Search This Blog

USIKU WA KAFARA (ROAD TO 2017) - 3

 







    Simulizi : Usiku Wa Kafara (Road To 2017)

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ******



    Neema alichelewa kwani kabla ya kurudi ndani ya gari alifikiwa na mzee juma ambae alimshika na kumvutia kifuani kwake

    "Mtulie msije mkafa kabla ya wakati ...kijana mmoja amfunge aliekuwa chini na mwingine amtoe huyo kinyago alie bakia kwenye gari"

    mzee juma aliongea akiwa kamkumbata neema kwa nyuma ya mgogo na muda huo misuli ya maumbile yake ikimsimama kuwa sambamba nyuma ya mak*lio ya neema.



    Dolla alikuwa kama ana karibia kupoteza fahamu kwa kuto kuamini anacho kiona na muda huo kijana alieshika panga na kamba alijipenyeza ndani ya gari kumchukua

    "niacheee" dolla alipiga ukelele mdogo

    "wewe nitakucharanga kama kuni utulie" yule kijana alimfokea dolla kisha dolla hofu ikamtawala akakamatwa na kufungwa kamba mikononi mwake na kushushwa chini...



    Tayari mzee juma alishakutwa na hamu ya kumuingilia neema lakini alihofia kwenda kinyume na amri ya yule kiumbe mkongwe walio muita jina la malikia na mzee juma alijua wazi yote yale wanayo yafanya pale yalionwa wazi na malikia....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " Haya fungeni na huyu nyau kisha muwaonganishe tuondoke....wewe mpumbavu acha kelele zako za kulia kama mtoto nitamuua yoyote kati yenu ambae ataongea au kuujiliza" mzee juma aliongea na kumsukumiza neema huku akimkemea baraka aliye kuwa ana ugulia maumivu ya kuchomwa kwenye paja..



    Wote walifungwa mikono yao kwa ustadi mkubwa kisha mzee juma akakata mti mrefu kisha waka msimamisha baraka na dolla kisha wakaufunga mti ule kwenye shingo ya baraka kisha ukafuata kwa dolla na kumaliziwa kwa neema , mti ule ulifungwa shingoni mwao hivyo wote walikuwa wamefungwa kwenye mti mmoja .



    Kisha wakainuliwa kwa pamoja mti mmoja mrefu ukiwa umepita pembeni mwa shingo zao zilizo fungwa kwa kamba ipasavyo.

    mze juma aka msogelea baraka kisha akauchomoa kwa nguvu ule mshale kutoka kwenye paja la baraka ,hapo baraka alishindwa kuvumilia alipiga kelele za uchingu.

    "kwani jamani tume wakosea nini" neema aliuliza lakini hapohapo kofi zito la mzee juma lilitua shavuni pake nae akalia kwa uchungu.

    "Nime waonya sitaki hata kidogo kusikia mkiongea nita wa chinja..... haya ongoza safari ianze" sauti ya kikatili ili wa fokea ...wakaanza kutembea kwa mstali ulio nyooshwa na ule mti ulio lalia mabega yao huku baraka akiwa mbele akitembea kwa kuchechemea na maumivu makali yakiukumba mguu wake...



    Maskini baraka!

    Ikawa vijana wawili wanawaongoza mbele huku nyuma wakifuatiwa na mzee mkatili ...naam mzee juma.



    ****************



    Gady hakuwa na ujanja wowote wakati akiwa pale chini akamuona kijana mwingine wa kundi lile la mbweha akifika eneo lile kwa nia ya kumsaidia muhaini mwenzake.

    "Nilidhani anaendelea kukimbia.... kumbe ulisha mdhibiti...." aliongea yule haini bweha

    "ah hana ujanja huo" yule aliempiga gongo gady alijibu na haraka waliifunga mikono ya gady kwa mbele kiustadi kisha wa wakamuinua

    "yule mwingine yupo na shija anapelekwa kwa njia ya mkato na wewe mpeleke huyu kwa njia hiyo mimi naenda kumuangalia mzee juma kwenye gari lao"haini yule aliongea akimaanisha tayari john kaushaanza kuongonzwa kuelekea kwa goroza kwa njia ya mkato

    "sawa naona tutakutana makao makuu" mwenzake alijibu na wakaachana....



    Gady akiwa chini ya uangalizi wa haini mmoja aliekuwa na shoka kali ,gady akasurutishwa kutembea kuelekea kwenye pango la goroza.

    safari ikaanzq



    Ndio mbweha hawa binadamu ambao ni vibaraka wa goroza walifanikiwa kuwanasa vijana watano akasalia sarah aliekimbizwa na dalu.....



    *************



    Sarah alikimbia kwa mwendo ambao kwa hakika kama angekuwa kwenye mashindano ya riadha basi hatu hussein bolt bingwa wa mbio asinge weza kumfikia sarah..



    Sasa sarah alikimbia bila kupiga yowe wala kuita msaada aliacha kupiga yowe baada ya kujua anapoteza pumzi na kelele zile zinamfahamisha adui yake sehemu alipo.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kuna wakati sarah aligeuka nyuma na hakumuona yule alie mkimbiza..na alipo zidi kutokomea sarah akakiona kichaka kikubwa haraka sarah akaingia mule huku akihema akiwa kalala kifudi fudi akihisi pumzi zikimuishia ....



    palikuwa kimya sana...



    Kimya kile kilimaanisha mtu alie mkibiza hakuwa kabisa eneo lile , sasa sarah akawa anawaza afanye nini ndani ya msitu ule...



    Lakini kabla hajafikiria mengi macho yake yakamshuhudia dalu mbali kidogo na kichaka kile akiwa na panga akiangaza huku na kule huku akiwa kajikunja kutokea kiunoni..



    Kumbe dalo alikuwa ana msaka sarah kwa kumvizia na mawindo yaliyo tawaliwa na ukimya wa hali ya juu..



    Macho yalimtoka sarah na muda huo alisikikia sauti ya kuburuzika kwa kitu pembeni yake alipo angalia alikiona kitu cheusi kirefu kikiburuzika taratibu...



    Alikua ni nyoka..!!!!! hakuwa nyoka au kijinyoka bali lilikuwa ni joka!



    Lahaula!!!! mbele yake kuna dalu na pembeni yake kuna joka refu....like share ije mapema...





    "Nakufa .." neno hili lilipita kichwani mwake....ilikuwa ni bora akamatwe na dalu kuliko kufa kifo cha kugongwa na nyoka...



    Sarah alijibiringisha kwa kasi na kutokea upande wa pili wa kichaka huku joka lile likimkosakosa kumgonga nalo likitanabahi na kurusha mate...na muda huo sarah alishatoka nje ya kichaka na kutimua mbio .



    Hii ikawa salama kwa sarah kuliepuka joka lile lakini kwa kulikwepa joka lile sarah akawa kajianika wazi na kumfanye adui yake amuone....naam dalu alimuona saraha akikimbia...



    "Mjinga unasumbua leo utazaa namimi hukuhuku" dalu alifoka huku akiwa ana mkimbiza sarah tayari dalu alishapata matumaini ya kumkamata...



    Sarah alihamaki huku akiendelea kutimua mbio akibadili uelekeo na akiurudi upande wa barabara.



    *****************;**



    Gadyson alitembea nyuma akifuatiwa na yule haini alie shika shoka kali, wakati anatembea gadyson kwa bahati mbaya alijikwaa na kuanguka chini kama mzigo yule haini akamfokea huku akimuinua gady alipo anguka pale chini aliinuka na kipande kidogo cha mti chenye unene wa vidole viwili akawa kakifumbata kwa mikono yake miwili iliyo fungwa .

    "Tembea kiume nyang'au wewe" yule haini alimfokea gady huku akimsukuma atembee.



    Gady alitembea kama hatua kumi kisha akaanguka tena na muda huu alijingusha makusudi! na alivyoanguka alijipindua chali...

    "wewe mshenzi unanitania" yule haini aliongea kwa hasira huku akimuinamia gady ili aikamate shingo ya gady...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati yule haini anainama gady nae alisukuma juu mikono miwili ilio shika kipande cha mti huku huku shabaha yake ikiwa imelenga uso wa haini..



    Yule haini alikuaa kafanya kosa kumuinamia gady aliye lala chali.!



    Wakati anainama alikutana na kipande cha mti ambacho kilizama kwenye jicho lake ! akashindwa kulizuia yowe huku akiachia chini shoka lake na mikono yake yote ikienda kwenye jicho lilitobolewa na kipande cha mti ,haini yule akapepesuka na kutanga tanga akikabiliana na maumivu makali kutoka kwenye jicho ambalo muda ule halikuwa jicho tena ila chongo lilio vuja damu.



    Shambulizi la gadyson lilikuwa limefanikiwa !



    Gady akabilingita mpaka kwenye ile shoka akaishika na kusimama nayo haraka akiwa kaishika kwa style ya kushambulia..akimtazama adui yake aliehangaika kutafuta njia ya kukimbia huko yowe la mtu yule likizidi kuamsha viumbe vilivyo kuwa mstuni mule..



    Gady akapiga hatua kumsogelea adui yake na kuinua shoka gady akamshumbulia kwa kumpiga shoka na kumnyamazisha kabisa, mwili wa kibaraka wa goroza ukaanguka chini huku koromeo lake liki mwaga damu!

    shoka lilikuwa lime chimba shingo yake na kuli kata koromeo.



    Pakawa hakuna yowe wale kelele zaina yoyote kilicho sikika pale ni mtiririko wa damu na sauti hafifu ya mkoromo kutoka kwenye koromeo la bweha haini kibaraka wa goroza...



    Gady alikuwa ameua! akawa kasimama na shoka liliotiririka damu likiwa kwenye viganja vya mikono ilio fungwa.



    Haraka haraka akazikata zile kamba alizofungwa kwa kutumia shoka lile kisha akaondoka akikikimbia akiwa na shoka akiuacha ule mwili ukitokwa na damu.



    Hakujua nini kimetokea kwe nzake na sasa alikuwa anakimbia kutafuta msaada na njia ya kuokoa maisha .



    Alikuwa hajawahi kumjeruhi mtu kwa siraha tangu azaliwe lakini leo amejikuta amemshambulia adui yake na kumuondoa uhai wake kitu hiki kikamfanya akimbie akiwa kachanganyikiwa, wakati akikimbia alijikuta akivuka barabara huku akikimbia bila kujua alijikuta kaitambuka barabara na kuingia upande wa pili wa wa msitu ule huku akizidi kutimua mbio.



    Hatimae akahisi kuishiwa pumzi ikamlazimu aanze kutembea huku akitweta...



    Wakati akitembea ghafla akahisi vulumai likija kutokea nyuma yake ,alipo geuka aliwaona watu wawili wakija upande wake huku waki kimbia mbio kana kwamba walikuwa kwenye mashindano wakiwa umbali wa hatua zisizo zidi miamoja na kumi wakija upande wake...



    Gadyson kuona hivyo alipiga hatua moja kubwa mpaka nyuma ya mti mkubwa akajificha pale kisha akachomoza kichwa chake kidogo akichungulia kule walipo tokea wale watu, akaona bado wana kuja upande wake.

    ikamlazimu gady kubaki pale nyuma ya mti huku akiwatazama watu wale ambao walizidi kuja upande wake ,na mara wakakalibia.

    "sarah..." gady alijikuta akilitaja lile kwa sauti ya chini baada ya kumuona mmoja kati ya wale wawili aliofukuzana wakija upande wake.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kumbe watu wale walikuwa ni sarah na dalu...

    dalu alikuwa anaendelea kumkimbia sarah huku akikaribia kabisa kumkamata.!



    Gadyson akamuona sarah akipita mbele ya ule mti aliojificha yeye na muda huo huo macho yake yakamuona dalu aliekuwa na panga akimkimbiza sarah wakiwa karibu kabisa.



    Hapo gadyson akatambua sarah anafukuzwa na mtu mbaya, dalu alipopita tu ndipo gadyson nae akaingilia mbio zile huku yeye gady akiwa nyuma ya dalu..



    Haikupita dakika gadyson alimkalibia kabisa dalu kisha gady akainua shoka lake na pigo zito la shoka lilitua kichwani kwa dalu !



    Dalu akajikuta akianguka chini huku akishindwa hata kupiga kelele wala kuomba maji .

    Sarah alisikia mtu akianguka lakini sarah hakutaka kusimama

    "Sarah simama nishammaliza huyu mimi ni gadyson" gady alipaza sauti

    sauti ilimfikia na kumshitua sarah ikamlazimu ageuka ndipo akamuona dalu akiwa chini huku gadyson akiwaamesimama imara.

    "Gadyson " sarah aliita kuhakiki alichokisikia

    "ndio nimimi" gady aliitaka huku akimalizia kumuua dalu

    "nini kimewatokea.." gadyson aliuliza huku akimsogelea sarah

    sarah hakujibu ila alimsogerea gady ubavuni kwake na kuanza kulia

    "tupo kwenye hatari bora nisinge kuja huku" sarah alilia na kumsimulia jinsi walivyo vamiwa kwenye gari na yeye alivyo kimbia.

    "sijui hawa watu wa ains gani ...hata sisi tulikamatwa ila mimi nilijitetea wamemchukua john...sarah tuondoke kwanza eneo hili sio eneo zuri" gady aliongea kisha akainama na kuchukua shoka yake shoka ambayo tayari ilisha dhurumu uhai wa vibaraka wa wili wa goroza..



    Gady akamshika mkono sarah na kuondoka nae kutafuta sehemu nzuri!



    Sasa mwezi ulizidi kung'aa mstuni mule na kufanya mtu kuonekana kirahisi ,gady na sarah wakatembea kwa muda wanusu saa mpaka walipofikia sehemu ambayo haikuwa na miti mingi na wakasogea chini ya mbuyu mkubwa wakakaa wakiwa wamechoka..

    "Hapa sijui wenzetu kimewakuta nini ...sijui tuelekee upande upi ili tutokee kijiji jirani yaani sielewi kabisa" gady aliongea akiwa kachanganyikiwa.

    "Kwani hatuwezi kurudi kwenye gari letu tulichukue na kuondoka maana kwa muda tuliokaa litakuwa lisha poa" sarah alitoa ushauri

    "wewe hauoni kama tutakuwa tunachezea roho zetu..kama tutakuta hawa watu tusio wajua wapo kwenye gari" gady aliongea kisha akajikuta anajikosoa mwenyewe

    "ila kuwakuta sio rahisi maana nilimsikia mwenzao akisema wana tupeleka makao makuu yao ..ila mbaya zaidi nakumbuka funguo yenyewe ya gari baraka aliitia kwenye mfuko wake wa suruale" gady aliongea na hapo moyo wa sarah ukaingiwa na hali ya kukata tamaa...



    Kimya kikapita...



    "Ila gady nakumbuka mchana uliniambia umetokea kunipenda" sarah alivunja ukimya na gady akapata hali ngumu kidogo kwenye kujibu swali lile

    "nd..ndio"

    "Naomba ukafanikiwa kutoka humu salama fika nyumbani uwaeleze yote juu ya safari hii na kifo kitakvyo nikuta" sarah aliongea kwa majonzi akiwa hana tumaini akijihisi mkosefu kwa wazazi wake kwa kutowashirikisha safari ile , alijua mpaka muda ule wazazi wake wanahangaika kumtafuta kwa kumpigia simu.

    "ah usiseme hivyo lazima tutoke humu salama" gady alisema huku akimkubatia kwa nguvu sarah wote machozi yakiwatoka

    "nikuambie kitu gadyson"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "niambie sarah"

    "MBEZI "B" NYUMBA NAMBALI 1002 HAPO NDIPO KWA WAZAZI WANGU NIKIFA FIKA UKAWAAMBIE YOTE YALIO TUSIBU KWENYE HII SAFARI NILIO WAFICHA" sarah aliongea kwa hudhuni..

    "Ah usiseme hivyo sarah..." gadyson alishindwa kumalizia kauli akihisi donge zito likimkaba kooni wakabaki wamekumbatiana pale.



    Tayari walikuwa wamesha maliza dakika thelathini wakiwa chini ya mti ule wakitawaliwa na majonzi....



    Kwa mbali hatua kama miatatu gady alimuona mtu kwa mbali akitembea huku mtu yule akiwa kambeba mtu mwingine mabegani kwake ,moyo wa gady ukashtuka akamuonesha mtu yule sarah

    "atakuwa nani yule au atakuwa baraka na john ?" sarah aliuliza

    "ah itakuwa..sasa wewe baki hapa mimi niwanyatie nijue ni kina nani...usijali utakuwa salama" gady alimbembeleza sarah

    "kuwa makini mpenzi.." hah! sarah alijikuta akimuita mpenzi gady ...gady hakuamini .

    wakabaki wametizamana kwa upendo kisha midomo yao ikakutana kila mtu akashindwa kuzuia hisia zake kwa mwenzake..

    "sarah subiri nakuja" ikamlazimu gady kujitoa katika busu zito kwani hawakuwa mazingira salama.



    Gady alimuacha sarah pale nayeye akiwa kashika shoka alianza kumnyatia yule mtu alie beba binadamu begani ,

    gady alikuwa akihama mti hadi mti na hatimae alianza kumalibia yule mtu!



    Ghafla akamuona yule mtu akisimama na kumtupa mtu alie mbeba begani kisha kuondoka !



    ile nadharia ya kuwa huenda mtu yule alikuwa mwenzao ikamtoka na kuhisi yule ni adui ...gady son akasubiri yule mtu alipo ondoka nakutoeka kabisa .nae gady akanyata mpaka pale .... gady hakuamini macho yake baada ya kufika eneo lile!



    Kumbe kulikuwa na shimo na ndani ya shimo gady aliziona maiti mbili ikiwemo moja ilio tupwa na yule mtu.



    Gady alipoangalia kwa makini alitambua miili ile ilikuwa ni miili ya baraka na john!



    Gady alikumbwa na hali ya kuto kuamini ilimtawala akaliachia shoka lake chini kisha akaingia ndani ya shimo lile fupi hata bila ya kufikiri.



    Machozi yalimtoka huku akishudia miili ya rafiki zake wakiwa wamekwisha kuawa kwa kuchinjwa sasa gady alijua wazi wapo kisiwa cha umauti.

    Mara akaiona funguo ya gari ikiwa kwenye luksi ya suruale ya baraka na hapo wazo la kujikomboa likamrudia haraka akaichukua funguo ile kisha akatoka mule shimoni .



    Ile anatoka tu shimoni akakutana na ugeni mpya machoni pake!



    Mbele yake kulikuwa na mtu alikuwa na amemulekezea mshale uliovutwa ipasavyo kwenye upinde wa kibaraka wa goronza....



    "hakuna atakae pona kati yenu usiku huu" yule mtu aliongea akiwa anazidi kuvuta ule mshale kumlenga gadyson.



    Balaaaa

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Sasa gady akajuua amekutana nakifo na huenda ulikuwa ndio mwisho wake.

    "tume wakosea nini " gady aliuliza

    "subiri utajua ukifika kuzimu" yule mtu mwenye upinde akamfokea

    muda huo macho ya gady yaka muona sarah kwa mbali akija kwa kuvizia , gady alihamanika akatamani amwambie sarah akimbie!



    Yule kibaraka wa goroza akaona hamaniko la gady kibaraka yule akajua lazima nyuma yake kutakuwa na kitu ikamlazimu kibaraka yule ageuke kujua nyuma yake kuna nini.



    Kosa kubwa!!!!





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog