kutoka nao nje....



    Alipoelekea hapakuwa mbali na nyumbani akaubwaga chini mwili ule na kuanza kuchimba



    Ardhi aikuwa ngumu,Aikumpa tabu kufanya uchimbaji ule



    Akafanikiwa kuchimba shimo la wastani kama alilohitaji



    Akausweka ule mwili ndani yake na kuufukia....



    Baada ya kumaliza kitendo kile akajirejesha chumbani kwake,alionekana wazi kuchoka kimwili na kimawazo pia....



    Akafungua mlango wake,macho yake yalichungulia ndani



    Akakumbana na mwili ule....



    Alishindwa kujizuia kutetemeka,akasita kuingia akabaki kaukodolea macho mwili ule kwa mshangao...



    Meno mdomoni yaligongana



    Wasiwasi ulimvaa



    Alitetemeka 'ni nani wa kunsaidia katika mtihani huu'



    Akajiuliza swali!



    Ghafla akamkumbuka Zena!



    Zena Kureysh



    Yeye ndo alikuwa msaada ulobakia



    Ila alimkosea ni vipi angemsaidia?!,ila akajipa moyo



    'Lazima aonane naye'



    Moyo wake ukamuagiza , na hapo ndipo alipomkumbuka mganga Nwalau Nwalau, akakumbuka ubani alopewa wa kumwita binti yule pindi akimuhitaji



    Kwa kuwa bado palikuwa apajapambazuka akaitoa baiskeli yake na kuipanda



    Akakanyaga "pedo" kwa kuchanganya



    Baiskeli ikawa ikikimbia,taa ilimmulikia njia mpaka eneo aliotupa ubani ule



    Akaanza kuutafuta



    Akautafuta bila mafanikio,mpaka akakata tamaa ile anageuka kuondoka Mara akauona....



    Akaachia tabasamu la furaha,tabasamu la faraja akakasogelea kamfuko kale tayari kwa kukachukua



    "Silvar!"



    Akashtushwa na sauti tamu,sauti ambayo aikuwa geni katika masikio yake



    Akasita kuiokota na kugeuka nyuma



    Ana kwa ana na mwanamke Yule alotunukiwa zaidi ya urembo



    Zena Kureysh



    Tena akimtazama kwa tabasamu zuri lililomuongezea uzuri,



    "Una haja ya kutumia tena hiyo,tambua kila ukifikiriacho Mimi nakijua,hivyo pindi ukiniitaji ntakuja baada ya kuyasoma mawazo yako"



    Silvar akashtuka....



    Ila akaachia tabasamu la faraja



    "Na unachokiitaji pia nakijua!"



    Zena akawa akimsogelea Silvar mpaka akamfikia,bado kijana yule alitetemeka yamkini bado alimuogopa



    "Usiniogope mpz Mimi nipo tayari kukusaidia ikiwa utakubali kuwa na Mimi tofauti na ivyo wewe ndo utabainika ndo muuaji na utauliwa na wanakijiji kama si kunyongwa na serikali"



    Silvar akashtuka kuskia kauli ile!,zena aliongea ukweli , na alijua asipokuwa makini maisha yake yatakuw hatarini



    Akawa kimya,hakuwa na cha kujibu



    "Twende kwako ntakusaidia"



    Zena akaongea na kumpa mkono,Silvar akaupokea....



    "Naomba fumba macho yako nikikwambia fumbua ufumbue wekea mkono baiskeli yako pia"



    Silvar akafanya kama alivyoambiwa



    Wakatoweka



    Sekunde ile ile wakatokea chumbani kwa kijana yule,



    Zena akauangalia mwili ule na kuachia kicheko cha kejeli!,akaunyooshea mkono ghafla ukapigwa na shoti



    Ukatoweka!!!!



    Silvar akashtuka kuona kitendo kile



    Akazidi kutetemeka!....



    "Kazi moja tushamaliza,nimekusaidia ila nawe naomba unsaidie nakupenda silvar"



    Zena macho yalikuwa mekundu,hisia zilimbana



    Aliitaji tiba



    Silvar alilijua hilo,ila aliogopa



    Afanye mapenzi na jini?!



    Kiumbe kisicho na asili ya binadamu



    Hapana!!!



    Akuwa tayari,hata hisia zilikaa kando,hofu, woga ukimtawala



    "usiniogope silvar nipe hata kiduchu"



    Zena Kureysh akazidi kusisitiza akimsogelea silvar



    Silvar kutokana na wasiwasi akuweza kuzuia mkojo kumtoka



    Akujua ni sa ngapi ulimbana,na wala hakuwa na taharifa kuwa ulimtoka



    Ghafla alishangaa kumuona zena kabadilika,kakunja sura ghafla na kumwangalia kwa hasira katika maungo yake



    Alipopeleka mkono akaulowanisha



    Kumbe alijikojolea!...



    Wakabaki wakiangaliana kabla ajashtushwa na kibao kikali kilichotuwa katika shavu lake



    Wakati akilishika shavu la pili nako likaadhibiwa kwa kibao kile kile



    Maumivu yakasambaa katika mashavu yake....



    Mbele Zena Hakuonekana.....

    Kitu ambacho kijana yule akukijua ni kuwa majini kitu ambacho awakupatana nacho ni mkojo!



    Najisi!!!



    Najisi yoyote kwao ilikuwa ni zaidi ya uchafu



    Baada ya Silvar kujikojolea kwa uwoga kitendo kile kilimkasirisha sana binti yule



    Alishindwa kuzizuhia hasira zake kutokumuadhibu kijana yule



    Hamu yote aliyekuwa nayo ikayeyuka....



    Kipigo kile alichopigwa Silvar kilimfanya apanue mdomo wake kutaka kuachia yowe



    Mdomo ukashindwa kufunguka,ni kama alikuwa bubu....



    Kicheko kikali kikasikika na ghafla akaanza kukabwa kwa nguvu,alipaliwa lakini kukohoa pia alishindwa



    Ni wazi alianza kuziona nyota nyota zikielea katika macho yake



    Pumzi zikaanza kukata,akawa akipumua kwa shida



    Miguu akaanza kuitupa tupa,kama vile anatapatapa sasa SILVAR alikiona kifo waziwazi

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara ghafla akazinduka!....



    Kumbe Ilikuwa ndoto?!



    Kivipi?!,mwili wote uliloana kwa jasho



    Akapokelewa na mwanga mkali ulozagaa chumbani kwake kubainisha mapambazuko!....



    Akapekecha macho yake



    Ni ndoto au kweli?!,akajiuliza lakini akuwa na jibu sahii



    Kitandani paliloana,ishara kwamba ni kweli alijikojolea



    Lakini kutokana na heka heka za ndoto ile tata kulikuwa na uwezo wa kujisaidia pale



    Ina maana alilala sangapi?!



    Hapana akulala,toka alipotoka kwa mganga anakumbuka jinsi alivyosumbuliwa na jini yule alomtambua kama Zena



    Ndio!!! Zena Kureysh



    Aliporudi jinsi mpz wake MERRY alipomkuta chumbani



    Akaitaji kulala naye



    Kisha?!....



    Akafa katika mazingira ya kutatanisha



    Ndio!,hata alipojaribu kumrudisha chumbani kwake kukwepa msala



    Aliukuta mwili ule ndani ukiwa umelala na alipo uweka mwili ule alokuwa nao na kurudi kwake alistaajabu kuukuta ndani!



    Aliporudi Mara ya pili akakuta mlango umejifunga kabla ajaamua kwenda kuufukia



    Ila aliporudi nyumbani chumbani kwake aliukuta



    Ina maana mauza uza Yale yote yalikuwa ndoto,?!



    Hapana! Akukubaliana na ilo



    Akajinyanyua na kutoa mashuka Yale akatandika mengine akachukua ndoo ya maji na kuelekea nje



    Wakati akielekea bafuni akakitupia macho chumba alicholala mpz wake Mery



    Kilikuwa kimefungwa kikimaanisha mkaaji bado amelala!



    Akapatwa na mashaka kidogo macho yake yakaangalia juu



    Alikuwa ni mtaalamu wa kusoma muda



    Ilikuwa ni saa kumi na mbili,ila kawaida ya binti yule uamka saa kumi na moja na kuanza kazi ndogo ndogo za pale



    Mpaka muda huo akuamka?!



    akaachana na mawazo hayo akaelekea bafuni kukoga



    Wakati anaoga bado mawazo yalikiandama kichwa chake



    Akapata wazo aende pale alipochimba angedhihirisha juu ya ndoto ile ambayo akujua ilianzia wapi au sa ngapi



    Akaarakisha kuoga



    Akatoka,akavaa na kuelekea eneo lile ambalo hapakuwa mbali na pale nyumbani



    Alipofika akapigwa na mshangao mwingine



    Hapakuwa na dalili ya kuchimbwa eneo lote lile



    Khaaa! Mguno ukamtoka



    Akadhibitisha ilikuwa ni ndoto



    Ndoto ya kuogofya!,unyonge ukamtawala



    Akapiga hatua zake fupi kurudi nyumbani,mikono akiiweka nyuma



    Alipofika nyumbani akashtuka baada ya kuona watu wengi nje ya chumba cha mpz wake Merry na ukunga ukisikika



    Akaongeza mwendo na kuzama moja kwa moja ndani



    'Khaaaaa!!!' Mguno ukamtoka,sambamba na kuyatoa macho kwa mshangao



    Mazingira ya eneo lile ayakutofautiana na aloyaona ndotoni, sijui usiku hakuwa na uakika



    Ila Merry alilala chini ulimi akiwa kautoa nje



    Macho kayatoa Pima....



    Silva akazidi kuchanganyikiwa.....







    CHINI YA BAHARI



    KATIKA HIMAYA YA BISAU



    Ulikuwa ni ulimwengu mwingine,



    ulimwengu waloishi viumbe aina ya majini!,Majini hawa wa bisau ni jamii ya majini waloeshimika kwa utajiri ktk jamii hiyo ya viumbe hao!



    katika kasri ya mfalme bisau Upande wa makazi ya alipo mtoto wake wa pekee wa kiume ZIDAU



    alikuwa kakaa katika kiti chake pembeni akiwa kazingirwa na walinzi walo onekana na wasio onekana!,



    Hakika kila kitu alicho vaa kilikuwa cha thamani,na alijaliwa sura "mubasharu" mbele za macho ya amwangaliaye!,



    kidoleni alikuwa na pete ilowaka waka!,pete yenye thaman zaid ya kitu chochote kwake,pete ilobeba mahusiano yake ya kimapenzi



    Japo mpaka muda huo akuwa na mpz ilipaswa mpz atakayempata aimiliki Pete ile



    Pete ya tozani



    Wakati akiwa hapo ghafla akaskia sauti ya baba yake maskioni pake!



    Sauti ile akuiskia yeye pekee,hata mama yake pia aliisikia



    "Mwanangu Zidau"



    "Rabeyka baba"



    "Mke wangu Miriam"



    "Rabeyka mume wangu"



    Kwa wakati ule wote wale walikuwa mbali mbali japo katika ngome ile ile



    Ila bisau alikuwa katika chumba chake mke wake alikuwa sebuleni na mwanao zidau alikuwa katika nyumba yake



    Ila waliweza kuwasiliana kwa mawazo!



    Baada ya wito ule mume akaamka toka kitandani akaangalia juu akiitingisha shingo yake ghafla akapotea

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Na kuja kutokea sebuleni!



    Zidau naye vivyo hivyo kama baba yake baada ya kuangalia juu kwa sekunde kadhaa akatoweka na kuja kutokea sebuleni pale



    "Twawaombeeni nafasi"



    Mfalme akatamka ambapo apakuwa na kizuizi walinzi wote wakasambaratika kwa kutoweka eneo lile.



    Mfalme akaanza kuongea



    "Mwanangu ZIDAU,mwanangu wa pekee katika falme yangu ya Bisau,mwanangu ulotukuka,sasa baba yako nimezeeka si wa Leo si wa kesho naweza kutangulia hivyo ni wajibu wangu kukutengenezea mazingira



    Naitaji uwe mfalme kwanzia sasa!.....



    Zidau akashtuka! Na si Zidau pekee aloshtuka hata mama yake Miriam, na viumbe vyote vilivyosikia kauli ile....



    " kabla sijakuachia ufalme nilazima upate mtihani ambao ukifaulu utakuwa umekubalika na "masowati" wote pili lazima uoe! , na si kuoa tu binti utakayemuoa ni lazima awe jemedari kama mama yako,



    Lazima tutoe mtihani atakayeshinda ndo mkeo hivyo vyote vitafanyika kesho hivyo saivi tunakupa mda ukamuombe MUNGU ufanikiwe na pili uanze mazoezi ya viungo ujaribu uwezo wa nguvu zako tayari kwa mitihani na mwisho naomba hiyo Pete uloivaa hapo kidoleni"



    Zidau akashtuka!!!



    Aachie Pete yake?!,Pete ilobeba nguvu zake zote?!



    No! Hakuwa tayari lakini alishangaa kuiona Pete ile tozani ikitoka yenyewe katika kidole chake



    Ghafla ikatoweka!



    Bisau akaachia kicheko kikali kilichotoka kwa mfumo wa radi , miale ya moto ikionekana katika mdomo wake



    "Najua umetumia akili nyingi sana kuiandaa Pete hiyo,pia najua umeweka nguvu zako nyingi sana katika Pete hiyo nimeipoteza hiyo Pete mtihani wako ambao utaanza kesho ni kuniletea Pete hiyo na si wewe pekee pia wanawake wote inapaswa waisake atakayeipata ndo malkia wako!"



    "Na je Mimi nikiipata wa kwanza!?"



    "Utaileta na tutairudisha palepale mpaka binti aipate kumbuka majini wengi sana watakufa kutokana na mahali ilipo kuwa na ulinzi mkali"



    "Mh!"



    "Mwisho pia majini wa kawaida wanaruhusiwa kuisaka na atakayeipata atakaimu nafasi yako ila kutokana na nguvu ulizokuwa nazo usihofu kuhusu ilo"....



    Zidau akaamka huku akiwa na majonzi na kumpa heshima baba yake ghafla akatoweka



    HIMAYA ya bisau ilitawaliwa na nderemo kauli ile ilisikika kwa kila mwana HIMAYA na wote wakaingia kazini kuisaka tozani Pete ya maajabu



    Wakianzia himayani kwao



    *****



    CHINI YA ARDHI



    HIMAYA YA KUZIMU



    Katika himaya iloongozwa na jitu la kutisha kijana mdogo mwenye sura mbaya Jb ( mzimu ulorejea)



    Aliketi katika kiti chake cha enzi huko kuzimuni pembeni alikwepo mke wake



    Walikuwa wakiangalia tv jinsi wanadamu walivyoishi duniani,ghafla radi Kali likapiga



    Hali ya hewa ikaanza kubadilika , matone makubwa ya mvua ya damu yakaanza kuishambulia himaya ile



    Yakawa yakidondoka mabonge ya damu na miili ya majini walinzi wa anga



    " kuntuntamkun haaaaaaa chini kum taaniyaaaa?! ( jambo gani linaloikumba himaya yangu?!)



    Jb akaongea kwa sauti kali



    Nje vilio vya maajabu vilisikika,mvua ikazidi...



    Jb akaikunja mikono yake katika kifua chake akawa akiangalia paa la nyumba yake ni kama alikuwa akitafakari jambo



    Akaanza kuzungumza vitu kwa sauti ya chini,macho yake yakazidi kutoa miale ya moto



    Ghafla akaachia cheko, ni cheko lililotoka kama radi , tayari alishang'amua ni jambo gani lililotokea



    Ni jambo gani lililoleta gharika katika HIMAYA yake ile!



    Akapiga mguu wake wa kuume chini,kishindo kikali kilichoambatana na shoti kikafatia....



    akaachia kicheko tena na ghafla akatoweka



    Sekunde ile ile alikuja kutokea katika ukumbi mkubwa,hakuwa peke yake alikuwa na wananchi wake



    Kilikuwa ni kikao cha ghafla alichoitisha....



    Bado mvua kubwa iliendelea kunyesha ikiachia mabonge ya damu na kuleta hatari kwa wana mizimu wale



    Baada ya kimya kifupi kila mtu akiwaza lake jb akafumbua kinywa chake



    Akaunguruma kidogo kwa sauti ilotisha,viumbe vile navyo vikaunguruma kama ishara ya kumjibu bwana mkubwa wao



    "Nadhani wengi wetu mmeshtushwa na gharika hili lililoivamia HIMAYA yetu hai,himaya ya wafu na kutokana na uwezo wetu tofauti tulojaliwa nao kuna wanaojua nini kilichopelekea gharika hili na kuna ambao awajui kitu....



    Wenzetu wengi sana wamekufa,na wenzetu wengi sana wapo hatarini kupoteza maisha yao tatizo ni nini has a?!..



    Mfalme wa himaya ya Bisau iliyoko chini ya bahati amezeeka sana na anataka kuachia ngazi na madaraka kumuachia mwanaye wa pekee aitwaye ZIDAU....



    Ila kama mjuavyo majini wengi sana upenda kutoa mitihani kwa wanao hitaji kukahimu nafasi zao hata kama ni mwanaye tofauti na sisi mizimu

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hivyo mfalme Bisau aliitaji kumpa mtihani mwanaye mtihani wenyewe ni kumnyang'anya Pete ambayo mtoto huyo aliitumia akili sana kuitengeneza na mbaya zaidi aliweka robo tatu ya nguvu zake katika Pete hiyo hata hivyo robo aliyobakia nayo ni kubwa kuliko nguvu za majini wa HIMAYA hiyo



    Ndipo Pete hiyo alipoitupa chini ya ardhi kwa kuipoteza na kumwamuri Zidau aisake na akiipata atakuwa kafaulu mtihani na si Zidau pekee na majini wote wanaohitaji ufalme huo kwa wanawake wa himaya yao atakayoipata atakuwa malkia wa falme hiyo....



    Kumbuka mbali na nguvu yake ya asili pia Pete hiyo ya Tozani inalindwa na roho zilizovikwa na Bisau mwenyewe



    Tozani (Pete ya ajabu) mfalme Bisau bila taharifa akijua italeta madhara kaamua kuitupia katika ulimwengu wetu....



    Imeleta gharika,imeleta simanzi,imetuletea majonzi.....



    Imeua walinzi wetu wengi kwa maafa hayo nami kama mfalme.....



    Jb akanyamaza, mwili wote ulimloa jasho,alitetemeka kwa hasira baada ya kimya kifupi akaendelea tena kwa ukali mishipa ikiwa imemsimama....



    SIWEZI KUKUBALI,LAZIMA BISAU ALIPE DAMU YA WANA KUZIMU TOZANI IMEDONDOKEA KATIKA HIMAYA YETU LAZIMA KILA KIUMBE AISAKE NA ATAKAYE IPATA NI MALI YAKE NI PETE YENYE MAAJABU YENYE UTAJIRI KWANZIA SASA KILA MZIMU KWA KUTUMIA NGUVU ZAKE AISAKE TOZANI



    Na kiumbe yoyote atakaye ingia kutoka "majini" hatutomuacha hai hata ikiwemo mtoto wake"



    Kelele zikasikika mizimu yote ilifurahia jambo lile



    Wote wakaungana kuweka nguvu zao pamoja kuizima mvua ile iloletwa kwa kudondoka kwa Pete ya tozani



    Pete ya ajabu



    Mvua ikakoma,wakaanza msako mkali kuisaka tozani....



    ****



    DUNIANI



    Bado watu waliendelea kuomboleza kwa kifo kile tata cha MERY,mama yake alishikiliwa na wanawake kadhaa akibembelezwa



    Sauti ilikauka na aikumtoka tena kutokana na kulia sana



    Silvar alinata kama sanamu,alishindwa kuiamini akili yake



    Ni ndoto au kweli?!



    Hakuwa na jibu la moja kwa moja



    'Je ni Zena Kureysh ndiyo muuaj?!,'



    Alibaki akijipa maswali mfululizo pasina majibu,taratibu machozi yalimtoka



    Alimpenda MERRY zaidi ya kitu chochote.



    Nje ya nyumba ile kitara cha polisi kiliwasili wakashuka maaskari watatu na kuongoza mpaka eneo la tukio



    "Tafadhali tunaomba nafasi"



    Askari mmoja aliongea na watu wakaanza kusogea kuwaacha maaskari wale wafanye kazi yao



    "Mmmh!"



    Askari yule aliyeonekana kuwa kiongozi wao akaguna baada ya kugundua kitu



    Wenzake wale wawili wakamtazama kwa mashaka



    "Ni nani ndugu wa karibu wa marehemu?!" askari yule akatamka akiwa angalia watu wale walokuwa makini kusikiliza atasema nini



    Mwanaume mrefu maji ya kunde akajitokeza na kusimama Mbele ya askari yule



    "Kwa jina naitwa insp Nurdin kutoka kituo kikuu cha polisi ni inspekta afisa upelelezi wa kesi za mauaji"



    "Mmmh!" Watu wote wakaguna baada ya kusikia jina lile



    Wengi walimfahamu insp yule kwa umaharufu wake wengi awakumtambua kutokana na kofia yake ya kipolisi kumfunika sura yake



    Insp NURDIN ndio alokuwa na jb katika riwaya ya mzimu ulorejea akichunguza vifo vile tata vilivyo sababishwa na mzimu yule alikuja duniani kulipiza kisasi....



    Pia insp huyu alimkamata Upendo katika kisa kile cha upendo baada ya kumtilia shaka kumuua rafiki yake IRENE

    Je ni vipi wangeshindwa kumfahamu?!



    Hata wewe ndugu msomaji nadhani unamfahamu!





    Insp Nurdin alimkazia macho mzee yule lengo lake ajitambulishe....



    "Kwa jina naitwa mzee Paul ni baba yake mzazi na marehemu"



    Nurdin akaandika maelezo Yale katika kitabu chake



    "Marehemu alikuwa anaishi na nani humu ndani?!"



    Akampachika swali na bila kujiuliza mzee Paul akajibu



    "Alikuwa akiishi mwenyewe"



    "What?!"



    Nurdin akapigwa na butwaa,ni wazi akulitegemea jibu lile



    "Alikuwa akilala peke yake humu chumbani afande kwani ni nini umegundua?!"



    Alijibu mzee Paul na kumpachika afande yule swali alionekana wazi kuwa na wasiwasi usoni , afande Nurdin akapotezea na kuuliza swali lingine



    "Ok basi usiku wa Jana alilala na nani?!"



    Akauliza tena macho yake makali yakiganda kwa mzee yule



    "Alilala peke yake,"



    Nurdin akatingisha kichwa kutokubaliana na jambo lile



    'Inaonesha wazi marehemu kauwawa iweje apewe majibu kama Yale?!'



    Akakuna kichwa chake hiyo ni baada ya kuitoa kofia yake na kuiweka mezani



    "OK!, ni nani wa kwanza kuugundua mwili wa marehemu?!"



    "Ni mke wangu"



    "OK mama embu tueleze ilikuwaje mpaka ukagundua mwanao amekufa?!"



    "Niliamka saa moja kama kawaida yangu ila cha ajabu nilishangaa kukuta mlango wa mwanangu MERRY, bado umefungwa ikiwa na maana bado ajaamka wakati si kawaida yake ua ana amka saa kumi na moja kila siku



    Ivyo nilihisi moja kwa moja kuwa ana matatizo ikabidi nikamgongee ambavyo hata hivyo akufungua nkashikwa na wasiwasi na kwenda kumwambia mume wangu ambapo tukisaidiana na majirani tulivunja mlango na....Ku mkuta ...mwanangu katika hali hii"



    Mama yule akaangua kilio,uchungu ulimkaba



    "Unasema mlivunja mlango?!...."



    Insp Nurdin akauliza kwa hamaki,



    Mama yule aka hafiki kwa kutingisha kichwa huku bado machozi yakimtiririka kwa uchungu



    'Inawezekana kweli?!, mbona huyu maiti anaonekana ameuawa tena kwa kunyongwa na kupigwa makofi ina maana muuaji alipitia wapi kama mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani?!'



    Nurdin aliwaza peke yake akijaribu kuangaza pengine angeona nafasi ambayo muuaji alipitia,lakini akufanikiwa kuiona



    Akazidi kuchanganyikiwa,akawatazama wale wenzake nao walikuwa katika tafakari kuu!



    Ni wazi Waligundua kile alichogundua insp ila awakuweza kusema kitu Mbele ya watu wakihofu kuaribu upelelezi



    "Mama na baba tutawahitaji kituoni kwa upelelezi zaidi,kwa sasa mwili utapelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi...."

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Insp Nurdin akazidi kutoa maelezo,akiwa bado anaendelea kuandika andika maelezo katika kitabu chake kile cha kumbukumbu za inspekta.



    ********



    CHINI YA BAHARI



    HIMAYA YA BISAU



    KOO YA MUZIDU



    Hii ilikuwa ni koo kubwa, katika himaya ya mfalme Bisau



    Koo yenye nguvu za kichawi,baba yake na Muzidu mwenyewe aliuwawa kikatili na mfalme Bisau baada ya mipango yake ya kutaka kupindua ufalme ule kugundulika



    Mtoto pekee wa kiongozi huyo wa koo aitwaye MUZIDU ndo akashika usukani wa kuiongoza koo hiyo yenye wafuasi wengi wenye nguvu za uchawi ulimwenguni



    Naye pia alikuwa na malengo kama ya baba yake na kila siku waliongezwa nguvu na mashetani walowaabudu wao



    MUZIDU alijua ipo siku moja angekuja kuitawala falme ile kwa mapinduzi au Ki haki



    Kusikia mfalme BISAU anaachia ngazi na kumwachia mwanaye wa pekee na wana majini wote mtihani wakuisaka tozani kwao lilikuwa ni jambo jema



    Kwa akili na nguvu zao walijua sasa falme ile ni yao,na awakuwa na shaka juu ya ilo



    Mbinu zikapangwa kwa kuwa walijua lazima mfalme angemwonesha mwanaye mahali tozani ilipo ilikuwa ni lazima wamwangamize mtoto yule kwanza kabla awajaisaka tozani na kitakachofatia ni kuisaka tozani kabla awajaichukua himaya hiyo rasmi



    MUZIDU akatoa amri Zidau asakwe na kuuwawa haraka sana....



    Wachawi wale wakaingia kazini







    Asubuhi na mapema Zidau alijiandaa na kuwaaga wazazi wake usiku kucha akulala akijaribu nguvu zake zilizobakia kuisaka tozani bila mafanikio



    Ni wazi aikuwa katika himaya yao,na ilikuwa nje! Katika ulimwengu mwingine



    Je ni ulimwengu UPI?!



    Kuzimu,duniani au katika sayari nyinginezo



    Hapana kwa vyovyote alijua lazima itakuwa duniani,ndipo alipoianza safari ile kwa kuanza duniani



    Kwa vyovyote nguvu zake zote alizielekezea katika kuisaka tozani na wala si katika maadui zake



    Alitambua wazi robo ya nguvu alizobakia nazo akuna jini aliyekuwa na nguvu kiasi icho



    Na pia alitambua robo tatu ya nguvu zake alizoiwekea Pete yake hapakuwa na jini wa kuweza kuishika



    Icho ndicho kilichompa kiburi



    Baada ya kutoweka pale alikuja kutokea katika sayari ya dunia



    Ulimwengu walioishi viumbe aina ya binadamu



    Alikuwa ni kijana Mzuri mwenye asili ya kiarabu,alichukua wasaa huo kutafuta hoteli na alifanikiwa kupata hoteli yenye hadhi



    Mkumbuke kijana huyu alitoka katika himaya ya kitajiri



    Hivyo alipenda kuishi kitajiri.....



    ****



    KOO YA MUZIDU



    Muzidu kwa kutumia nguvu zake alizokuwa nazo pamoja na nguvu zake za kichawi,hakupata tabu kugundua mahali Zidau alipokimbilia



    Naye bila kupoteza muda alitoweka na kuja kutokea katika ulimwengu wa kibinadamu



    Akauanza msako Mara moja akiwa na nia dhabiti ya kumwangamiza mtoto yule ili yeye ashike nyadhifa ile



    Mfalme Bisau alijua juu ya Nia ya muzidu kumsaka mwanaye kwa nia ya kumwangamiza,na alijua uwezo wake wa kichawi alokuwa nao



    Hakuwa tayari kuona mwanaye akiangamizwa ilhali yeye yupo hai



    Akaandaa walinzi wa siri kwenda kumlinda mwanaye kila aendapo dhidi ya viumbe waovu



    Lilikuwa ni kasino kubwa lililotawala matajiri wenye fedha zao



    Katika upande za mapokezi alikaa kijana yule wa kiarabu akiwa na bia yake mezani



    Aliamua kunywa kinywaji kile cha kibinadamu ili atulize akili japo akujua kama kitamlevya au laa!



    Wakati akiendelea kunywa kinywaji kile ghafla nywele zikaanza kumsisimuka na mapigo ya moyo kumwenda mbio



    Ilikuwa ni ishara ya hatari



    Kwa kutuma nguvu zake alijaribu kuitazama hatari ile,lakini akufanikiwa

    Ni wazi robo ya nguvu zake alizokuwa nazo zilidhibitiwa



    Katu akufikiri kama ni kiumbe wa himaya yao aliyekuwa maeneo Yale kwa Nia mbaya kwake,kwani alijua wazi ana nguvu zaidi ya jini yoyote katika himaya yao



    Iweje hashindwe kuing'amua hatari ile ilomuelemea kwa kasi sana?!



    Akacheka kwa sauti ndogo ya kifedhuli



    'Au kuna binadamu hapa mwenye nguvu zaidi yangu?!'



    Akawaza ila akatingisha kichwa kukataa kwani alikumbuka juu ya binadamu alosikia kuwa walikuwa na uwezo zaidi yao



    Si wengine bali ni waganga wa kienyeji



    Ila alitambua wazi viumbe hao wasingeweza kuwa maeneo kama Yale kwani walisifika kwa kuishi maisha duni,iweje waje maeneo ya kasino kama pale?!



    Hapana,alikataa akakumbuka pia juu ya watumishi wa MUNGU ambao pia walisifika kwa kuwa na nguvu zaidi yao



    Ila hao pia wasingeweza kuwa maeneo ya starehe kama yale,



    Sasa je ni kiumbe gani huyo anayetaka kumchezea?!



    Akainuka taratibu,aliitaji kutoka nje lakini ghafla akapamiana na mtu



    Wakatazana



    Zidau alipata kuyaona macho ya MTU yule yaliyokuwa yaking'aa...



    Alikuwa ni MUZIDU



    Kitendo cha kumgonga Zidau kilimpa hasira tayari alikusanya nguvu zake katika mkono wake na kurusha ngumi ambayo Muzidu aliiona na kujikunja ngumi ile ikapiga ewa



    Na kufanya kijana yule akose muhimili ambao Muzidu aliachia kombora ambalo alikuonwa na mtu likampeleka ZIDAU chini



    Nje ya kasino lile ghafla bin vuu kuna viumbe vilitokea vikaelekea mpaka lango la kasino ile ni wazi walinzi mabaunsa awakuviona viumbe vile vikajongea mpaka mahali walinzi walipo



    Wakaingia katika miili yao



    Ghafla ndani ya kasino kelele zikasikika,na walinzi wale watano walioingiliwa na nafsi za kijini kwa haraka wakaingia ndani



    Macho yao yakatua katika kundi la watu ambao katikati yao kulikuwa na mafahali wawili walokuwa na asili ya kiarabu wakipambana



    Viumbe vile ambavyo kwa macho ya kawaida ya kibinadamu walionekana walinzi walijipenyeza mpaka katikati ya watu na kutokea katika ugomvi ule



    Wakafanikiwa kuwatenganisha wapiganaji na kuwatoa nje.



    Walipoelekea katika gari na mlinzi mmoja akaliondoa gari kwa spidi,akiingia katika barabara kuu ghafla MUZIDU akaachia shoti Kali katika breki gari ile ikasimama ghafla na kwa kuwa kulikuwa kuna gari ilikuwa inakuja kwa nyuma ikaigonga



    Kishindo kikali kikasikika na gari ile ikaserereka miili ile ikarushwa nje



    Aikujigeuza Mara ya pili



    Ilikuwa ni ajali mbaya!



    Ajali ilochukua uhai wa miili ya viumbe vile,japo miili ile ilionekana ni mfu ila nafsi za kijini bado ziliishi na ziliiacha miili ile na kwenda katika mapori kupambana!



    Muzidu kwa kutumia ishara zake,na nguvu zake za kishetani alizokuwa nazo,alifanikiwa kuwadhibiti walinzi wale!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walinzi walotumwa na mfalme Bisau,kumlinda Zidau pasina kujua Bisau ana nguvu za kichawi kiasi gani!



    Kosa hilo lilimgharimu mfalme Bisau,na Muzidu akishirikiana na wachawi pamoja na nguvu zake za kishetani wakafanikiwa kumwangamiza Zidau! Na walinzi wake wale!....



    Mfalme Bisau jambo hilo lilimuumiza sana,lakini hakuwa na la kufanya



    Mfalme aliitajika jasiri



    Muzidu kumwangamiza Zidau ulikuwa ni ujasiri ambao kiongozi wa falme ile aliitajika awe nayo



    Na maneno ya mfalme ni sheria kuwashinda maadui ilikuwa ni moja wapo ya kigingi ambacho ilipaswa Zidau ashinde



    Kinyume chake alishindwa na kuuwawa duniani,hakika yalikuwa ni maumivu kwa mfalme lakini je angefanyaje?!



    Ni wazi sasa utawala ulikuwa unaondoka katika koo yake,tena ukiondoka na kumuachia maumivu makali ya kumpoteza mwanaye kipenzi....



    Baada ya habari kufika katika ulimwengu ule kuwa ZIDAU kauwawa majini wale wa himaya ya Bisau wakaongeza juhudi kuisaka tozani



    Wakijua mwenye nguvu zaidi yao awapo naye tena katika kinyang'anyiro kile....



    ******



    HIMAYA YA KUZIMU



    Ni msichana Mrembo,tofauti na wenzake kuwa na sura mbaya yeye alijaliwa sura nzuri na umbo matata....

    Kila mwanaume amwangaliaye akuacha kumtamani kama si kupenda kabisa

    Yeye alikuwa na cheo cha jemedari mkuu katika himaya ile ya kuzimu



    Kwa jina aliitwa ZENA KUREYSH



    Jini lililojaliwa nguvu na spidi bila kusahau uzuri usoni pake na umbo maridhawa



    Naye pia kama walivyo viumbe wengine wa himaya ile alikuwa katika msako wa kuisaka Tozani



    Pete ya ajabu!



    Aliziamini nguvu zake na hakuwa na shaka juu ya mahala Pete hiyo ilipodondokea



    Kwa kutumia nguvu zake akaangaza macho yake na kunong'ona



    "PETE YA TOZANI POPOTE ULIPO NAITAJI NIJUE UKO WAPI?!"



    Ghafla Giza likatanda,anga nalo likatawala wekundu , akawa akitingishwa na kuyumbishwa,ni kama kulikuwa na tetemeko la ardhi,



    Tozani pale ilipodondokea ikawa ikimulika,mng'ao wake ukiongezeka na kutingishika



    ",TOZANIIIIIIII nakuomba uwe katika mkono wa....



    Kabla ajamaliza akarushwa na kugongwa katika ukuta



    Tozani pale ilipodondokea ikatoweka....



    Na kuja kutokea pale alipo ZENA,



    Baada ya Zena kudondoshwa akajinyanyua na kuitazama kwa tabasamu Pete ile



    Akanyoosha mkono kuelekea ilipo akiwa na dhumuni la kuichukua



    Ghafla akatetemeshwa na kuachia yowe akarushwa tena katika ukuta ule



    " mamaaaaaaaaa"



    Akaachia yowe,ni wazi aligundua Tozani ilikuwa ina nguvu zaidi yake



    Je angefanyaje?!



    Uwezo wa kuichukua ulikuwa ni mdogo ila ilikuwa lazima aichukue



    ******



    KOO YA MUZIDU



    wachawi wote waliweka duara,mioyoni mwao walikuwa na furaha kwa kiongozi wao MUZIDU kumwangamiza Zidau ambaye majini wote hawakuwa na shaka kuwa ndo ambaye angekuwa mfalme!



    Uwepo wao pale ni kutazama ni wapi , ni katika ulimwengu upi mfalme Bisau alipoitupia tozani ile



    Katikati ya duara lile paliwekwa chombo kama beseni ambalo ndani paliwekwa robo maji....



    Wachawi wote wakashikana mkono , MUZIDU akasogea katika beseni lile na kulinyooshea mkono!



    Shoti zikatoka,na kulipiga beseni lile ghafla Pete ile ikaonekana ndani ya beseni ikiwa katika chumba cha ZENA



    Pembeni walimwona Zena akiwa anaitazama Pete ile kwa tabasamu mwanana!



    Tabasamu mubashara!!!



    Ilikuwa ni kabla ajaenda kuigusa na kupigwa shoti!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Tozani ipo katika ulimwengu wa kuzimu!,hapa ni kuzimu na ipo katika mikono ya huyu binti lazima tuipate muda huu "



    Aliongea kwa sauti ya taratibu kama anaongea mwenyewe na ghafla akaropoka



    "Tozani lazima iwe katika mikono yangu na naenda kuichukua nikiwa peke yangu nikiitaji msaada ntawaitaji ila kaeni tayari....Mimi ndo mfalme wa himaya hii mtarajiwa"



    Ghafla akatoweka akiwaacha viumbe wale wakiendelea na ibada zao za kishetani!



    *******



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog