Simulizi : Utajiri Wa Damu
Sehemu Ya Tano (5)
Baada ya Wakili Kwale kumuongoza yule mtu aliyegeuzwa mbwa aitwaye Mavata. Hakimu Makoteni alisema: "Sasa ni zamu ya Wakili Mabere Marando
anayemtetea Cheprisca kumuuliza maswali anayedaiwa kugeuzwa mbwa."
Nilianza kutetemeka baada ya hakimu kumruhusu wakili wangu kuuliza maswali lakini aliniambia kuwa niondoe shaka kabisa katika shauri hili hasa baada ya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kumsimulia jinsi nilivyoingizwa katika kesi hii. Alisimama akaweka vema joho lake la kiwakili.
Marando: Mavata umesema uligeuzwa mbwa, Je, wakati unageuzwa huyu (akanyoosha mkono kunielekea mimi), alikuwepo?
Mavata mbwa mtu: Huyu hakuwepo.
Marando: Je, wakati unakwenda kwa mzee Mitimingi uliwahi kukutana na Chepriska?
Mavata mbwa mtu: Hapana.
Marando: Unamjua au kufahamiana kabla ya kukamatwa na polisi?
Mavata mbwa mtu: Hapana.
Marando: That's all my load (Ni hayo tu mtukufu).
Hakimu Makoteni alimpa nafasi wakili wa mzee Mitimingi, Dk. Ngali kama atakuwa na la kuhoji.
Dk. Ngali: Wewe Mavata umesema uligeuzwa mbwa mtu na mzee Mitimingi, utaihakikishia vipi mahakama?
Mavata mbwa mtu: Mimi siwezi kuihakikishia mahakama kwa sababu nilikuwa mbwa, hiyo kazi wataifanya polisi.
Dk. Ngali: Baada ya kugeuzwa mbwa unasema ulikuwa ukijitambua, kweli au si kweli?
Mavata mbwa mtu: Kweli.
Dk. Ngali: Mahakama itakuamini vipi?
Mavata mbwa mtu: Nitaweza kuhadithia kila kitu hasa siku ambayo polisi walifika pale na kuniona kwa mara ya kwanza na mahakama ikitaka itawaita hao polisi
na kuwauliza, naamini maelezo yangu yatafanana na yao na mahakama itagundua kuwa nilikuwa na akili zangu.
Dk. Ngali: Siku hiyo walipofika polisi katika banda hilo ilikuwaje?
Mavata mbwa mtu: Nililia sana, nikasikia askari mmoja akisema bila shaka huyo mbwa hana chakula au kuna kitu kipo bandani kwake. Walipofika bandani
walishangaa kumuona mbwa ambaye ana sura kama binadamu. Wakati huo mimi nilikuwa nalia na machozi yalikuwa yakinichuruzika kama binadamu.
Wote waliokuwepo pale walipigwa na butwaa na wakasema huyu siyo mbwa ni mtu na wakati huo mzee Mitimingi alikuwa akitetemeka kama aliyekuwa na
homa kali. Mzee Mitimingi na wote waliokuwepo pale wakaondoka huku polisi wakimuagiza mlinzi ahakikishe ananipa chakula kwa sababu bosi wake kuanzia
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
hapo alikuwa chini ya ulinzi wa polisi.
Dk. Ngali: Ikawaje ukachukuliwa na polisi?
Mavata mbwa mtu: Siku ya pili niliona polisi wakiingia uani na kuja katika banda na kunichukua. Polisi mmoja akawa ananiambia nisiogope kwa sababu
wamekuja kwa kuwa wana imani kuwa mimi ni mtu niliyegeuzwa mbwa, wakanihakikishia kuwa aliyefanya unyama huo watamgundua na ubinadamu wangu
utarudishwa.
Wakati Mavata anahojiwa na mawakili na kujieleza akina mama fulani niliwaona wakilia kwani mara kwa mara walikuwa wakifuta machozi. Nilihisi kwamba
inawezekana wale ni ndugu zake.
Dk. Ngali: Ulipofikishwa polisi mambo yalikuwaje?
Mavata mbwa mtu: Nilifarijika sana kumuona mzee Mitimingi akiwa ameshikiliwa huku akiwa na binti yule (akanyoosha mkono kuelekeza kwenye kizimba
tulichokuwa tumeketi, moyo ukanifanya paa).
Mavata alichukua kitambaa mfukoni na kufuta machozi kisha akaendelea kusimulia.
Mavata mbwa mtu: Pale ndipo nilipomuona kwa mara ya kwanza mtu aliyempa dawa mzee Mitimingi zilizonigeuza kuwa mbwa.
Dk, Ngali: Ulimjuaje?
Mavata mbwa mtu: Polisi walikuwa wakimshurutisha anirejeshee ubinadamu wangu.
Dk. Ngali: Ni hayo tu mheshimiwa hakimu.
Hakimu aliandika mahojiano hayo kwenye jalada lake kisha akasema kwa kuwa serikali imeshaleta mashitaka ya wote kimaandishi na mawakili na nakala yake
sasa ni zamu ya Cheprisca yaani mimi kuhojiwa na wakili wangu.
Wakili Marando alisimama na kuniangalia. Alisogea nilipokuwa nimesimama huku akiwa na kalamu mkononi. Nilihisi kutetemeka lakini nilipiga moyo konde
na nilifarijika na maneno yake tulipokuwa faragha kwamba nisiwe na wasiwasi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakimu aliandika mahojiano hayo kwenye jalada lake kisha akasema kwa kuwa serikali imeshaleta mashitaka ya wote kimaandishi na mawakili na nakala yake
sasa ni zamu ya Cheprisca yaani mimi kuhojiwa na wakili wangu.
Wakili Marando alisimama na kuniangalia. Alisogea nilipokuwa nimesimama huku akiwa na kalamu mkononi. Nilihisi kutetemeka lakini nilipiga moyo konde
na nilifarijika na maneno yake tulipokuwa faragha kwamba nisiwe na wasiwasi kwani maswali yake yatalenga kuniondoa katika kesi hii.
Marando: Taja jina lako kamili.
Cheprisca: Naitwa Cheprisca Nahatani.
Marando:Umewahi kufanya kazi yoyote ya uganga?
Cheprisca: Sijawahi.
Marando: Ukiambiwa unahusika kumgeuza mtu na kuwa mbwa utasemaje?
Cheprisca: Nitashangaa kwa sababu kitu kama hicho sikijui na sijawahi kukifanya.
Marando: Hapo kizimbani umesimama na watu wawili, mzee Mitimingi na mganga wa kienyeji, je, unawafahamu hao?
Cheprisca: Namfahamu mtu mmoja tu, huyu mzee Mitimingi.
Marando: Unamfahamuje?
Cheprisca: Tumetoka kijiji kimoja na baba yangu ni rafiki yake, hivyo ni kama baba yangu na alipofika kule aliomba nije kumfanyia kazi ya uhasibu. Kwa hiyo
nikawa nakusanya fedha kutoka kwa madereva au watu wanaotaka kukodi malori yake kisha kuzipeleka benki.
Marando: Vizuri. Umewahi kuona kitu chochote cha ajabu katika nyumba ambayo mnaishi na mzee Mitimingi?
Baada ya swali hilo nilimuona mzee Mitimingi akitetemeka hasa kwa kuwa miili yetu pale kizimbani ilikuwa imegusana, nilihisi mtikisiko wa kutetemeka bila
shaka alidhani kuwa nitamkandamiza. Nilimeza fundo la mate.
Cheprisca: Sijawahi kuona kitu chochote cha ajabu labda siku ambayo polisi walifika na kufungua banda la mbwa nikamuona mbwa wa ajabu.
Marando: Mbwa mtu yule hujawahi kumuona kabla ya hapo? Au hukuwahi kumpelekea chakula au maji hata siku moja?
Cheprisca: Kwanza mbwa mtu mwenyewe hana muda mrefu pale nyumbani na mzee Mitimingi alituambia kwamba ni marufuku kusogelea banda kwa kuwa
mbwa ni mkali sana. Sikuwa na hamu ya kumsogelea kwa sababu mimi tangu nimezaliwa huwa siwapendi mbwa siyo kwa kuwasogelea bali hata kuwaona.
Wakili Marando alikaa kwa muda bila shaka ili kumpa nafasi hakimu aandike kile nilichosema kwa sababu nilitumia sekunde kadhaa kusema maneno mengi
ambayo asingeweza kuyaandika kwa sekunde mbili au tatu.
Marando: Huyo mbwa mtu akiitwa hapa mbele ya mahakama una hakika kuwa atasema hakujui?
Cheprisca: Alishasema hapa kuwa hanijui kabisa na ni kweli hatujuani.
Marando: Thats all my honor (ni hayo tu mheshimiwa).
Hakimu Makoteni anayesikiliza kesi hiyo iliyovuta watu wengi alimtaka mwendesha mashitaka kumhoji chochote Cheprisca kama analo jambo la kutaka kujua.
Wakili wa Serikali: Mshitakiwa umesema kati ya hao watu kizimbani unamjua mzee Mitimingi tu kwa kuwa ni kama baba yako. Ina maana humjui kabisa huyo
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mganga wa kienyeji? Mbona uliwahi kuleta dawa kwa mzee Mitimingi, ulipewa na nani?
Cheprisca: Sijawahi kupeleka dawa za kienyeji kwa mzee Mitimingi hata siku moja labda za hospitali ambazo alikuwa akinituma famasi tena kwa kunipa cheti
cha daktari.
Wakili wa Serikali: Kuna dhana kuwa ulikuwa ukipewa fedha nyingi sana na huyu mzee Mitimingi. Zilikuwa za nini kama siyo kumuunganisha na huyu mganga?
Marando: Objection (Pingamizi), mheshimiwa hawezi kumuuliza mteja wangu swali la kufikirika, hapa mahakamani hatutaki kusikia dhana ina maana hana
uhakika.
Hakimu: Kweli, uliza swali lingine.
Wakili wa Serikali: Sina mheshimiwa.
Aliketi na Hakimu Makoteni alimuita wakili wa mzee Mitimingi kama ana swali la kuniuliza lakini akasema hakuwa nalo.
Ikaja zamu ya mganga aliyemgeuza Mavata kuwa mbwa mtu. Alisimama huku akionekana dhahiri kutetemeka na kutokwa jasho jembamba. Ukumbi mzima
ulikuwa kimya kusubiri atasema nini kuhusiana na kitu alichokifanya.
Hakimu: Mzee tunaambiwa kuwa wewe ndiye uliyemgeuza mtu kuwa mbwa. Unasemaje kuhusu hilo?
Sangoma: (anakohoa)
Hakimu: Kwanza Tuambie jina lako kamili.
Sangoma: Naitwa Dk. Changa Ngumu
Hakimu: Hilo ni jina lako sahihi au unataka kututia changa la macho?
Sangoma: Ni jina langu kabisa nililopewa na wazazi wangu.
Hakimu: Wewe ni kabila gani?
Sangoma: Mimi ni Mfipa wa Sumbawanga vijijini.
Hakimu: Wewe huna wakili wa kukutetea?
Sangoma: Sina kwa sababu nimeshitukizwa kuletwa hapa mahakamani.
Hakimu: Umeshitukizwa? Kwani wenzako wamepataje mawakili? Ni kwamba nduguzo hawakujali kukamatwa kwako. Au huna uwezo wa kulipia gharama za uwakili ukawaambia hivyo?
Sangoma: Hapana. Hawajui utaratibu, kwani bei gani?
(Ukumbi mzima uliangua kicheka.)
Askari: Jamani hapa ni mahakamani, hakuna kuchekacheka, hairuhusiwi, ohooooooo.
Baada ya polisi kunyamazisha watu katika ukumbi wa mahakama, ulitulia pakawa kimya kama vile wahenga wanavyosema ‘shetani kapita,' zilikuwa zikisikika karatasi za hakimu ambaye alikuwa akizigeuzageuza. Baadaye aliamua kuahirisha kesi ili kumpa nafasi mshitakiwa atafute wakili wa kumtetea.
***
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni asubuhi ambapo watuhumiwa walikuwa wamejazana kwenye karandinga la magereza. Mahakimu na mawakili walikuwa bize wakiingia mahakamani tayari kuanza kuendesha kesi.
Mimi Cheprisca, mzee Mitimingi na Sangoma tuliwahi kuletwa kwa difenda, sijui kwa nini au labda kuepusha vurugu kwani watu walikuwa wengi sana.
Hata hivyo, wengi wao hawakujua kuwa tulikuwa kwenye difenda na walikuwa wakikodolea macho karandinga la magereza ili watuone. Nilimpongeza aliyeamua sisi tuletwe pale kwa kutumia gari hilo badala ya karandinga au basi la magereza ambalo nalo lilikuwa tayari limeegeshwa karibu na mahabusu ya mahakamani.
Tuliingizwa haraka haraka mahakamani bila watu wengi kutuona. Hazikupita dakika nyingi Hakimu Makoteni aliingia katika ukumbi wa mahakama baada ya taratibu za askari kupiga yowe ya ‘kooooooort kukamilika'.
Ukumbi ulikuwa kimyaa kwa sekunde chache kisha hakimu akaweka jalada lake vizuri mezani:
Hakimu: Washitakiwa mzee Mitimingi, Sangoma Changa Ngumu na Cheprisca, mpo wote?
Tuliitikia kwa pamoja, "Tupo."
Alisimama Wakili Marando akasema: I'm here for the second defendant called Cheprisca and Dk. Ngali is for the first defendant, mzee Mitimingi while Mr Kasabuvu is representing the third defendant Sangoma Changa Nguvu. (Nipo hapa kumuwakilisha mshitakiwa wa kwanza Cheprisca na Dk. Ngali ni kwa ajili ya mshitakiwa wa pili mzee Mitimingi na Bwana Kasabuvu anamwakilisha mshitakiwa wa tatu Sangoma Changa.)
Hakimu aliandika maelezo hayo ya Marando na akasema atakayeanza kumhoji mshitakiwa Sangoma Changa ni wakili wake, Bwana Kasabuvu.
Wakili Kasabuvu:Mshitakiwa wa tatu, unaweza kuieleza mahakama jina lako?
Sangoma: Naitwa Changa Chungu.
Wakili Kasabuvu: Ni muumini wa dini gani?
Sangoma: Sina dini.
Wakili Kasabuvu: Kwa hiyo wewe ni mpagani?
Sangoma: Hapana, upagani ni tusi, walipachika jina hilo wakoloni ili kutudhalilisha, mimi nafuata dini ya asili, kifupi ni muasilia.
Watu ukumbini waliangua kicheko.
Wakili Kasabuvu: Unafanya kazi gani?
Sangoma : Mimi ni mganga wa mitishamba.
Wakili Kasabuvu: Unamjua yule shahidi wa serikali aliyesimama kizimbani? (alimuuliza huku akinyoosha mkono kuelekea kwa Mavata yule jamaa aliyegeuzwa mbwa.)
Sangoma: Simjui.
Wakili Kasabuvu: Je, unamhafamu mzee Mitimingi?
Sangoma : Ndiyo na ni mteja wangu wa siku nyingi.
Sangoma Changa alieleza mengi sana kuhusu walivyofahamiana na mzee Mitingimi na jinsi alivyokuwa akimpa dawa za kumuwezesha kuwa tajiri.
Wakili Kasabuvu: Hapa mahakamani kuna madai kuwa yupo mtu aligeuzwa mbwa, unalijua tukio hilo?
Sangoma: Nalijua sana.
Wakili Kasabuvu: Unaweza kuifafanulia mahakama?
Sangoma: Mimi ni mganga wa asili, alikuja kwangu mzee Mitimingi na kutaka dawa ya kuzuia watu wasimuibie fedha zake na ili awe tajiri zaidi. Nilimuambia kuwa dawa hizo zipo lakini zina masharti, kwamba kwanza ni lazima watumishi wote alionao wajue masharti ya dawa.
Nilimueleza naye akaenda kuwaeleza wafanyakazi wake. Nilimpa dawa na nikamuambia kuwa atakayeiba atageuka mbwa au atakufa. Baada ya siku chache akaja na kuniambia mfanyakazi wake mmoja tayari amegeuka mbwa, nilimuambia kuwa hakuna dawa mpaka zipite siku sitini.
Siku ya sitini ndipo alipogunduliwa na polisi, hivyo alipoletwa kwangu ilikuwa rahisi kumtibu. Kwa hiyo hapo mimi nina kosa gani? Ni sawa na mtu akiweka seng'enge kuzungushia nyumba yake, akija mwizi akashika akanasa nani wa kulaumiwa?
Wakili Kasabuvu: Unaweza kutaja dawa zinazogeuza mtu kuwa mbwa?
Sangoma: Ni mchanganyiko wa vitu vingi kama vile gamba la konokono, karafuu, mbegu za komamanga, majongoo bahari,ubani, karafuu maiti, zafarani, mishumaa na mbegu za mtopetope au kungu,vyote ni halali.
Wakili Kasabuvu: Katika dawa hizo hakuna kiganja cha maiti au ngozi ya chui?
Sangoma: Hakuna.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakili Kasabuvu: Kuna madai hapa kuwa unahusika na ngozi na kiganja cha mkono wa mtu, vitu vilivyokutwa kwa mzee Mitimingi.
Sangoma: Si kweli, sihusiki kabisa.
Wakili Kasabuvu : Je, uliwahi kumpa mzee Mitimingi ngozi ya chui au kiganja cha mtu?
Sangoma: Sijawahi.
Wakili Kasabuvu: Mbona hapa mahakamani umeshitakiwa pamoja na mambo mengine, kumpa kiganja cha mtu na ngozi ya chui mzee Mitimingi, unasemaje kuhusu hilo?
Sangoma: Hilo hata mimi nashangaa. Sijampa vitu hivyo na wala sijui kwa nini polisi waliamua kunisingizia mambo hayo mazito.
Wakili Kasabuvu: Mheshimiwa hakimu ni hayo tu.
Hakimu Makoteni aliandika maelezo hayo na kumruhusu wakili wa mzee Mitimingi, Dk. Ngali amhoji sangoma huyo juu ya yale aliyozungumza na wakahojiana kama ifuatavyo:
Wakili Dk. Ngali: Umesema mzee Mtimingi ulimpa dawa ya kuzuia wizi wa fedha zake na kwamba ulimuambia atakayeiba atageuka mbwa, kumgeuza mtu kuwa mbwa ni kuzuia wizi?
Sangoma: Muulize mzee Mitimingi kama kuna mtu alidiriki kuiba baada ya tukio lile la mtu kuwa mbwa, sasa kama huko siyo kuzuia kuiba tuiteje?
Wakili Dk. Ngali: Mshitakiwa wewe unachotakiwa ni kujibu ninachokuuliza siyo kunigeuzia kibao kisha kuniuliza mimi.
Sangoma: Basi kifupi ni kuwa dawa ile ilisaidia kuzuia wizi katika nyumba ya mzee Mitimingi.
Wakili Dk. Ngali: Kwa hiyo wewe hukuwa na habari kuhusu mtu huyo kugeuka mbwa mpaka alipokuja mzee Mitimingi kukuambia?
Sangoma: Ndiyo.
Wakili Ngali: Alipokuja mzee Mitimingi kukuambia kuhusu dereva wake kugeuka mbwa baada ya kumuibia fedha zake, ulishangaa?
Sangoma: Nishangae nini? Nilimueleza tu masharti kuwa kumgeuza kuwa mtu tena ni baada ya siku sitini na nikamshauri amjengee banda na ili akome kuiba ni lazima kila siku amkung'ute fimbo kadhaa.
Wakili huyo alimjulisha hakimu kwamba hakukuwa na cha ziada cha kumhoji mteja wake. Ndipo hakimu akamruhusu Wakili Marando anayenitetea mimi Cheprisca amhoji sangoma.
Wakili Marando: Katika maelezo yako hujasema chochote kuhusu mteja wangu Chepriska. Yeye je, ulimpa dawa yoyote ya kumgeuza mtu kuwa mbwa?
Sangoma: Hapana, yeye simjui kabisa mimi.
Wakili Marando akamjulisha hakimu kuwa hana cha ziada cha kumuuliza mganga huyo wa kienyeji.
Hakimu Makoteni alisema amesikiliza kwa makini maswali na majibu lakini angependa kupata ufafafanuzi kutoka kwa mzee Mitimingi kuhusiana na kiganja cha mtu na ngozi ya chui aliyokutwa nayo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee Mitimingi ilibidi asimame pale kizimbani ndipo hakimu alipoanza kumhoji:
Hakimu: Mzee Mitimingi kiganja cha mtu kilikutwa nyumbani kwako. Hujasema chochote kuhusu hilo na pia kuhusu ngozi ya chui, unaweza kutueleza vilifikaje?
Mitimingi: Mheshimiwa hakimu, ni kweli vilikutwa nyumbani mwangu, lakini mimi sihusiki.
Hakimu: Huhusiki wakati hivyo vitu vilikutwa ndani tena kiganja kilikuwa kabatini chumbani kwako?
Mitimingi: Inawezekana nilifanyiwa njama ili kunimaliza.
Hakimu: Lakini naambiwa kuwa ulipofikishwa polisi ulisema vitu hivyo ulipewa na mganga wako, yaani sangoma ambaye yupo hapa umeshitakiwa naye, unasemaje kuhusu hilo?
Mitimingi: Mheshimiwa hakimu, mara nyingi polisi huwa tunakiri makosa kutokana na kipigo, ili kujiokoa unakiri tu ukijua kuwa huku mahakamani ukweli utajulikana.
Hakimu: Huku mahakamani sangoma kasema hajui chochote kuhusu hayo, anachojua ni kukupa dawa za kuzindika fedha zako na ni kweli alipoiba dereva wake akawa mbwa mtu, wewe unasemaje?
Mitimingi: Kama kasema hivyo sijui sasa lakini yeye ndiye mganga wangu.
Hakimu: Kakuruka sasa. Wewe unaonekana ulikuwa unapata utajiri wa damu.
***
SIKU YA HUKUMU
Ilikuwa asubuhi ambapo watu walijaa katika chumba cha mahakama kutokana na wengi wao kuwa na shauku ya kutaka kujua hukumu ya mganga kumgeuza mtu kuwa mbwa.
Mara baada ya hakimu Makoteni kuingia alianza kuchambua maelezo ya mawakili wote, ya Marando aliyekuwa akinitetea mimi, Cheprisca, Dk. Ngali aliyekuwa akimtetea Sangoma na Wakili Kwale aliyekuwa akimtetea mzee Mitimingi.
Hakimu: Maelezo yote yanaonesha kuwa msichana Cheprisca, hakuwa anajua kilichokuwa kinaendelea kati ya sangoma na mzee Mitimingi, hivyo kuanzia sasa wewe Cheprisca… (hakimu alikohoa kidogo na kuandikaandika kwenye jalada, wakati huo moyo ulikuwa ukinienda mbio kama niliyetoka kukimbia, aliniangalia na kusema:) Upo huru.
Ndugu zangu waliokuwa mahakamani hapo walipiga kelele za shangwe, wakatulizwa na polisi.
Hakimu: Sangoma Changa Ngumu una hatia. Umetoa dawa ya kumgeuza mtu kuwa mbwa, unahukumiwa miaka saba jela.
Na mzee Mitimingi unahukumiwa kwa kukutwa na kiganja cha mtu na ngozi ya chui ambayo ni nyara ya serikali. Utatumikia miaka kumi jela na kosa la kumgeuza mtu kuwa mbwa ni jela miaka saba kama sangoma wako, hivyo wewe mzee utakaa jela miaka 17.
Hakimu aliinuka na kutokomea, huku akiacha watu wakilia na wengine ambao ni ndugu zangu wakicheka kwa furaha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment