Search This Blog

SHAMBA LA URITHI - 5

 







    Simulizi : Shamba La Urithi

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Upande mwingine,, alionekana Timo, akiwa analiendesha gari lake, akachukua simu yake na kumpigia raiki yake,, akimuuliza habari za huko kazini,, Timo akasema,, "kesho naanza zamu tutawasiliana nikitoka kazini jioni. kisha akakata simu! na safari ikaendelea,

    wakiwa njiani Lulu akasema,, "kaka kunadada yetu kapotea tunaomba utusaidie kumtafuta!  pia kaka yetu kapotea na dada yetu mwingine!  Timo akasema tukitoka huku mtaniambia majina yao,, nitajaribu kuwatafuta,, nawaahidi lazima muwaone ndugu zenu sawa watoto wazuri?

    Watoto hao wakaitikia,, "sawa kaka,,

    Konje akaangaza angaza macho yake nje akauliza nyumba hiyo yenye rangi nyeupe ni ya nani?

    Timo akajibu,, "hiyo ni hospitali kuu ya wilaya....

    Lulu akadakia,, akasema,, "mbona hatufiki?

    Timo akasema tumesha fika ni kando ya hospitali hiyo!

    wacha nitafute sehemu nzuri niegeshe gari.

    akaliegesha gari,,wakashuka na kuingia sehemu maalumu kwa ajili ya michezo ya watoto... akalipia pesa getini kisha wakaingia ndani kabisa.



    Wakati huo huo likaonekana gari la Magereza likiegeshwa nje ya hospitali ya wilaya... akashuka askari akaingia ndani ya hospitali kuwafuata wahusika wa mochwari waje kuchukua maiti ya ye mfungwa aliyefariki gerezani!

    kule chini ya gari hilo alionekana Pamera akichungulia akamuona askari huyo ameshaingia ndani ya hospitali.. akaamua kutoka kule chini ya gari akazipiga hatua huku akiwa na wasiwasi kupita kiasi,, kwa sababu alikuwa amevaa sale za wafungwa! akazipiga hatua kukifuata kichochoro kilichokuwa kinapita kando ya ile sehemu ya michezo ya watoto!



    wakati huo huo alionekana Timo akizipiga hatua kutoka nje ya eneo hilo,akaongee na simu kwa utulivu... akazipiga hatua kukifuata kichochoro kilichokuwa kando... ghafla akakutana na Pamera akamtambua kuwa ni mfungwa,, akamkamata Pamera

    kumbe Timo ni miongoni mwa askari magereza wa gereza alilokuwa amefungwa Pamera... Timo akamchukua Pamera huku kamshikilia shati, akaongozana nae kuelekea mule nda ya michezo ya watoto,,  akawachukue wale watoto kisha amrudishe Pamera kule Gerezani,,,

    Timo hakujua kuwa,, dada wa watoto hao ndio huyo aliyemkamata!

    Timo akabaki hapo getini,, huku kamshikilia Pamera shati.  akamuagiza mmoja wa wahusika wa sehemu hiyo akawalete wale watoto,, ili waondoke.

        



    baada ya dakika kadhaa yule muhusika wa eneo hilo akaja akiwa kaongozana na watoto hao!  walipofika getini, wakastaajabu kumuona dada yao!!  wakakimbia kumfuata wakamkumbatia kwa furaha kisha wakamsalimia!  Pamera hakuamini akajikuta analia kwa furaha,,

    Timo akabaki na mshangao huku macho yamemtoka!  akajisemea moyoni,, "kumbe huyu ndiye dada yao wanaomuongelea kila siku?  sasa itakuwaje huyu ni mfungwa ametoroka gerezani! 

    Timo akawatazama wale watoto,kisha akamtazama Pamera,, akaingiwa na roho ya huruma baada ya kuwaona watoto hao wamemkumbatia dada yao kwa upendo wa hali ya juu! Pamera akainua uso wake kumtazama Timo,,, akasema,, "hawa ni wadogo zangu nimefurahi kuwaona,, akamsogelea Timo kisha akanyoosha mikono yake ishara afungwe pingu,, akasema,, "natamani sana kujua wadogo zangu wanaishi wapi?  lakini sina namna,, naomba uwatunze watoto hawa wasiokuwa na hatia!  mimi nimefungwa gerezani kwa ajili ya kutetea uhai wa mmoja wao ambaye hayupo hapa!  sina hatia,, eee Mungu simama na mimi,  natamani vyombo vya dora vijue ukweli lakini sina mtetezi,, nipo tayari kurudi gerezani, Timo akastaajabu, maneno ya Pamera yalimchoma akajisemea moyoni,, "inasikitisha sana,  bila shaka binti huyu kahukumiwa bila hatia wacha nifanye jambo,

    wakati Timo anawaza hayo,,  Lulu akasema,, "kaka naomba twende nyumbani sote na dada Pamera,

    Timo akamsogelea Lulu kisha akamshika mkono akasema tuondoke turudi nyumbani!

    kisha akamtazama Pamera kwa macho ya huruma,

    wakati huo Pamera alikuwa anatokwa na machozi hakuamini kama angewaona wadogo zake kwa mara nyingine!

    Timo akamwambia Pamera,, "usilie binti!  kila kitu kitakuwa sawa twende nyumbani.

    Pamera akafuta machozi haraka,, wakaongozana kulifuata gari la Timo.

    wakaingia ndani ya gari,, na safari ya kurudi nyumbani ikaanza...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                              *************************************



    Upande mwingine kule nyumbani kwa Timo, alionekana Kabi akiwa bado kasinzia kando ya nyumba hiyo,, huku kaegemea ukuta,, akashtuka kutoka usingizini.. akanyanyuka na kuzipiga hatua,, akaondoka zake,,,

    Kabi alitembea pasipokujua ni wapi anaelekea!  kwa mbali akaona kibanda,, akaamua kukifuata kibanda hicho.. alipofika akamsalimia muhusika kisha akasema,, "samahani naomba msaada wa kazi,, hata bila malipo nitafanya,, ilimradi tu nipate sehemu ya kuishi pia chakula!  yule binti akasema,, "sina uwezo huo,, hata mimi nimfanyakazi tu... natamani kukusaidia lakini sina namna,,, Binti huyo akatoa noti ya shilingi elfu moja akampa Kabi,,,



    wakati huo huo alionekana yule mwanamke aliyemsaida Subira,,akizipiga hatua kuelekea kwenye bihashara yake,, ni kibanda cha kuuza bidhaa ndogondogo na mahitaji ya nyumbani,, Subira alimuuliza maswali mengi kupita kiasi,, mwanamke huyo akawa anajibu maswali ya Subira huku akitabasamu,,, akajisemea moyoni,, "huyu mtoto mdadisi sana,, anauelewa mpana kuliko umri wake,, akageuza shingo yake na kumtazama Subira...

    waliendelea kuzipiga hatua hatimae wakakaribia kwenye kibanda,, Subira akashtuka kumuona Kabi akitokea kibandani akizipiga hatua,, akapaza sauti,, "KAKAAAAA!!!

    kabi akageuza shingo yake baada ya kuitambua sauti ya Subira akamuona mdogo wake!  Subira akatimua mbio kumfuata kaka yake!

    Kabi akasema,, "nilikuwa nawaza nitakupata wapi Subira mdogo wangu! 

    mbona uliondoka kule ziwani pasipo kunipa taarifa?

    Subira akasema,, "nilikutafuta lakini sikukupata... punde si punde yule mwanamke akafika.. Subira akamtambulisha Kabi kwa mwanamke huyo.. kisha wakazipiga hatua kukifuata kibanda hicho,, akaangalia maendeleo ya kibanda chake kisha wakaondoka kurudi nyumbani!

    baada ya lisaa limoja kupita,, walifika nyumbani,, Kabi akamsimulia mwanamke huyo historia ya maisha yao,, mwanamke huyo akawaonea huruma akamuuliza Kabi,, "unaweza kufanya kazi gani?

    Kabi akajibu,, "naweza kazi zote hata bila malipo ilimradi nipate sehemu ya kuishi na chakula pia, Mwanamke huyo akasema,, "kesho tutakwenda kwa mama mmoja ni mwanakikundi mwenzetu kwenye  KIKOBA..mama huyo huwa anamashamba ya ndizi yeye pamoja na mumewe.. huwa anauza ndizi hizo kwa jumla nitaongea naye akupe kazi,, naamini utapata kazi,



                           **********************************

    Upande mwingine kule kijijini alionekana,,Shangazi yao Pamera akiwa ndani ya nyumba hiyo ya urithi,,, akijiandaa kutoka! 

    baada ya dakika kadhaa akatoka akaelekea kwenye lile shamba,,,alipofika akapiga simu,,

    baada ya dakika kadhaa akaonekana mwanaume mmoja wa makamo akija hapo shambani, akalitazama shamba hilo kisha akatoa bahasha kubwa  imetuna iliyokuwa na pesa ndani yake,, akamkabidhi shangazi yao Pamera,,

    yule mwanaume akaingia ndani ya shamba hilo alilolinunua ili akague... akiwa ameongozana na shangazi yao Pamera walipofika katikati ya shamba hilo,,,,ghafla akajitokeza mfu aliyekuwa amevalia mavazi mekundu... akasimama mbele yao.. Wakatimua mbio huku wakipiga kelele,, shangazi yao Pamera akachanganyikiwa akaitupa bahasha iliyokuwa na pesa....

    Kumbe ni mzimu wa Joram baba yao Pamera..

    akaiokota bahasha hiyo kisha akatoweka kimiujiza!!!!!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                 

    Kule nyumbani kwa Timo,, alionekana Pamera akisimulia matukio yote mpaka siku aliyokamatwa!  Timo akasikitika sana,,  akasema,, "ondoa shaka nitawasaidia mtapata mali zenu halali zilizoachwa na wazazi wenu... nakuhakikishia nitalifikisha mbele ya sheria,



                       **********************************

     

    Asubuhi palipokucha,,,alionekana Kabi akidamka kutoka kwenye godoro lililokuwa limetandikwa kwenye sakafu...wakati huo yule mwanamke aliye wapa msaada wa hifadhi alikuwa nje akiandaa chai.. Kabi akafungua mlango na kutoka nje... akamsalimia mwanamke huyo.. kisha akaketi kando..

    mwanamke huyo akasema ,"chukua hii pesa kanunue vitumvua pale mbele ukikatisha kona,,

    Kabi akaipokea pesa hiyo akaondoka..... kabla hajafika mbali akahisi kubanwa na haja ndogo,, akasogea kando ya barabara ajisaidie haja ndogo!  akaona bahasha kubwa imetuna ikiwa chini kwenye majani!!!!!!!





    Kabi akaokota bahasha hiyo,,,, akaifungua bahasha hiyo,  akastaajabu kuona noti za shilingi elfu kumi kumi zimejaa ndani ya bahasha hiyo,! akaangaza angaza macho yake kushoto kulia,,alipohakikisha hakuna anayeshuhudia akaificha bahasha hiyo ndani ya shati lake alilokuwa amelivaa kisha akaendelea na safari ya kwenda kununua vitumbua,, akazipiga hatua kurudi nyumbani,,alipofika akaweka vitumbua kisha akamuita Subira pamoja na mwanamke aliyewapa msaada,, akawaonyesha bahasha hiyo ! wakastaajabu !

    yule mwanamke akauliza kwa mshangao ! ,," umepata wapi pesa hizi ?

    Kabi akajibu,, "nimeikuta bahasha hii kwenye majani.. kisha kabi akachomoa noti kiasi akamkabidhi mwanamke huyo,,,

    huyo mwanamke alipozihesabu zilikuwa ni milioni moja na laki mbili !

    mwanamke huyo akabaki mdomo wazi huku akimtazama Kabi kwa macho ya mshangao !  akajisemea moyoni,, "hakika Mungu hugawa ridhiki kupitia kwa mtu !mtoto huyu ana roho nzuri sana,, Mungu ambariki.

    Kabi akamtazama Subira kisha akatabasamu na  kusema,, "Mdogo wangu, sasahivi tutaishi maisha mazuri pia tuwatafute ndugu zetu, Kabi akahisi kumuamini mwanamke huyo akasema dada naomba unitunzie pesa hizi,,,

    mwanamke huyo hakuamini akajisemea moyoni,, "yawezekana vipi kaniamini kwa haraka kiasi hiki ??  akaipokea bahasha hiyo na kuiweka chini ya godoro.

    wakanywa chai,, walipomaliza Kabi akauliza,, "dada tutakwenda kule kwa rafiki yako ??

    ulisema atanipa kazi ! 

    mwanamke huyo akasema,," ndio tutakwenda,,



                              *****************************************



    Upande mwingine kule nyumbani kwa Timo,, alionekana pamera akiwa kavalia suruali ya Timo pamoja na shati la Timo ! akiwa jikoni anaandaa chai Timo akaja jikoni akasema,,,"zimekupendeza nguo hizi.. lakini nikitoka kazini nitakununulia angalau nguo chache upate za kubadilisha !  sio vyema kuendelea kuvaa nguo za wafungwa..

    Pamera akamtazama Timo kisha akasema,, "asnte sana kaka wewe unamoyo wa kipekee Timo akasema,, "asante, wacha niwahi kazini,

    Timo akazipiga hatua na kuondoka zake...

    ilipofika saa nane za mchana,,Konje, Lulu pamoja na Jack wakafika nyumbani wakitokea shuleni !

    wakamkuta dada yao kawaandalia chakula,, wakamsalimia kisha wakaingia chumbani kwenda kubadilisha mavazi wakavua sale za shule na kuvaa nguza za kawaida.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                        *****************************************



    Upande mwingine kule kijijini,, Shangazi yao Pamera,, alizidi kuchanganyikiwa alikuwa anaona mauzauza ya kutisha ndani ya nyumba,, aliyowanyang'anya watoto wa mdogo wake,, akaamua kufungasha lila kilicho chake, alipomaliza akatoka chumbani na kuelekea sebuleni ,,wazo likamjia akakumbuka kuwa ameacha hati ya nyumba hiyo,, akarudi kule chumbani kwa ajili ya kuichukua hati ya nyumba,,kabla hajaingia chumbani,, mzimu wa baba yao Pamera ukajitokeza na kuichukua hati ya nyumba hiyo,, kisha mzimu huo ukatoweka kimiujiza !

    Shangazi yao Pamera akaanza kuitafuta hati ya nyumba.... aliitafuta kila sehemu lakini hakufanikiwa kuipata... akaamua kuondoka zake na kuiacha nyumba ikiwa wazi. akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwake kwenye nyumba aliyoijenga yeye mwenyewe ! 

    hapakuwa na umbali,, alitumia dakika arobaini,,akawa amefika nyumbani kwake..... ghafla moto ukazuka na kuunguza nyumba yake... akapiga mayowe kuomba msaada kwa majirani wamsaidie kuuzima moto huo,,, majirani walijitahidi lakini ikashindikana... hatimae nyumba ikateketea kwa moto !  shaangazi yao Pamera akalia kwa uchungu,, akajisemea moyoni,, "sasa nitaishi wapi,, hii nyumba yangu imeteketea kwa moto ! 

    kule kwenye ile nyumba hapakaliki !!!

    wakati anajisemea hivyo huku akilia kwa uchungu !  mzimu wa baba yao Pamera ukajitokeza mbele yake ukitokea ndani ya nyumba ya shangazi yao Pamera inayoteketea kwa moto... hakuna aliyeweza kuona mzimu huo kwa macho ya kawaida... kisha ukatoweka kimiujiza !



     wakati huo huo kule nyumbani kwa yule mwanamke aliye mpa msaada Subira pamoja na kabi,,, wakaonekana wakitoka nje ya nyumba wakiwa wameongoza wote watatu !  Subira,,,,Kabi, pamoja na mwanamke huyo.

    wakaelekea kwa yule mama mwana kikundi mwenzake kwenye kikoba,  walipofika,,mwanamke huyo akagonga geti,, mlinzi akafungua geti akawakaribisha wakaingia ndani !  Kabi akashtuka kuliona lile gari aliloomba msaada wa lifti kuja mjini !  akamtazama Subira kisha akasema,, "kwenye hili gari nilimuona mdogo wetu.

    Subira akalitazama gari hilo pia na yeye alilikumbuka akasema hata sisi tulimuona Mage akiingia ndani ya gari hili tukiwa hospitali,, punde si punde mlango wa nyumba ukafunguliwa !  Kabi akamuona yule dereva akamkumbuka akamsalimia kisha akaendelea kumtazama kwa umakini ! 

    mwanaume huyo akasema karibuni,,

    mwanamke huyo aliyekuja na Kabi pamoja na Subira akasema,, "habari yako !

    mkeo nimemkuta ??

    kabla hajaongea neno lingine,,mke wa dereva huyo akafungua mlango akatoka huku kaongozana na mtoto Mage.!

    Subira na Kabi wakastaajabu kumuona mdogo wao !!





    Mage pia akastaajabu kumuona kaka yake pamoja na dada yake. akawakimbia na kuwakumbatia,, kila mtu akabaki mdomo wazi... yule dereva akauliza,, "huyu mtoto mnamfahamu?  kabi akadakia na kusema,, "huyu ni mdoo wangu tulipotezana kule nyumbani l,, kijijini kwetu! akasita kuongea,, kisha akaanza kusimulia kilichowatokea mpaka wakapotezana!  msamalia huyo aliyemuokota Mage,,,akasema,, "sawa lakini ninaombi,, ningependa aendelee kuishi hapa nyumbani kwangu kwa sababu anasoma!  pia sio mbaya kwa sababu umeshapafahamu hapa,,usisite kuja kumjulia hali mara kwa mara!  Kabi na Subira wakatazamana,, kisha wakamuuliza Mage,, "Eti mdogo wangu,, ungependa kuendelea kuishi hapa,, sisi tutakuwa tunakuja kukujulia hali mara kwa mara! 

    Mage akakubali,, kisha akauliza,, "dada pamera yuko wapi?

    Kabi akawa mnyonge akashindwa kujibu swali hilo,, kwa sababu hakufahamu ni wapi dada yao Pamera anapatikana! CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    yule mwanamke aliyewapa msaada akamfuata mke wa dereva huyo na kueleza shida iliyomleta!  akasema,, "huyu kijana anatafuta kazi,, nikaona ni vyema nimlete kwa sababu uliniambia unatafuta mfanya kazi kwa ajili ya shamba lako la migomba ha ndizi!

    ombi hilo likakubaliwa,, wakapanga siku ya kumpeleka kabi akaonyeshwe shamba hilo!



                          ************************



    upande mwingine kule nyumbani kwa Timo,, alionekana Pamera akiwa na wadogo zake,, Lulu,, Jack na Konje,,wakiwa wameketi sebuleni,, punde si punde Timo akarejea nyumbani,,,akaketi sebuleni huku mkononi kashikilia bahasha ndogo,, kisha akasema,, "nilikuwa mahakamani nimefungua kesi,, SHAURI LA MIRATHI yenu,, na hii ni barua ambayo inahitajika ipelekwe kwa shangazi yenu,, ni wito wa mahakama!  Pamera akafurahi sana kusikia taarifa hiyo,,

    Timo akaendelea kusema,, "pia inahitajika barua kutoka kwenu,, iwe kama uthibitisho wa makubaliano ya watoto wa marehemu! kesho nitaongozana na nyinyi mpaka huko kwa shangazi yenu!



                  *****************************



    Asubuhi palipokucha,, Kabi na Subira wakaongozana,, kuelekea nyumbqni kwa yule msamalia!  kwa lengo la kupelekwa kule kwenye shamba,,,,Kabi hakutaka kumuacha Subira popote aendapo,, aliongozana nae!

    walipofika wakagonga hodi wakafunguliwa geti na kukaribishwa ndani,, bila kuchelewa wakaongozana na msamalia huyo, wakaingia ndani ya gari na safari ikaanza...Kabi akastaajabu sana safari yao kwa sababu walipita barabara inayoelekea kijijini kwao!!  wakiwa njiani,,gafla gari likapata hitirafu!  likazimika,, alipojaribu kutazama tatizo ni nini,, akagundua kuwa kuna waya mmoja unaotoka kwenye betri ulikuwa umeregea hivyo betri hilo likaishiwa chaji!

    wakabaki hapo wakisubiri gari lingine lipite aombe msaada wa kuibusti betri ya gari lake!



    wakati huo huo alionekana Timo akiwa anatokea chumbani kwake,, akamkuta Pamera na wadogo zake wameshajiandaa tayari.. wakaingia ndani ya gari,, na safari ya kuelekea kule kijijini ikaanza,,,

    baada ya nusu saa kupita,,wakiwa njiani,,kwa mbali,, Timo akaona mtu anampungia mkono,, ishara kuwa asimamishe gari lake!

    Timo akapunguza mwendo na kulisimamisha gari lake!!

    yule msamalia akalifuata gari la Timo akaomba msaada,,,Timo akalisogeza gari lake sambamba na gari la msamalia huyo! kabi akageuza shingo yake kulitazama gari hilo,,, akashtuka kumuona Pamera akiwa ndani ya gari hilo, akapaza sauti kwa furaha dada Pamera!

    Pamera akashtuka kuisikia sauti ya Kabi,,

    Kabi akashuka haraka kutoka ndani ya gari,, akalifuata gari ambalo Pamera na wadogo zake walikuwemo ndani yake!  Pamera akashuka kutoka ndani ya gari pamoja na wadogo zake,,

    wakafurahi sana familia yao kukutana pamoja!  Timo akazidi kustaajabu!  hata yule msamalia akastaajabu!! Pamera akasema,, "sisi sote ni ndugu wa damu moja,, baba mmoja na amma mmoja,

    akamtazama Timo akamwambia,, "ni vyema tuongozane pamoja tukiwa sote mimi na wadogo zangu wote.. Timo akamueleza kwa kifupi yule msamalia kuhusu watoto hao,, msamalia huyo hakuwa na kipingamizi Kabi na Subira wakaingia ndani ya gari la Timo.. wakiwa familia yote!

    Timo akatoa msaada wa kubusti betri la gari la msamalia huyo,  likawaka,, kisha yeye akaendelea na safari ya kuelekea kule kijijini,,

    baada ya lisaa limoja kupita wakafika kijijini kwao Pamera!

    mpaka kwenye nyumba yao Pamera wakamkuta Shangazi yao kaketi nje huku alionekana kuwa na huzuni!  CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    shangazi huyo akashtuka kumuona Pamera akiwa na wadogo zake,, wamependeza kupita kiasi,, kisha Timo akamkabidhi bahasha shangazi yao Pamera!!  alipoifungua na kuisoma akashtuka akaingiwa na hofu kuwa anahitajika mahakamani,, anashtakiwa kwa kudhurumu mali za marehemu,, wakati warithi halali wapo hai!  ambao ni watoto wa marehemu.

    Timo hakutaka kupoteza muda,, akaongozana na Pamera pamoja na wadogo zake wakaingia ndani ya gari,, kisha wakaondoka na kurudi mjini!!

    Shangazi yao pamera akahisi kuchanganyikiwa!  akarudia kuisoma tena barua hiyo,, aliposoma tarehe,, alionyesha ni tarehe ya kesho!



                          *******************************



    Siku iliyofuata,, Timo pamoja na Pamera,, akiwa na wadogo zake,, wakaonekana wakishuka kutoka ndani ya gari na kuingia mahakamani,,, punde si punde Shangazi yao Pamera akaoneka pia akiingia mahakamani!

    bqada ya dakika kadhaa!  kesi ikaanza,, hakimu akasoma shtaka...Shangazi yao Pamera akashindwa kujitetea!!  kuhusu mashtaka hayo!  hakimu akaamua kutoa hukumu, akasema,, "Rudisha mali zote za marehemu,, pia unashtakiwa kwa kuchukua pesa za marehemu,,kwenye akaunti yake ya benki(bank acccount)

    pasipohidhini ya warithi halali,,ambao ni watoto wa marehemu.. hilo ni kosa la pili,, umehukumiwa kifungo cha miaka kumi(10) gerezani!  na adhabu ya viboko hamsini kabla ya kuingia... pia viboko hamsini siku ya kutoka! iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama yako... Shangazi yao Pamera akachukuliwa na askari kupelekwa gerezani,,



    Timo na Pamera akiwa na wadogo zake,, wakaondoka,, wakiwa njiani kabi akasema!  naomba tupite kwa yule mwanamke aliyetupa hifadhi mimi na Subira,, niliacha pesa zangu huko...

    Timo hakuwa na kipingamizi.. akaliendesha gari lake huku akielekezwa na Kabi,,, mpaka nyumbani kwa mwanamke huyo,, wakamkuta anapika.. akawakaribisha ndani, Kabi akasema,, "samahani naomba ile bahasha.. yulewanamke akafunua godoro akatoa bahasha hiyo akamkabidhi Kabi...

    Kabi akasema,, "asante kwa msaada wako Mungu akubariki,,, wacha sisis tukaanze maisha mapya na ndugu zangu,, kisha wakaondoka kuelekea nyumbani kwa Timo.



    ********BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA******



    pamera na wadogo zake wakawhauriana kuwa ile nyumba ya kijijini waipangishe,, fedha zitakazopatikana,, wazitumie kuwasomesha wadogo zao... pia wakaligawa kati kwa kati shamba la baba yao... ulande mmoja wakauza,, upande wa pili ambao lilikuwepo kaburi la baba yao,, wakaliacha kama ukumbusho wa kaburi la baba yao...



    Miezi ilizidi kusonga.....Pamera akaanza kunenepa akawa mrembo sana,,, Timo akaamua kumuoa Pamera,, akawa mke wake halali wa ndoa... Pamera akaamua kumfuata Mage kule nyumbani kwa msamalia akamchukua,,,,

    Pamera na wadogo zake wakaishi maisha ya amani na furaha ,,,Kabi akarudi shule kuendelea na masomo... pia Lulu ,,,Konje,,, Jack,,, na Subira,,wakaendelea na masomo....upendo wa Timo na Pamera ulizidi kukuwa kila siku,, wakaishi kwa amani kupita kiasi...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

         ********MWISHO WA HADITHI***********

0 comments:

Post a Comment

Blog