IMEANDIKWA NA : ZUBERI MARUMA
*********************************************************************************
Simulizi : Sendaye (Malkia Wa Moyo Wangu)
Sehemu Ya Kwanza (1)
UTANGULIZI:
Lilikuwa ni pori lenye miti mikubwa ilojifunga funga na kuleta giza lililotengeneza taswira ya kutisha katika pori lile lenye wanyama wakali,milio ya wanyama mbalimbali ilisikika kwa mbali
Ila katika eneo moja katikati ya msitu ule vilisikika vishindo vya watu wawili wakikimbizana
Mtu wa mbele alokuwa akikimbizwa alikuwa ni baba wa makamo mwenye miaka 48 mpaka 50
Alikimbizwa na kijana mdogo mwenye miaka kama 20 au chini ya hapo kidogo
Mfalme Omoti alizidi kukimbia katika pori lile lenye wanyama wakali , ila kila alipogeuka nyuma kijana yule alizidi kumfikia kwa kasi!,
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kuwa Omoti alikimbia huku akiwa anageuka nyuma ghafla alijikwaa na kuanguka akajinyanyua ila ile anapiga hatua kitu chenye ncha Kali kikakita mgongoni
Omoti akajitahidi kupeleka mkono wake!,alitoa macho baada ya kugundua ni mshale akakosa nguvu na kwenda chini!
Kijana yule mdogo kwa umri na kiumbo pia akamfikia akimtazama kwa jicho la jeuri
"Huu sasa ndo mwisho wako mtemi omoti"
"i...i...i..saki una...niua?!"
"Kufa mfalme katili mwenye roho mbaya na sasa Mimi ndo mfalme wa kijiji hiki na kwa sasa kipo huru!"
"Ha...pa...naaaaaaaa"
Mfalme Omoti akapiga kelele ghafla akashtuka!...
Kumbe ilikuwa ni ndoto, mfalme Omoti alikuwa akiota ndoto ambayo akuielewa kabisa
Mwili wote ulimloa jasho!...
"Ni nini mfalme wangu?!"
Malikia wake alolala pembeni yake akamuoji
"Is..aki?!"
Mfalme Omoti akaongea huku akitetemeka
"Isaki?!,kafanyaje huyo Isaki!"
"Isaki kaniua!"
"Isaki kakuua?! Isaki gani kwanza mbona sikuelewi mfalme wangu"
Mfalme akatulia kwa dakika kadhaa ni kama alikuwa akifikiria kitu!
"Ni ndoto malkia wangu!,nimeota ndoto mbaya kuna kijana nlomjua kama isaki ananikimbiza katikati ya pori na kwa bahati mbaya nikajikwaa nikaanguka niliponyanyuka akanipiga kwa mshale!"
"Unamjua huyo kijana?!"
Mfalme akafikiria kwa sekunde kadhaa akatingisha kichwa ishara ya kutomjua japo kwenye ndoto alikuwa akimjua fika!
"Basi lala mfalme wangu kesho tutawaona washauri na waganga wakufunulie maana ya ndoto yako na washauri wakushauri kipi ufanye mfalme wangu
Malkia wake mdogo mfalme Omoti alotambulika kwa jina la Sendaye akazidi kumshauri mume wake yule
Mfalme Omoti alikuwa na wake wa nne watatu wakiwa rika lake ila mke wake mdogo alompenda kuliko hata hao watatu walobakia alikuwa ni sawa na mwanaye kiumri alikuwa na miaka 16
Ila alikuwa na ushauri kama wa mtu alokomaa akili!
Hili na mengine ya chumbani ndiyo yalomfanya mfalme ampende zaidi ya kitu chochote katika maisha yake!
Sendaye akamwekea mkono mfalme wake na kumbembeleza kama abembelezavyo mtoto hatimaye mfalme akalala!
Baada ya kuhakikisha mfalme wake kalala Sendaye akatabasamu! Akambusu katika paji lake la uso naye akaanza kuusaka usingizi
***
Kilikuwa ni kikao cha watu wa nne ,mfalme Omoti alikuwa kaketi katika kiti chake cha kifalme pembeni yake wanamwali wawili wakimpepea
Wawili walikuwa ni washauri wa mfalme na wa mwisho alobakia alikuwa ni mtabiri pekee wa kijiji kile alotafsiri ndoto za mfalme!...
Huyu alikuwa ni mganga mwenye uwezo wa ajabu katika kijiji kile kila alichotabiri kilikuwa kama alivyotabiri hivyo mfalme aliamini kile asemacho mtabiri yule
Mfalme akaeleza ndoto yake ambapo mtabiri alimsikiliza kwa Makini ,alionekana wazi kushtuka kwa ndoto ile CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mtukufu mfalme!"
Mtabiri akazungumza kwa sauti ya upole akionekana wazi kuogopa kile atakacho kusema
"Nakusikiliza mtabiri wangu nini maana ya ndoto hiyo!"
"Kwanza kabla sijakwambia naomba nikuulize unamjua huyo kijana ulomwota ana kuua?!"
"Isaki?!"
"Ndiyo!"
Kama ilivyokuwa kwa mke wake,Omoti akajaribu kumkumbuka lakini sura ile japo kwenye ndoto alionekana kuijua ila kiuhalisia akumtambua mtu huyo kabisa akatingisha kichwa kukataa kumfahamu Isaki
"Kwa tafsiri halisi wa ndoto yako mtukufu mfalme ni kuanguka kwa utawala wako!"
"Niniiiiiiiiii?!"
Mfalme Omoti akauliza kwa mshangao
"Na huyo Isaki ndo atakayeitawala Bomale"
"Haiwezekani! Nimesema haiwezekani...."
"Ndo maana mtukufu mfalme nikakuulza je unamjua huyo mtu ulomuota ili tumdhibiti mapema kabla ilo alijatokea"
"Simjui nimesema walinzi wangu wote waitwe ulinzi uimarishwe...."
"Lakini mtukufu mfalme mi na wazo"
Mshahuri namba moja akaufunua mdomo wake
Mfalme akamruhusu mshahuri yule kutoa wazo lake:
"Mtukufu mfalme We umesema umjuhi kabisa kijana huyo zaid ya jina lake wazo langu isike wote katika kijiji hiki wakusanywe pengine ungeweza kumuona"
"Tatizo naweza nisiikumbuke sura yake hata tukifanya ivyo"
"Basi itabidi wote wauwawe wenye jina hilo!"
Mshahuri namba mbili akaongea , mfalme akatabasamu kukubaliana na jambo hilo
Mbiu ya mgambo ikapigwa kijijini Isaki wote wakakusanyika kwa mfalme ,hapakuwa na isaki alosalia katika kijiji kile
Walikuwa jumla ya vijana 25 wenye jina lile, hawakujua sababu ya kuitwa kwao mfalme akaanza kupita mbele ya kila kijana akimwangalia usoni akijaribu kulinganisha sura ya mtu na ya yule wa ndotoni
20 wote walikuwa siyo na sasa walibakia wa tano akaenda wa 21,22,23 ghafla akiwa kabakisha mmoja yule wa 25 akatoka nduki!
Hakufika mbali mishale ya walinzi ikatua mgongoni mwake akatua chini kama mzigo
Mfalme na washauri wake wakasogea eneo lile kumuona yule alokimbia pindi alipomuona macho yalimtoka mfalme kwa mshtuko!
Naaam alikuwa ndiyo yule isaki alomwona ndotoni!'....
KIJIJI CHA BOMOLE
Mfalme Omoti anaota ndoto ya kutisha akikimbizwa na kijana alomtambua kama Isaki katikati ya pori na mwishoe kijana yule kumuua kwa kumchoma mshale
Tafsir anayoipata juu ya ndoto hiyo inazid kumtisha ni kwamba utawala wake huko hatarini kuvunjika na maisha yake pia yapo hatarini
Anakusanya Isaki wote katika kijiji chake na kuanza kuwakagua akiwa amebakisha mmoja Isaki wa mwisho anakimbia ila walinzi wanawai kumchoma mshale wenye sumu Kali
Isaki anaenda chini
Mfalme anamsogelea na ghafla anashtuka baada ya kugundua yule ndo Isaki alomwota
Ni Isaki yule yule alouondosha uhai wake na kumfanya aishi maisha ya mashaka pindi alipozinduka katika ndoto ile yenye maana mbaya!
Maana aloelezwa na mtabiri wake kwamba ni kuanguka kwa utawala wake
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Haaaaaaaa haaaaaaaaaa" mtemi Omoti akacheka kwa kiburi akimsogelea Isaki
Isaki alikodoa macho pasina ufahamu wowote aikujulikana ni mzima au maiti lakini kwa jibu la moja kwa moja kutokana na kupigwa na mshale wenye sumu Kali ilosambaa kwa kasi katika mwili wake ni wazi Isaki hakuwa mzima
"Mchukueni na mkamtupe katika msitu wa Igamilo akawe chakula cha wanyama"
Mtemi Omoti akatoa amri walinzi wawili wakamdakua Isaki pale chini mzobamzoba wakimburuta huku nyuma wakiacha mayowe ya ndugu zake
Wakamfikisha katika msitu ule na kumtupa katikati ya vichaka wakitegemea baada ya wiki kadhaa kuja kutafuta fuvu kwa ajili ya ushahidi kwamba Isaki alikufa!
Huku nyuma aman kwa mtemi Omoti ikarejea
Ila wiki ilipokata walinzi wale waliporudi katika msitu ule kutafuta fuvu la Isaki alikuonekana
Wakarudi kwa mfalme kutoa taharifa mfalme alichanganyikiwa akawakusanya tena Isaki wote lakini Isaki yule akuwepo!
Kaenda wapi?!......
Mfalme akazidi kujiuliza, mtabiri wake alimdhibitishia kupitia bao alompigia kuwa Isaki yupo hai ila aikujulikana yupo mahala gani!
Msitu ule ukachunguzwa , nyumba hadi nyumba vijiji vya jirani! Ila Isaki akuonekana
mwisho mfalme Omoti ikabidi akubaliane tu na hali halisi ila alijiongezea ulinzi Mara dufu!
***
ILIVYOKUWA KABLA YA KUUWAWA KWA ISAKI
Kilikuwa ni chumba kilichoezekwa nyasi ,katika kitanda cha ngozi juu alilala kijana alokuwa kifua wazi chini alivaa majani!
Yalikuwa ndo mavaz yao ya asili
Ghafla kijana yule akasikia kama mlango unafunguliwa na mtu akiingia alichofanya ni kugeuza shingo tu kumtazama yule alokuwa akija
"Funga mlango Sendaye!"
Kijana yule akatamka kwa sauti ya taratibu , binti yule akarudi kufunga mlango akapanda kitandani!
"Isaki mpz wangu nahis mfalme ameanza kuhis kitu juu yetu"
Binti yule akaongea akinong'ona kama vile kuna mtu jirani yao asiwasikie kumbe walikuwa wawili tu, Isaki akashtuka akaguguma kwa ujasiri kuuliza hakutaka kuonekana si jasir kwa binti yule japo ukweli moyoni aliogopa
"Sendaye malkia wa moyo wangu kwa nini unahis ivyo"
"Jana kanambia ameota ndoto unamuua...."
Isaki akacheka....
"Haaaaaaaaaa na ntamuua kwel yeye ndo kawaua wazaz wangu aitawale bomale kakuchukua mpz wangu kwa nguvu kukufanya mke wake Leo nimuache ipo siku ntamuua"
Sendaye akaachia tabasamu
" mpz nimefurah kwa ujasir wako lakin tafadhal nakuomba kesho asb toroka nenda kijiji cha mbali mambo yakitulia urudi mpz"
"Kwani kwenye hiyo ndoto kakubainishia sura yangu?!"
"Hapana ila amesema kesho atakusanya isaki wote na wasiwasi atakugundua isaki wangu tafadhal ondoka nenda mbali mume"
"Sawa sawa nimekusikia"
Wakalala,
Asubuh kijana yule Alizinduka alishtuka kutomkuta Sendaye akakumbuka alipoambiwa aondoke asb hiyo....
'Hapana siwez kuondoka katika ardhi ya mtwa baba,mtwa babu babu wa babu wa babu yangu nitakuwa si jasiri si kasema katika ndoto antambui nitaenda kitakachotokea na kitokee!...
Isaki akazidi kuweka kiapo na kweli akatoka na kwenda!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Watu walifurika katika uwanja Mkubwa kijijini pale wakaambiwa Isaki wapite mbele Isaki naye akatii akapita mbele na kukaa mwisho
Mfalme akaanza kukagua mmoja mmoja kadri alivyozidi kufikiwa ndivyo alivyozidi kuwa na wasiwasi alipobakia mmoja akaona hapaaaa da ntakamatwa si ndo akakimbia kabla mshale ijatua katika mgongo wake
Isaki akaporomoka chini!
Kwa amri ya mfalme baada ya kumgundua ndo yeye alomwota akaamrisha akatupwe katika msitu ule mnene
Aliwe na wanyama walinzi wakafanya ivyo....
'Ubishi wako ndo chanzo isaki ungenisikiliza usingekufa ona Leo hata mfupa wako ujaonekana'
Sendaye akiwa kitandani kamkumbatia mfalme aliwaza mwenyewe moyoni alikuwa na majonzi tele kumpoteza Isaki mwanaume alompenda
***
BAADA YA MIAKA SABA
JIJINI BAMALA
Dk Livingstone Kendraid alikuwa kaketi na jopo la madaktari wenzake macho yao yakiwa bize kuchanganya makemikali katika mahabara yake ndogo iliyopo nyumbani kwake!
Walikuwa katika utafiti wa dawa mbalimbali wakijaribu kuitafuta dawa ya gonjwa hatari oma ya madege ilozuka toka miaka tisa nyuma na mpaka sasa iliua maelfu ya watu katika nchi ile kwa ujumla bila kupata ufumbuzi
Oma ya madega ulikuwa ni ugonjwa uloambukizwa kwa njia ya hewa sasa taifa la kinte lilikuwa katika simanzi kubwa madaktar na wanasayansi wakubwa duniani walikuwa wakiungana kutafuta dawa au kinga tu ila ndani ya miaka tisa hiyo tangu kuzuka kwa ugonjwa huo hapakuwa na ugunduzi wowote ulogunduliwa
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya jopo lile kushindwa katika utafiti wao ule wakatoka katika mahabara ile kila mmoja akiwa amenuna mpaka katika laibrary kubwa wakaket katika meza kubwa yenye mavitabu kadhaa juu yake wakaanza kuyafungua
"Daaaaaah nimechoka miaka kibao nimeumiza kichwa juu ya dawa hii mwishoe inageuka sumu badala hitibu inaua"
Dk Livingstone aliongea kwa uchungu machoni pakiwa na ishara ya machozi
"Ishu kubwa naona ni hiyo trocity tuloimix ndani humo imegeuza hiyo systeric kutoka kutibu na kuwa sumu conc tutoe hiyo trocity tujue tutaichanganya na nini?!....
" bwana eeeeeeeh nyie wana sayansi vipi?!....
Ghafla wakashtushwa na sauti nyuma yao wote wakageuka sauti ilipotokea
Alikuwa ni kijana mrefu alofanana na dk Livingstone kila kitu ukuitaji kuambiwa kwamba huyo ni mtoto wake pekee
"Amuoni huku ni laibrary na sheria ya library ni kimya nyie mwapiga makelele si mkajadiliane huko maabara?!"
Kijana yule akiwa katika kiti cha peke yake akipitia kitabu kimoja akatoa malalamiko yake watafit wale ambao wote walikuwa ni wazungu wakatazamana
"Samahani mwanangu Jemes sikujua kama upo humu!"
"Ukujua nini baba lakini...."
James akaonekana kulalamika zaid
"Haaaaaaaa unajua wale panya wagonjwa wote wamekufa baada ya kuwanywesha ile dawa...."
Jemes akaachia kicheko!
Akanyanyuka eneo lile na kuwafata huku akiongea kwa majidai!
"Nilisha waambia kabla mkiichanganya hiyo trocity katika systeric inageuka kuwa sumu mkabisha mnaona sasa baba!"
"Nimekuamini mwanangu basi nakuomba tuungane tena kama awali kupata ufumbuz wa ili"
"Maneno si ndo hayo sasa"
Jemes aliitika akivuta kiti chake na kukaa ,usoni akiachia tabasamu zito
James ndiyo alogundua hiyo systeric kutoka katika mti wa mwarobain ambao ukimlambisha au kumlisha mwenye ugonjwa wa homa ya madega upunguza kwa kiasi kikubwa homa hiyo japo aiponyi
Baada ya kugundua akamwonesha baba yake aliye igeuza kidonge ikawa kama kidonge cha kupunguza makali sasa walikuwa wakiendelea kutafiti waongezee nini kupata dawa halisi ya kuponya
Baada ya majadiliano yale kukamilika wanasayansi wale wakaaga kwenda zao wakihaidi kesho kurejea kuendelea na utafiti wao nyumbani akabaki dk Livingston Kenrady na mke wake bi nice wistorn na mtoto wao James Kenrady
Walikaa katika meza moja familia ile ya kizungu watatu wale wakiendelea kupata chakula, ila moyoni mwa dk Livingston hapakuwa na amani kabisa!
Kushindwa kwa utafiti wake na kusababisha vifo vya panya ilimuumiza sana mtoto wake James akalitambua hilo!....
"Baba laiti kama ungeniruhusu nirudi kijijini Bomole ningeleta ile dawa tukaichanganya kwanza hata bila kuichanganya ni dawa tosha kwa nini unashindwa kuniamin baba sitoweza kugundulika kule!"
James aliongea kwa kujiamin akiwatazama wazazi wake kwa umakini ,baba na mama wakatazamana mawazo yao yakaenda mbali......
MIAKA SABA NYUMA
NCHINI MAREKANI
Ni miaka mitano sasa tangu bwana Livingstone na mke wake bi nice kufunga ndoa lakini awakubahatika kupata mtoto ilo lilikuwa nipigo kubwa kwao!
Ukweli walipendana na kila siku waliomba kupata mtoto ila aikuwezekana na matatizo Yalikuwa kwa bwana Livingstone mwenyewe alofanya siri yeye na mke wake
Mke wake akakubali kubeba gunia la lawama kwa wakwe na wifi zake angefanyaje kikubwa kilichompa ujasiri ni Upendo wa mume wake walijua ipo siku Mungu angewapa neema
Manyanyaso yalipozidi ilibidi dk Livingston na mke wake wahame marekani na kuamia nchini Kinte
Huko alifungua hospital yake kubwa na kuendelea na utafiti wake kama kawaida!
Siku zikasonga mpaka ulipokuja kuzuka ugonjwa wa ajabu oma ya madega akaacha utafiti wote alokuwa akifanya na kuamia katika ugonjwa huo!
Watu walizidi kufa,pasina kupatikana kinga wala tiba ,ikawa kazi ya dk Yule kijana kuzunguka pori kwa mapori kutafiti miti mbalimbali mpaka akajikuta ndani ya msitu mzito wa pande!
Msitu aliotupwa Isaki na walinzi wa mfalme Omoti dakika chache kabla ya kuwasili kwake
Akampa huduma ya kwanza na kumpaka baadhi ya madawa alokuwa nayo akamnyanyua na kumpakia katika gari yake muda huo huo akaliondoa gari kwa kasi mpaka jijini Bamala palipo hospital yake!
Tiba mujarabu ikiwa chini yake ikaanza Mara moja hatimaye Isaki akarudia hali yake ya kawaida akamwelezea kila kitu dk yule ambapo alistaajabu kwa akili za mfalme Yule!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Isaki akaomba abadilishwe ngozi kusudi siku akitaka kurudi bomole asitambulike awali dk alikataa ila baada ya mke wake pia kumshawishi akakubali na kupandikizwa ngozi nyeupe ( ya kizungu ) juu ya ngozi yake ya asili wakambadilisha na jina wakampa jina James kwa kuwa ngozi ile ilifanana sura na ya dk Livingston kila mtu alitambua ni mtoto wake wa kumzaa ,dk Livingston na mke wake nice walimpenda sana Jemes
Jemes akatafutiwa mwalimu wa kumfundisha English akaianza kozi hiyo Mara moja akisaidiwa pia na wazazi wake wale walozijua lugha zote mbili kiswahili lugha ya taifa la Kinte na lugha yake ya kingreza
Ndani ya wiki tatu tu James ( isaki) akakijua kingreza cha kuongea na kuandika akapelekwa chuo na kusomea kidogo maswala ya utafiti ( laboratory madacine) kilichokuwa katika hospital ya baba yake na kilichomilikiwa na mama yake
James akawa si Isaki tena wa kule kijijini huyu alikuwa ni James mpya ,japo kumbukumbu za kijijini azikumtoka juu ya kulipiza kisasi kwa mfalme Omoti
Pia juu ya kuwa na Sendaye malkia wa moyo wake
Baada ya miaka kadhaa James kukuwa kitafiti alihitaji kurudi kijijini kwa kuwa kule alizitambua dawa nyingi za kiasili ikiwemo pia hiyo ya oma ya Madega
Japo alishazisahau lakini alijua akienda angezikumbuka tu! Dk Livingston akamkatalia akutaka mtoto wake Yule aingie katika matatizo japo alikuwa katika sura ingine
Hasa juu ya udhaifu alokuwa nao juu ya Sendaye kwa vyovyote angemwachia lazima angeingia katika matatizo tu!
Akutaka hilo limtokee mtoto wake pekee alomchukulia Kama mrithi wake
"Plzzzz baba niruhusuni tu dawa ile ipo japo nimeisahau lakin niamini mama niombee kwa baba anruhusu"
Isike alizidi kuomba machozi yakimlenga lenga,mama yake bi nice akuongea kitu
"Baba nakuhaid sitokuwa na Sendaye wala sitomkaribia kwa kuwa ndo uoga wako nitafata kitakachonipeleka kule baba niamin mzazi Wang!...
" baba James....
Bi Nice akaita, Isaki na baba yake wakamtazama bi Nice naye akaendelea...
"Kuna vijana saba katika idara ya utafiti hapa chuoni wameleta maombi nao wanataka kwenda huko kijijini kutafiti dawa hiyo nami nimewaruhusu kwa nini tusimruhusu mtoto akaungane nao?!....
Katika hospital ile ya dk Livingston pia Kilikuwa na chuo cha utaft kilichosimamiwa na mke wa Livingston bi nice kama mkuu wa chuo siku chache tu alipokea ombi kwa wanafunzi wale ambao wote walikuwa ni wa Kinte yani waswahili
Dk Livingston hakuwa na kikwazo tena Kama mama kakubali kivipi yeye aendelee kukataa?!
" basi sawa mke wangu James jiandae we ndo utakuwa kiongozi wao mkutanishe na hao wanafunzi kesho kutwa waianze safari ,mwisho James nakusihi sana fata kinachokupeleka nadhani unautambua ukatili wa mtemi wako kaa mbali na mke wake Sendaye sawa?!...."
"Sawa baba"
Isaki akajibu japo moyoni aliapa kufanya kitu kwa Sendaye na mfalme Omoti ikibidi kufanya ivyo!
Kesho Yake akatambulishwa kwa wenzake na maandalizi yakaanza Mara moja!....
*****
KIJIJI CHA BOMOLE
Ile ndoto mfalme Omoti aloota usiku huu ilijirudia tena vile vile kama awali akiwa katikati ya msitu pande akikimbizwa na Isaki na mwisho kuchomwa mkuki wa mgongoni
Ghafla akashtuka!
"Mume wangu ni nini...."
Sendaye akamuuliza kwa mshangao
"Ile ndoto imenirudia mke wangu Isaki ameniua"
Sendaye akashtuka,ni miaka mitano sasa imepita toka aote ndoto ile na kukamatwa kwa isaki na kutupwa katikati ya msitu pande
'Ina maana isaki bado yupo hai?!'
Sendaye akawaza!,hapana! Hakukubaliana na jambo hilo kama Isaki angekuwa hai lazima angemtafuta miaka yote hiyo au ina maana aliondoka katika kile kijiji na sasa ndo amerejea?!
Sendaye akaachia tabasamu ambalo kutokana na Giza lililoshamiri chumbani mule mtemi Omoti wala akuliona tabasamu lile
"Usijal mfalme wangu lala kesho utamuelezea mtabiri atajua nini maana ya ndoto hiyo nahis huyo kijana yupo hai"
"Hata Mimi malkia wangu hisia zangu zinantuma nihisi ivyo ivyo lazima tufanye kitu haraka...."
Wakazidi kushauriana na hatimaye mwisho wakalala wakiwa wamekumbatiana!
***
Siku ilofatia ndo siku ambayo watafiti wale nane waliianza safari!,jijini Bamala na kijijini bomole hapakuwa na umbali Mkubwa sana ivyo ndani ya masaa mawili walitegemea kuingia ndani ya kijiji kile
Isaki akionekana wazi kuwa na uchu wa kumuona Sendaye
Mfalme Omoti alimweleza kila kitu mtabiri wake juu ya kujirudia kwa ndoto ile!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Isaki yupo hai mfalme na kuoteshwa ndoto hiyo na mizimu yenu ni kujulishwa kuwa Makini na inaonesha ndani ya miaka yote hakuwa hapa kijijini na sasa yupo njiani anakuja kwa ushauri tu mfalme kusanya jeshi lifanye msako kabla ya kutimia kwa ndoto hiyo!"
Mfalme Omoti muda huo huo akakusanya jeshi lake akaweka ulinzi imara katika mipaka ya nchi yake ,msako ukaanza Mara moja nyumba kwa nyumba misitu na hata vijiji vya jirani!
Wakati msako ule ukiendelea ndo kwanza gari ilowabeba Isaki na wenzake ilizidi kukata mbuga kukifikia kijiji cha bomole!,pasina kujua hatari wanayoenda kukumbana nayo!....
*je ni hatari gani hiyo?!, mfalme Omoti atafanikiwa kumkamata isaki na vipi kuhusu isaki ( James) atatambulika na Sendaye*
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment