IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA
*********************************************************************************
Simulizi : Chozi La Ukombozi
Sehemu Ya Kwanza (1)
Mwanadada aitwae NINO baada ya kusafiri kwenda OMAN (nchi ya kiarabu) yeye pamoja na jirani yake ambae alikuwa ni mtu wa karibu wa familia yao""""",,,,, walipofika OMAN baada ya mwezi mmoja kupita Nino alipata kazi ya u-house girl(mtumishi wa ndani) katika nyumba ya kifalme.... kijana mkubwa ambaye ni mtoto wa mfalme alimpenda NINO wakaanzisha mahusiano ya chinichini...hatimae NINO alishika ujauzito... na ilipokaribia miezi tisa(9) siri ilifichuka"" na mfalme ilipogundua aliamuru NINO atoswe baharini... Na Amri ya mfalme ikatekelezwa nino alitoswa baharini huku akiwa na mimba ya kukaribia kujifungua... mfalme alifanya hivyo kwa kuhofia ukoo wa kifalme kwenda mashariki ya mbali.
mvuvi mmoja alimsadia NINO alimuona baharini wakati anaviwa samaki... alimchukuwa na kumpeleka nyumbani kwake..mvuvi huyo alimpa msaada wa kumuhifadhi nyumbani kwake....ilipofika majira ya saa moja usiku nino alizinduka na kupata fahamu... alistahajabu kujikuta yumo mdani ya chumba akiwa peke yake..
punde alitokea yule mvuvi aitwae Abdul....kisha akaanza kumsimulia nino yaliyompata.. kumbukumbu ilirejea nino alikumbuka kuwa alitoswa baharini...
************
kule kwenye jumba la kifalme.. prince Moddy ambaye ni kijana mkubwa wa mfalme alionekana kuwa mwenye huzuni... baada ya nino kutoswa baharini... kwani alitokea kumpenda sana nino...aliumia sana kwa sababu nino alikuwa na ujauzito wake...alimlaumu sana baba yake lakini hakuna namna... amri ya mfalme haipingwi.....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
baada ya mwaka mmoja kupita ilitokea vita...wanajeshi wengi wa falme ya GHEMI waliuwawa vitani...vita ile ilitokewa baada ya kuwa na utata mkubwa wa kugombania mpaka. uliopita katikati ya bahari...falme ya GHEMI walidai kuwa mpaka huo upo ndani ya eneo lao...na falme ya BEHA walidai kuwa mpaka huo upo ndani ya eneo lao..... baada ya mzozo wa miaka mingi falme hizo ziliamua kupigana vita na atakayeshinda vita..ndiye atakaye miliki mpaka huo....
***********
kule upande wa Dhaho alipokuwa akiishi yule mvuvi Abdul.. Nino alijifungua salama mtoto wa kiume aliamua kumpa jina la babu yake aitwae
KOMBA... kwa sasa alikuwa anatimiza mwaka mmoja na miezi kadhaa.. nino alimpenda sana mwanae...kwa kuwa mvuvi yule hakuwa na mke aliamuwa kuishi na nino kama mke na mume.... Abdul alimpenda sana komba aliona ni kama mwanae wa kumzaa... waliishi kwa amani na furaha siku zote....
Prince moddy alikuwa akimkumbuka sana nino picha ya nino haikufutika kichwani mwake.. lakini alikuwa akiamini kuwa nino hajafa na kuna siku atamuona nino...
*************
Komba aliendelea kukuwa vyema..na sasa ana umri wa miaka minne.. sikumoja Abdul alikwenda kuvua samaki baharini.... alitega nyavu zake lakini aliambulia patupu... aliamua kusonga mbele zaidi akiwa humo baharini mvua kubwa ilinyesha huku ikiambatana na upepo mkali.. Abdul aliamua kushusha Ngarawa(kitambaa kikubwa cha kukusanya upepo kwenye mashuwa)
mvua ilikuwa kubwa na upepo ulizidi kuvuma kwa kasi ya ajabu... upepo huo uliweza kukusanya maji na kutengeneza mawimbi makubwa... punde wimbi lilipiga mashua ya Abdul..kutokana mashua hiyo ilitengenezwa kwa kutumia mbao ilipasuka upande mmoja na maji yakaanza kuingia ndani ya mashua... hatimae ilizama baharini kwa sababu mawimbi ya maji yalikuwa makubwa.. Abdul hakuweza kujiokoa punde alipoteza maisha kwa kumeza maji mengi na kukosa pumzi...
wakati huo huo wanajeshi wa falme ya BEHA walivamia kisiwa cha Dhaho ambacho kilikuwa katika eneo la falme ya Ghemi....wanajeshi hao waliuwa kila mtu aliyekuwepo eneo hilo...
nino alikimbia yeye na mwanae komba wakajificha...nino alimficha komba kunako mashua zilizokuwa zimepaki pembezoni mwa bahari misha nino akakimbia kuelekea upande mwingine.....
mwanajeshi mmoja alimuona nino wakati akikimbia.. mwanajeshi yule alichukua upinde na mshale akamlenga nino shingoni.... nino alidondika chini.... komba alikuwa anashuhudia tukio zima... kwa sababu kipindi mama yake anakimbia komba aliinua kichwa kuchungulia ni wapi mama yake anaelekea...komba alishuhudia wakati mama yake anapigania pumzi ya mwisho kisha akakataroho... komba alilia. akapaza sauti akimuita mama yake MAMA"""..yule mwanajeshi alisikia sauti hiyo akaelekea kule sauti ilipotokea...
mara ghafla.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara ghafla mkuu wa majeshi ya falme ya BEHA. aliamuru waondoke na amri ikatekelezwa"" hiyo ilikuwa ponapona ya Komba..aliendelea kujificha hapo mpaka alipohakikisha hakuna hatari yoyote..kisha komba akatoka pale alipokuwa kajificha na kuaza kutimua mbio.. kuelekea pale alipokuwa amedodondo mama yake... komba alimuamsha mama yake lakini hakuamka kwani tayari alikuwa ameshakata roho"",, komba alilia sana aliendelea kubaki hapo mpaka usiku ukaingia...komba alianza kuhisi njaa... aliamua kutimua mbio na kwenda nyumbani kuchukuwa chakula alichopika mama yake kabla hajafa"" komba alichukuwa chakula na kurudi mbio kule alipomuacha mama yake... alipofika alimpa chakula mama yake"" lakini mama uake alikuwa kimya...komba aliamini mama yake yuhai... kisha komba akaanza kula chakula huku akimlisha mama yake... alistahajabu mama yake hatafuni chakula.. komba aliendelea kula na alipohisi ameshiba... alijilaza juu ya kifua cha mama yake..
baada ya masaa machache komba alipitiwa usingizi..kutokana walikuwa ufukweni mwa bahari.. hivyo upepo uluvuma mfululizo.. komba alishindwa kuvumilia baridi hilo aliamka. na kumuamsha mama yake waende nyumbani.. nino hakuamka kwa sababu alikuwa amekufa.. komba aliamua kuondoka na kuelekea nyumbani....komba aliingia mpaka ndani akachukua shuka kisha akatoka nje... alikimbia kuelekea kurudi kule alipokuwepo mama yake... komba alimfunika mama yake kisha naye akajilaza kando huku kichwa chake kakiweka juu ya kifua cha mama yake.... wakali huo wote komba aliamini mama yake yuhai ila amelala tu... asubuhi palipokucha komba aliamka na kumuamsha mama yake.. lakini bado hakuamka..komba alihisi ule mshale uliokuwa umeingia ndani ya shingo ya mama yake huenda ndio unasababisha mama yake asiamke.. aliuvuta na kuuchomoa mshale ule.. alistahajabu kuona tudu lililotokeza upande wa pili kwenye shingo ya mama yake...komba aliogopa sana.. aliamua kutimua mbio atafute mtu ili ampe msaada mama yake....
*************
komba alikimbia umbali mrefu sana kutokana hapakuwa na mtu kwenye kisiwa lile cha Dhoha... kwani wote waliuwawa na majeshi ya falme ya BEHA... kwa mbali alimuona babu mmoja alimfata na kumwambia kuwa aende akamsaidie mama yake kaumia shingoni... babu yule aliingiwa na huruma.. aliamua kwenda kuona alichoambiwa na mtoto komba..
walipofika yule babu alipomuangalia nino aligundua kuwa nino alikiwa amekufa masaa mengi yaliyopita. ilibidi amwambie komba kuwa mama yako amekufa... komba alilia sana ingawa hakulichukulia kwa uzito jambo hilo kitokana na umri wake mdogo....
babu yule alimuonea huruma komba aliamua kumchukua akaondoka nae na kuanza kumlea..
******BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA******
babu yule kumbe aliwahi kuwa mwanajeshi katika jeshi la falme ya GHEMI....hivyo alijua vyema mbinu za upiganaji.. alianza kumfundisha Komba kupambana kwa kutumia upanga.. na mbinu mbalimbali za upiganaji. Komba alianza kuweza kupambana vyema.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Komba alikuwa mtoto hodari sana.. alikuwa mkarimu na mwenye busara... hakuwai kumkosea mzee yule... yule mzee aitwae Ramuh alimpenda sana komba aliikumbuka sana familia yake... kumbukumbu ilimuijia miaka 30 iliyopita aliwahi kuwa mkuu wa majeshi katika falme ya GHEMI... alikuwa mtiifu kwa mfalme... mfalme alimpenda sana alimuamini kwa kila jambo alilomwambia pia alimuamini kwa kila jambo alilolifanya... mfalme wa Ghemi alikuwa na kijana mkubwa aitwae mazy kabla hajazaliwa prince mody.. Ramuh alikwenda kupigana vita akiwa yeye pamoja wanajeshi wake...ramuh alilipanga vyema jeshi lake na kulipa muongozo na mbinu za kushinda vita hiyo... mbinu ya ramuh iliwafanya washinde vita nakurudi ghemi wakiwa hai bila kufa hata mwanajeshi mmoja... mfalme alistahajabu sana kuona wanajeshi wake wamerudi hai hakufa hata mmoja vitani.. .. kwa sababu aliamini jeshi lake litashindwa... hivyo aliamua kumpa ramuh uwongozi wa juu katika tawala yake..... mazy alianza kuingiwa tamaa na wivu juu ya ramuh..kwanini apewe uwongozi wa juu.. wakati yeye yupo... mazy aliamua kupanga njama ya kumuharibia ramuh mahusiano ya karibu na mfalme.... sikumoja aliba box lenye ramani ya nchi yao na kumwambia mfalme kuwa amemuona ramuh akiiba box hilo... mfalme alikasirika sana na kuamuru ramuh auwawe adharani kwa kunyongwa....siku moja kabla ya hukumu kutekelezwa.. ramuh aliamua kutoroka na kutokomea kusiko julikana huku akiacha mke na mtoto wa kiume katika falme ya ghemi....usiku huohuo mazy alivamia nyumba ya ramuh na kuchinja mke na mtoto wa ramuh......ramuh alikwenda kuishi mbali na falme ya ghemi... na hakuwahi kuoa wala kuwa na mtoto tena.. ramuh ambeye kwa sasa ni mzee wa miakasitini(60)aliona kile kitendo cha nino kutoswa baharini... siku ile komba alipomuomba msaada aende akamsaidie mama yake.. mzee ramuh alimkumbuka nino..na baada ya kugundua amekufa aliamua kumchukua komba na kumlea..
*******BAADA YA MIAKA ISHIRINI KUPITA*******
komba alikuwa katimiza miaka 25...alikuwa kijana mkubwa hodari shupavu na mwenye nguvu....komba alikuwa akijishughulisha na uvuvi... sikumoja akiwa baharini akivua samaki... kwa mbali aliona mashua mbili.. lakini alipotaza kwa umakini aligundua mahala pale hakuna amani... aliiongoza mashua yake haraka kuzifuta mashua zile.. alipofika aliona watu wakipigana.... kumbe mtoto wa mfalme wa ghemi alikuwa kavamiwa na wanajeshi wa falme ya goha..komba aliingilia kati kuwasaidia wanajeshi wa ghemi walikuwa wameuwawa na kubaki wanajeshi wawili pamoja na prince mody..komba aliwapiga wanajeshi wa goha kwa dakika chache... aliwauwa wote... prince mody alistahajabu sana mtu huyo ananguvu za aina gani... hakujua kuwa ni mtoto wake wa damu.. prince mody aliamua kuondoka na komba mpaka kwenye jumba la kifalme.. walipofika... prince mody alimsimulia mfalme yale yaliyotokea katika safari yao.. mfalme alifurahi alimshukuru komba kwa kuokoa maisha ya mwana wa mfalme... aliamua kuwa kuanzia siku hiyo komba aishi katika jumba la kifalme.. prince mody alifurahi komba kubakia hapo katika jumba la kifalme...
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Komba alimuomba mfalme arurudi nyumbani kutoa taarifa kwa mlezi wake... mfalme alimruhusu kisha akasema wewe pamoja na mlezi wako mtakuwa mkiishi humu katika jumba la kifalme.... komba alifurahi sana kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani katika kisiwa cha Dhaho.. komba akiwa njiani alivamiwa na wanajeshi wa falme ya Beha komba alipambana nao akawazidi nguvu waliamua kupanda farasi na kutokomea kusikojulikana... komba alizipiga hatua mpaka nyumbani alimsihi mzee ramuh kuwa wahamie kwenye jumba la kifalme...ramuh alikubali... na safari ikaanza ya kwenda kwenye jumba la kifalme....
**********
upande mwingine walionekana wanajeshi wa falme ya Beha wakiwa wamevamia kijiji kilichokuwa mpakani mwa GHEMI na BEHA watu wa kijiji hicho waliuwawa mpaka watoto wadogo wasiokuwa na hatia..... wanajeshi wale waliuwa kwa kuchinja shingo na kuchoma mikuki... kwa mnali alionekana Mtu mmoja kati ya wanajeshi wa Beha akishuka kutoka kwenye farasi na kuelekea upande mwingine alionekana akimfuata mwanamke mmoja aliyekuwa akikimbia huku kambeba mtoto wake mchanga kwa ajili ya kuokoa maisha yao.... mwanajeshi yule alimkamata mwanamke yule na kumnyang'anya yule mtoto mchanga aliyekuwa kam-beba kisha akamchinja mtoto yule... yule mama alilia sana huku akijaribu kumpiga mwanajeshi hiyo..
aligeuka na kumpiga mtama aina ya Kombati... mtama huu wanautumia sana watu wanaofanya mazoezi ya mchezo wa JUDO.. mwanamke yule alianguka chini... kisha mwanajeshi yule akaanza kum-baka mwanamke yule.. na baada ya kumaliza haja yake alichomoa upanga na kumchinja mwanamke yule... aisee yalikuwa ni mauwaji ya kikatili sana.
kumbe mwanajeshi huyo ndiye yule mtoto wa kwanza wa mfalme wa Ghemi aitwaye MAZY... alitoroka na kujiunga na jeshi la falme ya Beha baada ya kujaribu kupindua ufalme wa baba yake.. kutokana alikuwa hajajipanga vyema hivyo alishindwa... na kuamua kutoroka na kutokomea kusikojulikana.... alipojiunga na jeshi la falme ya Beha mfalme wa Beha aliamua kumpa wadhifa wa uwaziri katika tawala yake...mfalme huyo alifanya hivyo ili awe karibu nae na ampe ramani ya kuingia kwenye falme ya Ghemi kupitia milango ya siri.... kisha akawa anajipanga kuandaa jeshi tangu miaka 30 iliyopita....
***********
Ule upande mwingine alionekana komba pamoja na mzee ramuh wakiwa katika farasi kuelekea falme ya Ghemi... baada ya lisaa limoja kupita walifika...walifunguliwa lango kuu na kuingia ndani.
(DAMU NZITO KULIKO MAJI) princy mody alifurahi sana kila alipokuwa akimuona komba... aliwapokea na kuwakaribisha ndani kunako jumba la kifalme..... mzee ramuh alikuwa akiijua siri yeye peke yake kuwa Komba ni mtoto wa damu wa prince mody.. kwa sababu siku nino anatoswa baharini alikuwa akishuhudia tukio zima pia aliona nino anatoswa baharini huku akiwa mjamzito.. na miaka 20 iliyopita wakati komba alipomfata kumuomba msaada akamsaidie mama yake alipofika kule ufukweni alimkumbuka nino. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
na ndio maana aliamua kuondoka na komba na kuchukua jukumu la kumlea....
komba aliishi hapo huku akiendelea kufanya mazoezi pamoja na jeshi ya Ghemi... alionekana kuwa mwenye mbinu nyingi za upiganaji.. mfalme alifurahi sana kumpata mtu hodari na shupavu...mfalme alizidi kufurahishwa na kupendezwa na matendo ya komba.. aliamua kumpa uwongozi wa kuliongoza jeshi la ghemi... siku moja komba akiwa katika matembezi kwenye msitu mmoja.. kwa mbali aliona jeshi kubwa la Falme la Beha wakija kwa kasi upande wa falme ya ghemi.. aliweza kuwaona kwa sababu Ghemi ilikuwa kwenye muinuko wa milima mikubwa.. komba aliopo ona hivyo alirudi haraka kwa mfalme na kutoa taarifa ya kile alichokiona... mfalme aliamuru jeshi lake likae tayari watarajie kutokea kwa vita muda wowote kuanzia sasa jeshi la Ghemi lilijipanga baraabara na lango kuu likafunguliwa kisha wanajeshi wote wakatoka huku wakiwa juu ya fasi... wakiongozwa na Komba... walifika kwenye uwanja wa vita... na vita ikaanza... walipigana takribani masaa sita.. jeshi la falme ya Beha lilionekana kuzidiwa mbinu za upiganaji na jeshi la falme ya Ghemi... wanajeshi waliosalia waliamua kupanda farasi na kutimua mbio....baadhi ya wanajeshi wa ghemi waliuwawa lakini kwa idadi ya watu wachache tofauti na wanajeshi wa beha...mkuu wa jeshi la beha ambaye ni Mazy alimuangalia Komba kwa jicho la chuki.... huku akimnyooshea upanga kisha akapanda farasi na kutokomea..
*************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment