Search This Blog

TAMBIKO - 1

 







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Tambiko

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Hongera sana mke wangu,,nimefurahi sana kwa kunizalia mtoto...sijui nikupe zawadi gani?? kwa mimi binafsi sijaona zawadi inayostahili zaidi ya upendo wangu wa dhati kwako..hahahahahah

    pia mama yangu atafurahi sana..kwa sababu alikuwa ananisumbua kuhusu mjukuu...kila siku mjukuu mjukuu mjukuu,,mpaka umekuwa ni wimbo ambao nilichoka kuusikiliza masikioni mwangu....

    sauti iyo ilisikika ndani ya wodi ya wazazi..na aliyekuwa anaongea maneno ni mume wa mwanamke huyo aliyekuwa kajifungua mtoto wa kiume...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA*****



    Mtoto aliendelea kukuwa..kwa afya njema wakampa jina mtoto wao wakamuita MALIWA.....mama wa mtoto huyo anaitwa Conso

    na baba wa mtoto huyo anaitwa Shinje.

    Shinje alifurahi sana...akapunguza unywaji wa pombe..akawa anarudi nyumbani mapema kujumuika na familia yake..tofauti na mwanzo alikuwa akitoka kazini anapitiliza bar anakunywa pombe anarudi nyumbani usiku wa manane akiwa kalewa kupita kiasi..

    Conso alifurahi sana baada ya mumewe kubadilika na kuachana na vitendo vya anasa za kidunia....

    hata marafiki wa Shinje,,wakaanza kustaajabu,baada ya kuona rafiki yao hanywi pombe tena.....

    miezi ilizidi kusonganga,,hatimae Maliwa akafikia umri wa kutambaa...



    Siku moja,,majira ya usiku wa saa saba..Conso na Shinje wakiwa wamelala....ghafla walijitokeza watu wawili humo chumbani...watu hao ni wachawi...bibi mmoja na mwanaume wa makamo.

    watu hao ni majirani na ni watu wa karibu na familia ya Shinje....bibi huyo aliyekuwa uchi wa mnyama...akapuliza dawa ya kichawi kutoka kiganjani mwake...kisha akamchukua Maliwa na kumnyoa baadhi ya nywele kisogoni...kisha akamrudisha kitandani..

    bibi huyo pamoja na yule mwanaume wa makamo.wakatoweka kimiujiza.....



    **********************



    wakajitokeza kwenye kiwanja mpira kilichokuwa kimezungukwa na miti mikubwa ya mkaratusi.

    yule mwanaume wa makamo akanyoosha mkono wake kuuelekezea kwenye ardhi..ghafla akajitokeza kuku(jogoo) mweupe pamoja na kisu....akamchinja kuku huyo...kisha akaongea maneno ya lugha ya kichawi....maneno hayo hayaeleweki kwa sababu hayana maneno ya kibantu...hivyo ikawa ni kama maneno ya kilugha...

    akachimba shimo dogo na pana kiasi kwa kitumia kisu hicho...

    yule bibi akachukua zile nywele za Maliwa akazitumbukiza ndani ya shimo hilo...kisha wakamtumbukiza yule kuku!!! wakashirikiana kulifukia shimo hilo...

    walipohakikisha wamemaliza kuifanya kazi hiyo wakatoweka kimiujiza...



    Asubuhi palipokucha,,Maliwa alidamka na kuanza kulia mfululizo huku macho yamemtoka...Conso na Shinje wakaingiwa na wasiwasi..wakahisi huenda Maliwa anaumwa..wakamkimbiza haraka hospitali.....

    lakini vipimo vikaonyesha kuwa Maliwa hana tatizo lolote...wala ugonjwa wowote!

    wakaamua kurudi nyumbani....



       *******BAADA YA SIKU SABA KUPITA******



    hali ya Maliwa ikawa njema kama ilivyokuwa mwanzo...lakini kila ikifika usiku wa manane wakati Shinje na Conso wamelala....Maliwa yeye anakuwa macho..anakesha mpaka asubuhi...

    kitendo hicho kilimfanya Conso na Shinje waingiwe na wasiwasi...

    Shinje akasema..itabidi tuandae safari twende kijijini kwa mama..huenda bibi yake anamuita...tumpeleke japo ambebe mjukuu wake apate za bibi yake...

    Conso hakuwa na kipingamizi akakubali alichokisema mumewe...



    Shinje akaondoka na kuelekea kwenye bihashara zake.. Conso akabaki nyumbani akitazama Runinga huku akicheza na Maliwa..

    Conso alikuwa anamtazamawanae jinsi anavyotambaa kuzunguka sebule huku uso wa Maliwa ukionekana kuzungukwa na furaha isiyo kifani....



    ************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana yule bibi ambaye ni jirani yake Conso...akiwa ndani ya nyumba yake..

    akiongea na yule mwanaume wa makamo..kumbe ni wanandoa(mume na mke) mumewe akasema,,tumebakiza kazi moja tu..inatakiwa kipatikane kipande cha nyuzi ya nguo aliyoivaa Maliwa sasa hivi...ili tuikamilishe kazi ya tambiko...si unajua yule mteja wetu anatakiwa apakwe dawa kabla jua halijazama..na dawa hiyo haiwezi kufanyika bila kupata angalau kipande cha nyuzi ya nguo aliyoivaa leo mtoto huyo....ili afe..na dawa itaanza kufanya kazi..



    Kumbe mwanaume huyo wa makamo,,pamoja na bibi huyo ni wanganga wa kichawi...walipokea pesa za Tajiri mmoja..alizowalipa ili wamfanyie tambiko na zindiko la mali zake zizidi kuongezeka.

    kwa hiyo ikahitajika damu ya mtoto chini ya mwaka mmoja..

    Bibi huyo akasema,,"wacha mimi niende nyumbani kwao,kwa sababu wamenizoea hivyo itakuwa rahisi kupata kipande hicho cha nyuzi,,sasa hivi.

    bila kupoteza muda bibi huyo akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwa Shinje..akagonga mlango..Conso akamkaribisha jirani yake,,bila kujua kuwa jirani huyo hana nia njema na familia yake.

    bibi huyo akaketi kwenye sofa...akasema,,"Hongera sana yani tangu umejifungua sikuja kukujulia hali,,nilikuwa naumwa..si unajua uzee huu?

    Conso akajibu ,,"asante bibi karibu sana....kisha akambeba Maliwa na kumpatia bibi huyo ambebe.

    Bibi huyo alikuwa makini kumtazama Conso usoni ili Conso asijue kinachoendelea...

    Conso akazipiga hatua kuelekea jikoni kuleta matunda bibi hiyo ale...akamuacha sebuleni akiwa kambeba Maliwa....





    Bibi huyo alipo ona Conso kaondoka..akavuta kipande cha nyuzi kutoka kwenye nguo ya Maliwa.

    akaikunjakunja na kuifunga kwenye pindo la khanga yake..akatulia tuli..punde si punde Conso akaja na sahani iliyojaa matunda..akaiweka mezani...akamkaribisha bibi huyo.

    bibi huyo akachukua  kipamde cha nanasi na kuanza kukitafuna....alipomaliza akamuaga Conso ma kusema,,"asante sana mwanangu wacha miminnirudi nyumbani..nikaendelee na majukumu ya hapa na pale..

    wakati ananyanyuka kile kipande cha uzi kikadondoka..kumbe wakati anakifunga kwenye pindo la khanga yake...hakukiweka vyema kutokana na haraka haraka zake ili asishtukiwe..

    Conso akamsindikiza bibi huyo mpaka nje ya geti la uzio wa nyumba yake...kisha akarudi ndani...



    *********************



    bibi huyo akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea nyumbani kwake..ili awahi kwenda kuikamilisha kazi ya tambiko....alipofika akamkuta mumewe tayari amesha andaa vitu vya kufanyia tambiko,,, akasema,," umefanikiwa?

    bibi huyo akacheka cheko la kizee kisha akasema,,"mimi ni bibi flani hivi amazing kama msemo wa vijana wa kisasa wanavyosema....

    bibi huyo aliongea maneno hayo ya kujisifu huku akifungua lile fundo alilolifunga kwenye khanga yake,,,akiamini kuwa kile kipande cha nyuzi kimo ndani ya fundo hilo..aliendelea kufungua huku akiongea maneno ya kujisifu na majigambo..

    ghafla macho yakamtoka!!! baada ya kuona hakuna kitu chochote wala kipande cha nyuzi!!

    akajisemea moyoni,,"mimi ni mjinga wa mwsho..yani nimepoteza muda wangu bure bila mafanikio yoyote!!!

    Mumewe akauliza,,"kikowapi kipande hicho??

    mkewe akajibu,,"nitakuwa nimekidondosha bahati mbaya,,kama sio mule mule ndani ya nyumba ile..basi kimedondoka njiani!!

    malumbano yakaanza baina ya mke na mume...wakajikuta wanatukanana na kuanza kutoleana siri zao!!! mume wa bibi huyo akapatwa na hasira..akaingia jikoni na kuchukua panga..akamkatakata mkewe...

    bibi huyo akapoteza maisha.... mzee huyo wa makamo akaivuruta maiti ya bibi huyo na kuitumbukiza ndani ya kisima cha maji..kilichokuwa nyuma ya nyumba yake..kisha akaleta mafundi wakafunika kwa zege akisingizia kuwa ameamua kukifanya kiwe choo...haluna mtu aliyeweza kutambua hilo...



    ************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    siku zilisonga hatimae safari ya Shinje na Conso,,ya kwenda kijijini kwa mama yake Shinje ikawadia...

    siku ya leo wakadamka asubuhi mapema wakasafiri kuelekea kijijini....gari lilikwenda kwa mwendo wa masaa mengi kiasi..ilipofika saa moja jioni waliwasili kwenye kijiji cha MBULIGA..ambacho ni kijiji chao Shinje alipozaliwa..

    wakakodi taxi kutoka kwenye kituo cha mabasi mpaka nyumbani kwao Shinje...hapakuwa na umbali mrefu..baada ya dakika kumi walifika...

    mama Shinje alifurahi sana kumuona mwanae..pamoja na mjukuu wake Maliwa...akawapokea kwa furaha kupita kiasi..

    akawaandalia chumba cha kulala...



    *******************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog