IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA
*********************************************************************************
Simulizi : Shamba La Urithi
Sehemu Ya Kwanza (1)
katika nyumba iliyokuwa kando ya mto...zilisikika sauti za watu watu wakilia kwa uchungu..
kilio hicho kiliashiria kuwa katika nyumba hiyo kuna msiba..
akaonekana mke wa marehemu akiwa chumbani kwake kaketi juu ya kitanda akiitikisa maiti ya mumewe,,huku akilia kwa uchungu....Marehemu aliacha mke na watoto saba...watoto wa kike watatu,,na watoto wa kiume wanne...CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ikapigwa mbiu.kutangaza msiba.
kama ilivyokawaida,,kijijini mbio hiyo iliashiria kuwa kaya fulani kunamsiba..
Wana nzengo wakakusanyika nyumbani kwao Matiku..
majirani wakafanya mpango wa kuleta gari kwa ajili ya kubeba mwili wa marehemu kuupeleka mochwari...katika hospitali ya wilaya...na safari ya kuelekea mochwari ikaanza ..
watoto wa marehemu walisikitika san..walilia mfululizo.
******************
asubuhi palipokucha,, taratibu za mazishi ziliendelea...familia na ukoo wa marehemu Jebi wakakubaliana kuwa wazike leo hii hii...watoto wa marehemu wakasema mwili wa baba yao uzikwe kwenye shamba lake...
kauli ikapitishwa..kaburi likachimbwa katikati ya shamba la marehemu....
Ilipofika saa kumi za jioni..safari ya kwenda kuuzika mwili wa marehemu katika kaburi lililochimbwa katikati ya shamba la marehemu.
baada ya mazishi...majirani ndugu na jamaa wa karibu..wa familia ya marehemu..wakabaki nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya matanga..na kuifariji familia ya marehemu..
*************************
Baada ya arobaini kupita...zikafanyika taratibu za mirathi...lakini ndugu wa marehemu wakaanza kuwanyanyasa watoto wa marehemu pamoja na mama mzazi wa watoto hao ambaye ni ndugu wa marehemu...
wakawafukuza kwenye nyumba ya marehemu...
mama mzazi wa watoto hao aitwae Butogwa..aliamua kuwachukua watoto wake na kurudi kijibini kwao kwa baba na mama yake.....
maisha yalikuwa magumu sana kwa upande wao..kutokana na kukosa mahitaji muhimu kama pesa ya maradhi,,pesa ya huduma ndogi ndogo..pamoja na kukosa pesa ya watoto,,kwa ajili ya kuwalipia ada ya shule...
*****BAADA YA MIAKA MITATU(3) KUPITA*****
siku zilisonga hatimae ikapita miaka mitatu..ukoo wa marehemu Joramu...ukaamua kugawana mali lza marehemu pasipo kuwashirikisha watoto wala mke wa marehemu..
Marehemu hakuwa na mali nyingi,,alikuwa na Ng'ombe kumi na tano(15) na nyumba moja pamoja na shamba kubwa lenye ukubwa wa mita mia moja (100) za mraba..
kaka mkubwa wa marehemu..ambaye ndiye aliyetoa agizo kuwa familia ya marehemu. waondolewe ndani ya nyumba na kufukuzwa kwa sababu marehemu hakufunganga ndoa na mama wa watoto wake..hivyo wakagawana mali za marehemu...
Nyumba ya marehemu Joram akarithi dada wa marehemu...
shamba la marehemu,, akarithi kaka mkubwa wa marehemu..
Ng'ombe akarithi wadogo wawili wa kiume wa marehemu..
pia wakagawana pesa za Joram ambazo zilikuwa benki...
waligawana peaa hizo bila kutoa hata shilingi kuwapa watoto wa Joram!!
*************************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kaka huyo wa marehemu..aitwae Jazi akafurahi sana kwa sababu hakuwahi kupata shamba wala aridhi ambayo anaimiliki yeye mwenyewe..
akamua kulima mazao ya chakula...(mahindi na maharage) kutokana na ukubwa wa shamba hilo akaamua kuzitoa zile pesa zote alizogawana na ndugu zake,,,pia akatoa peza zake nyingine zote akawekeza katika kilimo cha mahindi katika shamba la irithi,,alilowadhurumu watoto wa marehemu Joram.
akalipa pesa kwa ajili ya shamba lake kulimwa kwa Trekta.....shamba likalimwa..na kupandwa Mbegu za maharage na mahindi....
Jazi,,alilitembelea shamba lake mara kwa mara..kuangalia maendeleo ya mazaao ya shamba lake,, alifurahi sana..baada ya kuona mazao yanaendelea vyema....pia mvua ilikuwa inanyesha mfululizo......akajisemea moyoni,,"kijiji kizima kitanikoma..nikivuna mazao haya..nitapasa pesa nyingi....watanijua mimi ndiye Jazi...tajiri wa kijiji hiki....
baada ya miezi kadhaa kupita Jazi alivuna..mavuno..akapata mavuno mengi sana kuliko wanakijiji wote..kutokana na ukubwa wa shamba hilo.....akafurahi sana,,akauza na kujipatia mamilioni ya pesa..kipato chake kikaongezeka mara tano zaidi..akawa na pesa nyingi....akaanza majigambo....
siku moja,,Butogwa ambaye ni mke wa marehemu
alipata maradgi ya ghafla..akapoteza fahamu...baba mzazi wa wa Butogwa..akafanya mpango wakamkimbiza haraka kwenye kituo cha afya (Dispensary) kwa ajili ya kuokoa maisha yake..walipomfanyia vipimo..ikagundulika kuwa anauvimbe ndani ya ubongo wake!..hivyo atalazimika kupelekwa kwenye hospitali ya mkoa kwa ajili ya upasuaji.. baba mzazi wa Butogwa akapata mstuko naada ya kusikia taarifa hito..kuwa mwanae lazima afanyiwe upasuaji kichwani....
taarifa hiyo ikamfanya apatwe na shinikizo la damu ghafla(presha) akadondoka chini na kupoteza maisha papo hapo...
mmoja kati ya watoto wa marehemu..aitwae Pamera, akatimua mbio kurudi nyumbani kumpa taarifa bibi yakw kuwa babu yao amefariki!!!
bibi pia akashtuka akapatwa mshtuko wa moyo akadondoka chini na kupoteza fahamu!!!
majirani wakamkimbiza haraka bibi huyo kwenye kituo cha afya...lakini walikuwa wamechelewa...bibi huyo alifariki dakika chache zilizopita kabla hajapelekwa kwenye kituo cha afya.
likawa pigo kubwa kwa watoto hao..baada ya kumpoteza babu na bibi kwa wakati mmoja...
Pamera akaamua kwenda kule kwa baba yake mkubwa kutoa taarifa...pia akaomba msaada wa kifedha ili mama yao Butogwa afanyiwe upasuaji...
lakini Baba yake mkubwa akamfukuza Pamera huku kumpiga kipigo kizito kama mwizi...kisha akasema,,"nisikuine tena hapa nyumbani kwangu...tena nenda kawaambie hao kunguni wenzako wasithubutu kukanyaga nyumbani kwangu..
Pamera akaondoka huku akilia kwa uchungu huku akiugulia maumivu makali..kutokana na kipigo alichopigwa na baba yake mkubwa....alipofika kule hospitali akakuta mama yake kafariki dakija mbili zilizopita....Pamera alilia kwa uchungu mkubwa....kwa sababu Pamera alikuwa ni mkubwa katika uzwa wa familia yao akajitahidi kuwafariji wadogo zake..kwa kuwaambia maneno ya faraja.
kesho yake zikafanyika taratibu za mazishi...
kwa kweli lilikuwa pigo kubwa kwa Pamera nacwadogo zake sita(6) kwa kuwapoteza bibi na babu pamoja na mama yao mzazi kwa siku moja..
******BAADA YA MIEZI MITATU KUPITA*******
Pamera na wadogo zake waliishi kwa shida sana.ikafika kipindi wakawa wanakosa hata mlo kwa siku,,kutokana na kukosa msaada wala hakuna kati yao aliyekuwa na kipato.. Pamera akaamua kutadura vibarua vya kulima mashamba ya watu..na kufanya usafi katika mashamaba ya watu ili aweze kupata pesa ya kuwasaidia wadogo zake.....waweze kupata mlo na lesa ya lujikimu.
maisha yaluwa magumu kupita kiasi..wakati mwingine Pamera alifanyishwa kazi siku nzima bila malipo..
*******BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA******
Msimu wa masika ukawadia(mvua za mfululizo)
Jazi ambaye ni baba mkubwa wa Pamera akaajiri watu walime na kupanda mbegu za mazao ya mahindi na maharage...kazi hiyo ilifanyika ndani ya siku nne..kwa sababu shamba hilo lililimwa kwa Trekta na kupandwa mbegu na watu wengi..waliowalipa kuifanya kazi hiyo.
Jazi alifurahi sana kwa sababu shamba lake lililiandaliwa kwa siku chache na kupandwa mbegu. tofauti na mashamba ya wanakijiji wengine.....
Miezi ilizidi kusonga,,Jazi akawa anakwenda kwenye shamba lake kutazama maendeleo ya mazao yake yaliyopandwa katika shamba lake la urithi...
siku ya leo aliamua kuingia ndani ya shamba kukagua...alitembea mpaka katikati ya shamba hilo...alipoangaza angaza macho yake kutazama mazao yake..shamba likabadilika na kuwa msitu wenye giza na miti mikubwa kupita kiasi..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akaingiwa na hofu kubwa akatazama huku na kule hakuona njia..akaanza kupiga mayowe ya uwoga huku akitimua mbio bila kujua ni wapi anaelekea...
alikimbia masaa mawili mfululizo akajikuta katokezea nje ya msitu huo wenye giza kiasi..akageuza shingo yake kutazama msitu huo..akastaajabu kutokuona tena ule msitu..sasahivi lilionekana shamba la kawaida..
macho yakamtoka akatimua mbio kurudi nyumbani kwake....akamsimulia mkewe...mkewe akamshawishi waende kwa mganga kuchunguza tatizo ni nini? mkewe akamuelekeza ni wapi mganga anapatikana.
Jazi akasema,,"kesho mapema nitakwenda.
**********************
Asubuhi palipokucha safari ya kwenda kwa mganga ikaanza..Jazi akachukua baiskeli yake na kuelekea kwa mganga..
Mganga huyo anapatikana kwenye milima ya DONGOBESHI.
aliendesha baiskeli yake kwa mwendo wa masaa matatu mfululizo..hatimae akafika milima ya DONGOBESHI...akafanikiwa kumkuta mganga mchawi....
Jazi akaelezea shida yake kwa mganga..
mganga huyo akaanza kupiga Tunguri zake..kisha akamtazama Jazi na kusema,,"kunatatizo kubwa sana ambalo umelisababisha wewe mwenyewe...umedhurumu mali isiyokuhusu...
Jazi akashtuka!!! kusikia maneno hayo kutoka kwenye kinywa cha mganga...
Jazi akauliza kwa mshangao,,"TATIZO?? je? ni tatizo gani hilo?
mganga akasema,,"Ndio ni tatizo tena kubwa kuliko,,ambalo litasababisha kuondoa uhai wako..
Jazi akadakia,,"Naomba unisaidie mganga..nitakulipa kiasi cha pesa unachokitaka.
mganga akachukua chungu cheusi..akasema sitaki pesa yako...lakini nitakusaidia,,na ukifanikiwa,,utarudi kuleta shukrani kwa mizimu..utaleta kuku mweupe na mayai ya kobe..
Jazi akasema,,"hakuna tatizo mganga...naomba maelekezo nini cha kufanya?
mganga akasema..nitakupa dawa lakini kwa masharti.....dawa hii nitakayokupa..hakikisha unaichanganya na mchanga uliyokanyagwa kwa unyayo wa mtoto yoyote wa familia ya mmiliki halali wa shamba ulilodhurumu..kisha mchanga huo utaunyunyizia dawa hii na kuumwanga kwenye jiko linalowaka moto...mtoto mwenye unyayo huo..atakufa siku hiyohiyo..kisha lazima azikwe kwenye hilo shamba...
kwa kufanya hivyo..utakuwa umeuwa nguvu za mzimu wa marehemu aliyekuwa anamiliki shamba hilo...kisha mganga akamkabidhi Jazi kijiko na kikopo cha plastiki kipana kiasi..akasema,,"usichote mchanga huo kwa viganja vyako..tumia kijiko hiki..alafu tumbukiza mchanga huo kwenye kikopo hiki.
Jazi akashtuka akasema,,"sasa huo mchanga nitautoa wapi?
mganga akasema,,"hiyo hainihusu ni kazi yako..
wajibu wangu ni kutekeleza kazi yangu ya kukusaidia.
************************
Upande mwimgine kule kwenye nyumba ya marehemu babu na bibi yao Pamera..walionekana wadogo zake pamera wakiwa wamebeba vidumu kuelekea mtoni kutekaaji....wakati huo Pamera alikuwa amekwenda kutafuta kibarua ili aweze kulata pesa ya kuwapatia chakula wadogo zake sita....
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwabali alionekana mke wa Jazi akija katika nyumba hiyo,,alikuwa ameleta ujumbe kuwa,,Pamera aende kuchukua nguo zao zilizobaki katika ile nyumba ya marehemu Joram..
lakini akakuta mlango umefungwa...akaamua kuchukua kipande cha mkaa kilichokuwa kando ili aandike ujumbe huo ukutani..kama Pamera akifika aweze kuona kwa urahisi na ausome ujumbe huo..wakati anafuata kilande hicho cha mkaa..ghafla akakanyaga kipande cha chupa iloyovunjika...ikatoboa ndala na kumchoma kwenye unyayo..akahisi maumivu makali akavua haraka ndala akakanyaga chini kwenye mchanga.
akaacha kuendelea kukifiata kile kipande cha mkaa akashikilia mdara moja mkononi..akachechemea na kuondoka zake kiridi nyumbani kwake..
**********************
Upande mwingine alionekana Jazi akiwa anaendesha baiskeli yake akitokea kwa mganga...
akiwa njiani alikuwa anapanga mikakati ya kuupata mchanga uliokanyagwa kwa unyayo wa mmoja kati ya watoto wa arehemu Joram.
akaamua kununua matunda ili iwe janja ya kuingia nyumbani kwao Pamera.
baada ya mwendo wa masaa mawili kupita akaikaribia nyumba hiyo..alipotazama kwa mbali akaona mlango umefungwa...akafurahi sana akajua kuwa hakuna mtu ndani ya nyumba hiyo...akashuka haraka kutoka kwenye baiskeli..akaanza kutazama chini akitafuta alama za nyayo..ghafla akaona alama ya unyayo na kando kuna matone ya damu...akachukua kile kikopo akafungua ufuniko akachota mchanga huo kwa kijiko..akauweka ndani ya kikopo na kufunika ufuniko..akapanda baiskeli yake na kuelekea nyumbani kwake...
akiwa njiani alionekana kuwa na furaha sana,,akajisemea moyoni,,"kwisha habari yao..mimi ndiye Jazi.
Baada ya nusu saa kupita..akafika nyumbani kwake..akaingia jikoni akawasha jiko la kuni....kisha akachukua ile dawa aliyoambiwa aichanganye na mchanga huo..kisha akaumwaga mchanga kwenye moto.......baada ya dakika tano kupita..akatoka jikoni na kuelekea mdani ya nyumba yake....alipoingia sebuleni...mara ghafla Macho yakamtoka.....
Jazi akahisi kuchanganyikiwa baada ya kumuona mkewe kadondoka chini huku povu jeusi likimtoka mdomoni...Jazi akajaribu kumtikisa mkewe huku akimuita jina lake....lakini tayari alikiwa ameshakufa dakika chache zilizopita.
Mazi akatoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi...
bila kuchelewa ikaligwa mbiu ya msiba kuwajulisha wanakijiji waote....wakakusamyika na taratibu za mazishi zikaendelea....
******BAADA YA WIKI MOJA KUPITA******
Jazi akaamua kwenda kule kwenye shamba lake la urithi,,alipofika alistaajabu kukuta shamba lipo tupu uyadhani hapajawahi kulimwa wala kupandwa mahindi!!!
Jazi akaingiwa na hofu..akakumbuka maneno ya mganga kuwa...aanaweza kupoteza uhai...akaamua kwenda nyumbanikwao Pamera,,
alipofika alimkuta Pamera na wadogo zake..wakiwa wanakula ugali na chumvi...
Jazi akasema,,"Pamera mwanangu,,nimeamua kurudisha mikononi mwenu lile shamba la marehemu baba yenu...kisha akaondoka bila kuaga...
taarifa hiyo ilikuwa njema kwa Pamera na wadogo zake...wakafurahi sana...pamera akaacha kula akatimua mbio kuelekea kule shambani huku wadogo zake wakimfuata kwa nyuma.
baada ya dakika kadhaa kupita walifika shambani
wakafurahi sana kuona mahindi na maharage yamestawi!!...
Pemera akajisemea moyoni,,"baba mkubwa anatujaribu au kweli kadhamilia kutula shamba letu? wacha tuone.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Miezi ilizidi kusonga,,hatimae msimu wa mavuno ukawadia...
siku ya leo Jazi alikwenda kwenye shamba hilo..ili aone kama yale mahindi na maharage yaliyotoweka kimiujiza je yapo?
akastaajabu kukuta yapo!!! Jazi akaingiwa tamaa.akaamua kukodi watu,,akawalipa pesa wavune mahindi na maharage yote shambani humo....
kazi hiyo ilifanyika siku tatu mfululizo!! kutokana na ukubwa wa shamba...wakawa wamemaliza kuondoa mahindi na maharage shambani humo.
Jazi alipata mazao mengi sana..zaidi ya magunia mia moja(100) akayaweka latika ghala.akisubiri kuyauza ili ajipatie pesa..
*************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment