Search This Blog

SUNDI - 3

 







    Simulizi : Sundi

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Mbigili akawa wakwanza kumuona Dereva huyo akamkumbuka!

    akanyanyuka harakaharaka,,akajifanya anafanya mazoezi ya kurukaruku,,huku kageuza mgongo wake ukitazama upande wa getini,,,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mbili aliamua kufanya hivyo ilimradi,,yule dereva asimuone!

    Bi'Sundi akastaajabu sana,,kisha akatabasamu,,akamshukuru Mungu kwa kumponya mwanae mpaka kapata nafuu,,na sasahibi anaweza hata kurukaruka,,tofauti na hali aliyokuwanayo mwanzo!



    Dereva huyo akaendelea kuzipiga hatua kuelekea katika wodi ya wanawake! kutazama hali ya dada yake ambaye ni mgonjwa mahututi..



    Mbigili akawa anamtazama dereva huyo kwa makini,,alipohakikisha dereva huyo kaingia katika wodi za wanawake.....

    akapata mwanya wa kutoka eneo hilo la getini..akamawambia mama yake,,"nahitaji kurudi wodini kwa ajili ya mapumziko!

    Bi'Sundi hakuwa na kipingamizi akanyanyuka na kuongozana na Mbigili,,lakini akastaajabu kumuona Mbigili anatembea harakaharaka huku uso wake ukionekana kuwa na wasiwasi!

    (UTU UZIMA DAWA) bi'Sundi akagundua kuwa mwanae hayupo sawa kifikra,,akaamua kumuuliza,,"mbona unaonekana hauna amani? nini kimekusibu,,,naona furaha yako imetoweka ghafla.

    Bi'Sundi aliongea maneno hayo kwa kilugha,,lakini Mbigili alielewa kile anachomaanisha mama yake!

    hakujibu kitu chochote,,aliendelea kuzipiga hatua za harakaharaka,,akamuacha mama yake umbali mrefu...akaingia ndani ya wodi aliyokuwemo mwanzo...akapanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi..pumde si pumde akaimgia daktari kuangalia maendeleo ya hali ya  hali ya Mbigili.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upande mwingine kule kwenye wodi ya wanawake,,alionekana yule dereva akiwa kasimama kando ya kitanda alichokuwa kalala dada yake,,alisikitika sana kumuona dada yake akiwa katika hali ya kutoridhisha,,kiukweli alikatisha tamaa kwa sababu alikuwa haongei wala hafumbui macho,,,baada ya dakika kadhaa,,,mwanamke huyo akaonekana,,akitapatapa,,akirusha miguu na mikono!

    dereva huyo akashtuka,,,alipomtazama kwa makini dada yake akagundua kuwa anapigania pumzi.....akaamua kutimua mbio kutoka ndani ya wodi hiyo kwenda kumuita daktari...

    alipofika katika ofisi za kituo hicho cha Afya,,akamukuta nesi mmoja,,, akalazimika kutoa taarifa kuwa mgonjwa wake anahangaika kule wodini..anarusha miguu na mikono mtululizo!

    nesi akasema,,"wacha mimi niende kutazama hali yake,,alafu wewe nenda katika wodi ya wanaume kamuite daktari,yupo kule anaangalia hali za wagonjwa!

    Dereva huyo akatimua mbio kuifuata woei ya wanaume....

    alipoikaribia wodi hiyo,,, akaigia kwa pupa ahuku akisema,,"DAKTARI NAKUOMBA UKAMUANGALIE DADA YANGU..tafadhali hali yake si shwari!

    Bila kuchelewa daktari huyo akatoka haraka ndani ya wodi hiyo...

    wakati dereva huyo anaongea maneno hayo,,alikutanisha macho na Mbigili,,,lakini kutokana na kuchanganyikiwa kwa sababu ya hali mbaya ya dada yake,,hakuweza kumtambua Mbigili kwa harakaharaka,, akaongozana na daktari huyo mpaka katika wodi ya wanawake!

    Manesi wakisaidia na daktari huyo,,j'ykoa uhai wa mwanamke huyo..wakaamua kumkimbiza kwenye chumba cha wagonjwa mahututi wanaohitaji msaada wa pumzi kwa kutumia mashine.(Oxygen)!

    wakamuweka ndani ya chumba hicho(I.C.U)

    qakati huohuo dereva huyo alibaki nje,,akiwa katika dimbwi.la mawazo,,,ghafla wazo likqmjia kuwa alimuona mtu kule katika wodi ya wanaume,,mtu huyo anafanana na mtu aliye muuwa rafiki yake!!!

    wakati anawaza hayo,,akamuona daktari anatoka kwenye kile chumba alichokuwa ameingizwa dada yake...akaamua kumfuata daktari,akamuuliza hali ya dada yake,,anaendeaje?



    Daktari akainamisha uwo wake chini,,kisha akasema,,"nasikitika sana kukutaarifu kuwa dada yako amefariki dunia.

    Dereva huyo akahisi kuchqnganyikiwa...

    baada ya dakika kadhaa manesi wakafanya taratibu za kuipeleka maiti mochwari..



    wakati huo huo,,kule katika wodi aliyokuwemo Mbigili...akaonekana kukosa amani,,,akajisemea moyoni,,"nipo matatani,,bila sha mtu yule ameniona,,ninaimani amtatoa taarifa kwenye vyombo vya dora,,,wacha nifanye jambo...

    akanyanyuka na kumwambia mama yake kuwa amepona anahitaji kurudi nyumbani muda huohuo..

    Bi'Sundi akasema,,"wacha tumsubiri daktari,,aje kutoa ruhusa,,

    Mbigili akasema,,"mimi naondoka kama unamsubiri daktari wewe msubiri tu.

    aliongea maneno hayo huku akitoka nje ya wodi hiyo,,,

    kwa mbali akamuona yule dereva akitokea upande wa mochwari,,akajisemea moyoni,,"huyu bwege..lazima nimfanyie kitu mbaya,,bila kufanya hivyo sitaishi kwa amani,,na nitakuwa matatani kukamatwa....

    Mbigili akaamua kutoka nje ya geti hilo,,,,pumde si punde yule dereva naye akatoka nje ya geti hilo,,akazipiga hatua huku akiwa na huzuni ya kifo cha dada yake! akajikuta anatembea kwa miguu...kuelekea nyumbani kwa marehemu dada yake,,,kutokana na umbali aliokuwa anaishi dada yake,,,dereva huyo alilazimika kupita katikati ya pori kuelekea nyumbani kwa dada ya lke kwa ajili ya maandalizi ya msiba...

    kumbe Mbigili alikuwa anamfatilia kwa nyuma,,

    dereva huyo akahisi kunamtu anatembea nyuma yake,,,akageuza shingo yake kutazama upande wa nyuma!

    TAHARUKI!!!!



    Dereva huyo akashtuka kumuona Mbigili,,akamkumbuka,,akatimua mbio akaifuata njia iliyokuwa inaelekea kwenye bwawa la maji,,,

    Mbigili akamkimbiza kwa mbio zake zote.

    wakajikuta wametokezea kando ya bwawa hakuna upenyo wa kukimbilia,,

    dereva huyo akaamua kujitosa ndani ya bwawa angalau aogelee,, akatokezee upande wa pili,,,kumbe ndani ya bwawa hilo kuna mamba wengi,,,

    watu waliokuwa wanaishi kando ya bwawa hilo,, walikuwa hawalitumii,,kutokana na vifo vya watu walioliwa na mamba kila siku,,,,wakati derva huyo anazipiga mbizi kwa nguvu zake zote..ghafla akanaswa na mamba,,akakatwa vipande viwili akafa papohapo...

    Mbigili akafurahi sana, kwa sababu kazi imekuwa rahisi kwake hivyo,,akapata imani kuwa hakuna mtu yeyote mwingine aliyeshuhudia kuwa yeye aliuwa mtu kule jijini Dar es salaam.

    akazipiga hatua kurudi nyumbani kwao,,,akamkuta mama yake ameshafika nyumbani!!!



    Siku zilizidi kusonga,,Mbigili akaendelea kufanya vitendo ambavyo vilimshangaza mama yake! hakukoma kunywa pombe kupitiliza...yeye lila siku alitoka asubuhi na kurudi nyumbani usiku wa manane akiwa kalewa kupitiliza...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA******



    Bi'sundi akaugua,,,lakini Mbigili hakujali wala hakuonyesha jitihada za kumpeleka hospitali mama yake atibiwe!! badala yake akawa anampatia vidonge vya kutuliza maumivu tu,,Panado.

    Bi'Sundi alimsihi sana Mbigili ampeleke hospitali,,kwa sababu anajisikia kuwa hali yake si njema! lakini Mbigili hakutaka kumsikiliza mama yake,,akawa anamwambia,,"mama umri wako umekwenda sana,,,wewe huumwi bali ni maradhi ya uzee,,mara nyingu huwapata wazee wenye umri mkubwa kama wako,,hata nikikupeleka hospitali hautapona,,hivyo ni kupoteza muda tu...

    Maneno hayo yalimfanya Bi'Sundi asikitike,,,

    Kesho yake Mbigili alidamka mapema,,, akaondoka zake pasipokujua mama yake atakula nini!!

    Baada ya masaa mengi kupita,,Bi'Sundi akaamua kunyanyuka kitandani  aende kule dukani kwake angalau akachukue hata soda anywe kutuliza njaa kali aliyokuwanayo!!

    alipozipiga hatua kadhaa akadondoka chini,,,kwa sababu mwili wake haukuwa na nguvu,,,,akajitahidi kujivuruta..mpaka.akaukaribia mlango wa kutoka nje ya nyumba....

    punde si pumde akaonekana Mbigili akiingia ndani ya nyumba,,,akashtuka kumuona mama yake mejilaza kwenye sakafu! akakumbuka kuwa mama yake hajala chakula chochote tangu yeye alipoondoka nyumbani asubuhi.....

    Bi'Sundi akaongea sauti ya chini akimwambia Mbigili aingie chumbani kwake akachukue ufunguo aende kule dukani kumletea chakula chochote!

    Mbigili akafanya kama alivyo ambiwa na mama yake..akachukua ufunguo na kuelekea kule dukani.

    alipofungua mlango akaanza kuangaza angaza kona zote...akaamua kuchukua biskuti nyingi na soda....wakati anataka kutoka ndani ya duka hilo,,,akaona lile sanduku la mbao analolitumia Bi'Sundi kutunzia pesa za mauzo ya duka lake!

    Mbigili akalifungua sanduku hilo akastaajabu kuona pesa nyingi kiasi.....akajisemea moyoni,,"siachi hata shilingi,,tena bora alivyonionyesha sehemu anayoficha ufunguo....

    siku ya leo nilikuwa nawaza nitapata wapi pesa la kunywa pombe,,aisee watanikoma leo.mimi bosi.

    akalifunga sanduku hilo,,kisha akatoka nje ya duka akafunga mlango lakini hakuweka kufuri....nia na lengo lake akishafika nyumbani amkabidhi mama yake ufunguo,,ili asimshtukie!

    baada ya dakika kadhaa akawa amefika nyumbani,,akampa zile biskuti mama yake pamoja na soda,,alipohakikisha mama yake ameshiba,,akaamua kuondoka zake,lakini Bi'Sundi akasema,,"hali yangu si njema,,rudi kule dukani ukatazame chini ya meza utaona sanduku,,chukua laki mbili uje unipeleke hospitali,,Mbigili hakujibu kitu akaondoka zake,,,akaenda kule dukani akachukua zile pesa zote....akaelekea kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.

    siku ya leo walevi wenzake walimkoma,,alinunua pombe yote...akasema wanywe bure....watu walizoea kumuita Mbigili hatimae jina la Jumbe likatoweka kabisa.....kumbe wakati anakunywa pombe na walevi wenzake...

    Mlevi mmoja akamuibia zile pesa zote akaondoka nazo pasipo Mbigili kujua...



    Upande mwingine alionekana ye mlevi,,akizipiga hatua huku akiyumbayumba,, akapita jirani na nyumba yao Mbigili,,kutokana na ulevi aliokuwanao,,akadondosha mfuko wa plastiki uliokuwa na pesa hizo....hakuweza kugundua hilo,,akaendelea kuzipiga hatua na kutokomea kabisa..



    baada ya dakika kadhaa kupita,,akaonekana Bi'Sundi akizipiga hatua kutokea ndani ya nyumba,,,kwa lengo la kuketi nje kujipumzisha kwenye mkeka apate hewa...

    akaona mfuko kwenye njia kando ya nyumba yake,, akauokota mfuko huo,,,alipoufungua akaona pesa nyingi...akauchukua mfuko huo na kuingianao ndani mwake akauficha,,,kisha akatoka nje kuelekea pale kwenye mkeka..



    Ilipofika majira ya saa moja za usiku..Mbigili akahisi kalewa kupita kiasi,,kwa sababu alikunywa pombe nyingi mfululizo..akaamua kunyanyuka atoe ule mfuko aliokuwa kauweka kando ya kiti alichokuwa ameketi....alipotazama pale chini macho yakamtoka,,ni baada ya kutokuuona ule mfuko uliokuwa na pesa zote.....

    Mmiliki wa kilabu hicho cha pombe za kienyeji,,akaamua kumfuata Mbigili kudai pesa yake!!

    KIZAAZAA!!!!!!





    Mbigili,,akahisi kuchanganyikiwa! pombe zikamruka,,akaanza kuleta ugomvi,,akilalamika kuwa pesa zake zimeibiwa...wale.walevi wakaanza kumshambulia kwa maneno makali,,wakimsizitiza alipe pesa za pombe alizoagizia watu wanywe bure...

    ghafla wazo.likamjia kichani,,akachukue bastola yake kule nyumbani,,,huenda wakampa pesa zake!

    kabla hajaondoka wakamnasa wakisema,,"huondoki pasipo kulipa pesa za watu...

    Mbigili akaamua kudanganya kuwa kuna kiasi cha pesa kule nyumbani kwao,,hivyo akaongozana na mmiliki wa kilabu hicho kuelekea nyumbani kwao Mbigili.

    walipofika,,Mbigili akaingia ndani akamkuta mama yake kalala..

    akazioiga hatua kuingia ndani ya chumba chake akachukua bastola kisha akatoka nje,,

    yule mmiliki wa kilabu,,akatimua mbio kuokoa uhai wake..Mbigili akajisifu kuwa yeye ni kidume hakuna mtu anayeweza kumbabaisha..



    Asubuhi palipokucha,,hali ya Bi'Sundi ikawa mbaya,,alidamka yu mgonjwa sana...hata kuongea hawezi...

    Mbigili akaonekana akizipiga hatua kukifuata chumba cha mama yake,,akamkuta mama yake anatetemeka,,,Mbigili akamnyanyua mama yake na kumtoa nje,,akidhani anahisi baridi,,hivyo akamtoa nje ya nyumba aote jua la asubuhi....

    Wakati anambeba,,,Mbigili aliona mfuko mweusi kando ya kitanda,,mfuko huo unafanan na ule mfuko aliokuwa ameweka pesa alizoiba kule dukani kwa mama yake.....

    alipohakikisha kamlaza mama yake nje kwenye mkeka,,akaamua kurudi kule chumbani kwa mama yake,akauiba ule mfuko,akaupeleka chumbani kwake.

    kisha akaenda kuoga,,baada ya dakika kadhaa kupita akatoka nje ya nyumba,,akazipiga hatua kuondoka aelekee kilabuni,,,CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ghafla,,Bi'Sundi akanyoosha mokono wake ishara ya kumuita Mbigili...lakini Mbigili hakwenda kumsikiliza mama yake,,akaondoka zake huku akisema nakwenda kukuletea chakula.

    kumbe Bi'Sundi alikuwa anataka kumwambia ampeleke hospitali haraka iwezekanavyo,,kutokana na hali yake kiafya anavyoisikia!



    Mbigili akaelekea kwenye kilabu cha pombe,,alipofika...akastaajabu kuona walevi wote wanamkimbia.

    hata mmiliki wa kilabu hicho,,akakataa kumuuzia pombe!

    Mbigili akamsihi sana mmiliki huyo...amuuzie pombe,,pia akasema,,"nimekuja na pesa yako yote unayonidai....

    kumbe mmiliki huyo,,alikwenda kuwaambia wanakijiji kuwa huenda Mbigili ni jambazi,,kwa sababu,,anamiliki silaha!

    taarifa hizo zilienea kijiji chote,,

    mwenye kiti wa kitongoji..akatoa taarifa kwenye vyombo vya dora,,,mipqngo hiyo ya kumnasa Mbigili ilifanywa kimyakimya pasipo yeye kujua.

    alipo ona hapewi pombe akaamua kuondoka zake huku akifoka na kutoa maneno makali yenye vitisho!



    Upande mwingine kule nyumbani kwao Mbigili,,alionekana Bi'Sundi akihangaika,,hali yake ilizidi kuwa mbaya kila dakika zilivyozidi kusonga!! akatazama huku na kil kuomba msaada wa kupelekwa hospitali,,lakini hakuona mtu yeyote,,,baada ya dakika Kadhaa kupita Bi'Sundi akapoteza maisha...kwa kukosa matibabu!



    kwa mbali akaonekana Mbigili akizipiga hatua,,kuelekea nyumbani kwao,,,

    alipofika akastaajabu kumkuta mama yake katulia tuli pale kwenye mkeka,,nzi wakiwa wakiwa wamemzunguka mdomoni!

    Mbigili akaingiwa na wasiwasi,,,akajaribu kumuamsha mama yake...lakini hakuamka! akamtikisa pia hakuamka!

     akagundua kuwa mama yake amekufa! macho yakamtoka! akahisi kuchanganyikiwa,,,akatafakari nini cha kufanya!!! akaamua kubeba maiti ya mama yake na kuipeleka ndani ya nyumba!!! akazipiga hatua kuingia chumbani kwake...akafungua begi lake,, akatoa simu,,,akaiwasha akampigia Apolo,,akamtaarifu kuwa Mama yao amefariki!!! wakati anaongea na Apolo alikuwa kasimama upande wa dirisha la chumbani kwake.

    alipoangaza angaza macho yake kwa mbali,,akaona maaskari wakiwa wameshikilia silaha za moto,,wakiifuata njia ya kuja nyumbani kwao,,,

    Mbigili akachukua bastola yake,,,akatoka nje na kutimua mbio kuondoka eneo la nyumbani kwao,,,aliamini maaskari hao wamekuja kumkamata,,kutokana na tukio la mauwaji alilolifanya kule Jijini Dar es salaam!

    wakati anakimbia akakutana na kundi la wanakijiji wakiwa wameshikilia mapanga na marungu,,,

    wanakijiji hao walikuwa wengi....walipomuona Mbigili wakaanza kuonyeshana,,kwa kunyoosha mikono yao kuelekezea ule upande aliokuwepo Mbigili,,,

    wazo likamjia,,'akajisemea moyoni,,"atakayenisogelea tu nitamwaga Ubongo....wakati anatafakari nini cha kufanya....ukasikika mlio wa risasi ikitokea nyuma yake!!!!!

    TAHARUKI!!!





    akashtuka,,akageuza shingo yake,,akaona maaskari! wakafyatua tena risasi nyingine angani, huku wakisema Mbigili ajisalimishe,,,

    bila kuchelewa akachomoa bastola na kuanza kufyatua risasi kuelekea ule upande walipokepo maaskari hao....

    wanakijiji waliokuwa wamebeba mapanga na marungu..wakatimua mbio,,baada ya kusikia milio ya risasi!

    Mbigili akapata mwanya wa kukimbia na kutokomea kusikojulikana..



    Upande mwingine,,kule Jijini Dar es salaam,,alionekana Apolo,,kachanganyikiwa na kifo cha mama yake,,,akaandaa safari ya dharura,,kutoka Dar es salaam,,kuelekea kijijini kwao.....akaingia ndani ya gari lake akiwa kaongozana na marafiki zake wawili,,na safari ikaanza.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ilipofika majira ya saa mbili za usiku,,,wakawa tayari wamefika kijijini....Apolo akashangazwa kutokuona dalili zozote za wananzengo,,kuwepo pale nyumbani kwao! hapakuwa na mtu hata mmoja! ukimya ulitawala...

    Apolo pamoja na marafiki zake hao wawili,,wakazipiga hatua Kuingia ndani ya nyumba! akawakaribisha sebuleni!

    Akazioiga hatua kukagua ndani ya vyumba,,,akashtuka kumuona mama yake akiwa kitandani!! akasogea jarbu na kitanda hicho...akasikitika sana,,akaanza kulia kwa uchungu,,,akimlaumu Kaka yake kwa nini katelekeza maiti ya mama yake ndani badala ya kuipeleka mochwari,,ili taratibu za mazishi zifanyike!

    akatoka ndani ya chumba hicho akazioiga hatua za kinyonge,,huku akilia kwa uchungu!! marafiki zake wakamfariji ,,,

    Apolo akasema,,"itabidi tumpeleke mochwari usiku huu huu,bila kufanya hivyo maiti itaharibika na kuanza kutoa harufu mbaya..

    bila kuchelewa,,wakaibeba maiti ya Bi'sundi na kuiweka ndani ya gari la Apolo,,,,,wakaondoka zao kuekea mochwari!



    Asubuhi palipokucha,,Apolo pamoja na marafiki zake wakadamka na kuelekea mochwari,,,,lakini Apolo alishangazwa na kitendo cha kaka yake,,,mpaka sasahivi hajaonekana,,hata kwenye simu hapatikani!

    Apolo akaamua kuchukua maiti ya mama yake kule mochwari..ili msiba aupeleke nyumbani kwake Jijini Dar es salaam!

    walipokamilisha tafatibu zote za kuitoa mochwari maiti ya Bi'Sundi...safari ya kuelekea Dar es salaam ikaanza.

    waliwasili Jijini Dar es salaam,,saa nne za usiku.



    Asubuhi palipokucha wakafanya taratibu za mazishi,,Bi'sundi akazikwa..

    Apolo alisononeka sana kuhusu kaka yake kutokuhudhuria msiba wa mama yao...mbaya zaidi,,simu ya Mbigili haipatikani hewani,,na haijulikani ni wapi alipo!



    ****BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA*****



    Apolo alikata tamaa ya kuonana na kaka yake! alifanya jitihada za kumtafuta lakini hakufanikiwa kumpata..



    Kumbe Mbigili kakimbilia Nchini Kenya,,,akawa anaishi huko,,,akafanikiwa kupata kazi,,ya udereva kumuendesha katika gari Binti wa tajiri mmoja huko Kanya,,,Binti huyo anaitwa ANITA.

    Siku zilizidi kusonga,,,lakini Mbigili akaingiwa na tamaa ya penzi la Anita...

    sikumoja  Mbigili akavunja ukimya akaamua kumchombeza Anita.

    lakini Anita akaishia kucheka tu,,akiamini ni sehemu ya utani wa Mbigili...hivyo hakujibu chochote..

    Kitendo hicho kilimfanya Mbigili awe mnyonge...



    Sikumoja nyakati za usiku,,alionekana Anita akitokea ndani ya jengo akiwa kaongozana na rafiki zake wa kike...akaagana nao kisha akazipiga hatua kuelekea sehemu ya kuegesha magari..akamkuta dereva wake(Mbigili) anamsubiri...akafunguliwa mlango akaingia ndani ya gari,,,ghafla simu ya Anita ikaita,,,akaipokea kwa furaha,,,,,alipigiwa na mchumba wake anayeishi huko nchini Tanzania..

    wakati Anita anaongea na simu hiyo,,Mbigili alionyesha sura unyonge wa hali ya juu,,kutokana na wivu wa mapenzi....lakini hakuna namna,,ilibidi awe mpole na kuishia kutazama tu.



    Wakati huo huo,,upande mwingine,,alionekana Apolo akiwa nyumbani kwake anashusha mkono wake aliokuwa kashikilia simu,,kutoka sikioni,,kisha akajilaza kitandani,,,



    Siku zilizidi kusonga,,Mbigili hakukoma kumchombeza Anita..lakini Anita hakujibu kitu chochote alibaki kutabasamu tu..

    Siku moja nyakati za usiku,,wakati Anita anatokea kwenye sherehe ya rafiki yake,,,akiwa ndani ya gari,,akastaajabu kumuona dereva wake(Mbigili)akikatisha kona,,kuiacha barabara ya rami,,na kupitia barabara ya vumbi inayoelekea mstuni,,,Anita akauliza kwa mshangao,,huko ni wapi tunaenda?CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mbigili akabaki kimya hakujibu kitu chochote...ghafla akabofya kitufe cha kufunga milango(automatic Lock) milango ya gari ikajifunga kabisa,,,,Anita akaanza kuingiwa na wasiwasi,,punde si punde,,Mbigili akaongeza mwendo wa gari,,akaliendesha kwa kasi zaidi kuliingiza mstuni!







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog