Simulizi : Jini Wa Daraja La Salenda
Sehemu Ya Nne (4)
Baada ya Balkis kuondoka majira ya saa nne usiku, Muddy aliamua kurudi tena maeneo ya Daraja la Salenda kufanya uchunguzi wa jumba lile la ajabu. Aliingia kwenye gari lake na kwenda hadi sehemu aliyokutwa na Balkis. Alisimamisha gari lake na kufunga kila sehemu kwa usalama wa gari lake kisha aliteremka na kutembea taratibu kuifuata njia aliyopita na Balkis. Kila alivyolitafuta lile jumba la kina Balkis hakuliona, alijikuta akitoka sehemu moja kwenda nyingine bila mafanikio. Saa zilimkatikia kwa kuzurula kulitafuta lile jumba ambalo aliamini kwa muono wake akiwa ndani yake kama akiwa kwa mbali angeliona kutokana na kuwa na taa kila kona ya jumba lile zilizokuwa na mwanga mkali. Lakini kila alipotupa macho labda ataziona taa angani, kulikuwa na kiza tu kilichotawala angani. Bado hakuamini alirudi sehemu aliyoanzia zaidi ya mara kumi ili aanze upya kulitafuta jumba la kifahari la kina Balkis. Muda ulizidi kukatika, kutokana na kutembea sana kulitafuta jumba hilo alijikuta akichoka sana na kukaa chini ya mti mmoja apumzike
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kidogo ili arudi kwenye gari lake na kurudi nyumbani kulala kwani usiku ulikuwa mkubwa. Alipokaa chini ya mti usingizi haukuchelewa ulimchukua, ulikuwa usingizi mtamu ajabu uliomfanya alale kama yupo kitandani. Kibaridi cha alfajiri kilimshtua kwenye usingizi mzito na kujikuta amelala pembeni ya ufukwe chini ya mnazi, sehemu ambayo ilimchanganya kidogo. Alitembeza macho yake na kuwaona watu waliokuwa wakiteremsha samaki kwenye boti. Sehemu ile ilimchanganya sana na kujiuliza pale ni wapi? Pamoja na kuwa amejilaza chini ya mnazi bado hakuna mtu aliyekuwa na habari naye kwani kila mmoja alikuwa na hamsini zake. Wengi walipita pembeni yake wakiwahi kununua samaki walioletwa na majahazi asubuhi ile. Akiwa bado amekaa chini akitafakari yupo wapi, kijua nacho kilianza kuchomoza kwa mbali lakini bado baridi iliendelea kumchonyota mwilini. Alijinyanyua taratibu alipokuwa amekaa na kuanza kutembea taratibu pembeni ya bahari huku akijitahidi kuyakumbuka maeneo yale ambayo yalikuwa mageni kichwani mwake. Aliona akikaa kimya atazidi kupotea, ilibidi amuulize kijana mmoja aliyekuwa na kapu lililoonekana limejaa samaki wabichi, alionekana ni mchuuzi aliyelangua na kwenda kuwauza mitaani. “Samahani ndugu,” Muddy alimuuliza baada ya kumkaribia. “Bila samahani kaka yangu.” “Kwanza ni vizuri kutanguliza salamu kuonesha uungwana, habari za asubuhi?” “Nzuri tu.” “Eti hapa ni wapi?” “Kigamboni.” “Mungu wangu, kuja huku si lazima utumie pantoni?” “Kutoka wapi?” “Mjini.” “Ndiyo.” “Sasa mimi nimefikaje bila kutumia Pantoni?” “Kutoka wapi?” “Mjini.” “Kwani wewe umefikaje huku?” “Hata najua, hii kali ya mwaka.” “Samahani kaka, mbona kama unajishangaa kwani wewe mara ya mwisho ulikuwa wapi?” “Njia panda ya barabara ya Ali Hasani Mwinyi na Masaki.” “Ulikuwa ukifanya nini?” “Mmh! Tuachane na hayo, hebu nioneshe njia ya kuelekea kivuko cha Pantoni?” “Twende pamoja na mimi naelekea huko huko.” Muddy aliongozana na yule kijana kuelekea kwenye kivuko cha Pantoni, njiani alijawa na mawazo jinsi alivyojikuta Kigamboni wakati yeye alikuwa maeneo ya Daraja la Salenda. Alijiuliza kuhusu gari lake atalikuta kwenye hali gani, alipofika kivukoni bahati nzuri alikuta kivuko ndiyo kinapakia abiria na magari. Alipanda na kutulia kwenye siti huku kichwa chake kikiwa hakikubaliana na kilichotokea. Bado alijawa na mawazo juu ya kujikuta Kigamboni bila kujielewa, kivuko kilivyofika mwisho aliteremka na kuelekea kwenye daladala za kuelekea Mwenge iliyomrudisha mpaka njia panda ya kuelekea Masaki. Alipofika alilikuta gari lake lipo katika hali ya usalama. Aliingia ndani ya gari lake na kurudi hadi kwake, alishangaa alipofika kwake kumkuta Balkis amekaa mlangoni akilia. Alijikuta akishtuka, akateremka kwenye gari bila kufunga mlango na kumfuata alipokuwa amekaa. “Mpenzi unalia nini?” “Muddy hunipendi.” “Mimi?” Muddy alishtuka kusikia vile. “Muddy nazungumza na nani?” “Na mimi.” “Ulikuwa wapi?” “Nilitoka kidogo alfajiri kuna sehemu nilikwenda mara moja.” “Muddy unanipenda?” “Tena sana.” “Niambie ukweli ulikuwa wapi?” “Kama nilivyo kueleza mpenzi,” Muddy alijua Balkis alikuja asubuhi ile. “Nikuambie nini mpenzi zaidi ya hayo.” “Mbona kichwani una majani na mwili na nguo zimechafuka?” Kauli ile ilimshtua Muddy na kujikuta akijikagua upya na kujikuta kweli alikuwa amechafuka kwa mchanga wa bahari pia kichwani alikuwa na majani. Alijikuta akipatwa na kigugumizi, alijifikiria amjibu nini Balkis aliyekuwa akimtazama usoni huku machozi yakimtoka.
. “Muddy nipo hapa toka saa tano usiku baridi lote limeniishia nikijua haupo mbali, kumbe umekwenda kwa wanawake zako,” Balkis alijiliza kiuongo. “Nisamehe Ba..Ba..lkis,” Muddy alijitetea baada ya kujua kuwa ameumbuka. “Niambie ukweli ulikuwa wapi?” “Nilikufuata kwenu.” “Kufanya nini, wakati niliondoa kwako hukuniambia kitu?” “Nililipenda jumba lenu nilitaka kuliona kwa macho yangu nikiwa kwa nje.” “Si ungenieleza unataka kupajua kwetu ili nikupeleke kuliko kunichunguza au huniamini?” “Nakuamini lakini basi tu, yaani nimechanganyikiwa, jumba kama lile sikuwahi kuliona hata mchana huwa silioni maeneo yale.” “Narudia tena, kwa nini usiniulize jumba letu lilipo? unaweza kulitafuta mwaka mzima na usilione.” “Naomba unisamehe kwa yote yaliyojitokeza.” “Muddy nilishakusamehe tangu siku ya kwanza nilipokuona ukipasuliwa moyo wako kwa kisu butu bila ya ganzi na mkeo wa bandia, niliamini mtupo uliotupwa haukujua ungeangukia wapi na muanguko wako ungekuwa mkubwa sana na usingesimama tena.” “Nashukuru Balkis kwa kuyaokoa maisha yangu, nisamehe kwa yote, siyo kwamba sikuamini la hasha, bali nilipenda kuuona utukufu wa utajiri wa familia yako. Bado nipo njia panda kujiuliza jumba zuri kama lile limejengwa lini maeneo yale.” “Maeneo gani?” “Si pale pembeni ya njia panda ya kuelekea Masaki.” “Nataka nikutaadharishe kitu kimoja, yaani usije tena maeneo yale kwani baba yangu akikuona anaweza hata kukutoa uhai.” “Atanijuaje?” “Mbona anakujua, aliponiuliza nilimdanganya, sasa kama atakuona tena maeneo yale lazima atajua namdanganya na atakufanyia kitu kibaya.” “Je, akinikuta kwenu?” “Kwa sasa baba yupo, hivyo hutuwezi kwenda tena mpaka tutakapooana.” “Kwa hiyo utakuwa unakuja kulala hapa?” “Ndiyo maana yake.” “Si umesema nyumba hii itapigwa bei itakuwaje?” “Usiwe na wasiwasi kila kitu niachie mimi, ukitoka mahakamani nitakupeleka kwenye nyumba yako mpya.” “Nitashukuru mpenzi wangu.” Balkis baada ya kuingia ndani aliisikia nyumba ukinuka sana, aliogopa kusema kwa kuhofia kumuudhi mpenzi wake. Alitafuta mbinu ya kumuondoa Muddy ili afanye usafi ndani mle. Alimtuma kitu ambacho alijua hawezi kukipata karibu, alijua nafasi ile ingempa fursa ya kuwaita wajakazi wake kufanya usafi kwa muda mfupi. Alimuomba samahani kabla ya kumtuma: “Samahani mpenzi wangu.” “Bila samahani.” “Najua umechoka lakini naomba nikutume kitu.” “Nitume tu mpenzi wangu.” “Kwa vile nataka kufanya usafi, naomba kaninunulie udi sehal” “Upo sehemu gani?” ”Kwenye maduka wanayouza manukato utaupata.” “Hakuna tatizo wacha niwahi.” “Nioneshe ufagio.” Baada ya kumpa ufagio Muddy alitaka kuondoka na gari lakini Balkis alimkataza alijua
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akitembea kwa miguu atachukua muda mrefu kurudi kuliko akitumia gari. “Unaweza kuupata karibu wala usitumie gari.” “Hakuna tatizo.” Muddy aliondoka na kumwacha Balkis akijifanya anafagia, baada ya kuondoka tu, aliacha kufagia na kujishika kwenye paji lake la uso. Haikuchukua sekunde wajakazi kumi walikuwa mbele yake wakiwa wamepiga magoti. “Rabeka mwana wa mfalme una shida gani?” Waliuliza kwa pamoja. “Nataka mfanye usafi wa nyumba yote, sitaki kusikia harufu mbaya kama hii.” Mara moja wajakazi walianza kusafisha nyumba nzima, ilikuwa ajabu waliondoka vitu vyote vya ndani na kuviweka vipya na vyenye thamani kwa muda mfupi, ndani pakabadilika, pakapendeza na kuvutia kila kona ya nyumba ilinukia kwa harufu nzuri. Muddy alijikuta akitembea umbali mrefu kutafuta udi sehal, kila alipouliza watu hawakuujua. Alijikuta akikata tamaa na kuamua kurudi kumweleza Balkis kuwa udi wenye jina hilo kila alipouliza watu hawakuujua. Kutokana na kwenda umbali mrefu ilibidi wakati wa kurudi apande gari, jasho likimvuja kwa kutembea. Alipofika nyumbani aliingia ndani lakini alishtuka kukuta nyumba yake ikiwa imebadilika na kupendeza sana, aliviona vitu tofauti kiasi cha kuamini kuwa alikuwa amekosea, hakukuwa kwake. Alitoka nje ili akaitafute nyumba yake lakini mlangoni alikutana na Balkis akiwa amebeba siagi na jam. “Vipi mpenzi mbona nimekuona umeingia na unatoka?” “Ha! Hapa ni kwangu?” Alishtuka. “Eeh! Kwako, kwani vipi?” “Umefanya usafi mkubwa hivi kwa muda gani?””Usinione nipo hivi mimi ni mwanamke wa shoka.” “Na mbona kuna vitu vipya?” “Sasa kipi cha ajabu, yote haya nimeyapanga kwa muda mrefu, nilipokuwa nakuja kulala hapa. Nilimtuma mtu avilete vitu hivi, wakati unaondoka vilikuwa vinaingia.” “Sasa nyumba ikiuzwa?” “Achana na wazo hilo hebu nenda kaoge ufungue kinywa.” Muddy hakujibu kitu alichukua taulo na kwenda kuoga, nyumba ilikuwa ikinukia kama ujinini kwa akina Balkis. Muddy alipotoka kuoga alikuta chai imeshatayarishwa juu ya meza, ilikuwa tamu ambayo Muddy aliwahi kuinywa nyumbani kwa akina Balkis tu. Pamoja na kuisifia chai lakini Muddy kila alipomuangalia Balkis moyo wake haukuamini kama alikuwa na mwanamke mzuri kama yule tena tajiri mwenye mapenzi ya dhati kwake.
“Muddy nihakikishie kuwa huwezi kurudiana na Ashura?” “Nakuhakikishia kukupenda siku zote na kamwe sitarudiana na yule mwanamke muuaji.” “Muddy unayosema yanatoka moyoni au mdomoni?” “Yanatoka moyoni mwangu?” “Ukinigeuka?” “Nifanye lolote.” “Muddy kama unayosema ni kweli basi kitu nilichotaka kukifanya naachana nacho.” “Kipi hicho?” “Nilitaka kusimamia kesi yako kuhakikisha hawachukui kitu chochote.” “Kwa nini usifanye hivyo?” “Naacha ili maisha yako yakiwa mazuri mtu yeyote asikuguse.” “Kwa hiyo nitakuwa na maisha mazuri zaidi ya haya?” Muddy aliuliza. “Mara kumi ya haya.” “Usiniambie!” “Kwangu fedha si tatizo, ninachokitaka kutoka kwako ni mapenzi ya kweli, sihitaji kitu kingine.” “Nakuahidi utayapata hapa.” “Basi tegemea kuishi maisha ya raha mpaka kufa kwako.” “Asante mpenzi wangu,” Muddy alisema huku akimkumbatia Balkis. *** Muda ulipofika Muddy aliitwa mahakamani na hukumu ilikuwa ile ile ya kugawana mali. Kwa vile alishaelezwa na Balkis maisha yake baada ya hukumu, hakuchanganyikiwa baada ya kuelezwa yale. Baada ya hukumu ile, Muddy pia alitakiwa kumlipa fidia ya fedha ambayo ilimfanya asipate kitu katika mali zitakazouzwa, vikiwemo gari na nyumba. Ashura alishangaa kumuona Muddy pamoja na pigo zito yupo katika hali ya kawaida. Baada ya hukumu Muddy alitoka nje ya mahakama na kwenda moja kwa moja kwa Balkis aliyekuwa akimsubiri. Muddy alishtuka kumuona Balkis akiwa pembeni ya gari la kifahari. “Karibu mpenzi.” “Asante.” “Pole na masaibu yote.” “Asante,” walikumbatiana, kitendo kile hakuna aliyekiona zaidi ya Muddy peke yake. “Nina imani mambo yamekwenda kama nilivyokueleza?” “Yaani umekuwa kama wewe ndiye uliyeyapanga yote, hakuna hata kimoja kilichokwenda kinyume.” “Basi huyo ndiye Ashura ambaye pia hilo si jina lake halisi.” “Una maana gani kusema hivyo?” “Nitakueleza, kila mwanaume aliyemchezea mchezo huu anamjua kwa jina hili lakini jina halisi anaitwa Shuuna.” “Ina maana hata hayo majina aliyotumia kwa hao mabwana wa awali unayajua?” “Nayajua.” “Alikuwa anaitwa nani?” “Twende kwanza nyumbani ukapumzike, mengine tutazungumza tukifika.” Muddy aliingia kwenye gari na kuondoka, kabla ya kuingia kwenye gari Ashura alishtuka kumuona Muddy na mwanamke mrembo aliyejitambulisha kuwa ndiye mkewe siku aliyokwenda kwake kumuonya. Alijikuta akikosa raha na kujiona wamefanya kazi bure sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Waliona kama hawakufanya kitu na kujikuta akimuuliza mwanaume wake. “Yule mwanamke mwenye fedha Muddy kamtoa wapi?” Ashura aliuliza. “Hata mimi nashangaa, ni wazi wameanza uhusiano kipindi mkiwa wote.” “Ndiyo maana hata ilipotolewa hukumu hakushtuka.” “Hata mimi nilishangaa kuona anakubali kila kitu.” “Kwa hiyo tutakuwa tumefeli?” “Hapana, hatujafeli kwani tulivyovitaka tumevipata, ila kuna biashara nyingine nzuri,” mwanaume wa Ashura alisema. “Biashara gani?” “Tukafungue mashitaka ya kudai kuhujumiwa penzi lako lililosababisha muachane na mumeo wakati bado unampenda.” “Aisee, wazo zuri sana! Kweli wewe bwana mipango, sasa mpango huo tuufanye lini?” “Kwanza tupajue wanapoishi ili tufanye mpango wa kufungua mashitaka.” “Hilo wazo, mbona mwaka huu tutatengeneza fedha mpaka zitukimbie.” “Hiyo ndiyo kazi yetu.” “Lakini Mussa kuna jambo nimekumbuka.” “Jambo gani hilo?” “Unakumbuka yule mwanamke alivyotuonya kuhusu tabia yetu kuwa itatutokea puani?” “Sasa wewe unamuogopa, atatufanya nini mwanamke yule?” “Mmh! Nashangaa moyo unanienda mbio nilipomkumbuka.” “Si kwa vile amekuchukulia mumeo.” “Yule si mume wangu nilikuwa naye kibiashara zaidi.” “Basi mpango wa haraka ni kudili na Muddy kuhakikisha anaokota makopo.”
Wakati wakipanga kuchukua fedha za Balkis, muda huo Muddy alikuwa akikaribishwa kwenye jumba la kifahari. “Karibu mpenzi wangu hapa ndipo kwako ishi kwa furaha na mapenzi ya kweli,” Balkis alimkaribisha kwa sauti tamu. “Ha! Siamini.” “Hata lile gari ni lako.” “Usiniambie!” Muddy alizidi kupigwa na butwaa. “Ukweli ni huo, leo usiku kutakuwa na sherehe fupi ya kufunga ndoa yetu ili uweze kunitumia kihalali kama mkeo.” “Hakuna tatizo, asante sana mpenzi.” Muddy alishukuru kwa kupiga magoti huku machozi yakimtoka na kujiuliza bila ya Balkis maisha yake yangekuwaje baada ya kufanyiwa utapeli na Ashura. **** Ashura na mwanaume wake baada ya kutoka mahakamani waliongozana na madalali kwenda kuuza mali za Muddy zikiwemo gari na nyumba siku ile ile, kutokana na mipango iliyopangwa mapema. Baada ya kufanikiwa kuuza gari na nyumba waliendelea kufurahia mafanikio yao kufuatia kazi yao ya utapeli na kujipanga kwa ajili ya kupambana na Balkis kuhakikisha wanapata fedha kupitia kwa Muddy. Pamoja na kupata vitu walivyovitaka kutoka kwa Muddy, bado Ashura moyo wake ulikosa raha, alijiuliza atamtazamaje Muddy siku wakikutana kutokana kuonekana ameingia kwenye maisha mazuri tofauti na awali walipokuwa pamoja. Baada ya kumuacha Muddy na kuonesha kuchanganyikiwa, alitegemea kusikia amejinyonga. Kufuatia kupona kifo hicho, Ashura alitegemea siku ya hukumu angemuona Muddy akitoka mahakamani na kuanza kuokota makopo, lakini ilikuwa ni kinyume na mategemeo yake. Wasiwasi wake Muddy lazima angelipa kisasi, wazo lake lilikuwa kumuwahi kabla hajawahiwa yeye. Akiwa amekaa na mwanaume wake, Ashura alimueleza jambo: “Mussa nina jambo linaniumiza akilini mwangu.” “Lipi tena mpenzi?” “Nina wasiwasi na Muddy kutulipizia kisasi.” “Ni kweli hata mimi nilikuwa na wazo hilo.” “Sasa tufanye nini kabla hajafanya lolote, maana akitulia atajipanga na yule dada anaonekana ana fedha hivyo anaweza kutufanyia kitu kibaya.” “Ondoa hofu hawawezi kutufanya lolote zaidi ya sisi kuwamaliza wao.” “Hayo ndiyo maneno.” Ashura alipata faraja. *** Wakati Ashura na Musa wakipanga mipango yao, usiku wa siku ile ufukweni mwa Bahari ya Hindi maeneo ya Daraja la Salenda kulikuwa na sherehe kubwa ya harusi kati ya Balkis na
Muddy. Katika kundi la watu wote waliokuwepo kwenye sherehe ile Muddy peke yake ndiye aliyekuwa mwanadamu, lakini waliobakia walikuwa majini. Lakini hakuwajua kwa vile walikuwa katika maumbile ya kibinadamu, Muddy alimuoa rasmi Balkis na kuwa mkewe wa halali. Ilikuwa sherehe kubwa kuwahi kutokea katika maisha ya Muddy. Baada ya harusi walilala kwenye kitanda cha bembea kilichowabembeleza mpaka kunakucha. ***** Taarifa ya ndoa ya Balkis ilifika chini ya bahari kwa Mfalme Barami Hudirud, kitendo kile kwake alikiona kama ni dharau kutoka kwa mwanaye kufunga ndoa na mwanadamu. Alimfuata mkewe aliyekuwa amekaa kwenye bustani akibembea kwenye kiti. “Mama Balkis,” alimwita kwa sauti ya juu iliyomshtua. “Mtukufu Mfalme wa chini ya bahari, mbona sauti kali, kuna usalama?” “Mwanao ananitafuta nini?” “Kwani kafanya nini tena mtukufu mfalme?”?”Tunamkataza nini na anafanya nini?” “Amefanya nini?” “Anaweza kuvunja amri yangu?” Mfalme Barami alisema huku akipiga ngumi kifuani kwa hasira. “Mume wangu, lakini si bado anaendelea kuleta vizazi vya wanawake?” “Kwa nini ameolewa na mwanadamu?” “Ha! Ndiyo kafanya hivyo!” Malkia Huleiya alishtuka. “Eeh! Tena nasikia watwana na vijakazi walikuwepo kwenye harusi hiyo.” “Usiniambie!” “Kwa jinsi alivyovunja amri yangu, wote waliohudhuria harusi ile watakutana na adhabu kali,” alisema kwa hasira mpaka povu likamtoka mdomoni. “Mume wangu usimguse mtu yeyote ni wewe uliyempa amri mwanao kwa watwana na vijakazi juu ya kuheshimu amri zake.” “Basi kama sivyo hivyo nitamtuma mtwana mkuu Muhuru akammalize huyo mwanaume.” “Bado hujatumia busara, kumbuka kosa lako lolote litatugharimu, kitendo cha kukataa kumuondoa mwanaume wa kwanza huku kilizua patashika na ulipotaka kumuua ulisikia alichosema mwanao. Hivi umuue huyu aliyefunga naye ndoa itakuwaje?” “Sasa kuna haja gani kuendelea kuleta vizazi vya wanawake wakati ameishajiamulia kuolewa na mwanadamu?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ILIPOISHIA: “Bado hujatumia busara, kumbuka kosa lako lolote litatugharimu. Kitendo cha kutaka kumuondoa mwanaume wa kwanza huku kukiwa na patashika ulipotaka kumuua ulisikia alichosema mwanao. Hivi umuue huyu aliyefunga naye ndoa itakuwaje?” “Sasa kuna haja gani kuendelea kuleta vizazi vya wanawake wakati ameshajiamulia kuolewa na binadamu?” SASA ENDELEA... “Labda ana sababu zake, ngoja akija tumuulize.” “Hakuna cha kumsubiri, tumtume Muhuru aende akamwite mara moja.” “Siamini, kama jana kafunga ndoa leo aje huku, hebu kuwa na subira mume wangu.” Walikubaliana kumsubiri ili aje awaeleze kwa nini amevunja amri ya mfalme wa bahari, tena akiwa binti wa mfalme. BAADA YA MIEZI MIWILI Maisha ya Muddy yalibadilika ghafla, kila aliyemuona alimshangaa. Mmoja kati ya watu waliomshangaa alikuwa ni Ashura aliyemuona akitoka super market akiwa ameongozana na Balkis katika mwonekano wa mahaba mazito. Roho ilimuuma na kujikuta akipata wivu wa kutaka kuwa na Muddy. Aliamini kuwa kilio cha Muddy alichokitoa siku alipomuacha, kama angemuomba warudiane angeweza kukubali. Alipanga kumtafuta na kumuomba msamaha. Ashura aliamua kumtafuta Muddy kwa udi na uvumba kila kona ya mji. Lakini alishangaa kila alipomuona Muddy na kumfuata alipomkaribia Balkis alitokea bila kujua ametokea wapi, kitu ambacho kilimkosesha amani ya moyo wake. Hata alipojaribu kumfuatilia kwa nyuma alimpotea kimiujiza. Aliamini njia rahisi ya kumrudisha mikononi mwake ni kwenda kwa mtaalam wake aliyekuwa anakaa Mbagala Kimbangulile, Mzee Chujio. Aliwasha gari na kuelekea Mbagala kwa mtaalam ili akamvute tena Muddy kama alivyofanya mwanzo na kupelekea kuisahau familia yake. Alipofika Mtoni kwa Azizi Ali dada mmoja aliomba msaada kwenye gari lake. Hakutaka kumnyima lifti, alimsaidia. “Unafika wapi dada yangu?” alimuuliza baada ya kuingia kwenye gari na kufunga mlango. “Mbagala Zakheem,” alijibu yule dada kwa sauti ya chini. “Ooh! Mimi nafika mbele, nitakushusha kituoni.” “Nitashukuru.” Wakati safari ikiendelea mwanamke aliyeomba msaada alianzisha mazungumzo. “Dada yangu huku ni mwenyeji?” “Hapana nakwenda kumuona mtu mmoja Mbagala mwisho.” “Nani mganga Chujio?” “Mmh!” Ashura alishtuka. “Mbona umeshtuka?” “Walaa, siendi huko.” “Lakini dada shida ya nini kumuendea Muddy kwa mganga wakati mmekwisha achana?” Kauli ile ilimshtua sana Ashura. “Nani amekwambia mimi nakwenda kwa mganga, pia habari za Muddy nani kakueleza?” Ashura alishtuka kujiona yupo uchi japo amevaa nguo, alijuta kumpa lifti yule mwanamke ambaye aliharibu safari yake yote. “Ashura,” mwanamke aliyepewa lifti kwenye gari alimwita jina lake. “Ha! Umejuaje jina langu?” Ashura alizidi kumshangaa mtu aliyempa lifti kwa kumjua kwa mapana. “Nijue unataka kufanya nini nitashindwa kujua jina lako? kwanza jina lako si Ashura.” “Kama siitwi Ashura naitwa nani?” “Shuuna.” “Mungu wangu! Umenijuaje?” Ashura nusura aliingize gari kwenye mtaro kwa mshtuko, ilibidi alisimamishe pembeni maeneo ya Mbagala Misheni. “Kwani kuna siri, la muhimu achana na Muddy endelea na maisha yako, pia mpango wenu wa kumfuatilia Muddy na mkewe mtaokota makopo ninyi kabla ya huyo Muddy.” “Wewe ni nani?” Ashura alimuuliza huku jasho likimtoka. “Mke wa Muddy,” sauti ilijibu pembeni. “Muongo...Ha!” Ashura alijibu huku akigeuka kumtazama aliyejiita mke wa Muddy, wakati huo manukato makali yalinukia ndani ya gari. Hakuamini kumuona mtu aliyempa lifti amebadilika na kuwa mke wa Muddy, Balkis. “Punguza hofu, sipo hapa kwa shari bali kukuonya kwa kitu unachotaka kukifanya, kumbuka nilikuuliza mapema kuhusu kurudiana naye nawe ulinihakikishia hutarudiana naye tena. “Sasa sikiliza Ashura, huenda utashangaa kuniona hapa. Sitaki kujieleza sana, ila ukitaka vita na mimi ambavyo najua hutaweza kushinda endelea na mambo yako. Nitakufanya kitu kibaya ambacho kitabakia katika kumbukumbu zako mpaka unafukiwa chini. “Mwambie na mpumbavu mwenzako mpango unaopanga wa kutaka kuichukua mali yangu mtakufa kifo kibaya. Leo sikuja kwa shari nimekuja kistaarabu. Mara ya pili utashangaa na hutaamini kuwa ni mimi,” Balkis alisema kwa sauti kali kidogo iliyomtisha Ashura.
ILIPOISHIA: “Sasa sikiliza Ashura huenda utashangaa kuniona hapa, sitaki kujieleza sana ila ukitaka vita na mimi najua huwezi, nitakufanyia kitu kibaya ambacho kitabakia katika kumbukumbu yako mpaka unafukiwa chini. “Mwambie na mpumbavu mwenzako kwamba mpango mnaoupanga wa kutaka kuzichukua mali zangu mtakufa kifo kibaya. Leo sikuja kwa shari bali kwa ustaarabu, mara ya pili utanishangaa, hutaamini kuwa ni mimi,” Balkis alisema kwa sauti kali kidogo iliyomtisha Ashura. SASA ENDELEA... Baada ya kusema maneno yale, Balkis aliufungua mlango wa gari na kutoka nje huku akifyonya kwa sauti kali, alipolizunguka gari akatoweka. Baada ya kuondoka eneo lile, Ashura alishtuka kama mtu aliyetoka usingizini na kujiuliza alichokiona na kukisikia kama kilikuwa ni cha kweli au alikuwa akiota. Wazo lililomjia haraka aliamini kabisa kuwa ile ilikuwa ni ndoto, aliamua kwenda kwa mganga kupata tiba ya kumrudisha Muddy mikononi mwake. Alijishangaa mwanaume aliyemgeuza mradi amekuwa kero moyoni mwake kila dakika alijikuta akimpenda na kumtamani kuwa naye tena. Aliendesha gari huku akiapa kutompa msaada kiumbe yeyote kwa kuhofia kukutana na matatizo ambayo bado aliamini kuwa ni ndoto. Hakuamini kama mtu angeweza kugeuka mara mbili katika hali ya kawaida, kwake alijua ile ilikuwa ni ndoto mbaya tu. Alipofika Mbagala Rangi Tatu alikata kushoto na kuelekea Kimbangulile, alipofika kwa mganga alishangaa kukuta watu wakiwa wamejaa kuonesha kulikuwa na jambo. Alisimamisha gari mbali kidogo na nyumba ya mganga na kuteremka kisha akajisogeza kwenye kundi la watu ambapo kila mmoja alikuwa akisema lake. Alimsikia mmoja akisema; “Lazima yule atakuwa ni jambazi aliyefanyiwa kitu kibaya na mganga.” “Hapana mbona hakutoka mle ndani yule lazima atakuwa ni jini tu.” Yalikuwa naneno yaliyomchanganya Ashura na kujiuliza mganga amefanya nini, ilibidi amwite pembeni dada mmoja ili apate kumhoji vizuri. “Samahani dada yangu kuna nini?” “Mmh! Kuna jambo limetokea linawachanganya watu wengi.” “Jambo gani?” “Mzee Chujio ameuawa.” “Mzee Chujio gani?” “Yule mganga.” “Mganga?” Ashura aliuliza kwa mshtuko. “Eeh, unamfahamu?” “Sasa dada yangu nani asiyemjua mzee Chujio sehemu hii?” “Basi ndiyo hivyo, ameuawa katika mazingira ya kutatanisha.” “Una maana gani?” “Nasikia kuna dada mmoja mrembo alikuja na kuingia ndani kwa mganga na kuwaacha wateja wachache wakiwa kwenye foleni. Lakini inasemekana hakutoka, baada ya wateja kusubiri kwa muda bila kusikia wakiitwa ndani waliamua kuingia lakini cha ajabu wakamkuta mganga amelala chini akiwa amekufa na kutoka funza mdomoni kama aliyefariki wiki moja iliyopita.” “Funza mdomoni?” “Ndiyo.” “Sasa jamani mtu wa kutoka funza si mtu aliyekufa zaidi ya wiki?” Ashura alisema kwa mshtuko. “Hapo ndipo watu walipochanganyikiwa na kuamini kuwa yule mwanamke mzuri alikuwa ni jini.” “Jini! mna maana gani?” “Wanasema alikuwa mzuri sana, tena alikuwa akinukia na alipoingia ndani hakutoka.” “Alivaa nguo gani?” “Mmh! Hebu muulize yule dada aliyesimama katikati ya watu,” alimuonesha dada mmoja aliyekuwa akizungumza na watu huku akilia na kuweka mikono kichwani. “Naomba uniitie.” Yule binti alimfuata yule dada aliyekuwa akizungumza huku akitokwa na machozi, baada ya kusogea karibu ya Ashura, ilibidi ajitambulishe kuwa ni mmoja wa wateja wa mzee Chujio mtu aliyemtegemea kwenye mambo yake. “Samahani mdogo wangu hata mimi nilikuwa nimekuja kwa mzee Chujio lakini kuna habari zimenichanganya sana. Nini kimemsibu mganga wetu?” “Dada yangu hata kuzungumza nashindwa, siku tano zilizopita mzee Chujio alinisaidia matatizo yaliyonitesa kwa miaka kumi. Dawa alizonipa zilinionesha yote aliyonieleza, dada yangu walimwengu ni wabaya, niliteswa na mke mwenza na kufikia hatua ya kunuka mwili mzima hata kukaa mbele za watu nilikuwa siwezi. “Nilitengwa na watu,
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wanaume walinipenda kwa kuniona, lakini waliponisogelea walikuwa wakikimbia kutokana na harufu kali kama ya mzoga uliooza. Leo dada yangu nilikuwa nafuata dawa na kupatiwa kinga baada ya awali kuondolewa tatizo langu. “Ajabu wakati nasubiri kuingia kwa mganga alipita dada mmoja mrembo na kuingia ndani bila kufuata foleni. Kwa vile ilikuwa ni zamu yangu nilitaka kumfuata ndani kumtoa kwani hakuonesha ustaarabu, lakini wenzangu walinisihi nikamuacha amalize shida yake ndipo nami niingie. “Baada ya muda kidogo tulisikia watu wakibishana, kauli ya mganga ilikuwa ya juu akionesha kuna kitu hakukubaliana na yule mwanamke mrembo mwenye kunukia manukato. “Mganga alisema hawezi kufundishwa kazi na mtu, mara tulisikia sauti ya yule mwanamke mrembo akisema kuwa hana jinsi ile ndiyo zawadi yake. “Baada ya hapo kilipita kimya kirefu huku muda ukizidi kuyoyoma. “Baada ya nusu saa bila kusikia mazungumzo wala yule mwanamke mrembo kutoka, niliamua kuingia ndani kujua kilichokuwa kikiendelea. “Nilipoingia nikamkuta mganga akiwa amelala chini, kilichonishtua zaidi ni funza waliokuwa wakimtoka mdomoni kama mtu aliyekufa muda mrefu.”
“Funza?” Ashura aliuliza tena japo taarifa ya kutoka funza alielezwa mapema. “Funza dada, kama mtu aliyekufa muda mrefu.” “Unataka kuniambia kabla ya kutokea tukio lile ulionana naye?” “Tena alitoka nje na mgonjwa aliyekwenda kumfanyia tiba nyuma ya nyumba yake, aliponiona alitaka kujua hali yangu, nilimweleza ninavyoendelea na kuniambia vitu vyote alivyovitafuta kwa ajili ya kazi yangu vimepatikana...Yaani..,” Kufikia pale yule dada aliangua kilio mikono kichwani, Ashura aliingia kwenye kazi ya kumbembeleza. “Mdogo wangu hebu nyamaza kwanza.” “Dada inauma, haiwezekani niwe miye, nimeteseka muda mrefu, napata tiba mganga anauawa katika mazingira ya utata,” aliendelea kulia kilio cha kukata tamaa. Ashura, japo alijitahidi kujikaza na kumbembeleza kwa kumlalia kifuani, lakini moyoni alikuwa na maumivu makali kama angepata sehemu iliyojificha, basi naye angeangua kilio ambacho hakuna mtu ambaye angeweza kumbembeleza. Kifo cha mzee Chujio kilikuwa pigo kubwa maishani mwake, ndiye aliyekuwa tegemeo lake katika mambo yote aliyoyafanya ya kuwatapeli wanaume kwa kuwapumbaza kwa dawa. Alijiuliza nani atakayemsaidia katika maisha yake baada ya kifo cha mzee Chujio ambaye alimgeuza kama Mungu wa pili. “Unasema ulimuona?” Ashura kwa kuchanganyikiwa alijikuta akiuliza swali alilojibiwa awali. “Ndiyo.” “Unasema alipoingia ndani hakutoka?” “Ndiyo.” “Au wakati anatoka huyo mwanamke ulikuwa umesinzia?” “Dada yangu kusinzia tusinzie wote tulio kuwa tunasuburi huduma?” “Alivaa nguo gani?” “Gauni refu jekundu lenye maua shingoni na kifuani, sielewi maua yale ya rangi gani kutokana na kumeremeta.” “Mmh! Shingoni alikuwa na mkufu wenye herufi M?” “Eeeh.” “Mtandio wake wa bluu yenye maua ya kumetameta?” “Huo huo!” “Ana kipini cha mkufu?” “Eeeh dada, umemjuaje?” “Mmh! Kazi ipo,” Ashura aliguna na kusema kwa sauti ya chini. “Kwani unamfahamu?” “Kuna mtu nilikutana naye njiani uliponielezea alivyovaa nilikisia basi lazima atakuwa yeye.” “Kwa hiyo si jini kama watu wanavyomdhania?” “Mmh! Sijajua, kwani hakuna mlango wa kutokea nyuma?” “Dada kama wewe ni mteja wa mzee Chujio, chumba chake unakijua, mlango utoke wapi?” “Mna uhakika hakutoka?” “Angetoka tungemuona kama si mimi basi wenzangu wangemuona.” “Mmh! Nina wasiwasi alitoka hamkumuona.” “Sawa alitoka, kile kifo nacho cha muda mfupi mtu aoze na kutoka funza kwa sekunde chache kinatokana na nini?” “Inawezekana alimnywesha sumu kali iliyomuozesha tumboni na kuzalisha funza.” “Mmh! Labda.” “Basi dada, acha nirudi zangu hata mimi nimechanganyikiwa sana.” “Sawa dada, lakini mimi ndiye nimechanganyikiwa hata kuliko familia yake.” Wakati huo polisi walifika kuchukua mwili wa marehemu, alishuhudia mwili wa mzee Chujio ukitolewa huku familia yake na wateja wakiangua vilio. Ashura alishindwa kujizuia, alikimbilia kwenye gari lake na kujifungia, alilia hadi macho yakamvimba. Alijiuliza yule mwanamke atakuwa nani, japo ilikuwa vigumu kukubali kuwa Balkis ni jini, lakini mambo yaliyomtokea kwenye gari alipombadilikia kama kinyonga yalimfanya aanze kuamini kabisa mke wa Muddy ni jini. “Mungu wangu Muddy atakuwa ameoa jini?” Alijikuta akipayuka kwa sauti. “Haiwezikani lazima nifanye chini juu nimtoe kwenye balaa lile.” Ashura alijiingiza kwenye vita nyingine ya kujua hatima ya Muddy kwa Balkis kwa kuamini kuna njia ya kuyafukuza majini. Aliwasha gari lake na kurudi nyumbani. *duh!!tamuje?? ITAENDELEA
ILIPOISHIA; Katika kutembeza macho aliwaona wajukuu wa mzee Njiwa wakicheza nje ya uzio, aliona kama atamuua mmoja basi mzee Njiwa Manga ataacha kazi ya kuwatibu ili ashughulikie msiba na kuwafanya Ashura na mwanaume wake kuondoka ili warudi siku nyingine. SASA ENDELEA... Aliamini kama watatoka bila kupatiwa kinga yoyote angetumia nafasi ile kuwamaliza wote ili aweze kuishi na Muddy bila tatizo japo alijuwa kwa upande wa baba yake kulikuwa na vita nyingine. Kila alivyotaka kuteremka roho ilimkataza kwa kuwaonea huruma viumbe wasio na hatia. Kutokana na uwezo wake aliweza kuyasikia yote yaliyokuwa yakizungumzwa ndani na kupanga kama atakubaliana nao kabla ya kuwapa kinga naye, hatakuwa na budi kuua mtoto mmoja. Ashura na mwanaume wake waliingia katika chumba cha mzee Njiwa Manga na kukaa kwenye mkeka. “Karibuni,” mzee Njiwa Manga aliwakaribisha. “Asante,” walijibu kwa pamoja. “Mh! Niwasaidie nini?” “Mzee tunahitaji msaada wako, tuna vita nzito na mwanamke mmoja jini.” ”Mmejuaje ni jini wakati majini hayaonekani?” “Anatutokea katika umbile la kibinadamu na wakati mwingine katika maumbile tofauti, pia tunatokewa na mambo ya kutisha.” “Tena jana kamuua mganga mmoja Mbagala kifo cha kutisha,” Ashura aliongezea. “Mmh! Majina yenu?” Aliwauliza huku akichukua kibao cheusi na chaki. “Naitwa Shuuna.” “Shuuna...” mganga alilirudia jina lile kwa sauti ya chini huku akiliandika kwenye kibao. “Mbona unaonekana una majina mengi?” Mganga Njiwa Manga alimuuliza Ashura. “Lakini hili ndilo langu la kuzaliwa.” “Sasa nikusaidie kwa jina gani kwani yote uliyatumia na watu tofauti wanakujua kwa majina hayo?” “Kwa sasa natumia jina hili.” “Kama ukifanikiwa kurudi kwa Muddy utatumia jina gani?” Swali lile lilimfanya Ashura akae kimya na kukosa la kujibu kwa kuona kama siri yake inatoka nje. “Lakini mzee suala la Muddy tulishaachana nalo, kama kutusaidia msaidie kwa jina la Shuuna,” Tonny aliingilia kati mazungumzo. “Najua mmekuja pamoja lakini kila mmoja ana mawazo yake ambayo sitaki kuyaingilia kwa vile siyo kazi yangu,” mzee Njiwa Manga alijibu kwa fumbo lililomuacha gizani Tonny bila kujua dhamira ya Ashura kwa Muddy ilikuwa nini. “Naomba niachane na mwenzako kwanza, hebu nawe nieleze jina lako?” “Naitwa Antony.” “Antoniii,” alilirudia jina lile kwa sauti ya chini huku akiliandika kwenye ubao. Baada ya kuandika alitulia kwa muda akiandika vitu kwenye ubao na kukohoa kidogo kisha akauliza: “Nimeona yote, sasa shida yenu nini hasa?” “Mzee kama tulivyokueleza kuwa tuna tishio la mwanamke mmoja ambaye ni jini, anatishia maisha yetu.” “Kwa hiyo mnataka nini?” “Tunataka utukinge ili tuweze kupambana naye.” “Mnamjua jina lake?” “Balkis,” Ashura alijibu. Mganga aliliandika jina lile, kama kawaida alilirudia kwa sauti ya chini. “Balkis...Balkis.” Baada ya kutulia kwa muda alisema: “Lakini mbona mimi sioni madhara ya huyu mnayemuogopa?” “Mzee huyu ni mtu mbaya sana, amenitokea mara nyingi kwenye gari katika sura tofauti na kutishia maisha yetu,” Ashura alisema huku macho yamemtoka pima kwa kusistiza. “Mbona hapa panaonesha jini huyo ni mpole sana kuliko majini wengine?” “Si kweli, ana roho mbaya sana, amemuua mzee Chujio kifo kibaya sana,” Ashura alisema. “Unajua sababu ya kuuawa mzee Chujio?” mganga aliuliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kutokana na maelezo ya huyo mwanamke jini anasema aliingilia kazi yake na kuwa mbishi ndio akaamua kumfanya vile.” “Sasa hamuoni na mimi nikiingilia kazi si yangu anaweza kunifanya kama mzee Chujio?” “Hawezi.” “Kwa nini asiweze?” “Tunasikia wewe ndio kiboko ya majini.” “Ni kweli kazi yangu ni kutibu na si kushindana na majini.” “Lakini mzee kazi yako si kutusikiliza wateja shida yetu na kukupa kiasi ukitakacho,” Tonny alimueleza mganga.. “Sikiliza kijana, mimi si mchawi ni mganga wa kuwasaidia wenye matatizo, ndiyo maana nipo mpaka leo.Waganga wengi wamepoteza sifa zao kutokana na kuingilia kazi ya wachawi. “Tumekuwa tukifanya makosa ya kuingia kwenye kazi ya kutesa, kuua au kuingia kwenye vita na viumbe kama majini ambayo wakati mwingine huwa hayana matatizo na watu.” “Sasa mzee utatusaidiaje?” “Mpaka sasa sijajua shida yenu nini?” “Tunataka kinga ili tusiweze kudhuriwa na jini.” “Jini gani wa kuwadhuru ninyi?” “Balkis,” Ashura alijibu. “Balkis atawadhuru vipi bila ninyi kumchokoza?” “Yule hana cha kumchokoza bali huamua kuua bila sababu,” Ashura alitengeneza uongo. “Sitawapa dawa yoyote zaidi ya kauli ya Balkis mwenyewe.” “Mbona hatukuelewi, kauli gani?” “Mtaisikia muda si mrefu kutoka kwake Balkis.” Mzee Njiwa alitoka nje na kurudi na kitezo chenye moto, akakiweka mbele yake, akatoa mavumba kwenye chupa kisha akasema: “Hii dawa kazi yake kuyavuta majini mazuri, kama Balkis ni jini mbaya hatakuja nikimwita.” Baada ya kusema vile alianza kuweka mavumba kwenye moto huku akisema: “Balkis binti mfalme wa bahari, naamini wewe ni jini mwema nakuomba uje mbele yangu, lakini kama si jini mwema ukiingia himaya yangu ndiyo mauti yako...Balkis njoo mbele ya wanadamu hawa wana mashtaka juu yako.” Je, Balkis ni jini mzuri au mbaya?
“Nimewaonesha ishara nyingi za vitisho ili wajue mimi si kiumbe wa kawaida ili wachane na mimi, lakini wamekuwa wabishi, kabla ya kuja huku niliwapa onyo zito lakini wamekuwa kama kenge, hawasikii mpaka watoke damu masikioni. “Tena wana bahati kubwa leo ningepata dhambi nyingine, wakati natoka nyumbani niliwaona wamekaribia kwako lakini kasi yangu ilichelewa kidogo na kuwakuta wameshaingia kwenye ngome yako. “La sivyo kama ningefanikiwa kuwatia mikononi ningewaulia mlangoni kwako na kama ungewasikiliza na kuwapatia tiba kabla tiba yao haijatimia ningemuua mjukuu wako mmoja ili uhalalishe kazi hii na wangetoka ningewamalizia mbali, ” Balkis alisema kwa sauti isiyotaka mzaha, huku kauli yake ikizidi kuwatisha moyoni walioomba msaada wa mzee Njiwa Manga. “Nimekuelewa sana Balkis binti wa mfalme Barami, sasa ulikuwa unataka nini?” “Kama nilivyowaeleza waachane na mimi, waendelee na maisha yao.” “Wakifanya hivyo utakuwa na vita nao?” “Niwe nao ili iwe nini ikiwa kila mmoja na maisha yake, ila tofauti ya hapo nitakachokifanya Mungu anajua.” “Nina imani mmesikia yote aliyosema Balkis, niliwaeleza ni mpole mwenye huruma na upendo kwa viumbe wenzake. Napenda kuwaeleza kuwa maelezo yake ndiyo tiba yenu na mkitoka hapa mkienda kinyume na haya aliyosema, nisione mtu hapa, mtamalizana wenyewe, mmenisikia?” Alijibu kwa kunyanyua vichwa kwani hata midomo ilikuwa mizito, baada ya majibu yao ya kibubu mzee Njiwa Manga alimgeukia Balkis. “Nina imani wamekuelewa ila wakienda kinyume mimi simo.” “Wewe unasema hivyo lakini mioyo yao imejaa tamaa ya mali na uhai wa watu, narudia tena sitawaua ila nitawaadhiri mbele za watu, hilo litakuwa pigo kubwa na mkizidi nitawageuza mbwa.” “Nimekuelewa sana Balkis unaweza kwenda,” mzee Njiwa Manga alisema. Baada ya kuruhusiwa kutoka alinyanyuka na kutoka chumbani katika umbile la kibinadamu, wote walimsindikiza kwa macho hadi nje. Waliokuwa wamekaa nje kusubiri huduma macho yao yalishuhudia mwanamke mzuri akipita mbele yao huku wakijiuliza amepita saa ngapi kutokana na watu wengine kuwepo kwa muda mrefu. Balkis baada ya kutoka katika uzio wenye nguvu wa mzee Njiwa Manga alitoweka. Baada ya kuondoka Balkis, mzee Njiwa Manga aliwageukia wateja wake na kusema: “Nina imani tatizo lenu limekwisha?” “Mzee litakwisha vipi wakati umemsikia mwenyewe amesema nini,” Tonny alihoji. “Kasema nini?” “Si amesema tukifuatilia mambo yake atatugeuza mbwa,” Ashura alijibu. “Sasa mnataka kufuatilia mambo yake?” “Hapana.” “Sasa tatizo nini?” “Tulikuwa tunaomba kinga.” Tonny alisema. “Ya nini?” “Ili tujikinge na matatizo ya wanadamu na majini.” “Ili?” “Mzee kama hujui kazi yako, kwani wanadamu wanakuja kwako kutafuta nini?” “Tiba ya matatizo yao.” “Sasa mbona hutaki kutusaidia?” “Kwani shida yenu iliyowaleta hapa ni nini?” “Kuzuia nguvu za jini Balkis.” “Sasa niwape kinga ya nini?” “Anaweza kutugeuka na kutufanyia kitu kibaya.” “Hawezi na sina tiba yoyote labda muwe na tatizo lingine.” “Hatuna, ni hili hili la huyu mwanamke ndilo linalotutisha, unamuona kwa macho tu lakini ni kiumbe kibaya sana.” “Yule hana ubaya kama nilivyowaeleza, lakini mioyoni mwenu mna dhamira mbaya naye, kwa hilo mimi halinihusu kama mnataka ushindani dawa hiyo sina.” “Kwa hiyo huna msaada wowote kwetu?” Tonny aliuliza. “Msaada niliowapa ni mkubwa kuliko kukuchanjeni au niwape dawa ya kufukiza.” “Mzee msaada gani uliotupa zaidi ya kutuacha njia panda?” Tonny alizidi kuhoji. “Msaada niliowapa hamuujui lakini ni mkubwa sana, najua mmezunguka kwa waganga wengi kwa kazi zenu za dhuluma. Hamkuwahi kukutana na tatizo kisha mkatibiwa bila kunywa, kujifusha au kuchanjwa dawa? Mliyekuwa mnamuona adui ameeleza hataki kitu gani, sasa mnataka nifanye nini?” ”Basi inatosha inawezekana na wewe umemuogopa,” Tonny alisema kuonesha alitaka zaidi ya yale aliyoelezwa. “Kweli nimemuogopa nipo kwa ajili ya kutibu si kujiingiza kwenye matatizo ya kujitakia, kutokana na maelezo yake nilikuwa nampoteza mjukuu wangu kwa ajili yetu. Nawaeleza mkikosea kwenda kwa mganga mwingine kitakachowakuta hamtakisahau mpaka mnakufa.” “Tumeelewa.” Tonny alijibu kwa shingo upande. “Basi mnaweza kwenda ili niendelee na wenzenu.” “Sasa mzee tukupe kiasi gani?” “Nina imani hamkuona nilichokifanya, nendeni msitoe kitu chochote.” “Hapana mzee hata ya kuangalizia, sijui elfu moja?” “Hapana nimewasamehe kila kitu.” Walitoka huku wakiamini mzee Njiwa Manga uwezo wa kutibu umepungua ndiyo sababu ya kushindwa kuwasaidia kupambana na Balkis.
“Sauda,” walisema mashoga zake waliokuwa wakilia huku mikono ikiwa kichwani, wengine hata nguo ziliwaanguka bila kujua. “Sauda kafanya nini?” “Ame...” “Amefanya nini mbona mnanichanganya, mke wangu kafanya nini jamani?” mganga alijikuta kwenye mtihani mzito wa kujua mkewe amefanya nini kwani muda mfupi uliopita alimtuma dukani. Mara aliingia mwanamke mwingine aliyekuwa akilia huku akisema: “Haiwezekani Sauda atutoke kirahisi namna hii.” “Huu lazima uchawi haiwezekani njiwa amgonge afe,” mwingine alisema huku akijitupa chini kwa uchungu. “Jamani mke wangu kafanya nini?” pamoja na kuwasikia wakisema lakini hakuwaelewa. Mara watu waliingia na mwili wa mkewe ambaye alikuwa amekwishapoteza uhai. \“Ha! Amefanya nini?” Kakakuona alitaharuki. Alimvamia mkewe ambaye alikuwa amefunikwa kanga, akamfunua na kumwinamia! Hakuamini alichokiona mbele yake. “Sauda mke wangu umepatwa na nini? Kwa nini nilikutuma kwenda kuchukua dawa? Kwa nini nilikuwa na wazo baya? Maskini mke wangu nimekuponza, ulikuwa ukizungumza na wanawake wenzako, ona sasa umebadilika jina na kuitwa marehemu! Nini faida ya kazi yangu?” Mganga alilia kama mtoto mdogo huku akimgeuza mkewe ambaye alikuwa ameanza kupoa. Ashura na mwanaume wake nao walikuwa wametoka na kushuhudia tukio lile. Balkis naye hakuwa mbali, moyo ulimuuma kwa kitendo chake cha kuyachukua maisha ya kiumbe kisicho na hatia. Machozi ya damu yalimtoka. Kila mganga alipokuwa anamlilia mkewe kwa maneno ya uchungu na yeye ndivyo alivyokuwa akiumia na kulia zaidi. Ashura alipoangalia pembeni alishtuka baada ya kumuona Balkis
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
akiwa katika kundi la watu huku naye machozi yakimtoka. Baada ya kumuona alipatwa na mshtuko mkubwa, akaanguka na kupoteza fahamu. Hali ile iliwatisha watu wote waliokuwa pale. Mganga alimwacha mkewe na kukimbilia ndani kuchukua dawa ya unga kwa ajili ya kuzuia nguvu zozote mbaya. Aliimwaga hewani lakini Balkis aliwahi kuondoka eneo lile na kwenda kukaa njiani kuwasubiri Ashura na mwanaume wake. Mganga baada ya kufanya vile bado hakuamini, aliuchukua mwili wa mkewe na kuuingiza ndani kujaribu tiba zote anazozijua akiamini atafanikiwa kumrudisha mkewe. Alikuwa amesahau kuwa hakuna mtu wala kiumbe chochote dunia chenye uwezo wa kurudisha roho ya mtu au kiumbe zaidi ya Muumba peke yake. Licha ya kuhangaika zaidi ya saa nzima kurudisha roho ya mkewe iliyopotea, bado hakufanikiwa. Hatimaye alikubaliana na ukweli kwamba mkewe amefariki. Ilibidi atoe taarifa za kifo cha mkewe kwa ndugu na jamaa, mipango ya mazishi ikaanza. Kutokana na kuchanganyikiwa na kifo cha mkewe alisahau hata kama kuna wateja aliokuwa akiwashughulikia. Ashura baada ya kupata nafuu alijikuta akichanganyikiwa kwa kuamini kabisa kifo cha mke wa mganga kimefanywa na Balkis. Wasiwasi ulizidi kumpanda na kujiuliza kama ni yeye basi hata maisha yao yalikuwa hatarini. “Tonny nimemuona Balkis?” “Wapi?” “Alikuwa kwenye kundi la watu.” “Mwongo!” “Kweli! Tena alikuwa analia machozi ya damu.” “Mungu wangu! Unataka kuniambia aliyefanya haya ni yeye?” “Inawezekana kabisa, si unakumbuka kauli aliyotoa kwa mzee Njiwa Manga kuwa kama angetusaidia angemuua mjukuu wake.” “Sasa unafikiria anaweza kutufanyia kitu kibaya?” “Hata mimi nimechanganyikiwa.” “Sasa mganga atatusaidia nini?” Tonny aliuliza huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi. “Wee! Tena nyamaza, inavyonekana sisi ndiyo chanzo cha kifo cha mkewe.” “Kwa hiyo unaniambia nini?” “Tuondoke, ikiwezekana tusirudi tena na Balkis tuachane naye,” Ashura alisema huku akitetemeka. Wakati huo watu walizidi kusogea eneo la tukio, kila mtu alikuwa akisema lake juu ya kifo cha ghafla cha mke wa Kakakuona. Wapo walioelezea jinsi walivyomuona njiwa yule akimpiga kichwani mke wa mganga na kutoweka kisha kuanguka chini na kupoteza uhai. “Kweli kabisa Balkis ndiye aliyemuua mke wa Kakakuona,” Tonny alipata uhakika. “Sasa unaona tumechokoza nyuki wakati hatuna mbio.” “Sijui tufanye nini ili Balkis atuelewe?” “Nimekueleza tuachane naye.” “Atatuelewa?” “Mmh! Kazi ipo, kama amejua tunataka kumuua unafikiri atatufanya nini?” Ashura alisema kwa sauti ya kukata tamaa. “Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, kwa nini tusiendelee kuwa hapa ili mganga atupe hata kinga ili asitudhuru?” “Tonny hebu kuwa na akili, umesikia aliyefanya vile ni Balkis mganga atatufanya nini, hiyo milioni mbili yako itarudisha roho ya mkewe?” “Mmh! Na kweli, kwa hiyo unasemaje?”
ILIPOISHIA; Baada ya mazungumzo Ashura alijikuta mtu mwenye hofu kutokana na kauli za Balkis akiamini kabisa si kiumbe cha kawaida. Lakini katika mawazo yake alikumbuka kuna mzee mmoja kiboko ya majini ambaye angeweza kumsaidia katika mkakati wake. SASA ENDELEA... Balkis baada ya kutoka kwa Ashura alikwenda chini ya bahari kwa wazazi wake kuitikia wito. Alipofika chini ya bahari alipokewa kama ilivyo kawaida kwa mapokezi ya heshima kama mwana wa mfalme. Baada ya kuingia katika jumba la kifahari alipelekwa moja kwa moja kwenye bustani walipokuwepo wazazi wake. Mfalme Barami pamoja na kukasirishwa na kitendo cha mwanaye kukiuka maagizo yake, alijitahidi kuzuia hasira zake kutokana na kauli ya mkewe Malkia Huleiya kuwa asitumie nguvu kuamua jambo lile. “Naam mtukufu mfalme,” Balkis alipiga magoti mbele ya baba yake. “Karibu, kaa kitini,” Mfalme Barami aliondoa mkono kichwani kwa mwanaye kuonesha amepokea heshima ya mwanaye. “Heshima kwenu wazazi wangu mfalme na malkia.” “Tumeipokea.” Baada ya kukaa, alitulia kusikiliza wito wa baba yake. “Balkis,” Mfalme Barami alimwita mwanaye. “Abee mtukufu mfalme.” “Nimekupa kazi gani?” “Ya kukusanya vizazi vya wanawake.” “Ili vifanye kazi gani?” “Viwe tiba ya matatizo yangu.” “Umefanya nini?” “Sijafanya lolote.” “Taarifa zilizotufikia ni uongo?” “Ni za kweli.” “Sasa ndiyo tuliyokutuma?” “Kule duniani lazima uwe karibu na wanadamu ili uweze kufanya kazi zako kwa urahisi.” “Sawa, lakini umefunga ndoa.” “Eeh, nimefanya vile nina sababu zangu na muda si mrefu mtatambua.” “Hapana tunaomba uachane na yule mwanadamu mara moja.” “Kuachana naye haitawezekana, jamani si mnapata mnavyovihitaji, tatizo nini, tena kwa kasi kubwa tofauti na mwanzo.” “Sawa unafanya kazi nzuri, lakini hatuwezi kushea na wanadamu kwa hiyo ukitoka hapa tunataka jibu la kuvunjika kwa ndoa yenu mara moja.” ”Sawa nimekuelewa,” Balkis alijibu kwa mkato kuepusha kubishana na baba yake na kusababisha kufungwa kwenye chumba cha giza na kuharibu mipango yake yote. “Na agizo hili litimizwe baada ya kutoka hapa la sivyo nitakuja mwenyewe kumuua huyo mwanaume kwa mkono wangu.” “Sawa baba hakuna tatizo nitatimiza ulichoniagiza.” “Nimefurahi umenielewa, unaweza kwenda.” Baada ya mazungumzo yale Balkis alirudi na akili zake mwenyewe kwa kuamini safari ile ndiyo ya mwisho kurudi kwa wazazi wake. ***** Baada ya vitisho vya Balkis mwanaume wa Ashura alikumbuka kitu na kumueleza mpenzi wake. “Shuuna kuna kitu nimekumbuka.” “Kipi hicho?” “Njia ya kuweza kumdhibiti huyu mwanamke.” “Njia gani?” “Si unakumbuka baba yangu alitumiwa jini kidogo afe.” “Sijui.” “Ooh! Nilisahau kukuelezea mambo yaliyompata baba yangu, walimwengu walimtupia jini ili wamuondoe duniani.” “Hukuwahi kunipa habari hiyo.” “Basi yule atatusaidia, nasikia mganga yule anasifika kwa kukomesha viburi vya wadudu kama hawa.” “Anaweza kweli siyo yawe yale yale.” “Mzee yule ndiye kiboko wa kuyatoa majini sugu yanayogoma kutoka kote wanapokwenda kwa waganga.” “Sasa kama ana uwezo wa kuyatoa, kuyaua anaweza?” “Anaweza, kwake ni kitu kidogo mzee yule ni kiboko ya majini kila mtu anamjua.” “Isiwe ya mzee Chujio, si unakumbuka tulivyomuamini lakini mwisho wa siku tumeona jinsi alivyokufa kifo cha kutisha,” Ashura aliingia woga kidogo. “Hivi unamsikia mzee Njiwa Manga.” “Mmh! Pamoja na sifa ulizonipa bado yule mwanamke anatisha, inaonekana ana nguvu za ajabu.” “Sijawahi kuona uwezo wa ajabu kama wa mzee Njiwa Manga, yaani baba baada ya kushindikana kwa waganga zaidi ya wanne walikata tamaa na kuamini hawezi kupona. Lakini alitokea mtu na kutueleza twende kwa mzee Njiwa Manga Bagamoyo. “Kwanza tulitaka kukataa lakini alituhakikishia tatizo letu litakwisha, tulikwenda mpaka Bagamoyo na kuonana na yule mzee. Hakufanya tofauti na waganga waliotangulia kutoa majini, tulijua ni yale yale ya mgonjwa kuonekana amepona lakini akifika nyumbani anashikwa tena na mapepo. “Lakini mzee yule baada ya mgonjwa kurudi katika hali ya kawaida alimpa dawa ya kuoga na kunywa kwa siku saba. Mpaka leo hajatokewa na shetani wala kibwengo.” “Lakini sisi hatuna mashetani.” “Shuu yule si mganga wa majini tu ni mganga wa maradhi yote.” “Sasa sisi tunaumwa nini?” “Kwani ulikwenda kwa mzee Chujio kwa ajili gani?” “Nilikuwa na mambo yangu binafsi wala hayahusiani kabisa na majini,” Ashura alipindisha kwa kuamini mwanaume wake akijua kuwa alifuata dawa ya kurudiana na Muddy angekasirika. Ashura na mwanaume wake bado wanaonesha kiburi na kupanga mipango ya kumdhibiti Balkis.
LIPOISHIA “Nilikuwa na mambo yangu binafsi wala hayahusiani kabisa na majini,” Ashura alipindisha kwa kuamini mwanaume wake akijua kuwa alifuata dawa ya kurudiana na Muddy angekasirika. SASA ENDELEA... Ashura alikuwa na siri nzito moyoni mwake kama angefanikiwa kurudiana na Muddy, mwanaume aliyeamini kuwa bila ya mipango yao ya utapeli alikuwa ndiye sahihi kwake. Mpango wake ulikuwa kumuua mwanaume wake kwa kumuwekea sumu kwenye chakula ili aishi na Muddy katika maisha ya ndoa. “Kama nilivyokueleza kabla ya kujua kuwa yule mwanamke ni jini, nilikwenda kwa ajili ya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/---
kuangalia jinsi ya kumuingia na kuweza kuchukua mali yake. Lakini ilionesha si kiumbe wa kawaida na kama ulivyosikia, mzee Chujio alizidiwa nguvu na yule mwanamke. Lakini kwa mzee Njiwa Manga kutokana na historia ya watu hajawahi kushindwa suala la majini.” “Tonny mbona hatuelewani nani ana majini mpaka twende kwa mzee Njiwa Manga?” “Kumbuka tunataka mali ya Muddy na mkewe ambaye ni jini, huoni tunahitaji msaada wa mtu mwenye uwezo wa kupambana na majini.” “Mmh! Kama ana uwezo huo kuna umuhimu wa kwenda kwake.” “Hakuna njia nyingine kwa mambo niliyoyaona yamenitisha bila hivyo tunaweza kupotea.” Walikubaliana kwenda siku iliyofuta kwa mganga Njiwa Manga ili kutafuta uwezo wa kupambana na Balkis. **** Siku ya pili Ashura na mwanaume wake walikwenda Bagamoyo kwa mganga Njiwa Manga, kwa vile Tonny alikuwa hajakwenda kipindi kirefu, ilibidi aulizie sehemu anayoishi. Alielekezwa na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa mganga huyo, walipofika walikuta magari aina tofauti zaidi ya kumi kuonesha kuwa siku ile kulikuwa na wateja wengi. Ilibidi wakae kwenye benchi kusubiri kwa muda mbele yao kulikuwa na wagonjwa zaidi ya ishirini, walijumuika pamoja na kusubiri tiba. Wingi wa watu ulitaka kuwakatisha tamaa na kutaka kuondoka. “Tonny kwa nini tusiondoke turudi kesho mapema, huoni tutachelewa kutoka?” Ashura alimwambia mwanaume wake. “Kwani tunawahi nini? Kwa vile tumeishafika hata usiku tutarudi, nataka nikueleze ukweli pamoja na kujionesha siogopi kitu, lakini siri niliyokuwa nayo moyoni ni Mungu tu anajua. Kama yale maajabu yangerudia basi ningekufa kwa hofu. “Nilikuona ulikuwa mwenye hofu kubwa na niliyasikia mapigo yako ya moyo yakikimbia kama gari lililokatika breki na kunifanya nisimame kidete,” alisema Tonny. “Mmh! Wee acha tu, kama angezidisha ningekufa, yaani maneno yako yalinitia nguvu ya ajabu. Kwa kweli nimeanza kuwa muoga wa kila kitu hata upepo sasa hivi ukivuma naogopa najua amekuja,” alijibu Ashura. “Wee acha, baada ya kugundua yule mwanamke ni jini niliishiwa nguvu na kuamini simuwezi kwa lolote zaidi ya kutumia nguvu za ziada kuja hapa kwa mzee Njiwa Manga ndipo penye ufumbuzi bila hivyo tutaumia,” alisisitiza Tonny. “Kwa hilo hata tukikaa siku mbili sioni tatizo, sasa hivi namuogopa yule mwanamke kama kifo,” alimalizia Ashura. Wakati wakibadilishana maneno hayo, Balkis hakuwa mbali na nyumba ya mzee Njiwa Manga, wakati alipokuwa akitoka kwa wazazi wake chini ya bahari aliwaona Ashura na mwanaume wake wakikaribia kuingia kwa mganga Njiwa Manga. Alijitahidi kuwawahi wasiingie, kasi yake iliishia nje ya uzio wa nyumba ya mganga huyo. Alijipiga chini kwa hasira na kusababisha patokee mtikisiko mdogo uliowashtua watu, hakutaka kukubali kushindwa, alijigeuza njiwa na kwenda kwenye mti mrefu uliokuwa pembeni ya nyumba ya mganga Njiwa Manga. Aliweza kuwaona wateja wa mganga huyo akiwemo Ashura na mwanaume wake, lakini nguvu za dawa za mzee Njiwa Manga zilimzuia asiweze kufanya lolote. Akiwa na hasira alipanga kuwasubiri na kuwatia adabu baada ya kuonesha kiburi. Wasiwasi wake ulikuwa kwenye nguvu za yule mzee zingeweza kummaliza na kudhurumiwa mpenzi wake. Kwa upande wa mali yake aliamini hakuwepo wa kuichukua kwa vile ilikuwa ndani ya uwezo wake. Katika vitu alivyovipanga maishani mwake vilikuwa ni kubeba mimba ya Muddy kuwafanya wazazi wake hasa baba yake asiwe na nguvu ya kumlazimisha kuolewa na jini mwenzake. Alijua kama Ashura akifanikiwa kupata kinga ya kumdhibiti, lazima atamnyang’anya mume wake na kumlazimisha kuendelea kufanya kazi asiyoipenda ya kuchukua vizazi vya wanawake. Akiwa juu ya tawi la mti akichanganyika na ndege wengine, moyo ulimuuma na kujiuliza amfanye nini mganga ili asiwape uwezo wa kudhulumu haki yake. Alijikuta akiwachukia baadhi ya binadamu ambao aliamini kabisa hawakutakiwa kuhurumiwa zaidi ya kuuawa japo siku zote roho yake haikupenda kufanya vile. Akiwa anawatazama wateja waliokuwa wakienda kupata tiba kwa mzee Njiwa Manga, aliwaona Ashura na mwanaume wake wakinyanyuka na kwenda kuonana na mganga huyo. Alijikuta akipandwa na hasira lakini eneo lile lilikuwa lina nguvu za ajabu zisizowezesha nguvu za kichawi na kijini kuingia katika himaya yake. Alipotazama huku na kule, aliwaona wajukuu wa mganga wa Njiwa Manga wakicheza, akaamua kumuua mmoja. Kwanini Balkis alitaka kumuua mjukuu mmoja wa mganga Njiwa Manga?
ILIPOISHIA: Mzee Njiwa alitoka nje na kurudi na kitezo chenye moto na kukiweka mbele yake, alitoa mavumba kwenye chupa na kusema: “Hii dawa kazi yake kuyavuta majini mazuri, kama Balkis ni jini mbaya hatakuja nikimwita.” Baada ya kusema vile alianza kuweka mavumba kwenye moto huku akisema: “Balkis binti mfalme wa bahari, naamini wewe ni jini mwema nakuomba uje mbele yangu, lakini kama si jini mwema ukiingia himaya yangu ndiyo mauti yako...Balkis njoo mbele ya wanadamu hawa wana mashtaka juu yako.” SASA ENDELEA ... Moshi ulikuwa mwingi kiasi cha kujaa chumbani, baada ya muda upepo mkali ulianza kuvuma na kusababisha baadhi ya vitu kutaka kupeperuka lakini mzee Njiwa Manga aliutuliza kwa kusema: “Najua una hasira lakini naomba uwe mpole kama ulivyo, wewe ni mpole tena mwenye upendo kwa wanadamu.” Upepo ulitulia taratibu wakati huo Balkis akiwa katika umbile la njiwa alijikuta akizidiwa na nguvu na kudondoka toka juu ya mnazi na kujikuta akijitahidi asianguke na kuingia kwenye dirisha la chumba cha uganga cha mzee Njiwa Manga. Alitua pembeni ya mzee Njiwa Manga, Ashura na mwanaume wake walishtuka kumuona njiwa mzuri sana mwenye rangi nyeupe aliyepakwa wanja mwekundu uliozunguka katika macho yake. Manyoya yake yalikuwa kama ya plasitiki iliyokuwa ikimelemeta. “Karibu Balkis kwa mzee Njiwa Manga.” Balkis katika umbile la njiwa hakujibu kitu alitulia akiwatizama Ashura na mwanaume wake. Mzee Njiwa Manga alisema:”Najua hukupenda muda huu kuwa hapa, lakini nimekuita kwa nia njema kwa vile wewe ni jini mwema mwenye upendo kwa wanadamu. Nakuomba uwe kwenye umbile tunaloweza kuzungumza kibinaadamu.” Baada ya kusema vile kilipita kiza cha ajabu na baada ya muda ilirudi hali ya kawaida. Sehemu aliyokuwa njiwa alikuwepo Balkis katika umbile la kibinaadamu. Ashura na mwanaume wake kidogo wakimbie kwa hofu.”Msihofu, kama nilivyowaeleza kwa dawa niliyoichoma ni jini mwema tu anayeweza kuingia katika himaya yangu. Balkis asalam aleykumu.” “Waaleiykum msalaam,” alijibu kwa sauti tamu. “Karibu.” “Asante.” Balkis aligeuza uso wake na macho yake yaligeuka rangi na kutoa machozi ya damu, kitu kilichozidi kuwatisha Ashura na mwanaume wake. “Hapana Balkis huna sifa hiyo wewe ni mpole nimekuita hapa kwa makusudi ya kuwaeleza hawa wanadamu ubaya wao mbele yako.” Mganga Njiwa Manga alisema huku akimshika kichwani na kumpigapiga taratibu kumpunguza hasira. Balkis alitikisa kichwa kuonesha amekubali. “Balkis.””Abee.” “Nataka uniambie unataka nini wafanye hawa wanadamu wajue wewe si adui yao?””Wanajua wenyewe, nilizungumza nao nini,” Balkis alijibu kwa sauti tamu kama kinanda. “Naomba unieleze mbele yao.” “Nikisema mimi nitaonekana muongo, napenda waseme kwa vinywa vyao.” “Eti mlizungumza nini na Balkis?” mzee Njiwa Manga aliwageukia na kuwauliza. “A...ali...nikataza nisimfuate mume wake ambaye ni mtalaka wangu,” Ashura alijibu katika hofu kubwa. “Na kingine?” “Tusimfuatilie maisha yake.” “Mmefanya yote aliyowaeleza?” Wote walibakia kimya wakitazama chini, mganga alimgeukia Balkis na kumuuliza. “Wewe umeona nini?” “Hawa walio mbele yako ni viumbe wabaya kuliko hata nyoka, wamepoteza maisha ya wanaume zaidi ya wanne na Muddy kama nisingemuwahi alikuwa wa tano. Wamekuwa na tabia za kuwatafuta wanaume na huyu mwanamke kujifanya anawapenda sana, kisha
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
anajitambulisha kwa majina tofauti. “Kila mwanaume anamfahamu kwa jina tofauti kama waliokufa kwa ajili yao wakisimamishwa mbele yake watamtaja kwa majina tofauti, Muddy anamtambua kwa jina la Ashura lakini wengine walimtambua kwa majini ya Fatuma, Hilki, Masha. “Lakini jina lake halisi ni Shuuna, kwa utaalamu wako nina imani majina hayo yote umeyaona alipojitambulisha kwako na kujua sababu ya majina hayo?” “Ndiyo,” Mzee Njiwa Manga alijibu kwa sauti ya chini. “Hawa si viumbe wa kuonewa huruma hata mara moja, hebu angalia kila kukicha wamekuwa wakipanga mipango ya kudhulumu mali za watu na kuwatoa roho zao bila hatia kwa kigezo cha uzuri wa Shuuna. Hivi mimi na yeye nani mzuri?” Balkis alinyanyuka na kujigeuza pande zote kuonesha ufundi wa Maulana kumuumba katika umbile la uzani. “Ni wewe Balkis mwana wa mfalme wa chini ya bahari.” “Mbona siui watu kama ninyi? Mtauliza kwa nini nilimuua mganga Chujio, kiburi chake kilimponza. Nilijua mtakwenda kule na kutaka kinga ya kupambana na mimi kama alivyowasaidia kudhulumu na kutoa roho za watu wasio na hatia. Lakini kwa busara zangu nilimuonya na kuonesha kiburi kwake ndicho kilichomponza.
Nilijua mtakwenda kule na kutaka kinga ya kupambana na mimi kama alivyowasaidia kudhulumu na kutoa roho za watu wasio na hatia. Lakini kwa busara zangu nilimuonya na kuonesha kiburi ndicho kilichomponza. SASA ENDELEA... “Nimewaonesha ishara nyingi za vitisho ili wajue mimi si kiumbe wa kawaida ili wachane na mimi, lakini wamekuwa wabishi, kabla ya kuja huku niliwapa onyo zito lakini wamekuwa kama kenge, hawasikii mpaka watoke damu masikioni. “Tena wana bahati kubwa leo ningepata dhambi nyingine, wakati natoka nyumbani niliwaona wamekaribia kwako lakini kasi yangu ilichelewa kidogo na kuwakuta wameshaingia kwenye ngome yako. “La sivyo kama ningefanikiwa kuwatia mikononi ningewaulia mlangoni kwako na kama ungewasikiliza na kuwapatia tiba kabla tiba yao haijatimia ningemuua mjukuu wako mmoja ili uhalalishe kazi hii na wangetoka ningewamalizia mbali, ” Balkis alisema kwa sauti isiyotaka mzaha, huku kauli yake ikizidi kuwatisha moyoni walioomba msaada wa mzee Njiwa Manga. “Nimekuelewa sana Balkis binti wa mfalme Barami, sasa ulikuwa unataka nini?” “Kama nilivyowaeleza waachane na mimi, waendelee na maisha yao.” “Wakifanya hivyo utakuwa na vita nao?” “Niwe nao ili iwe nini ikiwa kila mmoja na maisha yake, ila tofauti ya hapo nitakachokifanya Mungu anajua.” “Nina imani mmesikia yote aliyosema Balkis, niliwaeleza ni mpole mwenye huruma na upendo kwa viumbe wenzake. Napenda kuwaeleza kuwa maelezo yake ndiyo tiba yenu na mkitoka hapa mkienda kinyume na haya aliyosema, nisione mtu hapa, mtamalizana wenyewe, mmenisikia?” Alijibu kwa kunyanyua vichwa kwani hata midomo ilikuwa mizito, baada ya majibu yao ya kibubu mzee Njiwa Manga alimgeukia Balkis. “Nina imani wamekuelewa ila wakienda kinyume mimi simo.” “Wewe unasema hivyo lakini mioyo yao imejaa tamaa ya mali na uhai wa watu, narudia tena sitawaua ila nitawaadhiri mbele za watu, hilo litakuwa pigo kubwa na mkizidi nitawageuza mbwa.” “Nimekuelewa sana Balkis unaweza kwenda,” mzee Njiwa Manga alisema. Baada ya kuruhusiwa kutoka alinyanyuka na kutoka chumbani katika umbile la kibinadamu, wote walimsindikiza kwa macho hadi nje. Waliokuwa wamekaa nje kusubiri huduma macho yao yalishuhudia mwanamke mzuri akipita mbele yao huku wakijiuliza amepita saa ngapi kutokana na watu wengine kuwepo kwa muda mrefu. Balkis baada ya kutoka katika uzio wenye nguvu wa mzee Njiwa Manga alitoweka. Baada ya kuondoka Balkis, mzee Njiwa Manga aliwageukia wateja wake na kusema: “Nina imani tatizo lenu limekwisha?” “Mzee litakwisha vipi wakati umemsikia mwenyewe amesema nini,” Tonny alihoji. “Kasema nini?” “Si amesema tukifuatilia mambo yake atatugeuza mbwa,” Ashura alijibu. “Sasa mnataka kufuatilia mambo yake?” “Hapana.” “Sasa tatizo nini?” “Tulikuwa tunaomba kinga.” Tonny alisema. “Ya nini?” “Ili tujikinge na matatizo ya wanadamu na majini.” “Ili?” “Mzee kama hujui kazi yako, kwani wanadamu wanakuja kwako kutafuta nini?” “Tiba ya matatizo yao.” “Sasa mbona hutaki kutusaidia?” “Kwani shida yenu iliyowaleta hapa ni nini?” “Kuzuia nguvu za jini Balkis.” “Sasa niwape kinga ya nini?” “Anaweza kutugeuka na kutufanyia kitu kibaya.” “Hawezi na sina tiba yoyote labda muwe na tatizo lingine.” “Hatuna, ni hili hili la huyu mwanamke ndilo linalotutisha, unamuona kwa macho tu lakini ni kiumbe kibaya sana.” “Yule hana ubaya kama nilivyowaeleza, lakini mioyoni mwenu mna dhamira mbaya naye, kwa hilo mimi halinihusu kama mnataka ushindani dawa hiyo sina.” “Kwa hiyo huna msaada wowote kwetu?” Tonny aliuliza. “Msaada niliowapa ni mkubwa kuliko kukuchanjeni au niwape dawa ya kufukiza.” “Mzee msaada gani uliotupa zaidi ya kutuacha njia panda?” Tonny alizidi kuhoji. “Msaada niliowapa hamuujui lakini ni mkubwa sana, najua mmezunguka kwa waganga wengi kwa kazi zenu za dhuluma. Hamkuwahi kukutana na tatizo kisha mkatibiwa bila kunywa, kujifusha au kuchanjwa dawa? Mliyekuwa mnamuona adui ameeleza hataki kitu gani, sasa mnataka nifanye nini?” ”Basi inatosha inawezekana na wewe umemuogopa,” Tonny alisema kuonesha alitaka zaidi ya yale aliyoelezwa. “Kweli nimemuogopa nipo kwa ajili ya kutibu si kujiingiza kwenye matatizo ya kujitakia, kutokana na maelezo yake nilikuwa nampoteza mjukuu wangu kwa ajili yetu. Nawaeleza mkikosea kwenda kwa mganga mwingine kitakachowakuta hamtakisahau mpaka mnakufa.” “Tumeelewa.” Tonny alijibu kwa shingo upande. “Basi mnaweza kwenda ili niendelee na wenzenu.” “Sasa mzee tukupe kiasi gani?” “Nina imani hamkuona nilichokifanya, nendeni msitoe kitu chochote.” “Hapana mzee hata ya kuangalizia, sijui elfu moja?” “Hapana nimewasamehe kila kitu.” Walitoka huku wakiamini mzee Njiwa Manga uwezo wa kutibu umepungua ndiyo sababu ya kushindwa kuwasaidia kupambana na Balkis.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment