Search This Blog

SHAMBA LA URITHI - 4

 







    Simulizi : Shamba La Urithi

    Sehemu Ya Nne (4)



                

    akanyanyua mkono wake uliokuwa umeshikilia Kiboko...Pamera akaingiwa na hofu akamtazama askari huyo kwa macho ya uwoga...ghafla askari huyo akasita kumpiga Pamera! akabaki anamtazama kwa macho ya mshangao!!! kisha akaondoka zake.

    Pamera akabaki anamtazama askari huyo kwa macho ya uwoga....hakuamini ka kanusurika kupigwa viboko!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    akabaki anajiuliza maswali yasiyokuwa na majibu,,"kwa nini kaacha kunipiga,,pia amenitazama kwa mshangao..

    kumbe askari huyo alisita kumpiga Pamera kitokana na umri pamoja na mwili mdogo wa Pamera...Pia alikumbuka kuwa anawatoto wa kike wenye umri sawa na Pamera!!!!akajifikiria je? ndiye angekuwa mtoto wake anafanyiwa hivyo ingekuwaje? akajikuta anaingiwa na roho ya huruma!! na ndiyo sababu iliyomfanya asimpige Pamera.

    Wafungwa wakaendelea kufanya kazi walizopewa..wakajifanya walikuwa hawatazami kinachoendelea!



    Baada ya masaa mawili kupita wafungwa walimaliza kazi hiyo...na kengere ikagongwa ya kuashiria kuwa ni muda wa chakula,,wafumgwa wote wakaenda kichukua sahani kwa ajili ya kupata chakula..



                           *********************



    Siku zilizidi kusonga,,,siku ya leo alionekana Kabi,akizipiga hatua kuelekea kule kwenye banda la chipsi..akiwa njiani mawazo yalimzonga kichwaninmwake aliwakumbuka sana ndugu zake..yeye aliamini kuwa ndugu zake walikufa na kuteketea kwa moto uliyounguza nyumba waliyokuwa wanaishi....akajikuta anapoteza furaha...



    wakati huo huo alionekana subira akiwa mtaani akitembea pasipokujua ni wapi anakoelekea...Subira alikuwa analala nje..kwenye vibaraza vya maduka hapo mjini...katika pitapita zake..akajikita anatokezea kwenye barabara ambayo anapita Kabi kwa muda huo huo...kwa mbali Subira akamuona Kaka yake(Kabi)

    Subira hakuamini macho yake! akatimua mbio kumfuata Kabi huku akimuita kwa kulaza sauti,,"KAKAAAAA!

    Kabi hakuweza kusikia sauti hiyo kwa sababu alikuwa katika dimbwi zito la mawazo...Subira aliendelea kutimua mbio alipomkaribia kaka yake akamrukia kwa furaha! Kabi akatahamaki!!! aliootazama kwa makini akashtuka kumuona mdogo wake!! akajikuta analia kwa furaha akamkumbatia mdogo wake..pia Subira akajikuta anatokwa na machozi! hakutarajia kukutana na kaka yake kwenye mazingira hayo..

    Kabi akauliza,,"wengine wako wapi??

    Subira akabaki kimya huku uso wake ukitazama chini...kisha akasimulia mkasa mzima mpaka alivyopotezana na ndugu zake kule hospitali.

    Kabi akasikitika sana...lakini akamshukuru Mungu kwa kumkutanisha na ndugu yake!! pia akafarijika baada ya kujua kuwa kumbe wadogo zake bado wapo hai...akamtazama mdogo wake kwa macho ya huruma kisha akauliza tena,,"je? dada Pamera yuko wapi?

    Subira akajibu,,"hata sijui aliko!

    Kabi akauliza ,,"umekula?

    Subira akasema,,"hapana sijala tangu jana..nahisi njaa.

    Kabi akamtazama mdogo wake kwa macho ya huruma akasema,,"nifuate,

    wakaongozana mpa kule kwenye banda la kuuza chipsi.

    walipofika Kabi akamtambulisha Pamera kwa bosi wake..akamuomba afanye kazi pamoja na mdogo wake..bosi huyo akakubali Pamera afanye kazi lakini bila malipo...wakaanza kumenya viazi na kuvikatakata....

    ilipofika nyakati za mchana wakapewa chakula..

    Kabi akala pamoja na mdogo wake...

    ilipofika nyakati za usiku...banda la chipsi likafungwa...Kabi akaongozana na Subira wakaondoka...

    Subira akauliza tunaenda wapi?

    Kabi akajibu ,,"tunaenda kulala...Subira akabaki kimya bila kuuliza swali lolote.

    wakaongozana mpaka kwenye nyumba ambayo haijamalizika ujenzi wakaingia kwenye nyumba hiyo...ndani ya chumba kimoja kilichokuwa kimetandazwa mabox mengi...Kabi akasema,,"hapa ndipo ninapolala...tutaishi hapa wote..wakalala

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                       ***************************



    Siku zilizidi kusonga...kule nyumbani kwa msamalia,,walionekana wadogo zake pamera,,lakini hawakuwa na furaha kwa sababu hawajui Subira yuko wapi....

    Siku zilizidi kusonga,,msamalia huyo aliwalea kama watoto wake..akaamua kuwapeleka shule..wakaanza masomo....

    sikumoja Subira pamoja na Kabi walikuwa njiani wakielekea kule kwenye banda la chipsi....



    wakati huo huo,Lulu,,Konje pamoja na Jack walikuwa ndani ya basi la shule,wakielekea shuleni

    Konje akaangaza angaza macho yake kutazama nje...akashtuka kumuona kaka yao(Kabi) pamoja na Subira!! akachomoza kichwa chake dirishani akapaza sauti,,"SUBIRAAAA.

    Kabi akashtuka...akahisi kaisikia sauti ya mdogo wake...akaangaza angaza macho akamuona Konje  ndani ya basi hilo la shule....akasema,,"tazama kule Konje yumo ndani ya gari..Subira alipogeuza shingo yake..pia akamuona Konje.....wakaanza kulikimbiza basi hilo huku wakimsihi dereva asimamishe gari...lakini gari lilizidi kusonga na kutokomea kabisa!



               *****************************



    Upande mwingine,kule kijijini..alionekana Shangazi yao Pamera akiwa ndani ya nyumba ya marehemu baba yao...akahisi kama kamuona mtu kwenye korido!!! mtu huyo akaingia chumbani!!

    akaamua kunyanyuka kwenda kutazama ni nani ameingia chumbani..wakati milango ya kutokea nje ilikuwa imefungwa....alipoukaribia mlango wa chumba hicho...punde si punde ikasikika sauti ya mlango wa sebuleni ukifunguliwa...vikasikika vishindo vya mtu akitoka nje ya nyumba hiyo.. ...shangazi yake Pamera akaanza kuingiwa na wasiwasi..akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea Sebuleni..alipofika akashtuka kukuta mlango upo wazi....





    wasiwasi ukazidi kuongezeka! akazipiga hatua za kunyatia huku macho yake yakitazama kwa tahadhari..akausogelea mlango akaufunga...kisha akazipiga hatua za harakaharaka kuelekea chumbani,,akaingia na kujifungia...akajilaza kitandani...lakini alikosa amani akashindwa kuendelea kuwemo ndani ya chumba hicho...akanyanyuka akato nje ya nyumba hiyo,,na kuelekea kwa rafiki yake wa karibu......akiwa njiani akahisi kasahau simu yake kule nyumbani!!akafungua mkoba wake,akaangaza angaza macho yake ndani ya mkoba,,hakuiona simu....akaamua kurudi nyumbani akachukue simu yake....alipofika akastuka akaona nyumba imezungukwa na maji mengi mpaka usawa a dirisha!

    akajiuliza,,"haya maji yametokea wapi na hakuna dalili ya mvua!!

    mbona maajabu? wakati anajiuliza maswali hayo ghafla yale maji yalitoweka kimiujiza...akaingiwa na hofu akatimua mbio na kutokomea kusikojulikana!



                           ***********************



    Upande mwingine kule kwenye shule wanayosoma wadogo zake Pamera..alioneka Konje akiwa na mawazo mazito,,,aliwaona ndugu zake lakini hajui atawapata wapi.

    akajikuta machozi yanamtoka mfululizo..mwalimu aliyekuwa akifundisha aliona Konje analia,akasitisha kuendelea kufundisha akamfuata Konje mpaka pale kwenye dawati...akamuuliza ,,"unamatatizo gani? mbo unalia!!?

    Konjo hakujibu kitu chochote...

    mwalimu akaamua kumuacha Konje na kurudi kule ubaoni kufundisha! lakini akajisemea moyoni,,"bila shaka kutakuwa na jambo linalomsumbua mtoto huyu...hata pia ndugu zake wapo katika hali hii wacha nikimaliza kufundisha nijaribu kuwadadisi wanatatizo gani?



                       ************************



    Wakati huo huo alionekana Kabi na Subira wakizipiga hatua kuelekea kule kwenye banda la chipsi,,wakiwa njiani..wakashtuka kuona watu wanakimbia ovyo...kwa mbali wakaona wanamgambo wakibomboa vibanda na kuzuia machinga wasiendelee kuuza bidhaa au kufanya bihashara kwenye eneo la barabara....

    Kabi na Subira wakaendelea kuzipiga hatua...hatimae wakafika kule lilipokuwepo banda la chipsi....Wakashtuka kukuta banda hilo limebomolewa na wanamigambo....Kabi akanyong'onyea..akabaki kajishika mikono kichwani..akaangaza macho yake akamuona bosi wake amefungwa pingu na kuingizwa ndani ya gari la wanamigambo hao...

    Subira akatokwa na machozi akasema,,"tutakula wapi?

    Kabi akageuza shingo yake na kumtazama mdogo wake kwa macho ya huruma..naye pia akajikuta anatokwa na machozi...

    wakazipiga hatua wakaondoka zao..walitembea bila kujua ni wapi waendako!!!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                   *****************************



    Upande mwingine alionekana yule mwanaume aliyemuokota mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia yao Pamera...

    yeye na mkewe walimlea mtoto huyo kama mtoto wao wa kumzaa...

    siku ya leo walimchukua mtoto huyo na kuelekea ufukweni kwa ajilinya matembezi pia kupunga upepo wa ziwani...



    wakati huo huo alionekana Kabi na Subira wakizipiga hatua..kwa mbali wakaona ziwa,,,Kabi na Subira wakastaajabu sana!!!! tangu wazaliwe hawajawahi kuona ziwa,walizoea kuona mito na mabwa kule kijijini kwao, wakaamua kulifuata ziwa hilo..walipofika wakastaajabu kuona watu wengi wakiongelea..Kabi na Subira wakajikuta wanafurahi na kusahau kuhusu banda la chipsi.

    wakavua nguo zao na kuingia ndani ya maji kuogelea..



    Baada ya lisaa limoja kupita..lilionekana lile gari la yule dereva pamoja na mkewe,,waliomuokota mdogo wake Pamera...wakaliegesha kisha wakashuka kutoka ndani ya gari...wakaongozana pamoja na yule mtoto...wakaelekea ziwani...

    mtoto huyo alifurahi sana akajumuika na watoto wenzake kuogelea,,,,

    kutokana na wingi wa watu waliokuwepo hapo kwa ajili ya kuogelea....Kabi na Subira hawakumuona mdogo wao...

    baada ya masaaawili kupita..yule mke wa dereva akamfuata mtoto huyo na kumwambie atoke ndani ya maji avae nguo waondoke wakapate chakula cha mchana!

    mtoto hiyo akatoka kwenye maji na kuvaa nguo zake mpya alizonunuliwa.....wakaongozana kulifuata gari waondoke...



    Kabi akahisi kama kamuona mtoto anafanana na mdogo wake! alipotazama kwa makini akamuona vyema kuwa ni mdogo wake...akapaza sauti kumuita..

    kutokana na upepo uliokuwa unavuma ziwani hapo,sauti ya Kabi haikuweza kufika mbali...Kabi akaamua kutoka ndani ya maji haraka..akatimua mbio kumfuata mdogo wake..akasita kuendelea kukimbia baada ya kugundua kuwa yupo uchi..akarudi haraka kule alipoziweka nguo zake akavaa haraka haraka...

    wakati huo Subira alikuwa akiogelea na watoto wenzake hakujia kinachoendelea...

    Kabi aliapomaliza kuvaa akatimua mbio kumfuata mdogo wake..alipofika kule nje akaliona gari linaondoka..akalikumbuka gari hilo ndilo alilolipanda kuja mjini..pia siku ile alimuona mtoto anayefanana na mdogo wake ndani ya gari hilo!

    akajaribu kulikimbiza gari hilo lakini hakufanikiwa kulipata..akajikuta anatokwa na machozi huku akishuhudia gari hilo linatokomea....akazioiga hatua na kuketi kando ya barabara huku kajiinamia....akaendelea kulia kwa uchungu.



    wakati huo huo kule ziwani,, alionekana Subira akimtafuta Kabi.. lakini hakuweza kumuona! akaamua kuvaa nguo zake akaendelea kumtafuta kaka yake..

    alimtafuta kila kona lakini hakumuona Kabi..akaanza kuingiwa na wasiwasi....akaamua kuondoka zake kurudi kule kwenye ile nyumba ambayo haijamalizika ujenzi,,,ni kule anapolala yeye na kaka yake.



    Baada ya lisaa limoja kupita,, Kabi akakumbuka kuwa alikuja na mdogo wake akaamua kumfuata ili amwambie waondoke...alipofika akaangaza macho yake lakini hakumuona Subira..akamtafuta bila mafanikio!! alipoulizia kwa watoto waliokuwa wanaogelea na Subira wakasema,"ameondoka.

    Kabi akatimua mbio kurudi kule barabarani..alipoangaza angaza macho yake,hakumuona Subira..akajisemea moyoni,,"bila sha atakuwa karudi kule tunapolala...wacha nimfuate...



                          ************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana Subira akizipiga hatua,,akakaribia kuifikia ile nyumba ambayo wanalala yeye na kaka yake....kwa mbali akaona watu wakiingia na kutoka ndani ya nyumba hiyo huku wamebebelea makarai!!!

    akazipiga hatua za haraka haraka..alipofika akaona mafundi wanaendelea na ujenzi.......huku mmiliki wa nyumba hiyo akiwasisotiza mafundi kuwa ndani ya wiki moja wawe wamemaliza ujenzi anataka kuhamia yeye na familia yake.



    Subira akajikuta anatokwa na machozi pasipokutarajia! akaamua kuzipiga hatua,,akaondoka zake,Subira alitembea huku macozi yakimtoka.. hata alikuwa hajui ni wapi anaelekea! 



                   **************************



    Upande mwingine, alionekana Kabi akizipiga hatua,kuelekea kule kwenye ile nyumba ambayo haijamalizika ujenzi, akiamini kuwa mdogo wake yupo huko.

    Kabi alitembea kwa mwendo wa lisaa limoja mfululizo.. akawa amefika..

    macho yakamtoka!!! akajikuta ananyong'onyea baada ya kuona ujenzi unaendelea kwenye ile nyumba aliyokuwa analala,,akahisi kuchanganyikiwa alipotahamaki akagundua kuwa Subira hayupo eneo hilo!!  akajiuliza moyoni,, "Subira atakuwa kaenda wapi? 

    Kabi akaamua kuzipiga hatua za harakaharaka kurudi kule ziwani,, kumtafuta Subira..



    wakati huo huo Subira alionekana akiwa barabarani anatembea,, akaanza kuhisi njaa!!  kwa mbali akaona mgahawa,,, akaamua kuuufuata mgahawa huo akaombe msaada wa chakula,, alipofika akaingia ndani ya mgahawa huo akaeleza shida yake kwa mmoja wa wahusika wa mgahawa huo...

    ikasikika sauti ikisema!  wateja wanataka huduma unaongea nini na huyo mtoto?

    sauti hiyo ilikuwa ya mama mmiliki wa mgahawa huo.

    Muhudumu wa mgahawa huo akamuonea huruma mtoto Subira.. akasema kaketi paele binti,, nakuahidi utakula!  Subira akamtazama muhudumu huyo kwa macho ya shukrani ya dhati, kisha akasema asante sana dada.

    Muhudumu huyo akazipiga hatua,, kuelekea upande wa jikoni... akachukua chakula lilichoagizwa na mmoja kati ya wateja waliokuja ndani ya mgahawa huo, akakipeleka kwa muhusika.. kisha akarudi jikoni akasema weka sahani moja ya wali nyama... bila kichelewa chakula kikawekwa, akakipokea na kumpelekea Subira!

    Subira akasali kabla ya kula,, alizoea kufanya hivyo kutokana na malezi ya kimaadili na kidini aliyowafundisha baba na mama yao!  kisha akaanza kula chakula hicho.

    kutokana na njaa kali aliyokuwa nayo alikishambulia chakula hicho ndani ya dakika kadhaa kikawa kimekwisha,, pia akashiba kabisa.. akazipiga hatua kumfuata yule muhudumu akasema,, "asante kwa chakula nimeshiba... Subira akazipiga hatua kutoka nje ya mgahawa.... Mama mmiliki wa mgahawa huo akamuona Subira anatoka bila kulipia chakula... akamuuliza muhudumu aliyemuhudumia Subira..,, "mbona yule mtoto anaondoka bila kulipia chakula?

    yule muhudumu akasema,, "ni mdogo wangu,, naomba unikate kwenye mshahara wangu..

    Mama mmiliki wa mgahawa huo,, akakasirika sana akaamua kumsimamisha kazi muhudumu huyo.. kisha akamlipa nusu ya mshahara wake na kumwambia aondoke muda huo huo!!

    yule muhudumu akasikitika sana,, lakini akawa hana namna,, akatoka na kuondoka zake,, kabla hajafika mbali.. akamuona Subira ameketi kando ya barabara,, akajisemea moyoni,, "bila shaka mtoto huyu anamatatizo!

    alipomkaribia akamuuliza,, "binti unaishi wapi? 

    Subira akajibu,, "sina pakulala ile nyumba tuliyokuwa tunalala mimi na kaka yangu,,,inajengwa.

    mwanamke  huyo akauliza,, "nani anaijenga?

    Subira akajibu,, "mwenye nyumba pia sijui tutalala wapi?

    Mwanamke huyo akauliza,, "kaka yako yuko wapi?

    Subira akajibu,, "tumepotezana na sijui nitampata wapi?

    Mwanamke huyo akaingiwa na roho ya huruma akaamua kumchukua subira na kwenda kuishi nae nyumbani kwake!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                        ****************************



    Siku zilizidi kusonga,,

    Upande mwingine kule Gerezani, alionekana Pamera akiwa amelala usingizi,, akaamshwa na mwanamke mmoja,kisha mwanamke huyo akamwambia Pamera aende akamfulie nguo zake za ndani, Pamera hakuwa na budi kukubali kwa sababu mwanamke huyo alikuwa mkorofi sana.. aliwaone wafungwa wenzake,,wakati mwingine aliwapiga, bila huruma.... Pamera akasema,, "nahisi uchovu kutokqna na kazi ngumu nilozofanya leo,, naomba nikufulie kesho?!

    yule mwanamke akamfata Pamera kwa lengo la kumpiga ghafla akatereza na kudondoka chini, akapigiza kisogo,, akafa papohapo!

    Wafungwa wengi walishuhudia tukio hilo,, wakaanza kupaza sauti na matusi wakimtukana mwanamke huyo,, wakisema bora ufe kwanza hatukupendi.. kelele hizo ziliwashtua maaskari wakaja!  wakakuta mfungwa mmoja ameanguka chini.. walipomtazama wakagundua amekufa,, askari mmoja akauliza,, "mfungwa mwenzenu kapatwa na nini?

    bila kuchelewa wakaelezea tukio zima!!

    askari huyo akaamuru maiti hiyo itolewe ndani ya gereza.. kisha ipelekwe mochwari... akateuwa wafungwa wanne... pamoja na Pamera akiwa miongoni mwao!  wakaibeba maiti hiyo na kuitoa nje.. wakaiweka ndani ya gari.......wale wafungwa watstu wakarudi ndani ya gereza,, apamera akabaki kasimama hapo... akaangaza angaza macho yake,, akaona maaskari hawatazami eneo hilo.. akaingia haraka chini ya uvungu wa gari... kwa sababu gari hilo. lilikuwa kubwa... akaweza kuning'inia chini ya gari hilo kwa kushikilia vyuma kwa nguvu zake zote!

    baada ya dakika kadhaa akaonekana askari mmoja akiingia ndani ya gari hilo na kuliwasha,, lango kuu likafunguliwa na gari likaondoka kuelekea mochwari.



    Wakati huo huo,, walionekana Lulu,,,,Konje na Jack,  wakiwa ndani ya nyumba ya yule msamalia...aitwae Timo, siku ya leo ni jumamosi hivyo hawakwenda shuleni,, walibaki nyumbani... Timo aliwapenda sana watoto hao kwa sababu walikuwa na adabu na utii......Timo akasema,,"leo mchana nitawapeleka matembezi,,mnapenda niwapeleke wapi?  Lulu akadakia ,akajibu tupeleke kwenye michezo ya watoto wenzetu,

    Timo akasema,,"nitawapeleka mkabembee,,

    watoto hao wakafurahi sana,, wakaanza kumuimbia Timo nyimbo walizofundishwa shuleni!  Timo akafurahi sana... kisha akasema nendene mkajiandae,,wakanyanyuka wakazipiga hatua kuingia chumbani,,,

    wakati huo Timo alikuwa akiwatazama watoto hao,, akajisemea moyoni,, "ama kweli watoto ni baraka ndani ya nyumba, awe mtoto wako au sio wako,, yani saijui kwa nini ninaamani ya moyo! tangu siku wayot hawa wameingia ndani ya nyumba yangu..



                  ********************************



    Upande mwingine alionekana, Kaba akiwa anazipiga hatua akando kando ya barabara,, hajui ni wapi anaelekea,, akaanza kuhisi njaa! akajaribu kuvumilia lakini akashindwa,, akazipiga hatua huku akiangaza angaza macho yake huku na kule,, kwa mbali akaona jalala akaamua kulifuata jalala hilo,, akakuta ukoko wa wali... , akauzoa kwa mikono yake na kuanza kula,  alipohisi kashiba akazipiga hatua kuifuata nyumba iliyokuwa kado yake, akaketi na kuegemea ukuta wa nyumba hiyo.. kumbe nyumba hiyo ndio ile nyumba ya Timo,, ambayo wanaishi wadogo zake!!!  Kabi aliendelea kuketi hapo akapitiwa na usingizi akasinzia kabisa!



    baada ya dakika kadhaa,,,wakaonekana wadogo zake Pamera wakiwa wameongozana na Timo, wakatoka nje ya nyumba na kuingia ndani ya gari,,

    wakati huo Kabi alikuwa kando ya nyumba hiyo, akiwa kasinzia usingizi mzito! wadogo zake hawakuweza kumuona kaka yao kwa sababu walikuwa upande wa mbele ya nyumba,, Timo akawasha gari na safari ikaanza..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                      ************************************



    Upande mwingine, walionekana yule mwanamke aliyesimamishwa kazi,  akiwa nyumbani kwake yeye na Subira,, akamuandalia Subira maji ya kuoga, kisha akaanza kuandaa chakula.. Subira akai gia bafuni,, akaoga, alipomaliza akarudi ndani,, mwanamke huyo aitwae Neema, akamwambia subira nikimaliza kupika tutakwenda sehemu,, nikatazame bihashara yangu,, kunamtu anauza bidhaa ndogo ndogo kwenye kibanda changu,, Subira akasema,," sawa dada hakuna tatizo.. Neema akamtazama Subira kisha akatabasamu,, na kuendelea na mapishi..



                        ********************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog