Simulizi : Roho Ya Giza
Sehemu Ya Tano (5)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Fundikira akaanza kuingiwa na hisia za kuibanjua amri ya sita..akaanza kumpapasa mwanamke huyo,,akambeba na kumlaza juu ya meza anayoitumia kuwekea baadhi ya vitu vidogo vidogo, Fundikira akaanza kuvua suruali yake,,punde si punde zikasikika sauti za nafsi mbili...nafsi moja ikimwambia asisite aendelee kufanya kitendo hicho...wakati huohuo nafsi nyingine ikimkataza asifanye kitendo hicho,,nafwi hiyo ikamwambia,, "huyu si binadamu wa kawaida bali ni pepo,, mshinde shetani.
Fundikira akabaki mdomo wazi pasipokujijua nini anafanya...akaacha kuvua suruali yake..akaivaa haraka na kufunga mkanda...kisha akazipiga hatua kurudi nyuma huku akimtazama mwanamke huyo kwa macho ya mshangao!
mwanamke huyo akashtuka! akanyanyuka kutoka juu ya meza akazipiga hatua za taratibu,,huku akijipapasa maziwa yake kwa kuyabinyabinya! Fundikira aliendelea kumtazama mwanamke huyo,,, kuanzia kwenye kiuno kushuka chini,,
mwanamke huyo aliendelea kuzipiga hatua kwa madaha,,huku akipinda nyonga zake, kutokqna na umbile lenye mvuto alilokuwanalo mwanamke huyo.
Fundikira akajikuta anameza mafundo ya mate huku akijiramba midomo yake!
wakati mwanamke huyo anazipiga hatua,,,ghafla akaikanyaga ile biblia iliyokuwa pale chini kwenye sakafu! punde si punde akaanza kupiga kelele,,kwa kihisi maumivu makali ya moto ukichoma mwili wake,
macho yakamtoka Fundikira,,akamtazama mwanamke huyo kwa makini,,,alipotazama miguu ya mwanamke huyo,,akaona mguu mmoja wa mwanamke huyo umekanyaga biblia! Fundikira akashtuka! akajisemea moyoni,,"bila shaka huyu ni pepo..
bilq kuchelewa Fundikira akajisafisha kwanza mwili wake kwa kutubu dhambi aliyoitenda pasipokukusudia,,,akamuomba Mungu kwa imani amuondolee majaribu hayo..kishaakaanza kusali kwa kukemea, mwanamke huyo akaanza kupiga kelele mfululizo,ghafla akaanza kuwaka moto kama kamwagiwa mafuta!
akaungua na kuteketea papohapo , ukawa ndio mwisho wa mwanamke huyo.
*************************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande mwingine kule kuzimu,, alionekana Lucifer akitazama tukio zima linaloendelea ndani ya kanisa la Fundikira....kitendo hiyo lilimkasirisha sana Lucifer...akaamua kuandaa mpango mwingine kabambe.....akatoweka kimiujiza na kujitokeza mbele ya kiongozi mkuu wa wafuasi wa Lucifer...kisha akasema,,"nakupa kazi na uifanye siku ya leo kabla mwezi haujaandama..... mke wa Fundikira auwawe kisha niletee kichwa chake.
Kiongozi mkuu akatii amri ya Lucifer..akasujudu miguuji mwa Lucifer....punde si punde Lucifer akatoweka kimiujiza kurudi kuzimu.
ilipofika saa moja za usiku...kiongozi mkuu akaitisha mkutano wa dharura,,akateuwa wafuasi wawili,,waende kupandikiza chuki,,kwa raisi wa nchi,,aamuru makanisa yote yaliyofunguliwa na watu binafsi yachomwe moto. na atakayekiuka auwawe.
bila kuchelewa wafuasi hao wawili wakatoweka kimiujiza.
***************************
Upande mwingine,,alionekana Raisi akiwa katika,jengo kubwa kwenye mkutano na waandishi wa habari akilihutubia taifa kupitia vyombo vya habari... pumde si pumde wakajitokeza kimiujiza wale wafuasi wawili....mmoja kati ya wafuasi hao akagusa kichwa cha raisi..ghafla raisi akasita kuongea,, akabaki kimya kwa sekunde kadhaa,,,akapoteza kumbukumbu kichani mwake,,akawa hakumbuki alikuwa anaongea kuhusu jambo gani! akawatazama waandishi wa habari kwa macho ya msisitizo,,uso wa raisi ukabadilika,,hata ule muonekano wa tabasamu ukatoweka,,akaweka sura ya kusisitiza jambo fulani!! kisha akasema,,"natoa tamko na lifanyiwe kazi kabla hapajakucha,,makanisa yote yaliyofunguliwa na watu binafsi yachomwe moto,,na atakayejaribu kupiga au kuzuia agizo hili auwawe kwa kukatwa kichwa papohapo....
alipomaliza kuongea maneno hayo,,akasema,,"mkutano umekwisha mwaweza kwenda.
waandishi wa habari wakabaki na mshangao, huku wakitazamana nyuso zao....
wakati huohuo...huko mitaani,, kauli ya raisi ilileta gumzo kwa wananchi..wakabaki wakijiuliza raisi kapatwa na nini!? kwa nini katoa maamuzi magumu kiasi hiyo...vikiwemo vitisho vya mauwaji!
bila kuchelewa maaskari wakavamia mitaa kutafuta makanisa ya watu binafsi....makanisa mengi yakachomwa moto.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*************************
Upande mwingine kule nyumbani kwa Fundikira,alionekana Fundikira akizipiga hatua za haraka kutoka nje ya nyumba yake...ni baada ya kusikia agizo la raisi kupitia Runinga yake.
taarifa hiyo ilimfanya Fundikira achanganyikiwe,,,alitembea huku akiongea peke yake na kumlaumu raisi kwa maamuzi hayo!
Mke wa Fundikira akaamua kumfuata mumewe kwa sababu alijua kuwa Fundikira hawezi kukubali..kanisa lake lichomwe moto....hivyo atauwawa na maaskari walioagizwa na raisi...kanisa halikuwa mbali kutoka nyumbani kwa Fundikira.. baada ya dakika kadhaa akawa amefika kwenye kanisa hilo..akawakuta maaskari wakilimwagia kanisa hilo mafuta aina ya petroli.
Fundikira akapaza sauti akiwasisitiza wasichome nyumba ya kumuabudu Mungu.. lakini maaskari hao hawakumsikiliza Fundikira hatimae wakamaliza kulimwagia mafuta kanisa hilo..akaonekana askari mmoja akiwa ameshikilia kiberiti..akilisogelea kanisa hilo alichome moto...Fundikira akaruka kama kipa.....kujirusha ule upande alipokuwepo askari huyo,,wakadodoka chini,,maaskari wakaanza kumshushia Fundikira kipigo kikali!
mke wa Fundikira akatimua mbio kuja kuwazuia maaskari hao wasiendelee kumpiga mumewe...ghafla mkuu wa maaskari hao akachukua bunduki kutoka mikononi mwa askari mwingine...akachomoa singe iliyokuwa mbele ya bunduki hiyo...kisha akamsogelea mke wa Fundikira! kutekeleza amri ya raisi.
Fundikira akaanza kusali akimuomba Mungu,,amnusuru mkewe pamoja na yeye wasiuwawe. akiwa katikati ya maombi! ghafla simu ya mkuu wa maaskari hao,,ikaita...alipoitazama ilikuwa inatoka makao makuu...akasita kumuangamiza mke wa Fundikira.
Wakati huohuo,,Raisi alionekana kushtushwa na taarifa zilizozagaa mitandaoni kuwa ameamuru makanisa ya watu binafsi yachomwe moto..na atakayeleta kipingamizi..auwawe!
kumbe wakati Fundikira anasali,,nguvu za giza zilizopandikizwa kichwani mwa Raisi wa nchi,,zikatoweka,,akili yake na ufahamu wa kawaida ukarejea....akaamuru kuwa zoezi hilo lisitishwe mara moja.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************************
Upande mwingine kule katika kanisa la Fundikira,,walionekana maaskari wakiingia ndani ya magari yao na kuondoka wakati huohuo,,ni baada ya kauli ya raisi kuamuru zoezi hilo lisitishwe.
Fundikira hakuacha kusali,,alipofumbua macho yake akaona magari ya maaskari yakiishilizia na kutokomea kabisa..
akanyanyuka harakaharaka kutoka pale chini..akamnyanyua mkewe,,,wakamsifu Mungu kwa kuokoa uhai wao.
Fumdikira na mkewe wakarudi nyumbani.
Wakati huo huo,,kule kuzimu,alionekana Lucifer akiwa na hasira kupita kiasi! akaanza kuwala nyama baadhi ya wafuasi wake!
kisha akatoweka kimiujiza na kujitokeza mbele ya kiongozi mkuu wa wafuasi wa Lucifer hapa duniani.. akamchukua na kutowekanae kimiujiza kurudi kule kuzimu.. ni kitendo cha sekunde moja wakawa wamefika kuzimu! akamuadhibu kiongozi huyo kwa kumtumbukiza ndani ya shimo lenye moto mkali..
kisha akateuwa wakala mwingine,,akasema,,"kesho unahitajika uifanye kazi kubwa ya ziada....sitokwambia cha kufanya bali utapata maelekezo utakapokuwa umelala usingizi..wakala huyo kutoka kuzimu,,akasujudu kwenye miguu ya Lucifer kisha akasema,, "Ewe mfalme wa dunia..naam nitaifanya kazi hiyo kwa moyo mkunjufu!
kisha akatoweka kimiujiza kurudi duniani.
ilipofika majira ya saa tisa za usiku..wakala huyo akiwa amelala usingizi.
Lucifer akajitokeza katika ndoto....kisha akampa maelekezo...
Asubuhi palipokucha,,wakala huyo akadamka,,akanyoosha mikono yake juu,,,likajitokeza bakuli lililokuwa limejaa damu ya binadamu,,akainywa damu hiyo na kutoweka kimiujiza.
akajitokeza kwenye soko kuu,,soko hilo lilikuwa na msongamano wa watu wengi...
wakala huyo akaangaza macho yake kulitazama soko pande zote...kisha akatoweka kimiujiza....
baada ya dakika kadhaa kupita,,likatokea tetemeko la ardhi! tetemeko hilo lilijitokeza kimiujiza,
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wakati huohuo,,alioneiana Fundikira na mkewe wakiwa katika mizunguko wakinunua mahitaji ya ndani! mke wa Fundikira akasema tupite sokoni nikaangalie mboga za majani! Fundikira akasema,,"hakuna tatizo mke wangu twaweza kwenda....walipolikaribia soko,,wakastaajabu kuona watu wanatimua mbio huku wakipiga mayowe. tetemeko hilo lilionekana eneo hilo la soko pekee....lilikuwa ni tetemeko ambalo halijawahi kutokea,,ardhi ilipasuka na kutengeneza mashimo makubwa yenye kina kirefu,,,majengo na vibanda vilivyokuwa katika soko hilo,,vikatumbukia ndani,,huku baadhi ya watu pia wakitumbukia ndani ya mashimo hayo,,,
Fundikira akatazama kwa macho ya umakini akagundua eneo hilo kuna nguvu za giza zimepandikizwa....akasema,,"tazama kule kunawatu wengi wamevaa majoho meusi,,wamewhikilia mabakuli makubwa,,,
mke wa Fundikira alipotazama hakuona kitu chochote...akasema,,"hao watu wakowapi? mbona mimi siwaoni!?
Fundikira akajisemea moyoni,,"pole sana mke wangu najua hana uwezo wa kuona viumbe wenye nguvu za giza wakiwa katika nafsi ya pili! punde si punde wakaonekana watu hao ambao ni wafuasi wa Lucifer,,wakinyoosha mikono yao iliyokuwa imeshikilia mabakuli hayo. punde si punde damu ikaonekana ikitoka ndani ya mashimo hayo na kuingia ndani ya mabakuli yaliyoshikiliwa na wafuasi wa Lucifer.
Fundikira akaanza kusali kwa kukemea.....akimuomba Mungu aziondoe nguvu za giza eneo hilo,,watu wasiokuwa na hatia wasiangamie.
ghafla wale wafuasi wa Lucifer wakahisi kunanguvu inawazuia..wasiendelee kuchukua damu ya watu wasiokuwa na hatia.....
Fundikira akaendelea kusali kwa imani, huku akikemea...punde si punde ukaonekana moto mkubwa ukiwaka,,kwenye ule upande walipokuwepo wale wafuasi wa Lucifer! wakaanza kuunguzwa miili yao...moto ulikuwa mkali kupita kiasi,,hatimae wakashindwa kuvumilia wakaanza kupiga kelele za maumivu makali...walipojaribu kutoweka Kikijiza...wakashindwa,,wakagundua kuwa nguvu za giza zimetoweka ndani yao.....wakaungua hatimae wakateoetea kabisa.. ghafla tetemeko la ardhi nalo likatoweka kimiujiza.,,walikufa watu wachache ambao tayari walichukuliwa damu mwilini mwao,,lakini wengiwao walinusulika kifo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***************************
Siku iliyofuata,,,kulikuwa na misiba mingi ya matajiri wana wafanya bihasha wa kubwa,,pamoja na viongozi wa serikarini! vifo hivyo vilifikia mamia ya watu ambao ni matajiri......kumbe wale wafuasi wa Lucifer walioteketea kwa moto siku ya jana...ndio hao matajiri,,waliokuwa wanapata mali na pesa nyingi kwa kumuabudu Lucifar....
hakuna binadamu wa kawaida aliyetambua,,kuhusu vifo vya matajiri hao vimesababishwa na nini,,tena ni vifo vya pamoja.
Fumndikira pakee ndiye alikuwa anajua siri ya vifo hivyo!
***************************
Upande mwingine,,kule kuzimu,,,alionekana Lucifer akiwa amechukizwa na kitendo hicho cha wanachama/wafuasi wake,,kufa.. akaandaa mpango kabambe yeye mwenyewe kwenda kumuangamiza Fundikira.
punde si punde,,akatoweka kimiujiza na kujitokeza ndani ya nyumba ya Fundikira,,,
wakati Huohuo Fundikira alionekana akiwa chumbani kwake akimfundisha mkewe kusali kwa imani! ghafla Lucifer akahisi nyumba ya Fundikira inawaka moto,,alipoutazama moto huo akagundua kuwa ni ule moto mkali kuliko moto wowote hapa duniani! akajisemea moyoni,,"inamaana huyu ananguvu gani kuhamisha moto wa kuzimu kuuleta hapa duniani...
wakati anajiuliza maswali hayo yasiyokuwa na majibu...akaanza kuhisi moto unamsogelea hapo alipo.
wakati huohuo alionekana Fumdikira akiendelea kusali kwa imani yeye pamoja na mkewe..
hatimae Lucifar akaanza kuunguzwa na moto huo...alipojaribu kutoweka kimiujiza, arudi kuzimu akashindwa......moto ulikuwa mkali kupita kiasi akaanza kupiga kelele,,huku akijisemea moyoni,,"aisee huu moto kumbe sio wa mchezo mchezo....maumivu yakauzidia mwili wake..hatimae akaanza kupiga kelele...
kule upande wa nje yakaonekana mawingu yakitoa sauti...sauti hiyo ilisikika masikioni mwa Lucifer pekee.....ikisema,,"HUWEZI KUNIJARIBU,,VIVYO HIVYO HUWEZI KUMJARIBU MWANADAMU ANAYENIABUDU NA KUNITUMIKIA MIMI MUUMBA WAKE..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ghafla nguvu za Lucifer,, zikarudi,,akatoweka kimiujiza na kurudi kuzimu....alipofika akaingiwa na hofu kubwa kisha akajisemea,,"kumbe mimi nacheza...huyu MUNGU ni amazing,,sio wa sport sport(si wa mchezomchezo)...lakini bado ninayo nafasi,, sitomjaribu mtumishi wa Mungu..badala yake nitalipa kisasi kwa watakaofuata matakwa yangu..
Siku zilizidi kusonga,,,Fundikira hakuandamwa na nguvu za giza,,
akaendelea kuwaelimisha watu jinsi ya kumtafuta mungu..
Familia yake ikaishi kwa amani,,na upendo.
******************MWISHO******************
0 comments:
Post a Comment