Search This Blog

NZITA - 1

 







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Nzita

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    ZANIDA alistuka usingizini... baada ya kuota ndoto kuwa anakimbizwa na mume wake huku kasikilia panga kwa lengo la kumkata.... alikurupuka usingizini huku jasho likimtoka....alinuanyuka kitandani na kuwasha taa...kisha akaketi juu ya kitanda.... alitafakari sana juu ya ndoto ile... aliwaza sana alijiuliza maswali yaliyokosa majibu... yapata mwaka wa saba sasa yupo ndani ya ndoa lakini hakubahatika kupata mtoto...ni baada ya kutoa mimba nyingi zaidi ya tano kipindi cha usichana wake enzi akiwa shule... kitendo kile cha kutokuwa na uwezo wa kushika ujauzito kilimnyima firaha.....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    alikumbuka maneno ya daktari miaka kumi iliyopita... """ pia kumbukumbu ya miaka ya nyuma ilimuijia ......alikumbuka

    ilikuwa ni mwaka 2006 Zanida akiwa hoi kitandani huku damu nyingi zikimtoka baada ya kumeza vidonge aina ya P2 kwa lengo la kuichoropoa mimba... baada ya kumeza vidonge vile yalipita masaa mawili"" ghafla zanida alianza kutokwa na damu mfululizo kupitia sehemu zake za siri(ukeni) aliogopa sana alijifungia chumbani kwake ili wazazi wake wasistuke juu ya kitendo kile... alipanda kitandani... akisubiri mimba ile itoke lakini damu ziliendelea kutoka mfululizo mpaka akaishiwa nguvu.. kutokana damu nyingi ilipungua mwilini.. zanida alishindwa kuvumilia aliamua kuita MAMA NAKUFA..

    (((UTOAJI WA MIMBA NI HATARI KWA MAISHA YAKO)))

    mama yake alikwenda mpaka ule upande kilipokuwepo chumba cha Zanida.... alipofungua mlango alishidwa kwa sababu mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani... mama yake aliogopa sana akaingiwa na wasiwasi mkubwa aliamua kumuita baba yake zanida..kutokana na damu nyingi kumtoka zanida hakuwa na nguvu za kunyanyuka kitandani hapo.... baba zanida alivunja mlango walistahajabu kukuta damu nyingi zimetapakaa kitandani hapo...wazazi wake walichanganyikiwa kukuta binti yao yupo katika hali ile....baba zanida alimbeba mwanae kisha akamuweka ndani ya gari....akaliwasha na kuelekea hospital.. wakiwa ndani ya gari mama zanida alilia sana alimuonea huruma binti yake huyo wa pekee... punde walifika hospital..akatundikiwa dripu ya damu. zanida alippfanyiwa uchunguzi iligundulika kuwa aliharibu kutoa mimba ikashindikana!!!! daktari alisema kurokana na mfuko wa uzazi kupasuka na kung'ang'ania ndani ya tumbo... inabidi afanyiwe upasuaji....baada ya kufanyiwa upasuaji daktari alisema binti yenu anaasilimia %95 za kutokuwa na uwezo wa kushika ujauzito kwani hivo vidonge vya kutoa mimba alivyomeza vimeleta athali kubwa katika mirija ya mayai... wazazi wake walisikitika sana..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********BAADA YA MIEZI SITA(6) KUPITA******



    zanida alipona kabisa lakini mzunguko wa siku zake za hedhi zilibadilika na kuvurugika kabisa... wakati mwingine zilijirudia ndani ya mwezi mmoja wakati mwimgine ulipita mwezi mzima bila kuziona siku zake za hedhi... baada ya kumaliza masoma zanida alipata kazi... aliajiriwa kwenye taasisi binfsi ya kifedha katika benki ya CRDB.... alikuwa na mchumba wake aitwae Adam kibwana.. walipendana sana walipanga kuowana na baada ya miaka miwili walifunga ndoa.... maisha ya Adam na Zanida yalikuwa yenye furaha sikuzote...lakini baada ya miaka mitatu kupita furaha ya ndoa yao ikaingia dosari"" ndoa ikawa ndoano... ni baada ya Adam musumbuliwa na mama yake mzazi pamoja na dada zake mama yake alimwambia kila siku mpaka ikawa kama ni wimbo masikioni mwa Adam.. kwamba kwanini mkewe amzalii mjukuu!!!! yapata miaka miratu sasa kama Zanida hazai basi oa mwanamke mwingine au tafuta mwanamke umzalishe... mama Adam alimwambia hivyo mara kwa mara.... kitendo kile kilimnyima sana amani Adam.. kwa kuwa alikuwa anampenda sana Zanida"" kadri miezi inavyozidi kusonga Adam alianza kuiingiwa na maneno ya mama yake... aliamua kutafuta mwanamke wa nje ambaye atamzalia mtoto.... adam alianza kupunguza upendo kwa Zanida akawa anarudi usiku sana nyumnani wakati mwingine harudi kabisa... kitendo kile kilimfanya zanida kuwa nyonge sana alikonda kwa mawazo... ilifika kipindi akiwa kazini akawa hafanyi kazi zake kwa ufasaha.... utendaji kazi ulipungua...sikunyingine hakawa haendi kazini kabisa na hatimae alisimamishwa kazi...

    miezi ilisonga na hatimae yule mwanamke wa nje wa Adam alishika ujauzito.... Adam alifurahi sana akaamua kumfukuza zanida ndani ya nyumba na kuanza kuishi na yule mwanamke mwingine..

    zanida alirudi nyumbani kwao kwa baba na mama... wazazi wake walimfariji sana hasa mama yake alimtia moyo kwa maneno mazuri((MAMA NI MAMA TU HABADILIKI)))



    baada ya mwaka kupita zanida alianza kusahau yale maisha ya ndoa aliyokuwa akiishi na Adam..

    sikumoja akiwa katika matembezi kuna gari lilisimama kando yake... kisha mwanaume akashuka... alistahajabu sana kumuona mtu yule kumbe aliwahi kusoma nae enzi za chuo kikuu.. pale mlimani.... walisalimiana kisha yule mwanaume alijitambulisha anaitwa INOCENT kisha zanida alimkumbuka... walipeana namba za simu...



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Inno aliliwasha gari na kuondoka zake... walianza kuwasiliana na baada ya miezi miwili walijikuta wameingia katika mahusiano ya kimapenzi... Inno hakutaka kuchelewesha mambo aliamua kumuoa kabisa Zanida..... walipendana sana hakuna mfanyo... lakini yalianza kutokea yale yale.... baada ya mwaka kupita inno alistahajabu kwanini zanida hashiki mimba... alianza kuingiwa na wasiwasi..... aliamua kupanga mpango wa kwenda kwa daktari yeye na zanida ili wafanyiwe vipimo... huenda kunammoja wao anatatizo la uzazi.... aliamua kumueleza mkewe zanida....

    zanida alikosa amani baada ya kuambiwa hivyo na mumewe Inno.. aliamini yeye ndiye chanzo cha tatizo lakini aliifanya iwe siri kati yake na wazazi wake...dhamila ilimkereketa akashindwa kabisa kustahimili kuendelea kuifichs siri ile""" alitamani sana kumwambia ukweli mumewe lakini aliogopa kwa kuhisi huwenda mumewe akampa talaka na akamuacha..... ilibididi amueleze ukweli.



    sikumoja inno alikuwa Gorden bar maeneo ya sinza mori.. inno alijumuka pamoja na marafiki zake huku wakizitandika karinya kisawasawa(wakinywa bia) inno alijaribu kuomba ushauri kwa marafiki zake juu ya jambo linalomtatiza kukaa ndani ya ndo kwa muda mrefu bila kupata mtoto...

    mmoja kati ya marafiki zake aliyeonekana kuwa na ulevi mwingi kichwani kwake... aliropoka aaagh fukuza tu... sogeza chombo kingine kipya ndani.. maisha yaendelee... wale wengine walimuunga mkono yule mwenzao aliinekana katoa ushauri wa busara sana.... kisha wakacheka sana na kugonga glasi zao kwa pamoja... inno alionekana kuupokea ushauri huo moja kwa moja bila kutafakari... kutokana aliona marafiki zake wa karibu wametoa wazo moja... wazo hizo alilipitisha kisha wakaendelea kuzitandika karinya...

    (((RAFIKI WA KWELI NI YULE ANAYEKUPA MAWAZO YA BUSARA NA UAMUZI SAHIHI HATA KAMA JAMBO NI GUMU ...)))

    waliagiza mzunguki mwingine wa vinywaji safari hii inno aliamuru kuwa muhudumu alete bia tisatisa mezani... iwe pongezi kwa marafiki zake kumshauri wazo zuri....



    *************CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ilipofika majira ya usiku saa sita kasoro inno aliwaaga marafiki zake na kuingia mdani ua gari lake kuelekea nyumbani.... zanida alistahajabu mpaka mda huo mumewe hajarudi nyumbani na si kawaida yake.....ilibidi ampigie simu kabla hajafanya hivyo alisikia mngurumo wa gari...akazipiga hatua alipochungulia dirishani aliona mumewe karudi.... baada ya kumfungulia mlango inno aliingia chumbani na kupanda kitandani... kitendo kile kilimshangaza zanida... ilibidi amfate mumewe kule chimbani... alipomuuliza kwa nini kacjelewa kurudi!!!!! aisee alichokoza moto inno aligeuka mbogo alianza kumtolea maneno ya kashfa mkewe... """usiniulize maswali ya kijingajinga... kwanza mwanamke mwenyewe huzai mimi nakushughulikia kila siku hata hushiki mimba... nimechoka kukaa na goli kipa asiyejua kudaka mipira. inamaana mashuti yote hayo ninayopiga mwaka mzima hujadaka hata moja unaacha mipira yoye inaingia galini bila mafanikio... sasa basi kuaanzia kesho nikirudi sitaki kukukuta ndani ya nyumba yangu rudi nyumbani kwenu.... zanida alianza kulia huku akimsihi mumewe asimuache... basi mume wang nakuruhusu mzalishe mwanamke yeyote lakini nakuomba usiniache"""zanida alimwambia hivyo mumewe huku akilia kwa uchungu... maneno yale yalimkera Inno akamfata zanida ili aanze kumpiga.... mara ghafla inno aliteleza kwenye vigae na kudondoka"""aliangukia kisogo kutokana alikuwa amekunywa pombe nyingi inno alitoka damu nyingi sana....pia damu zilianza kutoka puani na masikioni.....





    Inno alikimbizwa hospitali haaraka.....walipomfikisha hospitali walikuwa wamechelewa kwani inno alikuwa kaishakata roho muda mrefu tangu nyumbani kwake...

    zanida alilia kwa uchungu sana... hakuamini kilichotokea....

    taratibu za mazishi zilifanyika... inno akazikwa kenye makaburi ya kinondoni... baada ya siku arobaini kupita ndugu zake inno walimfukuza zanida kwenye yumba ya mume wake walimwambia kuwa hana mtoto hivyo aondoke zake... zanida alilia sana.. hakuwahi kuwa na furaha sikuzote za maisha yake...

    zanida arirudi nyumbani kwao...... kwa baba na mama...baada ya miezi kadhaa kupita zanida alianza kubadilika akawa anakunywa pombe kupita kiasi!!!! hii ni kutokana na mawazo juu ya kupata mtoto...maisha yake ualikuwa ni kuolewa na kiachwa.. kwa sababu hakuwa na uwezo wa kushika ujauzito(mimba) alianza kwenda kwenye kumbi za starehe za kukesha...baada ya miezi kadhaa kupita alikata tamaa ya kuolewa tena alianza kuuza mwili wake... zanida aliishi maisha yaliyojaa hatari kubwa kwani wakati mwingine wanaume waliokuwa wakimnunu kwa lengo la kujiburudisha kingono""" wengi wao walikuwa hawatumii kinga hivyo akawa anahatarisha maisha yake...



    *************



    HAKUNA KULALA ????(HAKUNA KULALA)

    HATA KAMA HUJALA??(HATA KAMA HUJALA)

    ACHA KUCHEZA KWA MAPEPE (PEPE) ??????

    ACHA WATU WATAKUSHANGAA??????



    ulisikika wimbo huo wa msanii mkongwe nguli wa muziki hapa nchi JUMA NATURE ukiimba kwenye spika kubwa za club ''''Alionekama zanida akikata mauno kama feni aliucheza wimbo huo kwa madaha huku akizungusha kiuno chake na kujipapasa papasa mwilini mwake... kutokana na kigauni kifupi alichokuwa amekivaa kilimbana vyema hivyo maungo yake ya mwili yalionekana kuvutia...sana"""CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wanaume wakwale(mafataki)

    walim-mezea mate zanida... ghafla simu ya zanida ikaita aliweza kuisikia kwa sababu alikuwa ameiweka kwenye mtetemeko(vibration) zabida aliacha kuendelea kucheza akatoka nje haraka kupokea simu hiyo... kutokana na kelele za muziki kusikika sana aliamua kwenda kando kabisa ili aongee na simu.... aliipokea simu na kuzipiga hatua za harakaharaka.... ile sehemu alipokuwa amesimama palikuwa nagiza.... ghafla walitokea vijana watatu wa kihuni.. wakamnasa zanida nakumzutia kunako giza zaidi walimziba mdomo ili asipige kelele... lengo la vijana hao watau ilikuwa wam-bake zanida... wakati zanida anafurukuta ghafla kuna gari lilikuwa linakuja upande ule hivyo taa za gari zilimulika eneo lile yule dreva alipo ona tukio lile aliamini kuwa vijana wale sio watu wazuri wanataka kumdhulu zanida... aliamua kuendesha gari kwa kasi mpaka eneo lile.. wale vijama watatu baada ya kuona hivyo waliamua kukimbia na kutokomea kusikojulikana huku wakimuacha zanida gauni lake limechanika.. zanida alimyanyuka pale chini na kukimbilia pale gari lilipokuwepo.. yule mtu alimwambia ingia mdani ya gari zanida hakusita aliingia haraka....

    mapigo ya moyo ya zanida yalikuwa yanapiga kwa kasi kutokana na uwoga.... mtu yule alijitambulisha kwa zanida kuwa yeye anaitwa Nassoro...

    naii.... i.. itwa zanida"zanida alijitambulisha huku akipumua pumzi za kukatakata....nassoro alimuuliza unaishi wapi... zanida alijibu mimi naishi popote tu... nassoro alistahajabu"""" popote!!!! unamaanisha nini??? nassoro aliuliza''

    zanida hakuimgea chochote... alikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema samahani kaka naomba unisaidie nipate sehemu ya kulala usiku wa leo tu.. si unaona nguo yangu imechanwa hivyo siwezi kutembea uchi... nassoro alimuuliza umaonaje nikupeleke nyumbani kwangu kisha utaindoka kesho asubuhi... kwani mimi naishi peke yangu.... zanida alikubali kisha wakaelekea nyumbani kwa nassoro....



    ***************



    zanida alistuka akanyanyuka kitandani kisha akaelekea sebuleni....kumbe zanida hayo yote ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka ya nyuma iliyopita enzi za usichana wake kumbe alikuwa akiwaza.... ni baada ya kustuka usingizini alipo ota ndoto kuwa anakimbizwa na mume wake huku kashika panga."""

    zanida alipofika sebuleni alifungua friji na kuchukua maji ya kunywa kisha akarudi chumbani..... mume wake zanida alikuwa amesafiri kikazi"""""

    ndiye yule nassoro aliyemsaidia kule maeneo ya club ni miaka minne sasa imepita kumbe nassoro aliamua kumuoa zanida. nassoro alimpenda sana zanida huu ni mwaka wa nne sasa tangu alipoanza kuishi na zanida...

    zanida alipanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi...



    ***************

    palipokucha zanida alikwenda magomeni kwa rafiki yake kipenzi aitwaeJasmin ujio huo wa zanida nyumbani kwa jasmin ilikuwa ni kwenda kuomba ushauri... zanida ilibidi amwambie ukweli jasmin kwa sababu alimuamini sana... jasmini alimwambia kuwa atampeleka kwa mganga mmoja anayepatikana yombo.... niamini mganga huyu atakusaidia na utapata mtoto""""kesho nitakupeleka.... jasmini alisema hivyo..



    zanida aliondoka na kurudi nyumbani kwake... alipokuwa njiani aliwaza sana.... mmmh! kwa mganga!!! sijawahi kushiriki mambo ya kishirikina!!! lakini itabidi tu... alijisemea moyoni zanida. baada ya muda alifika nyumbani kwake ilikuwa ni majira ya saa mbili za isiku... kutokana alikuwa amekula chakula kule nyumbani kwa jasmin hivyo hakuona haja ya kupika chakula..

    aliingia chumbani kwake..kisha akajiandaa kwenda kuoga... na baada kama ya dakika kumi hivi kupita alipanda kitandani na kuanza kuutafuta usingizi....



    ************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Palipokucha alidamka na kujiandaa kwenda nyumbani kwa jasmini ili waende yombo kwa mganga... kabla hajaondoka mara ghafla simu yake iliita alipoipokea ni jasmin alikuwa akimpigia.... jasmin alimwambia zanida kuwa yeye yupo njiani anakuja kwake ili waondoke.. zanida alijibu ok sawa shosti utanikuta""

    jasmin hakuwa mbali sana kutoka nyumbani kwa zanida.. na kwa sababu alikuwa akiendesha gari hivyo haikuchukua dakika nyingi jasmin alifika.... alipiga honi ya gari.. zanida akachungulia kupitia dirisha la sebuleni alipogundua kuwa ni jasmin... zanida alitoka nje.... alielekea moja kwa moja mpaka pale gari lilipokuwa limepaki... alifungua mlango akaingia ndani ya gari... jasmin aliliwasha gari na safari ya kwenda yombo kwa mganga ikaanza.. walipokuwa njiani zanida alikuwa anamdadisi jasmin juu ya mambo ya kishirikina...

    jasmini alimjibu majibu ua mkato... zanida aliamua kukaa kimya huku akiendelea kubofya simu yake.... kutokana na foleni kuwa kubwa hivyo iliwalazimu kukaa barabarani masaa zaidi ya matatu.... mnamo majira ya saa tisa alasili waliingia yombo.... kwa sababu jasmin alikuwa anapafahamu vyema kwa mganga yule aitwae SUMBI hivyo alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa mganga huyo... walipofika waliambiwa mganga yule alihama eneo lile miaka miwili iliyopita"" walipojaribu kuulizia ni wali anapatikana,,, waliambiwa kuwa anapatikana mkoani MOROGORO kwenye milima ya ULUGULU.... zanida aliishiwa nguvu na kukata tamaa"""sasa huko morogoro tutampataje? aliuliza jasmin. kisha akajibiwa'mkifika morogo maeneo ya nane nane mkimuulizia maeneo hayo mtaoneshwa kwa sababu wakazi wa maeneo hayo wanamfahamu... hivyo watawapeleka mpaka kwenye milima ambao anapatikana... alijibu hivyo kijana wa mwisho wa mganga SUMBI..

    waliamua kuondoka..... walipoingia ndani ya gari walipanga mpango wa safari ya kuelekea morogoro.. itawabidi twende siku ya jumamosi nitakuwa Off~ (siku ya mapumziko ya kazi) Alisema hivyo jasmin.... zanida hakuwa na budi kukubaliana na jasmin.... kisha jasmin aliliwasha gari wakaondoka..... jasmin aliliendesha gari moja kwa moja mpaka nyumbani kwa zanida....walipofika zanida alishuka... mara ghafla simu yake iliira alipoitazama aligundua kuwa mumewe anampigia... alipoipokea zanida aliishiwa mguvu.... baada ya mume wake kumwambia kuwa anatarajia kurudi siku yoyoye kuanzia mwezi ujao kwani kazi iliyompeleka Amerca amekwisha ikamilisha....zanida hakuraka kumueleza jasmin kuhusu hilo.... waliagana kisha zanida akaanza kuzipi gatua kuelekea ndani...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ***BAADA YA SIKU TANO KUPITA***



    Jumamosi ikawadia... jasmin alikwenda nyumbani kwa zanida asubuhi na mapema... zanida alijiandaa kwa ajili ya safari na ilipo fika mnamo saa tano asubuhi safari ilianza ya kuelekea morogoro """ mnamo majira ya saa kumi waliwasiri morogoro... wakaelekea maeneo ya nane nane waliulizia kwa wakazi wa maeneo hayo...kijana mmoja akasema anafahamu mganga huyo anapopatikana lakini mtanilipa shilingi elfu kumi... alisema kijana huyo"" zanida alifungua pochi yake na kutoa noti mbili za shilingi kumi kumi.. kisha akamkabidhi kijana yule....



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog