Search This Blog

JINA LA URITHI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Jina La Urithi

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Njile alimlea mwanae kwa upendo wa hali ya juu,,japo hakuwa na uwezo mkubwa  kifedha....mumewe alifariki, siku ambayo alizaliwa mwanae wa pekee,,siku hiyo Mume wa Njile,,alidamka mapema na kumuaga mkewe kuwa anakwenda katika shughuli zake za kila siku kama ilivyo kawaida yake,,lakini Njile alishangazwa sana na kitendo hicho cha mumewe kudamka alfajiri, na sio kawaida yake!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Njile hakuwa na kipingamizi,,

    mumewe akachukua kibuyu kilichokuwa na maziwa ya ng'ombe kabla hajatoka ndani ya nyumba akasema,,"nakupenda sana mke wangu,,mtoto utakayemzaa, kama ni wa kiume jina lake ataitwa  Laula,,na kama ni wa kiume ataitwa Minze....aliongea maneno hayo kwa msisitizo,,,

    Njile,,akaonekana kuyazoea maneno hayo,,haikuwa mara ya kwanza mumewe kumwambia maneno hayo,,tena huwa anaongea kwa msisitizo,,,Njile akaitikia kwa kutikisa kichwa,,kisha akavuta shuka na kuendelea kuuchapa usingizi.

    Mumewe akatoka nje ya nyumba akafunga mlango na safari ya ikaanza kuelekea kusikojulikana,,

    maisha yake yote alikuwa anajishughulisha na ukulima,,alikuwa analima mashamba ya watu na kulipwa pesa baada ya kumaliza kulima mashamba hayo!

    baada ya masaa mengi kupita, kule nyumbani,hali ya Njile ikaanza kubadilika,,akaanza kuhisi maumivu makali,,chini ya kitovu,,maumivu hayo yalizidi,,kumbe siku za kujifungua zilikuwa zimetimia,,,Njile akajikaza akajikongoja kutoka nje ya nyumba huku akitambaa kama mtoto mdogo!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huohuo alionekana,,mumewe akiwa njiani kuruei nyumbani,,alipokaribia maeneo ya nyumbani kwake,,akastaajabu kumuona mkewe,akiwa anatambaa pale nje ya mlango,,..akaamua kutimua mbio na kumfuata mkewe,,akambeba na kumkimbiza kwanye kituo cha Afya, palikuwa na umbali kama kilomita tisa hivi.. alijitahidi kumbeba mkewe pasipokuchoka,,lakininkila dakika zilivyozidi kusonga,,hali ya Njeli ilizidi kuwa mbaya zaidi,,uchungu ulimuuma kupita kiasi....mtoto akazidi kuteremka na njia ya uzazi ikawa tayari imefunguka,,,akasema nilaze chini,,najifungua muda si mrefu,,hatutaweza kufika hospitali..mumewe akaamua kufanya kama alivyoambiwa na mkewe,,akamlaza chini,,Njile akaanza kusukuma mtoto kwa nguvu zake zote! hatimae mtoto akatoka tumboni,,,mara ghafla akastaajabu kumuona mumewe anajishika shingoni,,huku akikoroma,,kama kabanwa na kitu ndani ya koo...macho yakamtoka!!! mumewe akaongea kwa sauti ya chini,,akisema,,mtoto huyu aitwe LAULA, punde si punde akadondoka chini na kutulia tuli!

    mkewe akabaki na mshangao! akashtushwa na sauti ya mtoto wake,,ni baada ya kulia sauti kali,,,akajinyanyua akang'ata kitovu kilichokuwa bado kimeungana na kitovu cha mtoto,,kisha akakifunga fundo!

    alipomaliza akamtunika mtoto wake kwa khanga aliyokuwa amejifunga! khanga hiyo ilionekana kutapakaa damu!

    ghafla zikasikika sauti za ngurumo zilizoambatana na upepo mkali! kiza likazidi kutanda! Njile akaingiwa na hofu kupita kiasi,,

    ghafla wakajitokeza watu wawili kimiujiza,,watu hao walionekana kuwa wazee kupita kiasi,,ni mwanamke na mwanaume!

    wakati njile anatahamaki,,,ikasikika sauti ikisema...hakika wewe ni MKOMBI(mwanaume),,umetimiza kile kilichokusudiwa,,

    ni sauti ya mwanaume mzee kati ya watu hao wawili waliojitokeza kimiujiza,,kisha akaisogelea maiti hiyo akachomoa kisu na kukata kipande cha nyama katika mwili wa maiti hiyo.

    Njile akatamani kutimua mbio,,lakini alishindwa kwa sababu mwili wake haukuwa na nguvu hata za kumuwezesha kutembea,,akastaajabu kumuona mzee huyo,,akimfuata,,na kumnyang'anya mtoto kwa nguvu! pumde si punde yule bibi akazioiga hatua kumsogelea mzee huyo aliyekuwa kamshikilia mtoto mchanga,,Njile alipowatazama kwa makini wazee hao akashtuka kuona ni baba na mama wa mumewe,,kilichomshangaza zaidi wazee hao walikufa na wakazikwa miaka mingi iliyopita....wakati anatafakari nini cha kufanya mara ghafla!!!!

    TAHARUKI!!!!!!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mzee huyo akachukua kile kipande cha nyama ya maiti ya baba wa mtoto huyo mchanga,,pamoja akamlambisha mtoto huyo,,kisha akamsogelea Njile kwa hatua za taratibu,,lakini hakuonekana kama anatembea,,miguu yake ilikuwa haikanyagi kwenye ardhi! mzee huyo naye akasema,,"mtoto huyu aitwe LAULA.

    Njile akaingiwa na hofu lakini akajikuta anakuwa jasiri,,na kumpokea mtoto wake mchanga! alipomgusa mtoto huyo,,akahisi anaishiwa nguvu,,mwili wake ukawa regevu maradufu! akaona giza totoro limetanda mbele ya macho yake akapoteza fahamu,,,hakujua kilichoendelea....



    Baada ya masaa kadhaa kupita,,akajikuta yumo ndani ya nyumba ya mwanamke ambaye alikuwa anaishi jirani na nyumba ya Njile,,mwanamke huyo alimpa msaada baada ya kumkuta Njile akiwa kalala kando ya barabara ndogo,huku mtoto mchanga akiwa juu ya kifuachake,,alimuonea huruma,,akamshawishi mumewe wampe msaada mwanamke huyo,,ndipo wakashirikiana kumbeba na kumpakiza kwenye kiti cha baiskeli,,wakaondoka nae mpaka nyumbani kwao,



    Njile akauliza kwa mshangao! ,,"hapa ni wapi,,na nimefikaje hapa?

    mwanamke aliyempa msaada akasema,,"mimi na mume wangu tulikukuta ukiwa umelala kando ya barabara, na ulikuwa umemkumbatia mtoto wako kifuani..mwanamke huyo aliongea maneno hayo huku akimuonyesha mtoto...Njile akachukua mwanae na kuanza kumtazama kwa macho ya huruma,,akajikuta anatokwa na machozi! akainua uso wake kumtazama mwanamke huyo,,kisha kafuta machozi na kusema,,"asante kwa kuokoa uhai wa mimi na mwanangu,,Mungu akubariki!

    pumde si punde Njile akahisi maumivu makali sehemu zake za siri...kumbe wakati anamsukuma mtoto atoke tumboni alichanika sehemu zake za siri,,sasahivi kapata ufahamu na maumivu anayasikia!

    ye msamalia akauliza ,,"ilikuwaje mpaka ukajifungua katika mazingira hayo!? Njile akasita kuongea kwa sekekunde kadhaa kisha akasema,,"ndugu we acha tu, ni stori ndefu,,ambayo hata mimi sielewi imekuaje! kifupi ni kwamba uchungu uliponishika nilihangaika sana,,,nilijitahidi kutoka nje ya nyumba,,angalau nipate msaada lakini,,Mungu si Athumani,wala Mabula,,wakati natoka nje ya nyumba,,ndio wakati ambao mume wangu alikuwa anarudi nyumbani...baada ya kuongea maneno hayo,,Njile akasita kuendea kusimulia...akajikuta anatokwa na machozi...

    ye msamalia akaingiwa na wasiwasi,,akihisi huenda mume wa Nje alimoiga mkewe n akumtelekeza huko....hivyo msamalia huyo akawa na shauku ya kutaka kujua mume wa Njile yuko wapi? na ni sababu zipi zilizomfanya amtelekeze mkewe katika hali ile!

    Njile akafuta machozi kisha akasema,,"mume wangu amekufa..

    msamalia akashtuka! akauliza kwa mshangao,,kafa??

    Njile akaitikia ,,"ndio kauwawa!

    Msamalia huyo akazidi kustaajabu! akajisemea moyoni ,,"mara kafa mara kauwawa! bila shaka mwanamke huyu atakuwa kaathiriwa na mazingira yale aliyojifungulia,,lakini naimani akili zake zitakaa sawa,, na ufahamu wake utarejea...lakini cha kushangaza Njile alionekana kuendelea kulia mfululizo tena kwa uchungu wa hali ya juu! kitendo hicho kilimfanya msamalia huyo,,ahisi kunajambo ambalo halipo sawa! na linamtatiza Njile.

    akauliza kwa sauti ya unyenyekevu,,"niambie umeoatwa na nini? naomba usinifiche jambo hata moja,,ili nijue namna ya kukusaidia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    aliongea maneno hayo huku akimfuta Njile machozi yaliyokuwa yametapakaa kwenye mashavu.

    Njile akaendelea kusimulia,,"wakati tupo njiani kuelekea hospitali...uchungu ulinizidia,,na chupa ya uzazi ilikuwa tayari imeshapasuka,nikamwambia mumewangu anilaze chini nijifungue,,kwa sababu niliamini hatutofika mbali,,kutokana na hali yangu ilivyokuwa,,wakati na najifungua,,,nikashangaa mume wangu anahangaika,,kuvuta pumzi,,huku akiwa kashikilia sehemu ya shingo yake,,mwanzo nilihisi ni utani,,lakini kadri sekunde zilivyozidi kusonga akadondoka chini na kutulia tuli..

    ghafla wakajitokeza wazee wawili,,ambao ni baba na mama yake..lakini wazee hao walishakufa miaka mingi iliyopita! wakati Njile anaendelea kusimulia,,ghafla yule mzee akajitokeza ndani ya nyumba ya msamalia huyo! Nje aliweza kumuona mzee huyo,,akasita kuendea kusimulia,,macho yakamtoka na hofu ikazidi kuongezeka,,

    Ye msamalia akastaajabu,,kumuona Njile amebaki kimya huku macho yake yakitazama uoande mwingine kwa muda mrefu...akaamua kugeuza shingo yake naye aone Nje anatazama kitu gani kilichomfanya akodoe macho. alipogeuza shingo yake,ghafla mlango ukafunguliwa kwa pupa!!!

    KIZAA ZAA!!!!!





    akashtuka,,,akashika kifua chake upande wa moyo,,huku akipumua kwa haraka,,,kumbe Njile alikuwa katika dimbwi zito la mawazo,,,akikumbuka matukio yaliyotokea miaka sita iliyopita,

    na aliyefungua mlango si mwingine,,ni yule mtoto wake,,kwa sasa anamiaka sita...hizo ni kumbukumbu zilizomjia katika mawazo,

    Njile akauliza kwa mashangao! ,,"kulikoni mbona umefungua mlango kwa pupa?

    mtoto Laula akajibu,,"nimeona limtu linaniita, linatisha!

    Njile akashtuka akaanza kudadisi kwa kumuuliza maswali mtoto wake,,"anafananaje?

    Laula akajibu,,"ni mzee nilishawahi kumuona,,

    Njile akamtazama mwanae kwa macho ya umakini huku akisikiliza kile anachokiongea Laula.

    Njile akahisi kuchanganyikiwa,,akasema,,"mwanzo ulimuona wapi?

    kama ilivyokawaida ya watoto,,huwa wanaeleza jambo kama jinsi alivyoliona,,hapunguzi neno wala haongezi neno,,Laula akasema,,"kunasiku alikuja nyumbani usiku,,nikakuamsha lakini haukuamka,,akqsema eti ni babu yangu..akanichukua na kunipeleka hukooo!!!!



    Njile akashtuka! akajisemea moyoni,,"bila shaka yale mambo yameanza upya! lakini kwanini mimi tu?

    alijisemea maneno hayo kwa uchungu...kisha akamkumbatia mwanae,,ghafla Laula akauliza,,"baba atakuja lini? mbona harudi?

    Njile akajikuta anaangua kilio!

    kwa sababu alimdanganya mwanae kuwa baba yake amesafiri...alishindwa kumwambia ukweli wa mambo yaliyotokea miaka sita iliyopita hivyo miaka hiyo yote Laula anajua kuwa baba yake kasafiri,,huwa anamuuliza mama yake mara kwa mara kuhusu baba yake! lakini Njile aling'ang'ania msimamo wake kuwa baba yake Laula kasafiri.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

       ****BAADA YA MIAKA MINNE KUPITA*****



    Laula alitimiza umri wa miaka kumi(10)

    siku zilisonga na maisha yakaendelea,,lakini katika kijiji hicho kukawa na uvumi kuwa Laula ananguvu za kimiujiza,,watoto wa lika lake walishuhudia maajabu mbalimbali wakati wakiwa wanacheza na Laula....lakini hakuna aliyeamini maneno ya watoto hao! kadri miezi ilivyozidi kusonga Laula akawa tishio kwa watoto wenzake! hata shuleni walimu walimuogopa kwa sababu,,kila mwalimu aliyethubutu kunyanyua mkono wake kumpiga Laula,,basi mwalimu huyo,,anapoteza uhai usiku wa siku hiyo hiyo...

    pamoja na hayo yote,,Laula huyafanya hayo pasipo kujitambua,,na wakati anafanya matukio hayo,, huwa anapoteza kumbukumbu juu ya alichokifanya!

    failia ya Laula ikawa ni tishio la kijiji hicho,,,

    siku moja nyakati za usiku wa manane,, Laula alidamka kutoka usingizini,,lakini macho yake hakuyafumbua! akazioiga hatua kuufuata mlango,,ghafla akatoweka kimiujiza! akajitokeza kwenye eneo la makaburi,,akaendelea kuzipiga hatua na kulifuata kaburi moja lililokuwa katikati ya makaburi mengine! kaburi hilo linasadikika kuwa ni kaburi la Muanzilishi wa ukoo wao,,alizikwa miaka zaidi ya miamoja iliyopita,,na jina lake aliitwa LAULA,,na mrithi wa jina lake ni Laula huyu ambaye ni mtoto pekee wa mwanamke Njile!

    kumbe kuna siri nzito ambayo alikuwa anaijua Baba yake Laula...mbaya zaidi alikufa pasipokusema maana chimbuko la Jina hilo alilomrithisha mwanae wa pekee.



    ilikuwa hivi,,enzi za ujana wa baba Laula,,alikuwa anaugua ugonjwa ambao haikujulikana ni ugonjwa gani,,kumbe baba baba mzazi aliwahi kumtukana marehemu baba yake ambaye ni babu yake baba Laula,,na siku ambayo anakufa mzee huyo alisema,,daima kizazi chako hakitafanikiwa kuishi katika dunia hii,,aliongea maneno hayo na kukata roho papohapo...

    miaka ilizidi kusonga,,hatimae baba Laula akazaliwa,,,lakini aliishi na kufanikiwa kuoa  Lakini akaanza kuota magome ya miti katika mwili wake akapelekwa hospitali lakini haikufahamika anaumwa ugonjwa gani,,,ndugu zake wakaamua kumpeleka kwenye tiba mbadala wakampeleka kwa mganga wa kienyeji....mganga akasema,,mkitaka mtu huyu apone,,ni lazima akafukue kaburi la muanzilishi wa ukoo wake,,achukue jino la mbele katika fuvu la muanzilishi wa ukoo wake...ikalazimika afanye hivyo! siku hiyo akadamka usiku wa saa sita akaelekea makaburini! alipolikaribia kaburi hilo mara ghafla!!!!!





    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akahisi miguu yake imekuwa mizito kupiga hatua,,lakini akajipa moyo,,akalisogelea kaburi hilo,,punde si punde kaburi likafunguka akafanikiwa kuona mabaki ya mifupa ya muanzilishi wa ukoo wake,,akatumbukia ndani ya kaburi hilo,akachukua jino moja la upande wa mbele katika fuvu la muanzilishi wa ukoo wake!

    akatoka ndani ya kaburi hilo,,,ghafla akahisi mwili wake umekuwa mwepesi akapapasa mwili wake akafurahi kuona yale magome ya miti yametoweka katika mwili wake,,akaweka jino hilo katika mifuko ya suruali aliyokuwa kaivaa kisha akaondoka zake...

    akajisemea moyoni,,"mtoto wangu wa kiume nitamuita Laula,,hii ni kama shukrani yangu kwa muanzilishi wa ukoo wetu,,mtoto wangu nitamrithisha jina lake.

    baada ya miezi kadhaa kupita,,mkewe akashika ujauzito,,akazaliwa Laula.

    hiyo ni historia fupi ya chimbuko la jina Laula.



    **************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog