Search This Blog

SENDAYE (MALKIA WA MOYO WANGU) - 4

 







    Simulizi : Sendaye (Malkia Wa Moyo Wangu)

    Sehemu Ya Nne (4)







    Walilia apakuwa na wakuwasaidia!....



    Kwa Mara ya kwanza Saut ya kukata tamaa ya Jemes ikasikika,kwa Mara ya kwanza naye alijua huu sasa ndo mwisho wao



    Mabaru manguvu alikuwa mlangoni?!,kivipi sasa angeokoka alimjua fika kijana yule ndio alimshika Paul na Martin shingo zao kwa mkono mmoja mmoja akawanyonga mpaka vifo vyao



    Hakuwa mtu wa mchezo mchezo



    Hakika, James pia alimuogopa



    Walilia apakuwa na wakuwasaidia!....



    Kwa Mara ya kwanza kila mmoja kywa upande wake akawa akijutia kuja ndani ya kijiji kile!



    Kauli ya ninge...uja baada ya matatizo na hili kwao lilitimia....



    ***

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mabaru Manguvu



    Alikuwa ni kijana shupavu ,mwenye mwili ulojengeka kimazoez ,muda wote alikuwa kavimba hakuwa mtu Wa kutabasamu

    Alikuwa ndo mlinzi mkuu katika himaya ile ya mfalme Omoti

    Katikati ya usiku ule nje alikuwa yeye na kijana Misogo vijana walioaminika



    Nyumba aliyelazwa Sendaye ilipakana na hiyo walioko kina Isaki,Misogo alikaa nje ya mlango Wa Sendaye huku Mabaru kijana Wa shoka akikaa katika mlango Wa wanaume wale!



    Ghafla wakat akiwa pale nje akasikia kelele mlango ukigongwa kwa nguvu, kelele zile hata Misogo alizisikia



    Mabaru akausogelea mlango na kuanza kuufungua tayari Misogo alikuwa nyuma yake hamu ya kutaka kujua kelele zile ni za nini ikiwavamia kwa kasi!...



    Ile wanaingia ghafla wakavamiwa



    Mabaru akiwa kashikwa na watu wawili Paul na Martin huku Misogo naye akiwa kakamatwa barabara na vijana Abdul na Elia Jemes akiusogelea mlango kwa dhumun la kuufungua lakin kabla ajaufikia akasikia kishindo nyuma yake ile kugeuka alishughudia mihili ya wenzao Paul na Martin ikiwa chini akuhitaji kipimo kujulisha kuwa tayari zile ni maiti!



    Abdul na Elia walijikuta wakimuachia Misogo na kuwafata wenzao na kuanza kuwaita kwa uchungu hata Isaki naye akuamini kile kilichoenda kutokea!



    Akajikuta akirudi na kuwalilia wenzao walikuja nane sasa wamebaki watatu, hata kama wangesalimik wangewajibu nini wazazi Wa watoto hao waliokwisha potea!



    Machoz yaliwamiminika



    "Ha ha ha ha ha himaya ya mfalme Omoti aitorokwi hivyo mkijaribu tena mtawafata wenzenu mapemaaaa kabla hata ya kesho yamebaki tu masaa machache kupambazuke"



    Misogo aliongea kwa dharau na kicheko cha kinafki,Mabaru hakuwa mtu Wa kucheka mtu Wa mahasira akaufungua mdomo wake



    "Na mkijaribu tena ujinga wenu nanyi tunawamaliza kesho ni mazishi tu!"



    Mlinzi yule alojaliwa nguvu aliongea kwa kibabe,watatu wale hawakujal maneno yake wao waliendelea kuwalilia wenzao tu



    Mabaru na mwenzake wakatoka! Na kuufunga mlango kama awali!



    "Mabaru kwa nini umeua usaghe?"



    ( usaghe ni mlinzi mkuu)



    Misogo alikuwa msaidizi wake



    "Sikuwa na budi kufanya hivyo sipendi kitu kiniangaishe kuwaua wale wenzao awatajaribu kufanya uo upumbavu"



    Pasina mzaa Mabaru akajibu!



    "Lakini mfalme atatuelewa kweli?!"



    "Mfalme! Mfalme! Mfalme! Kila kitu mfalme asituelewe kwa nini?!,kama walitaka kutoroka tungewafanyaje?!"



    Mabaru alifoka tofauti na matarajio yake Misogo naye akaja juu!



    "Ndo uwaue?!,wewe ni mpiganaji Mabaru ilipaswa uwazimishe mbinu hiyo ulikuwa nayo tatizo jazba zako tu!"



    "Ndo nshawaua sasa kawafufue"



    Mabaru akaropoka ila kabla Misogo ajajibu kwa mbali ikasikika sauti nyororo ikiita!, sauti tamu



    "Misogooooooooo!"



    Wote wakapeleka macho yao sauti ilipotokea!,kati yao Mabaru na Misogo walishindwa kujizuia kuulamba mdomo



    Hakika alikuwa binti Mrembo mithili ya Malaika Wa kiasili,mwendo wake tabasamu Lake



    "Mtu wako huyo!"



    Mabaru akaongea kinafki ,Misogo akaishia kutabasamu tu na kupiga hatua kumsogelea binti yule Mrembo!



    "Sidai malkia Wa moyo Wangu"



    Misogo alitamka akitanua mikono yake Sidai akaingia katikati yake wakawa katika kumbatio tamu



    "Na hamu na wewe MpZ Wangu twende ukanridhishe dia hata nipate tone la usingizi nimeshindwa kulala kabisa mwenzio"



    Misogo akamwangalia mwenzake Mabaru akampa ishara ya kumruhusu aende wakiwa wameshikana mikono wakatoka kuelekea wanapopajua wao,



    Ilikuwa Ni kawaida ya Sidai usiku kutoroka kwao na kumfata Misogo misogo anaacha lindo na kwenda maporini kufanya ufuska na binti huyo!



    Hiyo alikuwa Ni kawaida yao na Mabaru alilitambua ilo!



    Katika lindo mabaru akabaki mwenyewe macho yake yakawasindikiza wawili wale wakiwa wameshikana kimahaba ghafla machozi yakaanza kumchuruzika!



    Mabaru alikumbuka mbali!



    Mwasi!



    Alimkumbuka mpz wake mwasi binti alotokea kumpenda kuliko kitu chochote, ila mwishoe akaja kumsaliti na kutoka na mfalme wake!



    Ndo Mke Wa pili Wa mfalme ghafla kitu kama chuki Kali ikajijenga kooni kwa Mabaru!



    Binti yule aliondoka na furaha yake!,mawazo tofaut yakajijenga katika kichwa chake!



    Usaliti!...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mfalme alimsalit tena kama mlinzi wake mkuu pasina kumuheshimu akatoka na MpZ wake kibabe hali ya kuwa alijua juu ya uhusiano wao,naye kwa nini asimsalit?!



    Wake wote Wa mfalme kanyang'anya kwanzia mke Mkubwa ,mwasi na hata Sendaye!



    Leo hii mke mdogo kamsalit na mtu mweupe kadhamiria amnyang'anye bila kutarajia Mabaru akajikuta akiachia tabasamu!



    Alipenda! Akajikuta akiwaza



    'Kadri siku zinavyozidi kwenda ndo hali inavyozidi kubadilika ukatili Wa mtemi Omoti unaongezeka,kanichukulia Mke Wangu mwasi eti naendelea kumlinda?!,hapana!,siwezi kuendelea kuwa mtumishi wake lazima nifanye jambo juu ya hawa tena si anampenda Sendaye zaidi ya hawa lazima niwasaidie siwezi kuwashughudia wakiuwawa kinyama hiyo kesho!"



    Mabaru wazo hilo lilijikuta likipata nafasi katika kchwa chake kwa ghafla naye akaamua kulifata



    Kwa kywa muda huo alikuwa pekee na Misogo alikuwa vichakani na mpenzi wake ilipaswa afanye jambo haraka haraka!



    Akaufungua mlango Wa kina Isaki watatu wale walishtuka kumuona!



    "Nifateni"



    Akatamka,ila Ni kama sauti yake aikufika masikioni mwao walibaki wameganda wakiitazama miili ya wenzao!



    "Nifateniiiii"



    Akatamka tena kwa sauti ila Ni kama alipiga kelele katikati ya viziwi akitegemewa kusikiwa!



    Ni wazi watatu wale waliaribika kisaikolojia na kurudi katika hali yao ya kawaida ingewachukua muda sana!



    Na ilipaswa Mabaru manguvu awatoe haraka sana!....



    Angefanyaje?!.....



    Utata utatani!



    Mabaru manguvu baada ya kumuona Misogo akitok na mpz wake mawazo yanaenda mbali!,naye anamkumbuka mpz wake Mwasi alonyang'anywa na mtemi Omoti mawazo yanabadilika anajikuta akitaman kuwaokoa.



    Ila anapofika ndani na kuwaomba watoke kina Isaki wanaonekana katika mabumbuwazi wakiishangaa miili ya wenzao



    Mabaru akafikir kidogo akaona akiendelea kuwaita wale watakutwa na Misogo na kufanya kazi yake iwe ngumu akupenda ilo litokee akawasogelea na kuwashtua kwa kuwagusa!....



    Wakashtuka!



    "Nimesema tuondokeni mida mibaya hii nataka kuwasaidia tutakutwa sasa!...



    Wote wakashtuka



    Mlinzi yule aliyewaulia wenzake alitaka awasaidie au akawamalizie?!,hapana yule hakuwa wa kutoa msaada kumbukumbu za kila mmoja ziksrudi wakati alipokuwa kawashika wenzao shingo zao akiwanyonga tena kwa mkono mmoja pasina huruma!



    Alikuwa Ni mtu mwenye roho mbaya!,mtu asiye na roho ya kutoa msaada , Leo hii katika usiku huu eti anadai anataka kuwasaidia!



    Wote wakabaki wakimshangaa!,Mabaru alijua Ni nini kilichowashangaza pengine ni kutokumuamini kutokana na roho aliyewaonesha hapo kabla!



    " Mimi ni binadamu si Malaika nimejitolea kuwasaidia japo nimewaulia wenzenu alikuwa kusudio langu! Nisameheni kwa ilo, hilo lilishatokea yatupasa sasa tugange yajayo nyanyukeni tutoke nipo tayari kuwasaidia kuwatoa katika kijiji hiki.....



    Safari hii awakuamini ilikuwa ni Kama wamepata habari ya kushinda biko!,pasina kujishauri wakanyanyuka ,Mabaru akageuza kutoka nje nao wakimfata kwa nyuma akaelekea chumba cha Sendaye na kukifungua!



    "Malkia Sendaye nimekuja kukuokoa kesho mfalme hatokuacha mzima lazima utoroke ndani ya usiku huu huu..."



    Mabaru aliongea kwa sauti ya chini, Sendaye akanyanyua kichwa chake taratibu machozi yakimchuruzika akamwangalia Jemes huku akiendelea kulia akapanua mikono yake kumkumbatia!



    i...i...i..saki wang"



    Sendaye akajitutumua kulitaja jina lile!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Isaki?!...."



    Watu wote wakashangaa akiwemo hata Jemes mwenyewe Sendaye alimtambuaje!



    Mabaru alibaki mdomo wazi, alimjua fika Isaki lakini Isaki hakuwa mzungu



    "Hatuwezi kuondok hapa lazima Isaki umuue mfalme Omoti atuwez ondoka!....



    Sendaye alizid kusisitiza Mabaru alihis labda kachanganyikiwa



    " twende Sendaye muda ndo huu saa tisa sasa tutakutwa....



    "Hapana kesho hakuna kitakacho aribika Lazima Isaki atamwangamiza Omoti!, lazima Isaki Wangu umuue huyu mtu, kamuua baba yako, kamuua mama yako usimuache mzimaaaaaaa"



    "Lakini mimi siyo Isaki...



    Ilibidi James ajikane kusudi Sendaye akubali kuondoka ,Sendaye akamkata jicho



    " eti unasema?!,we siyo Isaki Wangu?!,ina maana ndoto zangu za uongo hapana sijawai ota ndoto ya uongo wewe ni Isaki Wangu kwa vyovyote vile naamin hilo!....



    "aya sawa mi ni Isaki wako nakuamrisha tuondoke kesho namuua mtemi Omoti upaswi kuwa hapa kwa usalama wako twende Mke Wang....



    Ikabidi Isaki amuhadae kusudi Sendaye alainike na kweli Sendaye alilainika!,wote walishangazwa na kauli ile ya Jemes ila kwa kuwa wote walitamani kutoka awakuuliza kitu!



    Sendaye alitambulika katika kijiji kile kwa kuwa na ndoto za kweli hata Mabaru alilitambua ilo,vile vile Isaki japo ni muda mrefu awakuonana hakuwa mgeni kwake!



    Wakaanza kuondoka kwa mwendo wa kunyata kuelekea kunapo Giza!



    Walielekea njia ya pori kubwa lililo na urefu wa kutisha na wanyama wakali lakin hakukuwa na mwenye wasiwasi kwao kuokoka kwenye mdomo wenye meno makali

    Ya Omoti lilikuwa ni jambo zuri zaid



    wakikimbia mabaru alikuwa akitafakari sana kauli ya Sendaye juu ya Jemes ila aikuleta maana!



    Isaki yupo hai!;,akupingana na wazo hilo ila yule akuwa Isaki, Isaki akuwa mzungu!?



    Akakumbuka msneno James aliyoyaongea na kumlainisha Sendaye akazid kutoelewa juu ya watu wale!



    Utaratibu wa kubadili ngozi au kuwepo kwa ngozi bandia akulijua kwa kijijini pale jambo hili lilikuwa geni!



    NDANI YA USIKU ULE ULE



    KATIKA HIMAYA YA MFALME OMOTI



    Katika mateka ya panya ambapo paka waliwakamata panya wale na kuwaifadhi kila Siku wakimtoa mmoja mmoja na kumfanya kitoweo!



    Mlinzi alikuwa ni paka Mkubwa mweusi



    Leo hii paka yule aliwafungulia panya wale walokuwa watano akala wawili na watatu walobakia akawafungulia na kuwatorosha....



    Kitendo kilichofanya paka waanze kumsaka paka mwenzao kwa usaliti aloufanya lengo likiwa kumuadabisha



    Ghafla mfalme akashtuka!



    Kumbe alikuwa akiota!



    Mwili wote uliloa jasho!



    Nini maana ya ndoto ile?;,muda ule ule akaamua kutoka kuelekea kwa mtabiri wake alimpa nyumba katika kiwanja chake



    Usiku ule ule akamuamsha na akiogopa pengine angeisahau ndoto ile akaanza kumsimulia!



    Mtabir alishtuka!



    Macho akayatoa!



    "Wale vijana mateka wanaohukumiwa asubuh wapo?!...."



    Pasina kumjibu mfalme naye akahoji!



    Mfalme akaangaliana na mkewe Mwasi, na baadhi ya walinzi walowafata



    Pasina kuambiana wote wakaelekea mahali walipowaifadhi mateka wale!



    Wakashtuka kukuta mlango wazi tena Mabaru hayupo wakakimbilia ndani walipokutana na miili miwili ya watafiti wale hali ya kutoelewa ikaendelea baina yao



    "Nini kilichotokea?!"



    Mfalme akauliza kwa ukali, akiiangalia miili ile!



    "Paka Mkubwa kala panya wawili walobakia kawafungulia katoroka nao!"



    Mtabiri akajibu kwa kuitafsiri ndoto ile!...



    "Na Sendaye?!....



    Mfalme akatamka,muda ule ule akageuka kuelekea alipoifadhiwa sendaye Mke wake akiwa pembeni yake,mtabiri na walinzi kadhaa wakimfata kwa nyuma



    Kwanza kwa mbali walishtuka kuuona mlango ukiwa wazi alamu ya hatari ikagonga katika vichwa vyao!...



    Wakaongeza mwendo na kuzama ndani

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Patupu!....



    Mwili ulimnyong'onyea mfalme akajikuta akikaa chini!



    Kizunguzungu kikali kikamkamata!



    Huku nyuma Misogo alishamalizana na Mpz wake Sidai sasa alikuwa akirudi katika windo lake pasina kujua mambo yalishaharibika!



    Kwa mbali aliona mlango ukiwa waz na kama chemli chemli akashtuka na kuzidi kusonga mbele kuwahi!



    " misogooooo yupo wapi, Misogo kamtorosha Mke Wangu?!....



    Mfalme Omoti alizidi kulalamika hasira na Jazba zikiwa zimempanda!



    Ghafla Misogo akatokea akishtuka waziwaz,mfalme,mtabir na walinz pia walishtuka kumuona tena Misogo!



    "Mke Wangu na wale mafedhuli wako wapi?!"



    Mfalme akauliza kwa ukali akiwa kashika mshale



    "Sendaye?!...."



    Misago akauliza kwani alikuwa bado ajapata picha ya kilichotokea



    "Unajfanya ujui siyo sasa sitokuacha...."



    Mfalme akauvuta mshale wake kwenye upinde taratibu akajiandaa kuuachia kummaliza Misogo!





    "Hapana mfalme usimuue kabla ajatupa mwanga wa kilichotokea hapa!...."



    Mshauri wa mfalme akapaza sauti yake,mfalme alimsikiliza sana mshauri wake yule na alimwamin kwa kila ashaurichapo hivyo akasitisha jambo lile Mara moja!



    "Haya eleza Mara moja ni nini kilichotokea hapa?!"



    Mfalme akamwambia kwa ukali



    Misogo sasa ilibidi akili ifanye kazi zaid hata ya kompyuta



    "Mtukufu mfalme wakat tukiwa tunaendelea kulinda Mara ghafla tulisikia mlango ukigongwa kwa nguvu huku kwa mateka wa Mabaru ikabidi Mabaru afungue ule mlango kujua kunanini,Mimi nikiwa nyuma yake....



    " kwa hiyo uliacha lindo lako na kuvamia la mwenzako!...



    Mfalme akauliza kwa ukali , mtabiri akampa ishara atulie Misago Akaendelea



    ....Ile tunaingia vijana wale walituvamia na kuanza kutushambulia Mimi nikikamatwa na vijana wawili na Mabaru akikamatwa na wawili yule mmoja mzungu akaufungua mlango na kutoka kwa kuwa wale wawili walitudhibit...



    "Mtadhibitiwaje hali ya kuwa nyinyi ni vijana tunaye waamin....



    " punguza jazba na lawama mfalme huu si muda wa kulaumiana yapaswa tujue nini kiliendelea tujue tutasevuje jambo hili!....



    Mshahuri akazidi kumshahuri mfalme,mfalme ikambidi awe mpole



    "Ehe kijana endelea ikawaje?!..."



    Mshahuri akauliza



    "Basi yule mzungu akaenda kumfungulia Malkia na kutoroka nae huku nyuma wale vijana walonikwida walinifunga kamba na wakati wakinifunga wale walomshika Mabaru walizidi kumshika kwa nguvu baada ya kunifunga Mimi wakatoka na kumfata mwenzao nje!.....



    " muda wote huo kwa nini msipige kelele mlipo ona mmezidiwa walinzi wengine wakaja kuwasaidia?!"



    Mfalme alishindwa kukaa kimya na kuhoji!



    "Moja ya sifa ya ujemedari ni kupambana mpaka kufa!,ila si kupiga kelele haya kijana endelea...."



    Mtabiri akamzodoa mfalme wake Misago akaendelea



    "Ila kwa bahati nzur Mabaru alijitutumua na kuwasukuma wale vijana wawili walomshika wote wakaanguka chini akakoroma kama simba wale vijana wakajinyanyua wakiwa na mshangao na kutaka kuanza kupambana ila walikutana na Mabaru mwingine....



    Mabaru aliwashika shingo alipowa achia tayari walikuwa maiti!...



    " aaaaaaah....aaaaah vizuri sana ikawaje sasa?!"



    Mfalme alifurah akaoji katika hali ya sintoamini



    "Baada ya kuwamaliza Hawa vijana wawili akaja kunifungua wote tukatoka nje.....



    " mhuuuuu"



    "Kwa bahati mbaya tulipofika nje atukuamin baada ya kuona chumba cha Sendaye kipo wazi tulipoingia atukumkuta Sendaye ikabidi tuanze kuwasaka



    Misago akazidi kuongopa!,kwani akili ilifanya kaz Mara tatu ya kawaida alijua akisema ukweli kwamba alienda kwa mchumba ake na nyuma aliacha ulinzi salama angeuwawa



    Ila moyoni mwake akumtilia shaka kabisa Mabaru Manguvu kwamba ndo kashiriki kuwatorosha Sendaye Jemes na wenzake ila alijua itakuwa lazima Mabaru kadhibitiwa wale wakatoroka kutokwepo kwake pale alijua lazima hatakuwa kawafata.



    Alimjua vizur Mabaru alijua akiwakamata lazima atawa angamiza hivyo ikabidi yeye ajitengenezee mazingira mazuri kwa upande wake

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    " basi tukaingia porini na kuanza kuwakimbiza baada ya masaa kadhaa tukawaona ila cha ajabu walikuwa na spidi ya ajabu na walionekana kutochoka Ghafla Mabaru akapata wazo la kuntuma Mimi nirudi huku kutoa taharifa hii ili nyinyi mjue kilichoendelea muongeze walinzi kusudi asb msiwe na shaka juu yetu.....



    Misogo akaitimisha akiwa kajitoa kabisa kwenye mstar ule wa hatari na kujiweka salama!



    "Mwalamaaaa!..."



    "Mfalmeeeee"



    "Mwanamtakala!"



    "Mfalmeee"



    "Unganeni na Misogo ingieni porini mpaka kuna pambazuka muwe mna habari nzur kwangu nnachotaka kuletewa ni vichwa tu haya poteeni"



    Ila kabla ajaondoka mtabiri ambaye pia alikuwa ndo mganga mkuu wa kijiji kile akafungua mdomo wake



    "Kabla awajaondoka shikeni hii pembe ina itwa mwanavaa hii ndo mtaitumia kuwasiliana nasi mkiwa kazini...."



    Misago akaipokea



    "Utaipuliza Mara tatu huku ukisema Mwanavaaa mwanavaaaa mwanavaaaaa basi tutaungana kimawasiliano"



    Akawakabidhi pia dawa Fulani ya kama majivu ya mkaa na kuwa ambiya kila watakapochoka wailambe dawa ile itaondoka na uchovu wote na kuwarudisha katika nguvu za awali



    Wakatoa na mbwa watatu walowanusisha nguo ya Sendaye mbwa wale wakaanza kutoka nduki vijana wa nne wakifatia nyuma! Hasira zikiwa katika nyuso zao



    Ila moyoni mwa mtabiri alikuwa na hali ya sintofahamu katika maelezo ya Misago na ndoto ya mfalme Omoti , ndoto ya mfalme ilijieleza wazi kuwa paka ndiyo aliyewafungulia panya ila kwa kuwa bado aikuleta picha halisi katika kichwa chake ikabidi avunge!



    *****



    NDANI YA MSITU PANDE



    Giza lilitawala,nuru iliondoshwa na wingu zito lililotanda katika anga lile miti mikubwa ilonawiri ilitapakaa ndani ya msitu ule Mkubwa ulosifika kwa kuwa na wanyama wakali!



    Msitu mkubwa ambao Siku chache nyuma watafiti walivumbua dawa ya homa ya madega!



    Na leo hii watafiti wale walokuwa jumla ya nane na sasa walibaki wa tatu baada ya wenzao kuuwawa.



    Tena wakiwa katika mwendo wa kukimbia!



    Ghafla wakasikia kishindo nyuma yao!



    Wote kwa pamoja wakageuka



    Alikuwa ni Sendaye aliyeanguka Jemes akamkimbilia na kujaribu kumuamsha



    "Nimeumia Isaki Wangu siwez!,siwezi hakika kuamka hapa!,"



    "Jitahidi kukipambazuka tuwe tumetoka kwenye huu msitu"



    "Siwez! Hakika siwez mpz"



    Pasina kuongea kitu akijua fika pale ni kupoteza muda Mabaru Manguvu alimsogelea Sendaye na kumnyanyua akamweka mgongoni na kuanza kukimbia naye



    Walifika katia moja ya kisima akamshusha wakanywa maji!



    Kwa kuwa vijana wale walikuwa hawana mazoezi ikawalazimu kupumzika pasina kujua vijana wa nne wenye mbwa watatu walishaingia katika msitu ule wakija kwa kasi



    Wakati wakiwa wamepumzika Mabaru aliwaacha na kwenda kutafuta dawa ya majani flani akayatafuna na kumpaka katika mguu wake!



    Maumivu yakapungua!



    Wakaendelea na safari!



    Ilikuwa ni lazima waumalize ule msitu japo bado walikuwa na safari ndefu walihema wakulalamika walilalamika ila walisonga

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa bahati nzuri awakukutana na wanyama wakali mpaka muda huo!



    'Wooooooow wooooooow wooooooow'



    Kwambali wakaanza kusikia sauti za mbwa!



    "Tumekwisha"...



    Mabaru Manguvu akazungumza kwa kukata tamaa



    Yeye ndo alikuwa nyuma ya wenzake



    Jemes alikuwa mbele akifatiwa na Sendaye wake nyuma alifatia Abdul,Elia na Mabaru alikuwa wa mwisho wakazidi kusonga



    " waleeeeee"



    Kijana mmoja kati ya wale walokuwa na mbwa akafoka!



    'Haaaaaaaa yule si Mabaru ina maana Mabaru katusaliti'



    Misago akawaza



    "Yule wa nyuma si Mabaru?!"



    Mwanamtakala akauliza na kumzindua Misago alokuwa mbali kimawazo



    "Achia mshale dawa ya usaliti ni mauti"



    Misago akaongea kwa Saut ya taratibu akiukumbuka uongo aliousimulia ila angeusafisha kwa mafanikio alilijua ilo na ili kufanikisha alipo ona wenzake wanasita wakiwa katika bumbuwazi akatoa mshale katika kite na kuuvisha katika upinde!



    Mshale wenye sumu Kali



    Akasimama na kuuvuta akauachia



    Mshale ukapaaaa na kwenda kuuchoma mgongo wa Mabaru Manguvu



    "Mamaaaaaaaaaaaa!"



    Mabaru Manguvu akaachia ukelele ulowashtua wenzake wakasimama wote walishtuka Mabaru akaenda chini akiangukia mgongo mshale ukamalizikia



    "Ki....ki....ki!...ki..."



    Alitaka kuwa ambia akimbie alishindwa kumalizia ghafla Mabaru manguvu naye akapoteza maisha!



    Vijana na mbwa wao wakazid kuja kwa kasi wakiwa na matumaini sasa ya kupeleka vichwa kwa mfalme wao kama maagizo yao yalivyo waagiza!



    Maskin Sendaye , Jemes na wenzake walibaki wakimlilia mkomboz wao Mabaru wakisahau ujio wa vijana wa kazi wakiongozwa na Misago!.....



    Misago kumuua Mabaru Manguvu kwake kulikuwa na faida kama mbili hivi!



    Moja ile nafasi ambayo Mabaru alikuwa nayo kicheo katika sekta yao ya ulinzi Misago aliitaman sana!,na alipanga kwa siri sana Siku moja angemuua Mabaru na Siku hiyo alifanikisha juu ya jambo hili!



    Pili kumuua Mabaru pia kwake kulikuwa na Faida ya kuuficha ukweli wa kile alichokieleza angejua angeeleza nini lakini kwa kuwa alitambua Mabaru alishirikiana na vijana wale wakat maelezo yake yalikuwa tofaut na vile alivyo ona ilikuwa lazima afanye vile!



    Wakati wakiendelea kuwafikia vijana wale ghafla kama nguvu za ajabu zikamvamia Isaki pale chini

    Akaropoka kwa sauti ya juu!



    "Tukimbieeeeeeeni wanafika"



    Muda ule ule akajinyanyua sambamba na kumvuta mkono Sendaye ambaye alishangazwa na ujasiri ulomkumba Isaki kwa ghafla muda ule



    Wakaanza kukimbia,Misago aliona tukio lile akasimama na kuushika mkuki katika upinde akawapa ishara na wenzake wafanye hivyo hivyo ,kila mmoja akawa kampima mtu wake!



    Misago akiwa kampima Isaki ,Mwalama kampima Elia,Mwanamtakala kampima Abdull Misago akaachia amri



    "Pigaaaaaaaaaaaa" wote wakaachia mishale yao sambamba na yeye



    "Mamaaaaaaaaaaaa"



    Mayowe yalisikika Abdul na Elia wakaenda chini,mishale ikiwa nyuma ya migongo yao ila ule alopigwa Isaki alijikuta akiukwepa pasina mwenyewe kujielewa.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Moyo ulimsukuma kuwarudia wenzake lakin alipogeuka nyuma aliwashughudia maadui zake wakimpima kwa mshale ikamlazimu kuendelea kumvuta Sendaye Wake kwa nguvu!



    Moyoni mwake alikuwa na uchungu sana!



    Vijana wale walipofikia ile miili wakasimama



    Mwanamtakalaaaaa



    Ikyareeeee



    Acha Mimi niendelee kumfukuza huyu mtu mweupe wewe mbebe huyu na Mwanamtakala mbebe yule mpaka mahali alipo Mabaru kateni vichwa vyao muelekee kwa mfalme mi huyu anishindi muda tu narejea na kichwa chake na cha Sendaye!



    Vijana wale wakakubali na kuanza kuiburuta miili ile kurudi nayo alipotoka!,Misago na mbwa wake wakanza kusonga mbele!



    Sendaye na Isaki walizidi kukimbia na ghafla Isaki akaangukia magoti na kuachia ukunga Mkubwa alikuwa na uchungu usioelezeka kuwapoteza wenzake alokuja nao!



    Sendaye ikabidi aanze kumbembeleza na kumsihi waendelee kukimbia kwani bado walikuwa katika hatari kubwa Isaki miguu ilimlegea moyo ukaanza kumwenda mbio



    "Jemes rafiki yang acha hicho unachowaza jua ni hatari kwako na kwetu pia unajua sifa za huyo mfalme Leo hii aje agundue unatoka na Mke wake unajua ni nini kitatupata sisi?!"



    "Ha ha ha ha Daniel usinifunze nidhamu ya uoga nampenda yule binti na ntahakikisha nakuwa nae"



    Isaki ( jemes) alikumbuka onyo alilowah kupewa na mtafit mwenzake Daniel juz tu lakini akutaka kumsikiliza na Leo amewaponza wenzake wamekufa kikatili uchungu ukazidi kumvaa na kuzidi kulia!



    "Nisamehe Daniely ulinshahur mwanzo sikukusikia Leo hii aupo tena nasi Danieliiiiii,Nisamehe Patrick,.....



    "Wooooow wooooooow wooooooooow"

    -

    Wakati Isaki akizidi kulia ghafla akasikia sauti ya mbwa ni kama kitambulisho cha hatari wakaangaliana na Sendaye kwa wasiwasi wakaambizana nyoyoni na ghafla wakainuka na kuanza kukimbia,kuikwepa hatari ile lakini hata hawakufika mbali!



    Kizunguzungu kikal kikamshika Isaki ghafla na kumpeleka chini, lilikuwa ni jambo la ghafla sana!



    Sendaye alichanganyikiwa akajitahidi kumuamsha Isaki pasina mafanikio



    Isaki hakuwa na ufahamu!



    Sauti za mbwa zikazidi kusikika zikikaribia ,Sendaye akajaribu kumnyanyua ambebe kwa uzito alokuwa nao napo pia akashindwa!



    Angefanyaje?!....



    Kwambali akawaona mbwa wakija kwa kasi wazo lililomjia ni kukimbia kuokoa maisha yake hakukuwa na njia yoyote ya kumuokoa Isaki



    Mwanamke akatoka nduki!



    ****



    Pale alipolala Isaki ghafla mbwa wale walifika na kuanza kumng'ata wakibweka kwa ukali,



    Misago akatabasamu na kuchukua kisu chake lengo achinje kichwa kile na kuondoka nacho!



    Taratibu akawasogelea mbwa wale walokuwa bado wakiendelea kumdonoa donoa Isaki na kutoka na mabonge ya nyama



    "Odo achaaaaaa....



    Akawapa amri mbwa wale,mbwa wakasitisha akamsogelea Isaki akamwelekezea kisu shingoni na kuanza kuikata shingo taratibu....



    *****

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    HIMAYA YA MFALME



    Mfalme wala hakurudi kulala,na hata angerudi usingiz angeupatia wapi?!



    Baada ya kuwatuma walinzi wake alitaka kujua kitakachoendelea ndani ya msitu ule mnene wenye kutisha,wenye wanyama wakali msitu mkuu wa kijiji kile!



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog