Search This Blog

SIKU 100 ZA MATESO YA KUZIMU - 2

 







    Simulizi : Siku 100 Za Mateso Ya Kuzimu

    Sehemu Ya Pili (2)





    Amosi alianza kutimua mbio kurudi kule alikowaacha wenzake, tendo lile wakati linafanyika huku nyuma vile vicheko vya watu wasionekana viliibuka tena.

    Wakati anazidi kukimbia ile sauti ya mama yake iliyokuwa ikiomba msaada ilisikika ikimwita kwa jina lake na kumwomba msaada. Amosi aliziba masikio alikwisha tambua mauzauza yale yalihusiana na majini.

    Aliendelea kukimbia bila kuchoka, Mungu si Athumani, akafanikiwa kutokezea kwenye fukwe, mahali alikowaacha wenzake.

    Alikuwa akihema huku akiwa na wasiwasi mkubwa.

    “Ni nini?..umepatwa na kitu gani?” alikutana na maswali lukuki kutoka kwa wenzake ambao aliwaacha ufukweni.

    “Kuna majini!! Nimekutana na majini...huko porini kuna majini!!” Amosi alijibu kwa wahaka, akili yake ilikuwa imepagawa vibaya sana.

    “Majini?” mtu mmoja akauliza kwa mshangao.

    “Ndio...Majini”

    “Kwa hiyo aliyekuwa anapiga kelele za kuomba msaada siyo mama yako?” Mzee William akahoji kwa kiherehere.

    “Ndiyoo.”

    Baada ya jibu hilo, wale watu walionusurika kwenye ajali ya ndege ya Panasonic Airline walibaki kimya, kila mmoja akifikiria lake ndani ya kichwa chake.

    “Nadhani kunusurika kifo kwenye ajali ya ndege ndio kumeifanya akili yako ichanganyikiwe...” Mzee William alisema.

    “Awali ulituleza mama yako ulimsafirisha kama maiti ndani ya ndege, sauti ya mtu inasikika ndani ya msitu, unasimama unasema huyo ni mama yako.

    “Unapuyanga msituni kama mwendawazimu unarejea hapa unatueleza ndani ya msutu huu kuna majini sijui vitu gani...hii si jambo la kiungwana, nadhani ulitakiwa kutulia na wenzako tukiongoja msaada. Hilo unalolifanya ni kuongeza hali ya wasiwasi kwa watu hawa ambao kimsingi wanahitaji msaada wa mwili na akili.” Alisema mzee William.

    Watu wote wakatikisa vichwa kuafiki maneno ya mzee yule. Macho ya wenzake yalimtizima kama punguani ambaye amethiriwa na Pombe.

    Amosi akaishiwa nguvu, alitamani aingie kwenye nyoyo za wale watu awaleze ukweli halisi juu ya vituko vilivyopo ndani ya kisiwa kile walichoangukia.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Unapuyanga msituni kama mwendawazimu unarejea hapa unatueleza ndani ya msutu huu kuna majini sijui vitu gani...hii si jambo la kiungwana, nadhani ulitakiwa kutulia na wenzako tukiongoja msaada wa kuturudisha katika nchi zetu. Hilo unalolifanya ni kuongeza hali ya wasiwasi kwa watu hawa ambao kimsingi wanahitaji msaada wa mwili na akili,” alisema mzee William.

    Baada kauli hiyo, Amosi akaishiwa nguvu, alitamani aingie kwenye mioyo ya wale watu awaleze ukweli halisi juu ya matukio ndani ya kisiwa kile walichoangukia. Macho ya watu wale yalimtizima kama punguani ambaye amethiriwa na Pombe, ambaye amenusrika kifo kwenye tundu la sindano.

    Kila mtu alimpuuza kwa kiwango kikubwa, alibaki amebung’aa huku uso wake ukionesha kuchanganyikiwa vibaya sana.

    Abiria wale waliketi sehemu moja kila mmoja akiwa na tumaini kubwa la kupata msaada wa siku inayofuatia, vikohozi na kwikwi za maumivu za hapa na pale zilisikika.

    Amosi naye akaketi hatua chache huku kichwa chake kikiwa kimevurugwa vibaya sana, dakika thelathini zilipita tangu kioja kile kitokee.

    Wakati huo ilikuwa yapata saa nane usiku, giza lilikuwa kubwa, hapakuwa na kilichokuwa kinasikika zaidi ya moto uliokuwa ukimalizia kunguza mabaki ya ndege ile ya Panasonic Airline, mawimbi ya bahari yaliyokuwa yakijibamiza kivivu ukingoni mwa fukwe pia yalitoa sauti ndogo.

    Kila mtu alimini hadi wakati huo hawakupata msaada kutokana majira yale kuwa ni usiku, mategemeo yao walimini siku inayofuatia ndio wakati wa ukombozi.

    Wakati mambo hayo yakipita vichwani mwao, kwa upande wa Amosi yeye alikuwa kwenye mgogoro mkubwa wa kifikra, matukio yalikuwa yamemtokea ndani ya muda mchache yaliharibu kabisa akili yake.

    Ubongo wake haukuwa kwenye suala la kuondoka, alichokuwa anakitaka kwa upande wake ni kumaliza ile sintafahamu iliyokuwa imeibuka ghafla katika msitu ule.

    Kila alipokuwa akifikiria uwezekano wa kutokea mambo yale katika maisha ya kawaida akili yake ilikuwa inakataa kabisa kukubaliana na jambo hilo.

    “Au inawezekana kweli nimechanganyikiwa!!” alijiuliza mwenyewe.

    “Hapana, sijachanganyikiwa nina uhakika wa yale niliyoyashuhudia ni sahihi kabisa” Amosi akawa kwenye mkanganyiko wa kupingana na fikra zake mwenyewe.

    Usiku wa siku hiyo, ulikuwa mrefu kwa kila mtu aliyekuwa kwenye kisiwa hicho aliona masaa yanakwenda taratibu mno, hakuna mtu aliyelihitaji giza, shauku ya kila mmoja ilikuwa ni kuona kunapambuzuka na msaada unapatikana.

    Kama wasemavyo Waswahili hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, hatimaye kukaanza kupambazuka. Kwa mbali, kile kibaridi cha asubuhi lilianza kuingia kwenye minofu ya miili ya watu wale, hata hivyo, hilo halikuwa ni tatizo kubwa kwao, walichokuwa wanakitaka kwa wakati huo ni msaada.

    Majeruhi wale walijikunyata lakini moyoni wakiwa na matarajio makubwa. Kila mtu aliamini kile kilichokuwa kikwazo kwao kuchelewa kupata msaada, kimetoweka, walichokuwa wanangoja kwa wakati huo ni kupambazuke vizuri kwa siku mpya.

    “Muda wa kupata msaada umewadia,” mtu mmoja miongoni mwao alisikika akisema, wengine wakatikisa vichwa kukubalina naye. Nyuso zao zilionekan kuwa na matarajio makubwa sana.

    Jua la asubuhi lilianza kuchomoza, kwa mujibu wa saa zao ilikuwa inaelekea kuwa saa mbili kasoro, watu wale wakasimama, shauku ya kuona helkopta ama boti za ukombozi ikawa ya juu.

    “Nadhani watakuja na Helkopta,” alisema mtu mwingine macho yake yakiwa angani kuangaza kila kona.

    Wingu na bahari vilikuwa tupu, hapakuwa na dalili ya boti wala helkopta.

    “Nitashangalia nikiona helkopta,” mwanamke mmoja alinong’ona

    “Mimi nitamshukuru Mungu” wakawa wanaambiana wao kwa wao. Hata hivyo muda ukazidi kuyoyoma bila kuona wala kusikia sauti ya helkopta ama boti

    “Tutapata msaada kweli?” mwingine aliuliza kwa mashaka.

    “Tuendelee kusubiri.” Akajibiwa na mwenziye.

    “Kweli watakuwa na taarifa juu ya kuanguka kwa Panasonic Airline?”

    “Nina uhakika taarifa zitakuwa zimekwishaenea dunia nzima.”

    “Sasa kwa nini hadi sasa hakuna dalili zozote za watu wa ukumbozi?”

    “Inawezekana wanaendelea kutafuta mahali tulipoangukia.”

    “Ni muda mrefu lakini umepita tangu tupate ajali. Na hii ni saa mbili”

    “Tuwe na subira,” alijibu mtu yule.

    Wakati wote ambao watu wale walikuwa kwenye presha ya kungoja vyombo vya ukumbozi, Amosi alikuwa ameketi kwenye mchanga akili yake ikiwa bado imechanganyikiwa vibaya mno.

    Masaa yakazidi kwenda, saa tatu, nne, tano, hadi inafika saa nane mchana, hapakuwa na dalili yoyote ya msaada.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Watu wakaanza kupatwa na njaa, wengine wenye wajeraha wakawa dhoofuli-hali, baadhi ya watu wakakata tamaa, wengine waliokuwa na roho ngumu bado waliendelea kuamini watapata msaada.

    “Amosi....Amosi..Amosi,” wakati huo huo sauti moja ilisikika nyuma ya mvualana yule, sauti hiyo ilitokea kichakani, iliita kwa kunong’ona, alipogeuka hakuamini alichokiona.



    Mama yake mzazi akiwa amesimama ukingoni mwa kichaka huku akionekana mwenye wasiwasi na mashaka, alikuwa amevalia gauni refu na la kupendeza, gauni hilo lilikuwa likiburuzika chini kiasi cha kuziba kabisa visigino vya miguu yake.

    Amosi alitambua vazi hilo ni yeye aliyelinunua masaa machache kabla ya mwanamke huyo kufariki dunia, wakati jambo hilo likiendelea kuvuruga akili yake, macho yake yakaendelea kutoamini kioja kingine kilichoibuka mbele yake.

    Mwanamke yule ambaye ni mama yake mzazi aliyekuwa mfu ndani ya ndege kabla ya kupata ajali na kuibuka kama mzimu katika mazingira yale tata, aliendelea kusimama ukingoni mwa kichaka kile huku akibadilisha mapozi kama vile bibi harusi aliyesimama mbele ya mpiga picha na kufotolewa picha zitakazopamba ukurasa wa jarida la mapenzi.

    Wakati kioja kile kikijidhihirisha kwenye mboni za macho yake, muda huohuo kumbukumbu ya mazungumzo yake ya mwisho na mwanamke yule alipokuwa hoi taabani kwenye hospitali ya St August akitaka anunuliwe gauni lile, ikamjia kichwani:

    “Nakufa..mwanangu nakufa..”

    “Usiseme hivyo mama madaktari wamesema unayonafasi ya kuishi.”

    “Hilo halitawezekana, nakuomba ufanye jambo moja.”

    “Lipi mama?”

    “Kaninunulie gauni, nataka gauni la harusi...nikifa hakikisha unanivisha gauni hilo.”

    Kumbukumbu ya mazungumzo yale ilipita kwenye kichwa chake, alibaki amemkodolea macho mtu yule aliyekuwa amesimama kwenye ukingo wa kichaka.

    Bado akili yake ilikuwa kwenye mkanganyiko mkubwa sana, hakuamini kama yale anayoyaona yalikuwa ni sahihi ama wazimu ulikuwa umeingia kichwani mwake.



    “Njooo,” mtu yule akatoa sauti tena na kumpungia mkono.

    Amosi akiwa kama teja aliyelewa na madawa ya kulevya, aliendelea kumkodolea macho yenye mshangao, akasimama na kupiga hatua kusogea kwenye kichaka kile.

    “Shika hii.” Mtu yule alisema akimpa, kipande kidogo cha mbao.

    “Wewe si ulikuwa umekufa..?” Amosi akasema akionekana kuchanganyikiwa vibaya sana, kabla ya kujibu ,lolote mwanamke yule akatabasamu ile anataka kusema kitu mara akasikia sauti ikimwita kwa nguvu nyuma yake, akageuka kutizama.

    “Unafanya nini hapo?” alikuwa ni mzee William, alisema akionekana kumshangaa.

    Amosi hakumjali, alichokuwa anakihitaji kwa wakati huo ni kuzungumza na mama yake aliyeibuka kama mzimu, hata hivyo, alipoyarudisha macho yake ili kuendelea na mazungumzo, akapigwa na butwaaa, baada ya kutomwona mama yake. Hakuweepo!!

    Tukio lile lilichukua sekunde moja ama mbili alizotumia kugeuza shingo yake kutizama mahali alipoitwa.

    “Mama wapi tena...” aliuliza Amosi akiwa kapigwa butwaa kwa kutoweka kwa mwanamke yule.

    “Kitu gani unafanya Amosi?” Mzee William akaendelea kumuuliza huku akiwa anamshangaa anavyoa haha kutafuta vitu ambavyo havieleweki.

    “Hujamwona mwanamke kavaa gauni jeupe hapa?” hatimaye Amosi akauliza kwa wahaka.

    “Mwanamke gani?....”

    “Aliyevalia gauni jeupe”

    “Hapana, hapakuwa na mtu hapo”

    “Siyo kweli, akili yangu haiwezi kunidanganya palikuwa na mtu hapa na kaniachia hiii...” akasema kwa sauti ya mahamaniko huku akimkazia macho yule mzee.

    Bado sura ya mzee William iliendelea kumtizama Amosi kwa mtazamo wa mtu aliyechanganyikiwa akili.

    “Amosi” mzee William akaita kwa upole

    “Naaam.”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwanini usijipe muda wa kupumzisha akili yako huku tukingoija msaada, labda haya maluweluwe yanayaokukumba sasa yanaweza kupungua?”

    “Hapana, niko sahihi, sina tatizo lolote kiakili....hebu niambie hiki kitu kanipa nani ili nione uhalali wa hicho unachokisema” Amosi alisema kwa sauti iliyopaniki huku akimtizama.

    Mzee Williaum akipiga kimya kidogo, kisha akatikisa kichwa kumsikitikia, akaonekana kupuuza kabisa madai ya Amosi, alichofanya ni kubadilisha mada ya mazungumzo yale, akasema:

    “Hadi sasa watu wamekata tamaaa ya kupata msaada, inaelekea saa saba mchana, hakuna dalili yoyote ya msaada, kuna wazo nimepata naamini tukilifanyia kazi linaweza kusaidia maisha ya watu eneo hili.” Alisema Mzee William, Amosi hakujibu kitu.

    “Tunatakiwa tupate chakula, hadi sasa ninapozungumza na wewe, kuna dalili mbaya ya watu kufa na njaa, lazima tupate chochote, aidha kwa kuwinda ama kuvua samaki.”

    “Kwanini mambo hayo unieleze mimi?” Amosi akauliza.

    “Kwasabu nakuona ni kijana mwenye nguvu, unayeweza kukamilisha haya kwa asilimia mia,” mzee William akajibu, Amosi akachia tabasamu dhaifu, akawa anakigeuzageuza kile kibao alichoachiwa na mtu aliyeibuka ghafla mbele yake na kutoweka.

    Wakati akifanya tendo hilo macho yake yakatua kwenye maandishi yaliyokuwa kwenye kibao kile, yalikuwa ni maandishi madogo yaliyoandikwa kwa Lugha ya Kingereza, yalisomeka hivi:

    “Find the bastard ” (Mtafute Mwanaharamu)

    Hali ile ikamfanya aduwalie kwenye yale maandishi, alijua tafsiri ya sentesi ile, lakini mantiki ya sentesi ile hakuijua.

    “Amosi vipi?” mzee William akamstua,

    “Find the bastard” badala ya kujibu akajikuta akisoma kwa nguvu yale mandishi kwenye kipande cha ubao ambacho kilikuwa bado kiganjani mwake.

    “Sikuelewi ujue?..”

    “Kitu nilichoachiwa na mtu aliyeniibukia hapa ni hiki,” alisema akimwonesha yale maandishi kwenye kile kipande cha ubao.

    Mzee William alitupa macho kwenye maandishi yale bado aliendelea kuamini akili ya mtu yule ilikumbwa na wazimu.

    “Utashirikiana na mimi kufanya niliyokueleza?” Mzee William akamwuliza huku maandishi ya kwenye kile kipande cha ubao akiyapuuza.

    “Nataka kujua kwanza maana ya haya maneno, huu ujumbe haujafika mikononi mwangu kwa bahati mbaya”

    “Kwahiyo unataka nani akuonyeshe mahali alipo huyo Bastard?” mzee William aliuliza kwa hasira, Amosi akagwaya.



    Ukapita ukimya mfupi baina yao, kila mtu akawa anatafakari uzito wa hitaji lake...Amosi alitamani aingie moyoni mwa mzee yule na amwaminishe ukweli wa mauzauza yaliyokuwa yakimtokea tangu waanguke kwenye kisiwa kile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Sina sababu ya kulumbana na wewe ama mtu mwingine yeyote ambaye haamini kile ninachowaeleza, natambua kwenye mazingira kama haya tunatakiwa kuwa kitu kimoja wakati wote, lakini nasikitishwa na namna mnavyoshindwa kuelewa na kuzingatia hisia zangu!”

    “Hatuwezi kuishi kwa kutii hisia za kila mtu, katika maisha, hukatazwi kuwa na hisia lakini usipende kila mtu afate hisia zako kama unavyotaka wewe,” mzee William aliendelea kumpasha, ukimya mwingine ukapita tena baina yao, Amosi akayagandisha macho kwenye kiubao kile chenye maandishi yaliyosomeka ‘Find the bastard’ kisha akasema:

    “Kwahiyo unataka nifanye nini mzee?”`

    “Lazima tufanya kitu ili watu wapate chakula, hali ni mbaya na hatujui msaada utakuja saa ngapi”

    “Tutafanya nini?”

    “Tuingie porini aidha tupate walau mataunda ama mnyama kama chakula”

    “Kuingia porini kwa kutafuta matunda sawa, lakini si kwa kutarajia kupata mnyama,” alisema Amosi.

    Kwa pamoja wakakubalina kuingia mstuni kutafuta matunda watakayoyatumia kama chakula.

    ******

    Wakati hayo yakitokea kisiwani, Geita Tanzania. Taharuki kubwa ilizuka kwenye familia ya mzee Mikidadi, taarifa ile ya kustua ambayo Kiba alimaliza kuisilimua, mbali ya kuwa ni mbaya lakini ulikuwa ni mkasa wa kusisimua kwenye masikio ya kila aliyepata bahati ya kusikia.

    Mzee Mikidadi aliyekuwa ameanguka akiwa hana fahamu kutokana na kushikwa na presha ambayo ilipanda na kufikia 140/110 mmHg alisababisha mstuko wa watu uongezeke mara dufu.

    Walichofanya ni kumkimbiza hospitali ya mkoa wa Geita, kwa muda mfupi tu familia ile iliyokuwa na furaha ilikumbwa na majonzi makubwa.

    Kiba akiwa ameongozana na wadogo zake wawili Sarah na Sophia walikuwa kando ya mlango wa wodi wakiwa wamejikunyata wakingoja taarifa kutoka kwa daktari juu ya afya ya baba yao.

    Muda wote ambao walikuwa pale katika benchi walikuwa wakilia kwa uchungu mkubwa, walikuwa na majonzi makubwa, kumpoteza mama na ndugu yao katika ndege ambayo haijulikani mahali ilipoangukia huku baba yao naye hali yake ikiwa ni tia maji tia maji, iliwafanya wawe na huzuni kubwa.

    Muda wa mfupi badaye, mlango wa wodi ulifunguliwa, dokta menene aliyevalia koti jeupe na miwani ndogo ya macho akawakabili.

    “Poleni sana,” alisema akiwa kasimama kando, walistuka baada ya kusikia sauti ya daktari.

    “Anaendeleaje mgonjwa?” wote wakauliza kwa wahaka, dokta hakujibu swali lile badala yake akasema:

    “Naomba kiongozi wa familia aje ofisini kwangu.” Kiba alisimama na kumfuata

    “Baba yako amekumbwa na nini hadi presha yake ikapanda kiasi hiki?”

    “Kapewa taarifa za msiba”

    “Msiba wa nani?”

    “Mke na mtoto, yanii mama yangu na mdogo wangu”

    “Poleni sana wamefariki vipi hao watu?”

    “Ni miongoni mwa wasafiri waliopotea na ndege ya Panasonic Airline 205,” alisema Kiba, Dokta alishusha pumzi ndefu, akavua miwani na kuipangusa vumbi akaivaa tena kisha akasema.

    “Kiba.”

    “Naam.”

    “Nasikitika kukwambia kwamba baba yako pia hatukonaye...amefariki dunia mapema baada ya kufikishwa hospitalini.”

    Ilikuwa ni wakati mbaya mno kwenye maisha ya Kiba, taharuki nyingine kubwa ulizuka pale hosptalini, familia ile ilikuwa imepoteza watu watatu kwa mpigo.

    Habari za vifo vya familia ile ikasambamba kama moto wa kiangazi nyikani, ikawa gumzo mkoa mzima wa Geita, siku iliyofuata vyombo vya habri nchini nzima stori kubwa ikawa ni juu ya kupotea kwa ndege na Watanzani wawili waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

    Hapakuwa na mtu hata mmoja aliyefahamu kama ndege ya panasonic Airline ilianguka kwenye kisiwa cha Guem katika bahari ya Pasific.

    ******CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Amosi na mzee Mikidadi wakiwa wameambatana na wanaume wengine wawili walikuwa wakiendelea kulandalanda ndani ya msitu kuona kama wanaweza kupata matunda yatakayowasaidia kwa chakula.

    Kwa dakika ishirini nzima wakiwa wanazunguka hawakuona chochote.

    Kwa Rehema za mwenyezi Mungu mara wakaona bustani ya nyanya na nanasi.

    Bustani ile ilikuwa imetengenezwa kiustadi, ilionyesha waziwazi mlimaji alikuwa ni mkulima aliyefuata kanuni bora za kilimo.

    “Alhamdulillah Mungu katenda miujiza,” mtu mmoja alilopoka na kulivamia lile shamba na kuanza kuchuma nyanya na kutafuna, waliamini kupitia nanasi na zile nyanya ndani ya bustani ile zingeweza kuwapa nguvu hadi wakati ambapo msaada utakapopatikana.

    Hali ilikuwa tofauti kwa Amosi, yeye alibaki amekodoa akiisaili ile bustani, alimini shamba lile halikujitengeneza lenyewe kwa bahati mbaya, pamoja na kwamba tangu waanguke kwenye kisiwa kile hakupata kumwona binadamu wa kawaida zaidi ya mauzauza lakini kupitia shamba lile akahisi kivyovyote vile ndani ya kisiwa kile kuna watu wanaishi.

    Swali kuu likawa Je watu wanaoshi ndani ya kisiwa hicho ni akina nani, ni binadamu wakawaida?, ama ni mizimu na majini?



    WAKATI anajuliza mambo hayo, wenzake walikuwa hawana habari wala kujali lolote, waliendelea kushambulia matunda yale kwa fujo.

    Matumbo yao yaliposhiba wakebeba kiasi kingine kwa ajili ya kuwapelekea wenzao waliowaacha afukweni. Waliamini kupitia matunda yale, yangewasaidia kujaza matumbo yao hadi ambapo msaada ungepatikana.

    Wakiwa wanarejea, wakiwa watu wenye matumaini ya kuendelea kuishi hadi msaada utakapo patikana.

    Ghafla...

    ilisikika sauti ya moja ikitokea vichakani, sauti hiyo ilikuwa ni ya mtu aliyeonekana kuwa taabani kutokana na mbio, ilikuwa ikiomba msaada. Meneno yake yalikuwa hayatamkiki vizuri, Pumzi zilikuwa zikimtoka mithili ya jibwa koko lililonusurika kumezwa na chatu.

    Amaosi na wenzake wakabaki wanashangaa, chakarachakara za nyayo za mtu huyo zilikuwa zikijongea kuja usawa wao kwa kasi. Hawakujua ni nani kutokanana na uwepo wa vichaka vingi.

    “Ni nini hiko?” mtu mmoja akauliza.

    “sijui”

    “Atakuwa mwenzetu?”

    “Sidhani”

    “Sasa atakuwa ni nani?”

    Jibu halikupatikana.

    Amosi akahamanika, akili yake bado ilikuwa juu ya mtu aitwaye ‘Bastard, ambaye mzuka wa mama yake ulimtaka amtafute.

    Je huyo ajaye ni Bastard? Akajiuliza kimoyomoyo, nafsi yake ikawa ni yenye hamaniko.

    Mara mtu mmoja alionekana. Alikuwa katika mashaka makubwa sana. Aliwajia huku akikimbia mbio za farasi.

    Nguo zake zilikuwa zimechanikachani, uso wake uliopauka kama muhogo ulikuwa na mikwaruzo na makovu megi.

    Ndevu nyingi zilizokosa matunzo zilikuwa zikining’inia kidevuni mwake, nywele zake zilizojisokota kiasi cha kutoa taswira kama ya mwendawazimu. Iliwatisha.

    “Msaada....nisaidie...” alisema huku akiwakimbilia akina Amosi.

    “Ni nani huyu?” mtu mmoja akauliza tena, hofu kubwa ikijitengeneza vifuani mwao.

    “Inakuja...inakuja...inakuja” mtu yule alilopoka baada ya kuwafikia.

    “Nanii!!?”

    “Muuwaji!!.” alisema

    Pale pale hawakungoja mtu yule awaeleze muuaji huyo ni nani na kwa nini anaua, walikurupuka na kutimua mbio kurudi ufukweni. Dakika mbili badaye wakawa ufukweni, walikuwa wakihema kwa nguvu. Taharuki kubwa walikuwa nayo usoni.

    “Kuna nini?”wenzao waliowaacha katika ufukwe walihoji.

    Kila mtu alikuwa akihema, nyuso zao zilikuwa zenye wasiwasi, wenzao wakawazunguka na kuendelea kuwahoji, huku yule mtu mpya akiwa mingoni mwao.

    “Mmepatwa na nini?” mwanamke mmoja alihoji.

    Timu ile iliyokuwa ndani ya msitu ikiongozwa na mzee Willium pamoja na Amosi wote wakamwangalia mtu yule mpya waliyekutana msituni. Mtu yule akatambua anatakiwa aeleze ni kitu gani alichokuwa akikimbia ndani ya msitu.



    “Majini” mtu yule mpya alisema.

    “Eeeeh!!!!!” watu wale walibweka kwa mshituko baada ya kauli ile.

    “Majini???” wakauliza kwa pamoja.

    “Ndio, kuna vumbe wabaya sana hapa...” alisema. Watu wote wakawa kimya wakimsikiliza.

    “Jina langu naitwa Boniphace Ngumije, mimi ni mtafiti wa wanyama wa baharini. Nilijikuta katika kisiwa hiki zaidi ya wiki nne baada ya dhoruba kali kutokea baharini.

    “Nilikuwa na wenzangu ambao wote wamekufa katika mazingira tata, nimebakia mwenyewe, na tangu ninase hapa mwezi mzima nimekuwa katika mateso makubwa.”

    “Nani anayekutesa?” mtu mmoja akauliza. Hadithi aliyokuwa akisimulia ilikuwa haingii kwenye akili za watu wale.

    “Majini”

    Maneno yale yalikuwa ni mfano wa hadithi za paukwa, hayakuwa na hayakuwa na ujazo wowote kwa watu wale, mzee Willium akajikuta anachukizwa na kitendo cha kukimbia kwa jambo la kihaywani kama lile.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Labda ungesema wewe ni mtu mwenye matatizo ya akili pengine tungekuelewa, lakini siyo ujinga unaouzngumza hapa” mtu mmoja akamwambia kwa dhihaka.

    “Kwa hiyo na ninyi mlikuwa mnakimbia kutokana na haya anayoyasema huyu?” mwanamke mmoja aliwauliza wanzao huku akimwangalia mzee William kama kiongozi.

    Aibu ikamshika mzee William akajisikia vibaya kuona alivyokurupuka na kukimbia kama kichaa kwa kutomsikiliza mtu yule aliyeibuka na kusimulia hadithi za paukwa.

    “Dickson wapeleke watu kwenye yale matunda” mzee yule alisema kwa sauti ya unyonge. Kitendo cha kutokewa na mtu yule katika vichaka na kutoa maelezo ya kusadikika, ilimuudhi.

    “Kwani mlipata chakula?” watu waliokuwa ufukweni, wakiwa katika njaa kali wakauliza.

    “Ndio”

    “Wapi?”

    “Ndani ya msitu”

    “Twendeni”

    Watu karibu wote wakaingia kwenye msitu ule, kwa njaa walio kuwa nayo, hawakutaka kabisa kusikiliza hadithi za mtu aliyejiita Boniphace Ngumije.

    Mzee William alikuwa amevimba kwa hasira kali, hakupenda kabisa namna Amosi na mtu aliyeibuka vichakani walivyokuwa wakileta hadithi mbaya kuhusu mahali walipokuwa wameangukia.

    Kwa upande wa Amosi wakati mambo yote hayo yakitokea ni yeye peke yake aliyepokea maelezo ya mtu yule kwa mtazamo tofauti.

    Nafsi yake ilikubaliana na maneno ya mtu yule kwa asilimia kubwa kutokana na mauzauza ambayo alikwisha yashuhudia kwa macho yake akiwa katika ufukwe ule, alimiani ndani ya msitu ule kulikaliwa na viumbe wasio wa kawada.

    Wakiwa wamebaki watu wachache katika ufukwe huku mlundo wa watu wakiwa ndani ya msitu,wakisaka chochote wka ajili ya kupoza njaa yao, muda mrefu ukapita bila kurejea.

    Lisaa lizima lilikatika, wenzao hawakurudi, masaa mawili yakakatika, wenzao hakuwaonekana.

    Baada ya kuona wenzao wamechelewa tangu walipoingia katika msitu kwa ajili ya kutafuta matunda yatakayopooza njaa zao, Mzee William alishauri wawafuatilie kujua wamepatwa na nini.

    “Kwani una wasiwasi?”Amosi akamuuliza katika namna ya kusuta. Hakupenda namna mzee yule alivyokuwa akipuuza mambo aliyokuwa akielezwa.



    “Hebu tukawatafute wenzetu Amosi”

    Amosi alitabasamu, Tabasamu la huzuni. Hakutaka kumwangusha mzee yule, watu wote waliokuwa wamebakia akiwemo Boniphace Ngumije wakaingia msituni kuwafuatailia wenzao.

    Walitembea kwa ziadi ya dakika 20 hadi 25 kufuata sehemu ambayo waliamini wenzao kwa wakati huo walikuwepo. Wakiwa umbali wa mita kama 19 kabla ya kufika eneo lile ambalo lilikuwa na bustani ya nanasi, hawakuamini walichokiona!!.

    Walibakia wameduwaa huku macho yao yakiwa hayaaamini tukio lililokuwa likionekana mbele yao, miili ya watu ilikuwa imelala chini kwa kutawanyika kila mahali, miili ile ilikuwa ni ya wenzao.

    Picha iliyoonekana ni kama kulitokea shambulio kubwa mno ambalo lilipelekea watu wale kuwa katika hali ile.

    Mambo yale waliyashuhudia wakiwa umbali wa mita kama 19, hawakuona dalili za mtu kuwa hai, mate mepesi yaliwamjaa vinywani, hofu na mashaka ikawashika.

    “Mungu wangu nini hiki!!” Amosi alisema kwa hamaki.

    “Kuna jambo baya limetokea…” mzee Willam naye alizungumza.

    “Wameuawa!!.” Ngumije naye akabwata!

    “Kitu gani kimewaua?”

    “Hata sijui.”

    “Tuko eneo baya na la hatari!” Ngumije akalipoka,

    “Huku ni kuzimu huku si bure!” kila mtu akawa anasema la kwakwe.

    Walizipiga hatua ndogondogo kusogelea miili ya wenzao.

    Hali waliayoikuta iliwatisha, miili ya wenzao ilikuwa imejeruhiwa vibaya sana, ni kama ilishambuliwa na mnyama fulani.

    Katika kutazama huku na kule mtu mmoja alionekana akiwa katika hatua za mwisho. walimzunguka, mtu yule alikuwa akigumia maumivu makali, huku akitapika damu.

    Mwili wake ulikuwa umetapakaa damu kama vile aliingia katika nbwawa la damu na kupiga mbizi!

    “Nini kimetokea?” mzee William aliuliza kwa kiherehere huku akimtingisha mtu yule.

    Alikuwa akihema kwa tabu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jeraha baya katika upande wa kulia wa kifua chake lilionekana. Kidonda kile kilikuwa kimechimbika na kuacha shimo kubwa, mnofu mkubwa wa nyama ulikuwa umenyofolewa na kuacha shimo ambalo lilikuwa likitiririsha damu nyingi sana.

    Hali aliyokuwanayo mtu yule, ndiyo ambayo walikuwa nayo watu wengine ambao kwa wakati huo walikuwa wamekwishafariki dunia.

    Walikuwa wamenyofolewa pande kubwa la nyama sehemu za kifua sanjari na michumbuko ya hapa na pale.

    “Nini kimetokea!!” Amosi naye alipayuka akiwa kando ya mtu yule.

    “Bastard,” ndilo neno pekee ambalo mtu yule alifanikiwa kuzungmza, akapiga kimya cha ghafla, macho akiwa ameyakodoa, mdomo wake ukibaki umeachama! alifariki dunia bila kuzungumza kwa kina walishambuliwa na kitu gani.

    Amosi na mzee William walitishika vibaya sana, kauli ile ya mwisho ya mtu yule, haikuwa kitu kigeni masikioni mwao.

    Masaa machache kabla ya tukio lile, Amosi alitokewa na mama yake ambaye alisafirishwa kwenye ndege ya Panasonic Airline akiwa maiti,ndege inaanguka kwenye kisiwa aliyekuwa maiti ikisafirishwa kwa ajili ya mazishi akaonekana akiwa hai, anamtokea Amosi na kumpa kipande cha ubao kilichondikwa ‘find the Bastard’ yanii mtafute Mwanaharamu!.

    Wenzao wengi wanakufa kwa kushambuliwa na kitu kisichojulikana, mtu mmoja ambaye yupo katika hatua za mwisho anaulizwa anasema neno moja tu ‘Bastard’(Mwanaharamu)

    “Hii nini maana yake sasa…bastard ndio anauwa hivi?” Amosi alibwata kwa fadhaa.

    “Tuondoke hapa, si salama kwetu,” Ngumije naye alisisitiza.

    “Kunauwezekano huyu Bastard ndiye kiunganishi cha mambo haya yote, nadhani tumtafute huyo mtu, kuliko kusubiri kifo” Amosi aliongea uso wake ukionekana kuwa tayari kwa lolote.

    Kwa mara ya kwanza Mzee William akatikisa kichwa kukubaliana naye.

    “Bastard ni nani?” Ngumije alihoji.

    Kwa kuwa yeye hakuwahi kujua kisa kile cha kuibuka kwa jina lile la Bastard ilibidi wamweleze.

    “Sasa huyo bastard tutamtafutia wapi humu porini?” aliuliza.

    “Sijui, lakini naamini huyo mtu yumo humuhumu, yupo tu sehemu fulani ndani ya msitu huu,” Amosi alimjibu.

    “Kwa nini unasema mtu? Umejuaje kama huyo Bastard ni mtu?” Ngumije aliemdelea kuhoji, Amosi akapiga kimya cha ghafla, akatafakari swali la mtu yule ambaye ni mpya kwenye msafara wa watu aliokuwa nao ndani ya ndege.

    “Unadhani bastard atakuwa si binadamu?” naye akamuuliza

    “Sijawahi kuona binadamu wa kawaida katika kipindi chote ambacho nimenasa katika aneo hili, hadi leo nilipokutana nanyi”



    “Kwa hiyo?”

    “Narudia tena kukuelezeni siyo wazo zuri sana kwa upande wangu maana nimeishi humu kwa zaidi ya mwezi mzima, mbali ya kukutana na mauzauza ya hapa na pale sijawahi kuona mahali kuna viashiria vya uwepo kitu kiitwacho Bastard.”

    “Kwahiyo unashauri tuachane na bastardi?”

    “Mimi nadhani tujikite kwenye kutafuta mawasiliano ili tuweze kupata msaada wa kututoa kwenye kisiwa hiki cha kijinga.”

    Amosi aliwaza kidogo, akamtizama mzee William ambaye alikuwa kimya wakati wote, kisha akasema:

    “Unaonaje tukigawana majukumu?”

    “Kivipi?”

    “Wewe utafute mawasiliano, mimi na mzee William tumtafute huyo Bastard mambo yote hayo tuyafanye ndani ya masaa mawili tu, kituo chetu cha kukutania kiwe ufukweni.”Amosi alimwambia.

    Kabla Ngumije hajazungumza chochote mara zilianza kusikika ngurumo za kutisha, ngurumo hizo zilikuwa zikija kwa kasi eneo lile walipokuwepo.

    “Mungu wangu nini hicho!!.” Amosi alibwata, ndani ya nukta hizohizo kiliibuka kitu cha ajabu mbele yao.

    “Mungu wangu tumekwisha!!” Amosi alipayuka baada ya kuona kiumbe kilichokuwa mbele yao.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog