Search This Blog

SENDAYE (MALKIA WA MOYO WANGU) - 3

 







    Simulizi : Sendaye (Malkia Wa Moyo Wangu)

    Sehemu Ya Tatu (3)







    "Hii ni oda kutoka kwa mfalme,mkuu anajua kila kitu na ndo alotutuma tuje kuwachukua haya ongozeni"



    "Hapana mwii! Lazima tuwa ambatanishe na wenzao wote tuwapeleke kwa mfalme....



    Kina Dani walisikia kila kitu , Ambrose akachomoa bastola alokuwa nayo katika kikundi kile cha watafiti walikabidhiwa bastola moja ya kujilindia dhidi ya wanyama wa kali



    Ivyo Ambrose alijua muda Wa kuitumia ndo ule akaielekeza mbele!



    " haaaaaaaa!"



    Wanafunzi wote wakashtuka!



    "Unataka kufanya nini?!"



    Isack mmoja wapo wa watafiti wale akauliza akimwangalia Ambrose kwa macho makali!



    "Lazima tuwaue hawa kusave huu mchezo kabla mambo ayajaharibika"



    Akawa ambia wenzake na palepale bastola yake ikacheua na walinzi wale watatu mashujaa Wa kijiji kile wakaporomoka chini!



    Ndipo walipojitokeza!



    "Mmefanya nini sasa mmekuja huku kuua au kutafiti?!"



    James aliuliza kwa hasira akiiangalia ile mihili ya walinzi wa wale



    Vijana wale wakatazamana kwa mshangao!



    "Huyu vipi sa unadhani wangekufikisha kwa Omoti wewe ungepona?!"



    "No body kwani mnadhani mkigundulika mmeua tena walinzi majemedari Wa kijiji mtapona nyinyi?!...."



    James akazidi kuwalaumu wenzake badala ya kuwashukuru kwa kumsaidia



    "Si mpaka tugundulike kwel we jamaa una hata shukrani tungekuacha tu wakufikishe kwa mfalme ukaonje joto ya jiwe!"



    Ambrose akionekana kukwazika akajibu kwa hasira!



    "Sasa cha kufanya bila shaka imayani hawajui kilichotokea itatubidi turudi mpaka himayani tukijifanya amna kilichotokea and then usiku tutakutana tujue kipi tutafanya....



    James aliongea kwa kujiamin katu hakujua kama wale vijana walitumwa na mfalme , yeye kufumaniwa kwake alijua walinzi wale walikuj kuwinda kwa bahati mbaya ndo wakaonekana



    " kwa ushahuri Wangu msirudi himayani tafuteni njia muondoke mfalme lazima hatakuwa amejua kila kitu!...."



    Sendaye akawapa ushahuri kwani aliionekana wazi kuwaonea huruma

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Amejua kila kitu kwani yeye ni Mungu kujua ya siri?!,au nani kamwambia?!,cha kufanya we rudi nyumbani jifanye ujui chochote nasi tutarejea samahani kwa yote yalotokea!"



    James akazidi kuongea akipuuza kila ushahuri alopewa, aliya amini sana mawazo yake



    Sendaye naye baada ya kufikiria kidogo akajua pengine Ni kweli mfalme wake ajui chochote na walinzi wale walikuja katik kuwinda alisahau kabisa alipoambiwa kwamba wametumwa Na mfalme kwanza aliwaza mfalme awatume yeye amejuaje mpaka awatume walinzi waje porini?!



    Wazo kwamba mke Mkubwa aliona kila kitu na kwenda kumweleza mume wake ambapo ndo alipotuma walinzi alikwepo kabisa katika kichwa chake!



    Akaombwa atishwe kuni zake



    James akamtwisha, wakaagana



    "Sendaye..."



    Ghafla James akamuita , Sendaye akageuka



    "Sendaye malkia Wa moyo wangu! Ahadi yangu unizalie kichuna wangu..."



    Sendaye akaganda!



    "Isaki!!!!!!!?"



    Akatamka kwa sauti ya taratibu pasina kuamini kile akionacho , kauli ile Isaki wake alipenda kumwambia kila Mara

    Ila sura ile aikuwa ya Isaki wake!,akahis pengine ni mawazo yake tu na sauti ile aikutoka kinywani mwa James akataka kutamka kitu



    Akaishia kutabasamu baada ya kuona wenzake na Jemes wakiwatazama kwa mshangao akageuka na kuendelea na safari yake huku nyuma James akaruka kwa furaha!



    *Laiti angejua?!*



    ******



    Sura ya pili



    Mfalme alitoa macho ya mshangao pasina kuamini kile akionacho

    Ni baada ya kumuona Sendaye akiwasili na mzigo Wa kuni akazibwaga chini



    Macho yake ( mfalme) yakatua katika nguo fupi alizovaa mke wake



    Zilichafuka kwa vumbi na hata mapajani kulijaa vumbi!



    Sendaye ilo alilisahau!



    Mfalme pasina kuongea kitu akajinyanyua kwa hasira mithili ya Simba aloraruliwa



    "Yaaaaaaaaaaaaaaaaaa.....



    Akaachia ukelele na kumvaa Sendaye akakishika kichwa chake na kukigonga ukutani kwa nguvu!



    sendaye aliachia yowe moja akadondoka chini!,macho kayatoa Pima damu zikimtoka kichwani , puani masikioni



    " mnasubiri nini naitaji hao watu hapa wakiwa hai au maiti.....



    Mfalme akakoroma



    Walinzi wote wakatok na mikuki ,upinde ngao na mishale Ni kama walikuwa wakienda vitani!



    Njia walokuwa wakielekea ndiyo hiyo hiyo Watu wale walokuwa wakijia!



    Bila shaka wangekutana njiani;



    Bado mfalme halikuwa na hasira kwa kuwa aliapa kumuua mke wake kwa mikono yake mwenyewe akupindisha wazo lake!



    Akawaita wake zake wawili katika uwanja Mkubwa Wa nyumba yake ile!



    "Hiki ninachokwenda kumfanya huyu Malaya itakuwa fundisho kwenu pindi mtakapofikiria kunsaliti sijui kama ni mzima au maiti kama Ni mzima huu mkuki ntakaomchoma utauondosha uhai wake na kama kashakufa kwa kumgongesha ukutani basi namuua kwa Mara ya pili mi ndo Omoti nakubadilikia pale utakaponsaliti"



    Mfalme Omoti aliongea akiwatazama wake zake kwa zamu kama kuwapa onyo au fundisho!



    "Nadhani mnajua Ni kwa kiasi gani mi nilimpenda huyu mtoto ila yeye wa kutoka na wagenii?!....



    Uchungu ukazidi kumpanda mfalme akaunyanyua mkuki juu na kuushusha kuelekea kifuani kwa Sendaye!



    " yaaaaaaaaa....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Huku akiachia yowe kama munkari kwa kile afanyacho!....



    *kah bado moto mkali!,nini kitaendelea katika riwaya hii je huu ndo mwisho Wa Sendaye na vipi kuhusu watafiti wale nini hatma yao?!....



    Macho yalimtoka mfalme Omoti alidhamiria kuua,hakuwa na mzaha juu ya hilo



    Akaunyanyua mkuki wake juu ile anaushusha.....



    "Acha mfalmeeee achaaaaaaaa"



    Akasikia sauti kutoka kwa mshauri wake , tena mshahuri wake mkuu amsikilizaye zaid ya mtu yoyote pale pale akastop macho yakimtoka Pima!



    Akamwangalia mshahuri wake yule kwa maana ampe sababu ya kumsitisha zoezi lake lile,naye mshahur akaanza kueleza sababu ya kumstopesha....



    "Mtukufu mfalme nimefikiria ni kweli mkeo Mkubwa kakwambia juu ya kumuona Sendaye akikisaliti na mtu mweupe.....



    Sendaye akatoa macho kwa mshangao kutokuamini kile akisikiacho mshahuri akaendelea...



    ....lau ingekuwa kweli lazima wale walinzi wangerudi na Sendaye na wale watafiti hapa lakini imekuwa tofauti malkia Sendaye kama ulivyomtuma karejea na kuni zake kabla ujatoa hukumu ungesubiri vijana ulowatuma warejee tupate uhakika ni ilo tu mfalme wangu!"



    Mfalme akafikiria kidogo akatingisha kichwa kuafiki kile alichoambiwa akamwangalia Sendaye kwa macho makali....



    "Wewe wa kunsaliti Mimi?!....."



    "Na nani mume Wang kwa nini wataka kunihukumu pasina kosa mwenzako nimekukosea nini mfalme Wang mpaka uniadhibu hivyo.....



    Sendaye aliongea huku machozi yakimtiririka



    Moyo wa huruma ukamvaa mtemi Omoti akamwangalia malkia wake kwa sek kadhaa kabla ajautupa ule mshale wake chini kwa hasira na kugeuka akaelekea panapo kiti chake cha enzi na kuketi!



    Sendaye akageuza kichwa kumwangalia mke Mkubwa kwa chuki,mke Mkubwa akaachia tabasamu la kumdhihaki!



    " Odobeeeee,...



    "Mfalmeeeeeee"



    "Mwakiiiiiiiiii"



    "Mfalmeeeeeeeee"



    "Mpaka sasa vijana niliyewatuma kina Mwizakiii,Isagooo,na twikas awajarejea walinzi wengine niliowatuma nao awajarejea naombeni mumchukue huyu mwanamke mkamfungie chumbani mkae hapo nje kumlinda asitoroke wakati tukisubiti hao wajeeee....



    " sawa Mfalmeeeeeeeee"



    Vijana wale wakamnyanyua Sendaye aliyezidi kulia wakamuingiza ndani na kumfungia...



    ****



    Kundi lile la walinzi lililotumwa na mfalme Omoti lilizidi kusonga mbele pasina kujua mbele yao vijana wale nane walikuwa wakija wakiwa katika mabishano makali!



    Kwa kuwa hali ya hewa ilikuwa ya utulivu,iliwezesha sauti kupaa na kuwafikia walinzi wale walokuwa takribani kumi



    "Tulikwambia lakini James chanzo ni wewe ikitambulika tumewauwa wale vijana wa tatu unategemea nini itakuwa hatma yetu...."



    Walinzi wale wakashtuka! Wakasimama na kuangaliana



    "Kina mwizakiii wamekufa?!"



    Misago alo onekana kuwa ndio kiongoz wao aliongea kwa kunong'ona ila kijana mwingine akajibu!



    "Tujifiche bila shaka wanakuja huku!"



    Wote wakakimbia na kujificha!



    ***



    Watafiti wale walizidi kusonga pasina kujua mbele wanasubiriwa na kundi la walinzi na kila waongeacho kilisikiwa!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nani atajua kwamba tumewaua hao vijana!,itajulikana wameliwa na wanyama na sisi tutaendelea na utafiti wetu kama kawaida"



    James alijibu kwa kujiamini!



    "Huku ukiendelea na mahusiano yako na mke mdogo wa mfalme kama kawaida yako!"



    Ambrose alikuwa rafiki yake Mkubwa akamuuliza kwa kumdhihaki,pasina kujua kauli yake ile iliwafanya walinzi wale washike mdomo kwa mshangao pasina kuamini kile wakisikiacho!



    "Aswaaaaaaaaaaaaaaa!,nampenda sana Sendaye tena sana na lazima tuondoke naye siku.....



    Kabla ajamaliza kauli yake akashangaa watu wakichomoka vichakani na kuwazunguka



    Mishale na upinde ukiwa katika mikono yao!



    Daniel akachomoa bastola ila kabla ajafanya kitu mkuki ukatua kifuani kwake akadondoka bastola ikimponyoka! Na kudondokea upande wake



    Kijana mwingine alotambulika kwa jina la Franciss kwa uoga akataka kukimbia naye kabla ajafika mbali mshale wa mgongoni ukamuangusha na kufia palepale



    " wote kaeni chini!"



    Misago aloonekana kuwa ndiyo kiongozi wao akatoa amri baadhi wakakaa akiwemo James ila watatu wakasita katika watatu wale mmoja alionekana kuitazama ile bastola wazo lililomjia ni kuifata kwa kuwa haikuwa mbali na aliposimama



    Alijidanganya!



    Ile anaruka kitendo cha kutua chini hakuwa na uhai tena wale wawili wakakaa chini upesi



    Tayari wenzao watatu walisha wapoteza,tena mbele ya macho yao



    Watano wale walobakia walishindwa kuvumilia kulia wakimkata jicho James ambaye alionekana kutojali!



    "Tumesikia kila kitu mlichokua mnaongea na atutowaacha wazima inoma,...



    Kijana mmoja akainama ishara ya kuitika



    Isyaka....



    Naye vile vile akainama



    Muga....



    Naye vile vile akainama.....



    Njoooni mbele



    Wote walotajwa wakasogea mbele



    " chaguen watatu mtakao enda msitu pande mkaisake miili ya kina

    Mwizak na wenzake walouwawa na Hawa na akyanan mfalme wetu atawatafuna nyinyi wazima wazima kila kitu mlichosema tutamwambia....



    Vijana sita wakatoka kuelekea msitu pande wanne walobakia wakiongozwa na Misogo akiwa kaishika bastola ile pasina kujua inatumikaje wakaanza kuwaswaga vijana wale wakiwalazimisha waibebe miili ya wenzao!



    Safari ya kuelekea kwa mfalme Omoti ikafatia mioyoni mwao wakiadhimia kumweleza mfalme kila kitu!



    Walikijua kichwa cha mfalme wao!

    Asingewaacha wazima!



    09



    Baada ya jopo lile la watafiti akiwemo James kuwekwa mikononi mwa walinzi wa mtemi Omoti wakiongozwa na Misogo safari ya kurudi kijijini ikaanza!



    Ilikuwa ni safari ngumu ila hatimaye walifika kwa mfalme ambapo walikalishwa chini



    "Eheee kina Mwizak wako wapi?!...."



    Mfalme aliuliza huku akiangalia barabarani upande ambao kina Misogo walitokea!



    "Mwizaki na wenzake wameuwawa na hawa wageni baada ya kuwafuma wakiwa na malkia ndo tumewatuma wenzetu wakaitafute miili yao msitu pande.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " unasema?!,yani unataka kunambia ni kweli malkia wangu amensaliti?!....



    Mfalme aliuliza kwa hasira macho akimtumbulia James aloweka kichwa chake chini kwa kiburi!



    "Wewe wa kunichukulia mke wangu?!....



    Mtemi Omoti alitamka akichukua upinde toka kwa mlinzi wake na kupiga hatua kumsogelea James!



    " ntakuua kifo kibaya sana iwe fundisho kwako na kwa wapumbavu wenzako....



    Mfalme alizid kuongea huku akizidi kusogea mpaka akamfikia ila kabla ajafanya kitu akasikia sauti nyuma yake



    "Ewe mfalme wangu! Punguza hasira ili iwe fundisho Ni lazima jambo hili lifanyike kesho asb katika viwanja vikubwa vya misoga tena wanyongwe mpaka kufa!...."



    Mtemi Omoti akafikiria kidogo huku akikuna midevu yake mingi kisha akaunyanyua mdomo wake taratibu....



    "Na adhabu hiyo aitowahusu hawa tu!,itamuhusu pia na Sendaye mwanamke nilompenda,mwanamke nilompendelea zaid hata ya wana wake zangu wengine wanaontwii ila kumbe Senda ni nyoka chui alojitwisha ngozi ya kondoo juu ya ngoz yake ya chui asitambulike hii itakuwa fundisho pia kwa wake zangu wawili walobaki"



    Watu wote walibaki kimya,hakuna ambaye aliwah kumuona mfalme akiwa kachukia namna ile!



    Akaamrisha shimo lichimbwe miili ile mitatu ifikiwe na watano wale walobakia wakafungwa tena ndani ya chumba kimoja kusubiri kesho hukumu yao



    "Pa pa paaa paaaaa paaaaaa paaaaaaaa paaaaaaaa paaaaaaaaa lamgambo likilia jamani kuna jambo wanakijiji wote kesho asb mnaitajika kiwanja kikubwa cha kijiji na mfalme bila kukosaaaa mtu yoyote



    Paa paaaaaa paaaaaaaa paaaaaaaa paa pa pa paaaaaaaa watoto, wababa,wababu, wabibi ,wamama, wakaka wadada kesho ndo kesho kiwanja kikuu cha kijiji pale kwa mfalme mwaitajika mfikeee woteeee bila kukosa mwambie na mwenzako mbiu ya mgambo imepgaaaaaaa"



    Kijana mmoja alisikika mtahani akipiga ngoma huku akitoa tangazo ilo mtaa kwa mtaa!



    Mambo yalikuwa yameiva kivipi sasa wangepona?!



    ****



    James na wenzake wakiwa katika chumba kile kitupu sasa matumaini ya kupona katika mdomo wa nyoka yule mtemi Isike yaliyeyuka kama barafu!



    Wote walibaki wamejiinamia machozi yalisha kauka katika macho yao na sasa ilibaki ishara ya majonzi!



    Kwanza kuwapoteza wenzao akiwemo Danny alogundua jani ambalo lingekuwa Dawa ya oma ya madega lilikuwa ni pigo japo walijua nao kesho wangeenda kupoteza maisha!



    Kama kumlahumu James walishamlahumu sana ila kijana huyo alionekana kutokujali



    Ndani ya chumba kidogo tena chenye vidirisha vidogo vilivyopitisha hewa ndogo hivyo ndani mule kulikuwa na joto Kali!



    James alilalia magoti yake kama wenzake ila yeye mawazo yake yalikuwa mbali alimkumbuka baba yake alokwepo mfalme kipindi icho na mama yake alokwepo kama malkia katika kijiji hiko!



    Tena katika nyumba hiyo hiyo ambayo kwa sasa aikuwa Mali yake



    Alikuwa mtoto pekee alopendwa na baba yake mfalme Mwale alomdekeza na mfalme mwale alikuwa na mke mmoja tu tofauti na wafalme wengi



    Bado Isaki alizidi kukumbuka siku hiyo baba yake alionekana kuchanganyikiwa akujua ni kwa nini baba yake alikuwa katika hali ile



    Usiku wa siku hiyo ndipo himaya yao ilipovamiwa na mfalme wa kijiji cha jirani walinzi wao wengi waliuwawa pia alishughudia baba yake akichomwa mkuki na mfalme Omoti kwa kuwa vijana wengine walikuwa wakija ikabidi mfalme Omoti ajifiche hapo ndipo kwa shida mfalme Mwale akamkabidhi mtoto wake mtabiri wake na kumwambia amlee ndo mfalme wa badae!



    Baada ya kauli ile mfalme Mwale akafariki mkewe akiwa katangulia hata kabla yake



    Mtabir yule usiku ule ule akatoroka katika kijiji kile na mtoto Isaki mpaka kijiji cha jirani tofaut na kile cha Omoti



    Asubui ya siku ilofatia Omoti akajitawaza kuwa mfalme pasina kujua Omoti alikuwa na mtoto!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo ndipo alipoanza kuiongoza himaya ile akiiunganisha na himaya yake ikawa himaya moja kubwa



    Yote Yale James aliyakumbuka



    Mpaka Mara ya kwanza alipo onana na Sendaye baada ya kurejea kijiji kile baada ya miaka mingi kuishi vijiji vya jirani



    Akarejea katika nyumba ilomilikiwa na mdogo wake wa baba mlez wake alokuwaga mtabir walo ondoka katika kijiji hiko baada ya Omoti kuvamia



    Akamweleza kila kitu kuwa mtabiri alikufa kwa ugonjwa ivyo yeye ameamua kurudi nyumbani!



    Mzee yule alotambulika kama mkwawi ( mdogo wake na mtabiri) aliuzunika ila mwisho akampokea Isaki kwa kuwa alijua ndo mfalme pale na kwendelea kumlea



    Siku hiyo Isaki akiwa msituni anakata kuni kwa Mara ya kwanza alikutana na binti Mrembo ambapo naye alikuwa akikata kuni!



    Alimkumbuka kabisa!



    Sendaye! Ndiyo alikuwa ni Sendaye malkia wa moyo wake!



    Mwanamke alomwingiza katika matatizo na kuichukua furaha yake leo hii aliendelea kujiinamia machozi yakimtiririka huku kumbukumbu zikizidi kumiminika katika ubongo wake na kuupasua moyo wake katikati!



    *je ni kumbukumbu gani hizo zinazomliza James anavyozikumbuka,je atasalimika katika mikono ya mfalme Omoti aloadhimia asb kuwaua katik viwanja vikuu vya kijiji kile*



    Moyo ulimsukuma kumsogelea binti huyo na kuhitaji japo kuongea naye,taratibu akaweka panga pembeni na kuanza kumsogelea



    Sendaye akufahamu kama kuna mtu alokuwa akija nyuma yake!,

    Ila alishtuka baada ya kufikiwa,moyo ulianza kumwenda mbio alionekana kutetemeka waziwazi ila Isaki alimtoa wasiwasi akamwambia wazi kuwa hana nia mbaya na yeye



    Akaanza kumsaidia kukata kuni maongezi baina yao yakafatia!,ikiwemo kujuana huo ukawa mwanzo wa urafiki wao,



    Kadri siku zilivyokuwa zinazidi kwenda ndivyo urafiki wao ulivyokuwa unazidi kukua tena kwa kasi ya ajabu!



    Penzi ni kama kikohozi hatimaye mahusiano ya Sendaye na Isaki yakatambulika mpaka nyumbani kwa kina Sendaye na kwa kipindi hicho yule alokuwa akiishi na Isaki mdogo wake na mtabiri alishafariki hivyo nyumba ile au eneo lile lilibaki eneo la Isaki



    Mipango ya harusi ikapangwa!



    Na hatimaye siku ya harusi ikatambulika!,ila mambo yalikuja kubadilika baada ya Sendaye kwenda kwa mfalme hakiwa na Isaki wake na kumwambia juu ya ndoa yao!



    Mtemi alikataa akasema kampenda mwanamke yule na lazima aishi naye!

    Mfalme alikuwa akiamua ameamua alikupingwa na mtu!



    Mambo yakabadilika hatimaye Sendaye akaolewa na yule asiyempenda



    Ila moyoni mwake alikuwa na penzi zito na Isaki na kudhihirisha ilo wakawa wakiendeleza penzi lao kwa siri sana! Pasina kushtukiwa!



    Kwa miaka mingi sana Isaki hakutaka kuoa japo Sendaye alimsisitizia ila alimwambia wazi awez kufanya hivyo kwani ana amini ipo siku angerejea katika mikono yake na aliamini mizimu ya kijiji kile ilikuwa upande wake!



    *James akiwa kajiinamia alikumbuka yote yale*



    Na si hayo tu alikumbuka mpaka siku Sendaye wake alipomwambia mfalme kaota ndoto kwamba yeye ( Isaki) anamuua kwa mshale na jinsi aluvyoenda kwa mtabiri na mtabiri kumwambia wazi kuwa maana ya ndoto ile ni kuvunjika kwa utawala ule!



    James pale alipo inama akajikuta akiachia tabasamu, akajiinua kidogo na kuyafuta machozi yalokuwa yakimiminika roho ya kijasiri ikamvaaa.



    Akaendelea kukumbuka jinsi Sendaye alipomshahuri akimbie ila yeye akusikia na alipoenda katika kikao kile walichokusanywa Isaki wote!,walipoanza kukaguliwa alipojaribu kukimbia hatimaye akachomwa mshale wenye sumu kali na kwenda kutupwa katikati ya pori pande eti aliwe na wanyama

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akakumbuka baba yake mlezi Dk Livingstone alivyomsaidia katika pori lile mpaka mjini akambadilisha ngozi na kumvisha ile ya kizungu akajikuta akiachia kicheko kwa nguvu!



    Vijana wale wa nne wakanyanyua vichwa vyao kumshangaa James bila shaka walitambua pengine mwenzao tena kiongozi wao Mr James alikuwa akienda kuchanganyikiwa!



    James baada ya kuona anatazamwa akajishtukia na kukata kicheko chake!



    Wenzake wakabaki katika alama ya kumshangaa, alama ya kutokumuelewa mwenzao wako kwenye matatizo kesho yake tena asubuh wanaenda kuuwawa tena adharani yeye anacheka?!



    Ina maana anafrahia jambo lile!



    Hasira dhidi ya James ikazidi kuongezeka!



    "Badala tuwaze jinsi ya kujiokoa usiku huu wengine tena walofanya tukafika hapa anacheka yamkini anafurahia hili"



    Paul kijana ambao muda mwingi alikuwa mkimya aliongea kwa uchungu Mara nyingi aliwafikiria wazazi wake jinsi walivyompenda Leo hii hata mwili wake wasingeuona hata kuuzika!....



    Alikuwa na uchungu usiothamilika!,



    "Nje kuna ulinzi wa kutosha unadhani tutatokaje!?"



    Elia kijana mwingine akadakia



    "Ahaaaaa vijana wawili hapa mlangoni ndo vijana wengi?!"



    Jemes naye akajibu watu wote wakashangaa



    Walikuwa katika chumba chenye Giza wao wenyewe walionana kwa shida,mlango ulikuwa imara hata ukichungulia nje uwezi kupaona vidirisha viwili vidogo vilikuwa juu!



    Je James alijuaje kama nje walikuwa wawili tu!

    Ila Jemes alijua mashaka yao



    "Historia ya kijiji hiki naifahamu na mpaka nikaomba kuja kufanya utafiti na nyinyi nilishachunguza mengi,kabla hata nyinyi amja plan kuja huku Mimi nilisha plan ila Mzee akunikubalia mpaka nanyi mlipomuomba madam wenu kuja kufanya research humu.....



    .....walinzi wengi huwa katika nyumba ya mfalme na katika magereza ubaki walinzi wawili tu tena wanaoaminika na mfalme kwa kuwa uyaamini magereza yao!....



    .....kivipi sasa tutatoroka?!,siye tupo watano tutagonga mlango ukifunguliwa tu tutawavamia walinzi hao wawili na kuwazimisha au kuwaua kimya kimya sisi tutakimbia sawa?!"



    Wote wakabaki kimya James aliongea kirahis tu ila lilikuwa ni jambo gumu ila waliogopa kujaribu



    "Ni bora kufa kwa kupigana kuliko kufa kama tutakavyokufa kesho"



    "Mmmmh lakini kwel"



    Kijana Martin akaitika na kuwapa moyo wenzao wakajikuta wanausogelea mlango na kuanza kuugonga kwa nguvu



    Kama alivyosema James ni kweli nje kulikuwa na walinzi wawili waliposikia mlango ukigongwa kwa nguvu wakaitana na kuufungua kujua kulikoni ile wanafungua na kuingia vijana wale watano wakawavamia na kuanza kuwapiga!



    Tofauti na mategemeo yao vijana wale walikuwa shupavu



    Martin na Paul wakauwawa mbele ya macho yao na kuzidi kuwatia uchungu na sasa walibakia watatu



    Abdull,Elia na James



    Wazo la Paul la kutoroka liliwatokea puani!



    "Na mkijaribu tena ujinga wenu nanyi tunawamalia kesho ni mazishi tu"



    Mlinzi yule alojaliwa nguvu aliongea kwa kibabe



    Watatu wale wakanywea mlango ukafungwa,wakabaki wakiiangalia miili ya wenzao kwa uchungu



    "Tumekwisha sasa"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa Mara ya kwanza Saut ya kukata tamaa ya Jemes ikasikika,kwa Mara ya kwanza naye alijua huu sasa ndo mwisho wao



    Mabaru manguvu alikuwa mlangoni?!,kivipi sasa angeokoka alimjua fika kijana yule ndio alimshika Paul na Martin shingo zao kwa mkono mmoja mmoja akawanyonga mpaka vifo vyao



    Hakuwa mtu wa mchezo mchezo



    Hakika, James pia alimuogopa



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog