Search This Blog

KOTI JEUSI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************





    Simulizi : Koti Jeusi

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alionekana mwanaume mmoja,, akiwa kwenye kambi ya Jeshi,akitazama picha ya mkewe pamoja na picha za watoto wake watatu,, akatabasamu huku machozi yakimtoka!  akazirudisha picha hizo kwenye mfuko wa suruali ya kombati.

    akanyanyuka na kuzipiga hatu kutoka nje ya hema dogo kiasi.

    mwanajeshi huyo anaitwa BAKARI,,, pumde si punde akaitwa kwenye ofisi ya mkuu wa jeshi.. Bakari akazipiga hatua kwenda kuitikia wito wa mkuu wake wa kazi... lakini alipofika kwenye ofisi ya mkuu huyo,, akastaajabu kusikia maneno anayoongwa mkuu wake wa kazi,, akisema,,"kunakazi ambayo umatakiwa uifanye pwke yako.. kisha akatoa picha 3 akasema,,nataka uwaangamize watu hawa,, hakikisha unachinja vichwa vyao na kuniletea,, hili sio ombi ni amri,, na usipofanikisha ndani ya siku tatu utajisababishia matatizo makubwa,,

    Bakari akazichukua picha hizo kwa shingo upande,huku akimtazama mkuu wake wa kazi kwa macho ya msisitizo.. kisha akapiga saluti na kuondoka na hizo picha...



    Baada ya siku tatu kupita,, Bakari alikuwa bado hajaikamilisha kazi hiyo ya mauwaji ya watu watatu(3) mkuu wa jeshi akaamuru Bakari akamatwe na kuwekwa gerezani kwa tuhuma za kuuza siraha za kivita,, kwa watu wasiojulikana.. ni baada ya kugundulika kuwa baadhi ya siraha hizo za kivifa hazipo ndani ya kambi hiyo... kumbe ni mbinu ya mkuu wa jeshi alifanya hivyo ili kutengeneza kesi na ionekane kuwa muhusika ni Bakari..

    Bakari akawekwa gerezani na kuhukumiwa kifungo cha miaka ishirini,, pamoja na adhabu kali ndani ya miaka hiyo ishirini!

    mkuu wa jeshi hakuishia hapo,, akaamua kuiangamiza familia ya Bakari kwa kuuwa mke na watoto wote wa Bakari!!

    Bakari akapewa taarifa juu ya mauwaji ya kikatiri yaliyoikumba familia yake,,mke na watoto... Bakari akajisemea moyoni,, "bila shaka huyu ni Mkuu wa jeshi, ( NDOLI )

    Bakari akasikitika sana,, kilicho muumiza zaidi hata hakushuhudia msiba pamoja na mazishi ya familia yake... akaandaa mpango wa kutoroka gerezani.



    Baada ya miaka kumi kupita,,, Bakari akafanikiwa kutoroka gerezani,,, na haikufahamika ni wapi alipo!

    siku zilizidi kusonga,,ikasadikika kunamuuwaji anauwa maafisa wa jeshi pamoja na viongozi mbali mbali wa ngazi za juu... muuwaji huyo hakufahamika kwa sura na kila anapofanya tukio la mauwaji,, anafunika maiti hiyo kwa koti jeusi....

    hali hiyo ilizidi kuwa gumzo,,

    Mkuu wa jshi akaanza kuingiwa na wasi wasi,, baada ya kuona maafisa wa jeshi wanauwawa! tena ni wale anaoshirikiana nao kwenye mipango haramu,, ya kuuza siraha za jeshi,, kwa majasusi mbalimbali kwa ajili ya kwenda kufanya uharifu!

    mbaya zaidi vifo vya maafisa hao wa jeshi,, vilifanana,,kila anapouwawa  miongoni mwa maafisa wa jeshi,, basi maiti yake hufunikwa kwa koti JEUSI..

    akajisemea moyoni,, bila shaka muuwaji agakuwa ni mtu mmoja kwa sababu matukio ya vifo yanafanana!!! je ni nani huyu?



                            ************************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine alionekana Bakari,, akiwa ndani ya chumba chake,, Baraka aliamua kwenda kuishi uswahilini huko Manzese... ili asifahamike kwa urahisi.. nia na lengo lake ni kulipiza kisasi kwa kuwapa adhabu ya kifo wale wote waliokuwa wanashirikiana na mkuu wa jeshi!

    Siku zilizidi kusonga,, Vyombo vya dora viliendelea kumtafuta mtu anayefanya mauwaji hayo ya viongozi wa ngazi za juu! bila mafanikio yoyote...



    Siku moja Bakari akandaa mpango wa kwenda kumuuwa,, mmoja kati ya maafsi wa jeshi waliobaki hai,,, ilipofika majira ya saa mbili za usiku.. Bakari akachukua begi dogo la kubeba mgongoni,, ndani hake kulikuwa na koti jeusi.. akalitoa na kulivaa,,

    koti hilo lilikuwa na kofia pana kiasi ambayo haikuweza kuonyesha uso wa Bakari kwa urahisi...

    alipomaliza kulivaa koti hilo,, akatokq nje ya chumba chake na kutokomea kusiko julikana,,,

    Baada ya lisaa limoja kupita,, vikasikika vyombo vya habari vikitangaza habari iliyowafikia hivi punde(BREAKING NEW'S)  kuwa Afisa wa jeshi.. wa kambi ya kijeshi MGULANI kauwawa na mtu asiyejulikana,, na maiti yake ikafunikwa na koti jeusi!



    Taarifa hiyo pia aliipata mkuubwa jeshi,, akashtushwa sana na kifo hicho... akajisemea moyoni,, "mbona kila kukicha watu ninaoshirikiana nao kwenye bihashara zetu haramu, wanauwawa tena kifo cha kufanana..

    wakati anatafakari nini Cha kufanya,, ghafla simu yake ikaita,,, akaipokea simu hiyo,, akashtuka kusikia sauti ya mkewe na watoto wake wakilia huku watoto wakisema,, "baba njoo nyumbani ni tunaangamia! kabla mkuubwa jeshi hajaongea chochote,simu hiyo ikakatwa,,, alipojaribu kuipiga haikupatikana kabisa!!!!

    punde si punde akaja mmoja kati ya wanajeshi wa kambi hiyo,, akatoa taarifa kuwa afisa anayehusika na utunzaji wa siraha za kivita amekutwa kauwawa,, nje ya uzio wa kambi!

    Mkuu wa jeshi akazidi kuchanganyikiwa,, kwa sababu ni muda mfupi katoka kusikia taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa afisa mmoja wa kambi ya Jeshi mgulani ameuwawa..,, pia nu dakika chache zimepita amepigiwa simu na famililia yake kuwa wapo hatarini kuuwawa..... kabla hajakaa sawa,, hapohapo kaletewa taarifa kuwa afisa mwingine kakutwa kauwawa tena nje ya uzio wa kambi ya kijeshi!







    Kule nyumbani kwa mkuu wa jeshi alionekana mtu akavalia Koti jeusi huku kafunika uso wake kwa kitambaa cheusi,, kaacha sehemu ndogo ya macho kuweza kuona....

    mke wa mkuu wajeshi pamoja na watoto wake wanne hawakuweza kuitambua sura ya mtu huyo....

    kumbe ni Bakari mdiye amevamia nyumbani mkuu wa jeshi... akaonekana akitoa gundi ya nailoni akawaziba midomo mke na watoto wa mkuu wa jeshi.... kisha akawafu kwa kitambaa cheusi kwenye nyuso zao..

    akawafunga mikono alipoangaza angaza macho yake,,akaona ufunguo wa gari.. akauchukua ufunguo huo... kisha akawachuku mke pamoja na watoto wa mkuu wa jeshi akatoka nao nje akaangaza angaza macho yake akaliona gari limeegeshwa ndani ya uzio wa nyumba hiyo...akajisemea moyoni,, "bila shaka huu ni ufunguo wa gari hili.. hakuna gari lingine hapa.. akafungua mlango na kuwaingiza ndani ya buti ya gari... kisha akaliwasha...... akashuka kutoka ndani ya gari hilo..akazipiga hatua akafungua geti... kisha akavua begi lake... akalishikilia mkononi na kuingia ndani ya nyumba ya mkuu wa jeshi... akatoa kemikali iliyokuwa ndani ya chupa,,akaimwaga chini kwa kuisambaza.. kisha akaingia jikoni akafungua koki za mitungi ya gesi,,gesi ikaanza kuvuja taratibu.

    kumbe ile kemikali ikichanganyikana na ile hewa ya gesi ni zaidi ya bomu.... utatokea mlipuko mkwa na hakitabaki kitu kikiwa salama ndani ya nyumba hiyo......kisha akatoa koti jeusi akalitupa chini kwenye sakafu.... akatoka na kuingia ndani ya gari akaliwasha na kuondoka zake... akaliendesha gari hilo mpaka bagamoyo... akaliingiza gari ndani ya jengo moja kubwa la kale. kisha akashuka kutoka ndani ya gari.. akafungua buti ya gari na kuwatoa mke na watoto wa mkuu wa jeshi.. kutokana na mbanano wa hewa walikuwa wamepoteza fahamu kwa kukosa mzunguko wa hewa safi kwa masaa mengi mfululizo....akawabeba mmoja mmoja na kuwaingiza ndani ya jumba hilo la kale... akawafunga kamba kewemye moja ya nguzo zilizokuwemo ndani ya jengo hilo...kisha akaketi kando yao.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                            **************************************



    Upande mwingine kule kwenye kambi ya jeshi,,alionekana mkuu wa jeshi,, akiamuru wanajeshi kumi wenye siraha aongozane nao mpaka nyumbani kwake...

    walipofika kabla hawajaingia ndani ya uzio.. ukasikika mlipuko mkubwa nyumba yote ikasambalatika!

    mkuu wa jeshi akahisi kuchanganyikiwa.. akashuka kutoka ndani ya gari akatimua mbio kuingia ndani ya uzio wa nyumba yake..macho yakamtoka akashika kichwa!!

    akazipiga hata za taratibu huku akizipiga hatua zataratibu machozi yakimtoka akiamini kuwa familia yake imeangamia na kuteketea mdani ya nyumba!  alipoangaza angaza macho yake... akaona koti jeusi.. likiwa sakafuni huku linawaka moto... akashtuka!  akajisemea moyoni,, "bila shaka ni yule muuwaji ambaye anafanya mauwaji kila kukicha!!  hivi ni nani huyu? 

    Mkuu wa jeshi akaamuru Jeshi la nchi nzima liingie mitaani na kukusanya makoti yote meusi yanayouzwa na wafanyabihashara wanaouza nguo..kisha wayachome moto.... pia akaitisha mkutano na waandishi wa habari pamoja na vyombo vyote vya habari....akatoa tamko rasmi kuwa makoti meusi hayaruhusiwi kuingizwa nchi.. kwa yeyote atakayepatikana akiuza au kuvalia koti jeusi,,  auwawe....kwa sababu huenda akawa anashirikiana na muuwaji anayeuwa na kuacha koti Jeusi kwenye eneo la tukio......wakati mwingine huacha amefunika maiti kwa koti jeusi baada ya kufanya tukio la mauwaji!

    Tamko hilo lilishtua taifa na kuzua gumzo mitaani...



    baada ya mkutano huo... akaamuru jeshi la nchi nzima liingie kila kaya na kukagua...kutafuta makoti meusi!

    wanajeshi wakatekeleza amri ya mkuu wa jeshi,, na kazi hiyo ikaanza maramoja!

    watu waliopatikana na makoti meusi walikamatwa na kuhojiwa na wapelelezi maalumu wana-saikolojia... lakini ikabainika kuwa si wahusika! na upelelezi ukaendelea,, kila mkoa wilaya na mitaa...yote Tanzania.



    Pia Bakari ali.zipata taarifa hizo,, akatoa vitu vyake vya muhimu akaviweka ndani ya begi lake dogo la mgongoni.....

    kwenye nyumba aliyokuwa amepanga Bakari hakuwa na vitu vingi zaidi ya kitanda godoro na meza iliyokuwa na Runinga juu yake.... kabla hajatoka ndani ya chumba hicho akavaa grovs,, akaacha katundika koti jeusi kwenye msumari uliokuwa kuwa ukutani.. pia akaacha kaandika ujumbe kwenye karatasi,,,akatoka nje na kufunga mlango wake akamuaga mmiliki wa nyumba hiyo kuwa anasafiri kuelekea Arusha.  na baada ya mwezi mmoja Atareje.



                           *******************************************



    Upande mwingine kule bagamoyo,,mafichoni, alionekana mke wa mkuu wa jeshi akizinduka na kupata fahamu,, alipoangaza macho yake akashtuka kujikuta ndani ya jumba hilo.. linaloonekana sio makazi ya mtu yeyote!!  pia alijikuta amefungwa kama miguunu huku mikono yake ikiwa imefungwa vyema kwa kama gumu iliyozungushwa kwenye moja ya nguzo zilizomo ndani ya jengo hilo!

    alipojaribu kuita alishindwa kwa sababu alikuwa kazibwa mdomo kwa gundi ya nailoni!

    pia hakuwaona watoto wake!  akahisi kuchanganyikiwa! akaanza kufurukuta ajinasue kwenye kama hizo lakini akashindwa!



                                *******************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huohuo walionekana wanajeshi wapo mitaani wakiendelea kukagua kila kaya,, wakaifikia ile nyumba aliyokuwa anaishi Bakari.. wakaanza kukagua nyumba nzima kila chumba hadi chumba..... walipokifikia chumba cha Bakari,,mlango ulikuwa umefungwa kwa ufunguo... wakaamua kuvunja mlango na kuingia ndani ya chumba hicho.

    wakashtuka kukuta koti jeusi likiwa limening'inizwa ukutani... koti hilo lilifanana na yale makoti yanayo onekana kwenye matukio ya mauwaji!  pia wakaona karatasi nyeupe inamaandishi yaliyoandikwa kwa kalamu!

    waliposoma aandishi hayo,,yalisomeka hivi;

                                                            "Msijisumbue kunitafuta kwa sababu hamna uwezo wa kunipata.. na sijaishia hapo nitaendelea kufanya kile nilichokusudia bado wanaharamu kumi(10) kisha kifo chako kitafuata wewe mkuu wa jeshi".



    Wanajeshi hao wakachukua karatasi hiyo na kuipeleka kwa mkuu wajeshi! wakamkabidhi,, akasoma ujumbe huo. macho yakamtoka akahisi kuchanganyikiwa.

    wakati anatafakari kitu cha kufanya,, ukasikika mlio wa simu yake ikiita,,alipoitazama akashtuka kuona ni namba ngeni! akaipokea huku akisita,,,akaiweka sikioni.....







    Akashtuka kuisikia sauti ya mtu anayehisi kumfahamu!  ikisema,, "hawezi kunipata kamwe,, mimi ndiye nitakulata wewe.. kisha simu ikakatwa! mkuu wa jeshi akaingiwa na hofu akajaribu kipiga simu hiyo,, lakininkwa sasa haikupatikana! mkuu wa jeshi akaamuru itumike mitambo maaulumu ya kutafuta mawasiliano ya namba iliyompigia,,mawasiliano hayo yanatokea sehemu gani(call tracker)  lakini walipojaribu kudadisi mawasiliano ya namba hiyo haikuonyesha eneo sahihi (unknown Location)

    kumbe Bakari aliweka mtambo maalumu kwenye simu yake... ili isioneshe ni wapi alipo..

    mkuu wa jeshi akazidi kuchanganyikiwa,,, akatafakari nini cha kufanya.



                               ***********************************



    upande mwingine alionekana Bakari akiwa anazipiga hatua kuelekea kwenye lile jengo la kale!  alipofika akafunika sura yake kwa kitambaa cheusi huku akiacha sehemu ndogo kwenye macho kwa ajili ya kuona vyema.

    akamfuata mke wa mkuu wa jeshi,, pale alipokuwa kamfunga kwa kamba.... alipomkaribia akamfunika uso kwa kitambaa kisha akamchoma sindano....

    sindano hiyo ni maalumu kwa kupoteza kumbukumbu na kufuta kila kitu kilichohifadhiwa ndani ya ubongo.....kutokana na nguvu ya sindano hiyo mke wa mkuu wa jeshi akapoteza fahamu.... Bakari akazipiga hatua akaelekea kwenye chumba kingine kilichomo ndani ya jumba hilo la kale,, chumba hicho kilikuwa na giza kiasi.. akawasha tochi alipomulika... wakaonekana wale watoto wanne wakiwa wamefungwa miguu na mikoni wamekalishwa chini,,,akafungua begi lake la mgongoni akatoa kichupa kidogo,, kilichokuwa na dawa maalumu ya kufuta kumbukumbu ndani ya ubongo wa binadamu,, akawafunika watoto hao nyuso zao kwa kitambaa kisha akawachoma sindano hiyo.. ndani ya sekunde watoto hao wakasinzia usingizi mzito wa nusu kifo!  akawabeba na kuwaingiza ndani ya gari,, kisha akarudi kule kwenye chumba alichokuwepo mke wa mkuu wa jeshi,,.. akiwa bado katika hali ya kutokuwa na ufahamu.

    akambeba na kumuingiza ndani ya buti ya lile gari alilolichukua kule nyumbani kwa mkuu wa jeshi...kisha akaliwasha na kuondoka zake akaliendesha mpaka mje kabisa ya mji,, kisha akaliegesha porini,,akashuka kutoka ndani ya gari... akafungua buti na kuwatoa watoto hao... akawaingiza kwenye gari upande wa nyuma akawafungua kamba pamoja na kuwaomdolea vitambaa kwenye nyuso zao...kisha akamchukua mke wa kuu wa jeshi.. akamkalisha kwenye kiti cha upande wa dereva.. akamfungua kamba pia akakiondoa kitambaa cheusi kilichokuwa kimefungwa kwenye uso wa mke wa mkuu wa jeshi.... CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bakari akaitazama saa yake ya mkononi ,kisha akajisemea moyoni,, "baada ya lisaa limoja watazinduka..... hawatafahamu chochote kilichotendeka,,,

    mimi siwezi kumuuwa mtu asiye na hatia,, najua kuwa watoto hawa pamoja na mama yao hawahusiki wala hawajui kinachotendwa na mkuu wa jeshi!  lakini hii ni adhabu tosha kwa mkuu wa jeshi kukaa mbali ja familia yake.. na hata kama akiwapata basi hawataweza kumkumbuka hivyo itakuwa ni kazi bure kwake... bila shaka anaamininkuwa familia yake imeteketea ndani ya nyumba yake..

    Bakari akatabasamu.. na kuwatelekeza huko porini wakiwa ndani ya gari.....yeye akaindoka zake na kutokomea kusikojulikana!



                         ******************************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog