Search This Blog

SOSO - 5

 







    Simulizi : Soso

    Sehemu Ya Tano (5)





    Yule doctor alipata taarifa kuwa kunakemikali imegunduliwa nchini tanzania na Mtafiti aitwae john... doctor huyo alimfahamu vyema john.. alianza kuingiwa na wivu ""inamaana mtu huyu bado yupo hai!!!!?? alijiuliza bila kupata majibuCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alikumbuka kuwa john aliwahi kwenda kwenye msitu yanapopatikana mapango ya SOSO... bila shaka chimbuko la kemikali hii itakuwa ni huko kwenye msitu huo aliokwenda john... Doctor huyo aliandaa safari siku hiyo hiyo... na kuondoka kuelekea kwenye msitu yanapopatikana mapango ya SOSO... alifika mtwara akalala... na palipokucha aliendelea na safari... akiwa njiank alikutana uso kwa uso na kiumbe yule wa ajabu alistahajabu hajawahi kuona kiumbe hicho tangu azaliwe....

    yule kiumba alipomuona yule doctor alitamani kumtafuna...kutokana na njaa kali alianza kuzipiga hatua za kizembe kuelekea pale gari lilipo kuwepo... yule doctor kuona hivyo aliliendesha gari kwa kasi zaidi.... kiumbe yule alilirukia kari na kulinyanyua juu... kiumbe huyo alikuwa na mguvu sana.. aliliponda ponda gari mpaka likabonyea akamtoa doctor na kumtafuna mzimamzima....



    kiumbe yule alizidi kusonga mbele na hatimae aliingia kabisa kwenye makazi ya watu... alianza kuleta balaa alitafuna watu watu wa eneo lile na baada ya wiki moja alisonga mbele.. baada ya kuona sehemu hiyo hakuna chakula tena... taarifa silienea nchi nzima vombo vya habari vilitangaza ujio wa kiumbe huyu.... wananchi walianza kuingiwa na hofu... wengi walianza kuhama miji yao... Raisi wa nchi aliamuru jeshi liende kumnasa kiumbe huyo wa ajabu... huwezi amini risasi hazikuweza kupenya kwenye ngozi yake na kuingia ndani...risasi zilindunda na kuanguka chini tu.. kiumbe huyo aliamua kukimbia baada ya wanajeshi kuanza kumshambulia kwa mabomu ya kurusha... alikimbia akatokezea katikati ya jiji la Dar es salaam.. watu walijeruhiwa kwa kukanyagwa na umati wa watu wakimkimbia kiumbe huyo..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    john alipata taarifa hizo... baada ya kuona tukio hilo kwenye Runinga... alimtambua kiumbe yule... bila shaka atakuwa ndiye yule mtu niliye mchoma sindano.... alijisemea john huku akionekana alisikitika na kujilaumu sana...alichukua kemikali ile na kuelekea uwanja wa ndege(Airport) ili awahi kwenda dar es salaam...

    baada ya dakika 55 aliwasili dar es salaa alikwenda moja kwa moja mpaka Lugalo jeshini...aliomba kuonana na Kamishna wa jeshi...alipewa ruhusa akaingia... aliomba kemikali ile itumike kumuangamiza kiumbe yule wa ajabu... lakini kamishna alipuuza.. kisha akamfukuza john aondoke zake.. aliona wazo la john ni la kijinga...kama risasi zinashindwa kumuangamiza kiumbe huyo...je hayo maji yako yataweza vipi.. alisema hivyo kwa kejeri kamishna huyo...john alimsihi sana hatimae kamishna alikubali..



    **********



    ililetwa bunduki maalumu inayoitwa REVOLVES SYRINGE"" bunduki hii hutumiwa sana na wawindaji wanapotaka kumnasa mnyama akiwa mzima bila kumdhuru...huwa inawekwa sindano maalumu ambayo inakuwa na dawa ndani yake..

    kisha john alichukuwa bomba kubwa na nene la sindano akaweka kemikali ile kisha bomba la sindano ile lilipachikwa kunako bunduki hiyo maalumu... kisha kamishna aliamuru iletwe ndege aina ya CHOPPER... wanajeshi baadhi pamoja na john waelekee sehemu ile ambapo kiumbe yule ameonekana... walipofika eneo hilo walifanikiwa kumkuta kiumbe yule akifanya uharibifu mkubwa katikati ya mji.. john alishuka kutoka ndani ya ndege na kupanda juu ya ghorofa refu.. kisha akachukua bunduki ile iliyokuwa na sindano iliyowekwa ile kemikali hatari...aliweka shabaha na kubonyeza kitufe cha kifyatulia.. shindano ile ilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye sehemu ya mgongo wa kiumbe yule.... ghafla alianza kuyayuka na kuisha kabisa akawa ujiuji...

    wananchi walifurahi na kumpongeza john kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kumuangamiza kiumbe yule....

    john alianza kupata tenda viwandani aliuza kemikali ile duniani kwote...baada ya miezi michache john aliwekwa kwenye orodha ya mabilionea watano nchini....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******MWISHO WA SIMULIZI HII*****





0 comments:

Post a Comment

Blog