Simulizi : Shamba La Urithi
Sehemu Ya Tatu (3)
siku ya leo Pamera alidamka asubuhi na kuelekea shambani..akavune mahindi ili apeleke kwenye mashine ya kusaga unga..wajipatie unga wa kupikia ugali na uji....akaingia shambani na kuanza kuvuna mahindi akiyaweka kwenye gunia...
wakati huu huu..alionekana Jazi akiikokota baiskeli yake..kuipeleka kwa fundi kwenye kijiji cha jirani...akapitia njia ya bondeni....njia hiyo inapita kando ya lile shamba!! akashtika kuona shamba hilo limeenea mahindi na maharage!
macho yakamtoka akajisemea moyoni,,"ni siku nne(4) zimepita tangu nivune...na shamba lilibaki halina kitu chochote!! iweje lei mahindi na maharage yanaonekana!!! ghafla akamuona Pamera anatokea ndani ya shamba hilo huku akivuruta gunia lililokuwa na mahindi ndani yake..
Jazi akaanza kuingiwa na hofu..akaamua kurudi haraka nyumbani kwake ili akayatazame yale magunia yaahindi aliyovuna siku nne zilizopita.
Baada ya mwendo wa dakika kadhaa,,Jazi alifika nyumbani kwake akapitiliza moja kwa moja mpaka kwenye ghala...akafungua mlango....akashtuka kukuta ghala lipo tupu...hakuna gunia hata moja!
Jazi akahisi kuchanganyikiwa...akatimua mbio bila kujua ni wapi anakoelekea!!!
Upande mwingine alionekana Kabi akiwa kando ya mto unaopita katikati ya korongo..akiwa amepoteza fahamu...
akazinduka na fahamu zikarejea..akanyanyuka taratibu akazipiga hatua kutoka kwenye korongo hilo..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakati huo huo walionekana wadogo zake Pamera,,wakiwa barabarani wakizipiga hatua...mdogo wao wa mwisho akahisi kupatwa na kizungu zungu..akadondoka chini na kupoteza fahamu!!!!
watoto hao wanne wakaingiwa na hofu,,kumuona mdogo wao kadondoka chini!!! wakaanza kulia wakidhani amekufa! ....
kutokana na uwoga na akili za kitoto wakaamua kutimua mbio na kutokomea kusikojulikana..wakamuacha mdogo wao pale chini barabarani akiwa amepoteza fahamu...wenyewe hawakulitambua hilo walijua amekufa....
*************************
Kule gerezani,alionekana Pamera akiwa ameketi kwenye sakafu huku amejishika tama,,ndani ya sero,maalumu kwa wanawake...Pamera alikuwa akiwafikiria wadogo zake..hali hiyo ilimfanya akose raha,,akajikuta analia kwa uchungu..
wanawake walioshindikana waliofungwa kwenye sero moja na Pameta walimnyanyasa kwa kumfanyisha kazi mbali mbali kama kiwakata kucha..kuwafulia nguo na manyanyaso mengi ya kinyama.....Pamera hakuweza kushindana nao kwa sababu alikuwa ni binti mdogo kuliko wafungwa wote...ni yeye pekee aliyekuwa na umri wa miaka kumi na tisa(19)
***********************
Upande mwingine kule kwenye korongo,,alionekana Kabi akinyanyuka kutoka pale chini alipodondoka..ni baada ya kusombwa na maji ya mto..na kutupwa kwenue korongo.....Kabi akazipiga hatua,,,akahisi maumivu makali akajishika kichwani ile sehemu aliyojigonga kwenye jiwe! akazipiga hatua za garaka haraka kuelekea nyumbani....
alitembea mwendo wa dakika kadhaa akawa amefika nyumbani..akashtuka kuiona nyumba aliyokuwa anaishi yeye na wadogo zake imeteketea kwa moto! akatimua mbio akaingia ndani ya nyumba hiyo..akaangaza angaza macho yake kila pande ndani ya nyumba hiyo...macho yakamtoka!! hakikusalia kitu hata kimoja...vitu vyote viliteketea kwa moto! Kabi akajikuta anadondosha machozi..akalia kwa uchungu.akiamini kuwa dada yake Pamera,,pamoja na wadogo zao wamekufa na kuteketea kwa moto...Kabi akajikuta anakata tamaa ya kuendelea kuishi katika kijiji hicho...akaamua kutoka nje ya nyumba hiyo iliyoteketea kwa moto...akazipiga hatua kadhaa akageuza shingo yake,akasema,,"Jamani ndugu zangu mmekufa na kuniacha peke yangu! ni bora tungekufa wote...tazama nimebaki mpweke,,nitakuwa mgeni wa nani mimi!!! Kabi aliongea maneno hayo huku akilia kwa uchungu..akanyoosha mkono wake akapunga mkono ishara ya kuwaaga wadogo zake...akazipiga hatua huku kaweka mikono yake kichwani akilia kwa sauti...Kabi akaamua kihama kijijini hapo na kuelekea mjini...akatafute vibarua..na kuanzisha maisha mapya akijisimamia yeye mwenyewe kwa kila kitu!
******************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande mwingine kule barabarani,,alionekana mdodo wake Pamera...ni yule mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya watoto saba....mtoto huyo alikuwa bado kalala barabarani huku akiwa katika hali ya kutokuwa na ufahamu,,jua lilikuwa kali sana liliwaka kama moto...
kwa mbali likaonekana gari aina ya TOYOTA PICKUP,,gari hilo lilikuwa na vioovyenye rangi nyeusi(Tinted) limebeba mikungu ya ndizi..likija upande huo huo...dereva wa gari hilo alikuwa na mkewe ndani ya gari...walikuwa wametoka kwenye shamba lao la migomba kukata mikungu ya ndizi..kwa ajili ya bihashara..watu hao mume na mke walikuwa wanaishi mjini....
walipokaribia kwenye eneo alilokuwa amedondoka mdogo wake Pamera.....wakamuona mtoto huyo..
wakaingiwa na roho ya huruma..dereva huyo akasimamisha gari na kushuka kutoka ndani ya gari hilo..akazipiga hatua kumsogelea mtoto hiyo...alipomtazama kwa makini akagindua kiwa bado yupo hai..huenda njaa ndio inamsumbua!! alipojaribu kumuamsha mtoto huyo hakuamka mwili wake ulikiwa na joto kali kupita kiasi..akambeba na kumuingiza ndani ya gari upande wa mbele..
mkewe akasema,,"bila shaka mtoto huyu amepatwa na maradhi..tumuwahishe hospitali.
Mumewe akaliwasha gari na safari ikaendelea..
**********************
kwa mbali akaonekana kijana mdogo akinyoosha mkono ishara ya kulisimamisha gari hilo..dereva wa gari hilo akaamua kusimamisha gari ili amsikilize kijana huyo anashida gani?
akafungua kioo nm cha upande wake....akauliza,,"unasemaje kijana..
kumbe ni Kabi ndiye aliyesimamisha gari hilo...Kabi akamsalimia dereva huyo kisha akasema,,"samahani kama unaelekea mjini naomba msaada wa kunisogeza mimi sina nauli..tafadhali naomba msaada wako..dereva huyo akakubali ombi la Kabi,,kisha akasema,,"panda huko nyuma..shikilia kwa nguvu.....kwa sababu ninaendesha gari kwa kasi kuna mgonjwa namuwahisha hospitali..
Kabi akashukuru kisha akapanda kwenye gari..hakujua kuwa mdogo wake ndiye anayewahishwa hospitali..hakuweza kumuona mdogo wake mule ndani ya gari kwa sababu gari hilo lilikuwa na vioo vyenye rangi nyeusi(Tinted)
Safari iliendelea hatimae wakafikajini..dereva huyo akasimamisha gari akafungua mlango akashuka kutoka ndani ya gari akamwambia Kabi,,,"Kijana hapa ndio mjini,,mimi nakatisha nji hii..kwani wewe unakwenda maeneo gani??
Kabi akasema,,"mimi nashuka hapa hapa nashukuru sana kwa msaada wako. Mungu akubariki..Kabi aliongea maneno hayo huku akishua kutoka kule nyuma ya gari
Dereva huyo akaingia ndani ya gari na kuliwasha..akaendelea na safari ya kuelekea hospitali..
wakati dereva huyo anafungua mlango na kuingia ndani ya gari..Kabi akahisi kama kamuona Mtoto anafanana na mdogo wake..lakini akawa ameshachelewa gari lilikuwa limeshaondoka...
Kabi akatimua mbio,,kulikimbiza gari hilo huku akisema,,"tafadhali simamisha gari..huyo ni mdogo wangu..alijitahidi kukimbia kwa nguvu zake zote lakini alishindwa kulipata gari hilo..akakata tamaa akasimama,akabaki kajishika kichwa...alilitazama gari hilo likizidi kutokomea kabisa..machozi yakamlenga machoni akajikuta analia ksa uchungu pasipokutarajia...,,"nitakuona wapi tena mdogo wangu!?
wazo likamjia akajissmea moyoni,,"lakini ninawasiwasi huenda sio yeye..kwa sababu ndugu zangu waliteketea na moto ndani ya nyumba..bila shaka nimemfananisha..
Kabi akajipa matumani kuwa amemfananisha si mdogo wake...
***********************
Kule gerezani,walionekana wafungwa wakiwa wamesimama kwenye mstari mmoja,,mikono yao ilikuwa imeshikilia sahani na kikombe...akaonekana Pamera amesimama huku machozi yanamlenga machoni....ilipofika zamu yake akakingac sahani na kuwekewa chakula...akazipiga hatua akajitenga peke yake akaanza kula chakula hicho...Pamera alikula lakini mawazo yake yote yalikuwa kwa wadogo zake,,"sijui watakuwa wapi muda huu!!? Eee Mungu mbona napitia mitihani mizito kuliko umri wangu?
naomba uniongoze ,,uniepushe na mabaya yote..walinde wadogo zangu huko waliko...
wakati Pamera akiwa katika dimbwi zito la mawazo...wakaonekana wanawake wawili miongoni mwa wafungwa katika gereza hilo la wanawake....wakimfuata Pamera..walipomkaribia wakamnyang'anya chakula,,wakamimina chamula hicho kwenye sahani zao..kisha wakaitupa chini sahani ya Pamera ikiwa tupu Pamera akalia kwa uchungu...huku akisema,,"manyanyaso yamezidi naishi bila amani,firaha yangu iko wapi??
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kumbe wakati Pamera anafanyiwa manyanyaso hayo..kuna mfungwa mmoja alikuwa anashuhudia..akanyanyuka na kumfuata Pamera..alipomkaribia akasema,,"pole sana mdogo wangu kwa unyama waliokufanyia...lakini usivunjike moyo...daima uwe unamkumbuka Mungu popo ulipo..na kwa chochote unachokifanya...mimi nipo hapa kwa kipindi cha miaka ishirini iliyopita..nimebakiza miaka miwili kifumgo changu kiishe,,ili niwe huru....sijapenda kufungwa..wala sijapenda kuishi hapa gerezani.
mimi nilisingiziwa kwa kuhusisha na vitendo vya unyang'anyi wa kutumia silaha.lakini ukwrli ni kwamba sikuwahi kufanya jambo hilo...bali ni chuki,,wivu na roho mbaya za binadaamu wenzetu.....ndio maana unaniona nipo hapa.
Pamera alimtazama mwanamke huyo kwa macho ya huruma...kisha akasema,,"pole sana dada yangu.....mimi pia nimefumgwa kwa kosa la kuuwa..lakini si kwa kukusudia..nilikuwa kwenye jitihada za kunusuru maisha ya mdogo wangu aliyenusurika kuuwawa na baba yetu mkubwa...
Pamera akajikuta anashindwa kundelea kusimulia mkasa wake...akaanza kulia..
Mwanamke huyo akamuhurumia Pamera akasema,,"hiki ni chakula changu naomba tule wote..Pamera akasema,,"asante sana,,Mungu kakujalia Roho ya utu..
wakaanza kula huku wakiulizana maswali mbali mbali..wakajikuta wametengeneza urafiki wa karibu zadi...
************************
Upande mwingine walionekana wale watoto wanne .ambao ni wadogo zake Pamera,,wakiwa wakeketi chini ya mti wanalia...wakiamini kuwa mdogo wao amekufa!............mtoto mmoja kati ya watoto hao akasema ,,"tuondokeni....nakumbuka
siku moja nilikwenda na baba mjini mpaka nyumbani kwa rafiki yake...
mimi nitakwenda huko kumuomba niishi nyumbani kwake...wale watoto wengine nao wakasemaa kwa pamoja,,"hata mimi pia tutakwenda pamoja...wakazipiga hatua kuifuata barabara inayoelekea mjini...
walitembea mwendo mrefu sana!! jua lilikuwa kali kupita kiasi..njaa kali ikaanza kusumbua matumbo yao...wakahisi kiu...lakini hawakuweza kupata maji.kwa sababu kando barabara hiyo hapakuwa na makizi ya watu!!!
waliendelea kutembea hatimae njaa ikazidi na nguvu zikawaishia...kwa mbali wakaona dimbwi dogo la maji yaliyotuama!! wakaamua kulifuata dimbwi hilo wakaanza kunywa maji hayo....yalikuwa ni machafu ma yanatoa harufu lakini hawakuwa na namna wakachota mji hayo kwa kutumia viganja vyao na kianza kunywa. kisha wakazipiga hatua kuufuata mti mkubwa wakaketi chini ya mti huo uliotengeneza kivuli kwa matawi yaliyokuwa yametanda juu ya mti huo.
walikaa hapo kwa masaa mawili mfululizo wakajikuta wanasinzia....
kutokana na njaa kali waliyokuwa nayo...walilala usingizi mzito.
kwa mbali likaonekana Joka kubwa aina ya chatu likitokea kichakani!....
Chatu huyo akatambaa kuja pale chini ya mti walipokuwa wamejilaza watoto hao..
Mtoto mmoja kati yao,akashtuka kutoka usingizini,,alipogeuza shingo yake akashtuka kuona Joka kubwa likitambaa kuja upande upande waoakakurupuka,akanyanyuka haraka haraka akapaza sauti,,"jamani nyokaaaaa..amkeni..kutokana na sauti kali aliyoipaza mtoto huyo,wenzake wakaisikia sauti hiyo wakashtuka kutoka usingizini,walipoangaza macho yao wakaliona joka hilo limewakaribia..macho ya kawatok wakapiga kelele,,wakanyanyuka haraka na kutimua mbio....kila mmoja alipita njia yake..kuondoka eneo hilo,na kutokomea kusikojulikana...watoto wawili walikimbia pamoja na wale watoto wengine wawili,walikimbia pamoja wakawa wamejitenga makundi mawili......Subira na Konje walikimbia umbali mrefu sana..wakahisi kuchoka wakaamua kupumzika...walipotahamaki wakajikuta wapo peke yao..Subira akasema,,"Jack na Lulu tumewaacha huko..turudi tukawafuate..
bila kuchelewa wakazipiga hatua kurudi kule walipotoka!
**************************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande mwingine,alionekana Jack akiwa na Lulu..wamesimama barabarani huku wanalia...wakaanza kuwaita wenzao...wakapaza sauti kwa kuwataja majina lakini Subira na Konje walikuwa mbali sana,,hawakuweza kusikia sauti za wadogo zao! Jack na Lulu wqkaamua kuifuata barabara hiyo inayoelekea mjini wakatembea umbali mrefu kiasi....wakaona gari limeegeswa kando ya barabara!!!wakaamua kulifuata gari hilo..walipolikaribia wakaangaza angaza macho yao lakini hawakumuona mtu yeyote kuwemo ndani ya gari hilo...walipojaribu kufungua mlango ukafunguka..wakaingia ndani ya gari hilo..wakakuta mkate na juisi..wakaanza kuushambulia mkate huo wakanywa na juisi...hatimae wakamaliza mkate pamoja na juisi...wakahisi kushiba..wakaamua kujilaza kwenye viti vya upande wa nyuma ya gari....
Kumbe dereva wa gari hilo hakuwa mbali na eneo hilo alikuwa anakagua shamba lake,,ni umbali wa mita mia kutoka hapo gari lilipo....
wakati huo huo,,alionekana Subira na Konje wakiendelea kuwatafuta ndugu zao ambao ni wadogo zao...waliwatafuta bila.mafa ikio yoyote,wakakata tamaa! Subira akasema,,"au watakuwa wameifuata barabara hii? twende huenda tukakutana nao huko mbele.
Subira na Konje wakaanza kutimua mbio,walikimbia umbali mrefu kiasi kwa mbali wakaona gari limeegeshwa kando ya barabara wakaamua kulifuata gari hilo kuomba msaada...walipolikaribia hawakuweza kuona dalili za mtu yeyote kuwemo ndani ya gari hilo...Subira akashtuka kuona nguo ya Lulu ikiwa imechomoza nje ya mlango wa gari...akasema,,"Konje tazama,,hii ni nguo ya Lulu!
Sauti ya Subira ilisikika vyema Lulu na Jack waliisikia sauti hiyo wakakurupuka haraka wakachungulia kwenye kioo cha dirisha la gari hilo..wakafurahi kuwaona ndugu zao wakatoka haraka ndani ya gari...wakakumbqtiana kwa furaha....huku wakiulizana hali zao.
Subira na Konje wakasema wanahisi njaa kali..Lulu na Jack wakasema kwa pamoja sisi tumekula tumeokota mkate na juisi.Subira akasema,,"mmeokota wapi??
Lulu akajibu,,"humu ndani ya gari..lakini umeisha!
Subira akafu gua mlango na kuanz kupekua pekua kule upande wa dereva..akaona maembe matano yakiwa chinini ya kiti..bila kuchelewa Subira na Konje wakaanza kuyashambulia maembe hayo...kisha wakaigia ndani ya gari hilo na kujificha chini ya viti vya upande wa nyuma ya gari hilo!!..
punde si punde...akaonekana dereva wa gari hilo akija kwenye gari lake! dereva huyo alionekana kuongea peke yake kama anafoka! akasema,,"yani huyu mzee lazima nimpeleke kwenye sheria..haiwezekani alime ndani ya mpaka wa shamba langu...
derva huyo akafungua mlango wa gari akaingia ndani....kutokana na jazba aliyokuwanayo hakugazama kitu chochote kama kipo sawa..akaliwasha gari lake na kuliondosha kwa kasi kuelekea mjini. baada ya dakika kadhaa akawa amefika mjini! akaliegesha gari lake kando ya barabara akashuka kutoka ndani ya gari,,akazipiga hatua kulifuata duka lililokuwa upande wa pili wa barabara.
watoto hao waliposikia mlango unafunguliwa wakachungulia wakamuona dereva huyo kafika mbali..wakafungua mlango na kutoka ndani ya gari wakatimua mbio.....wakavuka barabara bila kutazama kusho/kulia!! Lulu alikuwa wa mwisho kuvuka..kabla hajavuka akagongwa na pikipiki....
kutokana na uzito mdogo aliokuwanao pikipiki hiyo ilimrusha kando akadondoka na kupotza fahamu...wale watoto wengine wakarudi haraka pale barabarani kumtazama mwenzao...yule dereva wa pikipiki akatimua mbio na kutokomea kusikojulikana kwa kuhofia kuwa ameuwa!
kunamsamalia mwema akajitokeza,,akasema,,"wacha nimuwahishe hospitali..akambeba na kumuingiza ndani ya gari lake...Subira,,Konje na Jack wakaongozana na msamalia huyo mpaka ndani ya gari..na safari ya kuelekea hospitali.ikaanza.
*****************************
upande mwingine,,alionekana yule mtoto ambaya ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia yao Pamera...mtoto huyo alikuwa kalazwa hospitali ni baada ya kuokotwa kule barabarani alipodondoka na kupoteza fahamu..dada zake wajamkimbia wakidhani amekufa.
hali ya mtoto huyu ilizidi kuwa njema baada ya kupatiwa matibabu....daktari akasema mnaweza kwenda nyumbani..
yule dereva pamoja na mkewe,, wakamchukua mtoto huyo na kungozana nae mpaka kwenye gari lao.
Punde si punde lile gari lililombeba Lulu pamoja na ndugu zake..likaonekana likiingia ndani ya hospitali hiyo...
Subira akashtuka kumuona mdogo wao anaingia ndani ya gari..akasema,,"tazameni Mage yule kule...wakachumgulia dirishani wakamuona mdogo wao anaingia ndani ya gari..wakapaza sauti wakimuita mdogo wao,,"MAGEEEEE!!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walimuitadogo wao kwa mfululizo lqkini sauti haikuweza kutpka nje kwa sababu vioo vilikiwa vimefungwa!! walashuhudia gari hilo linaondoka pamoja na mdogo wao Mage!
Subira akamwambia dereva aliyekuwa anqendesha gari walilokuwemo ndani yake,,"tumemuona Mage....dereva huyo akastaajabu hakujua nini kinaendele!! kwa sababu huyo Mage hamjui..pia hamfahamu hata mtoto mmoja miongoni mwao! Subira akajikuta anatokwa na machozi,akajisemea moyoni,,"nitakuona wapi Mage?
msamalia mwema akaegesha gari lake kosha akashuka kitoka ndani ya gari..akambeba Lulu na kumkimbiza ndani kabisa ya hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu..
madaktari wakampa huduma ya kwanza ,,kisha akafanyiwa vipimo vya picha ya mionzi(X-RAY)
lakini picha zikaonyesha hajaumia ndani kwa ndani...
Wakati Lulu anafanyiwa vipimo,,Subira akatoka nje ya hospitali,,akamtazama Mage kule nje huenda lile gari limerudi! akaangaza angaza macho yake lakini hakufanikiwa kuona kile alichokifikiria..akazipiga hatua na kuzunguka nyuma ya hospitali akajiinamia huku machozi yakimtoka..
kule ndani ya hospitali walibali wale watoto wawili wakiwa ndani ya wodi aliyolazwa Lulu....punde si punde Lulu akazinduka na kupata fahamu!! wakafirahi sana kumuona ndugu yao kaamka...
yule msamalia akaanza kuwahoji maswali mbali mbali..wakamueleza kila kitu kilichowatokea..
msamalia huyo akaingiwa na roho ya huruma akasema nitawasaidia mtaishi nyumbani kwangu.
watoto hao wakafurahi sana....punde si punde daktari akaingia..akastaajabu kumkuta Lulu akiwa kama si mtu aliyepata ajali..Uso wa Lulu ulionekana kuchangamka kupita kiasi....daktari akasema,,"unaendeleaje na hali mtoto?
Lulu akasema,,"najisikia vizuri.
Daktari akauliza hujisikii maumivu sehemu yoyote ya mwili wako?
Lulu akajibu,,"hapana.
daktari akasema,,"nyanyuka kutoka hapo kitandani usimame..
Lulu akanyanyuka haraka..akasimama..
Daktari akamwambia yule msamalia,,"inaonyesha hana tatizo lolote...mwaweza kwenda nyumbani..lakini kama hali yake itabadilika ghafla,,muwahishe haraka hospitali.
Kutokana na furaha ndugu yao kupona,,wakajikuta wamesahau kuwa dada yao(Subira) hayupo pamoja nao....wakaingia ndani ya gari la msamalia na safari ikaanza ya kuelekea nyumbani kwa msamalia huyo..wakamuacha Subira pasipo wao kutambua!
*************************
Upande mwingine kule nyuma ya hospitali alionekana Subira akinyanyuka na kuzipiga hatua kurudi kule ndani ya wodi...
alipofika akashtuka! macho yakamtoka baada kukitazama kile kitanda alichokuwa kalazwa mdogo wake(Lulu) kitanda hicho kilionekana kuwa tupu...akaangaza angaza macho yake,pia hakuwaona wadogo zake wengine...Konje,,Jack na Lulu..kwa mbali akamuona yule daktari aliyekuwa katika wodi aliyolazwa Lulu....akamfuata na kumuulizia kuhusu mgonjwa aliyekuwa akimtibu.
daktari akasema,,"mbina mgonjwa amesharuhusi wa kurudi nyumbani...
Subira akahisi moyo wake umeripuka! akajisemea moyoni,,Mungu wangu...wamekwenda nyumbani?
nyuni wapi jamani..
Akatimua mbio kutoka nje ya hospitali..akaangaza angaza macho yake lakini hakuweza kuwaona wadogo zake...Subira akaanza kuingiwa na wasiwasi na hofu kubwa kuhusu wadogo zake.
***************************
Upande mwingine,alionekana Kabi akiwa anaranda randa mitaani...akitafuta angalau kibarua afanye ili ajipatie pesa ya kununua chakula....akafanikiwa kupata kazi kwenye banda la kuuza chipsi..akaanza kazi siku hiyo hiyo...akapewa gunia la viazi avimenye na kuvikatakata...lakini makubaliano yao,Kabi atafanya kazi bila malipo badala yake atakuwa anapewa chakula cha mchana na jioni anapomaliza kazi..Kabi hakuwa na kipingamizi...yeye alifurahi kupata sehemu ya kujipatia chakula..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
siku zilizidi kusonga...
Kule gerezani alionekana askari magereza akiwafungulia wafingwa wakafanye kazi...
Pamera akapangiwa kazi ya kupasua kuni...miongoni mwa wafungwa waliopewa kazi hiyo pia yule mwanamke aliyemsaidia Pamera chakula naye alipangiwa kazi hiyo....walipasua kuni nyingi...Pamera akahisi kuchoka kupita kiasi..kwa sababu walikuwa wanafanya kazi hiyo kwenye jua kali....yule mwanamke akamuone huruma Pamera,,lakini hakawa hana namna ya kumsaidia....
Pamera akaamua kupumzika akaliachilia shoka alilokuwa kalishikilia mikononi mwake akazipiga hatua kuelekea kwenye kivili kujipumzisha..
Askari mmoja wa kike akamuona Pamera ameacha kufanya kazi kaenda kupumzika..akachukua bakora ilyotengenezwa kwa mkia wa taa,,,askari huyo wa kike alikuwa anaogopeka kwa wafungwa wote wa gereza hilo..kutokana na roho yake ya kikatiri isiyokuwa hata na chembe ya huruma!!!!akazipiga hatua kumfuata Pamera...wafungwa walipomuona askari huyo anamfuata Pamera,,wakashtuka wakashika vichwa vyao... kwa sababu walijua Pamera atacharazwa viboko mfululizo bila huruma...
askari huyo akamkaribia Pamera.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment