Search This Blog

JINI WA DARAJA LA SALENDA - 2

 





    Simulizi : Jini Wa Daraja La Salenda

    Sehemu Ya Pili (2)





    Suzana alikwenda hadi mlango wa chumba cha wageni na kuingia ndani, Brighton mapigo ya moyo yalikuwa makubwa. Alijisogeza hadi kwenye kochi na kujilaza akiwa ameshikilia mkono mmoja kifuani kuizuia presha kutokana na vurugu itakayotokea chumbani. Siku zote Suzana alimhakikishia Brighton kuwa siku atakayomkuta na mwanamke ndiyo siku atakielewa kichaa chake. Akili nyingine ilimtuma awahi chumbani kabla Suzana hajafanya lolote. Alinyanyuka alipokuwa amejilaza na kwenda chumba cha wageni. Alipofika alifungua mlango na kuingia ndani, Suzana aliyekuwa akianua nguo yake ya ndani, alishtuka na kumuuliza: “Vipi mbona umeingia kama unafukuzwa?” “Aa..aa..,” alijibu kwa kubabaika huku akipepesa macho

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    chumbani kumtafuta Balkis. “Vipi mbona unatembeza macho chumba kizima kuna nini?” Suzana alimuuliza. “Walaa, niliweka CD yangu kwenye meza.” “Sasa ulivyokuja hivyo, umeniona mimi mwizi?” “Walaaa, nilikuwa najiuliza niliiweka huku au wapi?” “Brighton, umeanza lini kuweka vitu vyako humu chumbani?” “Suzana hii ni nyumba yangu, nina uhuru wa kuweka kitu popote.” “Mbona leo Brighton sikuelewi?” “Kivipi?” “Umekuwa mtu mwenye mawazo mengi pia mwenye hasira tofauti na siku zote.” “Nipo sawa.” Brighton bado hakuamini kama kweli chumbani hakuna mtu, wasiwasi wake huenda amekwenda choo cha wote kilichokuwa upande wa mwisho wa nyumba ile. Bila kuongeza neno alitoka na kwenda moja kwa moja msalani ili kumuwahi kama Balkis yuko huko asitoke. Alipofika msalani hakukuta kitu, alijikuta akibaki akilishangaa bafu huku akijiuliza Balkis amekwenda wapi, ikiwa hakuna mlango mwingine wa kutokea. Akiwa bado ameshangaa Suzana alisimama tena nyuma yake na kumuuliza: “Brighton upo sawa?” “Nipo sawa.” “Hapana, kuna kitu kinakusumbua hutaki kuniambia.” “Suzy, nipo sawa.” “Hapana Brighton una tatizo unanificha, mimi nani kwako?” “Mpenzi wangu.” “Nani wa kumueleza shida zako?” “Lakini Suzy mimi sina tatizo lolote,” Brighton aliendelea kujitetea japo maji yalikuwa shingoni. “Sikubali, kuna kitu unanificha, basi mimi nipo chumbani ukimaliza matatizo yako utanikuta.” Suzana alisema huku akielekea chumba cha kulala, baada ya kuondoka Brighton aliendelea kuelea kwenye bahari ya mawazo juu ya kitu kilichotokea muda mfupi pale alipomshuhudia Balkis akiingia chumba cha wageni na wakati huo Suzana alikuwa anaingia. Bila kupumzika, alikwenda moja kwa moja chumba cha wageni alichoingia Balkis. Lakini cha ajabu, Balkis hakuwepo chumbani wala msalani, alijiuliza atakuwa wapi? Alijikuta akirudi tena chumba cha wageni kupata uhakika kama kweli Balkis hayumo. Chumba cha wageni hakikuwa na vitu vingi vya kuweza mtu kujificha, kitanda na tivii ndogo. Alipofungua mlango na kuingia, alishtuka kidogo akimbie alipomkuta Balkis akiwa amejilaza kitandani akiwa amepitiwa na usingizi. Kwake aliona kama maruweruwe, alifikicha macho kutaka kupata uhakika wa kile alichokiona mbele yake. Akiwa bado kapigwa na butwaa, Balkis aligeuka na kufumbua macho, alipomuona Brighton aliachia tabasamu na kusema: “Mpenzi mbona umeingia bila hodi?” “Aah! Ulikuwepo?” “Kuwepo wapi?” “Chumbani.” “Chumba gani?” “Si humu ndani.” “Ndani wapi?” “Sijakuelewa, hebu nieleweshe vizuri, nilikuwa wapi kivipi?” “Muda mfupi ulikuwa wapi?” “Brighton, swali gani hilo? Nimekuaga nakuja chumbani na umekuja umenikuta, sasa unaniuliza swali gani hilo?” “Mbona nimekuja chumbani sikukukuta?” “Hukunikuta! Hapa unazungumza na nani?” “Suzana alikuja huku, kwa wasiwasi wa kukuona ilibidi nije ili isitokee vurugu lakini sikukuona.” “Sijui unamaanisha nini, hebu nenda kwa Suzana ukamuondoe wasiwasi, nimekueleza mapema acha kujitia jakamoyo.” “Umejuaje?” “Ukirudi nitakuambia, muwahi mchumba wako.” Brighton alitoka kwenda chumbani kwake na kumuacha Balkis akimsindikiza kwa macho. Ni kweli Suzana alimuona Balkis? Mbona hakuonekana mwanzo chumbani?Brighton alijitahidi kurudi katika hali yake ya kawaida kabla ya kuingia chumbani. Alipoingia alimkuta Suzana amekaa upenuni mwa kitanda akiwa ameshika tama. “Suzana mpenzi wangu vipi?” “Vipi nikuulize wewe?” “Mbona mimi nipo sawa, hebu twende tukaoge mpenzi wangu tuje tulale.” Alimshika mkono na kumnyanyua kisha waliongozana naye bafuni, baada ya kuoga walirudi kitandani. Kwa vile Suzana alikuwa na hamu na mpenzi wake, baada ya kuikosa huduma ya kitandani kwa muda mrefu. Brighton hakujiamini kwa asilimia miamoja kukifanya alichomuitia mpenzi wake. Lakini ilikuwa kama alivyoelezwa na Balkis kuwa dawa aliyompa inafanya kazi, Suzana aliweza kufurahia mapenzi kwa muda wote, Brighton alijikuta akijisahau kuwa Balkis naye anamhitaji, baada ya kumstarehesha mpenzi wake alipitiwa na usingizi mzito. Ulipofika usiku wa manane Brighton alishtuka usingizini na kujikuta akifanya mapenzi na Balkis tena chumbani kwake. Baada ya penzi tamu la Balkis ambao aliamini hakuwahi kupewa chini ya jua zaidi ya ndotoni. Alipepesa macho mule chumbani labda atamuona Suzana lakini hakumuona. Ili kupata uhakika Suzana yupo wapi alimuaga Balkis kwenda msalani, pamoja na kuwa na choo cha chumbani lakini alitoka kwenda cha watu wote. Ajabu Balkis hakumuuliza chochote, alitoka mpaka chumba cha wageni na kukikuta kitupu. Alikwenda hadi msalani pia hakumuona. Alijiuliza Suzana atakuwa wapi au ameondoka, lakini haikuwahi kutokea Suzana aondoke usiku tena bila kuaga. Alijikuta akijiuliza bila kupata majibu kuwa yupo ndotoni au kweli, alitoka hadi nje ya nyumba lakini hakukuwa na dalili zozote za kuwepo Suzana. Alimfuata mlinzi wa Kimasai na kumuuliza kama Suzana ametoka. “Rafiki shemeji yako ametoka?” “Sijaona yeye ikitoka, niliiona inaingia tu.” “Rafiki lazima ulilala, mbona ndani hayupo?” “Sijasinzia rafiki, shemeji haijatoka imo ndani.” “Kweli?” “Kweli kabisa rafiki.” Brighton aliamini kabisa mlinzi alipitiwa usingizi wakati Suzana anatoka, akiwa bado anajiuliza ni kweli Suzana alikuja au ilikuwa ndoto. Lakini akili yake ilimweleza kuwa Suzana alikuja kweli wala haikuwa ndoto na kufanya naye mapenzi na kila mmoja alipitiwa na usingizi mzito. Lakini aliposhtuka na kujikuta akifanya mapenzi na Balkis tena penzi tamu adhimu, bado alikuwa njia panda kujiuliza kilichotokea ni nini yupo ndotoni au ni kweli. Kwa maelezo ya mlinzi kuwa kweli alimuona anaingia lakini hakumuona anatoka ilizidi kumchanganya. Hata kama kweli alitoka bado asingeondoka bila kuaga, na kitu kile hakikuwahi kutokea toka waanze uhusiano wao. Akiwa bado yupo njia panda kwa kile alichokuwa akikiwaza juu ya kuyeyuka kwa mpenzi wake . Sauti ya Balkis alimtoa kwenye dimbwi la mawazo. “Brighton huku ndiko msalani?” “Aa..aah... nilikuwa napunga upepo.” “Imeanza lini na leo iwe ya pili?” “Ni kawaida yangu wala si leo.” “Kweli?” “Kweli kabisa.” “Kwa hiyo nikuache uendelee kupunga upepo?” “Hapana, wacha turudi ndani.” Brighton alirudi ndani na Balkis, walipofika kitandani bado alikuwa na

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mawazo, lakini hakutaka kuumia kichwa alimuuliza Balkis. “Eti Suzana wakati anaondoka ulimuona?” “Swali gani hilo Brighton?” “Ooh! Basi.” “Kwanini unaniuliza habari za mpenzi wako mimi zinanihusu mimi?” Balkis alimuuliza kwa sauti kali kidogo. “Hapana mpenzi, inawezekana ulikuwa ninaota.” “Kuota nini?” “Kuwa Suzana alikuja leo.” “Kama alikuja yupo wapi?” “Inawezekana nilikuwa naota.” “Kama ulikuwa unaota basi tulale,” Balkis alimkumbatia Brighton, hakuchelewa usingizi mzito ulimpitia. **** Suzana aliposhituka usingizini hakuamini macho yake alipojikuta yupo nyumbani kwake amelala kitandani. Alirudia kutazama tena ni kweli au alikuwa akiota, akili yake ilimjulisha kuwa jana alipigiwa simu na mpenzi wake Brighton kuwa amepata dawa ya matatizo ya nguvu za kiume na alipokwenda kweli alikuwa amepona. Alikumbuka Brighton alimpa penzi tamu na kujikuta wote wakipitiwa usingizi, lakini ilikuwa ajabu kuamka asubuhi na kujikuta amelala kitandani kwake. Alijiuliza simu aliyopigiwa alikuwa anaota au kweli, kila alipolazimisha labda ni ndoto akili ilikataa na kuamini kabisa alikwenda kwa Brighton. Alijiuliza labda baada ya kufanya mapenzi alirudishwa nyumbani, lakini kwa upande wake kitu kama kile hakikuwahi kutokea. Kingine kilichomshangaza hata kama alirudishwa akiwa amelala hakuwa na fahamu. Alikaa kitandani kwa muda na kukumbuka anatakiwa kujiandaa kwenda kazini. Aliamka na kwenda kujiandaa, alipofika kazini bado akili yake haikumpa alimtafuta Sharifa amueleze kilichomtokea. Suzana na Brighton kilichowatokea watakigundua? Wakikigundua watachukua hatua gani? Balkis atatimiza dhamira yake?



    @@@@@@@@@@@@@@@@@@@





    Alipofika alimkuta ndiyo kwanza anafuta vumbi kwenye kompyuta yake, Sharifa alipomuona Suzana aligundua ana matatizo. “Karibu shoga.” “Asante,” alijibu huku akisogeza kiti na kuketi. “Mbona uko hivyo?” “Mmh! Kuna kitu kimenitokea jana sikielewi hata kidogo!” “Kitu gani hicho?” “Unakumbuka jana nilikupigia simu?” “Ndiyo.” “Nikakueleza kuwa nimeahirisha kwenda kwa mganga?” “Ndiyo.” “Basi, Brighton si aliniita na kunieleza kuwa amepata dawa ya tatizo lake na kukosa nguvu za kiume.” “Ehe?” “Baada ya kunieleza vile nikaona hakuna sababu yoyote ya kwenda kwa mganga kwa vile dawa imepatikana.” “Ehe!” “Basi jana saa moja usiku nikaenda kwa mpenzi wangu.” “Lete raha dada.” “Tumekutana kama kawaida, baada ya kuoga tulipanda kitandani, si unajua usongo niliokuwa nao.” “Najua sana.” “Basi shoga, kama alivyonieleza ndivyo ilivyokuwa, mtoto wa kike nikajilia raha nilizozipoteza muda mrefu.” “Alikuwa na nguvu kama kawaida?” “Tena ziliongezeka mara mbili.” “Mmh! Makubwa, kampata mganga gani huyo?” “Anasema alikwenda hospitali.” “Jamani ona sasa, kumbe tunakimbilia kwa waganga tiba ipo hospitali, nilikueleza toka awali waganga wengine wanatengeneza ugonjwa, ionekane kweli tuna matatizo makubwa ili tuwape fedha nyingi.” “Shoga bado nakuja sijafika kwenye pointi yangu.” “Ipi tena?” “Sababu iliyonifanya nisiingie ofisini kwangu na kuja moja kwa moja kwako.” “Una tatizo gani?” “Tulipomaliza kufurahishana na mpenzi wangu huku nikifurahia mafanikio makubwa baada ya kupona tatizo lake, tulipitiwa na usingizi mzito. Lakini kwa maajabu makubwa nimeamka asubuhi na kujikuta nipo kwangu!” “Kujikuta kwako kivipi?” “Kitandani kwangu nimelala!” “Sasa kipi cha ajabu?” “Ina maana hujanielewa?” “Nimekuelewa! Yaani jana baada ya kukutana na mpenzi wako asubuhi ulipoamka ulijikuta umelala, sasa kipi cha ajabu kama ulilala usiku na asubuhi ukajikuta kitandani?” “Hebu nielewe vizuri nisemayo, jana nilikwenda kwa Brighton kama ilivyo kawaida, ninapokwenda hulala huko huko, hata safari yangu ya kuja kazini huianzia kwake.” “Hilo nalijua, sasa hapo tatizo nini?” “Jamani huoni tatizo! Nilale kwa Brighton niamke kwenye kitanda nyumbani kwangu tena nikiwa peke yangu.” “Suzana! Unayosema ni kweli au ulikuwa unaota?” “Sharifa, yaani niote mchana na usiku? Sikukupigia simu?” “Ulinipigia?” “Saa ngapi?” “Mchana” “Sasa huko kuota gani?” “Mmh! Basi kama ni kweli usemayo kuna namna lazima tuliangalie kwa macho mawili.” “Yaani toka nimeamka sijielewi kabisa.” “Umempigia simu Brighton kumuuliza?” “Huwezi amini kila nikipiga simu yake inaonekana anazungumza.” “Basi kuna umuhimu wa wewe kwenda kwake ili ukapate ukweli, japo mimi bado naamini baada ya kunipigia simu inawezekana kabisa ulipitiwa na usingizi na kuota ulikuwa na Brighton na asubuhi ulipoamka ukajishangaa upo kitandani kwako. Lazima utaamini kabisa umetokewa na kitu kisicho cha kawaida.” “Sharifa hiki ninachokueleza ni kweli kabisa si cha kuota, haya ni maajabu.” “Au ndiyo Jini Balkis?” “Jini Balkis! Kama ni Balkis, Brighton asingeweza kufanya kazi.” “Nimekueleza yule jini ana mambo mengi ya kukuchanganya pale unapokaribia kuujua ukweli.” Suzana anaanza kuingia kwenye mtihani mzito wa Jini Balkis, nini hatima ya yote?“Kwa hiyo kuna umuhimu wa kwenda kwa mganga?” “Ikiwezekana, lakini kwanza nenda kwa mwenzako ili umuulize kama kweli jana mlilala pamoja.” “Mmh! Itabidi nifanye hivyo.” “Asubuhi hii?” “Sharifa siwezi kufanya kazi vizuri, akili yangu bado ipo njia panda ukweli wa kitu hiki nitaupata kwa Brighton.” “Kazi?” “Lazima niombe ruhusa, nimechanganyikiwa, sijui itakuwaje kama huyo jini atakuwa kanivaa na mimi?” “Kama kukuvaa kakuvaa muda mrefu, sasa inawezekana ndiyo anajionesha kwamba na wewe upo kwenye mtandao wake.” “Mungu wangu! Kama ni hivyo nitakuwa nimekwisha,” Suzana aliingiwa na hofu. “Suzana acha kujikatia tamaa, hebu tafuta ukweli ili tujue tufanye nini, ikiwezekana twende leo leo, nitaomba ruhusa nikusindikize.” “Basi wacha nikaombe ruhusa niende kwa Brighton nikapate ukweli, bila hivyo nitachanganyikiwa.” “Haya shoga utanijulisha,” Suzana aliagana na Sharifa na kwenda kuomba ruhusa kisha alielekea nyumbani kwa Brighton. *** Balkis akiwa amejilaza kitandani na Brighton, alimuona Suzana akielekea pale, kama kawaida yake alimueleza mpenzi wake: “Suzana anakuja.” “Umejuaje?” “Nijue vipi, la muhimu jiandae kumpokea mpenzi wako.” “Sasa nimpeleke chumba gani?” “Mlete humu humu.” “Wewe unatoka?” “Niende wapi?” “Si chumba wa wageni.” “Mi sitoki, Suzana anakuja kukuuliza kama jana alikuja kulala hapa.” “Umejuaje?” “Nisikilize kwanza ndipo uliniulize maswali.” “Mh!” “Naomba unisikilize, ukijichanganya shauri yako.” “Mbona unaniambia hivyo?” “Ndiyo maana nakueleza, nisikilize kwa makini.” “Sawa.” “Suzana anakuja kuulizia kama kweli jana alikuja hapa, mjibu kuwa hakuja. Tumeelewana?” “Lakini mbona mimi nafahamu jana alikuja?” “Kama alikuja mbona asubuhi hukumuona?” “Hata mimi nashangaa.” “Wewe na Suzana mliota ndoto ya aina moja kuwa jana mlikuwa pamoja lakini kila mmoja alipoamka hakumuona mwenzake.” “Balkis! Mbona unanitisha, wewe ni nani?” “Kwani wewe unanionaje?” “Nakuona mtu wa kawaida, lakini unayozungumza yananishangaza sana.” “Mbona ya kawaida, ni kipawa ambacho mwanadamu hupewa na Mungu kujua yajayo.” “Mmh! Nilikufikiria vibaya.” “Ulinifikiria vipi?” “Labda jini!” “Brighton tokea lini jini akazungumza na mwanadamu?” “Huwa nasikia majini huweza kujigeuza na kuwa wanadamu na kuishi nao.” “Kama ningekuwa jini ungefanyaje?” “Ningekufa kwa mshtuko.” Mara kilipita kimya cha ghafla, kitu kilichomshangaza Brighton. Haukupita muda mlango wa chumbani uligongwa. “Mkaribishe Suzana,” Balkis alimwambia Brighton aliyepatwa na mshtuko. “Wapi?” Ilikuwa ajabu Balkis alizungumza kwa sauti ya juu, lakini Brighton aliuliza kwa sauti ya kunong’ona. “Kuwa muelewa, nimekueleza mkaribishe humu ndani.” “Ili atufumanie?” “Ndiyo.” “Ili iweje?” “Utajua akiishaingia ndani.” Sauti ya kugonga mlango iliendelea nje huku ikionekana kabisa kitendo cha kuchelewa kufunguliwa mlango kilimuudhi sana Suzana. “Brighton kama hutaki nije kwako si uniambie kuliko kunifanyia visa?” “Mkaribishe,” Balkis alimueleza Brighton kwa kumkaripia. “Ingia,” alimkaribisha akiwa na wasiwasi

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mkubwa. Suzana aliingia na kwenda kukaa kitandani, pembeni kabisa ya Balkis. Brighton alikuwa kama mtu aliyeshikwa na ganzi na kushindwa kuelewa kama mpenzi wake ameingia ndani. Suzana baada ya kuingia alimshangaa kwa mara nyingine. “Brighton upo sawa?” “Eeh.... aah.. Unasema?” Brighton alijikuta akibabaika kujibu. “Makubwa ina maana hujaniona naingia?” “Nimekuona.” “Hata kunikaribisha? Kweli mapenzi yamekwisha,” Suzana alizungumza kwa sauti ya kilio. “Suzana...,” Brighton alipotaka kusema alimtupia jicho Balkis aliyekuwa amejilaza pembeni ya Suzana huku akitabasamu. “Brighton, una nini mpenzi wangu?” “Si..si..sina,” majibu ya Brighton yalizidi kumshangaza Suzana. “Kuna nini humu ndani, mbona sikuelewi? Jana nilikuja ukawa katika hali hii hii na leo tena, kuna kitu gani mpenzi wangu! Kwa nini hutaki kuniambia?” “Brighton mkatalie kwamba jana hakuja hapa,” Balkis alimwambia kwa sauti aliyosikia Brighton peke yake. “Brighton mbona kama haupo na mimi! Una nini mpenzi wangu?” Suzana aliporomokwa na machozi na kumfuata Brighton alipokuwa amesimama kama kapigwa na shoti ya umeme. Alianza kumpapasa huku akiendelea kumuuliza jinsi alivyoonekana mtu aliyehama kimawazo. Je, nini kitaendelea? Brighton atamsikiliza nani kati ya Suzana na jini Balkis?



    @@@@@@@@@@@@@



    Brighton alikuwa kama yupo ndotoni akijiuliza yanayotokea mbele ya macho yake ni kweli au ni kiini macho. Chumbani kulikuwa na watu watatu, Balkis hakujificha zaidi ya kulala kitandani, tena peupe. Hata Suzana alipoingia, pamoja na kukaa pembeni yake hakuonesha kuona kitu cha tofauti mle ndani. Alizidi kuingiwa na wasiwasi kuwa huenda Balkis si kiumbe cha kawaida, hata sauti yake aliyompa maelezo bado ilionesha kuisikia peke yake. Kuhama kimawazo kulizidi kumnyima raha mpenzi wake ambaye naye alikuwa na yake yaliyotakiwa kupata majibu kutoka kwa Brighton. “Brighton jana nimekuja hapa na kulala na wewe, lakini ajabu nilipoamka asubuhi nimejikuta nipo kitandani kwangu. Ni kweli jana nilikuja au nilikuwa naota?” “Brighton, kataa! Sema hakuja?” Balkis alipaza sauti ya juu. Lakini Brighton alijikuta mdomo ukiwa mzito kumjibu mpenzi wake huku jasho la hofu likimtoka. “Brighton una nini mpenzi wangu, nijibu basi, si ni wewe ndiyo ulinipigia simu jana na kuniambia nije?” “Brighton kataaa,” Balkis alizidisha sauti iliyoumiza ngoma za sikio. “Brighton kuna nini hapo kitandani mbona unapaangalia sana, au kuna mwanamke?” “Ha..ha..kuna..ki..” “Brighton unafanya nini?” Balkis alipiga kelele iliyokuwa na mlio mkubwa kama radi iliyofanya ngoma za sikio za Brighton zisikie maumivu makali. “Brighton mpenzi wangu una nini au umeshavamiwa na jini Balkis?” “Nani?” Jina la Balkis lilimshtua. Kauli ile ilimuudhi jini Balkis, akapuliza upepo uliompata usoni Suzana ambaye aliishiwa nguvu na kupitiwa na usingizi mzito. Brighton alimuwahi kabla hajaanguka chini na kumlaza kitandani pembeni ya Balkis. “Suzana... Suzana,” alimwita kwa kumtikisa. Suzana hakujibu kitu, alionekana mwenye usingizi mzito. Brighton alimuona Balkis jinsi alivyompuliza hadi kupitiwa na usingizi mzito. “Balkis umemfanya nini Suzana?” “Acha upumbavu,” Balkis alimjibu kwa hasira. “Balkis mbona sikuelewi?” “Hunielewi kivipi?” “Itakuwaje umpulize mtu apoteze fahamu?” “Nilikwambia nini?” “Nilikwambia utoke, kwa nini hukutoka?” “Mimi ni nani yako?” “Kwa tabia yako ya miujiza siwezi kukuoa, unaonekana si mtu wa kawaida.” “Unasemaje?” Kauli ile ilimchefua Balkis. “Siwezi kukuoa.” “Kweli?” “Kweli,” Brighton alijibu kwa kujiamini. “Asante.” Baada ya kusema vile Brighton alishangaa kuona sura ya Balkis ikijikunja na kuwa kama mzee, uzuri wote ulipotea. Wasiwasi ilizidi kumjaa kwa kuamini huenda kweli Balkis si mwanadamu wa kawaida bali ni jini. Baada ya kugundua kuwa Balkis si kiumbe wa kawaida, aligeuka ili awahi kuchukua Biblia ili amkemee, hakupiga hata hatua moja, mkono wa Balkis alinyooka na kuwa mrefu, ukamrudisha alipokuwa, kisha alimshika sehemu za siri na kuzivuta kwa nguvu kama anatoa kitu. Brighton alihisi kama amepigwa shoti ya umeme sehemu za siri kisha alizisikia zikiwa za baridi kama zimetoka kwenye jokofu. Kwa sauti kali ya hasira Balkis alisema: “Hutasimamisha milele, na mkeo hatazaa milele.” Baada ya kusema vile aliingiza mkono sehemu za siri za Suzana ili amtoe kizazi, kabla hajamtoa Brighton alipiga kelele: “Hapana, Balkis usifanye hivyo.” “Lazima niwatie adabu, binadamu gani asiye na shukrani.” “Nisamehe Balkis nipo tayari kukuoa.” “Mpaka kwa shinikizo?” “Siyo hivyo, mambo yako yananichanganya nashindwa kukuelewa wewe ni mtu wa aina gani?” “Mimi ni jini?” “Eeh!” Brighton alishtuka. “Unashtuka nini, mimi ni jini la chini ya bahari.” “Mungu wangu nimekwisha miye.” ”Uishe kivipi, katika muda tuliokuwa wote uligundua tofauti gani kwangu?” “Sijagundua.” “Penzi langu na wanadamu wenzio lipi lilikuwa tamu?” “La kwako.” “Mimi na mchumba wako nani mzuri?” “Wewe.” “Nani aliyesema kwamba Suzana hafai kuolewa?” “Mimi.” “Nilijitoa kwako ili kurudisha furaha iliyopotea, pamoja na kukubali kunioa bado nilimheshimu mpenzi wako, kosa langu nini?” “Nisamehe.” “Nitakusamehe, lakini nakurudishia ugonjwa wako ambao hautapona milele.” “Nisamehe Balkis nilikuwa sijajua.” “Hujajua nini?” “Hata sijui nilimaanisha nini nimechanganyikiwa Balkis, nisamehe sana.” “Mimi nakusamehe, lakini nakuacha na matatizo yako na mpenzi wako.” “Hapana usinifanye hivyo.” “Kumbuka nilikuponya ili nipate raha zako na si kwa faida ya mtu mwingine, nikiondoka naondoka na raha zangu.” Balkis atamsamehe Brighton?

    “Nimekubali kuendelea kuwa na wewe Balkis usinifanye hivyo,” Brighton alijitetea kwa kupiga magoti mbele ya Balkis. “Kwa nini hutaki kunisikiliza?” “Nilichanganyikiwa baada ya kukuona ndani, nilijua lazima Suzana atakuona.” “Nilikueleza mimi ni nani?” “Jini.” “Jini huonekana kwa kupenda, Suzana asingeniona hata mara moja.” “Ningejuaje bila kuniambia?” “Kweli kosa ni langu la kutokukueleza mapema, nitakurudishia nguvu zako na leo hii nitaondoka na wewe kwenda kwetu kuishi maisha mazuri.” “Wapi?” “Ujinini,” Balkis alizungumza kwa sauti ya upole huku akijirudisha katika hali yake ya uzuri wa shani. “Na Suzana?” “Mwache tu, sitamdhuru, nitamrudisha kwake akiamka atajikuta kitandani amelala.” Baada ya kusema vile alimkumbatia Brighton na wote walitoweka mle ndani na kutokea pembeni ya bahari maeneo ya Daraja la Salenda. “Unanipeleka wapi?” “Brighton mpenzi acha woga, tunakwenda kwetu chini ya bahari.” “Si nitakufa na maji?” “Huwezi, ni sehemu nzuri sana ukifika hutakumbuka kurudi duniani.” “Nitaishi vipi na majini na mimi ni mwanadamu?” “Kama nilivyokueleza majini tupo kama wanadamu wa kawaida na kufanya mambo kama ninyi.” “Mmh! Sawa.” Walitembea taratibu kuelekea ndani ya maji, Brighton alikuwa na wasiwasi wa kuzama, wasiwasi wake labda Balkis anataka kumzamisha na kumuua baada ya kuonesha kiburi. “Balkis usiniue,” alijitetea. Balkis badala ya kumjibu alicheka sana, jambo lililozidi kumtisha Brighton, hakusimama aliendelea kusogea mbele katikati ya bahari akiwa bado amemshika mkono. Maji yalimfika magotini, tumboni yakaanza kuelekea kifuani mwishowe yakavuka mabega. “Balkis naomba unisamehe usiniue kwenye maji.” “Brighton hakuna mtu anaweza kuitupa shuka yake wakati wa baridi.” “Una maana gani?” “Wewe ndiye shuka langu, siwezi kukupoteza, bora nipotee mimi.” Wakati huo maji yalikuwa yamewafika chini ya kidevu, Balkis alimshika Brighton kichwani na kumzamisha ndani ya maji kwa nguvu, alitaka kupiga mayowe lakini alikuwa amechelewa. Aliposhtuka alijikuta wametokea kwenye mji mzuri ajabu. “Brighton, karibu sana huu ni mji wetu, nawe utaishi kama mfalme, mimi ni mtoto wa Mfalme wa Majini. Baba yangu anaitwa Bashami Hudirud.” “Asante.” Walikuja vibaraka weusi kama wanadamu wa kawaida lakini miili yao ilikuwa na nguvu sana. Juu walikuwa vifua wazi na chini walikuwa wamejifunga shuka kama nepi wakiwa wameongozana na vijakazi waliojifunga shuka nyeupe na kuiacha migongo yao nje

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakiwa wamebeba maua na farasi weupe wawili waliokuwa wametandikwa matandiko ya dhahabu. Vibaraka wenye nguvu walimbeba Brighton na kumketisha juu ya farasi, baada ya kukaa walimbeba Balkis na kumketisha kwenye farasi mwingine aliyekuwa mzuri kuliko aliyembeba Brighton. Baada ya wote kukaa kwenye farasi, safari ilianza kuelekea kwenye jumba la kifahari. Brighton alipatwa na wasiwasi kukuta mji unaosemwa ni wa majini ni mzuri ajabu na viumbe wake ni watu wa kawaida kama wa duniani. Ila njia nzima hakuna gari wala chombo chochote kinachotumia moto. Alikaribishwa ndani huku akipigiwa muziki wa vyombo vitupu lakini ulikuwa mtamu masikioni. Kabla ya kuingia ndani lilitandikwa zulia jekundu ambalo hakuwahi kuwaza kulikanyaga katika maisha yake. Baada ya kuingia ndani alikaribishwa na wasichana wazuri waliovalia magauni meupe yaliyowapendeza, walimwaga maua ya kunukia. “Brighton karibu kwetu,” Balkis alimkaribisha Brighton kwenye sofa lililotengenezwa kwa manyoya ya kondoo. “Asante,” alijibu huku akikaa kwenye sofa lililomfanya ahisi usingizi. “Jisikie upo nyumbani.” “Asante, mbona ni tofauti na nilivyofikiria?” “Kuhusu nini?” “Nilijua ninyi ni viumbe wa ajabu wenye mikia na meno ya kutisha, mbona ni binadamu kama sisi, kwa nini mnaitwa majini?” “Majini ni viumbe wenye uwezo mkubwa wa kufanya jambo lolote tofauti na wanadamu. Lakini nasi tunamuabudu Mungu kama ninyi.” “Mbona mnaua watu?” “Unatushangaa kwani hakuna wanadamu wanaoua wenzao?” “Wapo.” “ Mbona mnatushangaa sisi?” “Lakini nasikia majini hutumika kuwaua watu?” “Bado hakuna kitu tofauti na wanadamu, kuna wanadamu wachawi mbona hao hamuwazungumzii.” “Lakini mbona nasikia kuna majini kazi yao ni kuua tu sijui Jini Makata.” “Brighton hakuna wanadamu wanaotumwa kuua, hakuna majambazi wanaoua na kuchukua mali zao? Duniani sasa hivi kuna vita, wanadamu wanauana mamia kwa mamia bila sababu, hapo napo kuna majini?” Swali lile lilimfanya Brighton akose jibu, Balkis aliendelea kuzungumza. Je, nini kitaendelea?.





    @@@@@@@@@@@@@@@@





    IIPOISHIA; “Ewe mwanadamu, acha kumkosea heshima mtukufu mfalme, kila utakalojibu tanguliza neno mtukufu mfalme.” Mkuu wa watwana alimkumbusha tena Brighton. “Ndiyo mtukufu mfalme.” “Vizuri, Balkis.” “Mtukufu Mfalme.” “Unajua sababu ya kukutuma duniani?” “Ndiyo mtukufu mfalme.” “Mbona imekuwa kinyume?” “Mtukufu mfalme nimekwisha kujibu kila kitu.” “Bado hujanibu.” “Unataka jibu gani mtukufu mfalme?” “Sababu kuu ya kukutuma huko, hujanijibu.” “Ni kweli mtukufu mfalme shida kubwa ni kuongeza familia yetu.” “Sasa kwa nini umekaidi amri yangu, nakuomba urudi duniani akaifanye kazi niliyokutuma.” SASA ENDELEA... “Mtukufu mfalme, kupitia huyu mwanadamu nitapata mtoto unayemtaka. Nina imani tatizo lilikuwa damu zetu kukosa virutubisho. Lakini damu ya mwanadamu huwa ina virutubisho vingi.” “Hatutaki mtoto mchanganyiko.” “Lakini mtukufu mfalme si atakuwa mwanangu?” “Sipo tayari kuchanganya damu.” “Mtukufu mfalme, nami sipo tayari kumpoteza mpenzi wangu.” “Tunabishana?” mfalme Barami alikuja juu. “Baba hatubishani, ila ukweli ni huo.” “Mwana wa mfalme mwite mtukufu mfalme si baba,” mtwana mkuu, Kulani alimwambia Balkis aliyekuwa amemvunjia heshima baba yake na kusimama wima. “Wewe nani unayeingilia mazungumzo na baba yangu? Nani kakupa ruhusa ya kunikemea. Huna heshima, kibaraka mkubwa wee,” Balkis alimfokea mkuu wa watwana. “Balkis umekosa heshima?” mfalme Barami alimfokea mwanaye. “Sijakosa baba, natetea haki yangu.” “Kulaniiii, wachukueni mkawaweke kwenye chumba cha giza haraka.” Mfalme Barami alisema kwa sauti ya juu baada ya kumuona mwanaye amemvunjia heshima. Kulani na wenzake waliwabeba juu juu na kwenda kuwafungia katika chumba cha giza. **** Suzana alishtuka siku ya pili na kujikuta akiwa amelala kwa mara nyingine kitandani kwake. Alijiuliza kuwa pale kitandani ni kweli au anaota, kumbukumbu zake zilimkumbusha kuwa jana yake alitoka nyumbani na kwenda ofisini na kisha alitoka. Breki yake ya kwanza ilikuwa ofisini kwa shoga yake Sharifa na kumuelezea yaliyomsibu baada ya kulala kwa mpenzi wake Brighton, lakini ajabu siku ya pili alijikuta kitandani kwake. Alikumbuka baada ya kumuelezea shoga yake alimpa ushauri kabla ya kufanya lolote aende kwa Brighton kupata ukweli kama ni ndoto au kweli. Suzana akiwa bado amekaa kitandani aliendelea kuvuta kumbukumbu ya mambo aliyoyafanya jana yake. Alikumbuka baada ya kushauriana na Sharifa aliaga kazini na kwenda moja kwa moja kwa mpenzi wake. Alipofika Brighton alionesha kubabaika hata majibu yake yalikuwa kama mtu aliyemfumaniwa. Baada ya hapo hakumbuki kilichoendelea mpaka alipoamka na kujikuta tena kitandani kwake. Tukio la kujikuta kwake tena wakati anaamini jana asubuhi alikwenda kwa Brighton lilizidi kumchanganya akili. Kabla hajafanya lolote simu yake iliita alipoangalia ilikuwa ya Sharifa, aliipokea na kuzungumza. “Haloo Sharifa.” “Eeh, Suzy vipi, ndiyo ukaondoka kimoja na simu ukazima. Lakini hiyo ni tabia gani ukiwa na tatizo tuko pamoja likikuishia ananisahau?” Sharifa alilalamika upande wa pili. “Najua utanilaumu bila kujua.” “Suzy hata kama ulichokifuata kimekwenda vizuri, kwa vile uliniacha na mimi na maswali ulitakiwa kunijulisha.” “Sharifa nashindwa sijui nikuambie nini?” “Uniambie nini Suzy? Kitendo cha kukosa uungwana kwa kweli siyo kizuri hasa tukiwa watu wa karibu.” “Kabla sijakuambia kitu naomba nikuulize swali?” “Uliza tu. ” “Ni kweli jana nilikuja ofisini kwako asubuhi?” “Mbona unaniuliza hivyo?” “Shoga yangu nina maana kubwa sana ya kukuliza hivyo naomba unijibu usinidanganye.” “Ni kweli ulikuja.” “Si nilikuja kukueleza maajabu yaliyonitokea nilipolala kwa mpenzi wangu na kujikuta kitandani kwangu?” “Ndiyo.” “Ni kweli asubuhi sikufanya kazi nilikuaga nakwenda kwa Brighton.” “Ndiyo.””Basi dada yangu yaliyonitokea juzi kuamkia jana ndiyo aliyonitokea jana kuamkia leo.” “Una maana gani kusema hivyo?” Suzana alimweleza yote aliyokutana nayo na siku ya pili alipoamka na kujikuta kitandani kwake. “Suzana usiwe unachanganya mambo, pengine ulipotoka hapa badala ya kwenda kwa Brighton ulikwenda kwako ukalala na kupitiwa na usingizi mzito?” “Sijafikia huko kiasi cha kupoteza kumbukumbuku hivyo, nilipotoka ofisini nilikwenda moja kwa moja kwa Brighton. Jamani hata kama nilirudi nyumbani asubuhi ile ndiyo nilale nishtuke asubuhi ya siku ya pili?” “Mmh! Suzana kuna tatizo.” “Yaani huwezi kuamini sasa ndiyo inajidhilisha kuwa kuna kitu kinanichezea akili.” “Kwani Brighton yeye anasemaje?” “Lazima na yeye atakuwa na tatizo, siku mbili hizi simwelewi kabisa, amekuwa kama mtu aliyechanganyikiwa.” “Suzana umezidi ubishi kila kitu nilikueleza, lakini hutaki kuamini wacha yakukute.” Suzana yupo njia panda anataka kujua yaliyomzunguka ni kweli au ni ndoto.“Tuache masihara, hebu nipelekwe kwa huyo mtaalamu, kilea kidonda mwisho kukatwa mguu.” “Leo ndiyo unagundua, nilikueleza toka mwanzo kuwa majini wana hadaa inayokuchanganya na mwisho wa siku wanakuingiza sehemu mbaya.” “Sharifa huu si wakati wa kunilaumu, nahitaji msaada wako la sivyo nitachanganyikiwa.” “Kama upo tayari, twende pamoja Bagamoyo.” ”Lini?” “Leo hii.” “Saa ngapi?” “Safari yetu itakuwa saa tatu?” “Basi shoga tutakuwa wote hali inatisha.” Walikubaliana kwenda wote Bagamoyo, baada ya kukata simu Suzana alinyanyuka kitandani ili kujiandaa na safari ya Bagamoyo. Baada ya maandalizi waliingia kwenye gari kwenda nyumbani kwa Sharifa kumpitia kwenda kwa mganga Bagamoyo. Njiani alijitahidi kumpigia simu Brighton simu yake haikuwa hewani, aliachana naye na kuendelea na safari yake mpaka kwa Sharifa. Aliwakuta wameisha jiandaa wakimsubiri, walipomuona tu hawakutaka kupoteza muda. “Jamani tutatumia magari yote?” Suzana aliuliza. “Hakuna haja

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     ya kutumia magari yote, moja tu linatosha” “Hakuna tatizo.” Walikubaliana kwenda kwenye usafiri mmoja walipanda kwenye gari la Sharifa na kuelekea Bagamoyo. Walitumia dakika arobaini na tano kufika Bagamoyo, walipofika waliuliza wenyeji sehemu aliyopo mganga Njiwa Manga. “Samahani kaka,” Sharifa alimuuliza kijana mmoja aliyepita karibu na mlango wa gari lake. “Bila samahani dada yangu,” kijana yule alijibu huku akisogea karibu. “Habari za saizi?” “Nzuri tu dada.” “Eti, Njiwa Manga anaishi wapi?” “Njiwa Manga! Yupi, yule mganga?” “Eeh, huyo huyo.” “Unaona hii barabara kubwa?” “Ndiyo.” “Ifuateni, acha barabara ndogo mbili zinazokatisha kulia, ya tatu ufuate nenda moja kwa moja mpaka mbele utaona kuna nyumba ina bendera nyekundu hapo hapo kwa mzee Njiwa Manga.” “Asante,” Sharifa alishukuru huku akimpa elfu mbili. “Nashukuru dada yangu.” Waliachana na yule kijana na kufuata maelekezo yake, walipofika barabara ya tatu inayoingia kulia waliifuata na kwenda mwendo kidogo mpaka kufika kwa mganga Njiwa Manga. Walipaki gari sehemu iliyo salama na kutelemka, ilikuwa sehemu yenye eneo kubwa lililokuwa na nyuma kubwa moja na pembeni kulikuwa na mabanda madogo. “Karibuni,” binti mmoja aliyekuwa amevalia gauni refu na kitambaa kichwani aliwakaribisha. “Asante,” waliitikia kwa pamoja. “Karibuni kwenye benchi hapo chini ya mti.” “Asante,” walikwenda wote kukaa chini ya mti kusubiri maelekezo. Ilipita zaidi ya saa nzima bila kupata maelezo yoyote zaidi ya kukaribishwa kana wageni wengine na kuonesha sehemu ya kukaa. “Samahani dada,” Sharifa alimwita yule msichana aliyewakaribisha na kuendelea kuwakaribisha wageni wengine kama watatu, mmoja alikuja na gari na wengine wawili walikuja kwa miguu kuonesha walikuja na usafiri wa daladala. “Bila samahani,” alisema huku akisogea kuwasikiliza. “Eti mganga tumemkuta?” “Yupo, kama asingekuwepo nisingewaacha mkae mpaka muda wote huu.” “Kwa hiyo tutaonana naye saa ngapi?” “Mmh! Sijajua ila si muda mrefu, leo hakuna wagonjwa wengi.” “Wengine wapo wapi?” “Wapo ndani, wakipungua nanyi mtaingia.” “Haya,” waliachana na yule msichana aliyerudi sehemu yake kusubiri wateja wengine. Baada ya nusu saa waliitwa ndani, wakati huo ilikuwa imefika saa tatu na nusu asubuhi. Waliongozana wote watatu mpaka kwenye sebule kubwa iliyokuwa imetandikwa zuria bila kiti. Baada ya kuketi msichana aliyewafuata aliingia chumbani na kuwaacha wasubiri. Ilipita kama robo saa tena waliitwa ndani, waliingia wote watatu. Chumbani kulikuwa na mzee wa makamo aliyeonekana kula chumvi nyingi kutokana na kuenea mvi sehemu kubwa ya nywele zake. Alionekana ni mtu wadini kutokana na mavazi yake ya kanzu iliyokuwa nyeupe sana na juu alivalia kilemba cheupe. Pembeni yake kulikuwa na msahafu. “Asalamu aleykum,” mama Sharifa alimsalimia mganga. “Waleyku msalamu, karibuni.” “Asante,” waliitikia kwa pamoja. “Shikamoo,” Sharifa na Suzana walimwamkia mganga. “Marahaba mabinti zangu, karibuni.” “Asante.” “Haya, mna shida gani?” “Kuna vitu vimewatokea mabinti zangu, mpaka sasa vinawachanganya, japo kuna sehemu tulikwenda na kuelezwa tatizo lao, mmoja hakuwepo na mwisho wa yote ilionesha tatizo lile kwa upande wake ni zito hivyo alituelekezwa kuja kwako,” mama Sharifa alitoa maelezo mafupi. “Mmh, nimekupateni, nipe majina yao.” Nini kitaendelea, watapata msaada kwa mganga Njiwa Manga?





    @@@@@@@@@@@@@@@







    Jini Wa Daraja La Salenda-12

    ILIPOISHIA: “Haya, mna shida gani?” “Kuna vitu vimewatokea mabinti zangu, mpaka sasa vinawachanganya, japo kuna sehemu tulikwenda na kuelezwa tatizo lao, mmoja hakuwepo na mwisho wa yote ilionesha tatizo lile kwa upande wake ni zito hivyo yule tuliyemwendea alituelekeza tuje kwako,” mama Sharifa alitoa maelezo mafupi. “Mmh, nimekupateni, nipe majina yao.” SASA ENDELEA... “Naitwa Sharifa.” “Jina la mama yako?” “Habiba.” “Mmh! Na wewe mama?” “Naitwa Suzana.” “Jina la mama?” “Monika.” “Vizuri.” Baada ya kuyaandika majina yale kwenye karatasi nyeupe kwa kutumia wino mwekundu, mganga alifungua kitabu kimoja na kutafuta sehemu ya kusoma,alipoipata aliisoma kimya kimya huku akiandika baadhi ya vitu alivyoviona kwenye kitabu kile katika karatasi kwa lugha ya kiarabu. Baada ya robo saa ya kutulia na kusoma huku akiandika, alikohoa kidogo na kusema: “Nimeona vizuri, nina imani yaliyosemwa na mganga aliyetangulia yapo vile vile.” “Haa! Ina maana kweli sina kizazi?” Sharifa alishtuka kusikia vile. “Ni kweli huna kizazi, kilichoelezwa na mganga wa awali hakuna kilichopungua kwako wala kuzidi. Ila kwa Suzana yeye yake yameongezeka.” “Eeh?” Suzana alishtuka. “”Ila msiwe na wasiwasi” “Ninaweza kupona?” Sharifa aliuliza. “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.” “Na mimi matatizo yangu?” Suzana aliuliza. “Ni kweli kuna mambo yanaonesha hapa yamekuchanganya na kushindwa kuelewa ni kweli au ni ndoto?” “Ni kweli mzee wangu,” alijibu Suzana. “Kilichotokea kwako ni kweli wala siyo ndoto, ni kweli ulilala na mpenzi wako na asubuhi ulipoamka ulijikuta ukiwa kwako. Pia, jana ulipokwenda kuulizia yaliyokutokea juzi kama ni kweli, ulishangaa alfajiri ya leo kujikuta upo tena kwako kitu ambacho kimekuwa kikikuchanganya sana. “Ukweli ni huu, anayewasumbua ni jini la kike linaitwa Balkis, jini huyu yupo chini ya bahari akiwa mtoto wa kwanza wa mfalme wa majini yaliyoko huko. Baba yake anaitwa Barami Hudirud. Wakati alipotakiwa kuolewa alionekana hana kizazi hivyo alipewa kazi ya kuja dunia kutafuta vizazi vya wanawake mia moja kama dawa ya kumuwezesha kushika ujauzito. “Kazi ile aliianza muda mrefu kwa kuja kwa nadra duniani, sehemu yake kubwa ilikuwa Daraja la Salenda ambako aliwaingia wanawake na kwenda nao makwao, usiku alivichukua vizazi vyao na kurudi chini ya bahari. Kazi ilionekana ikienda taratibu mno, hivyo wazazi wake walimuomba aje rasmi duniani ili aweze kupeleka kwa urahisi vizazi vya wanawake wengi na kumfanya awahi kufunga ndoa. “Siku ambayo uliona sherehe ya ajabu ndiyo ilikuwa siku rasmi ya jini Balkis akiagwa kutoka chini ya bahari kuja duniani. “Katika watu mwenye bahati ya kuiona sherehe ile ni wewe na ndiye uliyemvutia jini huyo hadi akaamua kukufuatilia kila ulichokuwa ukikifanya, alipomuona mchumba wako alivutiwa naye, ili ajue siri yako alianzisha uhusiano na mchumba wako bila ya yeye kujua kwa kufanya naye mapenzi kwenye ndoto. “Alifanikiwa kuwapotezeni kwenye ukumbi wa starehe, shida yake kubwa ilikuwa kukuchukua na kwenda kukuficha chini ya bahari ili aweze kuishi na mchumba wako kwa sura yako. Lakini alipokupeleka alikataliwa na wazazi wake kwa vile sicho kitu alichotumwa. “Ile ndiyo iliyokusaidia kurudi duniani bila hivyo ungejulikana kuwa umekufa. “Baada ya kukurudisha aliingia nawe katika vita nyingine ya kuchangia mapenzi, baada ya kuona mapenzi ya mchumba wako yote yapo kwako. “Aliamua kumuondoa nguvu za kiume ili msiweze kufanya tendo lile na yeye alikuja usiku na kufanya naye huku akiwa amemrudishia nguvu zake kamili. “Lakini la kuja usiku ndotoni hakulipenda, alitaka aje kama mwanadamu wa kawaida na kufanya mapenzi ya kawaida ya kutambuana na siyo ya ndotoni. “Aliweza kujitokeza hospitali, mpenzi wako hakujua kama yule ni jini, alimuona kama mwanamke mzuri na kumpa tiba ya ajabu iliyomponya kwa kuzirudisha nguvu zake za kiume. “Bila kujijua mchumba wako akaingia kwenye mtego wa kukubali kuanzisha uhusiano naye, kwa makusudi alipotoka hospitali alikwenda kumsuburi njia aliyojua atapita. “Baada ya kutoka hospitali, alimtafuta bila kumuona na kujikuta akitamani kuonana na

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mrembo yule tena. “Wakati anatoka hospitali alikupigia simu mkutane nyumbani ili kukuondoa majonzi yote kutokana na kushindwa kukufikisha katika tendo la ndoa. Hata alipokueleza hukuamini, lakini alikuhakikishia kitu kilichokufanya uahilishe safari ya kwenda kwa mganga kumuangalizia matatizo yake. “Nina imani mmebahatika kumuona Balkis jinsi alivyo mwanamke mzuri sana, ambaye hakuna mwanaume atakayemtaka akamkataa. Mchumba wako akaingia kichwa kichwa kumtaka kimapenzi, naye kujifanya kana kwamba hana shida na mumeo. “Lakini alimuuliza maswali, kama mumeo angekuwa na akili angetambua kuwa yule si mtu wa kawaida.” Mambo yanazidi kufunguka, endelea kujua wasifu wa jini Balkis, nini kitaendelea? Kuyajua yote tukutane baadae

     LIPOISHIA: “Nina imani mmebahatika kumuona Balkis jinsi alivyo mwanamke mzuri sana, ambaye hakuna mwanaume atakayemtaka akamkataa. Mchumba’ako akaingia kichwa kichwa kumtaka kimapenzi, kana kwamba hana shida na mumeo, alipoonesha dalili za kumtaka alimuuliza maswali ya mitego, kama angekuwa na akili angetambua kuwa yule si mtu wa kawaida. SASA ENDELEA... Lakini kutokana na kuchanganyikiwa na mapenzi, hakupata muda wa kujiuliza, Balkis alimuuliza maswali kuhusiana na uhusiano wenu, hakushangaa mtu kuonana naye mara ya kwanza kumuulizia vitu ambavyo hata watu wenu wa karibu hawajui. Alipomuulizia kuhusu kumtaka yeye wakati wewe ni mchumba wake, mwenzio alikukana na kusema kuwa wewe ni mpenzi wake si mke wake. Alipoulizwa kama yupo tayari kuoa mwanamke mwingine na kuachana na wewe, kutokana na kiwewe cha mapenzi alikubali kuwa yupo tayari na kuusema udhaifu wako. “Alipoulizwa tena yupo tayari kumuoa yeye Balkis alikubali. Aliutumia udhaifu wa mchumba wako kujenga uhusiano wa haraka na kutaka kuwa naye siku ile, pia alikubali. Walikubaliana kwenda nyumbani kwa mchumba wako, ili kutowagonganisha, mchumba wako alitaka kukupigia simu ili usiende, lakini Balkis alimzuia asikupigie simu na kukueleza uende na ulipokwenda ulimuona jinsi alivyobabaika baada ya kuingia na kwenda moja kwa moja chumba cha wageni alichokuwa ameingia Balkis muda ule ule. Ulishtuka baada ya kumuona ameingia ghafla chumbani, ni kweli?” “Ni kweli,” Suzana alijibu kwa sauti ya chini huku akiwa anaona muujiza mkubwa kutokana na maneno ya mganga ambayo mwanzo aliyaona kama simulizi ya kusisimua isiyo na ukweli. Lakini swali lile lilikuwa kama kitu kilichomtoa kwenye bumbuwazi. “Basi kitendo cha kuingia na kwenda moja kwa moja kilimtia wasiwasi mkubwa mchumba wako kwa kujua lazima utamkuta Balkis na kumfumania. Hata lugha zenu ziligongana kitu kilichokushangaza. Kingine kilichokushangaza kilikuwa kwa mpenzi wako kuwa tofauti na siku zote kukujibu kwa ukali jambo la kawaida. Baada ya kumuona humuelewi, ulikwenda chumba cha kulala, yeye alirudi hadi chumba cha wageni na kushangaa kumkuta Balkis akiwa amejaa tele kitandani. Alipotaka kujua alikuwa wapi alimwambia akuwahi chumbani ili akurudishe kwenye hali ya kawaida. Baada ya kuingia chumbani, penzi alilokupa ndilo lilikuchanganya na kusahau yaliyotokea muda mfupi. Usiku jini Balkis alikuja kukuchukua ukiwa usingizini na kukurudisha kwako na yeye kulala na mchumba wako mpaka asubuhi. Wote mlipoamka mlishtuka lakini hakuna aliyejua ukweli wa tukio la usiku ni kama ndoto au kweli. Ulipokwenda kwake asubuhi ya jana kupata uhakika kwa kilichotokea, ndani walikuwa mchumba wako na Balkis, ndiye aliyemweleza ujio wako. Ulipofika alikuwa mule mule chumbani amelala kitandani. Wewe hukumwona ila mwenzako alimwona kama kawaida, kitu kile ndicho kilichompa kigugumizi. Hali ile ilikuchanganya na kumuona kama mtu mwenye matatizo, wakati huo Balkis alimwambia mchumba wako kwa sauti ya juu ya kumkemea kuwa akikuuliza useme hukuja jana ili ujue kilichotokea si kweli bali ni ndoto. Lakini kwa yeye kuwepo pembeni ya kitanda karibu na Balkis aliyekuwa amelala pembeni yako bila wewe kumuona, ilizidi kumchanganya. Mchumba wako alipatwa na kigugumizi kwa kujua utanamuona Balkis, kubabaika kwake kulikufanya umtilie wasiwasi na kumuuliza swali ambalo lilimchanganya pale ulipotaja jina la Balkis kama jini, jina ambalo lilikuwa la mpenzi wake, kumtaja kama jini ilimuudhi sana Balkis na kukupuliza upepo uliokufanya upoteze fahamu. Kitendo kile mchumba wako alikiona na kumpandishia na kutaka kujua amekufanyia nini, Kauli ile ilimfanya Balkis kukasirika na kuondoa nguvu za kiume za mchumba wako na kutaka nawe kukutoa kizazi.” “Mama yangu!” Suzana alishtuka na kushika mdomo kusikia vile. “Usiogope, hakukutoa kizazi baada ya mchumba wako kumuomba msamaha na kuwa tayari kumuoa baada ya kumkataa kutokana na vitendo vyake visivyo vya kawaida. Baada ya Balkis kumsamehe aliamua kuondoka naye kwenda kuishi chini ya bahari.” “Mamaaa!” Suzana alipiga mayowe ya mshtuko. “Mungu wangu unataka kutuambia Brighton yupo ujinini?” Mama Sharifa aliuliza. “Ndiyo, lakini kwa sasa yupo katika matatizo.” “Matatizo! Matatizo gani tena jamani?” Suzana aliuliza kwa huzuni. “Baada ya kufika katika mji wa majini, baba mzazi wa Balkis alishtuka kuona mwanaye amekwenda na mwanadamu akimsema ndiye mume wake badala kupeleka alichotumwa. Hapo palitokea kutoelewana kati ya Balkis na baba yake, baba akitaka mwanaye arudi duniani kuendelea kutafuta vizazi zaidi vya wanawake ili apate dawa ya kuweza kupata ujauzito ili aolewe na jini mwenzake. Lakini Balkis hakuwa tayari kuolewa na jini mwenzake baada ya kuonja penzi la mwanadamu. Yeye aliamini kuolewa na mwanadamu kusingekuwa na haja ya kuendelea kuwatoa uzazi wanawake. Kwani angekutana kimwili na mwanadamu angeweza kupata bila kutumia dawa hiyo. Hapo ndipo palipozuka mvutano wa mtoto na baba, Balkis aliamini kwa vile anapendwa sana na baba yake atakubaliwa, lakini baba yake hakuwa tayari kuchanganya damu ya jini na mwanadamu. Baada ya kuona mtoto wake amemkosea adabu, alimuamuru mkuu wa Watwana anaitwa Kulani, Jini mweusi lakini mwenye nguvu. Kumchukua Balkis na mchumba wako kuwapeleka katika chumba cha giza.” “Kwa hiyo ndiyo harudi tena?” Suzana aliuliza. “Anaweza kurudi lakini mpaka atoke sehemu aliyofungwa.” “Bila ya hivyo hawezi kutoka?” Sharifa aliuliza. “Inategemea na uamuzi wa mfalme wa bahari kumtoa.” Mambo yanazidi kuwa mazito. Je, Brighton atapona au atauawa katika mji wa majini? Mganga njiwa Manga atawasaidia?





    @@@@@@@@@@@@@@@

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     “Hawezi kumuua?” Suzana aliuliza kwa sauti ya kukata tamaa. “Hawezi, nina imani atatoka tu, kinachotakiwa ni kuvuta subira.” “Mmh! Na mimi tatizo langu?” Sharifa aliuliza. “Wewe tatizo lako limepata bahati moja kubwa ambayo sawa na bahati ya mtende.” “Bahati gani?” Sharifa aliuliza huku akijiweka sawa. “Kitendo cha kufungiwa Balkis katika chumba cha giza, kimewawezesha kuja huku bila ya matatizo. “Una maana gani?” Sharifa aliuliza. “ Majini ni viumbe wasiokubali kuona wanavurugiwa mipango yao, Balkis kama angekuwa hajafungiwa lazima angeizuia safari yenu.” “Angeizuia kivipi?” “Mngekutana na vitu vya ajabu njiani hata kupinduka na gari lenu.” “Si tungekufa?” “Msingekufa, mngeumia tu ili msiweze kumfuatilia.” “Na bahati nyingine?” “Bahati nyingine wakati wa kufanya dawa ya kurudisha kizazi chako hakutakuwa na upinzani wowote. Wala kazi yako haitahitaji vitu vingi vya kufanya na itaanza leo saa sita za usiku baharini.” “Kama angekuwepo?” “Mmh! Pangechimbika, waganga wengi wamepoteza maisha kwa ajili ya kutaka kuvuruga mipango ya majini. Pia tungehitaji vitu vya gharama ili kumdhibiti hapo kazi ingetakiwa kufanyika saa nane za usiku baharini katika maji ya shingo.” “Mmh! Sasa akitoka si ataweza kutuua?” “Balkis ni jini lenye huruma sana, katika maisha yake hapendi kufanya vitu vibaya, hata kuolewa ilikuwa ni shinikizo la wazazi wake tu ambao walimlazimisha kutafuta vizazi vya wanawake ili aweze kupata tiba ya matatizo yake ya kushindwa kupata ujauzito. “Mwanzoni alikataa katakata lakini aliahidiwa kupewa zawadi kubwa kama atapata mtoto hasa wa kiume. Alikubali kuifanya kazi ile kwa shingo upande, lakini moyoni mwake hakupenda hata siku moja kutenda kitendo chochote kibaya kwa wanadamu, siku zote aliwaza kuishi duniani na kuolewa na binadamu. “Hata kazi ya kutoa vizazi ilimchukua muda mrefu sana, kitu kilichowafanya wazazi wake kumleta duniani moja kwa moja ili aweze kupata vizazi hivyo kwa muda mfupi, bila kujua Balkis hakupenda kuifanya kazi ile. “Siku Suzana alipoona sherehe ya ajabu juu ya bahari, hiyo ndiyo ilikuwa siku rasmi ya kuja duniani kwa Balkis kusaka vizazi vya wanawake na kuvipeleka baharini. Aliandaliwa jini mwingine ambaye kazi yake ilikuwa ni kuvipokea vizazi hivyo juu ya bahari katika eneo lile la Daraja la Salenda na kuvipeleka kwenye stoo chini ya bahari. “Lakini ilikuwa tofauti na walivyotegemea wazazi wake, tangu Balkis alipofika rasmi duniani kwa kazi hiyo, kwa siku moja alipeleka vizazi vinne tu na chako kikiwa kimojawapo. Kazi aliyotumwa alisahau baada ya kuvutiwa na uzuri wa mchumba wa Suzana na kujikuta akianzisha uhusiano wa siri bila mwenzako kujua. “Katika harakati za kuhakikisha anamdhibiti mchumba wako, muda mwingi aliutumia kuhakikisha anamchukua jumla badala ya kuifanya kazi aliyotumwa. “Aliweza kuwagonganisha kwa kuziua nguvu za kiume za mchumba wako na usiku ulipoingia alizirudisha ili afaidi yeye. “Hali ile ndiyo iliyowasukuma kutafuta suruhu ya tatizo lenu, alipoona mmeanza kupata mwanga aliwachanganyeni kwa kuzirudisha kitu kilichokufanya uone kama hakuna tatizo.Balkis alipofanikiwa kumnasa mchumba wako kwenye mtego wake, hakupanga kuondoka naye mapema. “Mngeendelea kushea mapenzi bila wewe kujua mpaka angeshika ujauzito. “Kosa alilolifanya mchumba wako ni kwenda kinyume na yale aliyokuwa akielekezwa na Balkis. “Kubabaika kwake kulipelekea wewe kuingia wasiwasi na kutamka neno lililomchukiza Balkis na kukupulizia hewa iliyokupoteza fahamu. Hali ile ilimfanya Balkis aone mpango wake umeharibika mapema, ili asiweze kumpoteza mpenzi wako aliamua kuondoka naye kwenda chini ya bahari. “Kutokana na huruma yake aliamini kama ataolewa na binadamu atakuwa ameokoa tatizo la wanawake kutolewa vizazi. Lakini ilikuwa tofauti na walivyotegemea wazazi wake ambao wao walimtuma kuishi duniani ili kufanikisha kupatikana kwa vizazi vingi vya mwanamke vitakavyomuwezesha kupata dawa ya kushika ujauzito ili aolewe na jini mwenzake. “Walishangaa kumuona akiwa na mwanaume wa kibinadamu na kumtambulisha kwao kama ni mume wake. Kitendo kile kiliwaudhi sana, naye hakutaka kukubali.Baada ya mvutano Balkis na mchumba wako waliwekwa kwenye chumba cha giza.” “Sasa kama unasema wazazi wake hawakukubali wataweza kumtoa salama Brighton?” Suzana aliuliza. “Hapa inaonesha maisha yake yapo zaidi ya hapo, Kwa hiyo hawezi kuuawa.” “Kama umeona anaweza kuendelea kuishi, itakuwa wapi duniani au kuendelea kufungwa kwenye chumba cha kiza?” Suzana alikuwa na shauku kutaka kujua hatma ya mchumba wake. “Kwa kweli haioneshi ataishi wapi ila kuna maisha marefu ya mchumba wako.” “Vipi kuhusu kazi yangu ya kurudisha kizazi kuna vitu vinatakiwa kwenda kununua?” Sharifa aliuliza. “Anatakiwa njiwa mwekundu tu, kwenye mabanda yangu anapatikana.” “Na mimi kumpata mchumba wangu utanisaidiaje?” Itaendelea

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    LIPOISHIA; “Sasa kama unasema wazazi wake hawakukubali wataweza kumtoa salama Brighton?” Suzana aliuliza. “Hapa inaonesha maisha yake yapo zaidi ya hapo, kwa hiyo inamaanisha hawezi kuuawa.” “Kama umeona anaweza kuendelea kuishi, itakuwa wapi duniani au kuendelea kufungwa kwenye chumba cha giza?” Suzana alikuwa na shauku kujua hatima ya mchumba wake. “Kwa kweli haioneshi ataishi wapi ila kuna maisha marefu ya mchumba wako.” “Na kuhusu kazi yangu ya kurudisha kizazi kuna vitu vinatakiwa kwenda kununua?” Sharifa aliuliza. SASA ENDELEA... “Anatakiwa njiwa mwekundu tu, kwenye mabanda yangu atapatikana.” “Na mimi kumpata mchumba wangu utanisaidiaje?” “Kama akitoka kwenye chumba cha giza tutampata, lakini kumtoa kule ni kazi ngumu, haonekani kila nikimtafuta.” “Kwa hiyo utanisaidia vipi?” “Kwa vile kazi ya mwenzako ni nyepesi ngoja tuifanye usiku wa leo, ya kwako itabidi nichimbe sana kuona kama kuna uwezekano wa kumtoa hata akiwa chumba cha giza.” Walikubaliana kuifanya kazi ile usiku wa siku ile, mganga aliwaruhusu wakapate chakula na kupumzika ili kuvuta muda. *** Majira ya saa sita usiku Sharifa alisimamisha gari lake pembeni kabisa na bahari maeneo ya pwani ya Bagamoyo, sehemu aliyoelekezwa na Mganga Njiwa Manga. Hali ya hewa ilikuwa giza la wastani, kwa mbali ilionekana miale ya moto ya wavuvi wa usiku. Baada ya kusimamisha gari hakuteremka walisubiri maelekezo ya mganga. Mganga Njiwa Manga alianza kuteremka kisha aliwaita, wote walitoka nje ya gari. Baridi la ufukweni lilikuwa kali, kila aliyekuwepo pale lilimchonyota hadi kwenye mifupa. Mganga alitoa vifaa vya kufanyia kazi, njiwa wa kazi alikuwa ameshikiliwa na Sharifa. Wote walikuwa kimya wakimsikiliza mganga ambaye alikuwa akitembea kuelekea baharini, mawimbi muda ule hayakuwa makali sana yalipiga taratibu. Mganga aliingia majini usawa wa maji ya mafuti na kumwaga vitu huku akizungumza maneno kwa sauti ya juu. “Ewe jini la bahari nakuletea zawadi hii ili bahari iwe tulivu, pia nimekuletea zawadi ya njiwa ili kuniruhusu niifanye kazi yangu bila kikwazo.” Baada ya kusema vile aligeuka bila kutoka ndani ya maji na kumwita Sharifa. “Kavue nguo zote kisha ujifunge upande wa kanga halafu uingie ndani ya maji na njiwa wako.” Sharifa alifanya kama alivyoelekezwa na mganga, aliingia ndani ya maji na kuwaacha mama yake na Suzana wakiwa wamesimama huku wakiendelea kupigwa na baridi kali ya upepo utokao baharini. Aliingia ndani ya maji ya baridi huku akiwa na hofu ya kutojua mganga anataka kumfanya nini hasa akiwa amejifunga upande wa kanga bila kitu chochote mwilini. Alipomfikia mganga alisogea naye mbele hadi maji ya shingo njiwa wake akiwa amemnyanyua juu. Baada ya kufika kimo kile cha maji, mganga alimwambia Sharifa amuweke kichwani, naye alifanya vile. Mganga alimshika sikio la kushoto na kuanza kuomba kwa lugha ya kiganga. Aliomba kwa kuzungumza maneno haraka haraka bila kumeza mate kwa zaidi ya nusu saa. Baada ya robo saa Sharifa alianza kusikia vitu vikikoroga tumboni, Sharifa alishindwa kufanya kitu kutokana na mikono kuwa kichwani amemshikilia njiwa. Mganga aliendelea kuzungumza maneno ya kiganga akiwa bado amemshikilia sikio, tumbo nalo liliendelea kumkoroga huku mwili ukizidi kupungua nguvu. Mara alianza kuona kiza mbele na kuangukia ndani ya maji na njiwa wake mkononi. Mganga aliwahi kumdaka na kujitahidi kumsimamisha lakini miguu haikuwa na nguvu, alipiga kelele kuomba msaada kwa mama Sharifa na Suzana waliokuwa nje ya maji. Nao walijikuta wakiingia kwenye maji na nguo zao bila kujijua kuwahi kutoa msaada kwa mganga. Walipofika ndani ya maji ya shingo walimsaidia mganga kumsogeza ufukweni, walipofika ilionesha kama Sharifa amepoteza fahamu. “Mganga mbona hivi?” Mama Sharifa aliuliza. “Ni kawaida kuna kitu kilikuwa mwilini mwake kimetoka lakini baada ya muda atakuwa katika hali ya kawaida.” Pamoja na Sharifa kupoteza fahamu mganga aliwaomba wambebe hadi ndani ya maji ili aendelee na tiba yake. “Sasa baba si unamuona alivyo kwa nini tusisubiri arudiwe na fahamu kisha uendelee na tiba?” Mama Sharifa aliuliza akiwa amejawa na wasiwasi juu ya hali ya mwanaye. “Mama unanifundisha kazi?” Mganga alimuuliza kwa sauti ya ukali. “Samahani baba.” “Sipendi kufundishwa kazi kama ulikuwa unajua kwa nini mlimleta kwangu?” “Nisamehe baba yangu.” “Basi naomba kila utakachokiona hapa ukae kimya.” “Nimekuelewa baba yangu nisamehe sana.” “Haya mbebeni muda unakwenda.” Mama Sharifa na Suzana walimbeba Sharifa mpaka maji ya chini ya mafuti mganga alimuomba Suzana akae chini ili ampakate mgonjwa. Suzana alifanya kama alivyoelezwa na mganga kisha Sharifa alilazwa chali juu ya Suzana. Mama yake alimshika sehemu ya kichwani ili kisiingie kwenye maji. Baada ya kulazwa mganga aliendelea na tiba yake kwa kuendelea kusema maneno ya kiganga kwa zaidi ya nusu saa. Huku njiwa aliyekuwa amelowana akimshikilia kwenye tumbo la Sharifa. Baada ya muda mganga alinyamaza ghafla na kupita kimya kizito kikifuatiwa na upepo mkali. Baada ya muda upepo ulikoma. Suzana na mama Sharifa kila mmoja aliingiwa na wasiwasi kutokana na hali iliyojitokeza mle baharini. Kila moja alimuomba Mungu kimoyomoyo. Baada ya upepo kutulia ilisikika sauti ya Sharifa ikiita. “Mama...mama...mama.” Mama Sharifa hakuitikia alimuangalia mganga aliyekuwa bado akitazama upepo ulipotokea na kunyanyua mkono.



    @@@@@@@@@@@@



     ILIPOISHIA: “Nipo mimi” Suzana alijibu. “Haya fanyeni haraka mkimaliza mniite.” Walimbeba Sharifa ambaye hakuwa na nguvu hadi ndani ya gari na kumbadili nguo zake kisha walimwita mganga ili waondoke kurudi nyumbani. SASA ENDELEA... Mganga aliingia kwenye gari, Suzana aliliendesha mpaka nyumbani kwa mganga, walipofika walimteremsha Sharifa ambaye alitembea kwa tabu. Walipomfikisha sebuleni walimlaza kwenye mkeka na kumsuburi mganga aliyekuwa amemshika njiwa aliyekuwa tayari ameshamchinja tangu baharini. Mganga alimwomba mkewe awape nguo za kujifunga wateja wale kutokana na nguo zao kulowana na maji ya bahari walipokuwa wakimtoa Sharifa kwenye maji. Baada ya kubadili nguo alimpa mkewe yule njiwa na kumweleza amnyonyoe na kumchemsha. Mkewe alimchukua na kuondoka naye na kuwaacha kina Suzana sebuleni. Majira ya saa kumi za usiku mganga alimwamsha Sharifa na kumpa dawa ya njiwa aliyechemshwa kwa ajili ya kumla akiwa katika sufuria ile ile aliyochemshiwa. “Mle njiwa wote na unywe na supu yake,” mganga alimwambia Sharifa ambaye bado mwili wake ulikuwa hauna nguvu. Sharifa alianza kumla njiwa na kunywa supu yake kwa shida kwa vile alichemshwa bila kuwekwa chumvi, alipomuona kama anamshindwa kutokana na kutokuwa na kiungo hicho aliuliza. “Mbona hana chumvi?” “Huyo hawekwi chumvi, jitahidi umle vivyo hivyo, tena una bahati njiwa ni mdogo, watu wanakula kuku mzima bila chumvi.” Sharifa hakuongeza neno alimuinamia njiwa wake na kuendelea kumla taratibu mpaka alipommaliza, wakati huo Suzana na mama yake walikuwa wakikoroma. Baada ya kumaliza kumla njiwa aliruhusiwa kuendelea kulala na wenzake ambao walikuwa hawajitambui kwa usingizi. Wote waliamshwa alfajiri kwa ajili ya tiba ya mwisho ya kuoga maji ya bomba yaliyochanganywa na yale ya .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baharini. Baada ya kuoga waliingia kwenye chumba cha mganga kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani. Wote walikaa kwenye mkeka baada ya mganga kutulia kwa muda huku akipitia maelezo kwenye karatasi nyeupe iliyoandikwa kwa wino mwekundu kisha alisema kwa sauti ya chini: “Nina imani kazi yetu imekwenda vizuri sana tofauti na nilivyofikiria, shughuli kama hii niliifanya siku za nyuma kwa muda wa wiki nzima, tena nikiwa na majeraha mengi kutokana na kushindana na jini.” “Unataka kuniambia nimepona?” Sharifa aliuliza. “Umepona.” “Kwa hiyo nina uwezo wa kushika mimba?” “Bila shaka.” “Nashukuru sana mzee wangu,” Sharifa alinyanyuka kwa lengo la kumpigia magoti. “Hapana mama kaa tu, wakushukuriwa ni Mungu yeye ndiye mwenye kukubali au kukataa maombi yetu.” “Ina maana kama Balkis angekuwa hakufungwa kazi isingeisha leo?” Suzana aliuliza. “Kazi ya kushindana na majini ni ngumu msione imekwenda kirahisi kiasi kile, kama Balkis angekuwa hajafungwa vita ingekuwa kubwa asingekubali tuchukue kizazi katika stoo yake. Lazima ingetakiwa niwe na vijana wangu wa kazi na katika kumdhibiti wangetakiwa mbuzi wekundu wawili, shuka nyekundu mbili na vitu vingine vingi.” “Kutokana na kauli za mganga wa awali kuwa matatizo mengi ya tumbo yanatokana na jini Balkis kuchukua vizazi vya wanawake, lakini mbona ni wanawake wengi wana matatizo tofauti na idadi ya vizazi vilivyoko kwenye stoo ya Balkis?” Sharifa aliuliza. “Kama nilivyowaeleza majini wanaishi kama wanadam, jinsi matatizo yetu yanavyofanana basi na ya majini huwa ni vivyo hivyo. Majini wengi wenye matatizo ya kukosa uzazi hutumwa duniani kuifanya kazi kama ya Balkis, hivyo vita si vyake peke yake ni kwa majini wengi.” “Mungu wangu sasa tutapona vipi?” Suzana aliuliza. “Kupona inategemea na wewe kuonana na watu wenye uwezo kama sisi au kusimama katika imani yako.” “Kusimama kwenye imani una maana gani?” Sharifa aliuliza. “Kila anayesimama katika imani humtanguliza Mwenyezi Mungu mbele kwa kila jambo, kabla ya kulala huomba ulinzi wake na baada ya kuamka humshukuru kwa kumvusha usiku salama, kisha humuomba tena amlinde na mchana wote.” “Mbona tunafanya hivyo?” Alisema Suzana. “Unaweza kuwa unafanya kutimiza wajibu wa maombi lakini imani yako si kamili, siku zote imani husimama kwa matendo siyo kwa maneno.” “Unataka kuniambia aliyesimama kwa imani ya matendo mema hawezi kupatwa na tatizo hili?’ “Litaingilia vipi wakati Mungu ndiye mlinzi wake, hata hao majini wanamuogopa na kumuabudu yeye.” “Kutokana na maelezo yako sasa hivi nimepona kabisa?” Sharifa aliuliza. “Umepona na wala haitakutokea tena.” “Kwa mfano Balkis akitoka gerezani, akijua nimerudishiwa kizazi changu si litakuwa tatizo?” “Tatizo litabakia kwake, wewe utakuwa salama kuanzia asubuhi hii.” “Ile hali ya tumbo kuvurugika nilipokuwa pale baharini ilitokana na nini?” “Kizazi chako kilikuwa kikirudi sehemu yake.” “Baba tunashukuru kwa msaada wako,” mama Sharifa alisema kwa niaba ya mwanaye. Nini kiliendelea?

     ILIPOISHIA; Uso wake ulionesha huzuni kitu kilichomtisha mumewe ambaye alitaka kujua kulikoni. “Vipi mahabuba wangu?” “Mambo yameharibika.” “Kivipi?” “Mpango wetu umeingia kwenye mtihani wa kwanza.” “Mtihani upi?” “Kizazi kimoja kimechukuliwa.” “Tufanye haraka kabla hakijarudishwa kwa mwenyewe tumtume Kulani akaifanye kazi hii kabla hakujapambazuka.” “Tumechelewa tayari kimeisharudishwa kwa mwenyewe.” “Umejuaje?” “Damu ya sehemu kilipotoka nilipoigusa imeganda kidoleni.” “Ooh! Nani anataka kuchezea himaya yangu lazima nimkomeshe,” Mfalme Barami Hudirud alisema kwa hasira. “Hebu kaniletee damu ya sehemu iliyotoka kizazi ili nimjue ni nani?” SASA ENDELEA... Malkia Huleiya alikwenda hadi kwenye chumba cha siri na kurudi na damu ya sehemu iliyochukuliwa kizazi cha Sharifa na kumpelekea mumewe. “Naomba niilambe.” Malkia Huleiya alimlambisha mumewe, mfalme alitulia kwa muda kisha alisema: “Nimeishamjua, nitamtuma Kulani akishindwa nitakwenda mwenyewe. Lazima nitamuonesha mimi ni nani.” “Umemgundua ni nani?” “Kuna mshenzi mmoja anataka kushindana na nguvu zangu, nataka mpaka kutakapopambazuka awe amebakia jina.” “Kulaniiiiii,” aliitaka kwa sauti ya juu ambayo kama mwanadamu angeisikia basi angepasuka ngoma za masikio. Kulani aliyekuwa mbali alikuja mbio na kupiga magoti mbele ya mfalme. “Rabeka mtukufu mfalme.” “Nataka uende duniani, damu hii itakuongoza mpaka kwa mtu huyu, nataka umfutilie mbali, sawa?” “Sawa mtukufu mfalme.” “Haya ondoka mbele yangu, usirudi mpaka umemfutilia mbali kiumbe huyo dhaifu anayetaka kucheza na nguvu zangu.” Kulani alizama chini ya ardhi na kutoweka, baada ya muda alikuwa pembeni ya bahari eneo la Bagamoyo, aliilamba damu aliyopakwa kidoleni ambayo ilimuelekeza aende upande upi. Alitoka eneo baharini na kuelekea kwa Mganga Njiwa Manga. Alitembea taratibu toka eneo la bahari akiwa katika umbile la kibinadamu, hakuchelewa kufika kwenye makazi ya watu. Aliilamba tena ile damu iliyokuwepo kidoleni mwake, kwa vile kulikuwa na giza, sehemu ya Mganga Njiwa Manga ikawaka mwanga wa taa. Mwanga ule ulimuongoza hadi karibu kabisa na nyumba ya Mganga Njiwa Manga. Nia yake kubwa ilikuwa kwenda mpaka mlangoni na kugonga ili akifungua tu wakutane uso kwa uso na ammalize pale pale kisha aondoke kabla hakujapambazuka. Alitembea kuelekea eneo la nyumba ya mganga, ajabu alipokaribia nyumba yake alishangaa kuona moto ukiwaka kuizunguka nyumba ile. Hali ile ilimshtua sana, aligeuka na kutimua mbio hadi baharini ambako alikunywa maji mengi na kurudi hadi kwenye eneo la nyumba ya mganga. Alipoikaribia moto uliwaka tena, alilisogelea eneo la nyumba huku akimwaga maji aliyoyachukua baharini kwa lengo la kuuzima moto ule. Alifanikiwa lakini alipotaka kuingia kwenye himaya ile moto uliwaka tena. Alijikuta akifanya kazi ya kwenda baharini na kurudi, kila alipouzima moto na alipotaka kuingia uliwaka tena. Kulani alijikuta akitumia muda mwingi kwenda baharini kuchukua maji na kurudi huku moto ukizimika na kuwaka. Mpaka kulipokuwa kunakaribia kupambazuka hakuweza kuingia katika himaya ya Mganga Njiwa Manga. Kwa upande wake aliiona kazi imekuwa ngumu au maji yalikuwa marefu na kuamua kurudi chini ya bahari, aliogopa kutokana na kauli aliyopewa na Mfalme Barami Hudirud kuwa asirudi chini ya maji mpaka ahakikishe amemmaliza Mganga Njiwa Manga. Kulani alijikuta kwenye wakati mgumu katika kazi ile, tofauti na zilizotangulia ambazo alizifanya kwa muda mchache. Lakini ile ilikuwa ngumu kwake, baada ya kukutana na kikwazo cha moto. Aliamua kurudi hadi baharini akiwa katika umbile lile la kibinaadamu, alisubiri jua litochomoze ili aweze kwenda jirani kwa mganga na kumsuburi akitoka ammalize. Jua lilipotoka na watu kuwa wengi kujaa ufukweni kwa ajili ya kununua samaki na wengine wakipanda ngarawa kwenda kuvua. Kulani alijichanganya na watu bila ya kujulikana kama ni jini. Baada ya pwani kuchanganya na watu kuongezeka, alijitoa eneo la bahari na kwenda kwa mganga kwa kutembea kama mtu wa kawaida. Kila aliyemuona hakumdhania vibaya, aliacha eneo la bahari na kuingia makazi ya watu, alipokaribia maeneo ya nyumba ya mganga aliuona moto ukiwaka tena. Alikwenda kwenye nyumba ya jirani na kuomba kupumzika, kutokana na kuonekana kama mstaarabu, alikaribishwa na kupewa kiti. Mwenyeji wake hakujishughulisha naye aliendelea na shughuli zake na kumuacha Kulani akitupia jicho njia ya kutokea kwa Mganga Njiwa Manga. Jini Kulani ataweza kutimiza azma yake ya kumuua Mganga Njiwa Manga?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog