Search This Blog

NZITA - 5

 







    Simulizi : Nzita

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ule upande mwingine alionekana nzita akitembea.... kwa mbali aliona watu wakiongea kwa majibizano.. nzita alisogea mpaka jirani kabisa na watu hao.... """watu hao walikuwa wakibishana kuhusu mpira wa miguu... kulikuwa na mashabiki wa timu mbili tofauti... nzita alipowakaribia watu wale walianza kumuangalia nzita... walipokutanisha na nzita.....macho ya nzita yalibadirika na kuwa mekundu.. . ghafla watu wale kila mmoja alihisi chuki ya hali ya juu kwa mwenzake.. punde watu wale walianza kupigana wenyewe kwa wenyewe.... ulikuwa ni ugomvi mkubwa kama vita watu wale waliumizana mmoja alitolewa jicho mwingine alivunjika mkono walipigana mpaka wengine waliuwawa papohapo... alibaki mmoja huku akiwa hana jicho moja.... alipogeuza shingo yake kumtazama nzita wakakutanisha macho... ghafla mtu yule aliridi katika akili yake ya kawaida.... alistahajabu kujikuta katapakaa damu huku jicho lake moja likining'inia... alihisi maumivu makali sana... alipotazama pembeni aliona wale wenzake wote wamekufa.... aliogopa sana... kwani hakuwai kuuwa hata siku moja.... nini hiki kimetokea!!!! alijiuliza mtu huyo"" alipojaribu kukumbuka... hakujua chanzo kilichopelekea wao kupigana mpaka kuuwana wenyewe kwa wenyewe...... alipogeuza shingo yake ili amuulize nzita nini kimetokea hakumuona tena nzita.... alipojaribu kuangaza angaza huku na kule hapakuwa na kichochoro... cha kusema huenda mwanadada yule kak?atisha kona""" mtu yule aliogopa alishikilia jicho lake na kutimua mbio..



    ********

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    kule kwa mchungaji baada ya kumaliza maombi... mama zanida aliamua kumuomba mchumgaji kuwa alale nyumbani kwake... kwasababu anaogopa kuridi nyumbani kwake kwa yale aliyoyashuhudia.....mchungaji alistuka alihisi huenda mama zanida anataka Uroda(mapenzi)kutoka kwake.....mchungaji alisita kuongea... alijifikiria baada ya sekunde kadhaa alijibu"" sawa utalala chumbani kwa binti yangu.... kisha mchungaji akamuonesha chumba cha bintiye... mchungaji alikuwa na mke pamoja na mtoto wa kike aitwae sara...

    Ilipofika majira ya usiku baada ya kumaliza kula chakula... mama zanida aliingia chumbani kujipumzisha.... akiwa usingizini... nzita alikuja na kuibadilisha akili ya bibi yake...imfikirie na kumtamani mchungaji kimapenzi... kisha nzita akaanza kudondosha vitu vya sebuleni kwenye nyumba ya mchungaji"""na kutowe...... punde mama zanida alinyanyuka nakuelekea sebuleni huku akiwa kajifunga khanga moja.....na kuketi kwenye sofa....

    kumbe mchungaji alisikia vitu vikidondoka upande wa sebuleni.... alinyanyuka na kwenda kuangalia nini kimetokea.... alipofika sebuleni alistahajabu sana kumuona mama zanida akiwa kajifunga khanga moja iliyoonesha vyema maungo yake... mama zanida alinyanyuka na kuifungua khanga ile... mchungaji alianza kuingiwa tamaa... alijizuia lakini alishindwa alizipiga hatua mpaka pale mama zanida alipokuwepo... na kuanza kumpapasapapasa.....

    kule chumbani mke wa mchungaji alistuka kwanini mumewe kachelewa kurudi yapata nusu saa... aliamua kunyanyuka kitandani na kuelekea upande wa sebuleni....



    alistahajabu kumkuta mumewe akimpapasa mama zanida...... huku mama zanida akiwa uchi wa mnyama...mke wa mchungaji alichukia sana akataka kuanzisha ugomvi.......mchungaji alianza kuomba msamaha kwa mkewe.... lakini mkewe hakutaka kusikiliza wala kumuelewa... punde nzita alijitokeza....mama zanida pamoja na mke wa mchungaji waliogopa sana.... mchungaji alianza kufanya maombi lakini hayakuweza kusaidia chochote kwa sababu tayari alikuwa ametenda dhambi ya kuzini... pia alikuwa bado hajajitakasa...hivyo hakuweza kuwa na nguvu za kukemea.... nzita alitabasamu kisha akazipiga hatua kumfuata mchungaji... wakati huo mama zanida na mke wa mchungaji walikuwa wametimua mbio na kutoka upande wa nje....

    nzita alimsogelea mchungaji na kumnyanyua....kisha akamtoboa macho kwa kutumia kucha zake. na kumuachia"""

    kisha nzita alitoka upande wa nje.....aliangaza angaza hakumuona bibi yake wala mke wa mchungaji.... nzita akatoweka kichawi.....

    Mama zanida alikimbia bila kujua ni wapi anaelekea......

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **************



    palipokucha mama zanida aliamua kwenda kwa mganga....alipofika""" mganga alieleza yale yote yanayomtokea.. kisha mganga alimwambia ni kazi ngumu kumdhibiti nzita kwa sababu ni mtoto wa Kishetani.... ni wakala kutoka KUZIMU......na kumnasa nzita ili asiendelee kuleta madhara duniani""" itabidi achomwe na mfupa wa mama yake mzazi ... ili kumpata nzita kwa urahisi""" itabidi mama zanida atafute ni wapi maiti ya zanida ilipo... zanida hakuzikwa alitoweka kimiujiza baada ya kuuliwa na mwanae nzita siku ile chumbani kwake....mama zanida aliwaza kisha akasema ni wapi nitapata maiti ya zanida??? mganga alisema usiku wa leo utaota ndoto itakayokuongoza pa kuipata mifupa ya zanida.... kisha mganga akampa dawa na kusema dawa hii utaiweka ndani ya maji na kisha oga maji hayo....pia. dawa hii ukimwagia nzita itamdhuru.. mama zanida aliondoka..na kurudi nyumbani kwake.... alipofika alistahajabu sana hakuiona nyumba yake...utadhani hapajawahi kujengwa nyumba kiwanja kilikuwa tupu kama uwanja wa mpira wa miguu... mama zanida aliogopa sana. aliamua kutimua mbio... ghafla nzita alijitokeza.... na kumwambia umefanya kosa kubwa ambalo litagharimu maisha yako........kisha nzita akazipiga hatua kumfuata bibi yake... mama zanida aliogopa... haraka akajipapasa ili aitoe dawa ile..... alijipapasa hakuweza kuiona dawa hiyo...... kumbe dawa ilidondoka wakati anatembea pasipo yeye kujua.... nzita alipomkaribia bibi yake alianza kubadilika macho yake yalianza kuwa mekundu zaidi.... na mwili wake ukawa mweusi kama kapakwa rangi..... kisha akamshika shingo na kumnyanyua bibi yake.....kucha za mikono ya nzita zilianza kuchomoza na kuwa ndefu.... alipotaka kupeleka mkono wake kwenye tumbo la bibi yake... ghafla ilisikika sauti ikimwambia nzita acha"" huyo huyo ni hazina yetu....akifa na wewe hautoishi tena.... nzita aliamua kumuacha bibi yake.... na kugeuza shingo yake.... kumbe alikuwa ni yule mtu wa kutisha ambaye ni baba yake nzita... baada ya kusema maneno hayo alitoweka kimiujiza.... nzita alimuangalia bibi yake kwa jicho la hasira..kisha akatabasamu na kutoweka kimiujiza.... mama zanida hakuamini kama kabaki salama..... alitimua mbio.... yani sikuhiyo kungekuwa na mashindano ya mbio za wanawake mama zanida angeongoza kwa nafasi ya kwanza....



    ************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nzita alichukia sana kwa kitendo kile cha kukatazwa kumuuwa bibi yake.... nzita alikuwa na roho ya kikatili saba baada ya kupandikizwa roho ile na yule mtu wa kutisha..... nzita aliamua kumfuata baba yake huko kuzimu.... alianza kumlaumu sana...



    *************



    ule upande mwingine mama zanida alikimbia na kuelekea kanisani.. ni kanisa ambalo huwa anafanya ibaada kumiabidu Mungu....



    kule kuzimu nzita baada ya kulalamika kwa baba yake alitoweka na kurudi duniani akiwa anahasira na chuki ya hali ya juu... alipofika nzita hakuwa na huruma kwa binadamu yeyote... aliuwa kila aliyekutananae....... alipojaribu kutazama kichawi ili abaini bibi yake anapatikana wapi hakufanikiwa.... aliamua kuelekea kwenye kumbi za starehe alijibadilisha katika umbo lake la kawaida... nzita alikuwa mrembo utadhani malaika...aliingia katika kumbi moja ya starehe... wanaume walipomuona walibabaika kwa urembo aliokuwa nao na kila aliyejaribu kumuangalia nzita basi mtu huyo aliingiwa na roho ya chuki na ukatili wa hali ya juu na kuanzisha ugomvi bila sababu ya msingi... baada ya nusu saa club hiyo ilikuwa imetapakaa damu...watu walipigana mpaka wakauwana bila sababu... ilikuwa ni zaidi ya vita kuu ya dunia... kisha nzita akapotea kimiujiza na kuendelea kumtafuta bibi yake... ghafla alihisi kitu....





    alihisi kuwa bibi yake hayupo mbali na eneo hilo alilopo....nzita akaanza kutazama kichawi kwa nguvu za miujiza.....



    *********



    ule upande mwingine ndani ya kanisa mama zanida aliendelea kubaki mule ndani ya kanisa.....huku akiwa katika hali ya uwoga.....ghafla nzita alifika eneo lile la kanisa.....lakini hakuweza kutambua kuwa bibi yake yumo ndani ya kanisa......nzita aliendelea kuzunguka zunguka katika eneo la kanisa.... kwa mbali aliona watu wawili wakitembea barabarani upande wa nje ya kanisa nzita aliwafuata watu hao na kuwauwa kikatili kwa kuwatoboa tumbo na kuunyofoa moyo moyo....watu wale walipoteza maisha papohapo wakati huu nzita alikuwa na hasira na chuki dhidi ya binadamu.. alimuuwa bila huruma

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati huo mama zanida alikuwa akiendelea kusali akimuomba mungu wake.......baada ya kumaliza kufanya maombi aliamua kutoka nje ya kanisa kabla hajatoka aliona msaraba aliamua kuuchukua msaraba huo mdogo na kuanza kuzipiga hatua kutoka nje.... alichungulia alipo ona hakuna dalili yoyote ya nzita kuwepo eneo hilo alitoka nje kabisa.... wakati anatoka alikutana na mtu aliyejitambulisha kuwa yeye ni katekista wa kanisa hilo... pia mama zanida alijitambulisha waliongozana na kuelekea nje ya geti la kanisa wakaanza kuzipiga hatua kuelekea barabarani.... wakiwa wanatembea ghafla walihisi joto kali walistahajabu sana kwa kuwa ilikuwa ni isiku tayari... joto lile liliongezeka kuwa kali sana.... mpaka jasho lilianza kuwatoka.. waliingiwa na uwoga wa hali ya juu.... punde walianza kuona moto ukiwafuata.. waliamua kutimua mbio... huwezi kiamini mama zanida alikimbia kwa kasi kuliko yule katekista punde nzita alijitokeza mbele ya katekista kisha akamshika shingo na kumnyanyua juu.. nzita alianza kumtafuna mzima mzima alianza kunyofoa mkono mmoja na kutafuna vidole akanyofoa mkono wa pili. kisha alimtoboa macho na kuyanyofoa.... katekista yule alilia kwa maumivu makali huku sauti haitoki kwa sababu alikuwa kakabwa shingo..... kisha nzita alivuta suruali ya katekista ikatoka kabisa.. kisha nzita alivuta uume wa katikista ma kuanza kuutafuna mbichimbichi... damu nyingi zilimtoka punde alipoteza maisha..



    ********************



    kisha nzita aligeuka kutazama ni wapi bibi yake kaelekea... kisha akatoweka kimiujiza...



    ule kupande mwingine alionekana mama zanida akiendelea kutimua mbio.... ghafla nzita alijitokeza mbele ya bibi yake.... mama zanida aliogopa sana"" alitetemeka kwa uwoga wa hali ya juu huku haja ndogo ikimtoka mfululizo......nzita alibadilika na kuwa na macho mekundu.. huku uso wake ukionekana kujaa hasira.... kisha akaanza kuzipiga hatua za haraka haraka kumfuata bibi yake alipomkaribia alisita kumsogelea kwa sababu ya ule msaraba aliokuwa ameushika bibi yake....mama zanida alianza kutimua mbio kuelekea kwenye mapori alikimbia mpaka akatokezea kongowe.... kipindi anakimbia msaraba ule ulidondoka..... kabla hajafika mbali.. nzita alijitokeza tena..... nzita alimrukia bibi yake mama zanida alidondoka chini... kisha nzita akamkaba bibi yake..... wakati mama zanida anahangaika kutafuta pumzi kwa kugeuza geuza shingo yake... aliona kipande cha mfupa alikivuta na kukichukua.... punde nzita alinyanyua mkono wake ili atoboe tumbo la bibi yake haraka mama zanida alimchoma nzita na mfupa ule upande wa ubavuni... nzita alimuachia haraka kisha akanyanyuka... nzita alianza kupiga kelele zenye mngurumo wa ajabu..... ghafla alianza kuyayuka huku mwili wake ukiwaka moto....aliungua mpaka akabaki majivu...... kumbe nzita baada ya kumuuwa mama yake alimchukua kimiujiza na kumtupa katika pori hilo... na ule mfupa aliochukua mama zanida ulikuwa ni moja ya mfupa wa zanida......

    mama zanida alinyanyuka na kutimua mbio kuelekea upande wa barabara... alitokezea barabarani.... alipotokeza barabarani ghafla aligongwa na gari lililokuwa likiendeshwa kwa kasi....... mama zanida alipoteza maisha papohapo..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    *********MWISHO WA SIMULIZI HII************







0 comments:

Post a Comment

Blog