Search This Blog

TOZANI ( PETE YA AJABU) - 3

 







    Simulizi : Tozani (Pete Ya Ajabu)

    Sehemu Ya Tatu (3)





    KUZIMU:



    MUNGU baada ya kuiumba dunia na kumuumba nabii Adamu akamwambia ibilisi ( LUSIFAR ) Amsujudie Adamu

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ibilisi yule akakataa na kumwambia MUNGU "Mimi umeniumba kwa moto siwezi kumsujudia huyu uliyemuumba kwa udongo,huyu ambaye ataenda katika dunia kuleta maafa,kumwaga damu....



    Kwa kuwa ibilisi alienda kinyume na matakwa ya MUNGU MUUMBA,MUNGU alimfukuza na kumweka mbali na Rehema zake



    Akamwahidi moto wa milele ( moto wa jehannam)



    Naye sheitwan akiwa ameghafilika akamwomba MUNGU



    " kwa kuwa umenitoa katika rehma zako kwa sababu ya binadamu kiumbe dhaifu na kunihaidi moto basi naomba nafasi nimuadae binadamu ili nipate wa kuingia naye huko motoni....



    MUNGU AKAMKUBALIA!



    ila kwa kutupenda zaidi akatuletea manabii na mitume ambao walituongoza katika njia ilonyooka



    Nako ibilisi akaanza kazi ya kutuhadaa,na kujiita MUNGU japo aliishi duniani pia alianzisha na ulimwengu wake KUZIMU ambapo uko pia alieka moto wake,kuunguza viumbe wanaoenda kinyume na maagizo yake



    Akaanzisha dini yake ( free mason) na kuapa siku moja kuitawala dunia



    Lengo aende na viumbe wengi katika moto wa jehannam



    ******



    Baada ya jini Zena kugundua nguvu zake ni ndogo na hana uwezo wa kuichukua tozani



    Akapiga magoti na kuanza kumuomba MUNGU wake katika ulimwengu ule ( LUSIFAR) amwongezee nguvu



    Ghafla nguvu zikamjia!



    Akajiona ana uwezo zaidi....



    Akanyanyuka na kuisogelea tozani akainama na kuiokota ile anainuka akakumbana na ngumi ilomfanya akapepesuka



    Akakaa sawa na kumtazama alompiga....



    Alikuwa ni Muzidu!



    "Naitaji TOZANI...."



    MUZIDU akatamka ghafla upanga ukatua katika mkono wake



    ZENA Kureysh akaachia cheko,cheko la kiburi



    "Siwezi kukupatia tozani,kwa kuwa hii ni Mali yangu na ipo katika mkono wangu"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla Muzidu akaunyanyua upanga wake ulowakawaka kwa ukali na kumwendea ZENA kwa spidi



    Zena akamsubiria kwa hamu

    Ile MUZIDU kamfikia akaunyanyua upanga na kuuachia akikilenga kichwa cha Zena



    Akakumbana na hewa!



    Zena alitoweka na kutokea nyuma yake,ambapo alimrukia teke



    Muzidu akaserereka



    Ila aliwahi kuamka,na kumwangalia binti yule kwa chuki



    Akaachia shoti katika macho yake,ambapo binti yule alifumbua mdomo na kuzimeza ghafla akazitema na kuachia kombora



    Muzidu akapepesuka



    Zena akaachia cheko



    Nguvu alizoongezwa na Lusifa,pamoja na Pete aloishika zilikuwa ni hatari kwa Muzidu



    Zena akanyoosha mkono wake,shoti zikatoka na kumwendea jini yule mchawi



    Muzidu akapepesuka na kunyoosha mkono kuzuia



    Zena akamnyooshea mkono ishara ya kibao,Muzidu akakunja kichwa akampiga upande wa pili ,na kumrukia teke kwa ishara



    Muzidu akaenda chini



    Kwa ishara ile ile akamuoneshea kama kumuinua,kabla ajainuka akampiga chini



    Bado Zena aliachia kicheko!



    Muzidu akaanza kuomba,kimyakimya akimuomba mungu wake ambaye ni mmiliki wa himaya ile



    "Lusifa"



    Katu Hakuna aliyejua kuwa wote walimuomba mungu mmoja na wale wachawi walokuwa chini ya bahari katika himaya ya Bisau walizidi kuomba mpaka kushikana mikono kumuongezea nguvu mkubwa wao ila ilo alikusaidia....



    Bado Muzidu alipigwa na binti yule



    Wanakoo ya Muzidu wakatoweka waliamua kwenda kumsaidia kwa ukaribu kiongozi wao yule....



    Zena baada ya kuakikisha amemtesa vya kutosha , kiumbe kile akanyoosha mkono ishara ya kumnyonga



    Lakini ghafla akajikuta ameshikwa



    Yani ilikuwa kama kafungwa,...



    Ni wana wachawi wale walitokea na kumzunguka,baada ya Zena kugundua lile kuwa sasa anapambana zaidi ya nafsi moja akajikunja kukusanya nguvu yani akawa kama kasinyaa na alipotanuka



    Viumbe vyote vilivyomzunguka vikarushwa na kutupwa pembeni , ila avikukaa vikasimama vyote na kukunja duara ila kabla awajafanya chochote zena aliwarukia na kuwaachia mateke mfululizo....



    Ghafla Zena akaachia kombora lililo wakusanya pamoja na kuwa funga tena bila kamba wakawa wamenatiana



    Lakini ghafla Giza likatanda eneo lile , na mwanga uliporudi viumbe wote waliokuwepo pale wakasujudu....



    Kumuabudu asiye MUNGU wakasahau kauli takatifu



    SIKUWAUMBA BINADAMU NA MAJINI ILA WANIABUDU



    NI haki pia kwa majini kumuabudu ALLAH pekee,ila viumbe wale walienda tofauti na maagizo ya MUNGU



    Mkumbuke kuna majini Wema na waovu , kuna watakao enda peponi wale Wema na motoni wale waovu.....



    Viumbe wale wote walimsujudia "LUSIFAR" kama mungu wao mkuu wa kuzimu



    "Zena Kureysh achaaaaaaa!, Pete ni ya kwako lakini tambua hata Hawa ni wafuasi wangu Pete imetoka katika HIMAYA yao bila hiyo Pete himaya yao itakaa bila uongozi wapeee hiyo Pete wakaioneshe na akishapata ufalme akurudishie



    Zennnaaaaa wape peteeee watakurudishiaaaaa"



    Zena akamwangalia MUZIDU,aliyetingisha kichwa kuafiki jambo lile Zena akauliza kwa sauti......



    "Muzidu ukishavikwa ufalme utanrudishia hiyo Pete"



    "Ndiyo jemedari wa kuzimu na kuhaidi nikishaa apishwa kuwa mfalme ntakurudishia Pete yako...."



    Muzidu na wenzake wakaweka kiapo Mbele ya Lusifar shetani aliyelaaniwa kuirudisha TOZANI baada ya kumuonesha mfalme Bisau Pete ile ya maajabu!,kama ufunguo wa kuwa mfalme wa HIMAYA ile.....



    *******



    SURA YA TATU



    DUNIANI



    Inspekta wa jeshi la polisi Nurdin aliyatoa macho pima,akutaka kuamini kile akionacho,au kile akisomacho katika file lile alilopewa dakika kadhaa zilizipita



    Akainua kichwa chake na kumwangalia yule aliyempa faili lile



    Ambaye naye alikuwa kapigwa na butwaa , akarudisha macho yake tena katika faili lake lile na kulisoma tena pengine angekuta kilichoandikwa kimebadilika



    Hapana! Maneno yalikuwa Yale Yale....



    "Ili linawezekana kweli dokta" akauliza kwa sauti ya wasiwasi



    "Kisayansi aliwezekani na sijawahi kukutana na jambo kama hili hii ndo Mara ya kwanza katika miaka yangu 25 kazini!"



    Nurdin akashusha pumzi kwa nguvu kama vile katua mzigo mzito....



    Ni wazi alikuwa kuchanganyikiwa.......





    Akamwangalia daktari yule kwa sekunde kadhaa kama vile alijiandaa kumwambia kitu, na taratibu akakohoa kidogo kusafisha koo lake na kufumbua mdomo wake kusema kile alichoitaji kukisema....



    "matukio kama haya niliwahi kuyasoma katika vitabu vya riwaya,ila nilijua nihadithi tu ila kumbe yanatokeaga!?"



    Aliongea Nurdin akikumbuka kisa kama kile alishawah kukisoma kwenye kitabu cha riwaya ya gwiji HUSSEN TUWA kilichoitwa utata wa 9/12,



    kuna watu walokufa katika kisa kile wakaonekana walikufa kabla ya huo muda wao walokufa.



    ndo kilicho mtokea pale, ripoti ya uchunguzi wa miili ile ya walinzi wa kasino pamoja na miili ya vijana wale walopata ajali MUZIDU na mwenzake zidau,



    MUZIDU NA ZIDAU miili yao ilionekana ilikufa siku nyingi,na si siku hiyo ya ajali na hata wale walinzi walionekana wamekufa toka asbuh na si mchana ajali ilipotokea.



    Kwanin?!



    Bado hakuwa na jibu la moja kwa moja!



    Alijua kuna mambo ya ushirikina ndani ya matukio yale!,je angefanyaje!



    Alihitaji mapumziko,kichwa kitulie,



    Ni kwamba roho zile zilizotumwa na mfalme Bisau duniani kwenda kumlinda Zidau zilipofika pale katika kasino zikaingia katika miili ya walinzi wale!,



    Kitendo cha kuingia tu , kikawa kimeshaondoka na uhai wao miili ile ikawa ikitumiwa na roho zile mpaka katika ajali ile roho ziliiacha miili na wenyewe kwenda kupambana porini kabla Muzidu ajashinda...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa akili ya kawaida ilikuwa ni vigumu kwa insp yule wa jeshi la polisi kugundua vitu kama ivyo.



    Tayari alisha uruhusu mwili wa Merry kwenda kuzikwa baada ya uchunguzi kukamilika



    Uchunguzi ambao ulimdhihirishia wazi kuwa Merry kauwawa,akujua ni kwa nini yeye ndo alokumbana na kesi za maajabu ajabu namna ile



    *******



    Moyo wake ulimwenda mbio,amani ilitoweka,raha, furaha ilikaa mbali na yeye,...



    Aliwaza,na kuwazua pekee



    Silva hakuwa na rafiki aliyemwamini na kumpa siri zake,kwa kuwa naye alikuwa ni mmoja wa familia,mtu wa karibu wa ile familia aliudhuria katika vikao vyote vya mipango ya mazishi katika familia ile!



    Katika michango naye alitoa alichobarikiwa,



    Alisubiriwa Dada yake mkubwa na Merry aliyeishi n chini Marekani aje ndo Merry akazikwe



    Dada yake huyo alite tambulika kwa jina la NEEMA akiwa ndani ya ndege akuwa na furaha kabisa,alimpenda mdogo wake MERRY na alikuwa ana malengo siku moja amchukue na kuishi naye Marekani



    Kabla malengo ayajatimia ndipo alipopata habari ile ya kifo cha mdogo wake



    Kwamba Merry kauwawa?!



    Akaapa kutumia gharama zake zote mpaka ampate muuaji, iwe kiserikali au katika nguvu za Giza



    "Habari Dada?!"



    Akiwa ndani ya ndege akashtushwa na sauti nyororo, Neema akamwangalia Dada yule pasina kuamini kama yeye ndo kamsalimia.



    Alikuwa kaka kiti cha pembeni ya alichokaa yeye



    Akapokewa na tabasamu jembamba lililo ongeza urembo wa binti huyo!...



    "Mmh salama mdogo wangu kumbe unajua kiswahili?!"



    Neema akamjibu Dada yule huku akimzawadia tabasamu, katu akujua kama dada huyo angejua kuongea kiswahili kilichonyooka namna ile....



    Binti yule mwenye asili ya kiarabu akafumbua mdomo wake kumjibu Merry



    "Yah Dada kwani Mimi ni mtanzania baba yangu ni mwarabu na mama yangu ni mtanzania piwa"



    "Alaaa! Kwa hiyo saivi unaenda kwa mama?!"



    "Hapana wazazi wangu wote wapo Tanzania ila Mimi nipo Marekani kimasomo likizo hii ndo narudi kuwa salimia"



    "Mh vizuri na jina unaitwa nani?!"



    Binti yule kabla ajajibu akaachia kicheko hafifu!



    "Naitwa Zena!,"



    "Mmh jina zuri na pia nimependa ucheshi wako Zena!, Zena nani vile?!"



    Neema akauliza kama vile alikuwa anamjua ila amemsahau ndo anataka akumbushwe



    Wote wakaachia kicheko



    "Zena Kureysh"



    Binti yule akajibu,hakika tangu waanze kuongea uzuni yote alokuwa nayo dada yule ilitoweka



    "Pole sana Dada kwa msiba wa mdogo wako"



    Neema akashtuka!,



    Kajuaje nimefiwa?!, akajiuliza pasina kupata jibu kwa kuwa alikuwa kashamzoea akaona bora amuulize....



    "Umejuaje nimefiwa na mdogo wangu?!"



    Zena akaachia kicheko tena



    "Unaonekana una mpenda sana mdogo wako kwa sababu wakati ulipokuwa umejiinamia ukilia niliskia ukimtaja mdogo wako ukisema nenda salama mdogo wangu Merry"



    Neema akashtuka tena,hakukumbuka kama alisema maneno Yale japo ni kweli mwanzo wa safari alijiinamia akilia kisiri siri



    Ila alijua mawazo uondoka na ufahamu,akuona haja ya kum'bishia Dada yule



    "Nikweli Zena, nilimpenda sana mdogo wangu...



    " ila Mungu kampenda zaidi"



    "Hapana si Mungu! mdogo wangu amekutwa amekufa chumbani kwake kwa kunyongwa



    Ila cha ajabu mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani kuna kitu lazima nitajua!"



    Akazidi kuongea Neema kwa uchungu



    Moyo wa Zena ukampasuka paaaaaa



    Kengele ya hatari ikagonga katika kichwa chake



    "Mdogo wangu, Mimi nimeishi Marekani kwa muda mrefu nimesoma huko,sikuamini mambo haya ya ushirikina lakini kwa hili hata kwa waganga nitaenda ili nijue mwafaka wa mdogo wangu pengine ajafa!"



    Zena akamwangalia kwa macho makali!,ghafla shoti zikatoka katika macho yake na kumwendea dada yule



    Ghafla usingizi mzito ukamvaa,kichwa akakiegemeza katika kiti....



    Alikuwa ni hatari kwa maisha ya Zena,ghafla kivuli cha Zena kikatoka katika mwili wa Zena na kwenda kuingia katika mwili wa binti yule



    Mwili wa Zena ulobaki bila nafsi nao ukawa umelala



    Kwa macho ya binadamu wa kawaida yaliwaona Neema na Zena wakiwa wame lala!



    Ghafla Neema ( ambaye sasa aliingiliwa na roho au nafsi ya Zena akafumbua macho yake)



    Yani akaamka , ndege ndo ilikuwa ikitua uwanja wa KIA



    Akauangalia mwili wake ulokuwa bado umelala akatabasamu na kuupiga shoti



    Ghafla ukafumbua macho



    Ndege ilitua na baada ya kusimama abiria wakaanza kushuka



    Wakashuka abiria wote ndani ukabaki mwili wa Zena na mwili wa Neema uloingiliwa na nafsi ya Zena



    Nafsi ya Zena ilokuwepo katika mwili wa Neema baada ya kuona amna mtu anayemwona akaupiga shoti kwa kutumia macho yake mwili wake



    Na ghafla akatoweka!



    Ndani akabakia yeye pekee



    Akachukua mabegi yake na kuanza kutoka taratibu



    Mpaka nje ya uwanja,alipokodisha tax mpaka nyumbani kwao....



    Wengi walifurah baada ya kuwasili kwa binti yule ila wakati anashuka Silva alipomuona bado kidogo angedondoka

    Kwa mshtuko



    Silva alimuona ni Zena Kureysh japo watu wote walimuona ni Neema...



    Silva alianza kutetemeka akabaki ameganda kama sanamu........



    Mapigo ya moyo yalianza kumwenda mbio japo alijitahidi kuyazuia...

    Kijasho chembamba kilimtoka,kijasho cha uwoga,

    Alimwogopa Zena,akaruhusu mtiririko wa maswali kutiririka ndani ya ubongo wake,maswali ambayo katu hakuyajua majibu yake!

    "Ina maana Zena na Merry ni ndugu na Hawa ndugu zake wanajua Zena ni jini!,mbona wanameita Neema hapana kuna kitu au ni wenge langu pengine sura ya yule Dada imenasa kichwani kwangu,hapana!....

    Akapingana na mawazo yake baada ya kukumbuka tabasamu la Zena wakati akiingia chumbani,

    Tabasamu ambalo mtu ulitoa kwa yule mtu umpendaye...

    Baada ya Neema kuoga na kupumzika kidogo ndugu na majirani,marafiki wa karibu wakaelekea katika ukumbi mdogo kwa mkutano na mipango ya mazishi

    Baada ya kikao kufunguliwa....

    Na Neema akapewa nafasi ya kuongea

    " mwili wa marehemu mdogo wangu Merry tangu amekufa Leo ni siku ya tano kwa maoni yangu kesho tuuzike tu kusudi tukizidi kuuweka unaaribika"

    Watu wote wakapigwa na butwaaa

    Wakatazamana,Silvar akamwangalia Zena kwa wasiwasi mawazo yake ayakuwa pale alikuwa akikumbuka kikao kilichopita cha Jana yake kabla huyo Neema ajaja

    "Sikubali mwanangu azikwe bila ya Dada yake kuwepo apigiwe simu ajulishwe"

    Mama yake Merry aliongea kwa uchungu , ndugu wengine wakaridhia baba Merry akaenda kuchukua vocha na kujiiunga kifurushi cha kimataifa

    Akampigia dakika chache ikapokelewa.....

    Baada ya salamu Neema akamwomba baba yake akate ampigie yeye

    "Mwanangu Neema mdogo wako Merry atunae tena duniani!"

    "Unasemaje baba kafanyeje?!"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikabidi mzee yule aanze kumsimulia kuwa alikuwa chumbani kwake akiwa chini ya kitanda amekufa na ripoti za polis zinasema wazi ameuwaa na mlango ukuvunjwa wala amna mahali mtu alipopita....

    Kama ilivyokuwa kwa fikra za wazazi, ndugu na baadhi ya watu kuhusisha maswala hayo na ushirikina hata kwa Neema ilikuwa ivyo ivyo

    "Baba naomba mdogo wangu asizikwe mpaka mimi nije najua mdogo wangu ajafa ntakuja kupambana mpaka nijue mwisho wake kama ni mkono wa mtu nitajua baba.....

    Neema aliongea kwa uchungu,alimpenda sana mdogo wake iweje Leo aseme kirahisi rahisi kwamba Merry akazikwe wakati Jana aliapa kupambana?!

    Watu wote wakabaki wameduwaa

    'Kama ni uchawi walijua naye pia kasha ambukizwa'

    Hakukuwa na alijua kuwa yule si NEEMA halisi,...

    " ila mwanangu Jana ulisema kutokana na mazingira ya mdogo wako kabla atujauzika mwili lazima.....

    "Shhhhh! Mama ni kweli ile ilikuwa hasira na sikufikiria ndo maana nikaropoka maneno Yale , tukiingiza ushirikina tutapoteza ela , pia tutamkosea na MUNGU wetu

    Sisi tulimpenda ila MUNGU kampenda zaidi , kama ni mkono wa MUNGU tumuachie yeye na kama ni binadamu pia tumwachie yeye mweza wa yote"

    Baada ya maneno Yale Zena akageuza kichwa chake na katika macho yake shoti zikatoka na kuwaendea ndugu zake wale

    Akaziyeyusha nyoyo zao,wakakubali kuachana na jambo lile

    Siku ya mazishi ikapangwa!

    Akukuwa na mwenye mashaka tena, wote walisahau na kuchukulia ni kifo tu cha kawaida

    Kasoro watu wawili ambao walikuwa tofauti na mawazo Yale

    Insp Nurdin pamoja na kijana Silvar

    Kila mmoja alikuwa akifikiria kivyake,na insp Nurdin alijitahidi kuwa karibu na ndugu akitegemea kugundua chochote

    Lakini mpaka hapo a kugundua chochote, bado alikuwa ndani ya Giza akijiuliza u wapi mwanga bila mafanikio....

    Siku zikayoyoma hatimaye siku ya mazishi ikafika , naye insp yule akiwa ndani ya nguo za uraiani akawa pamoja na wafiwa akichunguza kila hatua na akimchunguza kila mtu aliyekuwepo maeneo Yale

    *******

    simanzi, majonzi na hali ya kuongea mwenyewe ilimtia shaka insp yule kwa Mara ya kwanza akatamani kuzichunguza nyendo zake

    'Jirani tu tena wa kiume aumie namna hii angekuwa wa kike pengine tungesema ni rafiki yake ila wa kiume mmmh au alikuwa mpz wake?!'

    Akawaza

    Alitaka kumfata moja kwa moja lakini moyo ukasita

    Akaapa kuanza kumchunguza kwa nje kwa kuwafata watu na kuwauliza juu ya jamaa huyo kama alikuwa na uhusiano wowote na marehemu!

    'Lakini nikimfata hata yeye ni kamuuliza mbona unaonekana aupo sawa na umeguswa zaid na huu msiba marehemu alikuwa nani yako?!,'

    'Hapana orterval anaweza akanambia alikuwa mpz wangu , so kipi kitafuata?!

    Yah sitoenda kwanza mpaka niwe na uhakika nje, kuna kitu kinanisukuma juu yake lazima atakuwa anajua kitu'

    Yalikuwa ni mawazo alowaza insp Nurdin macho yake akiwa ameyanatisha kwa Silvar alokuwa kakaa na wenzake maeneo ya makaburini pale ila kimawazo hakuwa na wenzake wale

    kuna kitu kilimsukuma Silvar amfate Zena na kumdadisi kitu

    Macho yake akayaangaza kama anatafuta kitu

    Na ghafla akamuona Zena kasimama katika gari yake pembeni kabisa ya makaburi Yale

    Akiwa mwingi wa mawazo

    ( kilikuwa ni kiini macho kwake kwani watu wengine awakumuona )

    Basi Silvar akajipa ujasiri na kumfata

    "Zena" akaita Zena akageuka na kumzawadia tabasamu

    "Silvar wangu" naye akaitika kwa kumwita jina

    " Mimi si wako Zena sahau juu ya ilo"

    Zena akujibu kitu akaishia Ku tabasamu na kifungua mlango wa gari Silvar bila kujibu kitu akapanda baada ya kukaa vizuri akaamua kutoa dukuduku lake

    "Zena we unausika na mauaji ya Mery"

    Zena akashtuka lakini ghafla wote wawili wakamwangalia yule mtu alokuwa akiwafata kwa spidi

    Alikuwa ni insp Nurdin.

    KIUALISIA (nje ya kiini macho)

    Ni kwamba SILVAR pale alipo Iona gari hapakuwa na gari zaidi ya mti mdogo tu ulokomaa na alipoanza kuufata na kuanza kupanda gari na kukaa kwenye kiti ni aliruka na kuukalia ule mti

    Insp Nurdin alipomuona kijana yule kajitenga na kwenda kukaa juu ya ule mti mdogo naye akaamua kupiga hatua na kumfata kabla ajamfikia akamsikia akisema mwenyewe...

    "Zena we unausika na mauaji ya Merry"

    Nurdin akashtuka.....



    Ni wazi alihisi maskio yake yanamdanganya,

    'Ina maana huyu kijana anamjua muuaji na mbona anaongea mwenyewe?!'

    Wazo lile likapita katika kichwa chake,akazidi kukaza mwendo akiwa na dhamira nyingine!

    Dhamira ya kuondoka naye akaisaidie polisi,kwa kumtumia yeye aliamini angeng'amua chochote.....

    Upande wa pili wa Zena na Silvar

    Waliuona mshtuko dhahiri ambao insp yule wa jeshi la polisi aliupata baada ya kusikia maneno ya kijana yule

    "Nadhani kuvunja kwako masharti ndo chanzo cha mauaji yake na huyo anayekuja ni insp kasikia kila kitu unacho ongea lazima ukajieleze na kuisaidia polisi kalale kidogo ndani upate adabu ndo utaujua umuhimu wangu kwako"

    Kauli ile ikamchoma Silvar yeye ndo alikuwa msaada mkubwa kwa wazazi wake kama angefungwa je wazazi wake wangesaidiwa na nani!

    Akamwangalia Zena kwa macho ya huruma yakidhihirisha kuitaji kitu

    Msaada!

    Yaliitaji msaada,na baada ya Zena kugundua lile akaachia kicheko hafifu

    Akamwangalia insp yule aliyekuwa hatua kadhaa kabla ajawafikia akampiga shoti

    Ghafla insp NURDIN akasahau kila kitu,pale pale akageuka na kurudi alipotoka

    Silvar na Zena Wakakumbatiana kwa furaha,na hapo penzi lake likachipua rasmi na kukua kwa kasi sana.

    MIEZI KADHAA MBELE

    Maisha ya Silvar yalibadilika sana,lile wenge alilokuwa nalo lilitoweka

    Alinenepa,akumuogopa tena Zena

    "Mpz kesho ndo naelekea Mandaka chuo cha ualimu ntakumiss sana mpz wangu"

    Silvar alimuaga mpz wake,kwa kuwa kilikuwa ni chuo cha "bording" Zena hakutaka kumchanganya mpz wake yule

    Miaka mitatu kwake ilikuwa kama siku moja ivyo alijua itaisha na watakuwa pamoja!



    ****

    Silva akaingia rasmi chuoni,miezi sita ya awali kimya kilitawala hakumwona Zena wala kusikia habari zake,likizo ilifika akaenda nyumbani akitegemea kumuona aikuwa hivyo

    Akaambiwa Neema alishaondoka na mbaya zaidi alipata ajali ya ndege wakati akirudi marekani.

    Ni wakati Zena alipo utelekeza rasmi mwili wa Neema alisababisha ajali hili ipatikane sababu!

    "Au atakuwa kafa katika ajali hiyo nini?!"

    Akawaza,akisahau kwamba alishawahi kumwambia angerejea pindi akimaliza masomo yake,binadamu ni mwingi wa kusahau....

    Hatimaye siku ya kurudi chuo ikafika Silva akaaga na kurudi zake chuoni....

    Sasa akamsahau kabisa Zena,na kumsaliti akawa na huyu na yule,...bado badiliko lolote alikutokea....

    Ni wakati akiwa mwaka wa tatu

    Darasa lilikuwa kimya watu wakiwa bize na kusoma,ghafla mlango wa darasa ukafunguliwa na mwalimu akiongozana na mwanafunzi wa kike Mrembo akaingia....

    Macho ya wanafunzi wote yalikuwa kwa binti yule

    Alikuwa si mrefu sana wala mfupi wa ' wastani' mwenye macho mlegeo , macho ambayo akimwangalia kwa Mara ya kwanza utosita kusema katoka usingizini

    Mashavuni alijaliwa 'dimpoz' zilizomwongezea urembo,alikuwa na kifua kidogo kilichobeba matiti madogo mfano wa vifuu vya Nazi

    Hakika sifa zake sitoweza kuzielezea ukavuta picha ni Mzuri kiasi gani

    Ila wee jua binti huyu alikuwa ni zaidi ya Mrembo...

    Mwalimu akanyamaza kwa sekunde kadhaa akiwa sanifu wanafunzi jinsi walivyopagawa na mtoto yule....

    Akakohoa kidogo

    Wanafunzi wakarudi darasani kutoka katika fadhaiko la mshangao

    "Huyu ni mwanafunzi mwenzenu atajitambulisha,ni mgeni mpeni ushirikiano haya Dada jitambulishe kwa wenzako"

    Binti yule akaachia tabasamu,kwa sauti nyororo akaanza kuongea

    "Kwa jina naitwa Epi kavishe nimwanafunzi mwenzenu naitaji ushirikiano...."

    Wanafunzi wote wakaangua kicheko,hakika alikuwa na sauti ya kuvutia

    Baada ya utambulisho akaruhusiwa kwenda kuketi!

    Akaenda mpaka dawati alilopo Silvar akakaa,watu wote wakaguna

    "h!" Akamsalimia tena silvar

    "h" naye Silvar akaitikia akimsindikiza na tabasamu mwanana.

    ******

    HIMAYA YA MUZIDU

    Himaya yote ilizizima baada ya Muzidu kufanikiwa kuipata tozani

    Shamrashamra zilishamiri kila upande mwa nchi ile

    Wakifurahia kuhama kwa ufalme kutoka HIMAYA ya Bisau mpaka HIMAYA ya Muzidu

    Naye mfalme Bisau kwa kuwa alijua kila kitu kuhusu Tozani pindi alipoitupa kuzimu na kuangukia mkononi mwa binti Zena kabla aijaenda kuombwa na fedhuli yule aliyemuulia mwanaye

    Aliapa pindi akiiweka mkononi asiirudishe ili azushe ugomvi kati ya Zena na Bisau

    Si Pete ya mwanaye?! Uhalali wa kubaki nayo alikuwa nayo yeye

    Bila kujua MUZIDU akaipeleka Pete na kumkabidhi

    Bisau alifurahi kuipata

    "Mwanangu amekufa ila robo tatu ya nguvu zake zipo humu kama si kuziweka huku na hisi angeshinda nitailinda Pete hii kwa hali na Mali

    " nini?!" MUZIDU akauliza kwa mshangao pasina kuamini kile akisikiacho Bisau bila wasiwasi akaongea....

    "Umemuua mwanangu kisa asiweze kuisaka hii pete , umeisaka wewe kwa kutumia uchawi wako mpaka umeipata tena kwa kupewa ukiambiwa uirejeshe hii ni Mali ya mwanangu sitokupa kamwe".....

    Ghafla Muzidu akabadilika na kuwa joka kubwa....

    Likatema mate kumwendea Bisau





    Kabla mate yale ayajamfikia Bisau naye ghafla akatoweka,



    mate yale yakatowekea hewani!,



    pale pale Muzidu akajirudi katika umbo lake la kawaida na ghafla akanyoosha mkono wake chini,



    beseni la njano lenye maji robo likatokea, akacheka kwa sauti na kulielekezea mkono ,shoti ya umeme ikatoka katika mkono wake mpaka katika maji yaliyopo katika beseni lile,



    ghafla akayatoa macho yake kwa mshangao, mambo yalienda tofauti na alivyotarajia,maji yalikuwa meusi tii ishara ya giza,



    akakunjua mkono wake na kuikutanisha yote miwili ghafla hali ya hewa ikaanza kubadilika,



    giza likatawala kilichokuwa kikionekana ni uwekundu wa macho ya viumbe vile,



    ghafla pakasikika radi, radi ambalo lilikuwa ndo sauti aloitoa Muzidu baada ya kukusanya nguvu zake zote na alipoikunjua mikono kombora kali likatoka katika mikono yake na kuliendea beseni,



    mtetemeko wa kutoka kwa kombora lile ulimsukuma Muzidu na kwenda kuanguka nyuma kidogo,



    kombora lile lilipoyafikia yale maji ghafla maji yalibadilika rangi na kuwa mekundu kama damu...



    kombora lile pia lilisababisha ufa ambao maji yale yalogeuka na kuwa damu yalianza kutoka katika ufa ule ambao sasa ulikuwa umeachia,



    na kuanza kujiumba muundo wa nyoka...



    nyoka yule akaanza kuwatemea mate wachawi wale ambapo walimomonyoka na kuwa mkaa! kabla Muzidu ajatoweka.



    Alipokuja kutokea akawa karibu na yule nyoka ambapo zilikuwa ndizo nguvu zake zilizomgeuka akammeza na kuzirudisha nguvu zake mahali pake.



    Nguvu zile ziliacha madhara kwa raia wake wema kwa waovu, lengo la kuzitoa ni ili apate kujua mahali alipo mzee bisau na pete ya tozani aloitaka kwa gharama yoyote ile.



    Kushindwa kwa nguvu zake ni jibu tosha kuwa Bisau alimzidi nguvu, kama Bisau ananguv zaidi yake kwa nini sasa ajifiche na asijioneshe?!.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wazo hilo likakivamia kichwa chake kabla ajashtushwa na sauti ilokuwa ikimnong'oneza.



    "Hahahaha Muzidu unajidanganya,mimi sikuogopi kamwe ila damu ya mwanangu naya mke wangu utazilipa,nguvu nilizonazo nauwezo wa kupambana na wewe nkakuangamiza ila sitaki kukuua



    Yupo atakaye kuua na ndo itakuwa furaha yangu!"



    Sauti ile aloisikia katika masikio yake ikakoma, hasira zikazidi kumpanda Muzidu akaliunga lile beseni na kujaribu kumtafuta bisau bado maji yalibaki meusi!



    ayakumuonesha bisau mahali alipo na hata taswira yake tu! kwa kuwa tayari Muzidu alikuwa mfalme mamlaka yote yalikuwa chini yake akatoa amri,



    "naitaji bisau asakwe popote pale na aletwe kwangu akiwa maiti au mzima, siitaji ulinzi wowote katika kasri yangu walinzi wote ingieni kazini atakayempata kama ni wakike atakuwa malkia wangu na kama ni wakiume ni tampa nusu ya utawala wangu! ni bisau au tozani iletwe hapa!"



    Alimalizia mfalme Muzidu na viumbe vyote vikatoweka.



    SURA YA TATU



    DUNIANI



    Mfalme Bisau baada ya kutoweka akiikwepa sumu kali ya hasimu wake MUZIDU alikuja kutokea juu ya bahari,



    alitembea juu ya maji! pasina kuzama,alikuwa akielekea nchi kavu ,



    ghafla radi likapiga na kugeuka wimbi lililomfata kwa kasi!,bisau akanyoosha kidole chake cha shahada kuliendea lile wimbi lililomfata kwa kasi



    "ashhadduh allah illah aillah wa,wa ash haduannah muammad rasullu llah,"



    jini yule akashahadia,



    kama nilivyosema hapo awali, Kuna majini wema na waovu, Mungu muumba alituumba sisi binadamu na majini ili tumuabudu,



    ivyo kuna majini wanao muabudu Mungu,wanaoswali,wanaosoma quruan tukufu



    Wanao saidia wenye matatizo na kufanya mema yote,



    hao wataingia katika pepo,



    ni kama jini huyu alimtegemea MUNGU ndo maana hata alipo ona lile wimbi akashahadia na ghafla wimbi lile likatoweka na kurudi lilipotoka,



    'alhammdullilah rab llalamin'



    jini yule alimshukuru Mungu na kuendelea na safar kuelekea nchi kavu,



    kumbuka wimbi lile ndilo maji ambayo yaligeuka na kuwa damu ambayo ilileta maafa kwa wachawi wale wa kijini kule chini ya maji!,



    BISAU baada ya kufika nchi kavu akaiangalia anga kwa macho yake makali,ghafla akaskia adhana,akuwa na shaka muda wote alipenda kuwa na udhu akukuwa na aliyemwona akasogea eneo lilikuwa na mchanga,akakimu swala na kuanza kuswal palepale,



    wakati akiwa bado yupo ndani ya ibada ile ghafla upepo mkali ukavuma,na kukusanya tatakata mchanga ukaanza kupaishwa juu na kuunda kimbunga,



    kimbunga kile kikawa kikija uelekeo wa alipo jini yule,



    Na ghafla vikazuka viumbe vya kutisha,viumbe vilivyotoka ujinini na kuja duniani kwa kazi moja tu



    Vyote vikiwa na hari ya kumkata Bisau,mfalme aliye waongoza vizuri kwa muda mrefu



    SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA

    ILIPOISHIA..................



    MUNGU umuepushia mja wake hatari pale awapo ktk Ibada yake wala Bisau akutetereka baada ya kuuona ujio wa maadui zake wale, wala akuhama kifikra



    akasema "allah wakbar" na kurukuu,kutaja jina lile la Mungu mkubwa



    Viumbe vile vikatoweka!,



    MUNGU MUWEZA,UWEZESHA PANAPOSHINDIKANA,



    Baada ya kumaliza ibada alijua pa kuelekea, akatoweka



    ***



    Silva alilala,pembeni yake alikwepo mwanamke Mrembo,ni mwanamke alotokea kumpenda zaidi ya kitu chochote,



    ni mwanamke aliyemwondosha uchungu wa merry na jini zena,



    jini aliyetoweka miaka kadhaa nyuma,



    alikuwa ni Happy Kavishe binti aliyemuumiza kichwa mpaka kumpata,



    na leo ndo ilikuwa mara ya kwanza kumzawadia tunda lake,utamu aloupata aliapa na wala hakuwa tayari kumuacha,



    akamwangalia binti yule alokuwa amelala akataman kumwamsha amwombe tena ila ghafla akasita,mapigo ya moyo ya kaanza kumwenda mbio,



    nywele zikaanza kusisimka,meno mdomoni yakaanza kugongana, pua zake zilipokelewa na harufu kali ya marashi,



    na ghafla akashtushwa na sauti nzito



    "asalam aleykum warhamattulah taghala wabarakat"



    akageuza shingo kuangalia mahali sauti ilipotokea



    naaam akapokewa na sura ya kijana wa kiarabu kichwani alijifunga kilemba alivaa kanzu ya ughaibuni ya ghali ilomeremeta



    mkonon alikuwa na tasbih ilowaka waka, hakika alikuwa ni kijana mzuri,katu usingeweza kudhani kama yule ni mzee alokuwa amestahafu ufalme katika nchi yake eti kutokana na uzee,



    alikuwa ni jini Bisau akusubiri aitikiwe kwa kuwa alijua kijana yule asingeweza kumuitikia akaendelea...



    "Umma wenu unaonekana umma bora kuliko umma zote zilizopita kwa kuwa mnakumbushana mema na kukatazana mabaya!



    Ewe mja wa mwenyezi MUNGU vitabu vitakatifu vinakukataza juu ya kuzini 'usiikurubie zinaa' Mola anatukataza inakuwaje wewe unazini?! Basi kama Quruan tukufu ujui amri ya sita kwenye amri za mungu ni usidhini iweje wewe utende kosa hilo tena kwa kuchekelea na kujiona kidume?!...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Utachomwa tubu kabla muda ujaisha kwani utaitaji kutubu na autakuwa na muda huo,hili silo lililonleta nilikuwa nakukumbusha tu



    Lililonleta ni juu ya Zena Kureysh



    Silvar akashtuka,jini yule akaachia tabasamu pana usoni mwake akafungua mdomo na kuendelea....



    " ni ipi ahadi ulomuhaidi kwamba utamsubiri mpaka utakapomaliza masomo?!



    Umemsaliti na sasa bado kidogo atarejea ni kipi utajitetea kwake?!,uaminifu wako kwake uko wapi?!,binadamu ampendeki Zena atokuacha mzima



    Silva akayatoa macho,alihisi roho ilikuwa ikitaka kuchomoka ,



    "Najua kwa sasa umpendi Zena sasa nimekuja kwako kwa ajili ya msaada ni kweli Zena anahasira juu yako na muda si mrefu atakuja akija Mwambie yeye ndo anamakosa kuondoka na kukaa muda mrefu na ili mrudiane ihitaji tozani....



    Mwambie akuletee tozani ili umsamehe hapo basi utaipunguza au kumaliza hasira yake nipo juu ya msaada wako naomba utambue kwa kuwa a nakupenda basi ataisaka tozani na Pete hiyo ina utajiri mkubwa sana na ukiwa nayo utaweza kumdhibiti asikudhuru kwa kuwa unaweza kunuia asiwe anakuona



    Sina la ziada nikuage pindi ukihitaji msaada basi nitakuja kukusaidia asante"



    Jini yule akatoweka,Silvar avikulalika tena,ni wazi aliona maisha yake na ya mpz wake mpya hapo hatarini ni kipi angefanya?!



    Tozani ikamjia kichwani

    Akaachia tabasamu jepesi,macho yake yakamtazama Happy alokuwa kalala fo! fo! fo! Bila ufahamu wowote,hiyo yote ni kutokana labda na uchovu wa alichomfanyia binti yule.



    'Mmmmmh!' Akaachia mguno,macho yake yakaa ngalia juu ya dari alikuwa akikumbuka kitu



    "Najua kwa sasa umpendi Zena sasa nimekuja kwako kwa ajili ya msaada ni kweli Zena ana hasira juu yako na muda si mrefu atakuja



    akija Mwambie yeye ndo anamakosa kuondoka na kukaa muda mrefu na ili mrudiane ihitaji tozani....



    Mwambie akuletee tozani ili umsamehe hapo basi utaipunguza au kumaliza hasira yake nipo juu ya msaada wako naomba utambue kwa kuwa a nakupenda basi ataisaka tozani



    na Pete hiyo ina utajiri mkubwa sana na ukiwa nayo utaweza kumdhibiti asikudhuru kwa kuwa unaweza kunuia asiwe anakuona

    Sina la ziada nikuage pindi ukihitaji msaada basi nitakuja kukusaidia asante"



    Silva alikumbuka maneno Yale akaachia tabasamu hasa pale alipogundua kuwa Pete hiyo ( tozani ) ilikuwa na utajiri mkubwa tena yenye nguvu pindi akinuia Zena asimuone asingemuona akajikuta anacheka mwenyewe naaam akajikuta akiipenda tozani



    Akajikuta akitamani kuwa nayo,akajikuta akitamani kumuona Zena hata muda huo amuagizie amletee tozani



    Binadamu tumeumbiwa tamaha,...



    Silvar tamaha ilimvaa,ndoto za utajiri akaziota! akapitiwa na usingizi akiwa 'amechatama' domo lake wazi kwa tabasamu!



    Na hata alipolala akaota! Yupo ndani ya ghorofa akiwa tayari ni bonge la tajiri kavaa nguo za gharama akiwa pamoja na mke wake HAPPY



    HAPPY KAVISHE



    naye akiwa kavaa nguo ghali,nje 'parking' yalipaki magari ya gharama....



    Zilikuwa ni ndoto za alinacha kuota kajenga nyumba ya ghorofa juu ya mti



    Makubwa!!!



    ***



    KATIKA HIMAYA YA KUZIMU



    MIAKA MICHACHE NYUMA



    Baada ya jini Zena kumkabidhisha fedha za kutosha mpz wake Silva za kwendea chuoni



    Na kumtakia maisha mema huko alijua miaka mitatu si mingi kwao ni sawa na siku moja ivyo aliamua kutomsumbua katika masomo yake



    Kwani Silva alifikia ',bording' ikiwa na maana katika chumba alicholala alilala na wenzake ivyo asingeweza kumtembelea kama alivyokuwa akimtembelea chumbani kwake.



    Uwezo wa kumtembelea usingizini na hata kufanya naye tendo la ndoa alikuwa nao ila akutaka kumchanganya kijana Yule



    Pia lengo la kutomsumbua ndani ya hiyo miaka mitatu alikuwa na malengo ya kumchunguza je angeweza kuvishinda vishawishi?!



    Ili kuangalia uaminifu wa kijana yule,ndani ya miezi sita tu Silvar alibadilika akaanza umalaya Leo yupo na huyu kesho yule



    Zena alivumilia,akutaka kujitwisha mzigo wa dhambi kwa kuua kila kiumbe kwa kuwa mpz wake ndo mwenye makosa



    Akawa tu akimwangalia anavyofanya!



    Siku zikasonga,miaka ikayoyoma mpaka pale alipopokea wito kwamba

    anaitajika kwao katika msitu Pande uliopo duniani



    Kuzimu waliishi mizimu ila Zena hakuwa mzimu kuzimu alikwepo kama mlinzi aliyewekwa kwa sababu maalumu kisa chake mpaka akawa kuzimu kipo katika riwaya ya kurasa nyeusi....



    Kwao kabisa palikuwa ndo uko msitu Pande, hivyo akafunga safari na kwenda...



    alikuja kutokea nje kidogo ya pori lile siku hii aliamua kwenda kwa miguu kwa kupitia njia za binadamu



    Kwani alikuwa katika umbo la kibinadamu japo hapakuwa na aliyemuona katika wapita njia alokutana nao



    Alikuwa na uwezo wa kutoweka na kutokea kwao ila kuna kitu kilimsukuma atembee



    Ilikuwa ni alhamis saa kumi na mbili na nusu asubuhi



    Akafika langoni



    Lango ambalo binadamu walisubiriana ili waweze kupita kwa pamoja msituni



    Pale palikuwa na watoto wa tatu,wanafunzi



    Wawili walikuwa wasafi mmoja alikuwa mchafu,wale wawili walikuwa wakimcheka yule mtoto mmoja mchafu



    Zena akasogea mpaka eneo lile walokuwepo



    "Wewe Abrah mchafu usiongozane na sisi utapita mwenyewe porini"



    Mtoto mmoja alisikika akimsakama mwenzake aliyetambulika kwa jina la Abrah ambapo mda wote alikuwa akilia



    Njiani walimpiga



    "Na leo alhamisi lazima utarudishwa tu nyumbani mchafu kuogaaa"



    Mwenzake akamsaili akimtia ' kijukuu' cha kichwa



    Wakashikana mkono na kuanza kukimbia wakimwacha yule kijana pale chini



    Moyo za Zena uliumia sana akaitaji kumsaidia ila wito ule ulikuwa ni wa umuhimu zaidi!



    Akaachana naye akitingisha kichwa na kuondoka zake akaingia katikati ya pori kabla ajatoweka na kutokea kwao



    Alichokutana nacho kilimstaajabisha!



    23



    Nyumbani kwao kulikuwa na ugeni,tena si ugeni mdogo



    Mfalme wao alikuwa kawatembelea na lengo la kwenda pale ni kumchumbia binti yule.



    Mfalme huyo alotambulika kwa jina la Zuberi alikuwa ni kijana mdogo pengine mfalme mdogo kuliko wote katika jamii hiyo ya majini



    Aliujua uhodari wa Zena katika kupambana hivyo kuwa naye kama malkia wake lingeiongezea sifa himaya ile



    Na si sifa tu Bali nguvu na Imani pia,tofauti na matarajio yao Zena akakataa



    Wengi walitegemea angefurahia jambo lile ila ilikuwa ni tofauti na mawazo yao



    Zena alimpenda Silvar na hakuwa tayari kumsaliti japo yeye alimsaliti...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hasira, ghadhabu vikampanda na bila kutegemewa akatoweka eneo lile



    Alijihisi mnyonge kunyimwa Uhuru wake kuishi na ampendaye



    Akaja kutokea nyuma ya shule ile ya msingi



    Akashtuka baada ya kuona watoto wakizomea,akakaza macho kuangalia Mbele aliyekuwa akizomewa



    Mapigo yake ya moyo yakaanza kumwendea mbio...



    Sura ya Yule mtoto ambaye nusu saa lililopita alimshughudia akipigwa na wenzake



    Alikuwa ni Abrah



    Abrah Tuesday



    Alikuwa Mbele kama mfano kwa watoto wachafu



    Mwalimu wa zamu akaagiza wanafunzo wote wamzomee



    Naye yule mtoto akawa akilia,



    Bila kutegemea machozi yakajikuta yakidondoka machoni mwa binti huyo wa kijini



    Zena Bin Kureysh



    Kwa nini?!, akajaribu kuwaza hilo pasina jibu



    Akabaki tu akiangalia....



    Mwalimu wa zamu akaingia ofisini na kutoka na walimu si chini ya kumi na moja



    Kila mmoja akiwa ameshika fimbo,wote wakaanza kumchapa mtoto Yule mdogo ambaye alikuwa darasa la tatu



    "Unateseka kisa umasikini , Abrah unadharaulika kisa umasikini naapa nitakutajirisha kwa kukukabidhisha tozani pindi nikiirejeshewa nawe utakuwa tajiri katika ulimwengu huu



    Utakuwa bilionea wa kwanza duniani teseka kwa muda ila ntakutafuta ngoja nikamuone kwanza mahabaty wangu"



    Alinong'ona Zena na kuachana na tukio lile na kuelekea usawa wa msitu,alikuwa akielekea kwa Silva kumpa malalamiko yake juu ya kulazimishwa kuolewa na mtu ambaye akumpenda



    Huku nyuma mtoto yule nguo zake zilichanwachanwa na walimu kisha akafukuzwa mpaka apate sare nyingine



    Alikuwa kavimba mwili mzima,naye huku akilia akaelekea usawa wa msituni pasina kujua atapitaje katika pori lile lenye kutisha akiwa peke yake



    Zena akujua mawazo yake juu ya kumkabidhi Tozani mtoto yule yalinaswa na viumbe majini wa pori lile ila hakuna alojali kwani kama ni utajiri



    Viumbe vile vya pori lile vilikuwa ni matajiri,



    Akaendelea na safari....



    ***



    Tayari Silva alikuwa kashamaliza masomo yake na anasubiria barua yake ya ajira



    Tayari mipango yake ya ndoa yeye na mpz wake Happy ilishaanza



    Mpaka muda huo toka jini Bisau alipomtokeaga miezi sita ilishakata



    Si Bisau wala Zena aliyemtembelea



    Alishasahau kila kitu



    Siku hiyo mida ya saa moja asubuhi wakati akijiandaa kuamka



    Ghafla hali ya hewa kidogo ilibadilika,kaupepo kama cha feni kalimpuliza na harufu ya manukato yakanuswa na pua zake



    Aliijua harufu ile



    Ni harufu ya jini alomsubiria kwa muda mrefu



    Zena Kureysh



    Akakaa mkao wa kumngojea ghafla sauti ile ikajirudia katika maskio yake



    "Najua kwa sasa umpendi Zena sasa nimekuja kwako kwa ajili ya msaada ni kweli Zena ana hasira juu yako na muda si mrefu atakuja

    akija Mwambie yeye ndo anamakosa kuondoka na kukaa muda mrefu na ili mrudiane ihitaji tozani....



    Mwambie akuletee tozani ili umsamehe hapo basi utaipunguza au kumaliza hasira yake nipo juu ya msaada wako



    naomba utambue kwa kuwa a nakupenda basi ataisaka tozani



    na Pete hiyo ina utajiri mkubwa sana na ukiwa nayo utaweza kumdhibiti asikudhuru kwa kuwa unaweza kunuia asiwe anakuona

    Sina la ziada nikuage pindi ukihitaji msaada basi nitakuja kukusaidia asante"



    Baada ya kuikumbuka kauli ile aloambiwa na Bisau akatabasamu na kumngojea Zena kwa hamu



    Na ghafla....





    Zena akatokea, moyo wa Silvar akapiga paaaaa!

    Mapigo ya huo moyo yakaanza kumwenda mbio....



    Ghafla katika pembe ya chumba kile Bisau akatokea....



    Bado alikuwa kavaa kanzu yake ile huku mkononi kashika tasbih



    Hakuna aliyemwona kati ya wawili wale,akabaki akiwa angalia kwa macho yake yenye nuru Kali



    SILVAR alikuwa kashika mdomo kwa mshangao,huku Zena akimtazama kwa tabasamu bashasha...



    Ghafla machozi yakaanza kumtoka Silvar,



    "Usilie mpz wangu nimerudi naomba unsamehe habiby"



    Zena aliongea kwa sauti ndogo lakini tamu,ghafla naye machozi yakaanza kumtoka



    Wote wakawa wakilia!!!



    Wakakumbatiana lakini kilio cha Silvar kikazidi,kwikwi ilomshtua hata Zena....



    Akamuachia na kumwangalia vizuri usoni....



    Katika pembe ya chumba kile Bisau akatabasamu na kumnyooshea mkono Silvar shoti zikatoka mpaka katika kichwa chake



    Akarudisha mkono wake sawa.....



    Zena baada ya kumuona mpz wake analia namna ela , akamkazia macho



    Lengo amsome fikra zake lakini jini Zidau Alisha gundua lile ndo kisa cha kumpiga shoti kijana yule



    Zena hakuweza kuyasoma mawazo ya kijana huyo akashtuka kwa jambo lile ila akuuonesha mshtuko wake waziwazi



    Aligundua hapo kuna kitu!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Hapakuwa sawa,akaangaza macho yake katika kila pembe akugundua kitu



    "Mpz wangu unatatizo gani plz nambie usilie ivyo!"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog