Search This Blog

BAHARI YA HINDI - 2

 







    Simulizi : Bahari Ya Hindi

    Sehemu Ya Pili (2)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakati Roda anajiuliza maswali hayo..ghafla ikasikika sauti ya mtoto wa kiume ikiongea kwa lugha ya kiarabu,, sauri hiyo ilijirudia rudia(mwangwi) Roda akastaajabu..akachungua tena....lakini hakumuona mtu anayetoa sauti hiyo!!!

    akaingiwa na hofu akageuza shingo yake kutazama mbele ili atimue mbio kurudi kule sehemu ya abiria,, akashtuka kumuona yule mtoto akizipiga hatua kutokea kule sehemu ya abiria akija upande ambao Roda kasimama!!!Roda akaingiwa na hofu kwa sababu alimuona mtoto huyo kaingia chooni alafu sasa hivi anamuona anatokea kwenye sehemu ya abiria...

    yule mtoto akazidi kuzipiga hatua kumsogelea Roda...wakat huo  Macho yalikuwa yamemtoka Roda akataka kupiga kelele kutokana na mauzauza aliyoyaona....ghafla akaonekana abiria mmoja wa kiume akija upande huo huo kwa lengo la kwenda chooni kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo,,,

    wasiwasi ukaanza kupungua kwa Roda....akamtazama yule mtoto kwa macho ya uwoga.

    yule mtoto akafungua mlango na kuingia chooni huku akimtazama Roda kwa macho ya msisitizo,,,,Roda akaamua kuzipiga hatua kutoka kwenye korido hiyo,,na kuelekea kule kwenye sehemu ya abiria...

    yule abiria wa kiume akafungua mlango na kuingia chooni....

    kabla Roda hajafika mnali akasikia sauti ya mtu akipiga kelele huku akigonga gonga mlango ufunguliwe atoke nje..ghafla sauti hiyo haikusikika tena...

    Roda akatimua mbio na kuelekea kwenye kiti chake..akaketi,,huku akipumua kwa mfululizo,,aliogopa hata kugeuza shingo yake kutazama kushoto wala kulia...ghafla wingu likatanda nda mvua ikaanza kunyesha.



    ***************************



    wakati huo huo upande mwingine walionekana mabaharia kadhaa wakiingia kwenye moja ya chemba inayoelekea kule kwenye injini za Meli...bila kuchelewa ukaletwa mtungi wa gesi maalumu kwa kuchoma(kuunganisha) chuma chepesi..na kazi ikaanza mara moja.

    wakaiziba paipu hiyo kisha baharia mmoja akatoka na kupandisha kule juu kumpa taarifa Sam kuwa tayari wameshamaliza kufanya matengenezo,,hivyo awashe mitambo Meli iwake na safari iendelee.....

    upande wa nje mvua kubwa iliendelea kunyesha mfululizo,,Ghafla!!! likaonekana wimbi kubwa kupita kiasi likiifuata meli hiyo...likaizonga na kuifunika Meli  ikatoweka kimiujiza..







    Hakuna abiria yeyote aliyefahamu nini kimetokea!

    Kwa sababu kilikuwa ni kitendo cha sekunde moja tu...Meli hiyo ikajitokeza kwenye sehemu tofauti kabisa...hata Sam(Nahodha) alishangaza sana kila akiangalia muelekeo ulionesha tofauti katika kifaa maalumu (DIRA) (COMPASS) cha kuangalia muelekeo wa meli inapokwenda..kilionesha meli hiyo inaelekea magharibi mwa bahari ya hindi..akashtuka akatazama nje ya meli hiyo kwa kupitia kioo cha Meli hiyo,,kilichokuwa maalumu kwa Nahodha kutazama ulande wa nje.

    Sam akashuka kuona bahari nyingine tofauti ma muonekano wa bahari aliyoizoea siku zote akiwa anakiendesha chombo hicho majini..

    akaamua kufungua mlango akatoka na kuelekea kwenye chumba cha abiria..akastaajabu kuwaona abiria hawana wasiwasi kabisa...wametulia tuli..

    Sam akaamua kuelekea  kwenye chemba inayotokezea ke chini kwenye injini za meli hiyo.

    alipofika akastaajabu kuwaona mafundi wa meli hiyo(mabaharia) wakiwa wanapiga stori bila wasiwasi! Sam akauliza,,"jamani mbona kama mimi naona meli inaelekea magharibi na bahari inaonekana tofauti kabisa inatisha kupita kiasi..wale mabaharia wakashtuka wakaamua kuingia kwenyechemba inayotokezea nje kabisa ya meli hiyo(upande wa juu)



    **********************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine alionekana Roda akiwa bado kaketi kwenye kiti chake..lakini alionekana kuwa na wasiwasi na hofu kubwa...akanyanyuka na kuzipiga hatua kuelekea kwenye korido inayotokezea nje ya meli....kwa mbali akamuona yule Bibi kizee akiishirizia kwenye kona...Roda akashtuka akageuka ili arudi kwenye kiti chake..ghafla akakutana uso kwa uso na yule mtoto akiwa amesimama mbe yake..Roda akaingiwa na hofu,,macho yakamtoka huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi ya ajabu..

    punde si punde taa zikazimika na kujiwasha zenyewe,, Roda akatazama ile sehemu aliyokuwa kasimama yule mtoto,,hakumuona tena...hapo Roda akagundua kuwa ile ndoto aliyoiota sio ya kawaida..na hicho anachokiona sasa hivi sio ndoto tena bali ni kweli,anashuhudia kwa macho yake...akatimua mbio kurudi kule sehemu ya abiria. ghafla taa zikazimika tena...

    abiria wengine hawakuwa na wasiwasi,,walijua huenda radi zilizokuwa zinapiga nje..zinasababisha,,mgusano wa nyaya (shot) ndio sababu taa zinazimika na kujiwasha zenyewe..

    Roda akashindwa kuvumilia akapaza sauti na kusema,,"JAMANI TUSIKILIZANE. humu ndani ya Meli kunamauza uza na nimeyashuhudia kwa macho yangu...

    kabla Roda hajaongea neno lingine ukasikika mngurumo wa kutisha sana..kisha taa zikazimika.

    sasa hivi taa hazikuwaka tena,,giza likatawala...ghafla ulengurumo ukatoweka..na ukimya ukatawala..

    taa zikawaka abiria wote wakaanza kupiga mayowe ya uwoga baada ya kuona baadhi ya abiria wakiwa wameuwawa na mtu asiye fahamika !! ni kitendo cha sekunde ikawa ni mtafutano ndani ya Meli hiyo..kila abiria alikimbia kutafuta sehemu ya kujificha lakini ikashindikana...kelele za vilio zilitawala ndani ya Meli hiyo..punde si punde..taa zikazimika tena!!!!

    abiria wote wakabaki kimya bila kujua hatma yao ni ipi?

    ikasikika sauti ya milango ya chuma ikijifunga...ghafla taa zikawaka....abiria walipojaribu kufungua milango haikufunguka ilikuwa imefungwa..hakuna aliyeweza kutoka nje ya Meli hiyo...



    *************************



    Upande mwingine,,walionekana mafundi wa meli hiyo(mabaharia)kule kwenye chemba ya kutokezea nje ya Meli hiyo wakiwa wanazipiga hatua mdani ya chemba....ghafla mlango ukajifunga...wakatimua mbio kuufuata mlamgo wa kutokezea nje kabisa,,walipoukaribia pia ukajifunga...kisha taa zikazimika...giza likatawala..lilikuwa ni giza totoro ambalo huwezi kuona kitu kilichopo mbele yako.. ghafla ikasikika sauti ya Baharia mmoja akipiga mayowe ya kuomba msaada...wale mabaharia wengine wakaingiwa na hofu!! punde si punde ikasikika sauti ya baharia mwingine akivurutwa na mtu asiyeonekana akapiga kelele ghafla sauti ikanyamaza na maji yakawarukia wale mabaharia wawili waliobaki ndani ya chemba hiyo..

    baharia mmoja akashtuka kumwagikiwa na maji usoni mwake..akajifuta maji yale akanusa...akashtuka kusikia harufu ya damu mbichi na sio maji!!! akamwambia mwenzake kuna hatari! hatupo sehemu salama..wakaanza kupiga kelele za kuomba msaada..



    kule kwenye upande wa injini zilipo alibaki baharia mmoja alikuwa ni mtumiaji wa kilevi aina ya bangi!

    alishindwa kuongozana na wenzake akabaki hapo kumalizia kuvita kipisi cha bangi..ghafla akasikia sauti za mabaharia wenzake wakiomba msaada..

    akaamua kuufuata mlango ili awafungulie wenzake..

    alipoufungua kikarushwa kiwiliwili cha mmoja kati ya mabaharia walioingia kwenye chemba hiyo..kikiwa nusu,,kuanzia kiunoni kushuka chini..

    kiwiliwili hicho kikadondoka mbele yake..akashtuka akajisemea moyoni,,"bila shaka hizi ni bangi zimenilevya, Binadamu gani anakuwa nusu!! akachuchumaa na kugusa damu,alipozinusa akagundua kuwa ni damu..akili ikamkaa sawa,,akanyanyuka haraka huku akiwa na hofu kubwa kupita kiasi..akaifuata chemba inayotokezea kule kwenye ulande wa abiria..gjafla akamuona ye Bibi kizee akiwa anazipiga hatua kuja upande wake..lakini alipomtazama kwa makini akaona Bibi kizee huyo miguu yake haikanyagi chini..anatembea hewani..

    alipogeuza shingo yake ili atimue mbio kutafuta chemba nyingine akakutana uso kwa uso na yule mtoto..wakatazamana machoni!! ghafla damu zikaanza kutoka machoni mwa Baharia huyo huku akihisi kukabwa shingoni..akakosa pumzi akashindwa kupumua akadondoka chini ma kupoteza maisha..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    **********************



    kule juu sehemu ya abiria,,alionekana Roda akiwa anatafuta sehemu ya kujificha..kwa mbali akaona kuna  chumba kipo wazi hakijafungwa mlango akatimuabio kukifuata chumba hicho akajifiche..akaingia haraka ndani ya chumba hicho akaufunga mlango haraka.....akasimama kando..ghafla akasikia mlango huo unafujinga wenyewe kwa ufunguo. punde si punde taa iliyokuwa inamulika ndani ya chumba hicho ikazimika na giza likatawala....Roda akaingiwa na hofu kubwa kupita kiasi baada ya kusikia vishindo vya mtu akitembea ndani ya chumba hicho..





    Hofu ikazidi kuongezeka! akapiga kelele ghafla taa ikawaka.na mlango ukafunguka wenyewe.Roda akaogopa hata kutoka nje ya chumba hicho,akabaki kasimama,,

    Kelele za abiria wakipiga mayowe ya kuomba msaada zilitawala ndani ya meli hiyo..

    Roda akazipiga hatua za taratibu kutoka ndani ya chumba hicho huku macho yake yakitazama kwa umakini wa hali ya juu...alipotoka  ndani ya chumba hicho..akatimua mbio..kutafuta uwezekano wa kujificha...



    *************************



    Upande mwingine alionekana Sam akiwa amejifungia katika kile chumba maalumu cha kuiongoza meli...Sam alikuwa na wasiwasi kupita kiasi..akatazama upande wa nje,kwa kupitia kile kioo cha nahodha kutazama upande baharini.

    Sam akashtuka kuona Giza limetanda ndani ya sekunde moja...Sam akaogopa akafungua mlango na kutimua mbio kuelekea sehemu ya abiria,,akashtuka kuina abiria wote wanatafuta jinsi ya kutoka nje ya meli hiyo,,huku abiria wengine wakiwa chini wameuwawa...damu zilionekana kutapakaa kila kona ndani ya meli hiyo!! utadhani ni uwanja wa vita.



    *******************



    upande mwingine alionekana Roda akiendelea kutafuta sehemu ya kujificha.......alipoangaza macho yake kwa mbali akaona chemba moja ikiwa wazi..akaamua kuifuata chemba hiyo akaingia haraka akajifiche...akapita ndani ya chemba hiyo akajikuta anatokezea kule chini kwenye injini za meli hiyo.akatereza nakudondoka akaangukia juu ya maiti ya mmoja kati ya mabaharia waliouwawa...Roda akapiga kelele kwa sauti kalinmfululizo..akanyanyuka haraka akatimua mbio pasipo kujua ni wapi anaelekea...akaingia kwenye chemba nyingine..akapita humo akajikuta anatokezea nje ya meli(upande wa juu) akastaajabu kumkuta ye bibi kizee akiwa amesimama peke yake.bila kuonekana mtu mwingine yeyote...Roda akajificha akaendelea kuchungulia ili aone Bibi kizee huyo anafanya nini..

    akamuona ananyanyua mikono yake juu ghafla Bibi kizee huyo akageuza shingo yake haraka akatazama ule upande aliokuwepo Roda..

    sura ya Bibi huyo ikabadilika na kuinekana kutisha sana kisha bibi huyo akamfuata Roda huku anazioiga hatua hewani hewani..Roda akajikuta anapiga kelele akatimua mbio kuridi ndani ya chemba ghafla Roda akamuona ye bibi kizee ndani ya chemba hiyo akiishirizia mguu wa mwisho kutoka ndani ya chemba hiyo..

    Roda akahisi kuchanganyikiwa akaitimua mbio kurudi upande wa nje ya meli..akaufunga mlango wa chemba hiyo kwa komeo la nje..

    akaangaza angaza macho yake pande zote..kwa mvali akaona taa inawaka baharini..akagundua kuwa ni boti ndogo inakuja upande huo..akaanza kupata matumaini...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******************************



    upande wa ndani ya meli hali ilizidi kutisha zaidi..yule bibi kizee alijitokeza mbele ya Sam akakutanisha macho na Sam...ghafla Sam akabadilika  akuingiwa na roho ya kikatiri kupita kiasi...bibi kizee huyo akatoweka kimiujiza..

    Sam akaingia ndani ya meli akabadilisha muelekeo wa meli ikawa inaelekea mashariki mwa bahari ya hindi...aliiongoza meli hiyo pasipo yeye kujitambua mpaka ukingoni mwa bahari..kwenye sehemu iliyoonekana kuwa na mapango na miamba mikubwa kupita kiasi...Kwa mbali akaonekana mwanamke amelala nchi kavu akiwa.nusu binadamu nusu samaki...mwanamke huyo akajivuruta akaingia ndani ya bahari na kutokomea kusikojulikana..

    Roda alishuhudia tukio hilo kwa sababu alikuwa kule nje juu ya meli hiyo.pia taa kubwa ya meli hiyo ilimulika vyema ulande wa nje...hofu ikazidi kuongezeka akakosa pa kukimbilia..aliogopa kurudi ndani ya meli kwa sababu alishuhudia mauzauza na mauwaji ya kutisha..ghafla meli hiyo ikaanza kuzama taratibu kuelekea chini ya bahari...Roda akaingiwa na wasiwasi!! macho yakamtoka akatafakari nini cha kufanya lakini alishindwa akaamua kuruka kutoka juu ya meli na kujitosa baharini...akastahajabu maji hayamgusi..huku akizidi kuelekea chini zaidi..akaanza kupiga kelele..lakini kelele hizo hazikumpa msaada..akazidi kuelekea chini..akiwa ndani ya maji hakuweza kuona kitu chochote kwa sababu ya giza kuwa totoro...lakini alizidi kustaajabu akajiuliza,,"mbona maji hayagusi mwili wangu? yani kama nipo angani..wakati anajiuliza maswali hayo yasiyokuwa na majibu..ghafla akaanza kuona mwanga  chini ya bahari..mwanga huo ulimulika pakawa kama mchana...akaanza kuona majengo na magari ya kifahari huku watu wakiendelea na shughuri zao kama wapo nchi kavu....alipoangaza angaza macho yake akashtuka kumuona yule bibi kizee....

    Macho yakamtoka Roda ghafla akaangukia juu ya paa la nyumba..akashtuka akaingiwa na hofu kubwa kupita kiasi... punde si pundeikasikika sauti ikisema..ebu katazame nini kimedondika juu ya bati... Roda akajaribu kupiga mbizi akadondika kutoka juu ya paa la nyumba hiyo..akaanguka chini..wakati anatahamaki...yule mtoto akajitokeza mbele yake akagusa mwili wa Roda....yule mtoto akaanza kubadilika...ngozi yake ikaanza kujivua yenyewe mwilini..kumbe ni mwiko kugusa mwili wa binadamu wa kawaida..kitendo hicho kikamshtua Roda macho yakamtoka..ghafla akasikia sauti ya kitu kikidondoka kutoka juu..aliponyanyua shingo yake alishtuka kuiona meli ikiangukia hiyo sehemu aliyosimama..ni ile meli iliyozama muda mchache uliopita yeye akajitosa baharini..

    Roda akatimua mbio ghafla akavutwa na mtu asiyeonekana......







    Akajikuta yumo ndani ya jumba la kifahari.akashtka sana hakujua amefikaje fikaje ndani ya nyumba hiyo..akaangaza angaza macho yake. hakuina mtu hata mmoja kuinekana ndani ya jumba hilo la kifahari...akazipiga hatua za haraka haraka akaufuata mlango alipojaribu kuufungua mlango haukufunguka ulikuwa umefungwa kwa nje.,,,akaamua kuchungulia dirisha..akastaajabu kuona ile meli imegota chini..huku bahari imebadirika rangi na kuonekana ni damu tupu..damu hiyo ilizunguka kwenye eneo la meli hiyo pekee..Roda akaingiwa na hofu,,akajiuliza,,"hivi mimi naota! au naona kweli mambo haya yanatendeka!!!?

    Roda akanyanyua mkono wake akajipiga kofi..akahisi maumivu..akagundua kuwa hayupo katika ndoto bali anayaona mambi hayo yanatendeka kweli!!! macho yalimtoka..ghafla akamuona Mwanamke mrembo kupita kiasi..mwanamke huyo alikuwa anatokea upande wa ndani ya meli..huku mdomo wake ukiwa umezungukwa na damu...

    Roda akastaajabu kuona zile damu mdomoni mwa mwanamke huyo hazisambai wakati maji ya bahari yamemzunguka mwanamke huyo!!!.lakini mwanamke huyo alikuwa anazipiga hatua kama anatembea nchi kavu...Roda akatazama miguu ya mwanamke huyo haikuonekana ilikuwa imefunikwa na gauni refu lililokuwa linaburuza chini. ghafla mwanamke huyi akatoweka kimiujiza haikujulikana ni wapi kaelekea..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roda akazidi kuchanganyikiwa..akajikuta anaangua kilio bila kujua hatma yake ni nini...

    kwa mbali akamuona yule bibi kizee akizipiga hatua kuifuata nyumna hiyo..Roda akaingiwa na wasiwasi,,hofu ikazidi kuongezeka..akatimua mbio akaingia kwenye chumba kilichokuwa karibu na sebule...akajifungia humo..akaangaza angaza macho yake akastaajabu kuona vitu vingingi vya thamani..vitu hivyo vilitengenezwa kwa madini ua dhababu tupu...ghafla kumbukumbu ikamjia! akakumbuka marehemu babu yake aliwahi kumsimulia kuhusu majini...pia akakumbuka kuwa makazi yao ni baharini sehemu yenye kina kirefu sana..ghafla akahisi kunusa marashi..marashi hayo yalinukia vyema kupita kiasi...

    akashtuka akajisemea moyoni,,"bila shaka nipo kwenye himaya ya majini.Eee Mungu ninusuru nitoke salama..



    Punde si punde akabmuona yule Bibi kizee kaingia ndani ya chumba hicho pasipo mlango kufunguliwa...bibi kizee huyo alioenda kwenye ukuta kama upepo na kujitokeza upande wa ndani.

    Roda akapiga kelele..lakini kelele hizo hata yeye mwenyewe hakuzisikia!!! ingawa alikuwa anapaza sauti kali lakini sauti haikutoka..

    yule bibi kizee akaketi kwenye kiti kilichokuwa ndani ya chumba hicho,, akaanza kumuongelesha Roda kwa lugha iliyofanana na maneno ya lugha ya kiarabu..Roda akabaki mdomo wazi huku amekodoa macho kumtazama bibi huyo...

    Ghafla Roda akanza kusikia na kuielewa lugha hiyo!! akajisemea moyoni,,"mbona sijawahi kujifunza lugha hii!!! iweje nasikia na kuelewa kile anachokiongea huyu bibi kizee!!?

    wakati Roda anawaza hayo yote..

    bibi kizee huyo akaonge tena kwa ligha hiyo..

    Roda akaelewa kilicho ongelewa bibi huyo alimaanisha kuwa,,"umefanya kosa kubwa ambalo ni vigumu kuepuka adhabu ambayo unastahiri kuipata..kulingana na kosa ulilolifanya.

    Roda akashtuka kusikia hivyo..hofu ikazidi kuongezeka,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi zaidi huku jasho likimtoka kwa uwoga wa hali ya juu.

    ghafla bibi kizee huyo akatoweka kimiujiza!

    ikasikika sauti ya milango ikijifungua yenyewe..kila baada ya sekunde..

    Roda akatimua mbio kutoka ndani ya chumba hicho akaelekea sebuleni akashtuka kumuona Tobi ameketi kwenye sofa,,Roda akastaajabu sana akauliza kwa mshangao,,"na wewe wamekuleta huku??

    Roda aliuliza swali hilo huku akimtazama Tobi..lakini Tobi alionekana kutokuwa na wasiwasi kuwepo sehemu hiyo..

    furaha ya Roda ikaanza kurejea taratibu,,kwa sababu kamuona mtu wake wa karibu anaye fanya nae kazi katika kituo cha habari.

    (uandishi wa habari),,,Roda akazipiga hatua za haraka haraka mpaka kwenye sofa alilokuwa amelikalia Tobi..akamuuliza,"kulikoni mbona upo hapa!? hivi unaweza kuitambua sehemu hii?

    Tobi akatabasamu tu,bila kujibu kitu chochote.

    Akabaki kimya kwa sekunde kadhaa kisha akanyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi.akazipiga hatua kadhaa,,akasimama akageuza shingo yake na kumtazama Roda..

    Roda akaanza kuingiwa na hofu..alishangazwa na kitendo cha Tobi kutokuwa na wasiwasi kabisa..yani Tobi alionekana kama hapo ni nyumbani kwake..au sehemu anayoijua..

    Tobi akasema,,"Roda...mbina unaonekana kuwa na wasiwasi? kuwa huru jisikie upo nyumbani.

    Machi yakamtoka Roda baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kinywani mwa Tobi!!

    Roda akaingiwa na hofu akauliza kwa sauti ya msisitizo,,"nijisikie nipo nyumbani??

    Tobi acha utani hii ni sehemu ya majini!! wewe huogopi??

    Tobi akacheka kwa sekunde nyingi. kisha akasema,,"bila shaka haujakosea..hapa ni nyumbani kwetu nilipozaliwa..na yule bibi kizee uliyekuwa unaongea nae ni mama yangu mzazi..na yule mtoto uliyekuwa unamuona mara kwa mara ndani ya meli ni mimi..

    Rose akaanza kumuogopa Tobi!! akajisemea moyoni,,"inamaana Tobi kayajuaje haya yote wakati nilimuacha Mombasa pale bandarini baada ya yeye kusahau tiketi yake nyumbani!!!

    kumbe Tobi alikuwa anajua kila kitu anachokiwaza Roda akilini mwake..

    Tibi akasema,,"ni kweli uliniacha lakini tulisafari safari moja pasipo wewe kujua...lakini kini ulifanya kosa kubwa ambalo limemfanya mama yangu ambaye ni Malkia wa bahari kukasirika sana.

    Roda akadakia,,akauliza kwa mshangao,,"KOSA!!! KOSA GANI HILO?

    Tobi akajibu,,"kunakitu ulibeba ndani ya begi lako..

    pia kuna kitu umekivaa mwilini mwako..vitu hivyo ni adui wa Malkia wa Bahari.ambaye ni mama yangu.

    Roda akauliza kwa mshangao,,"mbona sikuelewi Tobi!! inamaana wewe ni jini??? na mbona haukuniambia miaka yote hiyo tuliyofanya kazi pamoja,,na wewe ni rafiki yangu wa karibu!!

    pia kwa nini usinge niambia tangu jana kabla sijaianza safari?

    Tobi akasema sio jani..ni miaka kumi imepita..sisi kwetu huku ujinini.siku moja ni miaka kumi kwetu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roda akashtuka sana hofu ikazidi kuongezeka akamtazama Tobi kwa macho ya uwoga...

    Tobi akasimama akasema humu ndani,,hivi vitu vyote uvionavyo sio vipya kama uonavyo kwa macho yako,, wala hii siyo nyumba ya kifahari..Tobi  alipomaliza kuongea maneno hayo ghafla muinekano wa ndani ya  nyumba hiyo ukawa wa kutisha kupita kiasi..Punde si punde Tobi akabadilika na kuwa na muonekano kama mzee wa miaka tisini(90)





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog