Search This Blog

CHOZI LA UKOMBOZI - 3

 







    Simulizi : Chozi La Ukombozi

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    asubuhi palipokucha komba alidamka mapema na kuanza kufanya mazoezi ya kupambana kwa utumia panga...... mazoezi hayo huwa anayafanya peke yake pasipo mtu kumuona.......alipomaliza mazoezi hayo....aliamuru jeshi lijipange kwa ajili ya mazoezi ya pamoja...wakati komba amesimama akiwaangalia wanajeshi wake wakiendelea na mazoezi....punde alikoswa na mshale uliopita karibu na uso wake....alipogeuka kwa mbali alimuona prince mody akichukua mshale mwingine na kuuweka kwenye upinde....komba aliamua kujihami alichomoa upanga wake....na kuupangua mshale ule uliokuwa ukijakifuani kwake....kisha akakimbia na kupanda farasi wake akatoka nje ya ngome ya kifalme....na kutokomea kusikojulikana.....



    ****************



    ule ulande mwingine alionekana mazy akitoa mafunzo ya nguvu kwa jeshi lake....kisha akaandaa mpango wa kuvamia falme ya ghemi.......kisha akamtuma mmoja wa wanajeshi wake aende akachunguze kama kunaulinza katika mipaka ya ghemi.....mwanajeshi huyo kabla ajaanza kuingia kwenye mpaka wa falme ya ghemi alimuona komba......aliweza kumtambua komba kuwa ni mtu hatari sana...hivyo aligeuza na kurudi alipotoka........alikimbia mpaka kwa mazy...alipofika alitoa taarifa.....mazy alichukia sana akasema huo ni uzembe...kisha akachomoa upanga na kumchinja mwanajeshi yule....

    kisha akasema"" kwa yeyote atakayekuwa mzembe kama huyu nitachinja shingo yake....



    **************



    ule upande mwingine alionekana komba akielekea kule alipozaliwa kwenye kisiwa cha Dhaho....alikwenda moja kwa moja mpaka kwenye ile nyumba aliyokuwa akiishi na yule babu aliyemlea.....alikuta nyumba ile imechakaa sana alipoingia ulande wa ndani kulikuwa na uchafu ukiambatana na vumbi..pamoja na tando za buibui....komba aliamua kusafisha nyumba hiyo.....kisha akajiegesha hapo mpaka kesho yake....palipokucha alihisi kunawatu wanamfatilia!!!!alipochungulia dirishani aliona wanajeshi wa ghemi wakija kwenye nyumba hiyo....kumbe yule mzee ramuh alitengeneza maficho chini ya Aridhi ndani ya nyumba hiyo...kwa sababu komba aliishi hapo alikuwa anaujua mlango wa kuingilia huko chini mafichoni.....aliingia haraka....



    wanajeshi wale walivamia nyumba hiyo lakini hawakuweza kumuona komba waliamua kuchoma moto nyumba hiyo kisha wakapanda farasi nakutokomea kusiko julikana....Joto kali lililosababishwa na moto lilimfanya atoke kule chini mafichoni alipotokeza upande wa juu alistahajabu kuona moto mkubwa umetanda ndani ya nyumba hiyo alikurupuka na kukimbilia upande wa nje ilikuokoa maisha yake......uso wa komba ulionesha kujawa na gadhabu ya hali ya juu kisha akajisemea moyoni"lazima nilipe kisasi"alipanda juu ya farasi wake aliekuwa amemfunga kando kando ya mti na kutokomea kuelekea kunako msitu



    Baada ya siku tatu kupita komba alitengeneza silaha,aliongeza mishale mingi ya kutosha

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******



    Uleupande mwingine katika falme ya GHEMI alionekana mfalme kaitisha kikao nakuamuru kuwa komba akamatwe akiwa hai au amekufa prince Mody alimuunga mkono baba ake na kusema kuwa yeye ataongoza wanajeshi katika msako wa kumtafuta Komba kisha prince Mody akaamuru amri ya mfalme itekelezwe"waondoke watu kumi"alisema prince Mody bila kuchelewa wanajeshi wale walipanda farasi na kutoka nje ya lango ya falme ya GHEMI kuelekea kumtafuta Komba walimtafuta bila mafanikio mpaka giza likatanda waliamua kurudi GHEMI nakutoa taarifa kwa mfalme kwamba wamemkosa Komba



    *******



    Wakati huo huo kule kwenye falme ya BEHA alionekana Mazy akijiandaa kwenda kuvamia falme ya GHEMI kisha wakaianza safari ya kuelekea huko wakipitia njia za msituni ili wasionekane kwa urahisi na kustukiwa mpango wao,wakiwa humo ndani ya msitu Komba aliweza kuwaona lakini hakushughulika nao......wanajeshi wale walizidi kusonga mbele wakiongozwa na Mazy ambaye kwa sasa ndiye Mfalme wa BEHA...baada ya dakika kadhaa walianza kuvuka mpaka wa GHEMI na kuingia ndani kabisa....kwa sababu mazy alikuwa anazijua njia za milango ya siri kuingia ndani ya ngome ya falme ya Ghemi...aliwaongoza wanajeshi wake mpaka wakatokezea upande wa ndani.....kwa sababu jeshi la Mazy lilikuwa imara walijipanga na kuanzisha vita humo ndani ya ngome ya Ghemi....vita ilikuwa ya kufa na kupona...wanajeshi wa Mazy walikuwa wakatili kupita kiasi walichinja bila huruma.....

    jeshi la Ghemi lilionekana kuzidiwa mbinu za upiganaji....waliamua kusalimu amri...na kuweka panga zao chini.....kisha mazy akaamuru mfalme atolewe upande wa nje.......punde aliletwa....

    mfalme wa Gemy alipotolewa nje alistahajabu kumuona mwanae wa kwanza aliyetoroka miaka mingi iliyopita kabla ajazaliwa prince mody..... akiliongoza jeshi la falme ya BEHA. mazy hakumjali baba yake......kisha akachomoa upanga na kutaka kumchinja mfalme.....

    kabla hajanynyua upanga wake mara ghafla....aliona mshale umepiga kwenye upanga....kisha upanga ukadondoka kando......alipotahamaki mara ghafla.... mshale mwingine ulirushwa na kutua mbele yake karibu na mguu....mazy alikasirika alimvuta mwanamke mmoja aliyekuwa pembeni yake...na kumuwekea kisu shingoni........

    kumbe aliyekuwa akirusha mishale hiyo ni komba alikuwa amejificha juu ya kuta zilizozunguka ngome ya kifalme....komba alipangawa baada ya kumuona mwanamke yule aliyewekewa kisu shingoni....baada ya kugundua kuwa ni rubi.....mara ghafla.



    mara ghafla prince mody alipaza sauti "muache mchumba wangu.hivi kaka unawezaje kupindu utawala wa baba yako mzazi????..Mazy aligundua kuwa kumbe huyo mwanamke ni mchumba wa wa mdogo wake.....aliamua kutumia nafasi hiyo kutoroka huku kamteka rubi.....komba aliamua kuacha kurusha mishale ili aokoe maisha ya rubi....wakiti huo mzee ramuh alikuwa kajificha ndani ya shimo la takataka.....aliweza kuona kila kitu kilichokuwa kinaendelea kwa sabavu shimo hilo lilikuwa kwenye kilima....aliamini kuwa komba ndiye aliyekuwa akirusha mishale hiyo...kwa sababu ni yeye pekee ndiye alimfundisha komba kurusha mishale kwa namna hiyo.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    punde mazzu aliamuru mfalme atekwe na kupelekwa BEHA....mazy alimchukua rubi na kumpandisha juu ya farasi na kuondoka nae...

    prince mody alisikitika sana..alimkumbuka komba.." laiti kama komba angekuepo angeweza kuwadhibiti....prince mody alijisemea moyini...

    kwa sababu kakuwa na uwezo wa kupambana na kaka yake Mazy..

    komba alipohakikisha mazy na jesgi lake wameindoka.aliamua kuingia ndani ya uzio wa ngome ya falme ya Ghemi.....ghafla prince mody alimuina komba...kisha akachomoa upanga na kusema wewe mshenzi ndio umesabavisha baba yangu katekwa!!! umeshindwa kutoa msaada sasa umejileta baada ya vita kuisha!!! tazama watu walivyouwawa...alipomkaribia alirusha upanga kwenye kichwa cha komba...

    komba alipangua kisha akakimbia uoande mwingine..prince mody alimfata komba akaendelea kuleta ugomvi huku akimtukana komba.. ...komba hakutaka kupigana na prince mody .....alikuwa akipangua tu....mara ghafla komba alikanyaga damu zilizokuwa zimetapakaa chini akatereza na kuangukia kisogo...komba alipoteza fahamu......prince mody aliona hiyo ndio nafasi ya kumuuwa komba....akatupa upanga akachomoa kisu.....alipomkaribia komba....

    ghafla ilisikika sauti ikisema"""" acha kuuwa huyi mtu hana hatia.....sikuzote amekuwa akikulinda...lio hii unataka kuondka uhai wake!!!!!!

    alisema mzee Ramuh....

    maneno yale yalimuingia Prince mody...akaacha kumchoma kiau komba.....kisha akaondoka kwa hasira kuelekea upande wa ndani ya jumba la kifalme....mzee ramuh hakutaka kusema kuwa komba ni mtoto wa prince mody kwa kuhofia kuwa komba atakuwa matatani ikigundulika kwa sababu mfalme wa ghemi aliamuru mama yake komba atoswe kwenye maji...miaka 24.iliyopita.



    ***********



    palipokucha komba alizinduka baada ya kupata fahamu...alistahajabu kujikuta kalala kwenye kitanda ndani ya jumba la kifalme.....aliposhika upande wa kiuno hakuona upanga wake..akanyanyuka haraka kutoka kitandani....ghafla Mzee ramuh aliingia....na kusema""unaendeleaje??? komba alistahajabu kisha akauliza""" kwani nilipatwa na nini ??!mbona nahisi maumivu makali kisogoni....

    ramuh aligundua kuwa komba hajakumbuka yale yote yaliyotokea jana...akamdanganya""ulidondoka ulipokuwa ukitembea....akaangukia kisogo na kupoteza fahamu.....komba alibaki kimya hakuuliza tena..



    ************



    ule upande mwingine alionekana Mazy akimpa mateso makali baba yake...alimtesa masaa matatu mfululizo kwa kumchapa viboko vingi visivyokuwa na idadi...kisha akaamuru mfalme apelekwe kwenye chumba kilichokuwa na maji yanayofika shingoni.......amri ilitekelezwa mfalme wa ghemi akawekwa ndani ya chumba hicho...mazy hakuwa na huruma hata chembe..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **************



    kule ghemi alionekana prince mody kuwa katika hali ya mawazo alimfikiria mchumba wake rubi na baba yake mzazi.....prince mody aliamua kutoka nje akazipiga hatua kutoka nje akapanda farasi wake na kutoka nje ya lango kuu la ngome ya falme ya ghemi...kaba hajafika mbali mara ghafla...



    mara ghafla alivamiwa na wanajeshi wa falme ya Beha...wakamzunguka...punde komba alitokea akamuokoe prince mody....komba aliwauwa wale wanajeshi waliotaka kumteka prince mody....

    kisha komba akauliza"" ulikuwa unakwenda wapi?? huoni kuwa ni hatari kwako kutembea peke yako bila ulinzi....pince mody alistahajabu kuona komba kaokoa maisha yake kwamara ya tatu......lakini prince mody hakuongea chochote wala hakumshukuru komba kwa msaada alioutoa kwake........aligeuza na kurudi Ghemi.....komba aliamua kumfuata kwa nyuma....wakafika ghemi waliingia ndani ya ngome ya kifalme.....prince mody alishuka kutoka juu ya farasi wake akazipiga hatua kuelekea upande wa ndani.....komba alimuta prince mody....akasita kutembea kisha akageuka na kumtazama komba...komba akazipiga hatua za harakaharaka kuelekea ule upande aliokuwa amesimama prince mody.kisha akasema"" kama nimekukosea naomba unisamehe sina mahusiano ya kimapenzi na mchumba wako rubi....

    prince mody alijawa na hasira baada ya kusikia komba akitaja jina la mchumba wake...akachomoa upanga na kuanza kumshambulia komba....komba alikwepa kwa kuhamahama upande wa huku na kule...punde alikuja mzee ramuh na kumkataza prince mody....ramuh akasema"" kwa nini unagombana na mtoto wako wa damu!!!!prince mody alistuka akasita kuendelea kumshambulia komba......kisha akamtazama mzee ramuh kwa macho ya mshangao......hata komba naye pia macho yalimtoka baada ya kusikia hayo maneno aliyoyasema mzee ramuh....

    kisha ramuh akaanza kueleza yale yaliyotokea miaka mingi iliyopita....alisimulia jinsi nino alivyotoswa baharinihuku akiwa na mimba ya kukaribia kujifungua.....akasimulia jinsi alivyokutana na komba akiwa na umri wa miaka mitano....pia akasimulia jinsi alivyomkuta nino kauwawa na wanajeshi wa Falme ya Beha baada ya kupigwa mshale wa sumu upande wa shingoni.prince mody aliuliza kwa mshangao

    ""unamaanisha nino alibaki hai baada ya kutoswa baharini!!!!! ?? inamaana huyu ndiye mtoto aliyezaliwa na nino!!!!

    ramuh alijibu"" ndio!! komba ni mtoto wako wa damu....prince mody alizidi kushangaa kisha akamtazama komba....kisha akazipiga hatua mpaka pale alipokuwa amesimama komba....akasema"" nisamehe mwanangu...prince mudy aliongea hivyo huku machozi yakimtoka.....komba alimkumbatia baba yake kisha akasema" usilie baba...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***************



    kesho yake asubuhi komba aliandaa mpango wa kuliweka sawa jeshi lake ili waende kuvamia falme ya beha kumuokoa Mfalme pamoja na rubi...

    wakati huohuo mazy alikuwa akiandaa mpango wa kumnasa komba ili amuuwe kwa sababu komba alionekana kuwa kikwazo cha mipango yake...mazy alimuita mlinzi mmoja alikuwa akimuamini....kisha akasema"" fanya juu chini hakikisha unamlete komba akiwa hai au amekufa.....Mlinzi yule alikuwa ni moto wa kuotea mbali alikuwa ni mrefu mnene na mwenye nguvu kupita kiasi...mikono yake ilikuwa na misuli mikubwa na mwili wake ulionekana na makovu mengi ya panga na mishale......mlinzi huyo alichukuwa wanajeshi kumi kisha wakapanda farasi na kwenda kumtafuta komba.....

    wakati huo huo prince mody pamoja na komba walionekana wakitoka kwenye lango kuu la ngome ya falme ya Ghemi....komba alionekana kuwa na jazba na hasira kali baada ya kugundua mfalme aliyetekwa ni babu yake.......pia mama yake aliuwawa na wanajeshi wa Beha......""lazima nilipize kisasi nitaangamiza jeshi la falme ya beha kisha maiti zao nitazichinja na kun'goa vichwa vyao......alijisemea moyoni.....

    prince mody na komba walikuwa wanaelekea beha ili wachunguze njia za kuingia ndani ya ngome kinyemela wamuokoe mfalme na rubi...

    wakiwa njiani ghafla walikutana uso kwa uso na yule mlinzi wa mazy huku akiwa na wanajeshi kumi juu ya farasi wao....komba alimuongoza farasi wake asimame...pia price mody alifanya hivyo hivyo.......wale wanajeshi kumi wa beha waliwavamia na mapigano yakaanza komba aliwachinja wote wakafa akabaki yule mlinzi......akashuka kutoka juu ya farasi na kuelekea ule upande aliokuwa amesimama komba na baba yake....kisha akaanzisha mapigano....

    mapigano hayo yalikuwa ya kufa na kupona kwani mlinzi yule alikuwa na nguvu kuliko komba na baba yake..prince mody aliingilia kumsaidia komba....lakini alikatwa upanga upande wa tumbo..akadondoka chini...

    komba alikasirika sana alipigana kwa nguvu zake zote....mapigano hayo yalidumu ndani ya masaa mawili mfululizo....mpaka komba akachoka...hata yule mlinzi alichoka.....komba alikumbuka mbinu za kupigana na mtu ambae anainekana kumzidi nguvu...mbinu hizo alifundishwa na mzee ramuh..

    komba aliruka na kumpiga teke la maungio ya mogoti..mlinzi yule alihisi maumivu makali...kabla hajakaa sawa alipigwa ngumi ya chembe...akainama....komba alichukua upanga wake haraka akaunyanyua juu na kukata shingo ya mlinzi yule....kichwa kilidondoka kando.....kisha komba akakimbia pale alipokuwa amedondoka baba yake.. ..alipomkaribia prince mody alizinduka na kupata fahamu....komba alimnyanyua baba yake haraka na kumuweka juu ya farasi prince mody alijikaza akarudi ghemi....kisha komba akakichukua kile kichwa chamlinzi yule na kuondoka nacho......kuelekea Bheha.....alipofika karibia na ngome ya falme ya beha...alichukuwa kipande cha mti..kisha akakichomeka chini ya aridhi...kisha akachukua kichwa cha yule mlinzi akakichomeka juu ya ule mti....kisha akaondoka kurudi ghemi.



    ************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mazy alistahajabu kuona mlinzi anayemuamini hajarudi mpaka muda huo....punde mwanajeshi mmoja aliingia ndani ya jumba la kifalme huku anakimbia......alipomkaribia mazy....akampa taarifa kuwa yule mlinzi kauwawa na kichwa chake kimetundikwa juu ya mti....nje jirani na lango kuu...

    mazy alichanganyikiwa...hofu ilianza kutanda juu yake...







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog