Search This Blog

SENDAYE (MALKIA WA MOYO WANGU) - 5

 







    Simulizi : Sendaye (Malkia Wa Moyo Wangu)

    Sehemu Ya Tano (5)







    Mbele yake alikuwa mtabiri wake ambaye pia ndo mshahuri wake mkuu pia kulikuwa na walinzi wake watatu na wake zake wawil



    " nahitaji unipigie kombe nione kinachoendelea ndani ya msitu"



    Mfalme Omoti aliongea kwa amri wala Mtabiri hakuwa mbishi akamtengenezea kombe lile akaseti vitu vyake katika beseni lenye maji tukio zima tena 'live' msituni likajionyesha pale!



    Hakika mtabiri yule alikuwa ni shida

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwanza aliona kwanzia vijana wake wakiingia katika pori lile wakiongozwa na mbwa



    Ghafla walishughudia kwa mbele Mabaru akiwa amasisha watafit wale waongeze mwendo



    "Ongezeni mwendo jamani tunafikiwa!"



    Wote wakashtuka mule ndani!



    "Inamaana Mabaru anashirikiana na hawa visebwengo?!"



    Mfalme akahoji kwa jazba



    "Na ndo alowafungulia hakiwa kama paka katika ndoto yako yeye ndo kawatorosha"



    Mtabiri akajibu akiwa na uhakika sasa wa kile alichokihisi!



    "Lakini mbona maelezo ya Misago nitofauti na hiki tunachokiona?!"

    Mfalme akahoji



    "Hapo ndipo hata Mimi ninaposhangaa" mtabir akajibu kwa mashaka



    "Bila shaka watakuwa wanashirikiana Hawa...



    Mfalme akajibu lakini ghafla alishtuka pale alipo ona Misago akiachia mshale wake uloenda na kumchoma Mabaru mgongoni ni kama aliwajibu na ni kweli wazo la misago lilikuwa kweli ilikuwa lazima amuue Mabaru kutoa shaka ya mfalme juu yake na kweli shaka ile iloanza kujijenga ikafutika palepale



    " itakuwa Mabaru alimtuma Misago ili aweze kuwasaidia ingekuwa ni kitu kimoja asingemuua kazi nzur Misago....



    Mfalme akaongea akitabasamu!



    Wakaendelea kuonyeshwa wale vijana wengine walivyouwawa na mpaka pale ambapo sasa misago alikuwa akimchinja Jemes au Isaki



    Mfalme alikuwa na raha ya ajabu!....



    Alijiapizia kumpa zawadi nzuri misago atakaporejea!



    ****



    KATIKATI YA MSITU PANDE



    Misago alizidi kuikata shingo ya Isaki damu zikaanza kutoka...



    Kwake ilikuwa ni furaha!



    *daaaah inamaana huu ndo mwisho wa Isaki nini kitakachoendelea Sendaye atakamatwa!,*





    KATIKATI YA MSITU PANDE



    Misago alishika kisu chake na kukipeleka katika shingo ya Isaki lakini ghafla macho yakamtoka Pima



    Ni baada ya kuona kuna ngozi nyingine ndani ya ngozi ile ambayo ni nyeusi



    Akastop na kumwangalia Vizur Jemes hata kule alipong'atwa na mbwa ngozi nyeusi ilionekana na mbwa alinyofoa ngozi nyeupe!



    Hamu ya kutaka kujua zaidi ikamvaa akaanza kuichuna ngozi ile kutoka shingoni kuja chini!



    Si yeye pekee alopigwa na butwaa kule katikati ya msitu!,hata mfalme Omoti aloshughudia kila kitu naye alishangazwa na jambo lile lilikuwa ni jipya kwake



    Baada ya kuichuna ngozi yote ya juu Misago sasa akaanza kukichuna kichwa



    Alishtuka!,macho yakamtoka Pima!



    "Isakiiiiiiii"



    Akatamka kwa ukali pasina kuamini kile akionacho!



    ***



    "Unajua Mimi na wewe ni marafiki tuloshibana Isaki hivi ukija kuwa mfalme utanisahau!"



    Kijana mdogo kiumri alikuwa akimuulza rafiki yake ambaye alikuwa ni mtoto wa mfalme ...



    Isaki kabla baba yake ajafariki,na kabla Omoti ajashika ufalme!



    Isaki akaachia tabasamu!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Misago wewe si rafiki yangu tu wewe ni zaidi ya rafiki yangu nakuhaidi kukupa cheo kikubwa upande upande wa mash wote uongoze ww....



    Misago akaachia kicheko



    " baba ako atakubali sasa?!....



    "Heeee mi sindo ntakuw mfalme kipindi icho....



    Misago aliwaza huku machozi yakimtoka si hayo tu pia alikumbuka kipindi flani alikuwa kakaa mahali akiwa na mawazo tele katika kichwa chake



    Aliwaza mateso ambayo baba ake alikuwa akimpa mama yake pindi akilewa



    Wakat akiwa katika mawazo yale Isaki akamfata



    " usiwaze rafiki yangu mi nakuhaidi kufanya kitu baba ako ataacha kumpiga mama yako"



    Isaki aliongea kwa sauti ya taratibu!



    "Kweli isaki?!....



    " kweli embu ningoje hapa....



    Isaki akatoka aliporejea baada ya dakika chache alikuwa na walinzi watano tena wenye mikuki na pinde zao



    "Haya twende"



    Misago akanyanyuka wakaelekea nyumbani ambapo walimkuta bado Mzee Igoma akimpiga mkewe alipo ona ujio wa walinzi wale alitetemeka na Isaki akatumia mwanya ule kuanza kumsema na kweli maneno yake yalimchoma Mzee Igoma akaacha kunywa pombe na kuacha kabisa kumtesa Mke wake



    Yote Yale Isaki aliwah kumfanyia enzi za utoto wao,akajikuta akimpapasa Isaki huku machozi yakizidi kumtiririka!



    Kubwa zaid alilowah kumsaidia ni pale ambapo Isaki alimwachia huru mama yake



    Kwani mama yake alihukumiwa gerezani na adhabu Kali baada ya kukutwa na hatia ya kumuua mumewe baada ya kumfumania na mwanamke mwingine



    Ila katika sikukuu ya kijiji kile Mfalme alitoa nafasi ya upendeleo kwa mwanae kuchagua kitu



    Isaki aliomba aachiwe mama yake na Misago huru!

    Kila mtu akiwemo Misago mwenyewe alishtuka akutegemea kama Isaki angeomba jambo lile



    Naye mfalme hakuwa na budi kumwachia huru mama yake misago



    Huo wote ni wema ambao Isaki aliwah kumfanyia , akujua kama ipo Siku ingepaswa alipize ihsani kwa kijana yule



    Moyo ulimuuma kutomjua mapema,alijua fika kuwa yule ndo mfalme wa haki wa kijiji kile



    Akajikuta akimpigia magoti Isaki na kuanza kumuomba msamaha huku machozi yakimchurizika!



    "Nisamehe mfalme wangu!,sikujua kama ni wewe Isaki bado upo hai ha ha ha ha"...



    Na ghafla kilio kikageuka na kuwa furaha akamnyanyua pale chini na kumkumbatia kwa nguvu!....



    Alafu ghafla akasimama na kuondoka tena akikimbia alikuwa akienda kutafuta majani ambayo ni dawa ya kumzindua Isaki pale chini!



    *******



    " hapanaaaaaaaaaaaaaaaaaa woteeee hapa sitaki mtu twendeni msituni nachotaka ni kufa kwa wasaliti wote na ambaye atansaliti naye atakufa vilevile "....



    Mfalme aliongea kwa ukali akionekana wazi kuchanganyikiwa baada ya kugundua yule mzungu ndo Isaki na Misago alikuwa kamsaliti



    " yametimia"....



    Mtabiri akajisahau na kuongea kwa sauti!



    "Eti nini?!...."



    Mfalme akaoji kwa hasira mtabiri hakutaka kumuongopea anamwambia wazi



    "Mfalme upaswi kwenda msituni naona ile ndoto inaenda kutimia...."

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni kama anamdhalilisha mfalme Omoti , mtemi alojiamini alichomoa mshale wake na kilichofatia ni yowe na dakika chache badae mtabiri na mshahuri wake mkuu alikuwa maiti chini



    "Hakuna wa kunipinga Mimi kwa majira sasa ni saa moja nilitoa amri kukipambazuka Sendaye na Isaki hapa waletwe hapa lakini mpaka sasa ak...."



    Kabla ajamalizia vijana wale wakiwa na miili ya watafiti wale wakawasili ila walishangazwa na hali waloikuta kwa mfalme!...



    Hapakuwa na muda wa kuizika miili ile ikawekwa katika chumba kimoja ikapakwa madawa ya asili waloijua wao kutoaribika



    Mfalme na baadhi ya walinzi wakaingia msituni kwa msako wao!



    ***



    Ghafla macho yalikuwa mazito kufumbuka alijitahidi kuyafumbua mwishoe kwa shida sana akayafumbua!



    Asalaleee!



    Ulikuwa ulimwengu wa ajabu akalitazama anga



    Du! Akashtuka anga lilikuwa jekundu tofauti na lile alilolizoea....



    "Ha ha ha ha ha Isakiiiiiiiiiiii, ha ha h ha Isaki



    Ghafla kicheko kiKali kikasikika sambamba na sauti ambazo ni kama alizijua,..



    'Nipo wapi hapa?!'



    Akawaza akijaribu kugeuza shingo kutafuta sauti ilipotokea



    Akajitahidi kujinyanyua na kukaa kitako!



    " haaaaaaaaaaaa"



    Akatoa mguno baada ya kuwaona wenzake,watafiti wenzake



    "Umetuponza Jemes"...



    Daniely alilalamika huku machozi yakimchuruzika,machozi ya damu



    " umetuponza Jemes"



    Paul naye akadakia



    "Umetuponza Jemes"



    Abdully naye akasema kwa uchungu



    "Umetuponzaaaaaaaaaaaaa"



    "Noooooooooooooo"



    Isaki akakataa kwa ukali na ghafla radi kali likapiga ghafla Giza likatanda pakakosa uwonano na taratibu pakaanza kupambazuka....



    Si kwa uwekundu tena!,Bali palipopambazuka palikuwa na uweupe kama wa duniani anga likiwa jeupe



    Alipotupa macho mbele yake alista ajabu kumuona baba yake katika kiti cha kifalme,na mama yake na hata mtabiri mganga mkuu wa kijiji chao!



    Isaki akapikicha macho yake pasina kuamini kile akionacho



    "Karibu katika himaya ya kuzimu mwanangu huku ndipo tulipo wazazi wako"



    Isaki alifrah kuwaona akatamani kunyanyuka pale lakini alishindwa akabaki kakaa vile vile



    "Sasa muda wa wokovu kwa kijiji cha Bomole umewadia ni muda wako wa kuwa mfalme wa kijiji kile.....



    Baba yake aliongea kwa furaha isaki akatingisha kichwa ishara ya kukubali!



    " nadhani wakati unakuja huku uliwaona wenzako wakikulaumu kwa kuwaingiza katika matatizo hao pia tutawatumia kukusaidia ila baada ya kushinda watatoweka yakupasa uizike miili yao kushujaa bado nafsi zao zipo hai kwakuwa miili yao ipo"



    "Nakukabidhi mshale huu ndio utakaotumia kumchoma nao Omoti una sumu yake ya asili!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baba yake Isaki akanyanyuka pale katika kiti chake cha kifalme na kumpelekea mshale ule akamkabidhi



    Isaki akaupokea!



    Baba yake yule akarudi katika kiti chake



    "Mganga wangu"



    Akamwita mganga yule ambaye muda mchache tulimuona mfalme akimuua baada ya kumpa taharifa za ndoto yake ile ya miaka ya nyuma kutimia!



    Mganga akamtazama mfalme wa mzimuni mule...



    "Mtibu Isaki akaifanye kazi duniani"...



    Mtabiri akanyanyuka mkono wake majani flani yakatua katika mkono wake akayaweka mdomoni na kuyatafuna na kuanza kumpaka Isaki mwilini



    ****



    Misago alishtuka macho yakamtoka Pima ni baada ya kurejea na kumkuta Isaki mkononi akiwa kashika mkuki



    " mmmmmmh"...



    Akaachia mguno kwani mkuki ule ulong'aaa wakati anaondoka kwenda kumkatia dawa hakuwa nao



    Ila sasa....anamkuta hakiwa kaushika tena akiachia tabasamu



    Akajaribu kumnyang'anya ili auweke pembeni dah Isaki aliushika kwa nguvu Misago akashangazwa na jambo lile



    Ila akaachana nalo akachukua yale majani na kuyatupia mdomoni!

    Ndo muda huo huo mtabiri kule kuzimu naye alipotupia majani Yale mdomoni



    Akampaka ndo muda ule ule Kule kuzimu mganga alipompaka



    Ghafla kizunguzungu kikali kikawa kikimjia!,Giza wazazi wake wakaanza kumpungia mkono kumuaga



    Giza likatawala na ghafla macho yakajifumba



    Akajilazimisha kuyafumbua pasina mafanikio,ila kihisia hali ya hewa ilibadilika Saut ambazo akuzisikia awali za ndege na wanyama zilianza kusikika kwenye maskio yake



    Akajilazimisha kuyafumbua macho yake na ghafla akafanikiwa



    Mbele yake alikuwa Misago aloachia tabasamu kwa furaha baada ya kuzinduka Isike



    Ila kabla awajafumbua mdomo kuongea chochote tayari walishazingirwa na jeshi la Omoti!



    Wote wakayatoa macho yao kwa mshangao



    "Ha ha haaa haaaaa haaaaa huu sasa ndo mwisho wenu!"



    Mfalme Omoti akaongea kwa Ukali na pasina kupoteza muda akatoa mkuki katika kite alichokivaa mgongoni akaupachika kwenye mshale wake



    Akauachia na mkuki ule ukachomoka kwa kasi kumuelekea Isakiiii alobaki katika butwaaa na kutokujua ilipaswa afanye niniiii



    Mfalme Omoti anagundua Isaki bado yupo hai hivyo ana amua kukusanya jeshi na kuvamia msitu Pande!



    Ambapo wanafanikiwa kuwaona



    na Omoti anatoa mkuki katika kite na kuupachika katika mshale wake



    Akauachia kumuendea Isaki!....



    "Hapanaaaaaaaa" Misago alipiga ukelele na kujirusha akampiga kikumbo Isaki Isaki akadondoka upande mwingine na mkuki ule ukamchoma Misago!



    Watu wote wakatumbua macho pasina kuamini kilichotokea!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla walipoinua macho yao kuangalia eneo alilodondokea Isike akwepo wakazidi kushangaa



    "Mnashangaa nini tafuta kila mahali!"



    Mtemi Omoti akatoa amri! Vijana wale wakajigawanya makundi



    Msako mkali ukafatia!



    ****



    Habari zile za kuuwawa kwa mganga mkuu wa kijiji kile au mtabiri baada ya kugundua kuwa Isike yu hai zilizagaa katika kijiji chote cha Bomole



    Watu wakaanza kujigawanya katika makundi,makundi



    Wengi waliuchoka utawala wa mtemi Omoti vijana wasiokuwa walinzi ila wakakamavu wakaungana.



    Si vijana pekee hata wamama,wadada wake kwa waume wakaingia msitu PANDE



    walikuwa tayari kwenda kumsaidia Isike katika msitu ule kutokana na utabiri kabla mtabiri ajauwawa walikuwa na uhakika wa kushinda



    Wakashika upinde na mishale wakiimba nyimbo za kishujaa na kuuvamia msitu pande!



    Mambo yalishabadilika ndani ya kijiji kile!



    ****



    NCHINI MAREKANI



    Wasiwasi ulitanda nyoyoni kwa baba yake Jemes Dk Livingstone na mama yake bi nice wistorn



    Moja ni baada ya kupoteza mawasiliano na James na hata wazazi wa watoto walo enda msitun kufanya utafit ule nao pia walihitaji kujua juu ya watoto wao



    Ulikuwa ni utafiti wa Siku mbili tu!



    Leo siku ya sita awakujua kilichoendelea!



    Wakakubaliana waiandaye safari wakajue kulikoni!



    Kwakuwa Dk Livingston alikijua kijiji kile kilichopo bara la Afc katika nchi ya Kinte vijiji vya ndani ndani ndani huko



    Kesho yake saa mbili walikuwa ndani ya ndege kuelekea nchini kinte ndani ya kijiji cha Bomole kilichopo ndani ndani ya mkoa wa Odovyi



    ****



    Mfalme Omoti alizidi kuchanganyikiwa walinzi wake wote waliuwawa kwa mazingira ya kutatanisha na sasa alibakia mwenyewe akiwa kajificha katika kichaka kimoja

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alijutia kuingia katika msitu ule!....



    Mambo yalimbadilikia....



    Ni wazi sasa ile ndoto aliyo ota ilikuwa ikienda kutimia!



    Ghafla akiwa pale katika kichaka ghafla Isaki akapita!



    Ni wazi alikuwa akimsaka na wala akumuona pale alipojificha!....



    Omoti akaachia kicheko akatoa upinde na kuuvisha katika mkuki aloushika akiwa palepale akampimishia Isike mgongoni akauachia



    Mkuki ule ukatoka kwa spidi Omoti akawa akiuangalia huku akitabasamu ,lakini ghafla alitoa macho ya mshangao baada ya kushughudia mshale ule ukigeuka na kuanza kumfata!



    Yani ukaanza kumrudia yeye!



    Mizimu ilianza kufanya kazi



    Akaachia ukunga akitoka pale alipojificha na kuanza kukimbia huku akipiga kelele zilizomshtua Isaki alipogeuka ule mshale ulokuwa hewani ukadondoka hivyo akuuona akapiga hatua kuanza kumkimbiza!.....



    Naaam ndoto sasa ilitimia!



    Jinsi alivyokimbia ni kama alivyokimbia kwenye ndoto



    Mfalme Omoti alizidi kukimbia kwa kasi ila kila alipogeuka nyuma Isaki alikuwa akimfikia kwa kasi vile vile!



    Kwa kuwa Omoti alikuwa akikimbia huku akigeuka nyuma ghafla alijikwaa na kuanguka chini kama ilivyokuwa kwenye ndoto akajitutumua na kujinyanyua ila ile anapiga hatua kitu chenye ncha Kali kikakita mgongoni!



    Ulikuwa ni ule mkuki alokabidhiwa na baba yake kule kuzimu



    Na sasa ulikuwa mgongoni kwa mfalme katili, mwenye roho mbaya ilojaa tamaa



    Omoti akajitahidi kupeleka mkono wake nyuma katika mgongo wake alitoa macho baada ya kuugusa mshale mwili ukamsisimka,maumivu makali yakaambaa akaanza kuona maruerue na ghafla akaenda chini!



    Isaki akamfikia pale chini na kumwangalia kwa jicho la jeuri



    "I....I...I..saki...unaniua?!"



    "Kufa mfalme mwenye roho mbaya Leo nimelipiza kisasi kama ulivyowaua wazazi wangu na utozikwa kwa heshima yoyote utaachwa huku uwe chakula cha wanyama wakali kwanzia sasa Mimi ni mfalme wa kijiji hiki...."



    "Oyooooooooooooooo"



    Ghafla wakasikia mshangilio Isaki akageuza kichwa kutazama



    Ahmad!!!



    alishtuka akaweka mkono wake mdomoni baada ya kuonwa amezingirwa na wananchi wa kijiji cha Bomole!



    Mwanzo akujua lile!



    'Wamekuja sangapi!'



    Akajiuliza pasina jibu sahii,akaachia kutabasamu akarudisha shingo yake kwa mfalme Omoti



    Akashtuka tena! Omoti akuwa hai tena na alipoutazama mkuki alomchoma nao! Nao aukwepo



    Ulitoweka katika mazingira ya kutatanisha



    Wananchi wakaanza kumwimbia Isike na ghafla macho ya Isike yakanata kwa binti mmoja Mrembo ambaye akumuona kabla



    "Sendayeeeeeeee"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akajikuta akiita kwa sauti



    "Isakiiiiiiiiiii"



    Sendaye naye akaitika kwa kuita akipenya katikati ya watu mpaka mahala alipo Isaki



    Wakakumbatiana



    "Sendaye malkia wa moyo wangu!"



    "Isaki mfalme wa moyo wangu"



    "Nakupenda sana Sendaye"



    "Hata Mimi nakupenda sana mfalme wangu"



    "Nashkur sana wananchi wangu kwa sapoti mlonipa sikuitegemea kwa kweli nawaahidi mtaishi kwa amani wote walokuf katika sekeseke hili tutawazika kishujaa kasoro Omoti tutamuacha humu aliwe na wanyama....



    Watu wakashangilia!



    Safari kutoka ndani ya msitu ule ikafatia wote wakiwa na furaha kwa kilichotokea



    ****



    Walipofika katika jumba la kifalme Isaki alishtuka baada ya kukuta ugeni ambao akuutegemea!

    Si Isaki pekee hata Dk Livingston na Mke wake nao walishtuka kumuona Isaki katika sura yake halisi



    Tena akiwa kama mfalme wa kijiji kile...



    Isaki akawaomba faragha wakiwa watatu kuzungumza



    " baba na mama nisameheni ila kilichotokea dah....



    Ikabidi aanze kusimulia akidanganya na kuficha baadhi ya mambo kukwepa kuaribika kwa mambo



    "Tuliingia katika kijiji hiki baba salama tu na tukaruhusiwa kufanya huo utafit na Dani akafanikiwa kugundua dawa hiyo...



    Ila sasa Siku tuliyotegemea kuondoka tulishangaa tukizuiwa na mfalme yule tukaonekana tunaiba maliasili yao adhabu ikatoka wote tuuwawe kwa kuchinjwa wenzangu wote wamechinjwa...."



    "Unasema?!...."



    Dk Livingston na mke wake bi nice wakauliza kwa pamoja



    "Ndio ila nilipofikiwa Mimi wakati mchinjaji ananchinja akagundua uwepo wa ngozi mbili ikabidi asitishe na anichune ngozi ya juu si ndo alishtuka baada ya kujua ni Mimi



    Akantoroshea msituni kwa kuwa alikuwa ni rafk yangu wa kitambo ,mfalme alipogundua alimuua akawa anatuma walinzi waje kunikamata walinzi wakawa wakikataa kwa kuhofia utabir wa mganga mkuu alotabir mi kuwa mfalme hivyo mfalme akaamua kunisaka mwenyewe kwa kuja mwenyew msituni Leo



    Wananchi kwa kuwa walichoka uongozi wake nao wakaunga tela kuja msituni ambapo kwa pamoja walimshambulia na kumuua



    Wakaniteuza kuwa mfalme!



    Dk Livingston akatabasamu!



    Kufurahia jambo lile ila tabasamu lake alikudumu baada ya kukumbuka vifo vya wanafunzi wale nane ambao wazazi wao walikuwa wakisubiri majibu!



    Wangewa ambia nini wakaelewa?!



    Wakapanga waeleze watoto wote nane akiwemo Jemes wote walikufa na ndicho kilichofanya mapinduki na kumuondosha mtemi Omoti madarakani na mwisho kuambulia kifo



    Kwa majonzi wakatoka nje na kuwaeleza hali halis wazaz



    Vifo huzuni majonzi vikatawala katika kijiji kile!



    Wazazi wakakubali watoto wao wazikwe palepale kijijini kwa kuwa miili ilishaharibika!



    Katu wazazi wale awakujua kama Isaki ndiyo Jemes hiyo ilibaki siri ya waliyofahamu



    Walichojua ni kwamba Jemes aliuwawa na mfalme na kuliwa na wanyama wakali!



    Isaki akamkabidhi baba yake dawa ya oma ya madege ilovumbuliwa na Dani



    Tiba ikapatikana!



    Wazungu mbali mbali wakawa wakitembelea kijiji kile kutazama kaburi walozikwa wanafunzi wale ..



    Kaburi lile likawa moja wapo ya kivutio kijijini pale



    Kijiji kikawa kiuchumi kwa kasi

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Isike na Sendaye wakazidi kupendwa na wananchi wao!



    Maisha yalojaa amani ,Upendo yakatawala kwa wana Bomole



    MWISHO!



0 comments:

Post a Comment

Blog