Simulizi : Merisa Jini Mwitu
Sehemu Ya Tano (5)
Ijapo kuwa dini au imani yam zee magesa ilikuwa mbali kidogo na ushirikina ila kwa sasa aliziona dalili zote zakuwepo kwa mkono wa mtu japo hakutaka kulitilia maanani sana kwa kuhofia kuchukiza mola wake kwa kumuamini binadamu au viumbe vilivyoumbwa nayeye huyo huyo mola mmoja.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Harusi ilivyunjwa kisheria mpaka pale bi kharusi atakapo pona, baada ya miezi kadhaa tatizo la anna lilipungua kwa asilimia 0.5 ambayo aliwezakuona ila ni kwa mbali sana Geb ndiye aliyekuwa mtumwa wake alikuwa akimtumikia anna bila kuchoka kuanzia asubuhi mpaka jioni na siku akienda katika biashara zake humchukua pia, watu walimuona wa ajabu sana na wenginekufikia kumcheka kupita kiasi siku moja walikuwa wameketi pahali hali ya kuwa anna ameegesha kichwa chake katika mapaja ya Geb
“ mpezi ?” aliita Geb kwa sauti ya upole na unyenyekevu wa hali ya juu kabla ya kuongea chochote simu yake ya mkononi iliita,aliitazama vizuri na kuipokea kisha kuiweka sikioni upande wa pili wasimu ile ulitoa salam na kujieleza kisha Geb alitoa maelekezo ya muda mfupi na kukata simu
“ naam! Kama kuna kitu ulitaka kukiongea hapo awali?” alioji anna “yap ni kweli nilikuwa nataka kukuambia kuwa nataka nikajaribu kukutafutia daktari india ili uweze kupata matibabu na kuona tena naumia kukuona katika hali hii” aliongea Geb kwa hisia za kweli kabisa japo aliweza kuishi na anna takribani miezi sita sasa hali ya kuwa nimpofu ila hali ile ilimuumiza sana ndani ya nafsi yake alipenda amuone tena anna akimtazama ila hali ya macho yake kupoteza nuru ndio kikawa kikwazo
“Geb kwanini unajitesa hivyo juu yangu? Naona watu wanavyokucheka kuwa na mwanamke kipofu,pili asiye na kizazi kutwa mimi ni wakukaa na kufanyiwa kila kitu geb ushapoteza pesa zako chungu nzima na tatizo langu limeonekana halina ufumbuzi leo unataka upoteze pesa zaidi kunipereka hadi india hali ya kuwa bado sito pona , sikia Geb najua unaumizwa sana na maneno ya watu juu yangu kuwa sizai sio hilo tuu pia kipofu mimi ningekuruhusu tuu kuoa mwanamke mwingine” aliongea anna kwa kwikwi huku akiashiri ametoa maamuzi lakin n yale ambayo hata moyo wake haukuridhia
“ anna usiseme hivyo mpenzi wangu mimi siko kama unavyofikiria kumbuka tumetoka mbali sana umenivumilia kwa mengi kwanini leo mimi tuu ndo nishindwe kukuvumilia wewe come on nielewe basi” aliongea tena Geb kwa msisitizo akimaanisha alichotaka kukifanya
“ Geb tuachane na hayo minimesha choka kukaa hapa nirejeshe nyumbani nikapumzike”alisema hayo huku akiinuka taratibu na kujikongoja huku akiipapasa fimbo yake na kuifungua vizuri kisha kusimama wima na kusubiri muongozowa Geb mahali pale iliwaweze kufika katika maegesho ya magari na safari ikaanza kuelekea nyumbani kwa kina anna.
Walipofika Geb aliongea na mama anna juu ya wazo lake la kumpeleka anna india kwa ajili ya matibabu na wote waliliafiki swala hilo ila bado kazi ilibaki kwa anna ambaye alikuwa tayari kujitoa hata ndani ya pendo lile kuliko kumpoteze pesa,kumpa aibu na fedhea mbele ya rafiki zake. Jukumu liliachwa mikononi mwa mama yake anna ambaye aliombwa kuongea na anna ili aweze kuikubari safari ile ambayo Geb aliwaza ni dhahiri kabisa anna angeweza kuona tena, mama anna alifanya kama alivyoambiwa na hatimaye anna aliweza kukubariana na wazo lile tiketi zilikatwa nawalikuwa tayari kwa ajili ya safari ambayo ilikuwa siku tatu mbele.
Kama ilivyo ada kwa Geb kumchukua anna nyakati za jioni na kwenda naye beach basi na siku hii ilikuwa hivyo hivyo Geb aliweza kupata mazoezi ya kuuweka mwili sawa kisha wakaketi wakiongea mambo mengi kuhusu maisha ghafra Geb alipitiwa na usingizi, kushituka hakumuona anna tena alimtafuta usiku kucha hakumpata alirejea nyumbani ilikutoa taharifa juu ya upotevu wa anna lilikuwa gumzo jipya mjini walitoa taharifa police na anna alitafutwa kila kona ya jiji hakupatikana mawazo yalimsonga mama kipenzi wa anna na kupelekea kupoteza fahamu kwa kipindi kirefu mzee wa Magesa alirukwa akili kwa kutazama maradhi ya mkewe na upotevu wa binti yao na ni Geb pekee akawa msaada juu ya familia ile , mambo yake mengi yalisimama na mpaka kujikuta uchumi wake ukishuka bila kizuizi sio makampuni biashara zake na nyumba na magari vyote alifirisiwa na vingine kuuza ilikuweza kuwatibia wazazi wake na anna na kumtafuta anna alipo.
Siku moja baada ya miezi kadhaa kupita Geb alipata wazo la kwenda kwa mtalamu kuangalia kilichotokea na pia kujua ni wapi anna alipokawa alipofika alionyeshwa juu ya mazingira ambayo alichukuliwa anna katika ufukwe ule wa bahari kisha kupelekwa katika himaya ya jinni mwitu kutumikishwa, ambako huko alitolewa upofu na kufanya kijakazi wa mfalme na familia yake hayo yalifanywa na merisa ilikuweza kuisafisha nyota yake nakurudishwa tena katik himaya ile ya kijini mtaalamu alimuhesabia Geb masiku machache yaliyobaki kwa anna kutoka kifungoni na kumuomba awe na subra sana juu ya kumuona tena
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“kijana yakubidi uwe na subra sana juu ya hili hasa kma bado utahitaji kuwa naye tena huyu msichana hii hiyama uliyokaikosea ni hatari sana hata nikisema nianzishe vitu bila shaka itanishindwa wale ni majini wenye uwezo mkubwa sana wakuishi kunako maji na nchi kavu, wamejaaliwa roho mbaya hata kwa majini wenzao ila kubwa niuvumilivu” yalikuwa maneno ya busara sana aliyokawa akiambiwa Geb, na alitakiwa kuvuta subra kuweza kumuona tena anna wake miaka ilienda na masiku yalisogea hakukuwa najibu lolote juu ya kurejea kwake anna ulimwenguni na Geb sasa alianza kuweka imani ya kusadikika kuwa uwenda amekwisha fariki huko aliko na ndomana imekuwa ngumu kuonana naye.
*************************************************
Kila aliyekuwepo ukumbini alishusha pumzi kwa simulizi ile yenye kugusa hisia za watu Geb sasa alikuwa mwenye kupata hofu na kunajambo lilikwisha anza mtia shaka rohoni walipojaribu kumuangalia angle alipokawa ameketi hakuwepo tena, tayari akili ya Geb ilitaka kutoa maamuzi ila yote aliyaona ni maamuzi magumu sana kwake kuyachukua alitamani kupata muda zaidi kufikiria ila dhahiri alikumbuka mbali walipokawa wametoka na anna
******************************
Jioni moja tulivu kupita kiasi Geb alipendelea kwenda pembezoni mwa ufukwe wa bahari akijifariji na kijiupepo mwanana mpaka jua lizamapo nay eye kurejea zake nyumbani wakati bado yupo katika ufukwe wa bahari alipita mahali ambapo watu wengi walikuwa wamejaa kuzunguka msichana aliyelala pembezoni mwa bahari ambaye alionekana kuchoka sana na kuzaniwa uwenda akawa amepoteza maisha kwa upande mwingine, kwa Geb kwake ilikuwa kawaida tuu kuona watu wamezingira vile alisikia sauti za watu wakinong’ong’ona juu ya kuonekana kwa msichana huyo ghafra alitokea msamalia ambaye alijitolea kumchukua nakumpeleka hospital.
Kizakilipo tanda Geb naye alikumbuka kurudi nyumbani ilikuweza kupumzisha akili yake, huku nyuma Yule dada aliperekwa hospitali na kupatiwa matibabu ila baada ya muda ilionekana akili yake haikuwa sawa yaliitajika matibabu ya kisaikolojia zaidi, walimtibia kwa Dar es salaam ikashindikana ikabidi wamuamishie Dodoma katika hospitali ya wagonjwa wa akili MILEMBE.Jioni moja aliketi peke yake na kujitenga mbali kabisa na wagonjwa wengine alionekana kama mtu mwenye mawazo kupita kiasi alionyesha dalili zote za kuwa na fahamu zake, wakati daktari anakagua wagonjwa ni msichana yule pekee alikuwa kajitenga mbali na wenzie alimsogerea karibu na kumsemesha “mambo mrembo?”
Ilikuwa ni salamu kutoka kwa daktari akiwa na lengo la kutaka kuhakiki akili za binti Yule
“Poa za kwako?”Alijibu na kumtaka hali pia,kili kuwa ni kitu cha kushangaza kwake kwa kuletewa mgonjwa wa muda mfupi na kurejewa na fahamu zake
“Mimi niko salama, pole sana unajua upo wapi hapa?”
“Hapana ila nimeelewa kamani hospitali ya wagonjwa wa akili” lilikuw jibu la pili ambalo lilimpa matumaini daktari Yule bingwa hakutaka kuamini juu ya muujiza uliokawa ukitokea mbele yake
“Upo Dodoma katika hospitali ya milembe Kama ulivyo Dai”chozi la binti Yule angavu kabisa lilitiririka juu ya mashavu yake na kuacha alama za michirizi ikifatiwa na sura yake kutandw na huzuni alikumbuka maisha aliyokawa akiishiawali alijiuliza nikipi alikosea mpaka kustahiki adhabu ile adhabu ya kuwa mbali na wapendwa wake kwa muda mwingi, adhabu ya kujikuta hospitali ya wagonjwa wa akili bila kutarajia, Machozi yalizidi kumtoka na kwikwi za kilio ziliongezeka hakuna aliyekawa akiifahamu vizuri historia ya binti Yule ambaye hata kimuonekano tuu hakufanana kabisa na mgonjwa wa akili .
Jambo la binti Yule kushusha machozi lilimuumiza sana Daktari aliyekuwa akimuangaikia kwa lengo la kumuamisha daraja Dk.lamek, siku moja ndani ya asubuhi tulivu kabisa Dk.lamek alipita ndani ya bwalo lile la wagonjwa akili na kumkuta binti Yule akiendelea na tabia ile ile ya kujitenga na kutoshirikiana kwa jambo lolote na wagonjwa wenzie ndipo alipoomba watu wa uangalizi waweze mchukua na kumpeleka panapo ofisi yake
“Mambo mpendwa?”Ilikuwa ni kwa mara nyingine tena ambapo Dk.lamek alipata nafasi ya kukutanisha tena uso wake na uso wa binti Yule mrembo ambaye hakupata kuona maishani mwake
“poa”alijibu kwa nukta
“unaitwa nani?”aliuliza tena Dk.lamek huku akiandika maelezo yale kwenye karatasi na kumuangalia usoni kikamilifu msichanayule aliyevutia kila kona ijapo kuwa alikuwa ndani ya sare za wagonjwa wa akili ila bado uzuri wasura yake ulikosa kizibo umbo zuri la mwili wake likakosa ifadhi rangi ya ngozi yake pia ilimfanya uzuri wake uzidi mara mia,
”Naitwa anna, anna Magesa” alilitaja jina lake kiufasaha zaidi
“mzaliwa wa wapi wewe?””mimi mzaliwa wa morogoro matombo huko” Dk.lamek alishangazwa na utimamu wa msichana Yule kiasi akataka kujua mengi juu ya mpaka kilicho sababisha yeye kuwepo mahali pale ukweli hakuwepo aliyekawa akitambua vizuri historia nzima mpaka yeye kufikia pale alipo hata yeye mwenyewe alikiri kujikuta mahali pale tena akiwa mzima wa macho wakati kwa mara ya mwisho alikuwa na wazazi wake pamoja mpnz wake wakifanya mikakati ya kwenda india kwa ajili ya matibabu anna hakuona sababu ya kumficha lamek jambo kwani alijua dhahiri ndio msaada pekee uliokawa umebakia pahali pale,baada ya maongezi ya muda mrefu lamerk aliamrisha wamshushe Daraja anna kutoka daraja AA mpaka AC ambapo walikaa wagonjwa ambao akili zao sasa zilikuwa zinapata afueni na kuwa timamu.
Masiku yalikatika na miezi kibao ilipita bila majibu hatimaye mwaka na mpaka miaka Geb alikaa kumsubiri anna wake mwanamke wapekee aliyemuahidi ndoa aweze kurejea mbele ya mboni za macho yake ila haikuwa hivyo, mawazo ya kumuoa anna yalianza kufutika katika akili yake siku moja katika pita pita zake aliingia ndani ya supermarket kubwa kwa ajili ya mahitaji mbali mbali alipo maliza mahitaji yake alilipa pesa na kuondoka na vitu vyake kwenda kunako maegesho ya magari mara akamuona dada aliyemuhudumia pale kaunta akija mbio huku akimuashiria amsubiri
“Vipi dada kuna tatizo?” alimuwahi kumuuliza Geb
“Am. hapana ni hii pochi yako uliisahau pale mezani kwang”
“Ooh shit! Mungu wangu asante sana dada angu” alimshukuru na kuifungua ndani kisha akatoa kiasi kidogo cha pesa na kumkabidhi ikiwa kama shukrani kwa wema aliomtende
“Usijali kaka angu nimefanya kwa ihisani na wala sikutarajia malipo unaweza kwenda karibu tena kupata huduma zetu” alimaliza na kisha kushika njia na kurejea panapo ofisi yake na kumuacha Geb aliyebaki akishangaa juu ya tabia na ukarimu wa msichana Yule alikuwa na umbo zuri lakuvutia rangi angavu yenyekupendezesha ngozi alikuwa mzuri na wakuvutia kweli Geb alitamani kuwekaukaribu na msichana huyo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miezi sasa ilikatika tangu Geb ameanza mazoea na Yule msichana wa pale kaunta supermarket mara kwa mara alikuwa akienda kumchukua na kwenda naye out mara nyinge hujitahidi kumletea lunch ofisini hatimaye Geb alimsahau kabisa msichana aliyeitwa anna na kuzama katika dibwi la mapenzi na muhudumu wa kaunta supermarket alitambulikwa kwa jina la Iren.
***************************
Ilikuwa ni mara ya nne sasa tangu baraa lilipoanza ndani ya hospitali ya wagonjwa wa akili ambapo anna alikuwa nimtu wa kubadilishwa adaraja kila kukicha na mara hii alipelekwa mpka AF ambapo alitarajiwa baada ya AG basi anna ataachwa kuendeleza maisha yake mtaani akiwa kama mtu mwenye akili timamu jioni moja wakiwa wanapewa chakula anna alipanga msitari wa kukingia cha kula na kuwa mtu wa mwisho kabisa watu walipewa chakula na kikaenea kila watu walikaa makundi kw makundi wakiongea lugha ambazo walikuwa wakizielewa wenyewe anna alibeba chakula chake na kujitenga kando na kuanza kula taratibu ghafra ilisikika sauti ya mtu akiita
“merisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa?”
Watu wote walishtuka wagonjwa wote walisogea pembezoni na kuacha uwazi ambapo anna sasa aliweza kuangusha kichwa chake chini na kulala mfano wa mtu aliyepoteza famahamu baada ya dakika mbili alifurukuta na kuanza kuruka ruka tena walitwa wakaguzi na kumtoa kisha kumpandisha daraja mpaka AA ambako huko walikaa wale wasiojielewa kabisaa alikuwa akifanya hivi mara kadhaakitu kilicho muumiza sana akili Dk.lamek ambaye tayari alikuwa amekwisha anza kuingiza moyo wake katika mapenzi na mgonjwa Yule wa akili pasi nay eye wala anna kujua kama moyo wa Dk.lamek uliangukia kifuani kwake.
Hata yeye mwenyewe alishindwa kuelewa kwanini aliumizwa sana na hali ya anna kuliko hali ya wagonjwa wote pale hospitalini ila akajipa moyo uwenda sababu historia yake anaijua ila haikutosha hilo peke ake maana walikuwamo wagonjwa wengine ambao pia alizitambua vyema historia zao na kumfanya hata atoe machozi ila kwa nini anna na huyu merisa aliyekuwa akimtaja kabla ya kurejea uchizi ni nani yake na alikuwa na tatizo gani naye kiasi yeye awekama chanzo cha yeye kuwa vile.
Alijiuliza maswali mengi ila takribani yote yalikosa majibu.
Usiku mmoja tulivu sana, na kutokana na siku ile kuwa ijumaa watu walilala mapema kupumzisha vichwa vyao kwa ajili ya kuanza wikend yao vizuri wakati Geb bado hajatulia vizuri kitandani mara alisikia mtu akigonga mlango wa chumbani kwake akaamka taratibu kujikongoja na kwenda kuufungua chakushangaza hakukuwa na mtu ila upepo mkali ulipita baada tu ya geb kuwa ameuacha wazi mlango alipohakiki kama hakukuw namtu hata aliyethubutu kubisha hodi chumbani kwake alifunga mlango na kurejea kitandani kutahamaki alkutana uso kwa uso na merisa ibilisi wa moyo wake hasidi wa mambo yake na mvunjaji wa ndoto za watu
“Wewe tena?” aliuliza Geb maana alimtambua vyema merisa hivyo hakutaka hata kujua alifikaje mahali pale
“yeah ni mimi”akainuka lipoketi na kuanza kutembea tembea hatua fupi fupi ndani ya kile chumba “nimekuja nina habari njema kwako Geb,kwanza kukujuza kuwa kila unachokimiliki sasa hivi sio mali zangu hata hizi ni zile ambazo zilitokana na mali ambazo nilikupatia mimi ila nimekuja leo kukuacha huru wewe pamoja na anna alinyosha kidole ukutani ambapo kilitokea kitu mfano wa sinema alionekana anna tangu alikohifadhiwa na kuwa kijakazi wa mfalme kisha kutupwa kando ya ufukwe wa bahari ambapo Geb alipuuza juu ya tukio la watu kumzunguka msichana alielazwa ufukweni mwa bahari mpka anna anafikia hatua ya kwenda hospitali ya wagonjwa wa akili ila pia kuna nguvu ambazo Geb alipewa na merisa na siku hii ndio ilikuwa siku ya kunyang’anywa nguvu hizo ambazo merisa alimvuta Geb na kumziba macho yake kwa kutumia mkono wa kushoto,Ghafra alikurupuka kutoka kitandani kiasi akamwamsha Irene ambaye alikuwa amelala naye
“vipi baby?”Aliuliza Irene
“amna kitu mpenzi ni ndoto tuu”alijibu huku akishusha pumzi kubwa na kurejea ndani ya shuka na kujifunika vizuri kisha kupitiwa na usingizi.
Yapata wiki ya pili sasa hali ya anna ilizidi kuimarika siku moja anna alikuwa ameketi pahali huku akiwaza la hapa na pale mara alitokea mkaguzi akamshitua na kumuomba anna amfate kwa nyuma ambapo alipewa rasmi taharifa zakuwa anaweza kuishi popote atakapo na kuwa huru kama mtu mwenye akili timamu japo kuwa Dk.lamek hakuwepo siku hiyo na alionekanakusafiri kwa safari za kikazi hivyo aliagiza anna apatiwe bussinesscard yake ilimradi panapo shida yoyote aweze kumtaharifu.lamek alikuwa tayari kujitoa kwakila namna alijikuta tuu akitokea kupenda na kutamani kujitoa kwa namna yoyote ile kwa jili ya anna historia ya anna ilimuumiza sana,kiasi ilifikia hatua kila akifikiria chozi lilikuwalikimtoka sio hilo tuu mara nyingine alitamani kumueleza anna ukweli wa hisia zake ila alihofia kumkwaza kulingana na maradhi yake.
Anna alitoka nje ya jingo lile akiwa hajui nini afanye na wapi aende alikuwa mgeni Dodoma hakuwa na ndugu jamaa wala rafiki na hata kama alikuwa nao basi alishawasahau alilala katika vituo vya madaladala kila kukicha alipigwa na baridi kali, upepo wa vumbi ulimuumiza macho yake kila kukicha alikuwa ni mtu wakutap tapa kwa makazi napo mawazo hayakukaambali naye aliwaza jinsi miaka michache ilivyotumika kumvurugia kila kitu katika maisha yake alilitazama bango kubwa lililopo katika lango la kutokea mabasi ambapo kulikuwa na tangazo la cocacola ambalo kulikuwa na watu wawili msichana na mvulana wakionesha tabasamu zito lililopita kiasi wakishikiria chupa zao za soda mikononi akajikuta akitabasamu mwenyewe maana picha ile ilimkumbusha mbali sana ambako alijua kurudi mahali hapo ilikuwa ni kazi kubwa ,kuirejesha nafasi yake iliyokapote ilikuwa yataka moyo, alilitazama tena lilebango na kutafakari kwa kina
“ni miaka mitano sasa tangu 2011,ilipo pangwa safari yangu ya kwenda india na kushindikana Geb atakuwa amekwisha nisahau na bila shaka atakuwa ameshaoa nakuzaa watoto na mwanamke mwingine “ alijisemea mwenyewe kisha akashusha pumzi ndefu na kuendelea na safari yake kushtuka anakutana na basi kubwa aina la ABC ambalo lilijitahidi kumkwepana na hatimaye lika msukuma nakumkwaruza sehemu ndogo ya mwili wake, kumbe alikuwa akitembea hali ya kuwa bado anamawazo kichwani kiasi hakuweza kuliona gari wala kusikia honi, alijikongoja pale alipo anguka na kujiegesha panapo mti mkubwa wa nyaya za umeme
“ pole sana binti ajakuumiza sana?” ilipita sauti nzito masikioni mwake kutazama alikuwa mzee wa makamo, aliweza hata kumfananisha hata na baba yake mzazi kiumri “hapana, kidogo tuu nahisi nitakuwa sawa “ alijitetea huku akimuonyesha sehemu yake ya bega ambayo kwa sasa ilikuwa ikivuja damu
“Mmh! Hiyo sio sehemu ndogo mwanangu naombanikupe msaada wa hospitali” walikubaliana na wote wakaondoka taswira ya mwanaume Yule aliyemuonyesha utu anna na kutaka kumsaidia ilikuwa tofutti sana na watu wengi wanao penda kusaidia mara nyingi watu wenye uwezo wakipesa ndo hutamani kumsaidia mtu ilikuwa tofauti kwa mzee huyu ambaye mpaka sasa anna hakulitambua jina lake, alionekana dhaifu na nimtu mwenye hali duni ila nafsi yake ilimtuma kufanya wema ule kiasi kidogo cha pesaalichokawa nacho chote alimpatia daktari kwa ajili ya matibabu ya anna walipo pewa huduma walisogea mbali kidogo na zahanati “Binti mimi naitwa mzee bernad,ila wengu hupenda kuniita uncle Ben” alianza kujitambulisha mzee Yule wa makamo” asante uncle ben mimi naitwa anna “ anna pia alijitambulisha kisha akaweka nukta kumsikiliza uncle ben ambaye alionekana kuwa na shauku la kusema jambo
“unajua anna, Dodoma au hata mikoa mingine inatofauti sana na Dar e salaam, na huku ni agharabu sana kukuta watu wakitembea bila kuwa na makazi maalumu, name nimekuwa nikikuona mahali hapa nina zaidi ya siku mbili hivi ukiwa auna melekeo mzuri embu niambie wewe kwenu hasa niwapi?” swali alilo ulizwa anna na uncle ben alitamani asiulizwe na yeyote ulimwenguni kwani alikuwa akikifukua kidonda ambacho bado kibishi ndani ya moyo wa anna machozi yalijaa ndani ya macho yake na kuanza kutiririka mashavuni kwa uchungu historia yake mwenyewe lakini ilimliza kila kukicha akiikumbuka, hakuwa na namna alimuhadithia uncle ben kila kilichotokea na mpaka siku ile kufika mahali pale ,kiasi ilimgusa uncle Ben ambaye naye aliwapoteza watoto wake wawili na mkewe katika mazingira ya kutatanisha baadaya kufuja mbali ambazo hakuzipata kwa njia ya halali na kulitumikia kanisa kwa kutumia mali hizo pasi na hofu yoyote kitu kilichokuwa tofauti na masharti ya mali hizo. Waliongea mengi na uncle ben alimkaribisha anna nyumbani kwake na kuishi naye kama binti yake.
***********************************
Ilipita miezina hatimaye mwaka ulikalibia kuisha siku moja mida ya jioni wakati uncle ben anatoka kutafuta chochote kitu alishangaa kumkuta anna amejilaza nje ya kibanda kile cha nyasi hukuakitetemeka mithili ya mtu anayehisi baridi kali alimsogelea karibu na kumshika “anna mama nini tatizo?” alimuuliza
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Uncle….si.sijisikii vizuri” aliongea kwa tabu kweli anna alikuwa na homa kali mno uncle alimuinua anna na kumuingiza ndani kisha kumfunika nguo nzito na kuwasha mshumaa kwani tayari giza lilikuwa limetanda “kulikoni anna nini cha mno “aliuliza uncle ambaye alitaka kujua namna ya kumsaidia “ nikichwa tuu uncle na homa kali pia najihisi mwenye kupata baridi kali” alijielezea anna jinsi anavyojisikia taratibu alisogea pembeni na kuchukua kikombe cha maji na tambara kubwa kisha akakilowesha maji kile kitambaa na kumfunikanacho juu ya paji la uso “sasa sikia binti yangu wacha nikakuangalizie dawa nakuja sasa hivi kwa lolote utamuita jirani akusaidie sawa?”
“Sawa”
Alinyanyuka taratibu bembezoni mwa kitanda cha anna akatoka mpaka mbele ya kibanda kile akaingiza mikono yake mfukoni akatoa shilingi mia mbili
“Daaah sijui nitapata wapi pesa ilinikamnunulie dawa binti yangu?” alinung’unika mwenyewe huku akiangalia anga jinsi ilivyotanda Giza “bila shaka yatakuwa nimalaria embu tuone itakavyokuwa” aliendelea kujadili Na halimashauri yake ya kichwa huku akikanyanga hatua kutoweka maeneo yakaribu Na nyumbani.
Zilipita sekunde dakika na sasa ikawa nusu saa tayari alikwisha pata dawa na kurejea nyumbani jirani kabisa na nyumbani kwake alishuhudia moto mkali ukiwaka na watu wakiizunguka nyumba yake kwa mandoo ya maji na michanga wakijitahidi kuzima moto huo kutazama vizuri bila shaka aligundua nikibanda chake ndicho kilichokawa kikiwaka moto “mungu wangu!” alihamaki na kushika mikono kichwani
“Binti wa watu jamani “aliendeleakuisononesha nafsi yake alikimbia Na kusogea karibu na eneo lile ilikupata taharifa juu ya binti aliyekawa amemuacha ndani ya kibanda kile
“Samahani kijana kuna binti nilimuacha humu ndani vipi amefanikiwakutoka?” alimuuliza kijana aliyesimama naye jirani
“Ndio kafanikiwa ila ameungua kidogo na dhani wamempeleka dhahanati ya hapo karibu” alijibu huku akiashilia kwa kidole kumuelekeza zahanati ya pale karibu ambapo alikuta anna akipewa huduma ya kwanza juu ya jeraha lile la moto masikini anna alikuwa ameungua usoni na sehemu yake kubwa ya uso iliharibika sana hakukuwa na uwezekano wakusema akipona itarejea taswira yake ya zamani bila shaka ilikuwa lazima abadilike,lilikuwa pigo kubwa kwa anna kwa mara ya kwanza alianza kupoteza tumaini la kuonana na Geb.
Siku zilipita Na anna akapata auheni Na kidonda kilianza kuonyesha matumaini
“Mzee mginjwa wako anaendelea vizuri tuu Na unaweza kuondoka naye baada ya kukamilisha malipo”aliongea daktari aliyefika wodi ya wagonjwa Kwa lengo la kuangalia maendelea ya wagonjwa
“Nikiasi gani itagharimu matibabu yote hayo”aliuliza uncle ben
“Uwenda yakafika laki tatu na nusu ila kwa uhakika zaidi ungeulizia pale mapokezi”ilikuwa Ni kiwango kikubwa Sana cha pesa hawakujua wapiwa ngeweza kukipata kukicha uncle ben alikuwa akitafuta pesa hizo ambazo bado matumaini ya kuzipata hayakuwepo na kiasi cha pesa walichokawa wakidaiwa kilizidi kuongezeka kila siku na mpaka kufikia laki tano siku moja jioni anna akiwa katika mizunguko yake ndani ya ile hospitali kwa mbali alimuona mtu aliye mfahamu Dk.lamek, alikumbuka amaagizo aliyopewa siku ya mwisho wakati anaondoka hospitalini hapo akakumbuka alipewa namba ya simu ya Daktari huyo ila aliipuuza leo aliuona umuhimu wake na kuamua kumfatilia, alimfata pale alipokawa amesimama akiongeana baadhi ya wauguzi wa hospitali ile. Ali msubiri mpaka alivyomaliza kuongea na wauguzi kisha akaomba kuongea naye
“Habari yako dokta?” alimsalimia anna ila lamek alionekana kutokujali kwani alimshukuria kama wagomjwa wengine tuu
“Salama nieleze unatatizo gani dada angu?” alimuuliza huku akiendelea kupekua faili alilokawa amepewa mkononi baada ya kuwapa maelekezo wauguzi wale
“Naitwa anna Nina matatizo?”jina la anna lilienda kuugusa moyo wa lamek bila kutarajia alishtuka na kumtazama vizuri upande mmoja wa sura yake alikuwa amejiziba na kanga kumtazama lamek aligundua kuwa ni kweli alikua ni anna tena ni anna magessa Yule Yule aliyekuwa akimtafuta kwa kipindi kirefu.
Wakajikuta wakikatisha maongezi na kuanza maongezi mapya lamek alianza kuelezea jinsi alivyochukua muda kumtafuta anna huku akijua hakuwa na mahala pakuishi kwa pale Dodoma alimuelezea anna alivyogombana na watu ofisini kwa kumruhusu anna kutoka wakati hakuwa na pakwenda kwa muda ule il mwisho ilibidi warudi katika mada ya tatizo la anna .
“nina daiwa laki tano katika hospitali hii na kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo pesa inavyozidi kuwa kubwa na kugharimu maisha yangu”
“usijali tatizo lako ni dogo na tangu sasa limekwisha, ila hujanieleza uliletwa hapa kwa tatizo gani?” baada ya swali hilo ndipo anna alipoamua kufunua ule upande mwinginewa sura yake ama alikuwa ameharibika mno
“kulikoni anna umekutwa na nini?”
“ni stori ndefu Dk ila nitakuhadithia usijali”
Waliongea mengi ya hapa na pale na lamek alimuhakikishia anna kuwa anamlipia kiasi chote cha pesa anayodaiwa pia alimchukua anna na uncle ben akaenda nao kuishi nao kwake ambapo alikuwa akiishi mwenyewe tuu pamoja na dada wa kazi.
Walikaribishwa ndani ya jumba lile la kifahari na wao wakawa miongoni mwa familia ile , masiku yalipita anna akiwa na mawazo tele juu ya Geb fikra zake zilitamani kumsahau Geb ila moyo ulikuwa mgumu kushawishika kwa hilo, kila alipojitazama katika kioo alihofu na taswira aliyokuwa nayo.
Siku moja jioni lamek alikuwa akipata chakula cha jioni na anna katika moja ya hoteli nzuri na yakifahali pale Dodoma huku wakipiga story za hapa na pale
“anna nimejaribu kukuangalizia daktari wa kuliondoa hilo kovu lako hapo usoni na hatimaye amepatikana “
“waow jamani asante lamek”
“usijali mimi naona nikama wajibu wangu kukusaidia katika jambo kama hili ndomana unaona hata leo nipo hapa kwa ajili yako” aliongea lamek maneno yaliyomfanya anna awemakini zaidi kumsikiliza
“unajua mbali na yote haya ninayo yafanya leo hii kwa ajili yako ni kwa ajili yangu pia”
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unamaana gani?” aliuliza anna huku akiwa na hofu kubwa
“tangu siku ya kwanza nakuona ukiwa katika hali ya uchizi nilitokea kukupenda mno ila sikuweza kupewa nafasi kwa wakati ule nikiwa kama daktari kukueleza hisia zangu,ila kwa kudhihirisha dhamila yangu kuwa ni ya kweli leo nimekutana tena na anna na ninakuelezea hisia zangu, anna ninakupenda na nina hitaji nikuoe” yalikuwa maneno yaliyoustahaja bisha sana moyo wa anna hakuelewa kama alikuwa ndotoni au ni kweli yalitokea , alisimama kisha akagonga meza kwa hasira
“lamek huu ndo msaada unaotaka kunisaidia?, samahani sana sitoweka kukubaliana na wewe maana bado moyo wangu upo kwa Geb na wewe unajua hilo kama msaada wako siwezi kuupata bila kuwa na wewe kimapenzi basi bora niendelee kuwa hivi hivi maisha yangu yote”hapana anna sikuwa na maana hiyo bado nahitaji kukusaidia japo kuwa nakupenda ila pia na elewa kama moyo wko upo kwa mtu mwingine ila daaah sawa basi niahidi iwapo huto onana na Geb na kurudiana naye tenautakuwa wangu?”Zilikuwa hisia za kweli za lamek zikisimama kulitetea kile kinachokiitaji, walielewana na anna alipewa matibabu huko india na kufanyiwa upasuaji wa sura yake ilikuweza kuliondoa kovu alilokawa nalo na kurejeshewa ngozi yake na sura yake ya awaliilimchukua masiku kadhaa kitandani mpaka atakapopona na kutolewa bandeji usoni.
Siku moja jioni kulitangazwa uzinduzi wa yard mpya ya magari ambaye mmiliki wa yard hiyo alikuwani Mr Gabriel Msigwa zikatajwa na namba zake za simu na mwenyew alonysha akitoa maelekezo mafupi juu ya yardi yake ya magari, anna alimgundua ni kweli alikuwa geb wake ndo Yule aliyekawa akionyeshwa kwenye runinga aliikariri vyema namba ile iliyotajwa pale ili asije kuisahau au kuipoteza kwa namna yoyote ile, bado ilibaki kuwa siri yake juu ya namba ya Geb aliyoipata baada ya masiku mengi kupita sasa iliwadia ile siku ya kutolewa ile bandeji usoni walitwa ndugu wa karibu ambao ni Uncle Ben na lamek mwenyewekisha wakamfungua taratibu mpaka mwisho kabla ajafungua macho anna alihisi ukimya uliojawa na mshangao juu ya watu wliokwa wanamtazama kwa wakati ule hasa uncle ben ambaye alionyesha kupotea kwa matumaini kadhaa mbili yake anna aliinua mkono wake na kupapasa uso wake ambao alihisi ngozi nyororo kupita maelezo ngozi ile ilitofautiana na ngozi yake ya awali kitu kilichomshangaza mno kwani anakumbuka kuaidiwa kurejeshewa hali yake ya mwanzo . Kutahamaki alikutana na chungu cha udongo kilicho na ngozi ya mwanadamu alipoitazama vizuri aligundua ilikuwa ni ile sura yake ya awali ilitolewa yote nay eye aliwekwa nyingine hakutaka kuamini alikisogerea kioo kilipo aliumia sana kuona taswira yake imeharibika alijua dhahiri utakuwa ni mpango wa lamek ilikuweza kupoteza taswira ya anna ili abaki kuwa wake maisha yote, japo anna alipojaribu kumtupia lawama lamek lamek alijitetea kuwa hayakuwa makubaliano yake na madaktari na hata yeye alishangaa kuona anna amebadilishwa sura .
Mpango wa lamek wa kumbadilisha sura anna ulikuwa wa siri kubwa mno, lamek aliweza kumpatia ktita kizito cha pesa kila daktari ili asiweze kuvujisha siri ile na ibaki kuwa ndani yao tuu, alijua kuwa amemuumiza sana anna juu ya kitendo kile ila hakuwa na namna wala jinsi zaidi ya kumtenganisha na taswira ambayo itamsumbua geb,
Baada ya masiku mengi kupita anna sasa ilibidi amsahau Geb na kufungua kurasampya wa maisha yake akiwa kama msichana mwanamusiki ila kabla ya yote alitamani kurudi dar-es-salaam kujua hali ya wazee wake ambapo alipewa taharifa za mama na baba yake kufarikimiaka mingi iliyopita na kuzikwa katika makabuli ya public kutokana na ukosefu wa wasimamizi aliikuta nyumba yao ikiwa gofu tuu nyasi kila kona zilitapa kaa haikuonekana kama ni nyumba ambayo walikuwa wakiishi watu ,taswira ile ilimuumiza zaidi ila hakuwa najinsi japo ulikuwa msiba mzito wakondokewa na wazazi wote wawili , aliludi nyumbani ambapo alishika gita lake na kuanza kuimba nyimbo za majonzi ,wkati akipiga gita lake zikamjia fikra za kuwa mimbaji mzuri “pamoja na huu umaridadi niliokuwa nao mbona nitaweza
Kuimbamusic aliwaza Sana juu ya Hilo mwishoni aliacha kupiga gita kisha akasema tangu sasa nitaitwa angle,”
*************************************************************
Tangu hapo niliitwa angle Na jina la anna lilifutika kichwani wangu mpaka nilipokuja kuonana Na Geb katik moja ya kasino mara ya kwanza mpaka kuniambia anamchumba roho iliniuma sana ila yote ni kwa sababu geb alikuwa hajui kama alikuwa akiongea na mtu ambaye alikuwa akimchoma sana moyo wake, Geb samahani kwa yote yatakayo tokea mahali hapa ila huu ndio uhalicia wa maisha yangu mimi ndiye anna wako niliyetolewa kizazi kwa ajili yako nimefanyiwa mengi yakudharaulika kwa ajili yako ilakubwa nililokuja kusema ni shukrani za dhati na kuwatakia maisha mema……………
***********************************
Mara ile screen ilizimakila mtu ndani ya ukumbi ule alikuwa ameshachoka kila mtu alimuonea huruma anna kwa tabu alizopitia mpaka alipofikia kwao ilikuwa simulizi yenye kuumiza mno ila ilimuumiza zaid anna na Geb ambao ndio walikuwa wahusika wakuu Geb alitazama huku na kule kuona ni wapi angeweza kumuona anna lakini anna alikuwa amekwisha ondoka ndani ya ukumbi ule, alimtafuta kwa simu yake ya mkononi mara kadhaa iliita ila baadae ilikata na kuzima kabisa hata alipo piga aliambiwa simu anayopiga haipatikani,alimtafuta bila mafanikio wakati bado anaangaika kumtafuta anna kwa simu yake ghafra alishikwa bega na mtu siye mjua
“samahani m naitwa mr lamek” alijitambulisha lamek huku akimpa mkono geb ,
” bila samahani “
“mimi ndiye lamek niliyekawa naongelewa mahali hapa ni kweli nimemkosea sana angle nilikuwa nakuomba unisaidie walau kuniombea msamaha kwa kosa la kumbadilisha sura yake “ aliongea mengi lamek hakuacha kuelezea juu ya ukweli alio kawa ameuweka siku nyingi ndani ya moyo wake mwisho wa siku alimchukua Geb na kumkutanisha na anna ambao walisameheana na kuombana radhi kwa kila chembe waliyokoseana na kufunga ndoa kisha wakaanza maisha yao upya wakiwa kama baba na mama na kwa kuwa anna alikuwa hana kizazi hivyo hawakuwa na matumaini ya kupata mototo hivyo wakaomba mtoto katika kituo cha watoto yatima na kumlea kama mototo wao na kusahau kabisa maisha ya awali ikiwemo na kufuta taswira ya misukosuko yote waliyopitia katika maisha yao.
JIFUNZE MAISHA SIO MTEREMKO KAMA UNAVYOFIKIRIA LEO UPO KWA WAZAZI AU WALEZI WANAKUPA KILA UNACHOKITAKA UWEZI KUONA MTIKISIKO WOWOTE HATA KAMA BABA ASIPO ACHA PESA YA CHAKULA KWAKO LAZIMA UTAKULA KWANI MAMA ATALIPIGANIA TUMBO LAKO ILI UWEZEKULA, ILA UTAKAPO ANZA KUSEMA LEO NATAKA NISIMAME PEKE YANGU EIZA NA MUME, MKE AU MPENZI NDIPO MAJARIBU MENGI HUANZA KUTOKEA ILA YOTE NI KATIKA NAMNA YA KUZITENGENEZA NAFSI ZENU JUU YA UVUMILIVU………………!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ANGALIZO KILA KINACHO TOKEA KWAKO LEO HII KILISHAWAHI KUTOKEA MIAKA YA NYUMA
MWISHO!!!!!!!!!!!!!!!!
0 comments:
Post a Comment