Search This Blog

MERISA JINI MWITU - 3







    Simulizi : Merisa Jini Mwitu

    Sehemu Ya Tatu (3)





    "amenijua je huyu msichana mpaka akaniita kwa jina langu?,alifika kufanya nini mahali hapa ? mbona yupo katika hali kama hii?kakutwa na nini dada huyu?" maswali yote kichwani mwake yalikosa majibu alipo mtazamadada yule machoni aligundua lihitaji msaada wa dhati kabisa mahali pale

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "tafadhali Geb nisaidie nina teseka mahali hapa "alisema msichana yule kwa sauti ya chini huku machozi yakimlenga katika mashavu yake, Geb alipiga goti na kuvua koti alilo kawa amelivaa na kumfunika yule msichana kisha akamuinua mahali pale palipo na majani mengi na kumkalisha katika moja ya jiwe lililo kawepo karibu na pale alipo kawa amemkuta msichana yule "unatatizo gani dada angu na mbona nimekukuta mahali hapa yaonyeshahaupo sawa lazima kuna kitu kinasumbua nieleze una nini au kimekukuta kipi?"aliuliza Geb



    "ni kweli ngumusana kumkuta mtu katika msitu huu tena akiwa katikahali kama yangu ila nakuomba unipe hifadhi kwa leo kesho asubuh tukiamka nitakuelezea tatizo langu"alimjibu dada yule huku akimuomba msaada wa hifadhi Geb



    "dada angu nitakuhifadhi wapi mimi maana mimi nimtalii tu katika msitu huu na hata sina mamlaka yoyote mahali hapa nitakuweka wapi dada angu?"



    "hapo hapo ulipo nikwausiku wa leo tuu ikifika kesho asubuhi nitakuwa ninapo pa kwenda tafadhali nisaidie kwa hilo tuu"aliongea maneno ya upole yule msichana yakamjaza hofu na huruma Geb mwisho geb aliamua kuondoka na yule msichana mpaka katika hema alilokawa akiishi na kulala wote.

    Asubuhi ilipofika Geb alichelewa sana kuamka kiasi watu waliogopa kila aliyejaribu kumgusa ili aweze kuamka hakuamka mwishoni ndipo alipo shituka na kukuta watu wote wakiwa ndani ya hema lake cha kwanza alipo amka alimuulizia yule msichana aliyekuwa naye ambaye alifanana sana na yule msichana aliyekutana naye katika zile falme za jini mwitu"yuko wapi yule msichana aliyekawa amelala hapa?"aliuliza huku akiangaza huku na kule



    "msichana yupi ?"Mike alikuwa wa kwanza kuhoji



    "kuna msichana jana nilimtoa huko bondeni akiwa hana nguo nikamstiri kwa koti langu na kuleta humu ndani alidai anatakahifadhi na ana matatizo makubwa akasema ikifika asubuhi atanieleza kilicho msibu" wote walicheka kwa kumdhihaki Geb na kuondoka huku wakiuhimiza kuaamka na kujiandaa maana muda ulikwisha enda isipokuwa Mike ambaye tayari kuna picha ilianza kumjenga katika kichwa chake



    "Geb unanini mbona hatukuelewi?"alisema mike iliaweze kuelezewa vizuri akiwa peke yake.



    "ni kweli gaider maana kama ingekuwa ni ndoto basi lile koti langu ningeliona ila cha ajabu hata koti langu nililo mpa kama msaada nalo aliondoka nalo ni kweli Mike nilimuona ule msichana na niyule niliyekutana naye katika falme za jini mwitu " aliongea Geb bila nukta hakutaka kusimamishwa hata alitaka aelezeee yote bila kukwama ila bado mike alikuwa njia panda akijiuliza ni jambo gani lililopo katika ule msitu na lilitaka kujidhihirisha katika upande wao aijawa nahofu sana ila hakujua cha kufanya alimuacha Geb akijiandaana yeye kutoka njee wakimsubiri baadaya muda tayari Geb alikuwa amekwisha jiandaa na safari ya kumalizia utalii wao ilianza kulikuwa na utani mwingi kati yao ila Geb na Mike walikuwa kimya muda wote kila mmoja akitafakari la kwakehakuna aliyejari ukimya wa watuwale wawili na wote waliendelea  na stori zao za hapa na pale, Geb ndiye aliyekuwa wa mwisho katika msafara ule ambapo sasa walifika katika mto wenye maji ya ajabu ambapo Mike sasa alikuwa akiwaelezea chimbuko la maji yale

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " maji haya yalitokea katika chemchem ndogo iliyopo katika ile miguu ya yule mwanamke katika ule mti na kutembea taratibu kama mfereji mdogo wa maji na kufika mahali hapa ambapo pamekuwa kama kituo kikubwa " wakati mike akielezea kuhusu mto ule Geb akiwa mbali kabisa kimawazo ghafra akahisi mtu akimshika bega alipo geuka hakuwa mwingine alikuwa ni ule msichana aliyemsaidia jana yake akiwa ameshika koti mkononi



    "asante sana Geb kwa msaada wako nimekuja kukupa kushkrani na kurejesha koti lako japo jana niliondoka nalo bila ridhaa yako na kuhusu nilifata nini mahali pale au nilikutwa na nini mpka nikawa mahali pale nitskueleza siku moja"



    " kwani wewe unaitwa nani?" aliuliza Geb kitendo kilicho wafanya watu wote wamgeukie na kumtazamaalikuwa akiongea na nani ila waliweza kumuona Geb akiongea ila ilikuwa kazi kujua Geb alikuwa akiongea na nani katika msitu ule tena ni mtu ambaye wao hawakumuona walakumsikia



    "naitwa merisa na ndiye mmiliki wamsitu huu kwasasa" alijibu yule msichana na kupotea Geb alitamani kumuuliza swali jingine ila kabla hata ajaliweka vizuri swali lile kichwani mwake msichana yulealikuwa tayari amekwisha potea katika mboni za macho yake kutahamaki aliwakuta wenzie wakimshangaa.



    "vipi Geb ulikuwa ukiongea na nani?"aliuliza mike



    "yule msichana niliye waambia leo asubuhi na kanirejeshea koti langu" wote walicheka kwa dharau



    "Geb acha kuota ndoto za mchana bwana msichana huyo mbona sisi hatuja muona ?" aliongea marry huku akionyesha kutomuamini kabisaaa Geb juu ya kile akisemacho mike alitazama uhalisia maana ni kweli Geb hakuwa ameshika koti tangu wanatoka hemani ila bado swali lilikuwa kwa nini ni Geb peke yake na si mwingine au Geb amefanya kosa gani katika ule situ mpka yamkute hayo yote ila bado jibu halikupatikana kwa uwakika .







    kwa  upande wa Geb bado halikumuingia akilini eti anaota juu ya jambo lile mbona yy aliona kama ni keli lilikuwa likitokea mbele ya macho yake mbali na hilo hakutokea hata mmoja aliyeweza kuamini kauli zake, ila alijiuliza kama sio ndoto kwa nini alikuwa akimuona peke yake msichana yule Geb alijipa maswali mengi kiasi kwa siku  ile hakuweza kuandika taharifa yoyote katika msitu ule alianza kuwa na hisia mbaya juu ya yule mwanamke na hata ule msitu pia, Jioni ilipoingia watu waliwasha moto na kuketi wakiuzunguka na kupiga stori ni Geb pekee aliyeonekana kuwa kimya na wala hakutokea yyte aliyekapatwa na wasi wasi juu ya hali aliyokuwa nayo Geb na baada ya muda kuwa umeenda sana kila mmoja aliingia katika hema lake na kulala isipo kuwa Geb bado aliendelea kuchochea moto na kutafakari yote aliyokuwa akiyashuhudia kwa macho maangavu ila watu waliyaita ndoto mara Mike alitoka katika hema lake na kumkuta Geb akiwa bado ajalala.



    "Geb nini tatizo mbona umekuwa unakosa furaha na kuwa na mawazo mengi kiasi hiko?"swali la mike lilimtoa Geb katika msongo ule wa mawazo



    "hivi una uhakika katika msitu huu amna tatizo lolote?" aliuliza Geb akiashiria kutaka kujua kitu kilicho na uhakika zaidi



    "sikia Geb mimi sina muda mrefu tangu niajiriwe katika huu msitu nikiwa kama muongozaji wa watalii hii ni safariyangu ya nne tangu nianze kazi mahali hapa na hapo nyuma sijawahi kusikia tatizo lolote  lilelikijitokezakatika msitu huu kwa wenzangu hata kwangu kwani Geb emunieleze tuu ukwelinikitugani nilisema watu wasifanye wewe ukajaribu kufanya hata kam ulifanya kwa siri we niambie tuuusiogope maaana hili nitatizo sasa na namna ya kutatua tatizo ni ngumu mpaka ujue chanzo chake nikipi?" Geb alijarbu kurudisha akili yake nyuma kujua kitu gani alikifanya wakati aliambiwa asikifanye ndani ya msitu uleila akili yake ilikataa kabisa Geb hakukumbuka jambo lolote wakati ule



    "siku mbuki mike na sijui kwanini ni mimi tuu"



    "basi usijali tatizo litaisha tuu tumebakiza siku tatu kutoka ndani ya msitu huu, ila ningependa ukajipumzishe maana muda umeenda sana" Mike alimsihi Geb na kuingia ndani ndipo Geb na yeye alipozima moto na kuingia ndani kulala asubuhi ilipofika kilammoja aliamka na kujiandaa na safari isipokuwa Geb hakusikika akiamka katika hema lake ndipo walipo anza kugongea kwa nje kama ilivyo kawaida kuwa walisha mzoea Geb alikuwa akichelewa kuamka walianzakuongea mara



    "oooh huyu bwana na yeye amezidi sasa kila siku anachelewa kuamka ndo nini?"mwingine



    "aaah hii sasa imezidi mbona kurudishana nyuma huku sasakilasiku mtu mpaka uamshwe utafikiri aujui majukumu yako y akazi bwana" kila mtu alisema la kwake na kwakuwa walijaaliwa midomo basi hakukuwa na wakuwakataza wasiongee mike aliyekuwa akimgongea Geb sasa alianza kupatwa na hofu ikabidi apitishe mkonowake sehemu ya hema iliawezekuvuta kamba ya kufungulia mlango, mlango ulipo funguka akaingia ndani bahati mbaya Geb hakuwepo alijaribu kumtazama huku nakule ila Geb hakuonekana alitoka nje huku jasho jembamba likimtoka



    "vipi ameamka sasa huyo kibosile ?" aliongea marry



    "Geb hayupo humu ndani"alijibu mike baada ya kuona shauku yao ya kujua alichokawa anakifanya Geb ndani kiasi watu wana mgongea asikii, sasa walipatwana hofu juu ya jibu a Mike ilibidi waingie kuhakiki kwa macho yao na kweli hawakuweza kumuona Geb walitoka kila mmoja akiwa aelewi cha kufanya lilikuwa swala gumu na zito kwa upande wa Mike kwani kibarua chake kilikuwa na hatia ya kunyemelewa na nyasi baada ya mtalii mmoja kupotea tena katika mazingira yasiyo eleweka hivyo walikubariana kujarbu kuzunguka sehemu za karibu kumtafuta uwenda wange weza kumpata.



    **********************



    mwanga wa jua ulimpiga usoni baada ya sehemu kidogo ya hema kuwa wazi palikuwa kimya mahali pale akasimama na kwenda kutazama katika moja ya dirisha ilikuwatazama wenzie kama na wao walikuwa tayari wamekwisha amka cha ajabu na chakushangaza  hakuona hema lolote mahali pale wakati bado anaendelea kuangaza huku na kule alishitushwa na sauti ya mwanamke mrembo ambaye sura yake haikuwa ngeni machoni mwake mkooni alikuwa na trai iliyobeba chupa ya chai mkate kikombe pamoja na sahani



    "pole na uchovu wa usingizi Geb najua leo utakuwa umechoka sana kufuatiwana safari yetu ya jana ila usihofu nimekuandalia chai ya tangawizi ikuchangamshe mwili" yalikuwa maneno ya upole kutoka kwa mwanamke yule huku akiiweka trai ile karibu kabisa na kitanda , Geb alimtazama kwa muda huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio hakuelewa imekuwaje mwanamke yule kuwepo mahali pale



    "umefata nini mahali hapa kwani kosa langu nilipi mbona kilakukicha unafata nyayo zangu nimekukosea lipi?" hofu yakuwa uwenda yule msichana akawa sio mtu wa kawaida sasa ilimuingia kichwani Geb hakutamani hata kumsogelea alijuta hata ni kwanini alimsaidia siku ile hakuwa mwingine ila ni merisa CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "usijali Geb mimi ni kiumbe wa kawaida sina lengo baya na wewe na nimekutoa kule ulipokawa na wenzako kukuleta hapa kwa makusudi maana nina maongezi na wewe na kwa siku ya leo hawato weza kukuona "



    "na kwanini ufanye hivyo huoni kama utakuwa unawapa kazi ya kunitafuta pasi na kujua nilipo niache niondoke tafadhali " Geb aliukaribia mlango na kutaka kuondoka ghafra hema likawa giza na hata pale palipotegemewa kupitisha mwanga napo hapakuwa na msaada juu ya giza lile totoro sasa ilisikika saut tuu ya msichana merisa .



    "kwa hapa ulipo usijidanganye auwezi kwenda popote mpaka nitakapo ridhia mimi na niekuleta hapa sina ubaya na wewe ilanakumbuka kuna siku uliniuliza mimi ni nani na ilikuwaje ukanikuta mahali pale na leo ndo nilitaka kukueleza yote hayo maana najua una siku chache sana za kukaa ndani ya huu msitu" baada tu ya kumaliza kuongea maneno  hayo mwangaza ulirejea tena na Geb alisogea karibu na kitanda kusikiliza msichana yule, baada ya kuketi karibu na kitanda merisa alimimina chai katika kikombe nakumkabizi Geb



    "kwa jina kama nilivyokueleza hapo awali ninaitwa merisa hapo mwanzo panapo msituu uliitwa THE CANNADA MAGIC GARDEN ilikuwa zamani sana kabla hata ya mimi kuwepo katika ulimwengu huu lilikuwa nipori la watalii mbali mbali lililo milikiwa na mama waki ghana ambaye aliitwa GRORY DANIEL kwa sasani marehemu mama huyu aliamia mahali hapa na kununua eneo hili na kuanzisha sehemu ya utali wakati huo alikuwa akihitaji nguvu zaidi kwa ajili ya ulizi katika uharibifu wa mazingira ndani ya pori hili ndipo alipoafuta mtu atakaye weza kumpa ulinzi mkubwa ambao utakuwa tofauti na binadamu akapewa himaya ya majini, walio stahimili kukaa mwituni kwa kipindi chote cha maisha yao huitwa majini mwitu ambao chimbuko lao ni watoto wafu na maiti za watu wazima watakao kufa na kuzikwa bila kufuata sheria ya dini yoyote



     " aliweka kituo na kumtazama Geb kwa makini ambaye alikuwa akiweka fundo lake la pili mdomoni ilikumsikiliza vizuri



    "pori lilikuwa na kujengewa heshima kubwa sana na kila siku kulikuwa kukivumbuliwa vivutio mbali mbali ambapo watu wengi walipenda kwenda kupata upepo na familia zao paliponamsitu usiona wanyama ila miti yenye harufu nzuri na hewa safi kila kukicha siku moja pori lilipata wageni, wageni ambao walikuwa mke na mume ambao walikuja kupata upepo katika kipindi ambacho mke alikuwa mjamzito waliweza kufika mapokezi na kupewa maelekezo yote na kupatiwa msindikizaji walizunguka nusu ya pole na sasa walikuwa katikati ambapo mwanamama JULIETH alianza kuhisi maumivu ya tumbo nakushindwa kabisa kutembea alilalama kwa uchungu nakukaa chini alishika tumbo lake nakuliminya katika kitovu chake damu zilianzakumchuluzika na hatimaye akajifungua ila mtoto hakuwa amekamilika japo alikuwa aihema ila ilikuw bado kupata taswira halisi ya kibinadamu hawakuwa na chakufanya wakatafuta mti na kuichimba shimo refu na kukizika kile kiumbe na juu yake waka pandikiza mti ikiwa kama kumbukumbu kwao iwapo wata jaaliwa kurudi tena katika lile pori, na wao waliamua kurudi ilikumkimbiza julieth hospitali baada ya kuona alikuwa akitokwa na damu nyingi walipo fika hospitali julieth alipokelewa vizuri na kuingizwa katika chumba cha matibabu baada ya nusu saa daktari alitoka na taharifa zilizo kawa zimemshitusha mume wa julieth,EVANCE kuwa mke wake kipenzi julieth alikuwa ameagadunia baada yakupoteza damu nyingi na kuto pata huduma yoyote kwa muda wa siku mbili  baadaya taharifa hizo ikabidi arejee nyumbani ilikuweza kuandaa mazishi ya mkewe njiani akaata ajari mbaya ya kugongwa na gari na kufa hapo hapo,

    na huo ndo ukaw mwisho wa familia hiyo ambayo iliacha mali nyingi zisizo na mlithi kitendo kilichopelekea kila ndugu jamaa na marafiki kuchukua mali ya marehemu na kuifuja vibaya, Baaadaya miaka kadhaa kilekiumbe kilichokawa kimezikwa katika ule msitu kilichukuliwa na himaya ya jini mwitu na kuhifadhiwa mpaka kilipo pata taswira ya binadamu na kulelewa huko katika himaya ya kifalme ambapo mfalme aliishi na mke wake muda mrefu bila kupata mtotona ni kwa muda sana walitamani kupata mtoto  ndipo ilipoletwa taharifa juu ya mtoto aliyezikwa akiwa hai ndani ya msitu ule na kijana aliyekuwa akiwinda mfalme akachukua jukumu la kulea mtoto yule kama mtoto wake wapekee wa kumzaa na kumtoa katika uhalisia wake wa kibinadamu na kumfanya kuwa jini mwitu kisha kumpa jina ataitwa MERISA ."

    .................*************.................





    Alipumzika kwa muda ambapo sasa alikuwa akitembea tembe huku na kule akitafuta wapi aanze tena ilikumuelezea vizuri historia ya maisha yake mpaka pale alipo fika alifikaje kabla ajaendelea alikutana na swali kutoka kwa Geb



    "na huyo merisa unaye msemea ndo wewe?" merisa alimtazama  Geb kwa makini kisha akatingisha kichwa kwakukubaliana na wazo lake kisha akasema



    " ndio ndo mimi merisa  ambaye chanzo changu ni binadamu ila nimelelewa katika himaya  ya kishetani, wakati wote niliishi katika himaya ile nikijua mfalme ndiye aliyekuwa baba yangu mzazi na nilijua nilizaliwa katika himaya ya kijini  ila jambo lililokuwa likinishangaza nikuwana roho ya utetezi kila itakapotolewa amri ya kuadhibiwa binadamu, wakati ule mti uliopandwa juu ya shimo nililokwa nimefukiwa basi na mimi nilikuwa na kupewa windo ambalo lilikuwa ni mahali pale palipo na ule mti, na kadri miaka ilivyokawa inazidi kwenda mti ule ulikuwa na umbo la msichana na kupelekea watuwengi kuja kutembelea maajabu yale ya mti kuwa na umbo la mwanaadamu  haikuishia hapo tuu ila usiku wasaa sita nilikuwa kazini nikiwinda hvyo macho ya lile umbile lamwanaadamuhuwaka taa ilikuweza kunifanya nikione kila kinachotokea katika mipaka ya windo langu haliyakuwa nikiwanimetulia sehemu moja.



     niliendelea kuwa mtumwa katika himaya ile nikiwa kama mtoto wa mfalme mpaka siku

    uliyoletwa mbele ya machoya mfalme ukiwa kama mkosaji sikuweza kustahimili kuona unapewa adhabu kali kiasi kile ndiponiipojitoa kukutete na kujikuta wote tukipewa adha  bu ile ndipo nilipo kawa nikihoji uhalisia wa mfalme kunipa adhabu ile kwa binti yake kipenzi na wapekee nikaelezewa historia yangu kuwa mimi ni nani ndipo nikaamua kukutetea kwa kila hali ili uweze kutoka katika himaya ile kitendo ambacho kilinifanya nifukuzwe katika himayaile ya jini mwitu na mpaka siku ile ukaja kunikuta nikiwa mtupu mahali palena ni wewe pekee unaye stahiki na kuweza kuendelea kunisaidia katika upande wa utetezi ilibinaadamu wengine waweze kuelewa uhalisia wangu ila itabidi iwe siri baina yangu mimi na wewe mpaka nitakapo kuambia sasa nikotayari viumbe wajue ukweli wote kuhusu mimi cha kwanza inabidi uachane na mpenzi wako uliye naye haraka sana na unioe mimi," Hili lilikuwa jambo zito la lakushusha katika moyo wa Geb kumuacha anna bila sababu kwake ilikuwa na sawa na kuuchoma moyo wake kwa kisu nakuutia ndimu katika kidonda kile pasi na kuogopa maumivu atakayo yapata.



    Ilipofika jioni wote walirudi katika mahema yao pasi na mafanikio ya kumpata Geb tukio kama hili halikuwahi kutokea katika eneo hili tangu kuanza kwake kazi Mike hakuwahi hata kusikia tetesi za watu kupotea ndani ya msitu huu baada ya kwenda kutalii sasa Mike aliwaza kuwa na nguvu ya ziada pamoja na ulinzi ilibidi kufanya mawasiliano na mapokezi iliwaweze kujua nikitu gani watafanya mike wali wasiliana na dada wa mapokezi naye aka ahidi kuzifikisha taharifa kwa mkurugezi mkuu na baada ya nusu saa atakuwana suluhu na kama alivyo ahidi baada ya nusu saa aliweza kuwasiliana na mike tena na kumuhakikishia kutumiwa jopola watu wa usalama ilikuweza kumtafuta Geb akiwa hai na hata kufa na kujua pia kitu gani kilichopelekea kutokuonekana kijana huyo, sasa kila mtu alikuwa na hofu ndani ya nafsi yake juu ya kilichotokea sasa walianza kuona dalili za kutokuwepo na usalama katika pori lile kila mtu aliogopa waliunganisha mahema kwa usiku ule hakuna aliyetaka kulala mbali na mwenzie kwa uwoga kwani kila mtu alihisi uwenda ingefata zamu yake kupotea katika mazingira yasiyoeleweka .

            CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      ****************************************

    mambo yalikuwa mambo upande wa anna harusi ilishapamba moto na alikuwa akisubiriwa Geb pekee kila aliyemjua Geb na anna na mahusiano yao alitamani kuliona jambo lile likifanyika haraka maana ilikuwa pea yenye kupendeza machoni mwa watu kilakukicha  sio kwa mama na baba anna pekeehata kwa walio salia nje ya familia ile, anna alipata taharifa juu ya ziara  ya Geb kuwa walishafika robo tatu ya safari yao namuda simrefu Geb atakuwa akirejea tanzania rasmi kwa ajili ya harusi yao, na hiyo ndiyo ilikuwa furaha ya anna mwenyewe pamoja na wazazi wake.



    siku hii ilikuwa mbaya kwa upande wa anna ambapo alipata Email yenye taharifa za kupotea kwa Geb msituni tena katika mazingira ambayo hayakuwa mazuri mazingira usiku  watu wote wakiwa wamelala anna aliumia sana alijua tayari amekwisha mpoteza Geb wake japo juhudi za kumtafuta zinafanyika ilikuweza kumpata Geb  akiwa hai na hata amekufa taharifa zilisambazwa nchi nzima katika ma televisheni na hata katika magazeti, magazeti ya siku hii mengi yalikuwa na kichwacha habari kilichosema



    " MWANDISHI HODARI WA THE WORLD EVENT CONPANY LTD APOTEA KATIKA MAZINGIRA YAKUTATANISHA HUKO CANNADA KATIKA PORI LA MERISA THE MAGIC GARDEN"



    habari zilizo zidi kumchoma moyo anna kila kukicha habari zilizopelekea kuona ndoto zake za kuolewa na Geb zikikatika mipango ya harusi ilivunjwa mpaka itakapo patikana hatimayake hakuwa na ndugu Geb isipokuwa anna na wazazi wa anna na ndo watu pekee waliokawa wakijishughurisha katika kumuombea akutwe hai nakurejea salama kila kukicha anna alikuwa mtu waujifungia ndani rafiki yake Betha alikuwa akijamara kwa mara kumfariji na kumtia moyo ila ilikuw sawa na kazi bure maana akiondoka umuachia anna kilio kama ilivuokawa mara ya kwanza anna aliiyona hatima mbaya katika ndoto zake ila hakuwa najinsi ya kulizuia lolote lililo pangwa na mungu kutokea.



    Yapata wiki sasa Geb hakuonekana mahali popote katika msitu ule watalii wote walisitisha safari zao kwa mudailikuwa ni heka heka juu ya kuvumbua ukweli alikokawa Geb. Dav,John,Mary na Janeth walirudishwa katika hoteli waliyokawa wamefikia kwa ajili ya mapumziko ya muda huku bado shughuri za kumsaka Geb zikiendelea kila mmoja alikuwa na hofu ya uhai wa Geb hakuna aliyeweza kuamini kama Geb atakuwa salama mahali alipo kawa, baada ya kumtafuta kwa muda mrefu matumaini ya kumpata Geb akiwa hai au amekufa yalitoweka ndani ya jopo lile la watu lililotumwa kumsaka walirudi mapokezi wakiwa hawana cha kueleza kwa urefu ilibidi itambulike Geb amepoteza maisha hata kama mwili wake haukuonekana pahali napo habari zikatapakaa dunia nzima na magazeti mengi hasa yanchini Tanzania yalipambwa na kichwa cha habari kuwa



    " MWANDISHI HODARI WA THE WORLD EVENT CONPANY LTD ALIYEPOTEA KATIKA MAZINGIRA YAKUTATANISHA HUKO CANNADA KATIKA PORI LA MERISA THE MAGIC GARDEN ASADIKIWA KIFO BAADA YA KUTAFUTA NDANI YA PORI HILO KWA MUDA MREFU PASI NA KUPATIKANA habari zaidi UK...."



    zilikuwa ni habari zenye kumuumiza moyo anna hakuwa kuwaza kumpoteza Geb aliumia sana katika hilo John,Dav,Mary na Janeth walirejea tanzania pasi na kuwepo Geb ambapo walikuta watanzania wakiwa katika majonzi makubwa ya kumpoteza mwandishi yule mahirililikuwa pigo kubwa katika kampuni ya THE WORLD EVENT ila pigo kubwa zaidi kwa anna aliyekuwa akitarajia ndoa na Geb,yalifanywamaombolezo kwa muda wa wiki sasa na kuamua kuzika jeneza ambalo halikuwa na mwili.



    Kwaupande wake Geb aliruhusiwa na merisa kuondoka na kufanyiwa mipango yote ya safari mpaka kufika tanzania ila alipaswa kufata yote aliyoambiwa na merisa ilikuweza kumsaidia kama alivyosaidiwa yeye wakati yupo njiani alikuwa na mawazo mengi sana aliwaza namna atavyopokelewa na anna na jinsi atakavyo mueleza jambo hili na atakavyo lifikiria kichwa kilimuuma sana ila hakuwa na jinsi alijipa moyo yabidi nifanya hivyo ili anna asije nifikilia vibaya wakati tayari yupo ndani ya Tanzania alichukua taxi na kuomba apeekwe moja kwa moja maeneo ya mikocheni ambapo ndipo alipokawa akiishi njiani alikutana na msafara mkubwa wamaombolezo ya msiba walikuwamo watu wazito kama raisi wa jamuhuli ya muungano wa tanzania, waziri wa habari ,makamu wa raisi mkurugenzi wa THE WORLD EVENT COMPANY na wengine wengi ilikuwamo picha moja kubwa mbele ya gari lililo onekana kubeba maiti  kwa uwingi wa watu Geb hakuweza kuiyona vizuripicha ile watu walivaa T-shirt zilizondika maneno na kubandikwa picha ya marehemu kwa pembeni Geb alitamani kujua kuhusu mazishi yale ila ilikuwa ngumu sana kwa jinsi msongamano wa watu ulivyokawa walisimama pembeni kuupisha msafala ule upite kisha wakaendelea nasafari yake walipo fika mahali wakakuta foleni ambapo Geb aliomba kununua gazeti huku akijisemea mwenyewe " nina muda mrefu sijafatili kuhusu nchi yangu tanzania baada ya kuwa nje kwa muda kiasi naombaniangalizie gazeti la Nipashe laleo kama lipo hapo " alisema hivyo huku akimpa pesa dereva iliaweze kufungua dirish ana kumuangalizia gazeti alilokawa amelihitaji



    "na kama haukuwa tanzania kwamudamrefu utasikia mambo mengi ya kusikitisha siumeona ule msafara wa pale njiani watu wakienda kuzika?" alisemahuku akiuliza yule jamaa



    "eeeeeh kwani nani aliyefariki maana anaonekana mtu mkubwa kweli kweli?"



    "kiasi sio sana ila kifo chake kina utata sana maana alikuwa huko cannada kikazi na akapotelea huko huko mpaka leo hawajui kama yuko hai au amekufana ndo wameamua kuzika jenezalisilo na kitu ilikumaliza matanga waliyoakyaweka kwa muda wawiki tatu huku wakisubiria jibu kutoka kwa watu wa usalama waliopelekwa katika hilo pori alilopotelea" alimaliza kuongea hayo huku akimkabidhi gazeti tena habari yake ni hii apa hata katika hili gazeti soma utaipata Geb sasa alianza kuoata taswira juu ya yote aliyokawa akiyaona pale bila shaka alikuwa ni yeye aliongezea yule jamaa



    " na hata hivyo alikuwa na mchumba wake ambaye walitarajia kufunga ndoa baada ya jamaa kurudi cannada ila ndo hvyo kila kitu kilikuwa tayari alikuwa anasubiriwa arudi tuu "masikini hakujua ni maumivu kiasi gani alikuwa akiyapata Geb juu ya stori ile ambayo Geb hakuwahi kuwaza kutokea aliwaza kuto onana na yoyote yule ambaye alikuwa akijuana naye akamuomba dereva abadilishe muelekeo hakutaka kwenda tena mikocheni mahali ambapo ndo alikuwa akiishi,



    " sikia naomba unipeleke lodge yoyote nzuri hapa town achana na ishu za mikocheni kwanza " kauli ambayo ilimshangaza sana yule dereva



    "kwani vipi bro kuna tatizo?" wakati akiuliza hvyo aligeuka nyuma kumtazama vizuri kutahamaki aligundua alikuwa ni Geb ambaye alisemekana kufa na ndio muda ule ulikuwa wakati w mazishi yake ghafra akajikuta akisimamisha gari kwa uwoga alitamani kufungua milango alishindwa kila alipobonyeza kitufe cha kushusha kioo hakiku bonyezeka Geb alikuwaakitokwa na machozi kama mtoto



    "ni...ni..ni wewe kweli?" aliuliza yule dereva huku akiwa na kigugumizi kikali, Geb alifuta machozi kisha akamshika mkono



    " ndio ni mimi Geb ila sikufa ila nahitaji sana msaada wako ndugu yangu tafadhali usiniogope nitakuelezea kila kilichotokea mimi sikujua kama huku ndio habari zilizotokea laiti ningelijua nisingerudi tanzania ila tafadhali naomba msaada wako " Geb aliongea maneno ya busara na hekima na upole pia kiasi aliweza kumuweka sawa yule jamaa walielewana mwisho yule jamaa ambaye sasa Geb alimtambua kwa jina la Roby aliamua kumpeleka kwake ambako alikuwa akiishi mwenyewe na kumuomba aweze kumuelezea kila kilicho msibu katika maisha yake mpaka kuzushiwa kufa , hakuweza kumueleza kila kitu ila kwa ufupi

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " nilitekwa na himaya nisiyo ielewa katika ule msitu na kupewa baadhi ya masharti ikiwa kuachana na anna na kumuoa msichana wa kishetani nilipo kubaliana na ombi lao ndipo walipo nipa ruhusa ya kurejea tanzania ila kubwa kwa hivi sasa nilikuwa nahitaji kuonana na anna kwanza ilikumthibitishia kuwa nipo hai maana najua atakuwa anaumia sana." waliweza kushauriana mambo mengi ila wazo la Geb kumuoa anna lilikuwa pale pale ilatatizo lilikuwa ni wapi pakuanzia ili anna aweze kuamini kuwa yeye bado yuko hai.



    .......................************...................



    Bado msaada wa roby uliitajika zaidi na Geb ilikuweza kufanikisha Geb anaonana tena na anna na kuendelea kuishi maisha yao ya kawaida kama hapo awali,

    Yapata wiki sasa mazishi yaliyosadikika kuwa ni ya geb yalikweisha isha na maombolezo pia yalikwisha ila kwa upande wa anna ilikuwa ngumu sana kuziamini mboni za macho yake kwa kuzika jeneza na kuamini kuwa Geb wake aliyempenda kwa moyo wote ametoweka tena bila hata kumpa salamu za mwisho.

    Mawazo hayo yalimtesa sana anna kiasi akakonda mpaka kupungua uzito aliishi maisha ya kulia kila kukicha, alisali akiomboleza juu ya kifo cha kipenzi chake Geb.na alikuwa akifanya dhihara ya makaburini lilipozikwa jeneza la Geb kila apatapo upenyo wa kutoroka nyumbani.sasa alikuwa Roby ambaye alitakiwa kujua kila hatua atakayo kuwa akipitia msichana anna siku hii asubuhi na mapema Roby aliamka na kujiandaa na safari ya nyumbani kwa kina anna ambapo sasa ndio kilikuwa kibarua chake rasmi baada ya kukosa muda wakuweza kulitumia gari lake likiwa kama Taxi.



    Wakati amejibanza pembezoni kabisa na nyumba yam zee magesa ghafra aliwaona wasichana watatu wakitoka ndani na kusimama nje ya nyumba mara ikatokea bajaji wakapanda na kuondoka roby aliweza kuwajua miongoni mwa wale walio kawemo pale alimtambua vyema anna hasa kw sifa alizowahi kupewa na Geb kwani alikuwa mweupe kupita wote, mtaratibu kupita wote ila hata kwa uzuri wa sura yake pia alikuwa mzuri kupita wote aliokuwa nao katika safari ile, Baada ya Roby kugundua kuwa malikia aliyetumwa kumfatilia naye alikuwamo ndani ya bajaji ile ndipo alipo kanyaga mafuta gari yake na kuwafuata kwa nyuma huku akiwa muangalifu asijejulikana kama alikuwa akifatilia safari ile tangu awali baada ya mwendo wadakika kadhaa bajaji ilipaki pembezoni mwa nyumba ya hali ya kawaida ndipo wasichana wale watatu walishuka na kuingia ndani .



    Hazikupita sekunde tatu anna alitoka ndani ya nyumba ile huku akilia alipotoka nje alikuta bajaji ikigeuka na kutaka kuondoka nayo akaiwahi kuiita kisha kuanza safari “samahani unaweza kunifikisha sinza makaburini?”aliuliza anna kwa sauti ya uchungu “yaah… ni buku mbili tuu” alijibu Yule dereva na kumuacha anna akijipekua pekua katika mifuko yake mpaka wanafika mahali pakushuka anna alikuwa bado hajaiyona pesa yakumlipa dereva bajaji



    “Daah samahani kaka angu nina hofu pesa itakuwa nimeiangusha huko nitokapo”aliongea anna kwa sauti ya upole



    “dada mbona unacheza na kazi za watu sasa unataka nikusaidie vipi ? “alijibu kwa ukali kiasi anna akaogopa na kusimama kando kidogo kitu kilicho mpa uwazi roby kujua nini kilikuwa kikiendelea aliweza kuhisi anaakigombezwa na deleva Yule wa bajaji hvyo ilimbidi kushuka nakusogea karibu na pale alipo simama anna



    ”kulikoni dada angu?” ndio lilikuwa swali lakwanza kutoka kwa robybila hata ya salamu juu ya hali iliyokawa mahali pale



    “daaaah we kaka angu acha tuu nimedondosha pesa huko njiani wakati na kuja huku nimekosa kabisa pesa ya kumlipa huyu kaka”? Roby alimtazama Yule kijana kwa muda



    “ hata mimi nimfanya biashara ila sio kweli ikitokea umepakia abilia mmoja bila kumtoza pesa utakuwa umeua biashara hapana hiyo sio kweli?” aliingiza mkono wake mfukoni na kutoa kiasi kidogo cha fedha na umkabidhi Yule jamaa ilikuwa kama elfu ishirini hivi



    “nooo sio pesa nyingi kiasi hicho ni elfu mbili tuu”aliongea anna huku akizionea uchungu pesa zile zilizotolewa na msamalia mwema makaburini baada ya sekunde chache bajaji aliondoka wakabaki anna na Roby peke yao ambapo ana alimshukuru Roby kisha akaondoka zake kuelekea kunako kaburi la Geb  alishinda huko siku nzima akisali na kulia mchna kuchaa kigiza kilipoanza kujongelea mawingu ndipo anna alipopatwa na akili ya kurejea nyumbani kwa kuwa.hakuwana pesa hakutaka tena masemango akaamua kujikongoja taratibu ghafra taxi ndogo ilisimama kwa kasi karibu na miguu yake ilionyesha dhahiri ilikuwa ikimuwahi yeye mara kioo kilishushwa hakuwa mwingine alikuwa ni Yule Yule roby aliyemsaidia kulipapesa kule makaburini



    “wewe tena ?” alisema huku akimtazama vizuri”yap vipi unaelekea wapi nikusogeze?”



    “ammm … samahani kaka angu unaweza tuu ukaenda”



    “Hapana kwa hali uliyokuwa nayo kiubinadamu siwezi kukuacha uende mwenyewe naomba nikupeleke nyumbani”

    Aliomgea roby kwa upole na  kuonyesha busara zote ambapo anna alitathimini ukweli wa maneno yale na akalitazama anga jinsi lilivyozidi kutanda kiza akaona ni bora apate  usafirina kurejea nyumbani roby alimpeleka anna mpka kwao na kuhakikisha amepokelewa na wazazi wake.



       ************************************************************



    ASubuhi moja katika kampuni ya THE WORLD EVENT CO kuliandaliwa kikao adhimu na moja wa wakurugezi wa  kampuni hiyo ilikuweza kufanya uteuzi rasmi katika pengo aliloliacha Geb ambaye kwao alikuwa marehemu kwa kipindi kile, walikutana wafanya kazi wote na ma afisa utumishi ilikuweza kujadili swala lile,waliongea juu ya umakini wa Geb,ufanisi wake wakazi ubunifu na hata utafiti wake wa mambo, nidhamu na ucheshi pia vilimfanya kuvutiwa na kila mfanya kazi aliyefanya naye kazi lilikuwapengo kubwa sana kwa kampuni na ilihitajika maamuzi magumu juu ya kuliweka pengo lile katika hali ya kawaida ilishaurika kutafutwa tena muhandishi wingine mahiri ilikuweza kuziba pengo lile kikao kilipo isha kila mmoja alirejea sehemu yake ya kazi. Wakati wapo katika sehemu zao za kazi mara simu ya Dav iliita .



    “hallow” upande wa pili wa simu ile ulijibu “ hellow”



    “samahani ninaongea na Dav aliyekuwa rafiki yake Geb ?”bila kufikiria jibu lilikuwa



    “ndio”



    “Ok! Nitakuitaji land mark hotel sasa hivi kuna habari kumuhusu nahitaji kukupatia “alipomaliza alikata simu alibaki akishikwa na bumbuwazi asijue nini cha kufanya maneno yalimrudia rudia kichwani mwake zaidi ya mara mbili aliinuka na kusogea karibu na aliyekuwa rafiki yake john na pia walikuwa wakiishi nyumba moja tangu enzi za uhai wa Gabriel msigwa ambayewengi walipenda kumuita Geb wakilikatisha jina lake.



    “John kuna simu nimepigiwa hapa ya umuhimu kidogo nilikuwa naomba funguo ya gari na nyumba ukiwa unahitajia kurudi nitakufata”

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “mmmh mbona mapema hivyo salama huko kaka ?” aliuliza John akiwa na hofu juu ya hali aliyokuwa nayo rafiki yake lakini Dav hakuonyeha kujali lolote alichukua funguo zote mbili na kutoweka mpaka kunako landmark hotel alipowasili alipiga simu kwa  Yule aliyemuita mahali pale ambapo alielekezwa kuingia chumba namba 102 alifanya kama alivyoambiwa na kugonga mlango wa chumba hiko aliwakuta vijana wawili mmoja alikuwa anaangalia pembezoni kabisa karibu na dirisha kiasi hakuweza  kumona sura wa pili ni Yule aliyekuja kumfungulia mlango aliingia na kujitambulisha kisha akaketi huku aimtazama Yule kijana nadhifu dirishani ghafra akageuka alikuwa ni Geb.



    “Mungu wangu  GEB?” Alishtuka na kuanguka chini mashavu ya Geb yalijawa na machozi uso wake ulipambwa na huzuni alichokiwaza zaidi ni kuwa jinsi gani atamjuza anna kuwa yeye yuko hai





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog