Search This Blog

SHAMBA LA URITHI - 2

 







    Simulizi : Shamba La Urithi

    Sehemu Ya Pili (2)





    *************************



    upande mwingine,,kule kwenye nyumba ya bibi na babu yao Pamera,,,,walionekana wadogo zake Pamera wakipukuchua mahindi..kutoka kwenye magunzi.....

    waliifanya kazi hiyo kwaasaaachache..hatimae wakapata mahindi ndoo tatu kubwa....wakafirahi sana..Pamera akawatazama wadogo zake kwa macho ya huruma..kisha akasema,,"nawapenda sana nawasihi...muishi kwa upendo huu huu pendaneni kama mimi ninavyowapenda..pia msisahau kusali na kumuomba Mungu kila wakati....tuishi kwa maadili mema kama walivyotulea wazazi wetu.

    nawaahidi tutavuna mahindi...tutauza..tukilata pesa nataka muanze kusoma,,nitawapeleka shule.

    kauli hiyo ya Pamera ikatengeneza faraja kubwa ndani ya mioyo ya wadogo zake..wakanyanyuka na kumkumbatia dado yao...katika uzawa wa familia yao,,walizaliwa wasichana sita na mvulana mmoja ambaye anafatana na Pamera....mtoto huyo pekee wa kiume anaitwa KABI..kabi alijitahidi sana kuwalinda wadogo zake,,kipindi dada yao Pamera akiwa kwenye vibarua......

    Pamera akachukua ndoo moja iliyokuwa na mahindi ndani yake akajitwisha kichwani akazipiga hatua kuelekea kwenyeashine ya kusaga ambayo ipo kijiji cha jirani.



    ******************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine alionekana Jazi..akizipiga hatua za haraka haraka..huku mguu wake mmoja ukiwa na kiatu,,na mguu mwingine akiwa peku....hakujua kiatu kilitoka wakati gani...akajitazama lakini hakujali...alizidi kusinga mbele...kumbe Jazi alikuwa anakwenda kule kwenye Milima ya DONGOBESHI kwa yule mganga!!....

    kwa sababu alikuwa anatembea kwa miguu..Jazi alitembea masaa mengi mfululizo...ilipofika saanane za mchana akafika kwenye milima ya Dongobeshi...akazipiga hatua mpaka kwa mganga.

    alipofika akaeleza shida yake...mganga akasema...umekosea masharti,,,na umebakiza siku chache za kuishi hapa duniani...kwa sababu mzimu wa mzee Joram hautokuacha hai...

    Jazi akaingiwa na hofu akasema,,"naomba unisaidie mganga....

    mganga akasema,,"bado nafasi unayo...sasa inahitajika kafara la damu mbichi ya uzawa wa familia ya Mzee joramu...namaanisha damu hiyo itamwagwa katikati ya shamba hilo juu ya kaburi la mzee Joram.....na nilazima damu hiyo iwe ya mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia hiyo..kisha utachimba shimo na kuzika maiti hiyo humo shambani..

    Jazi akahisi kuchanganyikiwa baada ya kuyasikia maneno ya mganga huyo....akasema,,"sawa mganga nitafanya hivyo....akanyanyuka na kuzipiga hatua...



    mganga akasema,,"bado sijamaliza..chukuwa dawa hii...huu ni unga wa nyama ya binadamu iliyokaushwa kwa moto...na kusagwa...ukachanganywa na mizizi ya miti mbalimbali..

    dawa hii utakoroga kwenye kikombe utakunywa kabla ya kufanya kafara....na ukishameza maji yake...haitakiwi upoteze hata sekunde moja...kisha utamuingilia kimwili,,,na kuchinja shingo yake..na kama ni wakiume utamkata nyeti zake kisha utachinja shingo yake.....hakikisaha unachinja shingo yake ndani ya sekunde kumi tu..na ikizidi hapo..basi litatokea tatizo kubwa ambalo litasababisha mizimu ichukue uhai wangu mimi....usikosee masharti.

    Jazi akaipokea dawa hiyo iliyokuwa imefungwa kwenye kipande cha ngozi ya mnyama Fisi.

    Jazi akaondoka  kurudi nyumbani kwake...

    akiwa njiani akawa anapanga mikakati ya kumnasa Pamera..kwa sababu Pamera ndiye mtoto wa kwanza kuzaliwa......akajisemea moyoni,,"itabidi kazi hii niifanye leo leo...aliyasema maneno hayo huku akizipiga hatua za harakaharaka kusonga mbele.

    Jazi alitembea umbalirefu hatimae akaanza kuingia katika ardhi ya kijiji chao...



    ************************



    upande mwingine alionekana Pamera akiwa kabeba ndoo kichwani akitokea mashineni kusaga unga......alikuwa tayari kashatoka kijiji cha jirani...na sasa anatembea kwenye ardhi ya kijiji chao.....kumbe njia anayopitia ndio njia ambayo inakutana na ile njia anayopita Jazi....ghafla wakakutana uso kwa uso....Pamera akamsalimia baba yake mkubwa..lakini hakuitikia..

    Jazi akaangaza macho yake huku na kule..kisha akamtazama Pamera kwa macho ya kutaka kufanya jambo fulani!!!  Jazi akazipiga hatua kumfuata Pamera...



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pamera akaingiwa na hofu,,kwa sababu aliona ujio wa baba yake mkubwa sio wa kawaida!

    Pamera akaanza kurudi nyuma....

    Jazi akaongeza kasi ya kutembea..huku macho yake yakionyesha kuwa kakusudia kufanya jambo fulani!!!

    Pamera akaishusaha ndoo kutoka kichwani akaiweka chini,,akatimua mbio bila kugeuka nyuma...Jazi akaanza kumkimbiza Pamera...

    Pamera akaamua kukimbilia vichakani huku akipiga kelele,,lakini kelele hizo hazikumsaidia chochote....akajikuta anatokezea kule kwenye shamba la marehemu baba yake..akaingia ndani ya shamba hilo na kujificha....



    Kwa mbali alionekana Jazi akiangaza angaza macho yake huku na kule..lakini hakujua ni wapi Pamera kakimbilia!

    Jazi hakukata tamaa akaendelea kumtafuta Pamera...akazipiga hatua akatokezea kwenye lile shamba la marehemu mdogo wake....alipotazama chini akaona nyayo za miguu..akatabasamu,,akajisemea moyoni,,"kumbe hayupo mbali na maeneo haya! bila shaka atakuwa kajificha ndani ya shamba hili...kwanza kanirahisishia kazi,,kwa sababu nilikuwa natafakari jinsi ya kuleta kwenye shamba hili.....

    Jazi akaokota mawe kadhaa na kuanza kuyarusha shambani  ovyo ovyo bila mpangilio....

    ghafla akasikia sauti ya Pamera akilia kwa sauti kubwa!! ,,"MUNGU WANGU NAKUFA!!

    Pamera alitoa sauti hiyo..kutokana na maumivu makali aliyoyapata kichwani! ni baada ya kupondwa na kitu kigumu kichwani mwake..

    kumbe yale mawe aliyokuwa anayarusha Jazi kwa mfululizo...moja ya jiwe kati ya mawe hayo,,lilimponda kichwani...akapata jeraha..



    *****************



    Wakati huo huo alionekana Jazi akiingia ndani ya shamba hilo ili akamnase Pamera na kufanya kile alichoagizwa na mganga....

    Hazi kabla hajaingia ndani zaidi ya shamba hilo..akamuina Pamera kadondoka chini kapoteza fahamu huku damu zinamtoka kwenye utosi!! akamfuata haraka,,bila kuchelewa akamvua nguo harakaharaka akasimama na kuvua suruali yake ili amuingilie kimwili Pamera..kabla hajafanya hivyo,,ghafla Pamera akazinduka, akapata fahamu..akashtuka kumuona baba yake mkubwa akiwa kadimama mbele yake huku suruali ikiwa kwenye usawa wa magoti...na nyeti zake zikionekana vyema...Pamera akaingiwa na roho ya ujasiri baada ya kugundua kuwa Baba yake mkubwa hana nia njema...akanyanyua mguu wake kwa nguvu na kukanyaga nyeti za baba yake  mkubwa!!

    Jazi akahisi maumivu makali kupita kiasi akadondoka chini huku kashikilia sehemu zake za siri...

    Pamera akapata upenyo wa kukimbia..akanyanyuka haraka na kutimua mbio..

    Pamera alikimbia kama anakimbizwa na mnyama mkali!



    alikimbia mwendo wa dakika kadhaa akawa amekaribia kufika nyumbani...akageuza shingo yake lakini hakumuona baba yake mkubwa! akaendelea kutimua mbio mpaka nyumbani..akawakuta wadogo zake wanacheza..akapaza sauti,,"CHUKUENI NGUO ZENU HARAKA!!!

    wadogo zake Pamera wakastaajabu!! wakabaki wanamtazama dada yao kwa mshangao!!!

    Pamera akaingia ndani ya nyumba...akawaita wadogo zake...wakakusanya nguo zao wakaziweka kwenye begi la marehemu bibi yao,,wakatoka nje ya ya nyumba wakatokomea kusikojulikana.....

    wakati huo Kabi hakuwepo nyumbani,,ni yule mtoto pekee wa kiume katika familia ya marehemu Joram.....Kabi alikwenda porini kukata kuni kwa ajili ya kupikia chakula...



    **********************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine kule porini,, alionekana Kabi.akiwa ameshililia panga anakata kuni...alipomaliza akazikusanya na kuzifunga kamba..akazibeba na kuianza safari ya kurudi nyumbani....alitembea mwendo nusu saa mfululilozo, hatimae akafika nyumbani.....akastaajabu kutokuwaona wadogo zake....akaamua kwenda kule kwenye mto kwa kudhani kuwa wameenda huko kuteka maji!!

    lakini alipofika huko hakufanikiwa kuwaona!!

    akajiuliza,,"inamaana watakuwa wamekwenda wapi? wacha nirudi nyumbani.



    wakati huo huo alionekana Jazi akitokea kule shambani ni baada ya maumivu kupungua...akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwake....lakini kichwani mwake alikuwa anawazo moja tu, akawaangamize wadogo zake Pamera,pamoja na Pamera mwenyewe...



    *******************



    Upande mwingine alionekana Pamera poja na wadogo zake wakikimbilia ndani ya msitu..ghafla Pamera akasita..akasimama! akakumbuka kuwa mdogo wake hayupo pamoja nao. ambaye ni Kabi.

    Pamera akawaingiza wadogo zake ndani ya kichaka akawaambia,,"hakikisha hamtoki hapa pasipo mimi kurudi..nawaahidi nitarejea mda mchache ujao,wacha nikamfate Kabi..nawapenda sana wadogo zangu..Pamera aliongea maneno hayo huku akiwatazama wadogo zake kwa macho ya huruma...kisha wakafanya sala fupi,wakimuomba Mungu awaepushe na jambo baya lolote linalowazonga.

    Pamera akanyanyuka akatoka kichakani na kutimua mbio kurudi nyumbani kumfuata Kabi..



    **********************



    Upande mwingine alionekana Kabi akizioiga hatua kuelekea nyumbani,,lakini alikuwa na wasiwasi kuhusu wadogo zake..akajisemea moyoni,,"hii ndio mida ya dada Pamera kurudi nyumbani atanigombeza asipokuwakuta watoto...kwa sababu alisema niwe nawaangalia na kuwalinda muda wote yeye anapokuwa kwenye vibarua.

    wacha niwahi kabla hajafika nyumbani...

    Baada ya dakika kadhaa Kabi akafika nyumbani..

    ghafla akakutana uso kwa uso na Jazi!

    Jazi akajisemea moyoni,"wacha nianze na huyu wa kiume..hao wa kike hawanishindi kitu chochote.

    Kabi akamsalimia baba yake mkubwa...Jazi akaitikia salamu...Kabi akamkaribisha ndani..wakati Kabi anazipiga hatua kuingia ndani..Jazi akavua mkanda wake wa siruali akamkaba mtoto Kabi kwenye shingo kwa kutumia nguvu zake zote.... Kabi akaanza kutapatapa kupigania pumzi..punde si punde Pamera akafika nyumbani akamuona baba yake mkubwa anamuangamiza Kabi!! Pamera akaangaza angaza macho yake akaona mzigo wa kuni..akachukua kipande kimoja kilichokuwa kinene kiasi..akampiganacho Jazi kisogoni...Jazi akadondoka chini..akaanza kutetemeka kama kapigwa na shoti ya umeme..damu zikaanza kutoka masikioni na puani....akatulia tuli...ghafla ikasikika sauti ya mtu akipiga hodi...Pamera akachanganyikiwa..akamuinua kabi haraka wakatoka nje..wakakutana uso kwa uso na shangazi yao..ni yule aliyewanyang'anya nyumba ya marehemu baba yao...Shangazi yao akashtuka kumuona kaka yake amelala chini huku damu zinamtoka puani na masikioni...akamkamata Pamera....Kabi akachoropoka akatimua mbio.kwa kuhofia huenda shangazi yao naye amekuja kuwaangamiza....Kabi alikimbia na kutokomea kusikojulikana..

    shamgazi yake Pamera akapiga simu kwenye kituo cha polisi...bila kuchelewa maaskari wakafika..walipomtazama Jazi tayari alikuwa ameshakufa dakika chache zilizopita. ...wakamkamata Pamera..wakaondokanae mpaka kwenye kituo cha polisi..





    Pamera akashtakiwa kwa kosa la mauwaji..akawekwa maabusu bila mdhamana ,mpaka uchunguzi utakapokamilika.

    Pamera alisikitika sana akalia kwa uchungu! kilichokuwa kinamuumiza zaidi..ni wale wadogo zake aliowaacha kule porini mafichoni!!

    Pamera akajaribu kujitetea lakini ikashindikana,,hakuna mtu aliyeweza kumuelewa.

    Shamgazi yake Pamera akafurahi sana....akaongea uwongo kuwa Pamera alitaka kumuuwa pia...



    ********************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilipofika majira ya jioni..walionekana wadogo zake pamera wakiwa bado wamejificha kule kichakani!

    wakaanza kuhisi njaa kali..pia wakaingiwa na wasiwasi,kwa nini mpaka sasahivi dada yao hajarudi kama alivyowaahidi kuwa amekwenda kumfata Kabi...

    watoto wasiyokuwa na hatia waliendelea kuvumilia kwa kumsubiri Pamera......masaa yalizidi kusonga hatimae giza likaanza kuingia...wawaamua kutoka ndani ya kichaka hicho wakatembea huku wakiwa na uwoga wa hali ya juu..kutokana na miti mikubwa iliyokuwa ndani ya pori hilo....walizipiga hatua huku wameshikana mikono kwa pamoja wakiwa wanalia....wakajikuta wametokezea barabarani...walipoangaza angaza macho yao wakaitambua sehemu hiyo..haikuwa mbali na nyumbani..wakaamua kurudi nyumbani.....walipokaribia nyumbani...kwa mbali wakaona moto unawaka nyumbani kwao..wakabaki wamesimama huku wanalia wakishuhudia nyumba ya marehemu bibi yao inateketea kwa moto...

    kwa sababu nyumba hiyo iliezekwa kwa nyasi kavu..moto uliwaka kwa kasi ya ajabu....mpaka ikateketea....Mmoja kati ya watoto hao..akamuona mwanamke akiaa amesimama kwa mbali...kishawanamke huyo akazipiga hatua..na kuondoja zake....yule mtoto alimtambua mwanamke huyo kuwa ni shangazi yao!! kwa sababu mtoto huyo alikuwa na upeo kiasi kuliko wadogo zake ambao ni wadogo kushinda yeye!! akawa amegumdua kuwa ,,shangazi uao ndio kahusika kuichoma moto nyumba yao!

    akawaambia wadogo zake,,"tuondokeni...wadogo zake wakamtazama kisha wakamuuliza,,"sasa tutaenda wapi? kwani dada Pamera yuko wapi? kwanini tusimfate tukamwambie nyumba yetu inaungua? walibaki wanatazamana kwa sababu hakuna hata mmoja kati yao ambaye angeweza kumsaidia mwenzake kutokana na umri mdogo waliokuwa nao....wakaamua kuzipiga hatua bila kujua ni wapi wanaelekea....



    ***************************



    Upande mwingine alionekana Kabi akiwa ndani ya nyumba ambayo haijamaliziwa ujenzi,,Kabi aliingia ndani ya nyumba hiyo tangu mchana..kwa lengo la kujificha kwa sababu alinusirika kunyongwa na baba yake mkubwa..Kabi alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa kupita kiasi..hali hiyo ikamfanya achanganyikiwe.....masaa yalizidi kusonga..akaanja kuhisi njaa kali!! akaamua kutoka ndani ya nyumba hiyo. akazipiga hatua kurudi nyumbani kwao...akatazame huenda dada yake amesharudi nyumbani....

    wakati huo Kabi alikuwa hajui kuwa dada uake yupo kwenye kituo cha polisi..kwa sababu yeye alikimbia na kumuacha Pamera akiwa kakamatwa na shangazi yao...

    Kabi alizidi kusonga mbele..akasita kutembea akaamua apite njia ya bondeni inayotokezea kwenye mto

    alitembea mwendo wa dakika ishirini mfululizo..akatokezea mtoni...akazipiga hatua kulifuata daraja lililopita juu ya mto huo..alipofika katikati ya daraja hilo, akatereza akadondoka na kudumbukia ndani ya mto.......maji ya mto yalikuwa yanapita kwa kasi ya ajabu kuelekea bondeni kwenye korongo!! Kavi alipiga kelele lakin hakupata msaada wowote...mto huo ulikuwa mkubwa pia sehemu aliyotumbukia ilikuwa na kina kirefu.....maji yalimsomba Kabi na kumpeleka kwa kasi...maji yakamzamisha Kabi..akafanya jitihada za kujiokoa arudi upande wa juu ya maji..akafanikiwa..ghafla akajigonga kwenye jiwe upande wa kichwani akapoteza fahamu...maji yakamsomba na kumtupa kwenye korongo..



    *************************



    Upande mwingine walionekana wale watoto watano ambao ni wadogo zake Pamera...

    watoto hao walishindwa kuvumilia njaa kali iliyokuwa inasumbua matumbo yao..wakaamua kuingia kwenye shamba la mwanakijiji katika kijiji hicho...wakachuma mahindi na kuanza kuyatafuna hivyohivyo yakiwa mabichi....kutokana na njaa kali waliyokuwanayo waliyaona ni matamu....wakaendelea kuyatafuna kwa pupa...walipohisi wameshiba wakaamua kujilaza ndani ya shamba hilo!!!



    ********************



    Asubuhi palipokucha...alionekana Pamera akipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka ya kosa la kuuwa...Pamera alijitetea lakini hakuwa na ushaidi ambao unathibitisha kuwa Marehemu alikuwa anataka kufanya mauwaji kwa mdogo wake!! Shangazi yao akatoa ushahidi wa uwongo mbele ya mahakama..akithibitisha kuwa alimkuta Pamera anampiga baba yake mkubwa kichwani kwa kizito...alipojaribu kutoa msaada Pamera akataka kumuangamiza pia..ndio akaamua kutoa taarifa katika kituo cha polisi!!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakimu alisikiliza maelezo ya pande zote mbili..lakini maelezo ya Pamera yakaonekana kuwa ni ya uwongo....hakimu akaamua kutoa hukumu..kuwa Pamera afungwe ,,atumikie kifungo cha maisha Gerezani....Pamera akahisi kuchanganyikiwa akaanza kuangua kilio! alilia kwa uchungu mkubwa usiokuwa na mfano...

    watu waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo..walisikitishwa sana na hukumu hiyo lakini hawakuwa na namna kwa sababu hakimu ndiye muamuzi wa mwisho.



    **********************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog