Simulizi : Jina La Urithi
Sehemu Ya Pili (2)
kule nyumbani Njile,,maisha yaliendelea,lakini mtoto Laula aliendelea kufanya matukio ya ajabu,,,habari zikazagaa kila kona ya kijiji,,kuwa Laula si binadamu wa kawaida....
mkuu wa kijiji hicho,akaamuru Njile pamoja na mtoto wake wafukuzwe,,wasiendelee kuishi katika kijiji hicho..CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Njile hakuwa na namna,,akalazimika kuuza kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba,,pamoja na nyumba yenyewe ,,,lakini hakuna mtu aliyejitokeza kununua hata kitu kimoja,,hakuna aliyetamani hata kupewa kitu bure..Njile akaamuaa kuondoka na mwanae Laula,, akaelekea mjini,,ni mbali na kijiji hicho!
Maisha ya Njile yakawa magumu kupita kiasi,,wakati mwingine hakuweza kupata mlo siku nzima,,
Laula akashindwa kuendelea na masomo,,Njile akafanya jitihada za kutafuta vibarua ilimradi apate pesa ya kumpatia mlo mwanae Laula,,
siku zilizidi kusonga,,wakiwa wanalala nje,,kitendo hicho kilimuumiza sana Laula. lakini hakuna namna.
siku moja nyakati za usiku,,Njile aliugua ghafla,,homa ilikuwa kali na hakupata msaada wa matibabu,,Laula akatimua mbio kutafuta msaada lakini hapakuwa na mtu yeyote kuonekana kupita maeneo hayo,,zaidi ya magari pekee,,Laula akakata tamaa akaamua kurudi kule alipokuwepo mama yake,,akakuta tayari ameshakata roho!
Asubuhi palipokucha ,,,Maiti ya Njile ikachukuliwa na maaskari,,na kuzikwa kwa sababu hakuwa na ndugu...
siku zilizidi kusonga,,Laula akawa chokoraa,,akaishi kwa tabu na misukosuko ya kila namna,,,
baada ya mwezi mmoja kupita,,wazo likajia Laula,,akaamua kurudi katika kile kijiji chao,,angalau akavhukue nguo za marehemu baba yake,pamoja na vitu vinavyobebeka, huenda akaviuza na kupata pesa ya kununua nguo za kuvaa yeye..
siku hiyohiyo safari ikaanza,,akatembea kwa miguu kuifuata njia ya kuelekea kijijini kwao,,hatimae,, akafika salama,,,akaifuata nyumba yao,,alipoingia upande wa ndani,,akastaaajabu kuona,,kila kitu kipo vilevile kama walivyoacha siku alipoondoka yeye na mama yake...akakifuata chumba alichokuwa analala mama yake,,,akafungua sanduku kubwa la mbao,,lililokuwa na nguo za baba yake,,akaanza kutoa nguo mojamoja...akafanikiwa kuchukua mashati kadhaa,,lakini akaona suruali moja ikamvutia,,,akaichukua suruali hiyo na kuivaa,ingawa ilikuwa kubwa lakini hakujali,,akaikunja upande wa chini kisha akafunga kamba kwenye sehemu ya kiuno,,,akachukua redio ndogo iliyokuwa chumbani humo pamoja na picha za mama yake zikiwemo pamoja na picha za babq yake akazishikilia mkononi,,kisha akatoka nje,,,kabla hajafika mbali,,akaamua kuziweka picha hizo katika mfuko wa suruari hiyo.
akashtuka! akahisi kama kunakitu ndani ya mfuko wa suruali hiyo,,akaingiza mkono wake ili aone ni kitu gani hicho!
TAHARUKI!!!!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akastaajabu kuona jino la binadamu! akalishikilia juu ya kiganja chake kisha akatabasamu,,,akajisemea moyo,,"bila shaka lilikuwa jino la baba yangu,,
lakini sijui yuko wapi! mama alisema baba kasafiri mmh! inamaana hatorudi tena! au atakuwa amepata mke mwingine!?
mpaka sasa Laula hajui ukweli kuhusu kifo cha baba yake!
akaendelea kuzipiga hatua na kuondoka zake.
Uoande mwingine,,alionekana mwanamke mmoja,,akitimua mbio na kuingia kwa pupa kwa mkuu wa kijiji! kisha akasema,,"wale watu waliofukuzwa hapa kijijini,,wamerudi tena! nimemuona mtoto wa Njile akitokea ndani ya nyumba yao!
Mkuu wa kijiji akaingiwa na hasira akasema,,"hii ni dharau! Nyumba hiyo ichomwe moto haraka iwezekanavyo....
akaamuru jinana wakachome moto nyumba hiyo.
Wakati huo huo,,upande mwingine, alionekana Laula akiendelea kuzipiga hatua kurudi mjini,,
baada ya masaa kadhaa kupita,,akahisi kuchoka na pia njaa ilimuandama! akapiga moyo konde na kuendelea kuzipiga hatua.
Kule Kijijini,,walionekana wale vijana walioamrishwa waichome moto nyumba ya Njile,,,wakiwa wamesimama kando wakisubiri nyumba hiyo iteketee kabisa ndipo waondoke eneo hilo.
Upande mwingine alionekana Laula akiendelea kuzipiga hatua,,hatimae akafika mjini,,,angalau akanza kupata matumaini ya kupata chakula, kwa mbali akaona genge dogo la kuuza samaki,,akaamua kulifuata genge hilo,,,alipofika akachukua samaki mmoja mkubwa kisha akaanza kula samaki huyo.
muuzaji hakuwa na wasiwasi kwa sababu,,baadhi ya wateja wake wengine hununua samaki na kula hapohapo...Laula akaendelea kumtafuna samaki huyo kwa pupa,,kisha akachukua samaki mwingine,,akaanza kula.....alipomaliza kula samaki huyo akazipiga hatua kuondoka zake,,pasipo kulipia pesa!
mama muuza samaki akapaza sauti,,"wewe mtoto.
lakini Laula hakugeuka,,akaendelea kuzipiga hatua!
yule mama muuza samaki,,akakasirika, akapaza sauti kwa hasira,,"wewe mtoto rudi hapa! Laula akasita kutembea akasimama,,akageuza shingo yake,akakutanisha macho na mama muuza samaki,wakatazamana nyuso zao! mara ghafla yule mama muuza samaki akatimua mbio huku akipiga mayowe.
Laula akaendele kuzipiga hatua na kutokomea kusikojulikana!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo huo,,kule kijijini,walionekana wale vijana wengi wakishuhudia nyumba ya Njile ikiendelea kuwaka moto,,vijana hao walikuwa wamesimama kando huku wakiimba kwa kilugha chao nyimbo za matusi,,wakiitukana familia ya Njile...
Nyumba iliendelea kuwaka moto hatimae ikateketea,,na moto ukaanza kupungua,,,,ghafla likatanda wingu kubwa!
winngu hilo lilisababisha taharuki,,giza totoro likatanda...
kwa mbali akajitokeza mtu kisha akatoweka kimiujiza! baadhi ya vijana hao walimuona mtu huyo lakini hawakutambua ni nani! hofu ikatanda juu yao,,giza lilizidi kutanda,,hakuna aliyeweza kumuona mwenzake! punde si punde ikasikika sauti ya mmoja wa vijana hao akisema,,"MAMAAAA NAKUFAAA!
ghafla ikasikika tena sauti ya kijana mwingine akisema,,"tafadhali usiniuwe, kabla hajaongea neno lingine akastaajabu anavutwa juu qngani na kuachiliwa akadondoka chini,,na kupasuka kichwa..
punde si punde lile giza likatoweka kimiujiza! pakawa na mwanga!
baadhi ya vijana waliobaki hai,,wakashtuka kuona wenzao wamekufa vifo vya kutatanisha! walipotazama ile nyumba iliyokuwa imeteketa kwa moto,, macho yakawatoka! hofu ikazidi kutanda hawakuamini walichokiona mbele yao!!!!!!!
KIZAA ZAA
Wakamuona Laula akiwa kasimama mbele yao,,mikono yake ikiwa imetapakaa damu! kila aliyejaribu kunyanyua mguu wake atimue mbio alishindwa,miguu yao ilikuwa mizito hakuna aliyeweza kunyanyua mguu,utadhani wamewekewa gundi kali!
hofu ikatanda juu yao....
Laula akazipiga hatua kuondoka eneo hilo! kabla hajafika mbali akaanza kubadilika taratibu,,kutoka katika umbile la mtoto Laula,,na kuwa mzee kikongwe! kisha mzee huyo akatoweka kimiujiza,,na nyumba ikaonekana kama haijachomwa moto,,ikawa vilevile,,kama inavyo onekana miaka yote! punde si punde wale vijana watatu walioonekana wamekufa,,wakafufuka na kurudi katika uhai wao!!!
wale vijana wengine wakahisi kama miili yao imeachiliwa hata wakaweza kunyanyua miguu yao,,wakatimua mbio! kila mmoja alipita njia yake!
na kutokomea kusikojulikana!
baada ya dakika kadhaa habari zikaenea kijiji kizima kuwa imeonekana miujiza,kule katika nyumba ya Njile,! mashuhuda ambao ni wale vijana wakasimulia matukio yote waliyoyaona! kijiji kikazizima wanakijiji wote wakaingiwa na hofu kutokana na uvumi huo,,kilichowashangaza zaidi,Nyumba imechomwa moto na ikateketea kabisa,,lakini Nyumba hiyo ikarudi upya na kuonekana kama haijachomwa moto!
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande mwingine,,alionekana Laula akiwa anazipiga hatua,,alitembea pasipokujua ni wapi anaelekea! kwa mbali akaona watoto wa lika lake,,wanacheza mpira wa miguu! Laula akatabasamu,,akaonekana kuvutiwa na mchezo huo,,akaamua kuwafuata watoto hao na kujumuika nao katika mchezo huo.
Laula akaonekana kujua kusakata kabumbu zaidi ya wale watoto wote,,,wakiwa mchezoni,kwa bahatimbaya mtoto mmoja akamkanyaga Laula akadondoka chini na kuvunjika mkono!
watoto wote wakaogopa kumuona mwenzao kavunjika mkono!
watoto wengine wakatimua mbio kurudi majumbani kwao..
lakini cha kushangaza Laula hakuonyesha kupata maumivu katika mkono wake! akanyanyuka na mkono wake ukajiunga na kurudi katika hali yake ya kawaida kama vile haujavunjika!
kitendo hicho kiliwafanya wale watoto waliobaki wakimshangaa Laula,waogope,,bila kuchelewa wakaanza kutimua mbio!
kwa mbali akaonekana yule mzee kikonge akimtazama Laula kisha mzee huyo akazipiga hatua na kutokomea katika kichochoro!
Laula akamuona mzee huyo,,akashtuka! akajisemea moyoni,,"huyu aliniambia kuwa ni babu yangu,,huwa ananifuata nyakati za usiku na kunipeleka kuleeee!
Laula alijisemea maneno hayo huku akitimua mbio kwenda kumfuata babu yake! angalau ajue ni wapi anapoishi! kwa sababu huwa anamuona nyakati za usiku tu,,na sehemu anayopelekwa huwa hakuna nyumba hata moja,,hivyo hakuwahi kubahatika kumuona nyakati za mchana.
Laula alipofika katika kichochoro hicho,,hakumuona tena mzee huyo! akaangaza angaza macho yake huku na kule lakini hakufanikiwa kumuona! Laula akabaki akijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu! akaamua kuondoka eneo hilo na kuelekea katikati ya mji!
masaa yalizidi kusonga! na giza likaanza kutanda,,Laula akaamua kuketi nje ya kibaraza cha duka moja lililokuwa limefungwa,,,akajilaza hapo,,baada ya dakika kadhaa akapitiwa usingizi! akalala usingizi mzito,kutokana na uchovu aliokuwanao! baada ya masaa kadhaa kupita akaijiwa na ndoto katika usingizi!
akahisi kunamtu anagusa mkono wake,,akafumbua macho yake!
akamuona babu yake ndiye amemshika mkono!,, Laula akanyanyuka na kuongozana na mzee huyo! wakatoweka kimiujiza! na kujitokeza kando ya makaburi! Laula akastaajabu kuona makaburi mengi ,,,alioojaribu kutafakari hapo ni wapi? ghafla akahisi mkono wake umeshikiliwa kwa nguvu, tofauti na mwanzo! akaanza kuhisi maumivu katika mkono wake! akasema kwa sauti kavu,,"babu unaniumiza mkono wangu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
lakini mzee huyo hakuachilia mkono wa Laula,,akaendelea kumuongoza mpaka ktikati ya makaburi,,mbele ya kaburi moja wakasimama,,Laula akashindwa kuvumilia maumivu hayo,,akaanza kulia huku akinyanyua uso wake kumtazama babu yake! Laula akashtuka kumuona babu yake amebadilika na kuwa mifupa mitupu,,aliweza kuona hivyo kwa sababu mifupa hiyo ilikuwa inaang'ara kama saruji! akaingiwa na hofu! punde si punde lile kaburi lililokuwa mbele yao likapasuka na shimo likabaki wazi! Laula akapiga kelele!
mara ghafla ukimya ukatawala!!!!!!!!!!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment