Search This Blog

JINI WA DARAJA LA SALENDA - 3

 





    Simulizi : Jini Wa Daraja La Salenda

    Sehemu Ya Tatu (3)



     ILIPOISHIA: Kila aliyemuona hakumdhania vibaya, aliacha eneo la bahari na kuingia makazi ya watu, alipokaribia maeneo ya nyumba ya mganga aliuona moto ukiwaka tena. Alikwenda kwenye nyumba ya jirani na kuomba kupumzika, kutokana na kuonekana mstaarabu alikaribishwa na kupewa kiti. Mwenyeji wake hakujishughulisha naye aliendelea na shughuli zake na kumuacha Kulani akitupia jicho njia ya kutokea kwa Mganga Njiwa Manga. SASA ENDELEA... Muda ulikwenda bila mganga kuonekana, kila alipopata wazo la kwenda kwenye nyumba ile alishangaa kuuona moto ukiwaka, lakini ulipotulia nyumba ilikuwa katika hali ya kawaida. Alijikuta yupo kwenye wakati mgumu akiamini kabisa ngoma ile ni nzito kwake kuchezeka. Kilichomchanganya zaidi ilikuwa ni kauli ya mfalme Barami Hudirud ya kuhakikisha anammaliza mganga

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     ndipo arudi, japo muda aliopewa ulipita. Kulani alipata pigo baada ya mwenyeji wake kutaka kuondoka, akiwa bado kichwa kinamuuma alimwambia: “Samahani kaka.” “Bila samahani.” “Nataka kuondoka kwenda pwani.” “Hakuna tatizo funga mlango wako mimi niache hapa nimekaa baada ya muda nitaondoka.” “Hapana kaka sikujui nimekukaribisha kibinadamu, lakini siwezi kukuamini kukuachia nyumba yangu, dunia haiaminiki siku hizi.” “Sawa.” Kulani alikubali kuondoka pale, lakini sehemu iliyokuwa nzuri kupaona kwa mganga ilikuwa kwenye nyumba ile iliyokuwa ikitazamana na ya mganga. Aliondoka kwa kuzunguka nyumba ile na kujigeuza haraka kuwa mjusi. Aliupanda ukuta haraka na kwenda kujificha chini ya bati bila kuonekana. Mwenye nyumba ile alishtuka na kuzunguka nyuma ili kupata uhakika kama kweli yule mgeni atakuwa ameondoka. Lakini ajabu alipozunguka nyuma ya nyumba iliyokuwa na uwazi mkubwa wa kumuona mtu kama anatembea kutoka pale, hakumuona mgeni wake. Alijiuliza kwa sauti: “Sasa atakuwa amekwenda wapi, mtu azunguke sasa hivi asionekane, mmh! Lisiwe jini lile, Mungu aniepushie mbali.” Kulani alimtazama na kutulia akiwa amejilaza kwenye ukuta chini ya bati. Baada ya kusema yale mwenye nyumba ile aliondoka na kumwacha Kulani palepale nyumbani bila kujua. Baada ya kuondoka, Kulani aliendelea kumsubiri mganga palepale ukutani chini ya bati katika umbile lile lile la mjusi kama atatokea Mganga Njiwa Manga amvae na kumuulia mbali. Alisubiri kwa saa kumi mpaka jioni ilipoingia ndipo alipomuona akiwa anamsindikiza mmoja wa wateja wake. Jini Kulani aliteremka na kurudi katika umbile la mwanadamu na kumfuatilia kwa nyuma bila ya mganga kujua. Nia yake ilikuwa kukutana naye wakati anarudi ili amvae. Taratibu alitembea kumfuata kwa nyuma mganga aliyekuwa mbele akitembea huku akizungumza na wateja wake. Njiani Mganga Njiwa Manga alianza kuhisi kama ardhi inatetemeka na mwili kuwa mzito, kitu kile kilichomfanya ageuke na kutazama nyuma. Alishtuka kukiona kiumbe cha ajabu kwa mbali kikija taratibu. Kwa haraka alichutama chini na kushika michanga huku akilikemea jitu lile ambalo liligundua limejulikana. Wakati Kulani akijitayarisha kumvaa Mganga Njiwa Manga baada ya kugundua amejulikana, kabla hajamfikia alirusha vumbi la mchanga lililomuingia machoni na kumpofua macho. Alipiga kelele za maumivu na kujipiga chini kwa hasira na kusababisha kishindo kizito kilichotikisa eneo kubwa la Bagamoyo. Kishindo kile kilisababisha watu waliokuwa karibu na sehemu kilipotokea waanguke na kupoteza fahamu. Nyumba nyingine zilipata nyufa kutokana na kushindo cha Kulani kupasua ardhi na kupotea. Baada ya robo saa hali ya eneo la Bagamoyo ilirudi kuwa ya kawaida. Baada ya kurudi hali ya utulivu Mganga Njiwa Manga alinyanyua alipokuwa ameangukia baada ya kurushwa na udongo uliotoka kwenye shimo alilozama jini Kulani baada ya kupofuka macho. Alimtuma mtu kwenda nyumbani kumletea dawa ambayo alikunywa na kujimwagia kichwani. Baada ya kuyafanya yale alikwenda hadi kwenye shimo lililokuwa limechimbika kama kumelipuka bomu. Sehemu ile aliweka dawa kisha aliondoka na kurudi nyumbani kwake. Alipofika nyumbani mwili ulikuwa umechoka sana, hakuweza kuendelea na kazi ya matibabu, aliwaomba wagonjwa wake apumzike baada ya kunusurika kifo toka kwa jini ambaye hakujua ametoka wapi. Siku ile hakufanya kazi yoyote, alilala mpaka siku ya pili huku akiviona viungo vyake vikipoteza nguvu. Hata alipolala hakuweza kujigeuza mpaka siku ya pili, kwake ulikuwa upinzani mkubwa katika kazi yake. Mara nyingi upinzani uliishia nje ya ngome yake, lakini hakikuwahi kiumbe chochote cha ardhini majini au angani kilichoweza kumdhuru. Pia katika kazi yake haikuwahi kutokea kiumbe kilichowahi kumvizia njiani kwa ajili ya kumdhuru. Wengi walivamia sehemu aliyokuwa akifanya kazi na kukutana na vikwazo. Lakini uwezo wa kinga yake ya mwili ndiyo uliomsaidia, bila hivyo angemalizwa na jini yule. *** Jini Kulani baada ya kuzama chini ya ardhi kwa kujipigiza kwa hasira, aliibukia pembeni ya bahari. Alitembea taratibu huku akipapasa ili kuingia majini. Baada ya kutembea kwa muda alibahatika kuyakanyaga maji. Pale pale alizama chini. Mfalme wa bahari alishangaa kumuona Mkuu wa Watwana Kulani amesimama mbele yake akiwa haoni. “Kuna nini tena kimekusibu mtwana wangu mtiifu?” “Mtukufu mfalme, safari yangu imekuwa mbaya.” “Kulani umefanya makosa, kwa nini jana hukurudi?” “Niliogopa mtukufu mfalme kurudi bila kutimiza ulichonituma.” “Umekitimiza?” “Hali yangu kama unavyoniona.” “Tatizo nini?” “Nimepofuka mtukufu mfalme.” “Lakini hujanijibu, umemmaliza?” “Sikuweza, yule mtu hata wewe sikushauri uende.” “Kwa nini?” “Amejidhatiti, ana nguvu za ajabu sijawahi kuona, ameizindika ngome yake haiingiliki, na yeye mwenyewe alichonifanya sitasahau mpaka nakufa.” Jini Barami Hudirud, mfalme wa bahari atakubali ushauri wa Kulani kuachana na Mganga Njiwa Manga?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hapana lazima niende, hawezi kushindana na nguvu zangu.” “Mtukufu mfalme, bado himaya ya chini ya bahari inakuhitaji lazima atataka kutumia nguvu za ziada kukumaliza. Nashukuru sikugusana naye ningeweza kupoteza maisha.” “Kwa hiyo tuwaache wanadamu watuchezee?” “Hapana, ila nguvu zinazidiana, yule mwanadamu ana nguvu za ajabu sana, nilijitahidi kuuzima moto alioutega kwenye himaya yake, nilishindwa kila nilipouzima na nilipotaka kuingia uliwaka tena nikajikuta kukipambazuka bila ya kuweza kuingia kwenye himaya yake. Ndiyo sababu ya kuchelewa kurudi na kuamua kubaki ili nihakikishe nammaliza akitoka kwake. Lakini haikuwa hivyo matokeo yake nimekuwa kipofu.” “Mmh! Nimekuelewa, basi mpelekeni akapate tiba.” Watwana wengine walimchukua Kulani na kwenda kumpatia tiba ya macho, baada ya kuondoka, mfalme alimgeukia mkewe aliyekuwa kimya akimuangalia Kulani kwa huruma. “Mke wangu umeona hali ilivyo, unanishauri nini kutokana na hali aliyorudi nayo Kulani?” “Mmh! Mume wangu hali inatisha, inaonesha wazi vita ni nzito, tukifanya mchezo tutakwisha, mpaka Kulani kusema hivyo ujue kuna kazi. Kwa nini tusiachane na mpango wa kumfuatilia huyo mwanadamu?” “Lakini mke wangu si unajua uwezo wangu? sijawahi kushindwa na kitu,” Mfalme alijitapa. “Naujua vizuri, hata Kulani anaujua lakini mpaka kakukueleza vile naomba umsikilize huenda kuna kitu amekiona kinaweza kukupotezea maisha kama utashindana na yule mwanadamu.” “Lakini kumbuka jini ana nguvu kuliko mwanadamu?’ “Lakini mwanadamu ndiye kiumbe mwerevu kuliko viumbe wote wa Mungu?” “Hilo nalijua lakini bado hawawezi kushindana na sisi.” “Mume wangu majini sisi hatuna ushirikiano, kuna majini wengine huwakinga mwanadamu na kuwafanya kuchanganya nguvu za kijini na akili ya kibinadamu lazima tu atakushinda.” “Kwa hiyo tufanye nini?” “La muhimu tuachane na mpango huo.” “Na suala la Balkis kuolewa na jini mwenzake?” “Hilo nalo ni gumu, tuendelee kumshawishi aweze kubadili mawazo na kuendelea na kazi ya kukusanya vizazi vya wanadamu na kutengenezewa dawa.” “Mimi nina hasira, jaribu kuongea naye wewe.” “Nitafanya hivyo jioni nitazungumza naye.” Walikubaliana mke wa mfalme azungumze na Balkis ili aweze kubadili uamuzi wake wa kung’ang’ania kuolewa na mwanadamu. **** Baada ya kuamka siku ya pili, Mganga Njiwa Manga bado mwili wake haukuwa na nguvu, wagonjwa wengi waliofika siku ile hawakupata huduma kutokana na hali yake. Ilibidi siku ile na yeye kutumia dawa za kujifusha na kunywa ili kujirudisha katika hali ya kawaida, baada ya kukumbwa na upepo wa jini Kulani. Kilichomshangaza kilikuwa rangi ya jini yule, alikuwa mweusi kama rami tofauti na majini wote aliowahi kukutana nao. Siku ya pili tangu akutane na dhahama nzito ya jini Kulani, aliendelea na kazi ya kutoa huduma kwa wagonjwa wanaotoka mbali. Baada ya kuingia katika chumba chake kutoa huduma, alitulia kwenye mkeka kisha aliweka ubani kwenye kitezo na kutulia kwa muda ili ajiandae kwa matibabu ya wagonjwa waliokuwa wameongezeka kutokana na kusimama kwa huduma yake. Ilikuwa ajabu baada ya moshi wa ubani kupanda juu, ulimfuata mbele ya uso wake na akaanza kuona picha asiyoielewa. Alikiona kiumbe cha ajabu kikitoka kwenye maji na ghafla kiligeuka na kuwa mwanadamu, kisha kilitembea taratibu toka kwenye ufukwe na kuingia maeneo ya watu. Baada ya kiumbe kile kilichojigeuza kuwa binaadamu kukaribia ngome yake, kilijigeuza umbile na kurudia lile alilotoka nalo chini ya maji. Ajabu kilipotaka kuingia kwenye himaya yake aliona moto ukiwaka kuzunguka eneo lake, ghafla kiumbe kile kilitoka mbio kurudi baharini na kuchota maji kisha kuja kuzima moto. Kiliendelea kuzima moto mpaka kulipopambazuka, kila kilichoendelea alikiona mpaka kupambana na jini lile. Hapo ndipo alipogundua jini lile lilitoka wapi, alicheka na kuona kinga aliyokuwa nayo ndiyo iliyomsaidia bila hivyo angekufa vibaya. Taratibu moshi ulipungua na hali ya ndani ikarudi kuwa ya kawaida, Mganga Njiwa Manga aliendelea kuweka tena ubani uliotoa moshi wa kawaida bila kuwepo na kitu kisichokuwa cha kawaida. Alimtuma msaidizi wake kuwaita wagonjwa. Nini kiendelea baada ya mganga kuonekana kudhibiti nguvu za kijini? Je, nini hatma ya Brighton katika chumba cha giza?



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    CHINI YA BAHARI Malkia Huleiya, mama mzazi wa Balkis alikwenda hadi chumba cha giza na kuomba Balkis atolewe, baada ya kutolewa alimpeleka kuoga na kukaa naye kwenye pwani ambayo huitumia kupumzika familia ya kifalme. Muda wote Balkis alikuwa akibubujikwa na machozi. Baada ya kukaa kimya kwa muda malkia Huleiya alimwita mwanaye. “Balkis” “Abee mama.” “Najua utatuona sisi wazazi wako makatili lakini unajua kabisa ubaya wa wanadamu na pia ni aibu jini kutoka katika ukoo wa kifalme kuzaa na mwanadamu.” “Mama kabla ya kuzungumza lolote naomba mumtoe mpenzi wangu na kama hamtaki awe huku naomba mumrudishe duniani.” “Hakuna tatizo.’ Alitumwa mtu kwenda kumtoa Brighton kwenye chumba cha giza na kumpa maji ya kuoga kisha kuwekwa kwenye chumba kizuri. Baada ya hatua zile mazungumzo yaliendelea. “Nina imani imefurahi?” Mama yake alimuuliza. “Siwezi kufurahi kwa vile sijatimiza dhamira yangu.” “Ipi?” “Ya kuolewa na mwanadamu.” “Hilo ndilo baba yako hataki kusikia.” “Lakini kumbuka tunachokifanya hakimpendezi Mwenyezi Mungu.” “Kipi hicho.” “Cha kuwafanya wanawake matasa.” “Ni kweli, lakini tunafanya hivyo kwa ajili yako.” “Kama unaona kufanya vile ni dhambi kwa nini msiniache na mpenzi wangu aliyekuwa tayari kukaa huku hata watoto wangezaliwa wangekuwa wetu.” “Mwanangu hujui vita ya wanadamu ni kubwa, huwezi kuamini kizazi kimoja kimechukuliwa. Kama kizazi kimechukuliwa je, mwanadamu watakubali aishi huku?” “Mwanadamu kanipenda mwenyewe wala sikumlazimisha.” “Lakini si ana mchumba wake?” “ Alimkana mbele yangu na kuwa tayari kunioa.” “Kwa sababu hakujua kuwa wewe ni jini.” “Hata alipojua alikubali ndiyo maana nimekuja kuishi nae huku.” “Lakini kumbuka baba yako alikuwa akikutegemea sana, ulichokifanya kimemchanganya sana.” “Lakini mama tatizo nini, kutafuta vizazi vya wanawake na kuzaa bila vita na wanadamu kipi bora, ona kama ulivyoniambia mkuu wa watwana Kulani kawa kipofu, kwa nini tusiachane na vita na wanadamu ili hamu ya mtoto apatikane bila kupata madhara zaidi.” “Uamuzi wako umemuweka baba yako katika wakati mgumu, kumbuka anakupenda kuliko kitu chochote, hakuota hata siku moja utamkosea heshima.” “Ni kweli najua baba ananipenda lakini alitakiwa kunisikiliza kuliko kuchukua maamuzi mazito, ona katumia nguvu nyingi matokeo yake Kulani kawa kipofu.” “Balkis mwanangu hakuna jini anayekubali kushindwa na mwanadamu.” “Ni kweli lakini kuna wanadamu nao huamini kabisa majini hawawawezi, kama wameweza kuchukua kizazi kimoja wanashindwa nini kuvichukua vyote?” “Balkis mwanangu kama ungekwenda kwa kitu tulichokutuma, nina imani kazi yako ingekuwa nyepesi sana kuliko ulichokifanya cha kuanzisha uhusiano na mwanadamu. “Kitendo kile kilituchanganya sana hasa baba yako, hata kuzungumza na wewe alishindwa na kunituma mimi. Anaamini hata matatizo ya Kulani chanzo ni wewe.” “Chanzo ni mimi kwa vipi? Wakati niliwakataza tuachane na vita na wanadamu lakini mkawa wabishi.” “Balkis mwanangu naomba uifanye kazi tuliyokutuma, tunaamini wewe ni mtoto mwenye heshima na usikivu. Nakuomba chonde chonde mwanangu msikilize baba yako.” “Mamaa kwa nini msinikubalie, kwani kuna ubaya gani?” “Kumbuka baba yako ni mfalme wa majini, ni aibu kwa mwanaye kuolewa na mwanadamu, ndiyo maana alikutuma kutafuta kizazi cha mwanamke ili kuhakikisha unapata tiba na kuolewa na jini mwenzako.” “Kwa hiyo nimrudishe Brighton duniani?” “Ikiwezekana.” “Mbona unasema ikiwezekana.” “Lazima tumuulize baba yako ataamua nini juu ya mwanadamu aliyejua siri yetu.” “Sasa naona unataka kuharibu mazungumzo, mmenikataza kuolewa na mwanadamu basi nimrudishe kwao.” “Lakini si atakuwa amejua siri yetu?” “Sasa mnataka kumfanya nini?” “Sijajua mpaka tupate maelekezo ya baba yako.” “Sikiliza kama nimekubaliana na uamuzi wenu wa kuachana na mwanadamu ili niendelee na kazi yangu ya kutafuta vizazi vya wanawake, naomba kwenye suala la kurudi kwao mpenzi wangu msiniingilie.” “Lakini kumbuka mwanangu chini ya bahari hii mwenye sauti ya mwisho ni baba yako.” “Hata awe na sauti gani uamuzi wowote tofauti na kumrudisha duniani hatutaelewana.” Nini hatima ya Brighton? Je, ataruhusiwa na mfalme kurudi duniani baada ya kuijua siri ya majini?“Mbona umefika mbali, ngoja nimpelekee taarifa hizi, atafurahi sana kusikia kuwa umekubali kurudi dunia kutafuta vizazi vya wanawake. Pia nitamueleza suala la mpenzi wako la kurudishwa duniani. Siamini kama atakuwa na maamuzi mazito ya kukuumiza.” “Mmh! Haya basi naomba nafasi ya kuzungumza na Brighton.” “Mmh! Basi ataletwa huku ili baba yako asijue chochote.” Baada ya kusema vile, Huleiya aliondoka na kumuacha Balkis akiwa amejilaza kwenye kiti cha uvivu. Japo moyo ulimuuma kumuacha Brighton mwanaume aliyeamini ndiye mume wa maisha yake. Bado hakuamini kama anaweza kutoa siri za majini. Lakini aliamini hakuwa akijua lolote katika siri za chini ya bahari kutokana na kufikia kwenye chumba cha giza. Baada ya muda Brighton alifikishwa bustanini na kukutana na Balkis, baada ya kukutana Balkis alimueleza hali halisi na yeye kuwa tayari kumrudisha duniani. Kwa upande wake Brighton alijikuta akizama kwenye dimbwi la mahaba ya Balkis na kumuomba atafute njia yoyote ili asirudishwe duniani. “Mpenzi kwa nini usimbembeleze baba yako ili tuishi pamoja?” “Hilo ndilo lilikuwa lengo langu lakini limeleta mtafaruku mkubwa ndani ya familia. Kwa hiyo nakuomba ukubali kurudi duniani ila sitakuwa mbali nawe.” “Mmh! Sawa lakini nitalikosa penzi lako.” “Ni kweli, lakini lazima nikubaliane na matakwa ya wazazi wangu.” “Sawa, sina jinsi,” Brighton alikubali kwa shingo upande. Malkia Huleiya baada ya kuzungumza na mwanaye alipeleka taarifa ya kikao kwa mumewe mfalme Barami. Alipofika alimkuta akimsubiri kwa hamu. “Karibu malkia wangu.” “Asante mfalme wangu.” “Mh, nijuze yaliyojiri huko?” “Mmh! Namshukuru Mungu yamekwenda vizuri.” “Kakubali?” “Ndiyo.” “Ooh! Afadhali.” “Lakini..” “Lakini nini tena malkia wangu?” Mfalme alishtuka. “Kuhusu yule mpenzi wake.” “Ana nini?” “Anataka arudishwe duniani.” “Ina maana hajui sheria yetu mwanadamu anayejua siri zetu huwa harudi tena duniani?” “Hapo ndipo penye tatizo.” “Tatizo gani?” “Mwanao anataka amrudishe duniani.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Haiwezekani.” “Amesema iwe isiwe lazima tumrudishe duniani.” “Yeye ni nani anayetaka kutulazimisha tufanye anavyotaka, siwezi kuwa na sauti mbili katika himaya yangu ya chini ya bahari.” “Lakini mume wangu..” “Hakuna cha lakini, aendelee na kazi ya kutafuta vizazi tena tutampangia kwa siku moja alete vingapi ili awahishe kutimiza lengo la kuolewa tuondokane na adha hizi.” “Mume wangu si vyema kila wakati kutumia nguvu, ifike wakati mwingine uwe unawasikiliza walio chini yako.” “Siwezi, nasema kauli yangu ni ya mwisho na maamuzi yangu yaheshimiwe,” mfalme alikuwa mkali. “Mume wangu hii itakuwa vita nyingine, kwa jinsi nilivyomsikiliza mwanao hawezi kukubali hili.” “Nitakachomsikiliza ni kumuacha hai, lakini si kumrudisha duniani.” “Mwanao amesema kwa hili hamtaelewana.” “Hebu kamlete hapa,” mfalme alisema kwa hasira. Alitumwa kijakazi kumfuata bustanini, Balkis alifika mbele ya baba yake kusikiliza kile alichoitiwa. “Abee mtukufu mfalme,” Balkis aliitikia akiwa amesimama mbele ya baba yake. “Kwanza nimefurahi kusikia umeweza kubadili uamuzi wako ila umeniudhi kwa kunilazimisha nifanye utakavyo.” “Baba kukulazimisha kitu gani?” “Kuhusu kumrudisha mwanadamu duniani.” “Sasa tatizo liko wapi? Mmemkataa asinioe sasa si nimrudishe nilipomtoa.” “Ina maana hujui sheria za majini, kama mwanadamu atajua siri zetu?” “Nazijua lakini huyu nimemleta miye hakujileta mwenyewe, wala hakuletwa kwa lipizo.” “Sheria za huku mwanadamu yeyote atakayeingia huwa hatoki salama, lakini kwa heshima yako hatutamuua bali ataishi huku milele.” “Kwa hilo baba sitakubali hata kwa kukatwa kichwa, ni mimi ndiye niliyemlazimisha kuja huku iweje mumshikilie?” “Hiyo ndiyo sheria ya huku kamwe haibadiliki.” “Nasema kwa hili itabadilika.” “Tunabisha?” “Hatubishani ukweli ndiyo huo, ikifanywa kinyume nikiondoka hapa sitarudi tena.” “Sooba,” alimwita mtwana msaidizi wa Kulani kwa sauti ya juu. “Rabeka mtukufu mfalme,” Sooba aliitika na kusimama imara mbele ya mfalme. “Mpeleke huyu kwenye chumba cha giza.” Balkis alichukuliwa tena na kurudishwa kwenye chumba cha giza. Nini kiliendelea?





     Baada ya mwezi mmoja na nusu kupita, Suzana akiwa ofisini kwake, muda mfupi baada ya kuingia alijikuta akiwa na mawazo mengi. Hiyo ilikuwa ni kutokana na maneno ya Mganga Njiwa Manga alipokwenda kwake jana yake kufuatilia suala la kurudi mchumba wake Brighton, aliyekuwa chini ya bahari katika chumba cha giza. Majibu ya mganga yalimkatisha tamaa tofauti na alivyofikiria kupatiwa matibabu kama ya Sharifa ya kuingizwa ndani ya maji ya bahari usiku wa manane. Alishangaa kuambiwa baada ya kukutana naye na kuchukua vitabu vyake vya uganga na kuvisoma kwa muda. Alipomgeukia alimueleza: “Kazi yako inanichanganya sana, mpenzi wako bado yupo chumba cha giza, inaonesha alitolewa na kurudishwa tena, kuna utata mkubwa juu ya hatima ya mumeo kutolewa chini ya bahari kurudishwa duniani.” “Mungu wangu! Si atauawa?” Suzana aliuliza. “Hawezi kuuawa, inaonesha uhai wake bado mrefu.” “Sasa itakuwaje ikiwa kila siku mambo yanazidi kuwa mabaya kwake, huoni kama maisha yake yapo hatarini?” “Ni kweli yapo hatarini lakini..” “Lakini nini mganga? Naomba msaada wako wa kumtoa huko.” “Nilikueleza toka siku ya kwanza kuwa ni vigumu kumtoa kwenye chumba cha giza kwani kila nikimtafuta haonekani. Kuna siku mchana nikiwa katika shughuli zangu nilikiona kivuli cha mchumba’ako, ilionesha ametolewa chumba cha giza lakini usiku nilipotaka kuifanya kazi ile sikumuona. “Kitendo kile kilinichanganya sana, hasa baada ya kuwa nimefika baharini na mbuzi wangu wawili, mweupe na mwekundu. Nilijikuta nikimtafuta tena lakini sikuweza kumuona. Niliamua kurudi nyumbani ili kuangalia upya, wasiwasi wangu nilidhani labda amekwisharudi duniani. “Nilimtafuta kila kona ya dunia mpaka chini ya udongo sikumuona, kila nilipomtafuta ilionesha bado yu hai, lakini alikuwa haonekani zaidi ya kiza kinene. Baada ya kuhangaika sana niliweza kukiona kivuli chake kwa taabu sana kikionesha yupo kwenye chumba cha giza. “Lakini kila nilivyojaribu kumvuta hakuonekana, huwezi kuamini kazi yako nimeifanya kwa muda mrefu bila mafanikio kuliko kazi nyingi nilizowahi kufanya. Wakati nikiendelea kuhangaika kutafuta nilishangaa kuona taarifa ikinionesha kuwa mumeo atatoka chini ya bahari bila kutumia dawa yoyote.” “Sasa atatokaje ikiwa bado ameshikiliwa na majini?” “Mara zote huongozwa na maandiko ya vitabu vya uganga ili niweze kumtibu mgonjwa, siwezi kukurupuka ndiyo maana dawa zangu huwa sibahatishi.” “Hakuna njia nyingine ya kunisaidia?” “Siwezi kukudanganya ila nakuhakikishia mpenzi wako atarudi bila dawa yoyote.” Suzana alikubali kwa shingo upande kwa kuamini sifa za mganga yule kuwa hashindwi na kitu ni za uongo. Aliona ni ajabu Brighton kurudi bila dawa yoyote. Baada ya kuondoka na kurudi nyumbani aliondoa tumaini la kurudi kwa mpenzi wake. Akiwa bado ofisini, katikati ya mawazo ya kukumbuka maelezo ya mganga yaliyomkatisha tamaa, baada ya kuonekana ameshindwa kumrudisha mpenzi wake na kuweka visingizio lukuki. Alishtushwa na sauti ya Sharifa aliyeingia ofisini kwake bila kumuona kutokana na kuzama kwenye dimbwi la mawazo. “Suzana vipi shoga mbona unaonekana upo mbali, una tatizo gani?” “Ooh! Shoga karibu.” “Mbona hivyo, una tatizo gani maana nimeingia bila wewe kuniona?” “Sharifa ina maana huyajui matatizo yangu?” “Nayajua lakini leo umekuwa tofauti na siku zote.” “Ni kweli.” “Tatizo nini?” Suzana alimtonya Sharifa aliyoelezwa jana yake na Mganga Njiwa Manga alipofuatilia kumrudisha duniani mpenzi wake. Kutokana na majibu yake juu ya mganga, ilionesha kabisa hakukuwa na uwezekano wa kurudishwa kwa mchumba wake. “Nina imani mzee yule si mganga, wala hana lolote! Anafanya kazi kwa kubahatisha, iweje aweze kumuona ashindwe kumrudisha? Kisa, oooh, nilimuona mchana usiku akapotea, mwongo mkubwa hana lolote yule,” Suzana alilalamika. “Lakini si alikueleza atarudi, tena kizuri hakukudanganya, au ulitaka akudanganye ili achukue

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    fedha zako?” “Kuna mtu gani anaweza kutoka kwa majini bila dawa au maombi?” “Muamini yule babu, analokueleza ndilo linalokuwa.” “Kipi cha kunifanya nimuamini zaidi ya sifa za kusikia?” “Basi shoga mguu huu ni wako.” “Una maana gani?” “Mambo yamejibu.” “Mambo gani?” “Kazi ya mzee Njiwa Manga.” “Kazi gani?” “Kweli Suzana umechanganyikiwa.” “Unafikiri kidogo, mtu siku zinakatika hakuna dalili zozote za kurudi kwa mpenzi wangu.” “Suzana kwa mganga Njiwa Manga si nilikwenda kwa ajili ya kurudishiwa kizazi?” “Ndiyo.” “Basi majibu yametoka.” “Ina maana wewe ni mjamzito?”

    “Ndiyo maana yake.” “Utani huo.” “Kweli shoga nimeamini yule babu ni mganga kweli.” “Kama ni hivyo basi hataki kunisaidia.” “Amekataa vipi wakati kakueleza ukweli juu ya ramli yake ilivyomuongoza. Ingekuwa hawezi kitu angekwambia japokuwa hajawahi kushindwa matatizo ya majini.” “Mmh! Kwa hiyo una uhakika kuwa Brighton atarudi bila kufanya dawa yoyote?” “Kama amekueleza atarudi ujue atarudi, si alikwenda baharini na mbuzi wawili. Kama angekuwa hataki kukusaidia asingeona umuhimu wa kwenda kujisumbua baharini saa nane za usiku.” “Mmh! Mimi nilijua labda ni njia ya kujitetea tu.” “Suzana, kwa taarifa nilizozipata kutoka kwa mama, Njiwa Manga kazi ya uganga huu ni mwaka wa thelathini na siyo watu wa hapa tu nchini, kuna watu wanatoka mbali kwa ajili ya kufuata tiba zake. Si hivyo tu, ameshachukuliwa sana na watu wa mbali kwa ajili ya kwenda kufanya matibabu, kuna kipindi alikuwa akiondoka zaidi ya mwaka, kitu ambacho baadaye alikiona kuwa si kizuri kwa watu wengi hukosa huduma zake na kuamua kutosafiri. “Si wewe hata mimi siku tulipokwenda baharini na hali iliyonitokea kisha kusema eti tayari kizazi changu kimerudi niliona ni uongo. Lakini hali iliyonitokea hivi karibuni na kufanya vipimo vyote na kujiona nina ujauzito nimekubaliana na mama kuwa, kweli mzee Njiwa Manga ni mganga wa kweli. “Kwa hiyo shoga yangu nakuomba uvumilie kama amekuhakikishia uhai wa mpenzi wako ni mrefu ni kiasi cha kuvuta subira, nina uhakika alichosema kitakuwa kweli.” “Mmh! Itabidi nikubali lakini moyo haunipi kabisa.” “Sikuzuii kufikiria hivyo, lakini amini usiamini mzee Njiwa Manga ni mganga wa kweli.” “Mmh! Haya,” Suzana alikubali kwa shingo upande. “Basi shoga mguu ulikuwa wako kukujulisha mzee Njiwa Manga amefanya mambo, punguza mawazo kila alilosema mganga litatimia mimi naamini Brighton atarudi bila ya dawa kama alivyosema.” “Kama alichokisema ni kweli nitampa zawadi kubwa.” “Hata mimi najiandaa kumpelekea zawadi kubwa, sijui hata nimpelekee nini?” “Utakachojaaliwa.” “Shoga baadaye.” “Sawa, wacha na mimi nianze kazi kidogo umeichangamsha akili yangu bila hivyo siku ya leo ingekuwa ngumu kwangu.” “Najua hata mimi baada ya kuona mabadiliko ya mwili moyo wangu ndipo ulipofunguka.” “Wacha na mimi nisubiri.” Sharifa alirudi ofisini kwake na kumuacha Suzana akijiandaa kuanza kazi za siku ile. **** Baada ya Balkis kupelekwa katika chumba cha giza, mfalme alionekana kuzidi kukasirika kwa kuona mtoto wake amemkosea adabu. Mkewe muda wote alikuwa ameinama bila kusema kitu, baada ya mwanaye kurudishwa chumba cha giza alimgeukia mumewe na kumuuliza kwa sauti ya ukali ambayo hakutakiwa kuitoa mbele ya mfalme. “Sasa ulinituma kufanya nini na umefanya nini?” “Kwanza punguza sauti yako ujue unaongea na nani?” “Nazungumza na mume wangu na aliyepelekwa katika chumba cha giza ni mwanangu,” bado malkia Huleiya hakushusha sauti yake. “Unabishana na mimi?” Mfalme aliuliza kwa sauti ya juu. “Sibishani na wewe kwa vile anayeteseka ni mwanangu.” “Lakini huoni kama amevunja sheria ya majini pia na wewe unanivunjia adabu kama mumeo na mfalme wako?” “Nimekuvunjia adabu kivipi wakati nakueleza kitu cha kweli?” “Kwa hiyo nivunje sheria kwa ajili ya mwanao?” “Kwani unataka aolewe na jini mwenzake au atoroke?” “Siwezi kuvunja sheria, majini wengine watanielewa vipi?” “Kwani si ni wewe ndiye uliyeiweka sheria hii kwa roho mbaya yako baada ya majini wengi kuwa na uhusiano na wanadamu. Umemkataza mwanao asiolewe na mwanadamu, anakuomba umrudishe duniani mpenzi wake hutaki. Kuna faida gani kuwa mfalme wakati huna mapenzi hata na familia yako.” “Kwa hiyo nawe unaungana na mwanao?” “Ndiyo na pia nasema hivi, Soobaaa,” malkia Huleiya alimwita mkuu wa watwana msaidizi kwa sauti kubwa. “Wa nini?” Mfalme Balami aliuliza. “Naam Malkia mtukufu,” Soba aliitikia akiwa amesimama mbele ya malkia. “Soba kamtoe haraka Balkis.” Soba alibakia amesimama na kusita kutekeleza amri hiyo kwa kuhofia kupingana na mfalme. Ni kweli kauli ya mganga Njiwa Manga itatimia? Mfalme wa majini atasalimu amri kwa mkewe?







    Soba alibakia amesimama kama sanamu, malkia Huleiya alipaza sauti yake tena: ”Soooba hujanielewa, kamtoe haraka Balkis chumba cha giza.” Bado Soba alibaki amesimama huku akisubiri mfalme ataamua nini baada ya mkewe kutoa amri ya kupingana na mumewe kwa mara ya kwanza. Siku zote alijua mwenye sauti ya mwisho ni mfalme, malkia sauti yake siku zote aliitoa kwa taratibu tena ya chini. Toka awe ndani ya jumba lile la kifalme hakuwahi kusikia amri kali ya malkia. “Sooooba, unanidharau?” Alimuuliza huku akiteremka sehemu ya juu alipokuwa amesimama pembeni ya mumewe. Soba bado alisimama kikakamavu kusubiri kauli ya mfalme aende au la, aliamini siku zote mke wa mfalme hakuwa na maamuzi tofauti na mumewe. Kitendo cha Soba kukataa kwenda kumtoa Balkis kilimuudhi sana malkia na kuona umevunjiwa heshima. Pembeni yake kabla hajafika kwa Soba alichomoa upanga uliokuwa kiunoni kwa mmoja wa walinzi wa nyumba ya mfalme na kulipunga hewani usawa wa shingo ya Soba. Wengi walijua anamtisha ili akubali kumfuata Balkis chumba cha giza alipofungiwa na mumewe. Soba naye aliendelea kusimama kikakamavu akisubiri kauli ya mfalme aliyekuwa amepata kigugumizi kwa kitendo cha mkewe kumvunjia heshima mbele ya wasaidizi wake na watwana. Panga alilopunga hewani bila hiyana lilitua kwenye shingo ya Soba na kutenganisha kichwa ni mwili. Kitendo kile kilimtisha kila mmoja aliyekuwepo pale, hata mfalme hakuwahi kuona hasira nzito ya mkewe kama siku ile. Kila mtwana aliyekuwa pembeni yake aliingiwa na mchecheto wa kuhofia maisha yake. Malkia Huleiya baada ya kuona mwili wa Soba ukianguka chini kama gunia na kichwa kikigaagaa chini, alishtuka kwa kuona ameua, alilitupa upanga chini kisha aliangua kilio na kukimbilia chumbani. Kila tukio lililotokea muda ule lilimshangaza kila mmoja. Mfalme alijikuta amebaki amesimama kama sanamu asielewe kilichotokea ni kweli au alikuwa akiota. Ulikuwa mwaka wa sabini na tano toka amuoe mkewe aliyekuwa msikivu na mtulivu pia mnyenyekevu kwa mumewe muda wote. Malkia Huleiya siku zote alikuwa kiumbe mwenye huruma na kumkanya mumewe pale anapotumia nguvu bila kutumia muda wa kufikiri katika maamuzi yake ya kutoa adhabu kwa majini yanapofanya kosa. Lakini siku ile kwa mara ya kwanza alifanya kitendo kilichomshtua kila mmoja aliyemfahamu. Hata adhabu anapotoa mfalme, yeye ndiye aliyesimama kutetea. Lakini kitendo cha kutenganisha kichwa na kiwiliwili cha jini hakuwahi kukifanya zaidi ya mumewe ambaye kila alipokosewa adhabu yake kubwa ilikuwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili. Kitendo cha mkewe kumuua mtwana mkuu msaidizi aliyekuwa akitegemewa na mfalme baada ya Kulani kuwa kipofu kilimfadhaisha sana. Alitoka sebuleni na kumfuata mkewe aliyekuwa amejitupa kitandani akilia kwa uchungu huku akijutia kitendo cha kumuua Soba. Japo Soba alionesha jeuri lakini moyoni alijuta kwa uamuzi mzito alioutoa kwa kumtenganisha kichwa na mwili. “Malkia wangu,” mfalme Balami alimwita mkewe kwa sauti ya upole. “Nisamehe mume wangu, nimeshindwa kuzuia hasira zangu, yote ni kwa ajili ya mapenzi mazito kwa mwanetu wa pekee Balkis.” “Najua mke wangu, lakini kitendo chako kimenifanya nijione nina mke mwenye

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    maamuzi mazito.” “Hapana sikutarajia kutoa uamuzi mzito kama ule, lakini yote umeyasababisha wewe.” “Hapana mke wangu, ningejuaje uwezo wa maamuzi yako bila kufanya vile?” “Si kwa kutoa roho ya kiumbe kisicho na hatia.” “Ile imeonesha kumbe hata nikiondoka au nikifa hakuna mtu wa kukuchezea, kwa kitendo kile Balkis namtoa kwenye chumba cha giza pia kumrudisha duniani mchumba wake bila masharti.” “Unasema kweli?” Malkia Huleiya alishtuka kusikia kauli ya mumewe. “Kweli kabisa, hii itakuwa kama zawadi kwa ujasiri uliouonesha mbele yangu.” “Asante mume wangu kwa uamuzi wako uliorudisha furaha yangu.” “Si kurudisha furaha yangu tu bali kuendelea na msimamo huo huo ili kuongeza heshima ndani ya himaya yangu.” Baada ya makubaliano alitumwa kibaraka kwenda kumtoa Balkis kwenye chumba cha giza lakini aligoma kutoka kama hawatamuachia Brighton. Waliamuliwa kwenda kuwatoa wote, walifanya hivyo na Balkis alikubali kutoka ndani ya chumba cha giza. Pia alitoa masharti kuwa, kabla ya kuzungumza lolote wahakikishe Brighton anatolewa chini ya maji na kurudishwa duniani. Kwa vile uamuzi ulikuwa amepitishwa ombi lake halikupingwa na baba yake. Lakini kabla ya kurudishwa duniani Brighton alipewa masharti na mfalme kuwa siku atakayoitoa siri ya majini ndiyo siku ya mwisho ya uhai wake. Baada ya kukubaliana na masharti, Brighton alisindikizwa na watwana kumi baada ya kumfikisha pembeni mwa bahari walimlaza pembeni. Ubaridi wa alfajiri na maji vilimfanya Brighton ashtuke na kujikuta amelala ufukweni, miguu ikiwa majini na mwili nchi kavu. Baada ya kunyanyuka alipokuwa amesimama kwa mshtuko. Aliifahamu sehemu ile ilikuwa ni eneo la daraja ya Salenda. Baada ya kujinyanyua alipokuwa amekaa, alitembea kuelekea barabarani ili apate lifti ya kumrudisha kwake. Je, kurudi kwa Brighton ndiyo mwisho wa Balkis kuchukua wanaume wa kibinadamu?

     Brighton alitembea kusogea barabarani kwa mwendo wa taratibu kutokana na mwili wake kukosa nguvu. Alikuwa akitembea kwa mwendo wa kuyumba yumba hadi alipofika chini ya mti uliokuwa pembezoni mwa barabara na kuuegemea kutokana na kuishiwa nguvu. Suzana akiwa kwenye gari lake akielekea kazini, alishtuka kuona kitu ambacho hakukitegemea kwa muda ule. Roho ilimwambia aamini kitu anachokiona lakini akili ya kawaida ilikataa kwa kuamini kitu kile. Baada ya kuvuka eneo lile bado roho ilimwambia kuwa kitu alichokiona ndicho chenyewe. Alisimamisha gari na kuliegesha pembeni, kisha aliteremka kwenye gari na kurudi sehemu alipomuona mtu aliyemfananisha. Alitembea taratibu hadi sehemu ile alipokiona kitu alichokifananisha. Brighton alikuwa kama mtu aliyelewa pombe kutokana na kuzidi kuishiwa nguvu. Suzana alipomkaribia, alipunguza kasi ya mwendo wake zaidi huku akimkazia macho mtu yule, alipomsogelea karibu aligundua aliyekuwa mbele yake ni kipenzi chake Brighton. “Brighton,” alimwita kwa sauti ya juu japo hakuwa mbali naye. Brighton alinyanyua kichwa na kumtazama aliyekuwa akimwita, macho yake yaliona maluweluwe japo alimfahamu aliyekuwa mbele yake. “Brighton,” Suzana alimwita tena huku akiogopa kumgusa. “Suzana,” Brighton alimwita baada ya kuitambua sura ya mpenzi wake. “Ni wewe Brigton?” “Ni mimi Suzana umejuaje kama nipo hapa?” “Ha! Siamini,” Suzana alimvamia Brigton na kumkumbatia kwa furaha. “Ni mimi mpenzi wangu,” Brighton alisema huku akitokwa na machozi. “Hapana Brighton, twende nyumbani,” alimshika mkono na kwenda naye kwenye gari. Suzana aliligeuza gari na kurudi nyumbani kwake kwa kuwa alijua nyumbani kwa Brighton kusingekuwa katika hali ya usafi baada ya nyumba kukaa kipindi kirefu bila ya matunzo. Alipofika nyumbani alimtengea maji ya kuoga, kisha akamtayarishia chakula. Baada ya kula Brighton alionekana kuwa na uchovu, aliamua kujilaza na usingizi mzito ukamchukua. Suzana alijikuta akiahirisha kwenda kazini ili aweze kuwa karibu na mpenzi wake aliyemtafuta kama maji kwenye ardhi kame. Alijikuta akiyakumbuka maelezo ya mganga Njiwa kuwa, Brighton angerudi bila tiba yoyote, hamu yake kubwa alitaka kujua mpenzi wake alikuwa wapi na aliishi maisha gani. Alijikuta akisahau hata kutuma ujumbe kazini kuwaarifu mabosi wake kama amepata dharura, muda mwingi alimuangalia mpenzi wake aliyekuwa amelala. Alimpapasa akiwa haamini kama kweli mtu aliyekuwa amechukuliwa na majini angeweza kurudi salama. Akiwa katika dimbwi la mawazo simu yake iliita. Alipoangalia juu ya kioo aliliona jina la Sharifa. “Haloo Sharifa.” “Suzana, upo sawa?” “Nipo sawa.” “Mbona hujaonekana kazini?” “Huwezi kuamini yaliyosemwa yametimia?’ “Yepi hayo?” “Brighton amerudi.” “Acha utani!” “Kweli kabisa na sasa hivi nipo pembeni yake.” “Suzana hebu acha kunirusha roho.” “Sharifa, naamini kabisa mzee Njiwa Manga ni mganga wa kweli.” “Si ulikuwa unamuona tapeli.” “Wee dada wee, kuchanganyikiwa kubaya.” “Kwa hiyo kazini itakuwaje?” “Naomba uniombee ruhusa kuwa naumwa nitakuja kuchukua ‘sick sheet’ baadaye.” “Mmh! Huwezi kuamini furaha niliyoipata leo haina kifani ili kujiridhisha na maneno yako nitaomba ruhusa kuja kumuona shemeji.” “Njoo dada umuone, huwezi kuamini amerudi amenenepa na kupendeza.” “Basi nakuja na sick sheet yako kabisa.” “Utakuwa umefanya jambo la mbolea.” “Basi nakuja,” Sharifa alionekana kuwa na mshawasha wa kumuona Brighton. **** Baada ya kutolewa kwa mpenzi wake chini ya bahari, Balkis alifurahi sana na kukubaliana na wazazi wake kurudi duniani kutafuta tena vizazi. Kitendo cha kukubali kulimfanya mfalme afanye sherehe kubwa ya kumuaga kwa mara ya pili. Sherehe ilifanyika juu ya bahari. Majira ya saa saba za usiku Balkis aliagwa eneo la bahari na kuingia duniani kwa mara nyingine tena. Aliondoka eneo lile kwa kutembea taratibu pembeni mwa barabara eneo la Daraja la Salenda kuelekea maeneo wanayoishi binadamu. Alipokaribia njia panda ya Masaki aliona gari dogo likisimama ghafla na kuteremka mwanamke na baadaye akafuatia mwanaume. Balkis amerudi tena duniani, nini kitatokea?





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakutaka kujionesha kwao, alisimama pembeni yao aone kuna nini. Cha kwanza kilichomvutia kilikuwa tumbo lililoonesha ujauzito la mwanamke aliyetoka kwenye gari. Kingine kilikuwa sura na mvuto wa mwanaume aliyefuatia. Mwanamke alionekana mwenye hasira sana kutokana na maneno yake. “Umenifuata ili iweje? Nimekwambia niache na maisha yangu na ujauzito huu nautoa.” “Lakini mbona umefikia huko mke wangu?” “Wewe si unaniona mimi si mwaminifu, basi kwa taarifa yako kuanzia leo achana na mimi.” “Mke wangu mimi mumeo nina haki ya kukuuliza jambo lolote linalokwenda kinyume na maadili ya ndoa.” “Kama umeniona nimetoka nje ya maadili ya ndoa si uniache.” “Siwezi kukuacha kwa vile bado ni mke wangu.” “Kwani ndoa lazima, ukiona hivyo ujue sina shida na wewe.” Mwanamke alionesha jeuri kwa mumewe, Balkis alitulia ajue mwisho wake. “Mke wangu bado tuna nafasi ya kulizungumza hili,” mwanaume alimbembeleza mkewe. “Ngoja nikueleze kitu, ujauzito huu sio wako na mwenye ujauzito huo utamuona muda si mrefu.” “Mke wangu umefikia hivyo?” “Ulikuwa hujui?” “Usifanye hivyo mke wangu bado nakupenda sana.” “Mimi sikupendi,” mwanamke alisema huku akifunua simu na kupiga namba, alimsikia akizungumza. “Eeh... nipo njia panda ya Masaki... njoo utanikuta.” “Mke wangu unampigia simu nani?” “Mume mwenzio anayejua kulea asiye na gubu kama wewe.” “Mke wangu ni maneno gani hayo?” “Najua litakuuma na mwaka huu wako, kama ulimwacha mkeo kwa ajili yangu sasa imekula kwako.” Maneno yale yalimchoma sana Balkis aliyekuwa amesimama pembeni yao akifuatilia mazungumzo yale. Alimuonea huruma mwanaume aliyekuwa akimbembeza mwanamke mpaka kumpigia magoti na machozi yakimtoka. Alitamani kuingilia ugomvi ule lakini hakuna ambaye angemuelewa kwa muda ule kutokea mbele yao. Alitulia kufuatilia mazungumzo yale bila kuzungumza chochote, mwanaume akiwa bado anaendelea kumbembeleza mkewe, gari aina Toyota VX lilisimama pembeni ya gari la wanandoa wale. Baada ya kusimama aliteremka mwanaume mwenye mwili uliojengeka kimazoezi aliyekuwa amevaa bukta na fulana ya mikanda. Yule mwanamke alimsukuma mwanaume aliyekuwa amepiga magoti na kumfuata aliyekuja na VX. “Vipi Sweet?” aliuliza yule mwanaume. “Si huyu ----- ndiyo anayeniwekea usiku.” Walizungumza wakiwa wamekumbatiana pembeni ya mwenye mke aliyekuwa bado amekaa chini baada ya kusukumwa na mkewe. Kitendo kile kilimtoa machozi Balkis na kuapa kuwashikisha adabu. “Pole sweet, twende zetu.” Walishikana mikono na kwenda ndani ya gari na kumuacha mwanaume akilia kwa uchungu huku akizungumza maneno yaliyokwenda na upepo lakini Balkis aliyasikia. “Kweli mwanamke shetani yaani yote niliyokufanyia umeniona sifai, nimekosana na familia yangu kwa ajili yako. Mwisho unanivua nguo mbele za watu, sioni faida ya kuishi bora nife.” Kauli ile ilimtoa machozi Balkis na kuona jinsi gani wanawake wanavyoweza kuwaingiza wanaume kwenye matatizo. Alimuona yule mwanaume kama mtu aliyechanganyikiwa akienda ndani ya gari na kutoka na kipande cha kamba ili ajinyonge. Alisogea kwenye mti wa pembeni na kuifunga ile kamba, akatafuta tawi zuri ambalo alifunga kamba ili ajinyonge. Kabla hajajitundika Balkis alijitokeza mbele yake, jamaa alishtuka kumuona mwanamke mzuri kasimama mbele yake usiku ule wa manane. Alipomuona alisogea pembeni ya kamba ili Balkis asijue kama alikuwa anataka kujinyonga. “Mudy kwa nini unataka kujiua?” Balkis alimuuliza. Balkis atamuacha Mudy ajiue nini adhabu ya mke wa Mudy? Kuyajua yote tukutane Risasi Jumatano. Mudy kama alivyoitwa na Balkis alishangaa kuona mwanamke mzuri mbele yake usiku ule tena akimfahamu kiufasaha. “Umenijuaje?” alimuuliza. “Kukujua si muhimu kuliko kujibu swali langu kwa nini unataka kujinyonga?” “Nani kakwambia?” “Mudy niambiwe na nani wakati naiona kamba ikining’inia?” “Basi tu nimeamua.” ”Uamue nini wakati umekataliwa na mkeo.” “Wewe umejuaje?” “Kwani uongo?” “Hata kama si uongo wewe umejuaje na usiku kama huu unatoka wapi huogopi?” “Mudy si muda wa kutaka kujua nimejuaje au natoka wapi? Unataka kuniambia wanawake wamekwisha mpaka umng’ang’anie mwanamke asiyekupenda?” “Sio kumng’ang’ania, bali kanitia umaskini wa kutumia fedha nyingi kwa ajili yake.” “Sikiliza Mudy, ulitakiwa kumshukuru Mungu kwa kukuonesha hili mapema, au ulitaka ufilisike kabisa ndiyo akuache.” “Kama hivi nimekosana na ndugu na jamaa zangu kwa ajili yake wakisikia ameniacha nitakuwa mgeni wa nani?” “Sikiliza Mudy, hakuna mtu anayechukiwa milele, kama utaomba msamaha watakusamehe.” “Mmh! Kwangu ni ngumu, kuwa na mwanamke yule niligeuka adui wa familia, wote waliniombea mabaya. Leo wasikie si utakuwa sherehe, kwa vile hunijui sikujui kwa nini usiniache nitimize dhamira yangu?” Mudy alimuomba Balkis amuache ajiue. Balkis atamuacha Mudy ajiue nini adhabu ya mke wa Mudy?

     “Sina budi kufanya hivyo.” “Sikiliza Muddy, ulitakiwa kumshukuru Mungu kwa kukuonesha jambo hili mapema, au ulitaka hadi ufilisike ndipo mkeo akuache?” “Nimekosana na ndugu na jamaa zangu kwa ajili yake, wakisikia ameniacha nitakuwa mgeni wa nani?” “Sikiliza Muddy, hakuna mtu anayechukiwa milele, kama utawaomba msamaha ndugu na jamaa zako watakusamehe.” “Mmh! Kwangu ni vigumu, kwa kuwa mwanamke yule alinifanya niwe adui wa familia, wote waliniombea mabaya. Leo wakisikia si itakuwa sherehe, kwa vile hunijui sikujui kwa nini usiniache nitimize dhamira yangu?” Muddy alimuomba Balkis. “Inawezekana wewe ndiye hunijui lakini mimi nakujua vizuri, toka ulipoanza maisha ya shida, hadi pale mpenzi wako wa kwanza alipoiba fedha kwao zilizokufanya upate utajiri na kukuvimbisha kichwa kwa dharau na kukufanya uwatelekeze mkeo na mtoto wako. “Mkeo kwa aibu kutokana na kuidharau ya familia yake, baada ya kumtelekeza aliamua kunywa sumu pamoja na mtoto wake. Kwa vile ulikosa shukrani wala fadhila, kifo cha mkeo na mtoto wala hakikuugusa moyoni mwako, ukaamua kuendelea na maisha yako na mpenzio mpya ambaye mlifunga ndoa ndani ya wiki tatu baada ya vifo hivyo. “Fedha zilikupa jeuri na kudharau wazazi na nduguzo waliokueleza tabia chafu za mkeo, kwako uliona kama wanaleta fitina ili muachane. Lakini ukweli uliuona baada mambo kuanza kukuendelea kombo, mke uliyemuoa tabia yake ni kuharibu ndoa za watu baada ya kukufilisi mwisho wake ndiyo kama ulivyokuwa ukitaka kufanya. “Lakini kwa tabia hiyo nitawakomesha, siwezi kuona familia zinahangaika kwa ajili ya upumbavu wa watu wachahe,” Balkis alisema kwa sauti ya hasira. “Kwani dada wewe ni nani na utawakomesha vipi?” “Utajua muda si mrefu.” “Samahani dada yangu wewe ni nani maana unanijua vizuri kuliko hata watu wangu wa karibu.” “Naitwa Balkis.” “Hii siri yangu nani kakwambia?” “Narudia tena usitake kumjua aliyeniambia,zaidi ya kujua ubaya wa mtu uliyekuwa naye. Kwa mchezo wake ndoa yako ni ya tano kuvunjwa na yeye na kila alipopita aliacha msiba, ningechelewa kidogo jina lako lingebaki historia midomoni mwa watu.” “Mmh! Wewe huku unatoka wapi usiku huu?” “Kwetu siyo mbali naomba ikiwezekana ukalale kwa vile najua huwezi kuendesha

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    gari kutokana na kuchanganyikiwa. Ningekuwa nimeaga nyumbani ningekupeleka kwako.” “Unataka nikalale kwako na mumeo?” Muddy aliuliza. “Sijaolewa.” “Unakaa na nani?” “Nipo na wazazi wangu.” “Ulijuaje kuna tukio hili?” “Nilipokuwa nimelala nilisikia mkibishana, nikatoka ndani na kusogea hadi pembeni yenu kwa vile kila mmoja alikuwa na hasira hamkuweza kuniona. Nilipowaona niliwatambua kutokana na maelezo ya watu juu ya matatizo yenu ya ndoa kutokana na kuijua tabia ya mkeo toka zamani. “Mambo mengi nilikuwa nayajua, nilipotoka nje na kuwakuta sikushangaa kusikia tambo za mkeo. Baada ya kuondoka nilijua nini kinafuata, nilijua utataka kujinyonga tu kama walivyofanya wanaume wengi walioachwa kama wewe. Kwa vile ulikuwa hujui upande wa pili wa mkeo. “Hata mkeo alipoondoka anaamini kabisa uamuzi utakaochukua ni huo, hushangai alikueleza uchukue kamba bila kukupa maelekezo. Kesho anasubiri kusikia kifo chako na kuchukua vitu vyako vyote bila familia yako kuambulia chochote. “Na hata akisikia hujafa lazima atafungua kesi ya kudai mgawane mali kuhakikisha anakufilisi kabisa. Utavumilia lakini mwisho wake ni kujiua kwa sumu au kamba. “Niliona kuna umuhimu wa kukueleza kilichokuzunguka katika ndoa yako, yule si mwanamke ila ni mwizi tena muuaji. Hebu niangalie mimi nilivyo mrembo, yule mkeo tapeli ananifikia?” Balkis alimuuliza Muddy huku akijigeuza na kupigwa na mwanga wa taa za barabarani. “Hawezi kukufikia.” “Sasa mwanamke kama mimi nikikupa penzi la kweli bila kuhitaji fedha zako unasemaje?” “Unataka kuniambia mwanamke mzuri kama wewe hujaolewa?” “Sijaolewa bado nipo kwa wazazi wangu kama nilivyokueleza awali.” ”Maeneo haya unakaa nyumba gani?” “Ingia kwenye gari nikakuoneshe.” Muddy aliingia kwenye gari na Balkis naye aliingia upande wa dereva na kuanza kuendesha gari. Baada ya mwendo mdogo gari lilikata kushoto na kuingia kwenye jumba la kifahari. Muddy pamoja na kuwa mwenyeji wa eneo lile lililopo karibu na Daraja la Salenda hakuwahi kuliona jumba zuri la kifahari. Baada ya gari kuingia katika jumba lile ambalo toka azaliwe hakuwahi kuingia, Balkis alimkaribisha hadi chumbani. “Karibu mpenzi nikupoze machungu yote.” “Asante.” Balkis alimshika mkono Muddy na kumuongoza, hakuamini mahaba aliyooneshwa na Balkis mwanamke mwenye uzuri wa ajabu. Nini hatima ya Muddy mikononi mwa Balkis? Kuyajua yote tukutane kesho hapa hapa UNLIMITED SWAGGAZZ!!!!! *story unaionaje? *mpk sasa umejifunza nini? *je tufanyeje ili kuepukana na balaa km hili???







    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    ILIPOISHIA: “Karibu mpenzi nikupoze machungu yote.” “Asante.” Balkis alimshika mkono Mudy na kuingia naye ndani, Mudy hakuamini mahaba aliyooneshwa na Balkis, mwanamke mwenye uzuri wa ajabu. SASA ENDELEA... Muddy aliingizwa kwenye jumba la kifahari lililokuwa na mapambo ghali ambayo aliwahi kuyaona katika picha za majumba ya Falme za Kiarabu. “Karibu sana.” “Asante.” “Muddy naomba ukaoge kwanza ndipo tupumzike.” Muddy alinyanyuka na kupelekwa kwenye bwawa la kuogelea lililokuwa mbele ya nyumba. Baada ya kuoga alipewa taulo laini la sufu na kupewa makubazi ya kuvaa kisha alirudi ndani. Kwa vile usiku ulikuwa umeingia sana alipelekwa moja kwa moja kitandani. Kila mmoja alilala chumba chake, Muddy alilala usingizi mzuri ajabu ambao hakuwahi kulala katika maisha yake. Alijikuta akitamani siku moja aishi maisha kama yale. Balkis aliingia katika mawazo ya Muddy na kuamini kama atatumia udhaifu ule basi atampata kirahisi. Majira ya saa kumi na nusu za usiku Balkis alimuamsha Muddy kisha alimpa chai yenye viungo na kumueleza: “Muddy muda wa kurudi baba yangu umekaribia, naomba nikurudishe kwako.” “Mmh! Sawa lakini bila ya baba yako nisingeamka mapema sijawahi kulala usingizi mtamu kama leo.” “Muddy, jitahidi kumuondoa akilini mkeo tapeli ambaye hatarudi kwako tena baada ya kukamilisha kilichomleta. Ukimuona anarudi ujue anaifuata roho yako. Kama utaachana naye nakuhakikishia kuishi maisha mazuri. Kama utakuwa mkweli na mwaminifu, nitayabadilisha maisha yako,” Balkis alimueleza Muddy ambaye hakuamini nguo zake kufuliwa usiku ule na kupigwa pasi kisha kupuliziwa manukato. “Kama unayosema ni kweli mke wangu hatarudi basi, nitakuwa na wewe.” “Muddy usitake kuniudhi, wewe ni mwanaume gani mkeo anachukuliwa mbele yako unaishia kulia, kwa kinywa chake kakueleza hakutaki, unataka upate ukweli gani?” “Ni kweli usemayo, lakini kumbuka yule bado ni mke wangu, hivyo tunaweza kuzungumza na kuyamaliza.” “Muddy nikueleze mara ngapi? Siku utakayorudiana na mkeo ujue ndiyo siku ya mauti yako. Wewe si mtu wa kwanza kufanyiwa hivyo, kama huamini kesho utaletewa karatasi itakayokutaka ufike mahakamani kwa ajili ya madai ya kugawana kidogo ulichobakia nacho. “ Kibaya ni kwamba una deni la mkeo ambalo litasababisha usipate hata fedha nusu ya kuuza vitu vyenu. Kwa vile hukujua deni alilokukopesha riba yake inazidi thamani ya vitu ulivyobakia navyo. “Kwa vile ni mzoefu wa mchezo ule, lazima atashinda kesi na wewe utachanganyikiwa, kitakachofuatia itakuwa ni kuokota makopo. Inawezekana una masikio ya kenge mpaka utoke damu ndipo usikie, usinitafute wala ukiniona usinifuate.” “Sasa dada utanisaidiaje?” “Niite Balkis.” “Sasa Balkis utanisaidiaje?” “Nakuomba chochote atakachokifanya asikushtue, wewe kubaliana nacho, mimi nitakuwepo mahakamani siku ya mwisho.” “Nitashukuru.” “Basi acha nikuwahishe kabla baba hajarudi.” Walitoka na kuingia kwenye gari, kisha Muddy aliendesha kurudi nyumbani kwake baada ya akili yake kuwa imetulia kidogo. Alipofika waliingia wote ndani, Balkis hakukaa sana aliondoka na kumuacha Muddy amalizie usingizi. *** Muddy alishtuka saa nne asubuhi na kujikuta akiwa na mawazo juu ya matukio yaliyomtokea jana ya kuachwa na mkewe pia kukutana na mwanamke mrembo mwenye mapenzi na huruma, Balkis. Pamoja na kuoneshwa ukarimu wa hali ya juu bado kitendo cha mkewe kumkataa kilimuumiza na kukumbuka vitu vingi alivyopoteza kwa ajili yake. Alikumbuka jinsi alivyotelekeza familia yake kwa ajili yule mwanamke na kusababisha kupoteza mke na watoto. Bado hiyo haikutosha, aliweza kutumia fedha nyingi alizowekeza mke wake wa kwanza vibaya kiasi cha kumtia katika umaskini. Pia alisababisha kutengwa na familia yake na kuwa adui yao mkubwa baada ya kugoma kutoa fedha za matibabu zilizosababisha dada yake mkubwa kupoteza maisha baada kukatazwa na mkewe asitoe kitu. Kila alipokuwa akifikiria yote yale moyo ulikosa amani, aliamini njia nyepesi ya kukimbia aibu ile ni kunywa sumu au kujinyonga. Akiwa katikati ya uamuzi mzito, hodi mlangoni iliyahamisha mawazo yake yaliyokuwa yamefanya atokwe na machozi na macho kuwa mekundu kutokana na maumivu ya moyo. Alifuta machozi na kwenda hadi mlangoni na kufungua, alikutana na kijana mtanashati. “Karibu,” “Asante, siingii ndani natoka mahakama ya mwanzo kuna barua ya madai toka kwa aliyekuwa mkeo.”

    . LAKINI likatokea jambo la ajabu, Muddy kila alipokuwa akikitafuta kisu hakukiona. Alihangaika nyumba nzima, hakukiona. Wazo lingine lilikuwa ni kutafuta kamba ili ajinyonge, vile vile alishangaa kuikosa kamba hata ile aliyotaka kujinyongea usiku na kuiacha kwenye gari, alipoifuata pia hakuikuta. Hakurudi ndani, alikwenda dukani na kuchukua sumu ya panya, aliichanganya katika chupa ya maji ya kunywa kisha akanywa yote na kwenda kulala akisubiri malaika wa kifo amchukue. *** Ashura mke wa Muddy alikuwa mwenye furaha, yeye pamoja na mwanaume wake walikuwa wakipongezana kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kumfilisi Muddy. “Nina imani kazi imekwenda vizuri,” mwanaume huyo alisema. “Ni kweli, lakini pamoja na kuyafanya yote bado namuonea huruma Muddy. Kwa nini tusimuachie gari na nyumba?” Ashura alisema katika hali ya kumuonea huruma Muddy. “Tukiwa na huruma hatuwezi kuifanya kazi hii, ona leo tulivyo na utajiri wa kutisha.” “Mmh! Kweli.” Wakati Ashura na mwanaume wake wakiwa katikati ya mazungumzo, mlango uligongwa. Wote walikaa kimya kusikiliza, mlango ulipogongwa tena mwanaume alinyanyuka na kwenda mlangoni. Alipoufungua alikutana uso kwa uso na Balkis, akamkaribisha. “Karibu mrembo.” “Ahsante sijui Ashura anakaa hapa?” “Wewe nani?” “Sasa kaka yangu badala ya kunijibu, unaniuliza mimi nani?” “Eeh, si vibaya kukujua wewe ni nani kwa vile unayemuuliza ni mke wangu na wewe ni mgeni kwangu.” “Mimi naitwa Balkis, ina maana Ashura ameshaachana na Muddy?” Balkis aliuliza swali la uongo. “Hiyo haikuhusu, sema kilichokuleta.” “Kilichonileta ni kuonana na Ashura.” “Karibu ndani.” Alimkaribisha sebuleni ambapo alimkuta Ashura amejilaza kwenye kochi. Ashura alimshangaa yule mgeni kutokana na uzuri wake wa ajabu, pia vito vya thamani alivyovaa mwilini mwake. Hata manukato yake yalikuwa mageni puani ambayo yaliifanya nyumba nzima kunukia. “Habari Ashura?” “Nzuri, umenijuaje?” “Ina maana jina lako ni siri? Wanapaswa kulijua watu wachache?” “Siyo kwamba ni siri ila sikujui.” “Huwezi kuwajua wote mdogo wangu.” “Mh! Nikusaidie nini?” “Nimetumwa na Muddy.” “Muddy! Muddy ndiye nani?” “Mumeo.” “Mimi nina mwanaume anayeitwa Muddy?” “Sasa unashangaa au unakataa? Ndoa yako na Muddy imevunjika lini wakati mpaka jana usiku majira ya saa sita mmenipita Daraja la Salenda mkiwa pamoja, leo hii unamkana?” “Basi muda mfupi baada ya kutuona wewe ndipo tulipoachana.” “Sasa nani kamuacha mwenzake?” “Maswali gani hayo?” “Ndiyo maana nipo hapa,” Balkis alisema kwa kujiamini. “Wewe ni nani kwa Muddy?” Ashura alihamaki. “Kabla sijakujibu nataka useme ukweli mbele ya mwanaume wako, upo tayari kurudiana na Muddy?” “Sipo tayari.” “Na ukirudiana naye tena?” “Nitembee uchi.” “Rudia.” “Nitembee uchi.” “Kaka umesikia?” Balkis alimgeukia mwanaume wa Ashura na kumuuliza. “Umesikia?” “Kuwa?”hi

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akirudiana na Muddy.” “Basi ni hayo niliyofuata hapa.” “Mbona umeniuliza hivyo?” Swali la Balkis lilimtisha Ashura. “Si umeachana na Muddy?” “Ndiyo, nirudiane naye kwa kitu gani alichonacho, tena muda si mrefu ataokota makopo.” “Usiokote makopo wewe, tena kabla sijaondoka nawapeni onyo mchezo wenu wa kudhulumu mali za watu utawatokea puani,” Balkis alimweleza Ashura ambaye bado alikuwa akimshangaa kwa maswali yake. Nini kiliendelea? Fuatilia katika Gazeti la Risasi Jumamosi. Vituko ndani ya daladala Abiria wawili ambao majina yao hayakujulikana, juzikati walitwangana makonde mazito baada ya mmoja wao kutoa nauli ya shilingi 200 badala ya 300. Abiria wa kwanza alipanda daladala hiyo Buguruni akielekea Gongo la Mboto na wa pili Vigunguti. Kondakta alipoanza kutoza nauli, abiria wa kwanza alitoa shilingi 200. Kitendo hicho kilionekana kumkera abiria wa pili kwa kumwambia kwa nini katoa nauli nusu. Abiria hao walianza kuzozana na kondakta akaungana na kauli ya abiria wa pili ya kumtaka wa kwanza kutoa shilingi 300 na si 200. Hali hiyo ilionekana kumkera abiria wa kwanza na kuamua kumrushia ngumi abiria wa pili. Kitendo cha abiria huyo kurusha konde kilisababisha timbwili kali kwa washkaji hao kuanza kutwangana kavukavu. Mbaya zaidi abiria wa kwanza alikuwa amekaa kiti cha mbele na walipoanza kurushiana makonde mazito gari lilianza kuyumba na kusababisha abiri wengine kuanza kupiga kelele ya kumuomba dereva asimamishe gari. “Dereva simamisha gari utatuua, tunakuomba sana tumeshinda salama tunataka tufike nyumbani tukiwa wazima, tafadhali,” alisikika abiria mmoja huku wengine wakimuomba Mungu awaepushe na balaa hilo. Wakati abiria wakipiga kelele, daladala hilo ilikuwa mwendo mkali. “Jamani mnataka kutuua kwa sababu ya shilingi 100? Acheni kugombana nitampa konda,” jamaa mmoja alisikika akisema. Gari liliposimama jamaa hao walishuka na kuanza kukunjana vema na abiria wengine wakaingia ndani ya gari na kumwambia dereva aendeshe. Mabondi hao wasiotambuliwa na shirikisho la ngumi Bongo waliachwa kituoni hapo wakitifuana.





    Muddy alishtuliwa katika usingizi mzito na sauti ya Balkis, aliposhtuka alijishangaa kujiona bado yupo hai hakufa kama alivyodhamilia. “Muddy vipi?” Muddy hakumjibu alimshangaa Balkis aliyekuwa ameshikilia barua mkononi. “Muddy mbona unanuka sumu ya panya?” Bado Muddy hakuwa najibu aliendelea kupepesa macho na kuitazama glasi aliyokunywa sumu ilikuwa juu ya sturi. “Muddy kwa nini unataka kujiua?” Balkis alimuuliza akiwa ameshika glasi iliyokuwa na sumu. “Umejuaje?” “Muddy nikufundishe mara ngapi swali mwenzake jibu na si swali kwa swali.” “Umeisoma hiyo barua?” “Niisome ili iwe nini, haya nilikueleza tokea awali kwa nini hutaki kunielewa?” “Samahani Balkis nimechanganyikiwa.” “Nilikueleza toka awali hutakufa bali unaelekea kwenye wendawazimu na usiponisikiliza sasa hivi utaokota makopo.” Muddy alishangaa jinsi Balkis mwanamke mrembo mara kumi Ashura ameonesha mapenzi ya kweli kwake. Kingine kilikuwa uelewa wa ajabu wa Balkis kuonekana kumfahamu vizuri yeye na Ashura bila kuhadithiwa na mtu. Hatua ya kupelekwa mahakamani ili wakagawane vitu pia deni la mkewe lililokuwa likizaa liba kila kukicha lilizidi kumchanganya. Alijikuta akinyanyuka na kuketi kwenye kitanda na kumuuliza Balkis. “Balkis unaonekana unajua mambo mengi juu yangu ya Ashura?” “Ndiyo maana nipo hapa kuokoa maisha yako, kwa vile lengo la mkeo wa uongo limetimia.” “Yote haya umeyajulia wapi?” “Utajua ukinipa moyo wako uliojeruhiwa niuponye.” “Kwa ukweli niliouona nipo tayari kukukabidhi moyo wangu.” “Je, Ashura akirudi kukubembeleza?” “Kwa uliyonieleza siwezi kurudiana na mwanamke yule ambaye kwangu ni muuaji.” “Nakuhakikishia kama utakuwa mkweli nitayabadili maisha yako, lakini chonde unigeuke baada ya kuwa na maisha mazuri utanisamehe.” “Nikuhakikishia nitakupenda kwa moyo wangu wote, najiona kiumbe mwenye bahati kupendwa na mwanamke mrembo tena mwenye maisha mazuri. Nakuapia kukupenda mapenzi ya dhati.” “Asante Muddy.” *** Balkis baada ya kujua Muddy ataletewa barua ya kuitwa mahakamani aliingia ndani kwa Muddy bila kuonekana na kwenda kukaa sebuleni kusubiri kitakacho tokea. Baada ya barua kuletwa na kukabidhiwa Muddy, alijua nini kitafuata. Baada ya kuisoma na kuonekana amechananyikiwa alitumia muda ule kuficha kila kitu ambacho angetumia kwa ajili ya kujitoa uhai. Hata alipokwenda dukani aliyemuuzia sumu ya panya, Balkis alijigeuza na kumuuzia kitu kingine kisicho na madhara yoyote. Kwa vile alikuwa amechanganyikiwa hakuichumza aliiweka kwenye glasi na kuichanganya na kuinywa kisha aliinywa. Lakini Balkis alikuwa amemuwekea dawa za usingizi ambazo zilimlevya baada ya kunywa na kulala usingizi mzito. Baada ya kumuona amelala, ndipo alimpomwacha na kwenda kwa Ashura mke wa Muddy. ****** Siku ya pili Muddy alifika mahakama kama ilivyopangwa, baada ya kesi kusikilizwa iliahilishwa wiki moja. Muddy alishangaa kutomuona Balkis mahakamani, baada ya kutoka mahakamani aliamua kwenda nyumbani kwao Balkis ili akajue nini kimemsibu baada ya kukosekana asubuhi ile kama alivyomuahidi kufika. Aliendesha gari lake ambalo kutokana na maelezo ya Balkis kuwa litapigwa mnada pamoja na nyumba na kugawana fedha zake, ambazo nazo zitachukuliwa na mtalaka wake na kumuacha bila kitu. Njia nzima alikuwa na mawazo juu ya hatima ya maisha yake kama atanyang’nywa kila kitu. Alipofika maeneo ya Daraja la Salenda alitembea taratibu kuitafuta nyumba ya kina Balkis ambayo aliamini ilikuwa maeneo yale. Lakini alijikuta akichanganyikiwa kutoliona jumba la kifahari alilopelekwa na Balkis. Mawazo yake yaliamini huenda amekosea eneo. Kutaka kupata uhakika wa sehemu aliyopelekwa usiku na Balkis, aliendesha gari

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mpaka sehemu waliyotelemka na mkewe usiku. Alipofika pale alirudi taratibu huku akipepesa macho kuangalia labda ataliona jumba la kifahari. Lakini hakuona chochote zaidi ya miti na bahari kwa nyuma. Alijikuta akijiuliza lile jumba alilolala mbona halionekani, alipanda ndani ya gari na kuanza kulitafuta kwa kuendesha gari taratibu kuelekea Masaki labda ataliona jumba lile. Aliendesha gari taratibu huku akipepesa macho labda ataliona jumba la kifahari kama lile ambao katika maisha yake hakuwahi kuona. Lakini gari lilizidi kwenda bila kuliona, majumba mengi alioyaona yalikuwa mazuri lakini hayakuweza kufikia hata robo ya uzuri wa jumba la kina Balkis Ambalo lilikuwa na eneo kubwa tofauti na majumba yaliyokuwa yamepangana pia maeneo yake yalikuwa madogo. Mpaka anafika Sea cliff Hotel hakuona jumba lile alilopelekwa na Balkis, aliamini kabisa atakuwa amekosea tu. Aligeuza gari na kurudi tena hadi sehemu aliyoachwa na mkewe usiku na kuonana na Balkis. Aliamua kutelemka kwenye gari na kutembea kwa miguu kufuata njia aliyopelekwa na Balkis, alikumbuka hakwenda njia ya Masaki bali alirudi kama anakwenda Daraja la Salenda. Muddy alitembea taratibu huku akipepesa macho huenda akaliona jumba lile la kifahari, lakini mpaka anavuka Daraja la Salenda bado hakuona jumba lile.

     Hakukata tamaa alitembea hadi Agha Khan, pia nyumba zilikuwa zile zile za siku zote alizozizoea. Baada ya kutembea kwa muda mrefu alijikuta akichoka sana na kuamua kurudi taratibu kulifuata gari lake ili arudi nyumbani. Alitembea kwa mwendo wa kivivu huku kiu na njaa ikiwa kali. Alimwita muuza maji ambaye alimletea maji, alikunywa kidogo na mengine alijimwagia kichwani kupunguza uchovu. Lakini ilikuwa tofauti na alivyofikiria, alihisi usingizi wa ajabu na mwili kuchoka maradufu. Alitafuta mti wa kivuli uliokuwa pembeni ya bahari na kujilaza chini yake. Usingizi mzito ulimpitia uliomfanya alale kwa muda mrefu, alishtuka saa moja usiku, giza lilianza kuimeza nuru ya mchana. Alijikuta amelala pembeni ya maji yaliyokuwa yakirudi baada kupwa kuanzia asubuhi. Alishangazwa na sehemu aliyojikuta kuwa eneo la ndani ya bahari wakati yeye alilala nje ya bahari kwenye miti ya pembezoni. Alinyanyuka na kujikung’uta kisha taratibu alielekea sehemu lilipokuwa gari lake. Wasiwasi wake mkubwa gari linaweza kuibwa au kuchukuliwa baadhi ya vitu. Alijiuliza kama gari litaibwa ataieleza nini mahakama, lakini ilikuwa ajabu gari lilikuwa lipo katika usalama pia hakuna kitu chochote kilichopotea. Alimshukuru Mungu na kuingia kwenye gari ili arudi nyumbani, lakini kabla hajawasha gari ili aondoke alishtuka kumuona Balkis. Balkis alitokea mbele yake na kulisogelea gari huku akichanua tabasamu pana, alipomfikia alimsemesha: “Muddy vipi?” “Safi.” “Za toka jana?” “Nzuri.” “Mbona upo huku?” “Mbona hukuonekana mahakamani kama ulivyoniahidi?” “Kwa hilo naomba samahani mpenzi wangu, nilitumwa na baba asubuhi nilijua nitawahi lakini amini usiamini ndiyo narudi. Na hivi nilikuwa nimetumwa tena nashangaa kukuona hapa.” “Balkis huwezi kuamini toka nizaliwe leo nimesulubika vibaya.” “Kwa nini tena mpenzi wangu?” “Baada ya kutoka mahakamani...” “Kabla ya kuendelea hebu nielezee imekuwaje huko?” “Kesi imehahirishwa mpaka wiki ijayo.” “Hakuna kitakachobadilika, kila kitu wamekwishakamilisha hata hakimu wa kesi yako ameshachukua chake mapema, kinachosubiriwa ni kukumaliza tu. Lakini nakuhakikishia fedha watakazochukua zitawatokea puani.” “Utawapeleka polisi?” “Wakafanye nini, ila utasikia tu nini kitawatokea.” “Alafu...” “Nimekuelewa Muddy, kwanza samahani kwa kutotokea mahakamani, umesema umesulubika kivipi?” “Hivi kwenu wapi?” “Muddy, si hapo mbele.” “Wapi?” “Unataka kupajua au kufika, twende maana sasa hivi nipo peke yangu.” “Sehemu gani?” “Si hapo mbele? Unaona nyumba ile kwa nyuma.” “Mbona jana tulikwenda huku?” “Si ndipo tunapopitia, kwani tatizo nini?” “Hakuna tatizo twende nikapumzike nimechoka hapa nilipo pia nina kiu na njaa kali.” Kama kawaida Balkis aliingia kwenye gari na kuliendesha, pamoja na Muddy kukaza macho ili ajue nyumba ile ipo wapi. Gari lilienda kidogo na kukata kidogo, Muddy hakuamini kuona jumba la kifahari lile lile alilolala jana yake. Baada ya kupaki gari sehemu yake aliteremka na kumfungulia mlango Muddy kisha alimshika mkono na kumuongoza mpaka ndani. “Karibu mpenzi wangu,” alimwambia kwa sauti ya mahaba huku akimlegezea macho na kumfanya Muddy asahau tabu zote alizokutana nazo. Kama kawaida alipelekwa kuoga kisha alifungwa vazi refu na kupelekwa kwenye meza iliyokuwa na vyakula tayari. Wakati akiendelea kula chakula kitamu ambacho kwake ilikuwa siku ya kwanza kukila, Balkis alimuaga kwenda kuoga. Aliondoka kwa mwendo wa madaha na kumfanya Muddy aache kula na kumsindikiza kwa macho huku akiusifia utundu wa Rabuka kumuumba binti mrembo kama yule. Kwake aliona kama ndoto kumpata msichana mzuri kama Balkis pamoja na uzuri wake lakini umemuonesha mapenzi ya kweli kiasi cha kumsahau mkewe Ashura. Akiwa katikati ya chakula, alimuona Balkis akisogea mezani akiwa amejifunga upande wa khanga. Kila dakika Balkis alizidi kujijaza moyoni kwa Muddy ambaye kwake aliona ngekewa kuokota dhahabu katikati ya soko la Kariakoo. Baada ya chakula kama kawaida alipelekwa kwenye chumba alicholala jana yake. Kwa raha za muda mfupi hakutamani kufa na kujilaumu kwa uamuzi wa kijinga aliotaka kuchukua. Kama kawaida alfajiri alirudishwa kwake huku akijiuliza kwa nini baba yake arudi alfajiri tu anatoka wapi. Kitu kingine kilichomchanganya kilikuwa jumba zuri analoishi Balkis lipo sehemu gani mbona hajawahi kuliona. Wazo lake lilikuwa mchana arudi tena kulitafuta. Lakini aliporudi alipitiwa na usingizi na kuamka jioni ya siku ile na wakati huo Balkis alikuwa amekwishafika na kumfanya siku ile aimalize nyumbani, lakini bado alitaka kutoka usiku ule kama Balkis akiondoka ambaye alikuwa halali pale na kwenda kufanya uchunguzi wake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    ITAENDELEA





0 comments:

Post a Comment

Blog