Simulizi : Bahari Ya Hindi
Sehemu Ya Tatu (3)
Piaa madhari ya nyumba hiyo ikabadilika na kuonekana ni ndani ya nyumba ambayo imechakaa kupita kiasi..yani kama nyumba ambayo imetelekezwa miaka mingi bila kuishi mtu ndani yake....Roda akaingiwa na hofu akatamani kupiga kelele lakini alishindwa!!
Tobi akasema..mimi ninamiaka zaidi ya mia moja(100)tangu nizaliwe..lakini ninaishi katika umbile la binadamu wa kawaida tangu miaka arobaini iliyopita...
Roda alishtuka kusikia maneno hayo aliyoyaongea Tobi.
Roda akauliza kwa mshangao!!! ,,"inamaana miaka hiyo yote tuliyokuwa tunafanya kazi pamoja ulikuwa ni jini katika umbile la binadamu?
Roda aliongea maneno hayo huku akimtazama Tobi kwa macho ya uwoga! mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi zaidi.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tobi akajibu,,"ndiyo ni kweli kabisa hayo usemayo.
Roda akageuza shingo yake kutazama huku na kule ili atimue mbio..lakini alishindwa hakuweza kuona sehemu ya kukimbilia...kwa sababu kila kona palionekana kutisha sana. punde si punde Tobi akanyoosha mkono wake,,ghafla muonekano wa nyumba hiyo ukabadilika..pakaonekana ni ndani ya jumba la kifahari..pia Tobi akajibafilisha na kuonekana muonekano wake wa kawaida!
macho yakamtoka Roda! nisu atimue mbio..
Tobi akasema..usiogope,,wala usikimbie kwa sababu hakuna sehemu ambayo utakimbilia.
naomba unisikilize kwa makini, kuna jambo ambalo nataka nikueleze ujue..
Tobi akaanza kusimulia..
Ilikuwa hivi....Siku moja majira ya saa kumi jioni, ulikuwa na marafiki zako Coco beach..ukaingia bafuni kwenda kubadilisha mavazi...wakati unatika bafuni,,uliokota mkufu, ukauvaa mkufu huo wa dhahabu shingoni mwako,,ukaingia baharini kuogelea...mkufu huo ulikuwa ni mtego ambao Mama yangu Malkia wa Bahari aliutegesha..ili mimi niweze kurudi duniani na kuishi kama wanavyoishi binadamu wengine,,hii ni baada ya mimi kuuwawa na Binadamu aliyekuwa ni Mchungaji..
wakati nipo kwenye mawindo yangu ya kutafuta chakula(Damu) mchungaji huyo aliniona akaniangamiza kwa maombi..nikafa na kurudi ujinini nikawa sina uwezo tena wa kurudi kuishi maisha ya Duniani..Mama yangu akatumia mkufu huo wa Dhahabu kuutegesha,,ili mtu yeyote atakayeuokota mkufu huo na kuuvaa shingoni mwake,,, mimi nitaweza kutoka ujinini na kuishi maisha ya Duniani...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
lakini wewe ulipouokota mkufu huo na kuuvaa,,nikatokea kukupenda sana,, nikalazimika kukufatilia kila sehemu unakokwenda,, nikapajua kazini kwako..nikaja kuomba kazi ili tufanye kazi pamoja na kutengeneza ukaribu zaidi...
nimekuwa nikishirikiana nawe kimwili kila nilipokuhitaji..pasipo wewe kujua...mara nyingi nilikuwa nakutokea usiku ukiwa usingizini,,lakini wewe ulikuwa ukiamini ni ndoto...La! hasha haikuwa ndoto, bali mambo hayo yalitendeka kweli....na nilikufunga kimiujiza ili usipendwe na mwanaume yeyote wala usimfikirie mwanaume mwingine zaidi ya mimi kuwa karibu yako kikazi.
macho yalimtoka Roda akadakia,,"kwa nini ulinifanyia hayo yote?
Tobi akasema,,"ni kwa sababu nakupenda sana.
Roda akauliza kwa mshangao,,"UNANIPENDA!!!?
nitawezaje kuwa na mpenzi jini?
Tobi akacheka kwa sekunde kadhaa kisha akajibu,"inawezekana na ndio maana nimekuwa na mahusiano na wewe kwa miaka mingi pasipo wewe kujua,, nilitamani ujue lakini ungeniogopa na ndio maana nikafanya iwe siri yangu.
**********************
Roda akasema,,"naomba kurudi nyumbani kwangu tafadhali..kama kweli unanipenda naomba ufanye jambo hilo..
Tobi akasema,,"hilo tu ondoa shaka lakini inabidi utimize masharti yafuatayo..
kabla Tobi hajaanza kueleza masharti hayo..ghafla akaonekana yule Bibi kizee akiingia ndani ya jumba hilo la kifahari..
Roda akaingiwa na hofu akasema,,"tafadhali nawaomba msinidhuru..nitafanya chochote mtakachokitaka..
bibi kizee huyo(Malkia wa Bahari) ambaye ni mama mzazi wa Tobi akaongea maneno yaliyofanan na lugha ya kiarabu akimaanisha,"hakuna atakaye kudhuru,,lakini kuna kosa kubwa ambalo umelifanya,,na siku ya leo ndiyo imgekuwa mwisho wa uhai wako..umenusurika kwa sababu wewe ni chaguo la mwanangu wa pekee..amekuchagua ili akuoe..
Roda akashtuka sana kusikia maneno hayo..pia alistaajabu ameweza kuelewa maneno aliyoyaongea bibi kizee huyo bila kujifunza lugha hiyo.
Bibi huyo akazipiga hatua na kupita kwenye mlango bila mlango huo kufunguliwa!!
Roda akauliza kwa mshangao! ,," unamaanisha kunioa niwe mke wako?? na itawezekana vipi wakati wewe si binadamu bali ni jini!
Tobi akajibu,,"inawezekana hakuna tatizo kabisa.
Roda akatumia ujanja akakubali ili Tobi asimdhuru
lakini akilini mwake alikuwa makini sana,,huku macho yake yakimtazama Tobi muda wote..
**********************
upande mwimgine kule nje ya bahari(nchi kavu) palionekana ni mchana wa saa saba hivi.
lakini kule chini ya bahari (ujinini) palionekana ni usiku wa manane,,masaa ya huko ni tofauti na masaa ya duniani...hivyo wakati binadamu wamelala usiku..Majini hutumia muda huo kufanya shughuri zao za kutafuta chakula(damu)
kwa sababa kwa masaa ya ujinini inakuwa ni nyakati za mchana..
Tobi akasema,,"nifuate,,aliongea hivyo huku akizipiga hatua kukifuata chumba kimojawapo kati ya vyumba vilivyokuwemo ndani ya jumba hilo la kifahari.
Roda akamfuata Tobi kwa nyuma hukua akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa,,wakaingia ndani ya chumba hicho kilikuwa kinanukia marashi,,
Tobi akasema,,"Penzi la kweli halifi,,likifa haliozi,,na kama likioza harufu yake hupendeza
Roda akauliza ,,"unamaanisha nini?
Tobi akamsogelea Roda akambeba na kumlaza kitandani...
Roda alikuwa makini sana kutazama Tobi anataka kufanya nini?
********************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Roda akauliza swali la kimitego ili ajue namna ya kutoka huko ujinini kurudi duniani.
Tobi akajibu..inawezekana lakink ni lazima kuzingatia masharti..
Roda akauliza kwa kudadisi zaidi,,"masharti gani hayo? sasa hivi Roda aliuliza huku akitabasamu kumtega Tobi atoboe siri.
Kama ilivyo kawaida mapenzi yana nguvu kuliko kitu chochote..Tobi akajikuta anaelezea siri ambayo haitakiwi binadamu yoyote wa kawaida ajue.
Tobi akasema,,"ni lazima uvae pete maalumu..kisha akanyanyuka na kufungua droo akatoa pete iliyokuwa na jiwe la RUBI NYEKUNDU
akasema,,"pete hii itamfanya binadamu wa kawaida atoke ujinini na kurudi Duniani ndani ya sekunde moja...naomba usiniogope sasa hivi sipo katika hali ya ujini mpaka nitakapokunywa damu ya mtoto mchanga..mimi ni yule Tobi uliyemzoea siku zote. kwa hiyo usiku wa leo tutalala wote kama binadamu wa kawaida kabisa..tafadhali usiniogope..
Roda akamuita Tobi kitandani huku akitabasamu,,Tobi alikuja haraka,.akamkumbatia ..kisha akasema,,"tafadhali Tobi naomba tusifanye chochote usiku huu...na ninaomba uniahidi kuwa autanifanya chochote!
Tobi akakubali kwa sababu alikuwa anampenda sana Roda..wakalala usingizi bila kugusana..
Roda hakuweza kulata usingizi..akili yake yote ilikuwa inawaza juu ya pete ile aliyo onyeshwa na Tobi..
Baada ya lisaa limoja kupita...wazo likamjia Roda akamtazama Tobi akamuona kalala usingizi mzito! Roda akanyanyuka kitandani taratibu,,akazipiga hatua za kunyatia akafungua droo na kuichukua ile pete ili aivae,aweze kutoroka na kurudi Duniani. ghafla yule bibi kizee (malkia wa bahari) akajitokeza..
Roda akaivaa pete hiyo harakaharaka..punde si punde akatoweka!! ni kitendo cha sekunde moja akajikuta yupo ufukweni mwa bahari..akastaajabu kuona miamba mikubwa na miti mingi midago midogo!! akapanda juu ya miamba na kuanza kutafuta njia...lakini kila akitazama huku na kule..aliona kazungukwa na miti..Roda akaanza kuingiwa na wasiwasi akajisemea moyoni,,"hapa ni wapi? mbona hapaoneshi dalili ya mtu yeyote kuwahi kufika eneo hili!!
Sehemu hiyo palionekana kutisha sana,,zilisikika sauti za ndege warukao...na ngurumo za upepo uvumao kwa kasi..
Roda akaingiwa na hofu kubwa...
*********************
Upande mwingine kule chini ya bahari,,alionekana Tobi akiandaa mikakati ya kwenda kumnasa Roda amrudishe kwenye himaya yake..
Yule bibi kizee (Malkia wa bahari) ambaye ni mama mzazi na Tobi..akaamua kumuamuru jini mmoja aende duniani..akalete damu ya mtoto mchanga aliyezaliwa dakika hiyohiyo ili Tobi anywe aweze kurudi katika hali ya ujini...arudi duniani kwenda kumtafuta Roda.
****************
upande mwingine kule Duniani lilionekana gari la wagonjwa(ambulance) likiingia ndani ya geti la Hospitali ya Muhimbili..gari hilo lilikuwa limebeba mama mjamzito..ambaye alikuwa ametimiza siku ziku ya kujifungua(kuzaa) manesi walimpokea mama hiyo harakaharaka na kumkimbiza kwenye chumba cha uzalishaji. mama huyo alijaribu kusukuma mtoto lakini ikashindikana....alitumia nguvu nyingi sana..akaishiwa nguvu akapoteza fahamu....
madaktari wakaamua kumpeleka haraka kwenye chumba cha upasuaji ili wamfanyie upasuaji wanusuru maisha ya mtoto...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ni kitendo cha sekunde kadhaa upasuaji ukaanza.
apunde si punde akajitokeza mwanamke mmoja aliyevalia mavazi ya kidaktari huku kafunika pua na mdomo wake kwa kifaa maalumu wanachokivaa madaktari na manesi kwa ajili ya kutokuvuta hewa chafu wakati wa ulasuaji.
mwanamke huyo akazipiga hatua hatua kadhaa akafungua mlango wa chumba cha uoasuaji akaingia upande wa ndani...wale madaktari waliokuwemo ndani ya chumba hicho wakashtuka..wakashangaa ni nani kaingia humo wakati upasuaji unaendelea!!
yule mwanamke hakuongea neno lolote akakifuata kitanda maalumu kwa ajili ya upasuaji..akaanza kushirikiana na madaktari hao...mwanamke huyo kumbe ni yule jini aliyetumwa akalete damu ya mtoto mchanga aliyezaliwa dakika hiyohiyo..
mwanamke huyo akazibadilisha akili za madaktari..wakajikuta wanamkata mtoto kwenye shingo pasipo wao kujitambua..
damu nyingi zikaanza kutoka shingoni mwa mtoto huyo mchanga hatimae akafa...yule mwanamke jini..akaitazama damu hiyo ghafla damu hiyo ikatoweka....
punde si punde mwanamke huyo naye akatoweka kimiujiza na kurudi ujinini..
Ghafla akili za madaktari zikarudi katika hali ya kawaida...wakastaajabu kuona mtoto huyo kakatwa shingoni na ameshapoteza uhai..wakamtoa haraka tumboni na kuanza kuishona ile sehemu iliyopasuliwa ya mama wa mtoto huyo...
madaktari walisikitika sana...tangu waanze kufanya upasuaji hawajawahi kufanya upasuaji wakamkata mtoto!!
Baada ya lisaa limoja kupita..mama huyo alipata fahamu akawa na shauku ya kutaka kumuona mwanae...akauliza,,"mtoti wangu yuko wapi??
nesi akasema,,"pole sana dada nasikitika kukwambia kuwa mtoto kafariki wakati unafanyiwa upasuaji.
Yule mama akapata mshtuko wa moyo.. akapoteza fahamu...madaktari walijitahidi kumfanyia huduma ya kwanza lakini ilishindikana..tayari alikuwa amepoteza maisha dakika chache zilizopita..
************************
Upande mwingine,,kule chini ya bahari ,alionekana
Tobi akinywa damu..
damu hiyo ni ya yule mtoto mchanga aliye uwawa kule hospitali, dakika chache zilizopita.
Tobi alipomaliza kunywa damu hiyo akapata uwezo wa kurudi Duniani..akafumba macho yake akagundua ni wapi Roda alipo!!!,,akatabasamu..ghafla akatoweka kimiujiza
Wakati huo huo alionekana Roda akiendelea kutimua mbio,,alikimbia bila kujua ni wapi aendako...
Baada ya lisaa limoja kupita akatokezea kwenye barabara,,,akaanza kupata amani...akazipifa hatua za harakaharaka huku macho yake yakitazama huku na kule..
Kwa mbali akaona gari limeegeshwa!! akaamua kulifuata gari hilo,,alipolikaribia akamuona mwanaume mmoja kafungua boneti analitengeneza gari hilo....Roda akamuongelesha mwanaume huyo...,,"habari yako kaka!!
mwanaume huyo hakujibu kitu chochote aliendelea kulitengeneza gari lake!
Roda hakuweza kuona sura ya mwanaume huyo kwa sababu alikuwa ameinamisha uso wake...
Roda akasema,,"kaka nakusalimia...
mwanaume huyo akageuza shingo yake,, na kumtazama Roda..
Roda akashtuka akaanza kutimua mbio...
Nibaada ya kumuona mtu huyo anafanana na Tobi kwa kila kitu..kuanzia sura mpaka mavazi!!
Roda alikimbia huku analia...
baada ya kukimbia umbali mrefu..akahisi kuchoka akaamua kutembea.....akaanza kuhisi njaa kali,,akiangaza macho yake huku na kule hakuina mtu hata mmoja kwenye barabara hiyo.....wasiwasi na hofu ikazidi kuongezeka!!
akajikuta ametokezea kwenye makazi ya watu..akastaajabu baada ya kuona shamlashamla za watu wakisherehekea mwaka mpya!! Roda akamfuata mtu mmoja akauliza,,"samahani dada,,nauliza eti haya ni maeneo gani?yule mwanamke akajibu..hapa ni kisiwani mpakani mwa Unguja na Pemba..
Roda akashtuka sana,,akauliza tena,,"kwani kuna sherehe gani inaendea??
yule mwanamke akashtuka akamtazama Roda kwa macho ya mshangao..akamuuliza,,"inamaana haujui kuwa leo ni mwaka mpya?CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Roda akasema,"mwakampya kivipi?..mbona huu ni mwezi wa sita(6) !!
yule mwanamke akasema leo ni tarehe 1/1/2017
Roda akashtuka!...akajisemea moyoni inamaana tangu mwaka 2007??? ghafla kumbukumbu ikamjia akakumbuka Tobi alimwambia kuwa siku moja ya kule ujinini ni miaka kumi ya Duniani!!
Roda akaingiwa na uwoga...kwa mbali akaona machinga anatembeza vioo vya kujitazama...akamfuata machinga huyo..akachukua kioo na kujitazama uso wake...akashtuka kuona uso wake unaonekana kama mama wa makamo kiasi!!! Roda akazidi kuogopa zaidi...akarudi kwa yule mwanamke..kisha akasemaa,,"mimi nimepotea...na wenzangu wote wamekufa baharini..baada ya meli tuliyokuwa tumepanda kuzama baharini...mimi niliogelea nikabahatika kufika nchi kavu..Roda aliongeaaneno hayo..yaliyokuwa na ukweli pamoja na uwongo kiasi ndani yake!!!
mwanamke huyo akasema,,"pole sana kwa majanga yaliyokupata..nitakusaidia kukupa sehemu ya kujihifadhi wakati unafanya mipango ya kurudi nyumbani kwenu..
Roda akafurahi sana kupata msaada...
mwanamke huyo alikuwa anauza bidhaa ndani ya duka lake...lakini alionekana kumtazama Roda kwa macho ya msisitizo!!!
Roda hakulitambua hilo...mwanamke huyo akasema,,"itabidi ukae hapa mapaka nitakapofunga duka tuelekee nyumbani kwangu.
Roda akasema,,"sawa dada hakuna tatizo nakusikiliza wewe.
yule mwanamke akauliza,,"umekula?
Roda akajibu,,"hapana sijala nahisi njaa kali..
wakati huo Roda alikuwa nje ya duka hilo kasimama...
Mwanamke huyo alikuwa upande wa ndani ya duka akainama..alipoinuka akawa ameshikilia sahani yenye chakula...ilikuwa ni Chipsi kuku..
Roda alipokea chakula hicho akaanza kula...
lakini mwanamke huyo aliendelea kumtazama Roda kwa macho ya msisitizo...kisha akatabasamu..
Roda alikishambulia chakula hicho mdani ya dakika tano tu..sahani ikawa tupu..akasema,,"asante sana dada yangu kwa msaada wa chakula.
*************************
Upande mwingine alionekana Tobi akijitokeza barabarani,,barabara hiyo ilikuwa tulivu...haikuonekana hata gari moja kupita kwenye barabara hiyo!!!akazipiga hatua kadhanaa akatoka kwenye barabara hiyo...akasimama kando kabisa.akanyoosha mkono wake..ghafla ikajitokeza ya nyumba moja iliyozungushiwa uzio akatoweka kimiujiza na kujitokeza mdani ya nyumba hiyo...
************************
ilipofika majira ya saa kumi na moja za jioni..yule mwanamke akafunga Duka..
Roda akajisemea moyoni,,"eneo hili hakuna biashara kabisa..yani tangu nimekaa hapa masaa yote hayo,sijaona mtu hata mmoja akija kununua hata kiberiti..mmh!!!
Yule mwanamke alipomaliza kufunga milango ya duka lake akasema,,"tuondoke twende nyumbani.
Roda akaongozana na mwanamke huyo..walitembea mwendo wa dakika saba,,hatimae wakafika nyumbani kwa mwanamke huyo..akatoa ufunguo kwenye pochi yake akafungua geti....wakaingia ndani ya uzio wakazipiga hatua kuufuata mlango wa kuingia ndani ya nyumba....akafungua mlango wakaingia ndani...akamkaribisha Roda,na kusema,"hapa ndio nyumbani kwangu...naishi na kaka yangu...nahisi atakuwa amelala wacha nimuamshe ili nimtambulishe kwako...
Roda akatabasam,,kisha akasema,,"sawa hakuna shaka..
Mwanamke huyo akazipiga hatua kuifuata korido ya kuelekea kwenye vyumba vya kulala ili amuamshe kaka yake akamtambulishe kwa Roda..
Punde si punde akaonekana mwanamke huyo akija sebuleni huku kaongozana na Tobi...
Roda alipogeuza shingo yake akashtuka kumuona Tobi..ghafla nyumba hiyo ikabadilika.....na yule mwanamke pia akabadilika akawa ni ye bibi kizee(malkia wa bahari) ambaye nia yake Tobi!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment