Search This Blog

USIKU WA KAFARA (ROAD TO 2017) - 4

 







    Simulizi : Usiku Wa Kafara (Road To 2017)

    Sehemu Ya Nne (4)





    Kibaraka yule alifanya kosa kugeuka, kwani alivyogeuka tu gady ali mrukia na kumzoa wote waks jibwaga chini upinde na mshale vikaanguka pembeni huku wao wakibiringita huku kila mmoja akimshambulia mwenzake kwa ngumi nzito ,...! likawa balaa gady akipigania uhai wake.



    Hatimae kibaraka alifanikiwa kujizuia kubiringita na akawa kamuweka chini gady huku akiwa kamkalia na kumtupia ngumi za uso.



    Lakini ghafla alipigwa na kitu kizito kichwani kutokea nyuma yake..



    Sarah alikuwa kafika na kulichukua shoka na kumpiga yule kibaraka!



    Muda huo huo gady akamsukuma pembeni haraka gady akainuka na kilulichukua shoka kutoka kwa sarah kwani aliona sarah hajui kulitumia ...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda huo kibaraka alikuwa anatafuta njia ya kukimbia lakini muda huo huo gady alimsogelea karibu na makali ya shoka yakaanza kuuchimba chimba mwili wa huyu kibaraka.



    Alimkata kila mahali na kufanya mtu usitamani kuiangalia maiti yake na sarah alifumba macho kwani kitu alichokuwa anakifanya gady ni cha kikatili, kisha gady akauburuza mwili ule na kuutupa shimoni mule ...

    "tuondoke sarah funguo ya gari ninayo ....wenzetu wameuawa " gady aliongea akamkamata mkono sarah wakaanza kuondoka , hakuthubutu kuacha shoka yake kwani alijua muda wowote wanakutana na adui...



    Mpenzi msomaji baraka na john walikuwa wameuwawa kwani walipo fikikishwa kwenye pango lile kizee kilichoitwa malikia kiliamulu wachinjwe huku damu zao ziki tiririkia kwenye chombo cha sadaka.



    Mpenzi msomaji sipendi nikusimulie yaliyo mtokea dolla na neema , ila nisipo kusimulia utajua vipi yaliyo wakuta?



    Neema na dolla waliwambwa kwa kufungwa kwenye jiwe kubwa ndani ya pango wakafungwa vitambaa vilivyo waziba midomo na pua wakawa wana hema kwa tabu , kisha mishipa yao ya damu ikakatwa damu zao zikaanza kutililika mpaka kwenye jiwe ambalo juu yakeulilazwa ule mwili wa gunzani usio kuwa na uhai .



    Damu ya neema na dolla ilipoanza kufika kwenye jiwe alio lazwa gunzani , taratibu uhai ulianza kuulidia ule mwili wenye futi nane naamu mwili wa gunzani.



    Uhai ulikuwa unatoka kwa neema na dolla na kuingia gunzani..Nedma na dolla walikuwa wanskufa kifo cha taratibu chenye maumivu makali.



    Yule malikia kikongwe alikuwa amepiga magoti mbele ya sanamu la goroza huku mawazo yake na hisia zake zikiwa hazipo dunia hiii.



    ****************************



    Sarah na gady walitembea kwa mwendo wa haraka mwendo ulio wa gharimu kutumia dakika arobaini wakiambaa barabara na hatimae kwa mbali waliiona gari yao hapo mioyo yao ikapta furaha na tumaini..



    Wakiwa wanaendelea kukalibia gari yao ghafla mbele yao kukatokea msichana aliekimbia huku nguo zake zikiwa zime chanika chanika

    msichana yule aliangukia miguuni kwa sarah

    "nisaidieni anataka kuni ua" msichana yule alipiga kelele na muda huo macho yao sita yakamuona mtu mrefu asie pungua futi saba akiwa mbele yao..



    Alikuwa ni gola na yule msichana alikuwa ni diana .



    Kumbe gola alipo ambiwa amrudishe diana kijijini yeye hakufanya hivyo ila alipo ondoka pale pangoni alikaa mstuni na kusubiri diana arudiwe na fahamu ndipo amuingilie kwa lazima na kumfaidi kigoli yule..na sasa diana alikuwa karudiwa na fahamu na kujikuta mikononi mwa gola alie anza kumchania nguo yake ya ndani ili ambake, diana alipo pata upenyo akachoropoka na kuanza kukimbia hatimae alikutana na kina sarah huku gola akiwa mbele yao.



    Gola akiwa na bisu kubwa mkononi mwake akampita gady kama vile hakumuona huku akimfuata kigoli wake diana , gady kuona hivyo akajua sarah na yule msichana mwingine watakubwa na hatari muda wowote...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gady akapiga hatua za haraka na kumshambulia gola kwa kumpiga shoka la mgongo lakini makali ya shoka yale yakishindwa kuuchana mwili wa wa gola.



    Shoka ili dunda na gola alimgeukia gady..



    Gady hakuamini kwamba makali ya shoka lile yalio ua maadui wake watatu yameshindwa kwenye mwili huu.



    Tatizo gady hakujua kuwa alio waua walikuwa ni bina damu vibaraka wa goroza na huyu alikuwa ni gola mlinzi wa falme ya goroza na hakuwa binadamu...



    Gady aliinua tena shoka ili ajaribu shambulio la pili na hapo gola akashika lile shoka kwenye makali , macho yakamtoka gady akajikuta akiachia shoka na muda huo mkono wa gola ukakamata shigo ya gady na na kumuinua kwa mkono mmoja huku akimning'niza hewani kwa kabali ya mkono mmoja.



    "Sarah kachukue bunduki ya baraka" baraka aliongea kwa tabu na muda huo sarah akatoka mbio huku diana akimfuata nyuma mpaka kwenye gari lao ambalo lilikuwa hatua kazaa kutoka pala ..



    Gola akiwa kamning'niza gady alie rusha rusha miguu na mikono, gola akainua mkono wake mwingine ulioshika kisu kirefu kisha kwa nguvu akakizamisha tumboni kwa gady na kumuachia akianguka kama mzigo huku yowe zito likimtoka gady..



    Sarah alifungua mlango wa mizigo na kuichukua bunduki kisha akarudi mbio na kukuta gady katupwa chini akipiga yowe .



    Sarah alikumbuka jinsi walivyo elekezwa na baraka jinsi ya kuitumia bunduki!



    Sarah akaemulekezea bunduki gola kisha akavuta chuma cha stanby na kufyatua risasi mbili zilizo kita kifuani kwa gola..



    Lakani gola hakuyumba wala kuanguka alikuwa kama hajapigwa na chochote ,risasi hazikumdhuru ...gola akaanza kupiga hatua kumfuata sarah kwa hasira...



    Sarah alihamanika na kugeuka akimbie lakini alijikwaa na kuanguka , na gola akamsimamia mbele yake huku akimtolea tabasamu la kuchukiza.



    Gady alijiinua tena huku akipata maumivu makali akijikaza na kusimama akaingiza mkono mfukoni kwake akatoa funguo ya gari kisha akapiga hatua kumsogelea gola alie mpa mgongo.



    Gady alipo mkalibia gady akatenda kitendo ambacho kilitisha kukitizama mara mbili.



    Kwanza aliirusha ile funguo ya gari pale alipo anguka sarah kisha akachomoa kile kisu kwenye tumbo lake na kukikita kwenye ubavu wa gola...

    "We die together..." gady aliongea kwa sauti hafifu



    ilikuwa ajabu mara ya kwanza shoka lilidunda kwenye mwili wa gola hata risasi haziku mdhuru gola lakini sasa hivi kisu kilizama ipasavyo kwenye mbavu za gola.... hii ilimaanisha kisu hiki cha ajabu sana.



    "Sarah chukua funguo hiyo kimbia kijiji hakipo mbali" gady alipaza sauti yake hafifu huku muda huo akichomoa lile bisu ubavuni mwa gola na kulizamisha mgongoni kwa gola ambaye hakupiga kelele aina yoyote.



    Sarah alishindwa kuamini kinachotokea gady alikuwa katapakaa damu akimshindilia visu gola...

    "Nimekwambia kimbia" gady alipaza sauti ya mwisho

    na hapo sarah akajua kinachotokea ., nacho ni kwamba gady alikuwa anajitoa muhanga.



    Gola alimgeukia gady na kumpiga ngumi nzito kifuani, gady akapepesuka nakuanguka chini akikiacha kile kisu kikiwa kimezama kwenye mgongo wa gola.



    Sarah aliinuka na kuchukua ile funguo na kuanza kukimbia kuelekea kwenye gari ambapo diana alikuwa nje akihamaki huku macho yake yakishuhudia mapambano mazito baina ya gady na gola.



    "Ingia tuondoke" sarah alimpigia kelele diana huku yeye akiiingia upande wa dereva na kuiweka bunduki upande wa pili, macho ya sarah yalisha shuhudia gady akitupwa chini kwa mara ya pili , hivyo ilikuwa wazi gady asinge pona mbele ya kiumbe yule...



    Gola aligeuka na kumuona sarah na diana wakiingia ndani ya gari . gola akachukia akachomoa kile kisu na kukirusha akiwa kamlenga diana.

    kisu kile kili mkosa kidogo diana sentimita chache badala yake kile kisu kili pasua kioo na kuangukia ndani huku diana akipiga yowe la woga.



    Gola akapiga hatua awahi kabla hawaja washa gari lakini ghafla miguu yake miwili ikakamatwa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa ni gady alio ikamata miguu ile miwili akizuia gola asimfuate sarah wake alie mpenda.



    Ghadhabu zikazidi kumpanda gola akawa na kazi ya kuitoa miiguu yake kwenye mikono ya gady.



    *****************--****************



    Mzee mkongwe akiwa bado kapiga goti mbele ya sanamu la goroza ghafla akasikia chafya nzito kutoka kwa gunzani , ni ule mwili ulio lala juu ya jiwe kwa muda mrefu.



    Mzee yule akafumbua macho huku akiwa na furaha..

    "Ahsante goroza. gunzani anarudi" aliongea kwa furaha , alipo angalia kwenye lile jiwe waliofungwa neema na dolla akagundua mmoja wao alikuwa amesha kufa na mmoja bado.



    Neema alikuwa amesha iaga dunia.



    Wazo lingine likamuijia yule mzee juu ya sadaka mbili zilizo bakia.



    Tayari walikuwa wameshaua vijana wanne sasa walibakia wawili ambao mbweha dalu na mwenzake walitakiwa wawafikishe lakini mpaka mda ule hawakufika, hii ikamlazimu mzee huyu kikongwe awatafute kwahisia na kuwaangaza vijana wake...hapo ndipo alipo shuhudia miili mitatu ya vijana wake ikiwa imeuwawa.

    Mzee huyu alishtuka kwani haijawahi kutokea tangu waanze kafara hizi za kila mwisho wa mwaka hajawahi kuawa hata kijana mmoja lakini leo vijana watatu wame uwawa.



    Mzee huyu alipo jaribu kutafuta kwenye hisia zake mtu aliuwa vijana wake ,ndipo taswila yake ilipo muonesha balaa lililoendelea kati ya gady na gola huku akimuona gady wakati ule akimchoma gola kisu cha ubavu.



    Mzee yule aliacha kila kitu na kutoka nje ya pango ma kuwakuta wanachama wake wakiendelea kuabudu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "acheni kila kitu tuka wasaidie wenzetu wanapambana na mwanadamu mbaya" alipaza sauti huku akinyoosha njia.



    Wanachama wakamfuata nae akawa mbele kuongoza msafara wa kwenda kumsaidia gola.



    ***************************



    Sarah aliwasha gari na kuanza kuliondoa eneo lile huku macho yake yakimshuhudia gady akiwa kamzuia gola kwa kukamata miguu yake.



    muda huo diana alikuwa siti za nyuma yake huku akishangaa michoro ya kisu cha gola kilicho pasua kioo na kuangukia kwenye siti! diana alihisi kuwa alishawahi kusimuliwa na mama yake juu kiumbe kilicho miliki kisu aina hii.!



    Akiwa kachanyikiwa alizidi kuongeza mwendo huku akipata tabu kuuzoea uskani huu wa gari hii manual.



    Gola aliinama na kumpiga ngumi zito gady iliotua kichwani ,Gady akahisi kizunguzungu ila bado aliishika miguu ya gola

    Gola akaishika shingo ya gady na kuikaba ipasavyo .



    Hali ikawa mbaya kwa gady akajikuta akiacha miguu ile na muda huo huo gola akainua mguu wake na kukikanyaga kifua cha gady kwa nguvu ..

    gola akaondoka ambio akilikimbiza gari lakina sarah.



    Sarah alizidisha mwendo wa gari huku roho ikimuuma kumuacha gady, mara ghafla alishuhudia mtu akitokea porini akikimbia sambamba na gari lake kihoro kikamkumba sarah baada ya kumuona mtu yule akiruka kutokea pembeni ya barabara kuja upande wao na mtu huyo alitua kwenye dirisha upande aliokuwa yeye.

    Alikuwa ni gola ambaye aling'ninia kwenye gari mkono mmojaukiwa umeshika vyuma za kuwekea mizigo juu ya gari...na mkono meingine akaupenyeza dirishani na kuikamata shingo ya sarah...



    Haraka sara alikanyaga breki za ghafla ili amtupe kiumbe huyu lakini hakuwa hivyo gari ilisimama na kiumbe yule hakutupwa alikuwa dirishani na mkono wake ukizidi kumkaba sarah...





    Wakati sarah anafunga brek diana alifungua mlango huku akiwa na kile kisu akiwa anakumbuka siku moja usiku mama yake alimsimulia kuna viumbe wanaishi duniani ,hawapigiki na wana kisu kimoja ambacho ni cha falme yao na kila anae kimiliki kisu hicho ni mlinzi wa ufalme ule wa kiza. na mongoni kwake kuna kitu kinacho mlinda na kufanya wao waishi...

    diana alihisi ndio kile kisu kwani siku ile mama yake alimtajia michoro ambayo ipo kwenye kile kisu ...naamu michoro hiyo aliiona kwenye kile kisu ambacho kilimilikiwa na gola.



    Hivyo diana alizunguka gari na kumkuta gola akimkaba sarah.



    Diana alimdandia gola mgongoni na muda huo akakizamisha kile kisu chini ya shingo ya gola .



    Kwa mara ya kwanza gola akatoa kwa na yowe kali huku akimuachia sarah.



    Diana kuona hivyo akachoma tena huku safari hii akiwa anachana kwa kushusha kisu chini!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo msitu mzima ukatawaliwa na kilio cha gola huku kitufe kidogo kikitoka kwenye mwili wa gola palipo chanwa na kisu kikianguka chini.



    Gola alizungusha mkono wake na kumkamta diana lakini gola alikuwa amechelewa tayari kinga yake ilishaanguka chini



    Sarah kuona hivyo haraka akachukua bunduki na kamulekezea kichwani gola na muda huo akafyatua risasi ilio kibanjua nusu ya kichwa cha gola huku mwili wa gola ukitupwa chini....



    Gola alikuwa kasambalatishwa .



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog