Search This Blog

MZIMU ULIOREJEA - 1











    IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Mzimu Uliorejea

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    KATIKATI YA JIJI



    USIKU WA MANANE

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upepo mkali ulivuma,ulioambatana na radi sambamba na mvua kubwa

    ilonyesha kwa hasira katikati ya jiji la MOSHI mkoa wa KILIMANJARO.



    Angani hakukuwa na nyota ilong'aa wala mbalamwezi kusawizisha nuru

    katika ulimwengu huo, kila mmoja alijifungia ndani ya nyumba zao wakiwa usingizini, wengine usingizi uliwapaa wakisikiliza dhoruba ilokuwa

    ikiendelea nje ya nyumba zao.



    Miti ilidondoshwa, dhoruba lilitawala baadhi ya nyumba bati zao

    ziking'olewa,kuta zikidondoshwa,na viumbe waliyomo katika nyumba hizo

    kuwa katika hatari ya kupoteza maisha.



    Kila mmoja akijaribu kuokoa uhai wake



    Katikati ya jiji katika jumba moja la kifahari waliyoko katika nyumba

    hiyo awakuguswa na dhoruba lile kutokana na u imara wa nyumba

    yao,



    walichukulia mvua ile kama mvua nyingine,iliyowapa starehe katika

    usingizi wao.



    USIKU HUO HUO UPANDE MWINGINE WA JIJI KATIKA MAKABURI YA NJORO MJINI MOSHI



    Hali ya makaburini pale aikuwa tofauti na hali ya katikati ya jiji,mvua iliyoambatana na radi ilidondoka eneo lile la makaburi, mlinzi alojulikana kwa jina la kipele alikuwa mita kadhaa

    akitetemeka na kupigwa na mvua ile

    katika geti la kuingilia makaburini

    pale palipopendezeshwa na uzio ulotengenezwa kuzunguka eneo lote la

    makaburi yale.



    Hakuwa na sehemu nzuri zaidi ya kujibanza kukwepa dhoruba

    ile, alishughudia baadhi ya miti ikidondoshwa na kumtisha kwenda

    kusimama katika miti hiyo.



    Akabaki kajikunyata akitetemeka, kuikubali hali hiyo.



    Mita kadhaa mbele!,toka geti la mlinzi mpaka katikati ya makaburi

    palikuwa na kaburi moja ambalo lilikuwa limejengewa kifahari!,



    juu ya kaburi lile kulikuwa na kibao kilichoandikwa jina JACOB P MSAKI kwa kunakshiwa tarehe yake ya kuzaliwa na siku aliyokufa,juu pakiwa na msalaba wa dhahabu.



    Katika kaburi lile ghafla mtetemeko ulianza, mtetemeko mdogo,



    mtetemeko ulokuwa katika kaburi lile tu!,tetemeko lililoacha nyufa na kuanza

    kumomonyoa kaburi lile..



    mara ghafla vumbi kutoka ndani ya kaburi lile likaanza kutoka



    Ajabu!!!...



    Vumbi ambalo alikuwa hata na chembe chembe ya tope,likapanda kuelekea juu



    Mara ghafla jeneza LA kifahari likatoka,pamoja ya kwamba lilikuwa limeoza pengine kwa kuwa lilifukiwa mda mrefu ila uzuri wake ulionekana wazi wazi



    Baada ya kupanda juu likatua pembeni ya shimo lile



    Ghafla mlango ukafunguka,na mtu wa ajabu alokuwa ndani yake Akaonekana



    Ni wazi mfu alikuwa kafufuka kiajabu,kiumbe wa ajabu kilichooza na kutembelewa na mafinyofinyo katika suti ilovubaa



    Kiumbe kile kikaiangalia dunia kwa jicho baya, jicho lenye mng'ao ulotisha pindi kiumbe hai kingine kama kingepata bahati ya kuliona,



    Ghafla kikaachia tabasamu pana, meno yalooza na mengine kutoboka yakaonekana, moshi mzito ukatoka katika domo lake



    Bado mvua ilikuwa ikinyesha sambamba na radi za hapa na pale



    Jitu akutishwa na hali ile



    Maji ya mvua yalimlowanisha na kumuongezea nguvu na furaha ya kuingia katika ulimwengu wa dunia hii,waishawo viumbe aina ya binadamu,jitu lile likanyoosha mkono mpaka katika jeneza lile alotokea muda mchache ulopita,



    shoti ya umeme ikatoka kuliendea jeneza

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ghafla jeneza likatoweka sambamba na eneo lile kusawazika,pakawa kama mwanzo,



    jitu lile likaachia mwayo mkubwa lililoambatana na radi ambalo lilimfikia mlinzi getini na kuchukulia radi lile kama maradi mengine yaloendelea eneo ilo



    Jitu lile likanyoosha mikono juu na kuachia cheko La dharau kisha likatoweka eneo lile



    KATIKATI YA JIJI



    KATIKA JUMBA LILE LA KIFAHARI



    Katika nyumba ile ya kifahari ambayo wenyeji wake walikuwa wamelala fofofo,nje ya nyumba ile palizuka kitu!



    ni kitu ambacho dakika chache nyuma

    Kilitokea katikati ya makaburi mjini Moshi



    Ni jitu lile la kutisha!



    Likaangalia kushoto,kisha kulia likaachia tena cheko!



    Cheko lililochukuliwa kama radi! Kwa waliobahatika kulisikia katika usiku ule mzito, usiku mnene,usiku wa manane



    Jitu likanyoosha mkono wake wa kulia juu ghafla shoti za umeme zikiambatana na radio zikatawala!



    Ghafla bisu lenye kumeremeta, kikatokea katika kono lake, jitu likaachia cheko jingine!....



    Akatoweka!!!



    NDANI YA JUMBA LILE LA KIFAHARI



    Katika jumba lile La kifahari,nje kuliibuka kitu



    Kitu cha kutisha



    Ni lile jitu,lililotoka makaburini ghafla likanyanyua mkono na kisu kikatokea

    Bisu lenye ncha Kali,jitu lile likaachia cheko sambamba na kutoweka

    Likaenda kuibukia katika moja ya chumba cha jumba lile



    ********



    Ndani ya jumba lile katika chumba kimoja kipana walilala watu wa tatu mtu wa makamo na mtoto wao mdogo

    Wote walikuwa wamelala fo fo fo fo

    bila kustushwa na mvua inyeshayo

    Ghafla katika pembe ya kuta za jumba lile likaibuka jitu



    Jitu lile lile



    Likimwangalia mwanaume alolala kitandani pale kwa dharau



    Akamnyooshea mkono ishara ya kumnyonga,mtu yule akawa akichezesha chezesha mguu ishara ya kutapa tapa



    Si kwamba mtu yule aliyetopea katika usingizi akumuona jitu lile



    LA asha! Ndani ya usingizi wake aliliona jitu lile na jinsi alivyokuwa akimnyonga,ni wazi siku hiyo ilikuwa ndo mwisho wa maisha yake

    Ni kweli asingeweza kusalimika



    "Niliapa kuwamaliza kwa hiki kisu ivyo sitokunyonga"



    Jitu liliongea na kukinyanyua kisu kile juu akakishusha kwa nguvu kuelekea tumboni kwa yule bwana



    "Tutaonana kuzimu mwanaharamu wewe"



    Jitu lile likatamka na kukishusha kisu kile katikati ya mbavu za mtu yule



    Damu zikaruka



    Jitu likacheka na kutoweka



    Likiuacha mwili uloaribika vibaya katika kitanda kile



    Mke na mtoto bado walilala fo fo fo fo

    Bado ilikuwa ni katikati ya usiku



    Ghadhabu zikiwa zimempanda jitu lile la kutisha likanyanyua bisu lake na kono lake pana,likaushusha katika mbavu za kijana yule

    Damu zikaruka



    Jitu likatabasamu,baada ya kuakikisha ameondoka na uhai wa kiumbe yule akatoweka eneo lile nyuma akiacha maafa makubwa sana



    ***



    Jitu lile baada ya kutoweka pale lilikuja kutokea barabara ya juu iendayo stendi,pembezoni ya barabara ile palikuwa na kituo cha bodaboda,

    ambapo pembeni palikuwa na mabenchi yalochimbiwa.



    Pembeni ya kituo kile cha bodaboda usiku ule jitu lile lilipo ibukia eneo lile hapakuwa na mtu kwenye mabenchi yale, kilikuwa ni kijiwe cha kahawa jioni,mchana wasafiri wakikaa kusubiri daladala za kuelekea stendi ,kituo hicho na stendi palikuwa na umbali tu mkubwa



    Jitu lile likakaa katika benchi lile,likifikiria jambo hili na lile

    Hisia za machozi yakitawala katika nyuso zake, ghafla akakumbuka kitu,kitu kilichomzidishia hasira akajinyanyua na kwa haraka akaanza kuelekea upande alojua yeye mwenyewe



    Roho ya kikatili ikitawala mawazoni mwake



    ***



    SHANT TOWN



    MOSHI



    Lilikuwa ni jumba jingine la kifahari, ukutani kulizungukwa na nyaya maalumu za ulinzi, getini kulikuwa na walinzi wawili kifuani walikuwa na silaha nzito za kivita



    Ghafla nyuma ya nyumba ile kikasikika kishindo bila kujiuliza Mara mbili mlinzi mmoja akiwa kashika silaha yake vizuri akatoka eneo lile kuelekea kule kishindo kiliposkika mlinzi mmoja akibaki katika geti lile akiwa kashika silaha yake tayari kwa chochote



    Ghafla kishindo kingine tena kikasikika sambamba na yowe,yowe lile likamsukuma mlinzi yule aliyebaki pale getini kuelekea kile nyuma alipoenda mwenzake



    Kosa!!!



    Hakuamini kile alichokiona,mwenzake alichomwa bisu LA koromeo macho kayatoa Pima,mlinzi yule akapepesa macho lakini akuona alosababisha taharuki ile



    Mshangao ukamvaa!



    Bumbuwazi likambumbukia!



    Wasiwasi na uwoga ukamtawala!



    Kwa kihoro akamkimbilia mwenzake na kuanza kumwita



    "Dully,Abdull, nini kimekupata swaiba,"



    Akawa akimtingisha kwa nguvu,ghafla akasikia cheko nyuma yake



    Mlinzi yule akageuka,mshtuko kwa kile alichokiona ukamtawala,macho yakamtoka pima,silaha ile nzito ya kivita ikamponyoka,ikadondoka,Kwa uwoga akiwa akirudi nyuma



    Jitu lile la kutisha lilikuwa Mbele yake likimwangalia kwa macho makali,macho yalomtisha mlinzi yule,bisu lenye mpini mpana,na ncha Kali likiwa katika kono lake lenye vinyweleo vya kutosha



    Liliachia tabasamu meno yake yalooza na kutoboka yakaonekana



    "Mliniua kwa mateso makali sana,ila Mimi sitokwangamiza hivyo nimerejea kwa ajili yenu tutaonana kuzimu mwanaharamu wewe"



    Jitu liliongea kwa jeuri huku likipiga hatua kumfata mlinzi yule,wazi lililomjia kijana yule ni kupiga kelele lakini hakupata muda huo kwani akujua ni sangapi jitu lile lilimfikia na kumchoma bisu lile la koromelo kama mwenzake,



    mlinzi yule akadondoka kama zigo na kutapatapa,akatulia tuli

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jitu likaivuka miili ya walinzi wale na kutokea Mbele ya lango la jumba lile,likazama ndani



    Alipoufikia mlango mkubwa wa kuingilia ndani ulofungwa akanyooshea kono lake mlango ukatii amri ya kufunguka,jitu likapita na mlango nyuma ukajifunga kama awali



    ****************



    Bado mvua ilikuwa ikinyesha,ila kidogo ilipunguza makali,jitu likaibuka chumbani katika jumba lile LA kifahari alosababisha mauaji nje ya walinzi wawili,macho yake yakatua kwa kijana alolala akikoroma katika kitanda kile ,kisha kwa mke wa kijana yule alovaa kaupande cha kanga katika maungo yake



    "Fatuma binti mrembo"



    Akaita kwa sauti mdogo ya kunong'oneza,sauti ilopenya mpaka katika maskio ya binti yule ghafla akafumbua macho yake

    Ana kwa ana na jitu,bisu mkononi

    Binti yule akashtuka



    "Kweli wew ni binti mrembo skatahi,nyumba hii ndo ilikufanya unsalitii eeh?!!!...c ungenambia unaitaji nyumba? Siwezi kukuacha mzima tutaonana kuzimu mwanaharamu wewe!"



    Wakati wote binti yule alikuwa akipikicha macho yake akihisi pengine yupo ndotoni



    Jitu lile lililotoka makaburini usiku ule mnene wenye mvua na gharika za kutisha



    Binti yule akabaki ameganda kama sanamu,akishindwa kupiga kelele wala kufanya chochote



    Hatua moja akapiga na hatua jingine akawa kamfikia binti yule akanyanyua bisu lake akamchoma moja kwa moja tumboni,binti akafa akiwa katoa macho ulimi kaung'atia



    Jitu likatoweka!!!



    Likijua kabisa litaacha taharuki pindi mume wa binti yule akiamka na kukuta maiti ya mke wake.



    SAA 11 ALFAJIRI



    Mvumo wa sauti ya simu yake ilimshtua katika usingizi wake

    Akajinyanyua na kuikwapua simu ilikuwa kitandani pale akuangaika kuangalia mpigaji kutokana na kumtambua kutokana na mlio wa simu yake alomsetia



    "Kuna mauaji ya kikatili yametokea usiku huu waitajika ofisini haraka sana dakika tano uwe umefika inspekta"



    "Ovar kamanda"



    Kijana yule alojulikana kama Inspekta NURDIN aliitika sambamba na kuamka hari ya kufanya kazi ikiwa imemtawala,akajimwagia maji haraka na kutoka katika nyumba ile ya kota,mpaka katika kituo chake kidogo cha kazi ofisini akukuta askari yeyote alowasili,ilo akujali macho yake yakatua katika lango LA mkuu wake,mlango ulikuwa wazi kumjulisha kuwa mkuu wake alikwepo akachepuka kuuendea lango ilo

    Akajiingiza ndani kwa tabasamu pana,



    "Duh hii serikali ya magufuli inafanya kazi vizuri mkuu unaogopa kutumbuliwa unawahi kazini hivi ama kweli hapa kazi tu"



    NURDINI aliongea kwa utani,tabasamu likipendezesha uso wake mdogo,tofauti na matarajio yake bosi wake yule akucheka wala kumwangalia macho yake yalikuwa bize katika kalabrasha (file) alilokuwa akiliandika alipomaliza akanyanyua kichwa chake na kumtazama kijana wake yule ambaye alikuwa kimya mzee yule wa makamo mwenye mvi nyeupe kichwani akakohoa kidogo kusafisha koo



    "Kama dakika kumi zilizopita nimepokea simu mbili tofauti mauaji ya aina moja yametokea yani walouwawa wamepigwa visu vya makoromeo...."



    "What?!!!...."



    "Yah na visu vyote ni vya aina moja kutokana na maelezo ya waloripoti tukio kushangaa aina hiyo ya visu naitaji kutuma madaktati na maaskari kwenda kuichukua hiyo miili kwa ajili ya uchunguzi LA kini kabla sijawatuma naitaji wewe uende kama afisa upelelezi mchunguzi na wewe ndo nakukabidhi file ili ripoti ipitie kwangu sawa?!"



    "Yes mkuu alitika inspekta yule akilipokea file lile na kupiga saluti moja kubwa na kugeuka kuondoka akaelekea katika ofisi yake na kufungua droo akaliweka file lile na kutoka na kajikitabu kadogo alikiweka ndani ya kabegi chake na kuingia ndani ya gari lake tayari kwa kuelekea eneo la tukio huku nyuma mkuu yule wa kituo akapiga simu hospitalini,wakatoka baadhi ya madaktari katika ambulance na kuelekea eneo la tukio,mkuu yule pia aka wahitaji baadhi ya maafande waelekee eneo La tukio kuchukua miili ile.akijua fika inspekta NURDIN atakuwa kashawasili eneo la tukio kwa uchunguzi kabla yao



    ***********



    Mke wa Ragiv Kumar alifumbua macho yake taratibu na kuupeleka mkono wake katika mwili wa mume wake akagusa kitu katika mwili wa mumewe



    Akashtuka na kupeleka mkono wake katika godoro alipokelewa na unyevu nyevu,mwanzo alihisi pengine ni mvua ila tangu lini mvua ikaingia chumbani mwao ikambidi apeleke mkono wake katika swichi na kuiwasha taa ya chumbani mule



    Kitu alichokiona kikamfanya mama yule wa kihindi aachie yowe moja na kutulia tuli akiwa kanyooka,macho ya mshangao akiwa kayatoa Pima



    Kelele alopiga ikamwamsha mtoto aloanza kulia kwa nguvu mpaka vyumba vya jirani vikasikia wakasogelea chumba kile cha wazazi wao na kuanza kukigonga bila kuitikiwa mwisho wakakata shauri kukivunja awakuamini walichokikuta hatua ya kwanza ni kupiga simu polisi alipopokea mkuu wa kituo kile kidogo cha MOSHI mjini na kuahidi kutuma maaskari muda ule mkuu yule wa kituo kile alishapata taharifa ya mauaji mengine ya binti na mengine ya walinzi na bosi wao yote yakiwa ya aina moja,ndipo alipompigia kijana wake NURDIN na kumwelekeza maeneo Yale kabla maaskar wengine hawajawasili.ilikuwa ni bado saa kumi na moja kasoro alfajiri.



    KATIKA NYUMBA ILE ILE YA KIFAHARI



    Alionekana kijana mdogo akishuka katika kitara cha polisi,ajabu akuvaa sare za jeshi akiwa na kabegi chake mgongoni akauendea mlango wa nyumba ile ndani kulikuwa na watu wengi,vilio vikiskika ilo akujali akaenda mpaka chumbani walipomaiti alipofika alijitambulisha na kuomba watu wasogee afanye uchunguzi wake,kabla ajafanya kitu akamulikwa na mwanga wa kamera inspekta akashtuka na kumgeukia alopiga akakutana na tabasamu pana LA binti mrembo mkononi akiwa kashika kamera na kabla inspekta yule ajafanya kitu Dada yule kwa wepesi wa ajabu akapiga tena picha mbili



    "Ooh shit binti unafanya nini?!"



    Akalalamika NURDINI macho yake yakiwa kifuani kwa Dada yule palipokuwa na kitambulisho cha kazi



    Mwandishi wa habari,mnoko



    Akalalamika NURDIN



    "Nakukabidhi kesi hii kwa kuwa nahisi inautata ndani yake,usiruhusu mwandishi yeyote wa habari kuchukua tukio ili kwa kuwa likitoka katika vyombo vya habari litasababisha woga kwa wananchi...nakuamini na sitegemehi kama utaniangusha.....



    Kauli hiyo ikajirudia katika kichwa chake,kumbukumbu pindi alipoambiwa na mkuu wake pindi alipokabidhiwa kalabrasha lile,macho yake yakarudi kwa binti yule wakatazamana akaanza kupiga hatua kumsogelea kama binti yule alijua lengo la inspekta yule akachoropoka katikati ya watu na kupotea eneo lile



    Kwa kuwa muda uliikuwa umeenda NURDINI akaachana naye na kuendelea kuchunguza maiti zile na eneo lile kiujumla (survey) kabla maaskari wengine awajaja



    Akiuliza maswali haya na Yale huku aloyaona yanafaa akiyaandika katika kajikitabu chake



    Pamoja na yote alishtushwa na kitu kimoja aina ya kile kisu na uchomwaji wake



    Kila alipoviangalia aliguna aliikumbuka sura flani katika tukio flani maeneo flank



    Yah! Ni sura ya jitu ilimjia akilini,kivipi?!



    Alishindwa kujielewa akabaki na butwaa,ghafla wakaingia maaskari wengine na daktari



    " naitwa daktar SAMSON MGHONJA ndiyo daktari nlochaguliwa kuichunguza miili hii"



    Daktari yule akajitambulisha



    "Naitwa inspekta NURDIN ndiyo mpelelezi mwandamizi wa kesi hii ripoti zote naitaji zifike kwangu"



    Akaongea inspekta yule naye dokta akatabasamu kuafikiana naye



    NURDIN akaaga akiwaacha polisi wale wakiendelea na upelelezi wao mdogo yeye aliitaji kufika eneo lile LA pili ambalo walinzi waliuwawa ndani mwanadada alikuwa kifo cha kikatili...



    Kwa mwendo wa gari yake alifika eneo lile wakati akiwa katika harakati za kuingia ghafla akampiga mtu kikumbo MTU yule akadondosha kitu,kwa haraka akainama kuokota na kumwangalia yule alompiga kikumbo



    Wote wawili wakapigwa na butwaa



    Alikuwa ni yule mwandishi wa kike



    "Naomba camera yangu"



    Yule Dada aliongea kishari zaidi



    "Haya matukio hayatakiwi kuripotiwa na vyombo vya habari binti ni usalama wa taifa....



    Aliongea NURDIN lakini pasipo kutegemea binti yule alijigeuza kwa wepesi wa ajabu na kurusha konde zito,kabla inspekta ajakaa vizuri akaukamata mkono wake na kuuzungusha kidogo



    Inspekta akaiachia kamera ile,Yule Dada akapiga hatua kukimbia,akajichanganya na watu na kutoweka eneo lile



    Mshangao aloupata NURDIN aukuelezeka,kwa unyonge akapiga hatua kuingia ndani akiacha taharuki eneo lile



    ****************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SAA MBILI KAMILI ASUBUHI



    Gari LA kifahari aina ya RANGE lilipakiwa eneo LA parking akashuka kijana mrefu maji ya kunde

    Alikuwa kavaa suti nyeusi ilomkaa vyema akaanza kupiga hatua kuelekea eneo la ofisi ile



    Ilikuwa ni kampuni ya kusafisha,na kusafirisha,pamoja na kupima madini



    Bwana MARTIN KYANDO mkurugenzi wa kampuni ile ndiye alikuwa kashuka katika range ile na kuelekea katika ofisi yake

    Alikuta vijana wake wakiendelea na kazi kama kawaida alifarijika sana kwa kuona vijana wake wakiwahi kazini mapema.

    Akapita mpaka kwa katibu muhtasari wake, wakasalimiana kwa bashasha naye akazama ofisini kwake

    Akakaa katika kiti na kuanza kupitia

    Magazeti ya siku hiyo



    Mngurumo wa simu yake ukamshtua na kuichukua simu yake akaipachika sikioni



    Akashtuka kwa habari aloipokea toka upande wa pili,macho yakamtoka Pima



    Ni juu ya vifo vile vilivyotokea usiku wa siku hiyo,mauaji ya kikatili kwa watu alowafahamu kabisa,akajinyanyua na kutoka pasina kuelewa

    anaelekea wapi



    Katu akujua kuwa yupo katika ( target ) ya jitu



    Kiumbe hatari alosababisha mauaji Yale na kiumbe alobakia katika orodha yake ni yeye



    Alikuwa akielekea hospitalini zilipo hifadhiwa maiti zile



    Zilikuwa ni za watu wake wa karibu

    NURDIN wafanya biashara wenzake



    "Ni kipi kilichotokea Mungu wang?!"



    Alijiwazia akipiga break katika hospitali ile ya mawenzi



    Wake na ndugu wa marehemu walikwepo eneo lile walikimbia na kumkumbatia MARTIN



    Huku wakiwa wanalia,japo yeye alikuwa ni mwanaume tena mwenye roho ngumu lakini alishindwa kuvumilia kuyazuhia machozi yasimtoke



    Waandishi mbalimbali wa habari walikwepo wakiuliza ili na lile



    INSPECTA NURDIN pia alikwepo eneo lile,kwa uchunguzi maalumu,kila Mara alitupia macho yake maeneo walikwepo waandishi akitegemea kumuona yule binti bila mafanikio



    'Yule binti atakuwa ni nani?!,na kwa nini atumie ubabe kwa askari kuichukua kamera na nani alomwambia juu ya tukio hill akawah eneo la tukio kabla yangu?! Hapana kuna kilichopo nyuma ya pazia kwa binti yule lazima ni msake halafu na kisu kilee!!!....embu ngoja'



    Aliwaza NURDIN na kuchepuka kumsogelea JACOB alokuwa bado akiwafariji wafiwa



    "Sorry,tunaweza kuzungumza?!"



    Alitamka NURDIN na kupelekea kijana yule amwangalie inspekta kwa mshangao,inspekta akamtolea tabasamu kumwondoa wasiwasi



    Ila bado JACOB akuwa na amani wakajisogeza pembeni



    "tunaweza kuelekea kituoni na mazungumzo na wewe!"



    "Mimi?!!"



    "Yah wala hata usijali ni mazungumzo ya kawaida"



    Wakaingia ndani ya gari na kuelekea kituoni kwa mahojiano

    Ilikuwa ni tayari saa nne na madakika asubuhi



    **********



    SHARFIA ZUBERI mwandishi wa kujitegemea aliingia ofisini na kwenda moja kwa moja mpaka kwa bosi wake



    "Hii habari ya leo sijui mtanlipa shi ngapi kwa maana nimempiga inspekta kwa unyeti wake,na ni lazima ichapishwe Leo leo"



    Aliongea binti yule akitabasamu mwariri mkuu wa gazeti lile akaipokea kamera ile na kuanza kuzikagua picha zile



    Macho yakamtoka Pima kwa kuto kuamini akionacho



    "Ni SAA moja saiv naitaji kwenda hospital ilipoifadhiwa miili kama vipi nipe changu nisepe kabisa"



    "Hapana Shary ni hatar wewe kwenda tutamtuma mtu hospitalin kumbuka wewe sasa unasakwa"



    "Oooh common nilishasahau ila poa babake peleka katika machine hizo picha nkalale saivi"



    Mwariri yule mkuu akujibu kitu akafungua kabati na kutoa burungutu akamkabidhi



    Dada yule akazihesabu zilikuwa ni milioni sita akatabasamu na kuondoka eneo lile



    Masaa manne baadaye yani SAA tano habari ile ilikuwa katika gazeti La athuhuri litokalo siku hiyo hiyo



    Ikawa taharuki katika taifa hili Dogo,taifa likazizima kwa habari ile



    Mkuu wa kituo kikuu cha MAJENGO akashika simu yake na kumtwangia NURDIN huku akiwa na hasira kwa kuvuja kwa habari ile



    *Huyo binti kwa nini anajiamin hivyo mpaka kufikia kumpiga inspekta na kukimbia na kamera?!....



    *habari zi mevuja na mkuu wa kituo amemuita ins Nurdin ni nini anataka kumwambia?!



    *insp Nurdin kama anajua kitu katika kesi hii kwani visu vile dizain kama kavishangaa na amemwita Martin ambaye yupo katika target ya jitu kwa



    KITUONI



    inspekta NURDIN aliketi kwenye kiti chake,mkono wake ukiwa bize kuandika baadhi ya vitu alivyogundua katika file lake



    File alilokabidhiwa na mkuu wake wa kituo,



    macho yake ya katua kwa kijana alokaa katika kiti cha wageni ofisini kwake



    Akaufungua mdomo wake ulotoa sauti yake ndogo ya upole ilobeba maswali ya mtego kwa aulizwaye



    "Pole bwana Martin Kwa kuwapoteza rafiki zako wa karibu ila je una weza ukajua au hata kuhisi tu sababu au muhusika wa vifo vyao?!"



    Martin akatingisha kichwa kukataa kujua sababu,ni kweli akuitambua sababu hiyo bado alikuwa katika fumbo ambalo kwake ilikuwa ni vigumu kufumbuka.



    Nurdin akafungua droo na kutoka na kisu,ni sample ya vile visu vilivyokutwa katika makoromeo ya maiti akamkabidhi kijana yule Martin Akakipokea na kukitazama



    "Kila ukionapo icho kisu huwa unakumbuka wapi?!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Martin akakipokea kile kisu na kukitazama kwa makini, huku macho ya inspekta wa jeshi LA polisi yakimwangalia kwa ukali na kwa udadisi wa hali ya juu



    Ghafla simu ya NURDIN ikaita,kwa mlio alousert wa mkuu wake akapokea



    "Unafanya nini Nurdin nilikwambia nini lakin?!"



    "Kwani ni nini mkuu?!,..."



    "Akuna cha nini nakuitaji ofisini haraka na gazeti LA hadhuhuri"



    "Ovar"



    Simu ikakatwa,kukatwa kwa simu ile na kutajiwa gazeti la hadhuhuri kukamkumbusha juu ya binti yule



    Binti mwandishi alomponyoka katika mazingira ya kutatanisha



    Macho yake yakatua kwa Martin aliye kuwa kakishikilia kile kisu akiwa mbali kimawazo



    Ni wazi jamaa yule alimkumbuka jitu....



    ***"****"***"



    SURA YA PILI



    MIAKA MITANO NYUMA



    MACHIMBONI MKOANI ARUSHA



    "Mama klare naomba ugali mkubwa nikapige kazi"



    Aliongea kijana mmoja mrefu mwenye mwili ulojengeka kimazoezi,baada ya kuingia katika kibanda kile cha mama ntilie kilichopo eneo lile la machimbo



    "Bora hata umekuja babaa!,nikukabidhi huyu kijana mwenzako alokuja kutafuta maisha huku mererani"



    Aliongea mama ntilie yule,macho yake yakiwa kwa kijana alokaa pembeni yake,alikuwa ni kijana mtanashati kizazi cha sasa huwaita masharobaro



    Kijana yule aloingia akamkatia jicho kijana yule alomkuta akamzawadia tabasamu, na kijana yule wakuja akalijibu



    "Kwa jina naitwa Jacob AU Jb kwa kisasa zaid cjui wewe mlugaluga unaitwa nani?!"



    Kijana yule alokuja kuagiza chakula akajitambulisha



    "Naitwa Martin natokea DSM nimekuja huku Moshi kutafuta maisha"



    Wote walokuwa wanakula wakaangua vicheko,Martin akaangalia chini kwa aibu



    "Huku si Moshi ni Arusha na upaswi kusema umekuja kutafuta maisha sema nimekuja kutajirika fala wewe"



    JB akamsahihisha,Martin alishangazwa na jinsi kijana yule alivyokula,ugali kilo moja alimaliza mwenyewe.ndo maisha ya mgodini baada ya JB kumaliza kula akajinyanyua na kumwambia MARTIN amfate



    "Mwanzo utateseka sana,una budi kuvumilia utakaa na sisi akuna atakaye kunyanyasa katika balo letu tupo wa wili Mimi na mshkaji wangu wewe utaongezeka wa tatu kama nyoka kazi yako ni kupandisha mchanga wenye madini juu mkiwa wawili na tolu au na Mimi wakati mmoja kati yangu Mimi na tolu akiendelea kupasua miamba utazoea tu dogo"



    JB alitoa maelezo marefu ambayo MARTIN aliyaelewa



    Walipofika kazini MARTINI akavalishwa tochi kichwani akavalishwa na kifaa flani cha oxygen na kufungwa kamba JB naye akavaa hivyo hivyo na wakaanza kushika kuelekea chini,walipofika chini kulipokuwa na giza wakaanza kuelekea lilipo balo lao walipofika walimkuta kijana mmoja alokuwa kifua wazi jasho likimtiririka mkononi akiwa na nyundo kubwa akipasulia miamba alipowaona akasitisha zoezi lile



    "Tolu nimemleta nyoka huyu tupige naye kazi"



    MARTIN aliongea akimwangalia yule walomkuta



    "Kwa jina naitwa ZUBERI karibu"



    Kijana yule akajitambulisha, muda ule ule bila kuchelewa akashika nyundo yake na kuendelea na kazi



    "Kusanya huu udongo wote pamoja"



    "Sawa kak..."



    Kabla ajamaliza kauli yake kwa ghafla ZUBER alimgeukia na kumtandika teke LA mbavu,MARTIN Akapepesuka na kudondokea mwamba ulochongoka na kutengeneza ncha Kali



    Damu zikaanza kumtoka



    Akatulia tuli,bila kujitingisha huku damu ikizidi kutiririka



    "ZUBERI umeua"



    JB akaongea kwa kubwabwaja macho kayatoa Pima,akiuangalia ule mwili kwa woga





    Wakati wote jb alokuwa akiteteneka,Uso wa ZUBERI ulikuwa wa kawaida



    JACOB alimfata MARTIN pale chini na kumuinamia alimsikiliza mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa mbali



    "Sasa umefanya nini ZUBERI"



    JB akamuuliza ZUBER kwa ukali akiwa kamtolea macho ya hasira



    "No swaiba nilikuwa namkaribisha jombaa kilingeni....



    ZUBERI akuweza kumalizia kauli yake JB alimvamia na kuanza kumshambulia mangumi,na mateke mpaka watu wa balo lingine ndo walokuja kuamua ugomvi huo



    ZUBERI alikuwa kajeruhiwa vibaya sana usoni damu zikimchuruzika

    Uongozi wa mgodi ule,ikabidi iwapandishe wote juu wakatibiwe kwanza



    Baada ya masaa kadhaa wote wakawa katika hali nzuri,wakarudi chini ya ardhi hayo ndo yalikuwa maisha yao,ubabe,ukatili,ili mradi maisha yasonge



    Kule chini ya mgodi ilikuwa ni kama kuzimu,kwani njia ya kuingia Chini ulipo mchanga wenye madini ilikuwa ni ndogo sana,walilazimika kutambaa kama nyoka kwa wakusanyaji,huku kukiwa na hewa isiyotosha

    Walipokusanya wakutosha waliupakia katika viroba na kupanda navyo juu kwenda kuumwaga wakipokezana taratibu.



    Siku zikasonga,MARTIN akaanza kuzoea hali ya kule,na pesa akaanza kuzikamata,



    Walikuwa ni vijana wa tatu walopendana,ilipofika jioni walienda club wote,walitokea kuwa marafiki wakubwa



    Kila alipo onekana MARTIN alionekana JB,na kila alipo onekana JB alionekana ZUBERI



    Siku hiyo wakiwa bar jioni baada ya kutoka machimboni ZUBERI akatoa wazo lake



    " muda wa kuwa matajiri milioneya sasa umewadia...."



    Aliongea ZUBER akainyanyua glass yake ya bia na kupiga nguchu moja akaiweka chini



    "Kivipi kaka ZUBERI?!"



    MARTIN kwa shauku alihoji



    "Mimi nipo muda mrefu sana hapa mgodini!,nimekuja huku kabla yako wewe JB,na pia nimekuja kabla yako we MARTIN"



    Akanyanyua chupa yake na kumimina bia katika glass yake kisha akaendelea

    "Siri nyingi sana za huku nazijua!,ili kama tunataka tutajirike balo liteme hatuna budi kumwaga damu!,damu ya mtu....



    Aliongea ZUBER kwa kujiamini!,

    Tofauti na mategemeo yake JB akakunja sura



    " alafu wewe msen..g...e ndo mawazo yako hayo kuua ndo maana ile siku nia yako ilikuwa ni kumuua MARTIN boya wewe nyie ndo mnaoua hata maalbino,sijui huna roho gani wewe...."

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Siyo hivyo MR Yale yalishaisha mbona?! Tutabaki kuwa wachimbaji siku zinaenda,siku zinarudi mwisho tutakufa na vifua vikuu bila kupata mizigo ya mahana si vibaya kutoa nafsi moja zifaidike nafsi tat....



    " ishiya hapo hapo zuu kama una cha kuongea



    "Lakini kaka j kwa nini tusijaribu tu kufanya hivyo



    MARTIN alichangia



    " katu siwezi kushiriki dhambi ya kuua,na kama mna nia hiyo Mimi sipo nanyi bora nijitenge nifungue balo langu...."



    "Siyo hivyo MR ni kuelewana tu"



    "No!,kuelewana katika kuua?!,hapana siwezi"



    Alimaliza JB na kujinyanyua akatoka eneo hilo alishavurugwa na alishachukia

    Baada ya JB kuondoka na kuwa acha vijana wale wawili wakaendelea na kikao chao



    "Sikia nikwambie MR wewe umekuja peke yako!,Mimi nimekuja peke yangu,na yule fala kaja peke yake exactly tumejuana humu humu,hivyo kama ameamua kututosa nasi tumtose asiyependa maendeleo hiyo ni hadui tumtoe kafara fala yule"



    Aliongea ZUBER kwa kujiamini, alitegemea MARTIN angeshangaa tofauti na mategemeo yake kijana yule akushangaa,Bali aliachia tabasamu hafifu



    "Sasa tutamwangamizaje?!"



    Kwa sauti ya upole MARTIN akaoji,



    "Ni rahisi tu, tukiwa baloni wakati nyie mwapandisha mchanga mkipandisha safari mbili,safari ya TATU Mimi nitamtwanga nyundo ya kichwa,nyundo moja atunaye tena"



    "Alafu..."



    "Swadakta!,damu itakayo mwagika ndiyo utajiri wetu,kuna mahali tutapaka tunuizie alafu huo mwili ntakuonesha njia za panya za kupita kwenda kuutupa....



    Wakagongesheana mikono kukubaliana kwa jambo lile,



    MARTIN aliutamani sana utajiri na aliazimia siku akirudi kwao harudi na gari la kifahari,akanunue majumba ya kifahari aliona malengo yake yakianza kutimia



    Baada ya kumaliza vinywaji wakajinyanyua wakiwa wamelewa na kuelekea ghetoni kwao wakiwa wamelewa

    Walimkuta JB tayari kashalala



    NO O7



    Ilipoishia



    Baada ya kumaliza vinywaji wakajinyanyua wakiwa wamelewa chakari na kuelekea ghetoni kwao

    Wakamkuta jb akiwa kashalala



    Songa...



    Wakamwangalia KWA macho ya dharau na kujipandisha kitandani tayari kwa kuipitisha siku hiyo na kuikaribisha siku mpya



    Siku ambayo kwao waliiona ni nzuri kwa kutekeleza matakwa ya mioyo yao

    Hata usingizi ulipowabeba ndoto walizo ota ni za ukwasi,wakiwa wameuaga umaskini.



    Usilolijua ni sawa na usiku wa Giza

    Asubuhi waliamka wote wakiwa ni wenye furaha,awakuwa na kawaida ya kupika walikula mgahawani.



    Siku hiyo mpya ilikuwa ni siku ya majonzi kwa GOD,toka yeye alipoamka moyo ulikuwa ukimuuma pasina sababu



    Ilikuwa ni dalili mbaya kwake na alilitambua hilo,baada ya kumaliza kunywa chai wakashuka mgodini na kuanza kazi



    Safari ya kwanza wakapandishs udongo juu na kumuacha ZUBERI chini akiwa anapasua miamba, lengo lake safari ya tatu ndiyo safari ambayo ingekuwa ya mwisho kwa kijana Yule

    Nafsi zao zilibadilika na kutengeneza utando wa ukatili katika mioyo yao



    Safari ya pili nayo ikawadia wakawa sasa wanamuesabia dakika

    Moyo wake ulizidi kumwenda mbio,na kumnyima raha



    Safari hiyo walikuwa wakishuka chini ndiyo ZUBERI angemaliza lengo lake

    Lakini aikuwa hivyo wakati wakimwaga ule mchanga ghafla wakasikia tetemeko la ardhi katika eneo lile

    Watu wakaanza kukimbia huku na kule kwa waliokuwa nje,kila mtu akitaka kunusuru roho yake



    Kwa waliokuwepo ndani ya mgodi tetemeko lile likaanza kuporomosha mapande ya maudongo na mamiamba na kuwafunika



    Akukuwa na uwezekano wa kuokoka katika kisanga kile



    Lilikuwa ni tendo LA dakika kumi lililopoteza mamia ya watu

    ZUBER akiwa mmoja wapo,ilibidi serikali wazuie wachimbaji kuendelea kuchimba eneo lile kupisha kufukuliwa kwa maiti zile



    Kwa upande wa MARTIN na JB walijawa na simanzi ilojenga kovu LA kudumu mioyoni mwao



    Huku siri ya MARTIN na ZUBERI juu ya kumtoa JB kafara ikibaki katika moyo wa MARTIN akijihisi na mkosi

    Ndo kilichomuumiza zaidi



    "Ndugu yangu!,tukiruhusiwa kurudi mgodini,mgodi utatema balaa umaskini baybay"



    Aliongea JB akiwa na tabasamu hafifu katika uso wake

    Baada ya huzuni ya muda mrefu tabasamu likapendezesha sura yake ile ya upole ila ilojaa ukatili ndani yake akafumbua mdomo wake kwa sauti iloanza kuleta matumaini



    "Kivipi kaka j"



    "Mgodi si umeua?!,umekunywa damu sasa ni muda wa kutajirika"



    Aliongea jb,MARTIN akuamini kile akisikiacho akajinyanyua katika kochi na kumkumbatia swaiba wake yule

    Mambo yakawa yamegeuka,wakasubiri kwa hamu siku mgodi ukifunguliwa ni baada ya wiki tatu wakaruhusiwa kuanza kazi tena,baada ya serikali kuridhika na hali ya hewa katika tetemeko LA ardhi

    Wakarudi katika balo lao,eneo alilofia ZUBERI



    Kama JB alivyosema lilikuwa ni eneo lenye Neema

    Madini ya kumwaga,kwa ushirikiano wakafanikiwa kununua mgodi ule ukawa chini yao.



    MARTIN hakuwa yule wa miezi michache nyuma



    Jb akuwa kijana yule wa machimboni wote waliota vitambi



    Wakanunua majumba ya kifahari jijini ARUSHA na magari ya kutembelea

    Jb akuacha kumkumbuka rafiki yake ZUBERI kila Mara alienda katika kaburi lake alilolijengea na kukatia majani

    Ilikuwa ni tofauti na MARTIN yeye aliangalia maisha yake tu



    "Nina habari njema kwako Mr"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Aliongea jb tabasamu likiwa limechanua katika uso wake



    "Habari ipi mkuu"



    Martin alioji!



    Ile tenda ya kupandisha wazungu mlima KILIMANJARO MOSHI si imetudondokea sisi



    "Waoooo"



    Martin akuamini akamkumbatia jb,ilikuwa ni tenda ya mabilioni

    Ikabidi waamie katika mkoa huo wakiwa moja ya mabilionea wakubwa nchini TANZANIA



    Wakafungua kampuni ya uuzaji na usafirishaji madini huku wakichukua tenda yote ya kupandisha wazungu mlimani



    uzuri mmoja wote hawakuwa na ndugu, ndugu ni wenyewe wawili...



    ************



    SURA YA TATU



    "Bosi kuna binti kanipa barua hii kanambia nikupe naye wakaondoka"

    Katibu muhtasari wa kampuni ile aliongea huku akimwangalia jb,alokuwa akizunguka na kiti



    "Yukoje yukoje huyo binti"



    Akauliza JB huku akiipokea barua ile



    "Alikuwa kajifunga kininja sikuweza kuiona sura yake"



    "What!!?"



    "Ndiyo bos!..."



    "Sasa wewe ulijuaje ni wa kike JE kama alikuwa ni wa kiume kavaa vile"



    "No bosi ni kutokana na sauti yake"



    "OK na shukuru kaendelee na kazi"



    Akatamka jb,Dada yule akatoka na kumuacha bosi Wake akifungua ile barua



    Ghafla macho akayatoa kwa mshangao pasina kuamini kile akionacho katika barua ile....



    "Kwako mpenzi"



    Tulizo LA moyo wangu,tabibu wa nafsi yangu bila shaka u mzima

    Yah hata mm pia ni mzima



    Dhumuni la barua hii ni kukweleza Yale yaliyoko katika moyo wangu

    Jb tambua NAKUPENDA wew pekee ndo muhasibu wa moyo wangu,sahau yote yalopita tugange yajayo



    Ile ilikuwa ni utoto na sasa tu ni watu wazima,ni muda wa kuganga yajayo namba yangu ni 0652281153 naomba nitafute plz kuna zawadi nataka kukupa sijawah mpa mwanaume yoyote hila ntakupa wewe mpz



    NAKUPENDA JB



    Ni Mimi



    FATUMA



    Jb akuamini kile alichokisoma akapikicha macho na kurudia kusoma tena maneno Yale ila ayakubadilika



    Akajinyanyua kwenye kiti kile na kutoka mpaka alipo karibu muhtasar wake



    "Umesema alikuwa kavaa nikabu?!!?"



    "Yap Bo's kavaa kininja kaziba sura yake"



    "Ok ! ahsante"



    Aliongea Jb akielekea katika lift akajiingiza na kushuka kuelekea chini

    Jengo lile lilikuwa linaghorofa nne hvyo yeye alikaa juu na baadhi ya wafanyakazi



    Na msaidizi wake Martin alikaa ghorofa ya Tatu



    Akashuka katika ghorofa hiyo na kuingia ofisini kwa rafiki yake yule kipenz Martin alipofika akakaa kwenye kochi na kumkabidhi rafiki yake barua ile



    MARTIN akaisoma



    Akuielewa



    Akairudia tena



    Lakini bado akuielewa



    Ndipo ilipobidi JB aanze kumsimulia



    ***



    ZAIDI YA MIAKA KUMI NYUMA



    Ilikuwa ni familia ya kifukara,iliyoishi katika nyumba moja ya udongo ilolalia upande mmoja



    Ilikuwa ni familia waloishi watu wa nne



    Baba mama na watoto wao wawili wa kiume,ambaye ata shule awakuweza kwenda kutokana na kuzidiwa ufukara



    Mbali na ufukara walokuwa nao familia ile ilitengwa na kijiji kutokana na imani za kichawi



    JB mtoto mkubwa wa familia ile alitokea kumpenda binti mmoja jirani yake na kuzifikisha hisia zake

    Binti yule alojulikana kwa jina la Fatuma aliishia kumcheka na kumkejeli kitu kilichomzidishia hasira na upendo wake ukageuka kuwa chuki



    Chuki iliyokuwa ikizidi kuutafuna moyo wake kila uchwao siku inayofatia!

    Kuna matatizo kibao tu yalitokea kwenye familia ikanilazimu niiache familia ile



    Sikurudi katika kijiji kile mpaka Leo hii

    Na huyo binti nikwambiaye ndo huyo Fatuma aloleta barua kwa katibu muhtasar wangu



    "Mh"



    Martin akaguna baada ya kuskia kisa icho



    "Amejuaje hapa na amejuaje kama umefanikiwa?!"



    "Si ndo hapo best miaka kumi mingi si mchezo"



    "Ila ilo si tatizo kaka sasa wewe ni Mtu maharufu mfanyabiashara mkubwa unajulikana!,hvyo hapo akuna la ajabu"



    (Jb akacheka)



    Martin akaendeleaCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Na mtoto kajitunza,kajitunza kwa ajili yako yapaswa uwoe kaka miaka inaenda ujana baybay ongea na mtoto huyo vizuri"



    Jb akafikiria kidogo ni kweli maneno Yale yalimwingia ipasavyo

    Bila kuaga akajiondoa na kuelekea ofisini kwake



    Akakaa akiwaza hili na lile,lile na hili mwisho akaamua kushika simu yake na kuandika namba kadhaa akazipiga

    Zikaita



    Ghafla zikapokelewa kwa sauti nyororo na nzuri

    Alikuwa ni Fatuma



    "Alooh nani mwenzangu"



    Jb akasita mwili ulimtetemeka mdomo ukawa mzito kufunguka

    Angeongea nini?!



    Akujua kuwa kuna alokuwa akimfatilia kwa karibu kila akifanyacho

    Kwa ajili ya manufaa yake



    Pia akuziona camera zilizotegeshwa katika ofisi yake ile kwa sababu maalum



    Ndiyo alikuwa ndani ya Giza tororoo.....



    SHARFIA ZUBERI katibu muhtasar wa kampuni ile na mwandishi wa kujitegemea wa gazeti La alasiri kiti kilikuwa cha moto



    Tabia yake ya udadisi na kutamani kujua kila kilichoendelea kilimpelekea kutegesha kamera katika ofisi ile.



    Kitendo cha kumuona yule Dada na kumpa barua,kubabaika kwa bosi wake alijua kwa vyovyote lazima angetengeneza habari

    Matokeo yake ayakuwa tofauti na alivyotegemea



    JB akazama katika penzi la binti yule Fatuma



    Kila kwenye kumbi za starehe walikuwa wote

    binti SHARFIA naye akuacha Ku post habari zao



    Kwa kuwa wote walikuwa ni wafanyabiashara wakubwa,ila katu Jb hakujua Sharfia ndiyo aliyevujisha habari zao pia akujua kuwa yule alikuwa ni mwandishi wa kujitegemea katika gazeti la alasiri hilo bado lilikuwa ni ficho lililojiifadhi katikati ya moyo wa binti yule mpole na mcheshi



    **********



    MIEZI MITATU BAADAYE



    Moyo ulimuuma,tamaa ya kumiliki Mali zote ikamtawala



    Akaweka nadhiri



    Kumwangamiza JB na kampuni yote ibaki chini yake



    Kwa uwezo wa pesa alokuwa nao uwezo wa kufanya chochote akitakacho alikuwa nao

    Ni vipi asifanye?!



    Mwanzo lilianza kama wazo,wazo alilopewa na mtu alomjua yeye likaja kubadilika na kuitaji kulifanyia kazi

    Ila kuna watu wawili ilikuwa lazima

    Awaweke sawa



    Mwanasheria wa kampuni ile pamoja na Fatuma mpz wa rafiki yake

    Akamuitaji mwanasheria yule wakapate naye lanchi



    Akamweleza wazo lake



    Mwanzo mwanasheria yule alikuwa mgumu kuelew lakini Martin alijaliwa maneno



    Uwezo Wa kushawishi



    Maneno ambayo yalimwingia ipasavyo mwanasheria yule mwisho akakubali



    "Mimi ninachokuomba unisaidie ni kufoji hati kuzi ghushi kutoka katika jina lake kuja katika jina langu swala la mauaji niachie Mimi naua ki intetnation hakuna atakayejua wala kuhisi kama twausika"



    Aliongea Martin kwa sauti ndogo,tabasamu la kejeli likiwa katika domo lake



    Swala hilo kwa mwanasheria yule lilikuwa jambo dogo sana akamuhaidi ndani ya masaa 48 litakuwa limekamilika



    Martin akafrah kuskia vile....



    Wakafunga kikao chao

    Na kurejea kazini....



    *************



    Moyo wake ukapasuka,kwa kutokuamini kile akisikiacho

    Lengo LA kuitwa pale alijua pengine ni kutongozwa



    Yah aliashajipanga jinsi ya kujibu

    Ukweli aliujua ndani ya moyo wake

    Fatuma



    Binti alojaliwa uzuri wa asili,macho madogo umbo namba nane

    Usikatae wito kataa maneno

    Kosa alilofanya ni kukubali kukutana na MARTIN



    Akamlaghai kwa maneno matamu na kufanikiwa kumtupa kitandani

    Akampa penzi tamu na katikati ya tendo akawakilisha ombi lake

    Ndipo moyo wa binti yule ulipopasuka



    "Na kama ukikubali hii nyumba ni Mali yako pamoja na gari ya kutembelea"



    Aliongea MARTIN huku ulimi wake ukitambaa katika mwili laini Wa binti yule....



    Akakumbuka jinsi alivyokuwa akimbembeleza JACOB kuhusu kumnunulia nyumba bila mafanikio

    Leo anapata nyumba ile ya kifahari pamoja na gari LA kutembelea

    Akazidi kupagawa



    "Na pia nitakupa walinzi ambao watakulinda bure na mshahara wao watachukua ofisini"



    FATUMA akakubali jambo lile kuiba hati zote ambazo zilikuwa ni original kwake lilikuwa ni jambo dogo kulinganishwa na utajiri atakaopewa

    Gari na nyumba



    Moyoni mwake a kumpenda kabisa JB alimpendea hela

    Alikuwa naye kwa ajili ya kumchuna bila moyoni mwake alimpenda sana kijana mmoja shombeshombe

    Alimpa kila alichoitaji

    Huu ni muda sasa wa kuishi na AMOUR

    Akajiwazia



    Mpaka anaondoka katika nyumba ile alikuwa kashaamua kumsaliti mpz wake yule



    Kazi kwa MARTIN ikabaki ndogo tu kuonana na wazee wa kazi

    Four silent killer

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wauwaji wa NNE wa kimya wasioacha ushahidi



    Makatili wenye roho mbaya zaidi ya roho ya simba au chui



    Alijua jinsi ya kukutana nao



    SHERATON PUB



    Ulikuwa ni ukumbi mdogo mziki ukipigwa kwa mbali ndani ya ukumbi huo



    wanaume na wanawake wakicheza kuendana na mziki katikati ya ukumbi huo



    Taa zilibadilika badilika rangi, kupendezesha eneo lile na kufanya washiriki wajiachie kufurahia tendo lile



    Nje kabisa ya ukumbi ule katika eneo walilokaa wanywaji katika meza moja walikaa watu wa tano wakiwa wamezama katika maongezi



    Ni MARTIN na four silent killer

    Martin akiwapa dili LA mamilioni



    Dili LA kumwangamiza rafiki yake kipenzi JACOB



    akawapa kabisa na advance ya kazi ile

    Akawapa na ramani ya eneo alilopo kijana yule



    Mambo yalipangwa yakapangika

    Vijana wa kazi wakaondoka wakihaidi usiku huo huo kufanya kazi ile ya kuichoropoa roho ya JB



    *********



    Ilikuwa ni bonge LA nyumba iliyozungukwa na ukuta mkubwa wenye nyaya za shoti juu yake!



    Ndani pembeni ya geti palikuwa na kajumba kadogo ambacho kilikuwa na walinzi wawili walijiegemeza katika ukuta na kupitiwa na usingizi

    Walikoroma



    Hawakuisikia gari aina ya tax lililopark nje wakashuka vijana wa nne wakiwa na silaha nzito kifuani



    Ilikuwa ni SAA nane usiku



    Wakalisogelea geti na kuligonga

    Walinzi wale wakakurupuka

    Na bila kuchukua tahadhari wakafungua geti



    Kitendo tu cha kufungua geti,risasi zilizofungwa kiwambo cha kuzuia sauti zikachimba vifua vyao

    Wakaporomoka chini



    Wakaisogelea nyumba ile



    Fatuma akufunga mlango

    Kama alivyoagizwa



    Hivyo ikawa rahisi kwa wazee wa kazi kuzama mpaka katika chumba kile

    Kama uigizaji binti yule alijuwa kuigiza

    Majambazi wale wakaanza kumtesa

    JB na mwisho wakamchoma kisu cha koromeo



    Baada ya mauaji Yale wakapeana 'signal' na binti yule aliye wapa makaratasi Yale ya hati ili kuaribu ushahidi isigundulike kama anausika wakamtwanga bibie yule risasi ya mguu



    Wakaubeba mwili wa jb na kuondoka nao mpaka pembezoni mwa bwawa wakautupa hapo



    Usiku huo huo



    Purukushani zile ziliwaamsha majirani waliofika eneo LA tukio usiku ule ule

    Na kuikuta TeX ndo inaishia



    Jambo lililoafikiwa ni kupiga simu polisi kabla awajampeleka binti yule hospitalini



    Aliyekuwa patroo usiku huo alikuwa ni inspekta NURDIN



    Ndo aliyepokea simu ile akiwa kituoni

    Akashtushwa na habari ile



    Alimjua fika JB



    Tajiri mkubwa ndani ya mji ule mdogo wa moshi



    Akaamua kuibeba kesi ile



    Akajivika yeye kama yeye akiwa na wenzake wawili wakaingia ndani ya gari ya polisi kuelekea eneo la tukio



    Usiku huo huo



    Wakakagua maiti zile,wakichukua maganda ya risasi zilizotumika



    "Mlisikia milio ya risasi?!"



    NURDIN alimuuliza shughuda mmoja ambaye alikana



    Akaandika katika kitabu chake



    Ni wazi aligundua bastola au silaha ilotumika ilifumbwa kiwambo cha kuzuia sauti



    Akazama ndani ambalo alimkuta mke wa jb FATUMA akiwa katika maumivu makali ya risasi huku akilia....



    "Wameondoka na mume wangu jamanii"



    Kama ni ualisia binti yule aliutendea haki



    "Wahusika hao unaweza kuwatambua sura zao?!"



    "Hapana walikuwa wamevaa kininja

    FATUMA akaongopa wakati ukweli wauaji wale sura zao zilionekana



    " je wakati walipokuwa wanampiga mumeo walikuwa wanaitaji nini?!"



    "Walikuwa wakitaja mzigo ila mwisho wakataja madawa mume Wang akakubali kwenda kuonesha mahali alipoifadhi ndo wakaondoka naye"



    FATUMA akazidi kuongopa,picha negative ikajengeka kwa wanausalama wale



    Kuwa jb alikuwa muuza madawa ya kulevya



    Wakaaidi asubuhi kumsaka

    Wakamuwaisha binti yule hospitalini



    Asubuhi mwili wa JB ukakutwa pembezoni mwa bwawa ukiwa umechomwa kisu cha shingoni

    Kwenye koromeo



    Ikawa ndo habari ya mjini



    Vyombo vya habari vikatangaza tukio lile tajiri muuza madawa auwawa na wenzake



    Kizaazaa

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Habari ile iliwashtua watu wengi sana,Fatuma alipoteza fahamu Mara kadhaa



    Huku rafiki yake wa karibu Martin akilisimamia swala hilo



    Mtu wa kwanza kushughudia mwili ule alikuwa ni inspekta NURDIN



    Yalikuwa ni mauaji ya kinyama



    KWA SEKUNDE KADHAA AKABAKI AKIKITAZAMA KISU KILE



    Kilivyoirarua shingo ya jb, Akaweka nadhiri ya kumpata muhusika,japo moyoni mwake alikuwa na uhakika kwamba JB ni muuzaji wa madawa ya kulevya kutokana na maelezo ya mpz wake fatuma



    Katika vipimo vya awali hakuna alama yoyote iliyo onekana ambayo ingeweza kumtia hatihani mtuhumiwa



    Kisu kile kilipopimwa haikuonekana alama ya vidole



    NURDIN akazidi kuchanganyikiwaa



    Ni wazi muuaji alivaa gloves



    Baada ya siku tatu mwili ule ukakabidhiwa kwa wenyewe

    Aliye kuwa mpz wake FATUMA na rafiki yake kipenzi MARTIN kwa mazishi



    Martini aliyasimamia mazishi Yale mwili ule ukafukiwa katika makaburi ya njoro



    Mali zote zikabaki chini ya MARTIN

    Akampa nyumba moja ya kifahari FATUMA



    Na ili kupoteza ushahidi akabadilisha wafanyakazi na kuwafukuza wote akaweka wapya



    SHARFIA akawa mmoja wapo wa wafanyakazi walotimuliwa

    Akajiingiza kwenye uandishi wa habari moja kwa moja



    ***********



    Ngriiiiiii ngriiiiiiiiii ngriiiiiiiiii ngriiiiiiiii ngriiii......



    Simu ya mezani iliita NURDIN akapeleka mkono wake katika mkonga na kuipachika sikioni



    "Ni kituo cha kati MAJENGO nikusaidie nini?!"



    "Sory naongea na afande NURDIN?!"



    "Yah"



    "OK afande Mimi ni jirani yake na JB na habari nzuri kwako afande"



    NURDIN akashtuka



    "Uk..oo wap....sai..v wew..."



    Akauliza kwa kigugumizi



    "Njoo uwanja wa majengo karibu na MAJENGO sec hapa"



    NURDIN akujibu kitu akajinyanyua na kutoka ndani ya kituo kile



    Kituoni na hapo shule ilipo apakuwa na umbali



    Dakika TANO aliwasili kiwanjani hapo na kutoa simu yake akapiga namba kadhaa simu ikapojelewa



    "Njoo hapa zilipo bodaboda utanikuta mi ni bodaboda nipo juu ya boxa nimevaa t shart nyekundu na jeans la bluu"



    NURDIN akachepuka kuelekea alipoelekezwa



    Alipotokeza tu akamuona kijana huyo akimjia



    "Panda twende"



    Bodaboda yule akatoa amri



    NURDIN akaigusa bastola yake ndogo ilokwepo kiunoni,Aliporidhika na usalama wake bila kuwaza Mara mbili akadandia pikipiki ile na dereva akaiondoa taratibu



    "Tunaelekea wapi!"



    NURDIN akahoji lakini bodaboda yule alikaa kimya akazidi kukanyaga mafuta



    "Nimeuliza tunaelekea wapi?!"



    Akaoji kwa ukali



    Dereva yule akaisimamisha pikipiki yake



    Akamgeukia NURDIN



    "Mimi ni raia mwema tu,jirani na anapokaa jb siku ya tukio saa nane usiku nlikuwa natoka kibaruani sasa nikawa naelekea home kulala ile nafika katika nyumba ya marehemu nje nikakuta TeX nyeupe na ghafla nikasikia vishindo kwa haraka nikachukua zile namba za gari na kuelekea kwangu nilipopiga simu polisi na baadaye mlipokuja mlikuta tayari wameshamteka marehemu"



    NURDIN alishtuka kupata maelezo Yale

    Yalikuwa ni maelezo mazito akakaa kimya kuendelea kuskiliza japo alikuwa na maswali rundo ya kuuliza



    " Leo nimefanikiwa kugunduwa inapopaki hiyo tax ndo maana nimekuchukua nikupeleke ukaishughudie"



    "Unauhakika ni yenyewe?!"



    "Na uhakika afande"



    "OK twende"



    Bodaboda yule akaiwasha pikipiki yake na kuelekea maeneo ya stendi ya MAJENGO



    Awakuchukua muda mrefu kufika maeneo Yale



    Yule kijana akamuoneshea ins tax hiyo



    "OK nashkur kwa ushirikiano wako nikikuitaji ntakutafuta"



    Aliongea NURDIN



    "Sawa afande"



    Yule kijana akawasha bodaboda yake na kuondoka



    NURDIN akaisogelea ile tax ilokuwa na tinted vioo vyote ambapo dereva alikuwa ndani yake....



    Akujali hilo akaielekezea simu yake upande wa nyuma na kuitwanga picha kadhaa,upande wa kati, kwa siri sana



    Akajongea eneo la mlango ulikuwa wazi akachungulia akamuona dereva ndani akiwa amelala akajiingiza ndani



    "Nipeleke uwanja wa mashujaa"



    Akaongea kwa sauti ya upole,akiwa kayakaza macho kwa jamaa yule



    Jamaa akuongea neno akawasha gari na kuondoka eneo lile wakaingia lami

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mimi ni afisa wa polisi Nurdin ndo jina langu naomba tuelekee kituoni"



    Alianza kuongea Nurdin sambamba na kutoa kitambulisho chake Yule dereva akatoa macho



    "Kwa kosa gani afande?!"



    "Utaenda kujua huko huko"



    "Hapana afande mi si muhalifu plz tuyamalize"



    Aliongea yule kijana huku dhahiri shahiri akitetemeka,woga ukimtawala,



    Nurdin akamkazia macho akimsoma usoni



    Hizo hazikuwa sifa za jambazi,jambazi aloshiriki katika mauaji ya kikatili kama Yale



    Majambazi ambawo awakuacha hata tone la ushahidi katika mwili wa jb

    Huyu mwoga hakuwa mmoja hapo

    Ila gari yake si ilikuwa eneo la tukio?!



    Yah pengine ni dereva wao



    Akajiwazia na kujijibu mwenyewe



    Akachomoa kakijitabu chake katika kabegi chake kadogo cha mgongoni



    "Waweza Ku park gari tujadili kwanza"



    "Sawa afande"



    Akajibu kijana yule sambamba na kuipaki gari yake pembeni ya barabara



    "Kwa jina unaitwa nani?!"



    "Kipele chaupele"



    "OK unaishi wapi?!"



    "Majengo kwamtei"



    "OK huwa unakodishaga gari yako?!"



    Dereva yule akashtuka kwa swali lile,mshtuko ulotafsiriwa vibaya na inspekta yule



    Akazidi kumkazia macho sambamba na kuikunja sura yake



    "Nd...I...i.o"



    Akaitika kwa kigugumizi



    "Ila kwa watu ninaowafahamu tu afande"



    Akaongea huku akitoa tabasamu la bandia akijaribu kutengeneza uchangamfu wa kibandia



    "Ok!"



    Akajibu NURDIN huku akiandika, tabasamu likisomeka katika uso wake ni wazi alilipenda jibu lile kwa sababu ni wazi lilimrahisishia kazi yake



    "Mara ya mwisho ulimkodishiaga nani na kwa kazi gani?!"



    "Mara ya mwisho juzi rafiki yangu Musa alikuja kulikodisha ila sijui ni kwa kazi gani!"



    MUSA alikuwa ni mmoja wa vijana wa 4 killer aliye shiriki kumwangamiza jb ndugu msomaji ok twendeleee.....



    "Lilivyorudi lilikuwa kwenye hali gani?!"



    Nurdin akazidi kudadisi Huku akiandika,mfukoni tape recordar yake ikirekodi kila kitu



    Lilikuwa ni swali LA mtego,



    "Lilikuwa s.s..a.waa"



    Dereva yule alibabaika kujibu swali lile,ni wazi jibu lake lilikuwa na walakini



    "Ukiwa muwazi kwangu sitokutesa tutaachana hapa hapa ila nikigundua unanificha ntakupeleka rumande na utafungwa hivi unajua gari yako imefanyiwa uhalifu siyo kesi ya wizi ni mauaji sasa wewe jifanye msiri kama utoenda kuisaidia polisi mpaka hayo majambazi yakamatwe"



    Jamaa akashtuka



    NURDIN akatumia mwanya huo huo kumtingisha Alishajua ni mwoga



    " kwanza naona napoteza muda wangu washa gari twelekee kituoni kule ukiteswa kidogo utasema kila kitu nakubembeleza umekuwa ndugu yangu?!"



    Insp yule akawa mkali kidogo



    "No! Afande tuyamalize tu ntakueleza kila kitu ila usije nitaja wataniua"



    Ilibakia robo Nurdin aangue kicheko

    Akajikaza!



    "Ok usijali kwa ilo nieleze"



    "Ni haidi kwanza hatutofika kituoni"



    "Of corze kama ntaridhika na maelezo yako



    " OK,afande ni kweli juzi gari yangu iliporudishwa katika siti za nyuma ilitapakaa damu japo zilifutwa ila niliweza kuzigundua"



    NURDIN akatumbua macho yake makali nyuma ya siti zile akuona cha maana akaachana napo

    Akaendelea kuandika

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Je ni nani aloikodisha?"



    Ni MUSA Rafiki yangu na tajiri kcmc anamiliki mabucha na baa nyingi"



    "Umesema ni tajiri MOSHI hii ina maana hana magari mpaka akodishe lako akafanyie uhalifu?"



    "Ana magari ila mi sijui nnachoangalia ni pesa ananipaga pesa nzuri sana''



    NURDIN akatingisha kichwa kwa masikitiko



    " Ok anakupaga sh ngapi?!"



    "Kwa usiku mmoja laki mbili na ananijazia mafuta full tank"



    "Duuu!!!"



    NURDIN akaguna akionekana wazi kushangazwa na jambo lile



    "OK unaweza kunipeleka anapoishi"



    "MUNGU wangu!,afande si ndo matatizo haya wataniua Mimi nikuelekeze tu! Uende"



    Kwa masikitiko akaongea kijana yule,inspekta NURDIN akamkata jicho



    "No! Washa gari twende"



    "Sawa afande"



    Akajibu dereva yule na kuliingiza gari barabarani kuelekea maeneo ya kcmc yalipo makazi ya MUSA



    *



    Ulikuwa ni mwendo wa dakika 15 ulowafikisha maeneo hayo ya kcmc



    Ilikuwa ni bonge la nyumba ambalo kwa nje lilizungukwa na ukuta mkubwa na geti ambalo apakuwa na shaka lililindwa na aina Fulani ya walinzi



    "Pita moja kwa moja usisimame"



    Insp akatoa amri dereva yule akatii, shida yake ilikuwa ni kuiona tu nyumba hiyo akatoe maelezo kwa bosi wake kamishna GUDLUCK SILVESTER



    Ili apewe kibali cha kuikagua nyumba hiyo na kimtia hatiani jamaa huyo

    Ikabidi warudi kituoni yule dereva alitegemea angeachiwa baada ya kutoa ushirikiano wa kutosha lakini haikuwa hivyo



    NURDIN alitambua ni wazi maisha ya kijana yule yalikuwa hatarini

    ivyo akamsweka rumande kama kumficha,na kumueleza kila kitu bosi wake yule



    "OK andaa file fatilia kesi hii mpaka uwatie wahalifu mkononi,kila kitu itabidi unieleze,na ukiitaji msaada wowote usisite kunambia



    " yas afande..."



    Akaitika NURDIN na kujinyanyua kidogo juu ishara ya heshima kwa bosi wake Yule



    Alifurahi kupewa idhini ya kufatilia kesi ile akajiondoa ofisini mule na kuelekea katika ofisi yake kwa ajili ya kuliandaa file LA kesi ile.



    Huku nyuma kamishna SILVESTER akaikwapua simu yake na kupiga namba kadhaa akaiweka sikioni

    Simu ikaita na kupokelewa na sauti nzito...



    "NURDIN ndo anafatilia kesi yenu na kaanza kwa mafanikio kamtambua MUSA muondoeni duniani Leo hii kabla mambo ayajaharibika"



    "OK mh ilo litafanyika"



    Upande wa pili ukajibu na simu ikakatwa



    'Ni nani aliye fichua siri hii'



    Akawaza MARTIN akiwa juu ya kifua cha binti mdogo,



    Ni binti ambaye angeweza kuwa mtoto wake.



    Ilo akujali,baada ya taharifa ile hamu ya tendo lile ikamuisha akajitowa na kumuacha binti yule alokuwa katika hali mbaya kihisia akishangaa

    Akajiondosha eneo lile na kuchepuka mpaka sebuleni akaketi na kupiga namba kadhaa katika simu yake



    "Dakika tano uwe umeshafika hapa home"



    Akaongea sekunde ile ile na kukata simu



    Akajinyanyua na kuelekea bafuni

    Alipotoka alimkuta alomuhitaji kakaa sebuleni



    Alikuwa kavaa koti LA laizar mkononi gloves nyeusi Jean's ya bluu raba nyekundu



    Kichwani alikuwa na kofia aina ya bushori akivuta sigara kubwa ambazo ni nadra kuonekana hapa nchini



    Alikuwa ni SAID au side kwa kifupi kama wengi walovyopenda kumuita

    Mmoja wa wauaji wa 4 killer's

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MARTIN akiwa kavaa taulo

    akaisogelea friji na kuifunguwa akatoka NA chupa ya whisky akaiweka mezani



    Side akatabasamu



    Ndiyo



    Ni kinywaji akipendacho,naye MARTIN aligusa mahala pake



    Akarudi katika friji na kuchukua nyingine na glass yake Akaketi,na kujimiminia kiasi kidogo baada ya kuifungua chupa yake Akapiga funda moja



    Akakohoa kidogo kusafisha koo



    "Kwa jumla mko wa nne,ila kwa sasa rafiki zenu wawili walistaafu kazi hii ya uhalifu na sasa wanalinda kwa marehemu JB,wakipokea mshahara mnene niwalipawo kama ahadi kwa mjane wa marehemu bi FATUMA baada ya kutusaidia kwa kazi yetu"



    "Nakumbuka nawe uliitaji kazi!,kusudi uachane na ujambazi yah kazi imepatikana ikiwa utanifanyia kazi"



    Aliongea MARTIN kwa sauti ndogo,sauti ya kusisitiza,side akatabasamu



    Tabasamu LA kutokuamini kile akisikiacho,ila MARTIN akaendelea



    "Naitaji uwe bodyguard wangu ikiwa utafanikisha kumwangamiza MUSA"



    "What?!!!!"



    Side alitoa macho ya mshangao,akapaliwa kidogo.

    Ni wazi akuamini kile akisikiacho

    MARTIN akacheka



    Cheko LA dharau kisha akaendelea kutoa ufafanuzi



    "Na ikiwa tusipofanya hivi,tutaumbuka sote MUSA ni mzembe sijui nini kimetokea anasakwa na wanausalama so naitaji mpigie simu ujue yupo wapi ukammalze si ombi ni amri

    Martin akiwa na USO wa ghadhabu hasira za wazi akaongea na kujinyanyua akapiga hatua moja kuondoka na ghafla akageuka....



    " rafiki yangu kamishna kanipigia simu kunijulisha kuwa kesi hii kakabidhiwa insp NURDIN na kampa idhini akamkamate MUSA baada ya kuridhika na ushahidi kuwa anausika katika mauaji akikamatwa akateswa atatutaja hivyo auwawe kabla mambo hayaja haribika akakamatwa akaingia katika vyombo vya dola"



    "Bosi kwa nini tusimwangamize huyo inspekta?!"



    "Tutazidisha upelelezi kwa makachero,hasira juu yetu itaongezeka bora na huyu tutazidi kumpa ugumu insp huyu kutufatilia dakika TANO kutoka sasa naitaji nipokee simu yako habari mbaya kutoka kwa MUSA kabla ajaingia mkononi kwa huyo insp"



    Akamalizia MARTIN na kuondoka eneo lile



    Side akajinyanyua alishaamua kumwangamiza rafiki yake



    " upo wapi best na shida na wewe "



    "Nipo home"



    "Poa naja"



    Akakata simu na kuidandia pikipiki yake Akatoka kwa speed kuelekea kcmc anapoishi MUSA



    Muda huo qruzer yenye maaskari wa kutosha wenye silaha nzito za kivita ilikuwa barabarani ikielekea huko huko kcmc wakiwa chini ya insp NURDIN





    Japokuwa MUSA alikuwa ni tajiri na mwenye miradi ya kutosha hakuwa na mtoto wala mke



    Wengi walichukulia kama Yale ni masharti alopewa na mganga wake lakini hiyo haikuwa kweli



    Bado alihitaji kula ujana



    Alibadilisha wasichana Kama nguo leo yupo na huyu kesho Yule ndo ilikuwa 'life style' yake



    Jambazi sugu lililojiamini



    Akuitaji ulinzi wa kutosha



    Alikuwa na kijana mmoja tu alomfundisha kushika silaha na kumpachika hapo getini akimjengea kijumba chake



    Leo hii akiwa sebuleni kwake akiangalia tv ghafla simu yake inaita anaicheki na kuibandika sikioni



    "Aloo! Swahiba"



    Akaongea kwa sauti ya upole akiachia tabasamu la mbali



    "Upo wapi best na shida na wewe"



    Upande wa pili akauliza kwa sauti ya mkwaruzo



    "Nipo home"



    Musa akajibu



    "Poa naja"



    Upande wa pili ukamalizia na simu ikakatwa



    Alikuwa akiongea na rafiki yake kipenzi SIDE



    Hakika akujua dhumuni la rafiki yake yule ambaye muda huo alikuwa njiani akija kwa lengo moja tu

    Kumuondosha duniani

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndiyo



    Side aliwasili katika jumba lile na kupiga honi Mara moja mlinzi akafungua geti baada ya kumchungulia na kumuona ni yeye



    Tofauti na mategemeo yake baada ya SIDE kushuka akamsogelea,mlinzi yule akamsubiri akijua kuna kitu alitaka kumwambia



    Kosa!



    Kwa wepesi wa ajabu side alimrukia na kumkaba kwa mkono mmoja mkono mwingine akauingiza mfukoni kwake na kutoka na kitambaa kama kianjifu

    Akampachika nacho puani



    Kwa sekunde kadhaa,akamshusha taratibu chini



    Akamvutia ndani ya kajumba chake na kumuacha huko



    Akaelekea upande wa nyumba ile na kuingia ndani



    Akamkuta MUSA bado yupo sebuleni akiangalia runinga



    Akakaribishwa vizuri izraeli huyo

    Wakaendelea na story za kawaida

    Wakati wakiendelea na stori ghafla side akachomoa bastola yake ndogo yenye kiwambo cha kuzuia sauti akamtandika risasi kadhaa za kifuani

    Akumpa muda hata wa kusali sala zake za mwisho



    MUSA akuweza kupiga hata kelele palepale kwenye kochi akiwa katoa macho akatulia tuli



    Damu zikitapakaa eneo lile

    Baada ya side kumaliza kazi ile kwa kupitia mlango wa nyuma akatoweka eneo lile



    Akijua ajaacha ushahidi wowote wa kumweka pabaya



    Alijidanganya



    Robo saa baadaye gari ile ya maaskari ilombeba insp NURDIN iliwasili katika nyumba ya MUSA



    Maaskari wale wakashuka kijeshi

    Na kuizunguka nyumba ile

    Wakapigwa na butwaa baada ya kukuta geti lipo wazi



    Walipoingia tu ndani katika kijumba cha mlinzi walipokelewa na maiti

    Mlinzi yule damu zilimtoka puani

    Umakini ukaongezeka baina yao

    Wakajipanga



    Kuna waliobaki nje,kuna walioizunguka nyumba ile na kwa kunyata wengine wakasogelea mlango mkubwa wa kuingilia ndani



    Walipozama ndani wakapokelewa na maiti ilolala kwenye kochi iloonesha wazi imetandikwa risasi kadhaa kifuani

    Awakupata tabu kutambua maiti hiyo ni ya MUSA



    Macho ya NURDIN yakaangaza eneo lile kwa sekunde kadhaa akisanifu uzuri wa sebule ile kisha yakatua katika mwili wa kijana pale kwenye kochi

    Akamsogelea na Kumwangalia kwa ukaribu



    Mapigo yake ya moyo yaliongeza kasi ya upigaji



    Alijua ile kesi si rahisi kama alivyoufikiria



    Katika kumkagua yule maiti akaibuka na simu mfukoni kwake

    Ndo kosa alilolifanya said



    Kutokuondoka na simu ile wakati alijua fika yeye ndo aliwasiliana na Saidi kwa Mara ya mwisho



    Kosa ambalo lilimgharimu na kutompa muda wa kulitafakari kipi cha kufanya

    Martin akapigia simu ambulance dakika chache ikawasili na kuichukua mwili ule kwa uchunguzi zaid



    Inspekta NURDIN akutaka kubanduka hospitalini



    Alitaka kuifatilia kwa u karibu kesi ile

    Ghafla akashtushwa na mvurumisho wa sauti



    Akaingiza mkono wake na kuuchomoa simu yake

    Akashtuka baada ya kuonana mpigaji ni bosi wake



    " umefika wapi katika kesi hiyo afande"

    Kamishna SILIVESTAR akaoji



    "Musa amefariki bosi?!"



    "What?!!!"



    "Yah mkuu tumefika katika nyumba yake tumekuta mizoga miwili wake na wa mlinzi wake miili ndo ipo hospitalini kwa uchunguzi"



    "Ooh down sheet!,umegundua nini afande"



    Mkuu wake yule akahoji akijifanya kushtuka



    Kumbe ukweli aliujuwa



    "Nimefanikiwa kupata simu ambayo nimeona meseji za mwisho alizo chat na jamaa mmoja aitwaye side na kumjulisha kuwa anakuja nyumbani kwake kwa vyovyote anahusika mkuu na lazima atiwe nguvuni"



    Mapigo ya moyo ya mkuu yule wa jeshi la polisi yakaongeza kupiga

    Baada ya kukataa simu akamtwangia swaiba wake MARTIN



    "SIDEVni mpumbavu kama huyo aliye mwondosha duniani naye inaitajika aa ngamizwe"



    Martin akashtuka



    "Kosa lake ni kumuachia simu marehemu hali ya kuwa anajua alichat naye muda mfupi,kijana wangu yupo mbioni kumkamata na kabla ajamkamata naitaji ili muwe salama naye apotezwe"



    Ikumbukwe ndugu msomaji,kamishna yule kila hatowapo habari akaunti yake inatuna



    Baada ya kukataa simu,akaachia tabasamu akimsikitikia insp NURDIN

    Upande wa pili MARTIN muda ule ule akapiga namba kadhaa na kuibandika simu yake kimapenzi



    "Vipi beby nakuomba muda huu ofisini"



    "Poa mpz naja"



    Simu ikakatwa



    Na nusu saa mwanamke mrembo mwenye umbo namba nane aliwasili katika kampuni ile baada ya kuonana na katibu muhtasari wake akaruhusiwa aingie



    Akaenda kuketi akimwangalia Martin kwa jicho La tamaa



    Jicho lililolegea kama kala kungu manga



    Mdomo akaung'atia kidogo



    Ni wazi alikuwa akiitaji kitu



    MARTIN alilitambua hilo.



    Akamsogelea pale alipokaa,akampa mkono binti akaushika na kunyanyuka MARTIN akamvuta



    Binti yule akadondokea kifuani kwake

    Martin akapeleka ulimi wake katika sikio LA binti yule



    Binti akatoa mguno hafifu wa kimapenzi



    Akaanza kuhema kwa shida.



    Binti yule akadondokea kifuani kwake,

    MARTIN akapeleka ulimi wake katika sikio la binti yule

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Binti akatoa mlio hafifu wa kimahaba

    Akaanza kuhema kwa shida



    MARTIN akampa ulimi binti yule akaupokea.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog