Search This Blog

SHUHUDA - 4







    Simulizi : Shuhuda

    Sehemu Ya Nne (4)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    upande mwingine alionekana karimu akiingia ndani ya nyumba yake kisha akawasha laptop yake.....lakini umeme ulionekana kuwa mdogo kutokana na hali ya hewa....kwa sababu yeye hakuwa anatumia umeme wa Tanesco.....kwa sababu alikuwa amefunga vifaa maalumu vya kuakisi mwanga wa jua na kuhifadhi...mionzi ya jua...(Panel solar) aliyokuwa ameifunga juu ya bati la nyumba yake........laptop yake ilikuwa na umeme kidogo uliokuwa umejihifadhi.....kisha akachukua kifaa maalumu kilichokuwa ndani ya kabati lake...akakiwasha kifaa kile....punde gari la peter lilionekana kupitia GPRS LOCATE FINDER...iliyokuwa imepandikizwa kwenye gari lake.....karimu aliona gari hilo likielekea keko....akaamua kuchukua kifaa kile kilichokuwa kama simu ya mkononi akatoka nje....aliamua kukodi bodaboda....ampeleke keko......

    baada ya dakika 20 karimu alifika keko...kisha akalipa pesa kwa deleva bodaboda....akaanza kuzipiga hatua akakiwasha kile kifaa...kilionesha kuwa hayupo mbali na gari la peter...aliliduata gari kwa kuongozwa na kile kifaa maalumu...punde alifanikiwa kuliona gari la peter likiwa limepaki kandokando ya barabara....alipotazama kwa umakini alifundua kuwa hakuna mtu ndani ya gari lile....ghafla alisikia....mtu akipiga kelele.....

    kelele hizo zilimaanisha ishara ya maumivu makali mpaka mtu huyo akapiga kelele....karimu aliamua kuelekea ule upande ambao alisikia kelele zinatokea.... alizipiga hatua huku macho yake yakitazama kwa tahadhali kubwa.....alipoangaza angaza macho aliweza kuona nyumba kubwa iliokuwa na muonekano wa kiwanda kidogo ambacho hakitumiki.....karimu alinyata akaingia ndani kabisa.....kwa mbali aliona watu wawili wakiwa wameshika bunduki mmoja akiwa upande mwingine...na mmoja akiwa upande wa juu .....alinyata akamchoma kisu cha moyo yule mtu aliyekuwa upande wa chini...mtu yule alipoteza maisha palepale.......kisha akamvuruta na kumficha kwenye chemba moja....kisha akaelekea upande wa juu alimkuta yule mtu kaweka bimduki chini...huku akijisaidia haja ndogo...punde mtu yule aliweza kumuona karimu...akakimbia kuifuata binduki yake.......karimu alirusha kisu kilikwenda moja kwa moja mpaka kwenye koo...kilitoboa koromeo kisha mtu yule alidondoka chini huku akitapatapa kutetea pumzi ya mwishomwisho....karimu alimuwahi na kunyonga shingo ya mtu yule akakata roho papohapo....kisha akamvuruta na kumficha asionekane.. ...karimu alichomoa bastora kisha akaanza kuingia ndani kabisa....akiwa anatembea huku akitazama huku na kule ghafla alisikia mlio wa risasi......karimu aendelea kuzipiga hatua huku macho yake yakitazama kwa tahadhali kubwa........akashuka upande wa chini........kabla hajashuka alisita akaamua kuchungulia upande wa pili....alistahajabu kumuona.....mtu amelala chini huku damu nyingi zimetapakaa chini zikitokea upande wa kichwani........mtu huyo alionekana kuwa kauwawa muda si mrefu...."" bila shaka ule mlio wa risasi ndio muda aliouwawa mtu huyu""" karimu alijisemea moyoni kisha akarudi ule upande mwingine.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***************



    akaanza kushuka upande wa chini......ghafla aliteleza kwenye ngazi bastora yake ikadondoka upande wa chini kabisa....



    upande mwingine peter alisikia kama kitu kimedondoka......alihisi huenda kuna mtu kaingia....alimuamuru mmoja kati ya walinzi wake aende akatazame nini kimedondoka......

    mlinzi yule alichomoa kisu na kuelekea ule upande alioagizwa akatazame nini kimedondoka...ghafla alipigwa teke aina ya( Double kick) akadondoka chini kabla hajakaa sawa alipigwa teke la uso.....lililomfanya ahisi kizunguzungu.....kabla hajanyanyuka..karimu alimuwahi akamkaba kabali aina ya ngeta......mtu yule alikosa pumzi akapoteza fahamu...kisha karimu akanyonga shingo ya mtu yule akafa papohapo.....



    peter alistahajabu sana kuona yule mlinzi amechelewa kurudi..peter alianza kuingiwa na wasiwasi akatimua mbio kuelekea upande wa nje....

    karimu aliendelea kunyata.....mara ghafla kwa mbali alimuona peter anakimbia kuingia ndani ya gari lake......karimu aliamua kulikimbilia gari hilo ili amuwahi peter kabla hajageuza gari na kutokomea.....alipokimbia hatua mbili mara ghafla..



    karimu alipigwa risasi ya mguu.....akakimbilia upande wa pili ili kujificha kwa sababu mtu aliyekuwa anafyatua risasi..alikuwa upande wa juu...alifyatua risasi mfululizo....wakati huo huo

    peter aliliondosha gari na kutokomea kusikojulikana...

    karimu alijisogeza mpaka kwenye gari bovu akajificha,,, kisha akaanza kutazama kwa umakini ili aweze kuona mtu yule aliyekuwa anafyatua risasi yupo upande gani...alipotazama kwa umakini alimuona mtu yule....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ule upande wa juu yule alionekana akiangaza kutafuta ni wapi karimu kakimbilia wapi!! hakumuona akaamua kushuka upande wa chini...wajati huo huo karimu alichoropokaharaka kutoka kule chini ya gari alipokuwa amejificha...

    akanyata kuelekea ule upande ambao yule mtu alipokuwa......karimu alijiamini kwa sababu alisikia ule mlio wa mwisho wa risasi....aligundua kuwa ilikuwa ni risasi ya mwisho...hivyo aliamini mtu yule hakuwa na risasi kwenye bastora yake....ghafla wakakutana uso kwa uso mtu yule alijaribu kufyatua risasi alipogundua risasi zimekwisha aliamua kutupa chini bastora na kutimua mbio.....karimu alimuwahi na kurusha ngumi usoni mwa mtu yule akadondoka chini..kisha karimu akampiga ngumi za mfululizo kisha akachomoa kisu na kumchinja mtu yule...

    karimu akaondoka huku akichechemea.....



    ***************



    ule upande mwingine alionekana peter akiliendesha gari lake kwa kasi ya ajabu...aliparamia magari ya watu na kuyachuna...

    kwa sababu aliendesha bila kufuata sbheria za barabara.....baada ya dakika kumi hivi alifika nyumbani kwake......peter alichukua simu yake na kumpigia kamishna..ili amwambie kuwa karimu...amemvamia....



    ule upande wa pili alionekana kamishna akiongea na simu ya mezani...simu hiyo ilitoka makaomakuu...kamishna aliambiwa kuwa karimu anahitajika aende makao makuu kunakazi anatakiwa apewe......simu ile ilimchanganya sana kamishna...aliwaza je wakijua kuwa alimshusha cheo na kumuamisha kitengo cha upelelezi na kumpeleka kwenye kitengo cha usalama barabarani bila sababu na taarifa kamili.....ghafla simu yake ya mkononi ikaita akaitoa mfukoni...alipoitazama aligundua kuwa peter anampigia....alipoipokea alistuka sana baada ya kusikia taarifa za karimu.. kisha akakata simu..

    ""mambo yameanza kuwa magumu.....bila shaka karimu hawezi kutuacha hai......alijisemea moyoni

    ghafla wazo lilimjia akaandaa mpango wa kumuamisha feisal ili karimu asijue mtoto wake yuko wapi...

    kamishna alitika nje na kuelekea kule alipokuwa amelipaki gari lake akaingia ndani ya gari na kuliwasha akaondoka zake kurudi nyumbani....



    **************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ule upande mwingine alionekana karimu akizipiga hatua akakodi bodaboda impeleke nyumbani kwake...akiwa njiani alipishana na gari la kamishna...karimu alimuina vyema kamishna lakini kamishna hakumuona karimu kwa sababu muonekano wa karimu ulikuwa tofauti....kutokana na zile ndevu bandia na kipara pamoja na lenzi za bandia alizozibandija kwenye macho yake.....

    karimu hakutaka kumfatilia kamishna..... akaenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake.....

    alipofika alilipa pesa kwa yule dereva bodaboda...kisha akaingia upande wa ndani......akachukua maji safi akaosha lile jeraha kisha akaitoa ile risasi kwa kutumia kisu....alihisi maumivu makali sana.......

    muda huohuo peter alituma majasusi wawili waende kuangalia huenda karimu karudi nyumbani kwake...kisha wamuangamize.....punde walifika nyumbani kwa karimu..karimu aliwaona majasusi wale akaamua ujificha..majasusi wale walipo kagua vyumba vyote hapakuonesha dalili yoyote ya mtu kuishi humo kwa sababu kulikuwa na vumbi pamoja na tando za buibui...waliamua kuondoka...... wakati wanatoka mara ghafla waliona damu kwenye sakafu....walistuka kwa sababu damu hizo zilionekana kuwa sio za muda mrefu.....kabla hawajakaa sawa karimu alifyatua risasi ikampata mmoja kwenye kichwa akafa palepale...yule mwingine alipotahamaki alipigwa risasi ya kifuani kabla hajadondoka chini akapigwa risasi ya kichwani akafa palepale...



    ************



    kamishna alifika nyumbani kwake....akapitiliza moja kwa moja mpaka chumbani...akavua nguo za kazi akavaa nguo za kawaida...kisha akatoka nje na kuingia ndani ya gari.....na kutokomea kusikojulikana....mke wa kamishna alishangazwa kwa kitendo kile...haikuwa kawaida ya kamishna kurudi nyumbani akiwa katika hali hiyo....

    kamishna aliliendesha gari mpaka nyumbani kwa peter.....

    alipofika aliandaa mikakati ya kumuamisha faisal...peter alisema"nitakusaidia kisha kamishna akaondoka zake...

    peter alitoka nje na kuingia ndani ya gari lake jingine.....akaliwasha na kuelekea kule shuleni alipokuwa anasoma feisal......



    alipofika alimsubiri feisari mpaka muda wa kutoka shule...muda ulipowadi peter alimuina feisal kwa mbali...akamuita feisal....punde alikuja haraka kwa sababu alimtambua peter...kwa sababu huwa anakuja mara kwa mara nyumbani kwa kamishna.....peter alimwambia feisal kuwa aingie ndani ya gari.....feisal aliingia....kisha wakaondoka...peter aliliendesha gari moja kwa moja mpaka nyumbani kwake.....alipofika alishuka kutoka ndani ya gari kisha akaongozana na feisal mpaka upande wa ndani......



    ******************



    upande mwingine karimu alionekana akitembea kariakoo majira ya saa moja za usiku kisha akasogea mpa jirani na duka moja linalouza simu mlinzi wa duka hilo alimfuata karimu na kumwambia haruhusiwi kuwepo eneo hilo kwa sababu duka limefungwa...karimu alitoa kipande cha karatasi kutoka mfukoni mwake.....akaikunjua karatasi hiyo...kisha akamwambia mlinzi unaweza kuitambua anuani hiii?? mlinzi alisogea ili atazame kwenye karatasi ile nini kimeandika....aliposogea karibu kabisa...karimu alimbana mlinzi yule kisha akamufunika na karatasi ile upande wa usoni...karatasi ile ilikuwa na unga wa sumu maalumu.....ni kitendo cha sekunde mlinzi yule alianguka na kupoteza fahamu...feisali alifungua duka hilo kwa kuvunja kufuli kwa kutumia kemikali maalumu....kisha akaingia upande wa ndani...alichukuwa simu mbili....kisha akatoka nje na kutokomea kusikojulikana..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *****************



    wakati huohuo kamishna alikuwa akiongea na peter kwa njia ya simu....walikuwa akiongelea juu ya mzigo haramu utakaoingia usiku wa leo...

    walipomaliza kupanga mikakati kamishna alikata simu......

    baada ya muda kidogo kupita...peter aliliwasha gari lake na kuelefkea bandarini.....



    wakati huo huo alionekana karimu akizipiga hatua huko mitaani...karimu akiwa anatembea aliona...night club aliamua kuelekea upande huo...huenda akapata mwanzo wa kumuongoza ili afahamu peter anapatikana wapi.....alipofika alilipia noti ya shilingi elfu 10 aliyokuwa amebakiza mfukoni mwake...kisha akaingia upande wa ndani........

    watu walionekana kucheza muziki...wengine wakinywa bia na pombe kali..karimu aliketi kwenye kiti kilichokuwa gizani...hivyo aliweza kuona watu waliotoka na kuingia....kwa mbali aliina mtu akamtilia mashaka....alimtazama kwa makini mtu huyo....aliona akipewa pesa kisha akatoa kipakti kwenye mfuki wa koti la suti....."""bila shaka mtu huyu hawezi kuacha kumfahamu peter...alijisemea karimu....kisha akanyanyuka na kumfuata mtu yule alipomkaribia karimu alimnong'oneza mtu yule akimwambia watoke nje waongee....mtu yule alitoka alijua huenda karimu anataka kufanyanae bihashara..... mtu yule hakuona haja ya kuingelea nje alimwambia karimu"" tuongee ndani ya gari langu.....karimu alikubali wakaingia mdani ya gari.... punde kuna gari lilikuja na kupaki kando kidogo....karimu alionekana kuliangalia gari lile kwa mshangao.....yule mtu alistuka alihisi huenda karimu ni askari...akataka kujihami kwa kudungua droo ya gari ili atoe bastora....karimu alimuwahi akanyoosha bastora kichwani mwa mtu yule....

    ilibidi awe mpole kisha karimu akamuamuru aliondoshe gari eneo hilo....wakiwa njiani karimu alimwambia asimamishe gari...mtu yule alifata kama alivyoelekezwa....punde karimu alimpiga na kitako cha bastora mtu yule alipotza fahamu....karimu alimpapasa mifukoni alimkuta na kete nyingi za madawa ya kulevya....pia alichukua simu ya mtu huyo..kisha akamtoa mtu yule na kumfungia ndani ya buti....akaliwasha gari na kuelekea nyumbani kwake.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***************



    wakati huohuo peter alifika bandarini alipokea mzigo huo haramu...cha kushangaza mapolisi walikuwepo lakini mzigo wa peter haukukaguliwa ulipitishwa hivyohivyo tofauti na mizigo ya watu wengine......peter alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake...



    wakati huo huo karimu alifika nyumbani kwake alianza kulikagua gari hilo aliona vinyago vya sura za bandia.....karimu alistahajabu sana mpaka sura ya kamishna ilikuwemo katiza hizo sura za bandia....punde simu ya mtu yule iliita....karimu alipoiangalia simu ile ilikuwa imeandikwa Boss Peter...karimu hakuipokea simu ile akaizima kisha akatoka nje ya gari na kumtoa mtu yule ndani ya buti..kisha akaingianae mpaka upande wa ndani....baada ya dakika kadhaa mtu yule alizinduka na kupata fahamu alipotazama huku na kule hakuona mtu ...alijiona yupo peku bila viatu...akanyanyuka ili atoke nje alipopiga hatua mbili aligisi amekanyaga maji.

    maji hayo yalikuwa yametapakaa sebule nzima ..wakati anatahamaki ilisikika sauti ya karimu ikitikea upande wa nyuma ..alipogeuka alimuona karimu kashikilia nyaya mbili za umeme nyaya hizo zilikuwa chini zimegusa maji..kisha karimu akauliza""unamfahamu peter???? yule mtu alikataa "hapana simfahamu wala simjui....karimu alichomeka nyaya hizo kwenye umeme....ghafla mtu yule alipigwa shoti za umeme mpaka akajisaidia haja ndogo na kubwa kwa mfululizo...

    karimu alizichomoa nyaya zile..kisha akauliza tena"".Unamfahamu peter???? mtu yule hakujibu kitu karimu akarudisha nyaya zile kwenye umeme...kabla hajazichomeka yule mtu aliropoka NDIO NAMFAHAMU..TWENDE NIKUPELEKE...

    karimu alimchukua mtu huyo na kuondokanae usiku huohuo...walipokaribia nyumba ya peter yule mtu alionesha "ni hapo anapoishi peter....Karimu aligundua mtu yule hamdanganyi...lakini hakumuacha hai alimuuwa na kumtelekeza hapo nje ya nyumba ya peter..kisha akaondoka zake ili akaandae mikakati ya kumnasa peter....



    ***************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    asubuhi palipokucha peter alipata tarifa za kijana wake wa kazi kuuwawa na mtu asiyejulikana....peter aliogopa sana aliamini ni karimu ndio kafanya mauwaji hayo...peter aliamua kuandaa safari ili atoroke na kwenda South afrika..

    baada ya lisaa limoja peter alitoka ili aelekee uwanja wa ndege..aliingia ndani ya gari alipotoka nje ya geti alikutana na karimu ....gari zao zilitazamana uso kwa uso.....





    pete alichanganyikiwa alipiga honi za mfululizo ili walinzi wake watoke nje ya geti kutoa msaada... karimu alionekanekana akichukua bunduki aina ya

    SMG ( SUB MACHINE GUN) kisha akatoka nje ya gari akaanza kufyatua risasi mfululizo kuelekea ule upande lilipokuwa limesimama gari la peter...milio ya risasi iliwafanya walinzi wa peter kutoka upande wa nje huku wakiwa na siraha za moto...gari la peter alikuweza kuingiwa na risasi kwa sababu lilikuwa linavifaa maalumu vya kuzuia risasi zisiingie upande wa ndani..(bulet proof)...alipo ona geti limefunguliwa aliliendesha gari mpaka ndani ya uzio kisha geti likafungwa...peter alitoka ndani ya gari haraka na kukimbilia upande wa ndani ya nyumba.....alikwenda kwenye kile chumba alichofungiwa feisal...peter alichuku bomu kisha akalifunga tumboni mwa karimu...kisha akatoka na feisal nje......wakati huo karimu alikuwa akiwashambulia walinzi waliokuwepo upande wa nje ya geti kisha akaingia ndani....alipoingia alikuta peter kamshikilia feisal....kisha peter akasema"" weka siraha chini na ujisalimishe Lah! si hivyo nampasia vipande vipande mtoto wako kisha peter akatoa remote control ya bomu bile....macho yalimtoka karimu....hakuamini...kwa mara ya kwanza anamuona mtoto wake akiwa na umri wa miaka kumi na tatu...alimuacha akiwa na umri wa miaka mitatu...kipindi cha miaka kumi aliyofungwa gerezani......karimu hakuwa na ujanja tena aliona ni bora asalimu amri ili aokoe maisha ya mtoti wake. akaweka siraha chini kisha akainua mikono yake kichwani....mara ghafla alipigwa kisogoni na kitako cha bunduki..karimu alihisi kizunguzungu punde akadondoka chini na kupoteza fahamu....akachukuliwa na kufungwa mikono na miguu kwa kutumia kamba imara..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    *************





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog