Search This Blog

KOTI JEUSI - 5

 







    Simulizi : Koti Jeusi

    Sehemu Ya Tano (5)





    Kule nje ya hospitali,, alionekana Bakari na Solo wakiliegesha gari, kisha wakashuka kutoka ndani ya gari hilo wakazipiga hatua kuelekea mochwari,,, Solo akasema,, "wacha mimi niende kuonana na daktari fulani hivi,, ninamazungumzonae! wakati wewe ukiendelea kushughulikia maiti ya mama kuitoa hapa mochwari.

    Solo hakutaka Bakari afahamu kuwa mkuu wa jeshi yupo hapohapo katika hospitali hiyo,, pia wodi aliyolazwa Solo anaifahamu. nia na lengo lake ni kwenda kumuangamiza mkuu wa jeshi!

    aliamua kufanya iwe siri,, kwa wakati huo,, akidhani huenda akimwambia Bakari,, basi hatomruhusu kufanya kile alichokikusudia, badala yake atamwambia washughulikie maiti ya Linda kuitoa hapo mochwari!  hivyo atashindwa kufanya alichokusudia kukifanya!

    Bakari hakuweza kushtukia kwa haraka mpango wa Solo,,hivyo akakubali Solo aende kuonana na daktari huyo!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Solo akazipiga hatua  za taratibu kuzipanda ngazi zinazoelekea juu ya jengo hilo,,ambako kuna wodi za kulazwa wagonjwa...alipofika upande wa juu,, akachomoa kitambaa kilichokuwa na sumu ya ungaunga.. akaifuata wodi aliyokuwa kalazwa mkuu wa jeshi,,

    kumbe mkuu wa jeshi alikuwa karuhusiwa kurudi nyumbani,, dakika mbili zilizopita! alikuwa ndani ya ngazi ya umeme(Lift)akielekea upande wa chini,, hivyo walipisha pasipowao kufahamu! kwa sababu Solo alitumia ngazi za kawaida kwa kutembea kwa miguu.. na mkuu wa jeshi alitumia ngazi ya umeme(Lift)

    mkuu wa alipofika upande wa chini,, akazipiga hatua kulifuata geti la kutoka nje kabisa ya hospitali hiyo!

    ghafla akaliona gari la jeshi likiingia kwenye geti,,, kumbe afisa mmoja wa jeshi alikuwa amekuja kumjulia hali,,, akafutahi kumuona mkuu wa jeshi akiwa na Afya njema,, akafungua mlango wa gari,, mkuu wa jeshi akaingia,, na kuondoka zao kurudi kambini!



    wakati huohuo, kule upande wa juu  ya jengo la hospitali,, alionekana Solo akiendelea kuzipiga hatua huku macho yake yakitazama kwa umakini,, asije akagundulika kuwa anataka kufanya mauwaji! alipoukaribia mlangu wa wodi aliyokuwa kalazwa mkuu wa jeshi,, akasita kutembea akageuza shingo yake,,akahakikisha hakuna mtu yeyote anayemuona yeye kuingia kwenye wodi hiyo!  akafungua mlango na kuingia ndani ya wodi!  akastaajabu kutokumkuta mkuu wa jeshi, ndani ya wodi hiyo!  ghala ukasikika mlio wa simu ikiita!!

    Solo akaangaza angaza macho yake! hakuiona simu hiyo,, akaamua kuufuata mlio wa simu hiyo,,akagundua unatokea kitandani!  alipofunua mashuka. yaliyokuwepo kitandani hapo,,akaona simu,,, akaichukua!  alipoikagua kwenye namba zilizopigwa kwenye simu hiyo akastaajabu kuona namba yake ya simu,,, akajaribu kujipigia kwa kutumia simu hiyo.. kumbe ilikuwa ni simu ya mkuu wa jeshi!

    Solo akajisemea moyoni,, "bila shaka huyu mwanaharamu,,hayupo kwenye hospitali hii,,, inaonyesha ameondoka muda mchache uliopita...



                      *************************



    upande mwingine,, alionekana mkuu wa jeshi pamoja na afisa wake,,, wakiwa ndani ya gari la jeshi,, ghafla mkuu wa jeshi akajipapasa mifukoni mwake,, akagundua kuwa simu yake haikuwepo kwenye mifuko yake hivyo ameisahau kule hospitali... akaamua kumwambia yule afisa ageuze gari warudi kule hospitali!



    wakati huohuo kule hospitali,, alionekana Solo akitokea ndani ya wodi aliyokuwa kalazwa mkuu wa jeshi,,, akazipiga hatua kuzifuata ngazi,, akaelekea upande wa chini kule mochwari!  akamkuta Bakari akiwa tayari ameshachukua maiti ya Linda na kuiweka ndani ya gari,, akimsubiri Solo  waondokezao,, Solo akaingia ndani ya gari,, kisha Bakari akaliwasha gari na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.

    walipolikaribia geti la kutoka nje kabisa ya hospitali hiyo,,, ndio. wakati ambao mkuu wa jeshi pamoja na afisa wake wakiingia ndani ya geti la hospitali hiyo!

    PATASHIKA!.



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                         



     Bakari na Solo hawakuweza kumuona mkuu wa jeshi kaitka lile gari walilopisha nalo pale getini! mkuu wa jeshi akaonekana akishuka kutoka ndani ya gari hilo ,akazipiga hatua kuelekea ndani ya jengo la hospitali hiyo,,,akaingia kwenye ngazi ya umeme(Lift) mlango ukajifunga nalift ikaanza kuelekea upande wa juu,,ghafla akaona pochi ndogo ya mfukoni (warlet) ikiwa chini akaiokota,,akaifungua na kutoa vitambulisho vilivyokuwemo ndani ya pochi hiyo,,alipotazama moja ya kitambulisho kati ya vitambulisho vilivyokuwemo ndani ya pochi hiyo,akaona picha ya Solo kwenye kitambulisho hicho pamoja na jina ,,,akashtuka! akajisemea moyoni,,"inamaana huyu mtu yumo humu ndani ya hospitali? sasa nipo hatarini yanipasa niwe makini, punde si punde mlango wa lift ukafunguka,,akatoka na kuzipiga hatua huku macho yake yakitzama kwa umakini wa hali ya juu,akafungua mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa muda mchache uliopita,akakuta chumba hicho kinafanyiwa usafi,,alipotazama pale kitandani,,akaona kitanda kimewekwa shuka jingine,,akauliza kwa mshangao! haujaona simu yangu hapo kwenye kitanda? yule nesi aliyekuwa anafanya usafi akajibu,,"hapana ,,,hapakuwa na simu wala kitu chochote. mkuu wa jeshi akajipa moyo huenda alipodondo kule nyumbani kabla hajaletwa hapo hospitali,sika,imu yake ilidondoka nyumbani kwake, akaamua kutoka ndani ya wodi hiyo na kuelekea nje ya hospitali hiyo!



     ************************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine,,alionekana Bakari na Solo wakiingia ndani ya nyumba yao...baadhi nya marafiki na jamaa wakaribu,,walikuwa tayari wamefika nyumbani hapo,,taratibu za mazishi zikafanyika wakamzika Linda. siku zilizidi kusonga ,,Bakari akaandaa mpango kabambe wa kwenda kumuangamiza mkuu wa jeshi! ghafla wazo likamjia,akajisemea moyoni,,hakuna haja ya kumuua...kwa sababu Solo anataka kulipiza kisasi cha ndugu zake kazi hiyo.,,wacha nimuache afanye kazi hiyo,,akazipiga hatua akafungua begi lake alilokuwa analitumia kuwekea nyaraka zake pamoja na vitu vyake vya muhimu,,akatoa bahasha ndogo akaifungua ,,ndani yake kulikuwa na picha akazitazama picha hizo moja baada ya nyingine! zilikuwa ni picha za watotot wa mkuu wa jeshi,,wale waliouwawa pamoja na picha za Solo na picha za Linda ambaye alikuwa ni mke wa kuu wa jeshi.,,,picha hizo zilionyesha kuanzia walivyokuwa wadogo mpaka walivyokuwa watu wazima....kisha akatabasam akajisemea moyoni,,"wacha nifanye jambo fulani. wakati huohuo,,pia alionekana Solo akiandaa mpango wa kumuangamiza mkuu wa jeshi,,akajisemea moyoni lazima usiku wa leo nimuangamize mkuu wa jeshi ,,ikishindikana ,,basi atakuwa na bahati ya kuishi miaka mingi!Solo akaingia ndani ya gari na kuondoka zake,, ilipofika majira ya saa mbili za usiku,,,akaonekana Solo kaliegesha gari lake kwenye hoteli ya kifahari iitwayo BLUELAND HOTEL,,Solo aliamini ni lazima mkuu wa jeshi aje kwenye hoteli hiyo ,,,kwa sababu ndio sehemu anayopenda kufanya makubaliano ya bihashara na wafanya bihashara wenzake katika bihashara zao haramu za madawa ya kulevya pamoja na silaha za moto na silaha nzito nzito za kivita...punde si punde kweli gari la. mkuu wa jeshi likaonekana likiingia ndani ya uzio wa BLUELAND HOTEL... Solo akamuona mkuu wa jeshi akishuka kutoka ndani ya gari hilo! akizipiga hatua kulifuata jengo la Hoteli hiyo. wakati huo huo,, alionekana Bakari akiwa nyumbani kwake,, akitazama ni wapi Solo alipo,,, kwa kutumia kifaa maalumu alichokitegesha kwenye gari la Solo pasipo Solo kujua! kifaa hicho (GPS) kilikuwa na uwezo wa kuonyesha mahali ulipo(LOCATION) Bakari akagundua kuwa Solo yupo Blueland Hotel... akaamua kuchukua begi dogo,, akafungua kabati ja kutoa koti jeusi,, akaliweka ndani ya begi hilo,, kisha akachukua ile bahasha iliyokuwa na picha za watoto wa mkuu wa jeshi tangu wakiwa watoto mpaka walivyokuwa vijana wakubwa... pamoja na picha ya Linda... akatoka ndani ya nyumba na kulifuata gari lake kuingia ndani ya gari na kuelekea huko BlueLand Hotel. baada ya dakika kadhaa. kupita,, Bakari akawa amefika eneo hilo.. akaliegesha gari lake kwa mbali,, kutoka kwenye hotel hiyo.... akachukua darubini maalu kwa ajili ya kuona kitu kilicho gizani(NIGHT VISION) akaanza kuangaza angaza kwa kutumia darubini hiyo......akafanikiwa kuliona gari la Solo.... aliotazama kwa umakini akagundua kuwa Solo hakuwemo ndani ya gari kwa wakati huo! Bakari akaamua kutoka ndani ya gari lake,akazipiga hatua kuelekea upande ambao lilikuwepo gari la Solo,, akaangaza angaza macho yake akaliona gari la mkuu wa jeshi,, akajisemea moyoni! bila shaka Solo amekuja hapa kulipiza kisasi yes ni jambo jema kwa upande wangu!! pia ni jambo baya kwa upande wa Solo kuwa na mzazi katiri kiasi hicho! muosha huoshwa.. wacha wauwane wenyewe kwa wenyewe.. akaingiz amkono wake katika mfuko wa suruali aliyokuwa ameivaa... akatoa ufungu bandia,,, akafungua mlango wa gari hilo.. akatoa koti jeusi ,, akaweka vkwenye kiti cha gari la mkuu wa jeshi kisha akaondoka zake! akaingia ndani ya gari,,,, kabla hajaliwasha gari,, zikasikika sauti za watu wakipiga moyowe phuku wakitimua mbio kutoka ndani ya hoteli hoyo kuja upande wa nje!! punde si punde ikasikika milio ya risasi ikitokea ndani ya hoteli hiyo! Bakari akaamua kuliwasha gari lake na kuondoka eneo hilo muda huohuo! akaliegesha gari lake mbali zaidi kutoka kwenye hoteli hiyo! akachukua darubini yake akawa anatazama kinachoendelea katika hoteli. punde si punde akaonekana mkuu wa jeshi akitimua mbio kulifuata gari lake,, akafungua mlango na kuingia ndani ya gari lake,, akaliwasha haraka,, na kuondoka eneo hilo.... kumbe Solo kapigwa risasi tatu kifuani na risasi moja kichwa akapoteza uhai palepale... ndio ukawa mwisho wa Solo. *************** Wakati huo Bakari hakujua chochote kuhusu kifo cha Solo... yeye aliamini Solo yupo hai. kwa sababu anamuamini katika upiganaji na kujihami yeye mwenyewe. Bakari akaamua kulifatilia gari la mkuu wa jeshi kwa ukaribu zaidi.. mkuu wa jeshi,, akahisi akaegemea nguo nzito kwenye kiti alichoketi! akapunguza mwendo na kutazama ni nguo gani hiyo! akashtuka kuona koti jeusi,,,, macho yakamtoka lakini akajipa imani kuwa muuwaji aliyekuwa anafanya mauwaji kisha anafunika maiti kwa koti jeusi,,, akeshamuangamiza kwa kumpiga risasi kule hotelini. hivyo hakuwa na hofu tena.. akaongeza mwendo wa gari lake,,,, Bakari aliendelea kulifatilia gari hilo,,, alipohakikisha wametoka eneo la mjini,,, Bakari akazidisha mwendo wa gari lake na kuligonga gari la mkuu wa jeshi ubavuni likatoka barabarani na kutumbukia ndani ya mfereji,, mkuu wa jeshi akapoteza fahamu kwa mshtuko.... Bakari akashuka kutoka ndani ya gari lake.. na kulifuata gari la mkuu wa jeshi,, akamtoa na kumuingiza ndani ya gari lake huku kamfunga kamba mikononi na miguuni! kisha akazipiga hatua kuelekea upande wa nyuma ya gari,, akafungua buti,,,akachukua dumu kubwa lililokuwa na petrol ndani yake... akalimwagia mafuta hayo gari la mkuu wa jeshi kisha akalichoma moto,,, akaingia ndani ya gari lake na kuianza safari ya kuelekea by mbani kwake! alipofika akamshusha mkuu wa jeshi kutoka ndani ya gari,, akambeba mpaka ndani ya nyumba yake! akamfungulia kamba kwenye mokono na miguu... kisha akamuweka katika chumba kilichokuwa tupu! akachukua ile bahasha akaiweka kando ya mkuu wa jeshi kisha akafunga mlango na kuondoka zake..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                   *************************



    Asubuhi palipokucha,, akaonekana mkuu wa jeshi akazinduka na kupata fahamu,,, alipoangaza angaza macho yake,, akaona yupo sehemu tofauti na nyumbani kwake,, alipojaribu kuvuta kumbukumbu,, akakumbuka tukio la mwisho,, kuwa alipata ajali...wakati anakumbuka hayo,,, ghafla akaona ile bahasha... akaifungua,, akaona picha za familia yake,, akashtuka,, picha hizo zilikuwa na mtiririko wa kadri miaka ya watoto wake ilivyozidi kwenda.. hatimae akaziona pich za wale vijana watatu aliowapiga risasi kwenye vichwa vyao wakafa.... pia akaona picha ya Solo pamoja na picha ya Linda! mkuu wa jeshi akahisi kuchanganyikiwa.... ghafla akaona karatasi imekunjwa,, akaifungua na kuanza kusoma maandishi yaliyoandikwa katika karatasi hiyo! macho yakamtoka,,, akajisemea moyoni,, "kumbe nimeangamiza familia yangu mimi mwenyewe!! haya yote yametokana na nini? mbona sielewi!! mkuu wa jeshi akajikuta analia kwa uchungu! punde si punde ukafunguliwa mlango,,, akaonekana Bakari akiingia huku kashikilia bastola iliyokuwa imefungwa kifaa maalumu isitoe mlio endapo risasi ikifyatuliwa(SILENSER) pia mkono wake wa kushoto alikuwa kashikilia picha moja.... akairusha chini,, pale alipokuwepo mkuu wa jeshi.. Bakari akasema,, "unamfahamu mtu huyo? mkuu wa jeshi akauliza,, "kwani wewe ni nani? na unataka nini kutokq kwangu? Bakari akajibu,, "nataka kuondoa uhai wako,, na si vinginevyo.....nimekwambia chukua hiyo picha kisha niambie unamfahamu mtu huyo katika picha?? mkuu wa jeshi akakataa kuchukua picha hiyo.. Bakari hakuwa anafanya mzaha! akafyatua risasi ikampiga mkuu wa jeshi kwenye goti... akapiga kelele kwa maumivu makali... akaamua kuokota picha hiyo,, alipoitazama akashtuka kuona ni picha ya Bakari! akasema ndio ninamfahamu,, alikuwa mwanajeshi wangu,, akafungwa jelw,, lakini alitoroka na sijui alipo.. tafadhali usiniuwe! Bakari akasema,, mimi ndiye bakari,, na hii sura unayoniona nayo ni sura bandia.... nilifanyiwa upasuaji na kubadilisha sura kwa sababu yako... wewe umeangamiza familia yangu kikatiri.... na ukanifunga pasipo kosa lolote....sasa mumeuwa familia yako kwa mikono yako mwenyewe! huo ulikuwa ni mpango nilioutengeneza mimi mwenyewe.... sasa wewe nitakuuwa kwa mikono yangu,,tena kwa mateso makali,..Bakari akafyatua risasi nyingine kwenye mguu wa pili wa mkuu wa jeshi.. akafyatua tena risasi nyingine kwenye bega,, pia akafyatua tena risasi nyingine kwenye bega la pili.. kisha akamfunga kamba..... akamkata masikio... pamoja na ulimi,,, akamtoboa macho kisha akamchinja na kumzika nyuma ya nyumba yake.... roho ya Bakari ikatulia ikawa na amani baada ya kumuangamiza adui aliyemuharibia maisha... akaendelea na bihashara zake,,, akaishi kwa amani mpaka leo. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



                            ****MWISHO******







0 comments:

Post a Comment

Blog