Search This Blog

USIKU WA KAFARA (ROAD TO 2017) - 5

 







    Simulizi : Usiku Wa Kafara (Road To 2017)

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Diana alikuwa mgongoni kwa gola hivyo wakati gola anaanguka chini walinguka pamoja huku ule mwili mzito wa hayati gola ukimlalia diana.

    Kisu kikaanguka karibu na kile kitufe ambayo ni kinga ya viumbe hawa .



    Sarah hakuamini alishuka kwenye gari huku akiukodolea macho mwili wa gola huku akimuona diana akijitoa chini ya mwili ule ....



    Kabla hajaenda kumsaidia ghafla akaliona kundi la washirikina wakija mbio wakiongozwa na yule kizee mkongwe malikia wa viumbe vile...



    "Tunakufa ...dada chukua hicho kisu ukichome hicho kitufe ukipasue" Diana alipaza sauti kumwambia sarah .



    Sarah haraka bila kujiuliza akachukua kile kisu kisha kwa nguvu zote akakichoma kile kitufe kika pasuka na kumwaga damu nyeusi ..na muda ule ardhi ilitikisika huku wale washirikina wakianguka chini na yule kikongwe akikumbwa na udhaifu akaanguka chini..



    Sarah hakuamini anachokiona akahisi yupo ndotoni!



    "mama...." diana alijikuta akitamka huku akipiga hatua kwenda kwenye lile kundi la washirikina waliokuwa hawa jiwezi...



    Diana hakuamini! kumbe hadi mama yake alikuwa ni mmoja wa wanachama wale

    "mama umefikaje huku na mbona upo kwenye sale zao" diana aliongea huku akilia sana akimtazama mama yake aliekuwa chinitaabani...



    Sarah akawa yupo kwenye mshangao ....



    *********;*************************



    Kule pangoni hatimae dolla nae aliaga dunia na hapo uhai wake ukaangukia kwa gunzani

    Gunzani aliinuka kwenye jiwe mwili wake ukiwa umerudiwa na uhai pamoja na nguvu...



    Aliporudiwa tu na uhai hisia zake zilimuonesha wenzake wapo kwenye matatizo...



    Gunzani akatoka nje kwenda kuwasaidia wenzake...



    Sarah akiwa pale akimuangalia diana akimlilia mama yake ghafla akamuona mtu akiibuka kutoka mstuni akiwa ni mrefu kuliko hata gola .....alikuwa ni gunzani



    "Wewe ondoka hapo" sarah alipaza sauti huku akijaribu kumfyatulia risasi gunzani lakini bunduki ilikuwa imeisha...



    Diana alishtuka na kuanza kukimbia lakini alichelewa ghafla alinyakuliwa hewani...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lah. huyu gunzani alimnyakua diana kama kifaranga kinavyo nyakuliwa na mwewe.....



    Sarah alikimbia kwenye gari ambalo likuwa na halijazima akatupia kisu na bunduki ndani ya gari kisha akiliondoa gari kwa mwendo wa ajabu akikikimbia kifo....



    ******-*



    Gari ilikuwa kwenye mwendo usio wa kawaida huku sarah akizidi kuchochea speed ,gari ikawa katikati ya barabara ikijaribu kuuacha msitu wa kifo...



    Ghafla kwenye kona sarah aliona gari nyingine ikija upande wake nayo ikiwa speed akajaribu kukanyaga blek kwa nguvu huku akikata kona....



    Sauti ya msuguano wa gurudumu (tire) na rami ikatawala eneo lile ,gari aliondesha sarah ikaburuzika na kuacha bara bara na kwenda kuu gonga mti kwa kishindo....





    Ilikuwa ni kishindo kikubwa kilichopelekea sarah kupiga kichwa chake kwenye kioo na kupoteza fahamu ,huku gari lake likifuka moshi mzito mweusi..



    Ile gari nyingine iliyo koswa koswa kugongwa na sarah gari ya sarah ilikuwa ni gari ya polisi ,polisi ambao walipewa taarifa na kampuni la kusafirisha watalii kuwa kuna gari imekwama mstuni...



    <<<<<<<<

    Kila gari la kampuni hili la kusafirisha watalii hua zina fungwa GPS ambayo huwa tambulisha hatua kwa hatua kila zinapo enda gari zao...Gps hiyo huwa julisha viongozi wa kampuni popote gari ile sehemu ilipo.



    Hivyo watu wa mitambo waliweza kuiona gari ya dereva wao baraka kupitia mitambo yao ikiwa imesimama katikati ya msitu kwa muda mrefu na haikuwa na dalili ya kuwashwa..

    Hii ili maanisha gari hii inamatatizo kwani walipo piga simu ya baraka iliita bila kupokelewa..



    Haraka uongozi wa kampuni wakafikisha taarifa kituo cha polisi kilichokuwepo bagamoyo na kuwasihi waifuatilie gari ile iliyo kwama katikati ya msitu ikiwa na watalii watano kutoka ndani ya nchi...



    Haraka gari yenye polisi kumi wakiwa na siraha za moto ikaondoka ikiwa mwendo wa mkali ikielekea sehemu walipo elekezwa...



    Gari yao ilikivuka kijiji cha mvila huku wakiwa kwenye mwendo mkali, ghafla kwenye kona kali walikutana gari jingine nalo ikiwa kwenye mwendo mkali zaidi ys wao...dereva wa gari ya polisi alihamanika huku akishuhudia gari iliyo endeshwa na msichana ikipoteza muelekeo na kutoka barabarani na kwenda kugonga mti......>>>>>>>>>>>>>



    Kumbe sarah alikuwa ameendesha gari kwa umabali mrefu sana na bila kupata ajali basi angeingia kijiji cha mvila.



    "Ah wazee hii ndo hii gari tulioambiwa tuifuatilie" afande mmoja alipaza sauti huku akiimulika ile gari kwa kurunzi yenye mwaga mkali...

    "kweli mpakieni kwanza huyo demu kaaumia vibaya tumuwahishe hosptal" mkubwa wao aliongea ,wakasaidizana kumtoa sarah kwenye gari akiwa hajitambui kabisa ,wakampakia kwenye gari yao wakageuza kurudi bagamoyo...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sarah alifikishwa hosptalini akapokelewa na kupelekwa wodini kupata huduma ... na taarifa hii ikafikishwa kwa meneja ya kampuni ya utalii ilio muajili hayati baraka..



    Sasa ikawa polisi wana jadiili kwani walijua huko mstuni kutakuwa na matatizo kwani kwa mwendo aliopatanao ajali sarah ulionesha kuna kitu alikikimbia huko alipo waacha wenzake.



    Polisi wakaamua kuongeza nguvu ikabidi waondoke na gari mbili huku wakiwa polisi ishirini na mbili...

    Safari ikaanza kuelekea eneo la tukio...



    1 january (1/1/2017)



    Saa kumi alfajiri.....



    Kundi la askali lilifika eneo la tukio ndani ya msitu ulionuka damu wakiwa na siraha zao wakitembea mwendo wa tahadhari ndipo walipo anza kukutana na maiti kila eneo

    kwanza waliona zile maiti za washirikina na wa livyo zidi kutafuta wakafanikiwa kuuona mwili wa kijana shupavu akiwa kalala kwenye dimwi la damu nae alikuwa ni gadyson...



    Katika maiti zote zilizo onekana maiti ya gola haikuonekana wala yule malikia kikongwe ..



    "jamani kuna mmoja mzima" polisi mmoja alipaza sauti akiwa kachutama mbele ya msichana diana alielala chini..!!!

    Polisi wote wakamsogelea wakiwa na hamu ya kujua nini kilimtokea msichans yule ....



    "Nini kime wakuta binti" kiongozi wa polisi hawa aliumuuliza diana baada ya kuona angalau anaweza kuongea japo kwa sauti dhaifu...

    "Ni maharamia wamefanya haya ...walitukamata kijijini usiku "diana aliongea huku akiwa omba wampeleke hosptali kwani hali yake sio nzuri...maelezo yake yakiwa hayajitoshelezi

    "Askali saba mchukueni mpelekeni kwenye gari mumuwaishe bagamoyo kwenye hosptal tulio mpeleka mwenzake..



    Haraka diana akachukuliwa na kupelekwa ndani ya gari , safari ya askali saba wakimuwaisha diana hosptal ikaanza.!!!



    Diana alipona vipi wakati jana usiku alikamatwa ns gunzani?????......



    Rejeaa ...jana usiku..



    Gunzani alimkamta diana kwa hasira akiwa kafura muda huo diana alipiga kelele za kuomba msaada..

    "Gunzani wamemuuwa gola hawa binadamu wabaya waue wao na rafiki zao " yule kikongwe aliongea kwa sauti ya kukoroma huku akilia ....muda huo huo gunzani akanyonga shingo ya diana na kuivunja ..pale pale diana akapoteza uhai wake kwa kudhurumiwa...



    Kisha gunzani akaufukia chini ya ardhi mwili wa diana ...kisha akambeba yule mzee pamoja na maiti ya gola...akawahimisha eneo lile kuwapeleka sehemu nyingine....



    "Wewe peke yako ndo umebakiwa na nguvu sisi ni wadhaifu nenda kawauwe wote wanaoshirikiana na yule msichana alie pasua kinga ya uhai wetu" ni maneno ya yule bibi kizee yaliyo penye kwenye sikio la gunzani mwenye ghadhabu....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gunzani kwa hali ya kuto tarajia alijigeuza na kuchukua umbo la dianâ pamoja na sura ya ya diana!!!..

    "Naenda kumuua yeye na rafiki na jamaa zake "Gunzani aliongea akiwa kwenye umbile la diana.........



    >>>>>>>>>>>>>>



    La haula!!!!! yule diana walimchukua wale askali alikuwa ni kiumbe gunzani ndani ya mwili na surah ya diana na walikuwa wanampeleka kwenye hosptal alio lazwa sarah..



    MWISHO





0 comments:

Post a Comment

Blog